KIJANA IBRAHIM SAIDI A.K.A SULTANI A.KA. USTAADHI AMBAYE LEO AMEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA JELA KWA KOSA LA KUMPIGA KOFI HADHARANI RAIS MSTAAFU ALHAJI ALI HASSAN MWINYI WAKATI WA BARAZA LA MAULIDI MNAMO MACHI 10, 2009 KATIKA UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE HALL JIJINI DAR.

Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Neema Chusi, Amesema kabla ya kusoma hukumu kwamba mahakama imezingatia jinsi mshtakiwa huyo alivyokubali kosa hilo na kuona kwamba anashtahili adhabu hiyo.

Akijitetea kabla ya kuhukumiwa kifungo hicho, mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Said alidai kuwa anakiri kufanya kosa hilo na kwamba anakubali kupewa hukumu na mahakama hiyo.

“Mimi ni kiumbe dhaifu, labda nisiiombe mahakama ila nimuombe mwenyezi Mungu Subhana wataallah kama atataka nitapunguziwa adhabu”alisema Said.

Said ambaye kabla ya kuongea maneno hayo alikuwa akizungumza lugha ambayo haikuweza kutambulika na mahakama hivyo kumfanya Hakimu Chusi kumtaka kubadili lugha hiyo ili mahakama iweze kumuelewa.

Baada ya mshtakiwa huyo kuondolewa kizimbani hapo huku akiwa chini ya ulinzi wa Polisi, ndugu akiwemo mama mzazi wa Said walionekana wakilia nje ya mahakama hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 51 mpaka sasa

  1. Ok pole sana kijana....lakini ulistahili hiyo.Mshukuru sana MUNGU pamoja na MWINYI kwa kukusamehe....nxt tym tuheshimu hata sisi wakristo kwani wewe ulileta udini.MUNGU akusamehe man.

    ReplyDelete
  2. Huyu Kijana kule gerezani atakutana na wenzake wataalamu wa kuwasha vibao!Watamfundisha adabu.Na akisha toka gerezani asubiri adhabu nyingine ataikuta!Katutia sana fedheha huyu kijana!

    ReplyDelete
  3. Yaani anapata kifungo peke yake bila kupelekwa kupimwa akili? Sasa akitoka jela si atakuwa hatari zaidi kwa jamii?

    Jana gazeti la Daily News liliwakariri majirani zake wakisema kwamba huyo kijana ni Chizi -- sasa nadhani kwamba huko jela huu uchizi wake utapata nafasi ya kuongezeka na sio kupungua.

    ReplyDelete
  4. kijana uliyofanya unahitaji laana ya huyu mzee uliyempiga! anyway amekusamehe lakini yaelekea akili ni butu!! maana kijana mdogo kama huyu kufikia kumpiga mtu mzima kofi ni uenda wazimu na maishani kwako utakuwa mtu wa hovyo tu

    Mangi K'koo

    ReplyDelete
  5. jamani wadau mbona adhabu ni ndogo kuliko kosa alilotenda au kwa vile amekiri kosa? mh haya kila la kheri kijana huko segerea.

    ReplyDelete
  6. duu maliza mwaka uje huku uswazi tumalizane na wewe kwa kukuwasha vibao, kila siku adhabu kama uliyomfanyia mzee ruksa, heee mtoto hujafunzwa adabu ndo maana ukaenda kuonyesha ubabe kwa mzee wa watu, ila udini uliwajaa sana kwani kusema kuhusu kondom ndo amekutuma wee ukatumie, yeye pale ni kiongozi wa serikal, alikuwa na nafasi wewe chiziii au unazitumiaga ndo maana zilikuumaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  7. JAMANI C ANGEMPIGA MKAPA AONE CHA MOTO MBONA ANGEMRUDISHIA MWENYEWE HATA BODI GADI ASINGEKUWA NA KAZI!HAYA BWANA UMEMUONEA MZEE WA WA2

    ReplyDelete
  8. Kwanza anaonekana kama vile ni mgonjwa! Au ana ukimwi ndiyo maana alikasirika mzee wetu kuongelea suala hili. Mweeee Watanzania tutakufa kama kuku its high time kuongea vitu hivi hadharani maana mijitu haisikii. Hadi leo watu bado wanaendeleza ngono kavu kavu huwezi amini. Pole baba yetu mzee mwinyi ulikuwa unafanya wajibu wako kama mzazi.

    ReplyDelete
  9. huyo dogo hskustahili adhabu hiyo,alitakiwa asemehewe kwani mzee mwinyi ndo alikuwa na kosa kuhubiri kondom katika hadhara ambayo haikubali matumizi ya kondom,kiongozi wa dini anaye tetea kondomu adhabu yake ni kutimuliwa kanisani au msikitini.hakuna dharula katika ngono. so kijana ametetea imani yake, hatofautiani na aliyempiga kiatu bush au mashaidi wa uganda kwa wakatoriki, pia rejeeni kisa cha kufukuzwa upadri, padre karugendo. mungu atamsaidia huyo dogo na mungu atamlinda.

    ReplyDelete
  10. Pole ndugu yangu katika iiman, mi nakuunga mikono yote, wala usihofu, huo mwaka ni mchache sana, punde tu utatoka. Ila ujumbe umefika. Hawa wazee wanasiasa watakoma kutumia majukwaa ya dini yetu kuongea upuuzi wao. Yote uliyoyasema ni true, hakuna haja ya sisi kusherehekea sikukuu za wakristo wala wao kusherehekea zetu na kama wanaona condom ni sawa waende kwenye vyombo vya habari. Huyu mzee anapaswa kututaka radhi sisi waislam dunia nzima. Umetimiza wajibu wako kama mwislam wa kufikisha ujumbe kwa njia uliyoiona mwafaka.
    Eti watu wanadai umemvunjia heshima huyo mzee, je kama yeye hajiheshimu je? wamwambia achambue ya kuongea kwanza, sio anaropoka tu!

    ReplyDelete
  11. Usemakweli, sielewi vipi mpaka huyu kijana akafanya kitendo hicho. Ila tu mara nyingi siku hizi mtu lazima apimwe akili kwanza halafu apelekwe mahakamani

    Usione kuwa hana akili timamu.
    Hapo alipokuwa anaongea lugha ambayo haieleweki labda ni kithibitisho kuwa akili yake haiko sawa sawa

    Kitendo alichokitenda si kizuri mwendawazimu ndo anaweza kufanya hivyo.

    Mimi nadhani apelekwe kwenye kitengo cha watu wasio na akili timamu.

    P.E.D

    ReplyDelete
  12. Huyu kijana haikumpasa kumpiga Mzee mwinyi, hana adabu, Mzee mwinyi ameshakua mtu mziama kwenda kumpiga vile sio vizuri hata kidogo, kama yeye kajiona hajakamilika, na kwa nini ampige mzee mwinyi, kwani nani kakwambia hapa ulimwenguni binadam gani amekamilika, hamna hata mmjo! ila inachotakiwa wewe mwenyewe umuombe mungu akusaidie na matendo yako!ukatende yalyo mema! na kwa jilani yako pia! nao ndio upendo! Sio dini ndio inayojaza binadam, bali ni wanadam wenyewe! wapo waliozaliwa na wazazi wenye dini tofauti! lakini UPENDO UNAUNGANISHA BINADAM tambua hilo,na imani bila upendo ni bure! unamchukia jilani yako unadai una imani wapi na wapi, unaenda kumpiga MZEE mwinyi unadai imani, yote ni kukosa upendo.

    ReplyDelete
  13. usijalı kıjana najua ALLAH yupo pamoja nawe umetumıa ADITH YA MTUME MUHAMMAD S.A W inayosema kama unaweza kulıondoa ovu bası tumıa mkono na NAMTUME ALISHASEMA ITAFIKA KIPINDI VIONGOZI AU WATU WATAHALIRISHA NGONO ujumbe umefıka kıjana japo wanakuona chızi.BRO MICHU USIIBANIE HII

    ReplyDelete
  14. Kijana ulifikiri kuendekeza udini ungepata support toka kwa maudhaaz wenzako
    haya sasa uliona ni dhambi kwa mwunyi kusema watumie kondom sasa ndio hivyo unaenda huko jela kwa wanaume na utaolewa huko ndio utajua je kuhamsisha kondom ni dhambi au wanaume kulawitiana huko jela ndio zambi
    sikupi pole kijana ndio fundishokwa wale wanaojiita walimu wa dini kumbe ni wachochezi tuu

    ReplyDelete
  15. Anon wa 3:23 udogo wa adhabu upo wapi. Ulitaka mzee Mwinyi naye aitwe amrudishie kibao kimoja? au. Hii adhabu ni kubwa sana ukilinganisha na kosa na mtu mwenyewe. Kwanza nafikiri hakimu amekurupuka kutoa hukumu, alitakiwa kutoa amri huku kijana achunguzwe akili yake kabla ya kupiga mvua. Sasa ikigundulika kuwa ni mchizi kama inavyojulikana nani atakuwa mwehu kati ya hakimu na mtuhumiwa?. Huyu hakimu ametumia "UNDUE INFULENCE" ya nafasi ya mzee mwinyi katika kufikia hukumu, alichotakiwa kuangalia kwanza kwa huyu kijana ni je ana "SOUND MIND?", Maana kama mtu ni unsound mind basi Combination kati ya "ACTUS REUS" and "MENS REA" haikuwepo hapo

    "actus non facit reum nisi mens sit rea" which means that "the act does not make a person guilty unless the mind is also guilty". huyu kijana anaonekana not guilty in mind. Na alitakiwa kuachiwa huru na kibano kiwageukie walinzi wa Mzee mwinyi.

    ReplyDelete
  16. Waislamu takbiiiiiiiiiiir! Tuungane kumuokoa mwenzetu. Kapimwa akili na matokeo hayajatoka, wanamfunga, haki iko wapi? Waislamu tusikubali jamani, twendeni gerezani tukamtoe. Anahitaji kumuona dokta huyu.
    Ustaadhi Hemedi,
    Tandale kwenye Internet.

    ReplyDelete
  17. Atafia gerezani huyo!

    ReplyDelete
  18. yaani mtu akipandisha jazba akapimwe akili?think again. im happy sheria imekula kote ukijumlisha na parol inamaana ni miezi 5 na nusu. then anakuwa celebrity baada ya hapo. gerezani hatoonekana juu ni high profile. atawekwa mahala pa zuri tu. duh bongo new york nimekubali.

    ReplyDelete
  19. Jamani,hii case mbona imekwenda haraka?Mbona kuna ndugu yangu alimpiga mumewe mpaka sasa ni miaka 3 kesi haijaisha?Au ni kwa sababu aliyepigwa hapa ni rais mstaafu?
    Huyu jamaa naona kashukuru Mungu,mimi nilifikiri wangemuua kimya kimya asirudi tena duniani-Hongera dogo!Umepona.

    ReplyDelete
  20. Asalaam Alaykum.

    Kwanza napenda kusema hivi, huyu kijana ndio amefanya makosa na anatakiwa ashtakiwe na alipe kwa kosa alofanya lakini mie nauliza hivi. Mwaka moja aloupata je angeupata hta kma angempiga mpita njia tuu ama kapata mwaka sababu kampiga Raisi mstaaf? Maana hili ni kosa lkn mwaka moja? Mmmmh hapo huyo alomuhukumu amechina.

    ReplyDelete
  21. Mtume amesema "si katka sisi asiyewahurumia wadogo (watoto) na kuwaheshimu wakubwa(wazee au viongozi)." Watu wa balagha manaelewa maani ya "si katika sisi", inaweza kuwa "si mwenzetu."

    Mdau USA.

    ReplyDelete
  22. HASARA MBILI:

    1) MZEE KAANDIKA REKODI MBAYA YA RAISI WA KWANZA KUSHAMBULIWA NA RAIA DUNI. NA KAPATA MAUMIVU, POLE MZEE WANGU.

    2)KIJANA KAPOTEZA MWAKA WA NGUVU KAZI. INAWEZA ISIWE HASARA KWAKE KWANI HUENDA NI MIONGONI MWA WATU WALIOKATISHWA TAMAA KWA SERA ZA TANGU WAKATI WA MKOLONI, HANA CHA KUPOTEZA. ATAKUTANA NA WENGINE KAMA YEYE NA HUENDA AKAWA MBAYA ZAIDI.

    HII NI MBAYA PALE SEHEMU YA JAMII INAPOWEKWA KATIKA HALI YA KUWA HAWANA CHA KUPOTEZA KWA KUFANYA KITENDO CHOCHOTE.

    ReplyDelete
  23. Mstaafu Rais anaahaki ya kuhubiri anachotaka na huyo kijana anahaki ya kuamini anachotaka yeye lakini hakuna mtu ambaye anastahili kuchukua sheria mkononi mwake.

    Kumzalilisha yoyote kwa kumpiga kibao hilo ni kosa na anastahili kuchukuliwa hatua japo sijui sheria zetu zinasemaje kwa mtu anayemchapa kibao mwenzake.

    Ninachofahamu ni kama ukimpiga mtu na kumjeruhi unastahili kwenda jela mwaka mmoja kama mahakama itakutia hatiani na sijui swala la kumtia kibao mtu.

    Hakuna ujumbe mzuri ambao unaweza kuutoa kama kujieleza na sio kuanzisha fujo au kumpiga mtu, kwani hiyo sio njia ya Amani na ni ukiukaji ya haki za binadamu.

    Mfano Mama yako akikosea au Baba akikosea je utampiga kibao kila watakapokuwa wanakosea? kwa mtimamu yoyote wa Akili jibu ni hapana, ila kuna njia sahihi ya kuwaelimisha au kuwaeleza kwamba maneno ambayo wameyasema sio sahihi.

    Mjusi

    ReplyDelete
  24. Nina swali moja tu, "mboona hii kesi imeenda haraka, hamna kuharishwa kwa kesi wala kurushwa kwa tarehe,hamna dhamana hata kama amekubali kosa, sionagi kama hii uwa inatwenda kwe wengine?

    ReplyDelete
  25. Binadamu tunapofika Mahali na kuanza kumtetea mtu na kusahamu kuwa binadamu huyo anaetewa amelifanya kosa la kupinga kauli ya Mola tena Hadharani ni kweli jamaa kafanya kosa lakini pia tujiulize hivi mzee mwinyi amezisahau nguzo za kislamu?ikiwemo kuamini vitabu vya mwenyezi mungu na kauli ya makatazo ya zina yamo katika quran mtu kama mzee mwinyi mwingi wa elimu ya dunia na ya akhera anapotowa tamko ambalo (INDIRECT)ana halalisha zina kauli yake inafanya watu wengi kuendeleza zina almradi watasema natumia condom ndio hapo jamii inapopotoka na machafu kuwa mengi ndani na nje ya uwislamu Au ndio nae mzee mwinyi ameungana na wale watu ambao kwamba wameliwafiki jambo la MABARADHULI kuwa ndani ya uongozi Makanisa ? ndani ya bible hukumu ya mahanisi inajulikana zina haikubaliki katika Ukristo na uislamu sasa unapobadilisha hali hiyo inakuwa unarekebisha na kuweka vipengele ndani ya dini kwa maslahi yako na sio kwa Mmungu wako Tukumbuke hapa wakati wa mwalim julias na uongozi wake hakuna siku hata moja aliyonyanyuwa mdomo wake na kusema sasa nguruwe aliwe Bayana lakini Mzee mwinyi alisubutu hilo hasara gani kwa mzee wetu wakati wakutubia yeye ndio hivyo tena Mmungu amvuwe na amtowe katika giza lililo Mgubika la ulimwengu na ampe muangaza wa akhera yake

    ReplyDelete
  26. Huyu kijana alimpiga mzee Ruhsa sheria ikachukua mkondo wake. Sasa wale waliompiga huyu kijana na ambao wameonekana moja kwa moja mbona sheria haijafuata mkondo au kwa vile yeye ni mlalahoi??!!
    Je wale waliompiga ni sheria gani iliwaruhusu kufanya hivyo???
    Haki isifuate upande mmoja tu jamani yaani kutoka juu kwenda chini.
    Polisi wana wajibu wa kuwachukulia hatua wote waliompiga. Na hao wanajiita watetea haki za binadamu inabidi pia watetee haki za huyu kijana na kushinikiza wale wote waliompiga wafikishwe mahakamani.

    Binadamu wote ni sawa mbele ya sheria..........inaelekea Tannzania sio.

    Mzawa!

    ReplyDelete
  27. alipatiwa lawyer huyu jamani....wanasheria wa bongo mko wapi...sio lazima mlipwe ...pro bono hamuijui nyie....huyu wakimpima akili sio mzima..sasa haraka haraka ya nini kumhukumu....

    ReplyDelete
  28. Misupu ilushe hii kwa hawa jamaa wa ccmmarekani.blogspot.com hili watanzania wenzetu nje ya nchi wajionee kituko hiki

    ReplyDelete
  29. Hukumu ya huyu kijana haikuchelewa hata kidogo, lakini hukumu ya mafisadi bado ni kitendawili hingawa udhaidi wote hupo wazi na waliyoyafanya ni mabaya mno ukilinganisha na la huyu kija. Je hiyo ndio haki tunayotakiwa kumuonyesha mwenyezi mungu?

    ReplyDelete
  30. Kusema kweli mawaidha ya mzee hayakuwa mabaya ,lakini angegoja siku kama ya maadhimisho ya vijana duniani,au siku ya ukimwi duniani,ndio angeebuka na hiyo mada yake ya makondom, hapo ni pake,lakini pale ilikuwa sio mahala pake, ile ilikuwa siku yamaazimisho ya kuzaliwa kwa mtume s.a.w kuhamasisha KONDOM haikuhusu hapo kabisa, kuhusu kijana only ameover react.

    ReplyDelete
  31. wakati alipokuwa anaongea rugha isioeleweka sanyingine alikuwa anapiga maduwa INSHALLAH mungu atamuhukumia .
    huyo hakimu hana lolote kujishebeduwa tu kwa kina Mwinyi. huyu kijana ana onekana mlala hoi leo, lakini kesho atalala peponi wakati hakimu atakuwa makaa ya motoni na kujishebeduwa kwake kafanya chap chap afungwe duh less than a wk?.
    duh kijana anabonge la faith mpaka amekubali aadhibiwe mashallah.!
    na kumuomba subuana watahala.huyu hata akifia jela si mwenzetu peponi moja kwa moja.

    maulidi una advertise Condom na ngono wapi na wapi? ? ? ? ? ? ? ? ??????????????? ? ? ? ?
    give me a break .

    TAKHBIR .......

    ReplyDelete
  32. Iliandikwa kwamba alikwenda kupimwa kama ana au hana matatizo ya akili. Si mtaalamu lakini naamini unatakiwa muda wa kutosha kuweza ku-establish kama kweli anayo matatizo au hana - mara nyingi inabidi ahojiwe mara kadhaa na wataalamu wa maradhi hayo. Kinachonitia wasiwasi ni kwamba kama kweli ni "chizi" - atakuwa ni mlemavu aliyeonewa kama ilivyo kawaida hapa kwetu watu wenye ulemavu rahisi sana hukosa haki zao (waulize wahandisi na wajenzi wa daraja la Manzese). Mtoto mwenye matatizo ya kusoma husemwa kuwa mjinga, miaka saba ikapita akarejea mitaani. Mimi mmoja siamini kuwa kitendo cha kumpiga kofi mtu mwenye kuheshimika na kupendwa na watu kama Rais mstaafu AHM ni kitendo cha uhuni wa kawaida. Uchizi kama anao huko gerezani hautopungua.

    ReplyDelete
  33. Huyu kijana anafikiri anatenda Sharia kwa mujibu ya imani yake. mara nyingine imani inaweza kukupeleka kubaya. jamaa anafikiri yupo Somalia. Dini ni imani binafsi na kila mtu ana haki ya kuamini anachotaka. Mtazamo wake wa kuona kwamba watu wa dini tofauti wasiwe karibu ni mtazamo ambao watu anaokwenda nao msikitini wanaamini. Serkali inabidi ingalie msikiti gani anakwenda na kama kuna vikundi vya chuki kusudi wawazuie kabla awajaleta balaa. SMH!

    ReplyDelete
  34. hii ni njisi ilivyo rahisi kwa vijana wa kiislamu kutumiwa isivyo kuangamiza maisha ya wengine wasio na hatia.eti kwa sababu hawakubaliani na mawazo ya watu wengine.... just imagine huyu kijana angetumiwa na watu wenye imani potofu. sasa hivi anajifanya anaomba msamaha lakini kama angejipasua alikuwa na nafasi ya kuomba msamaha. kama siyo kuacha wajane na yatima. sijui ni kwanini hii kesi imeshughulikiwa haraka namna hii, ni supersonic trial...sidhani kumshambulia kiongozi au hata mmatumbi unachukua mwaka mmoja kwani hili si shitaka moja...kuna mlolongo wa kesi hapa, sidhani adhabu hii itakuwa ni fundisho kwa wengine, sijasoma sheria lakini kesi hii itakuwa inatumika katika kesi zanamna hiyo huko mbeleni....haya ndio mambo ya tanzania yetu.

    ReplyDelete
  35. kesi imeenda spidi ya ajabu. Kumbe mahakama zinajua kufanya shughuli haraka...sasa mbona kesi nyingine zajivuta?? maswali kibao kichwani

    mtoto

    ReplyDelete
  36. Kumbe mahakama zetu zinao uwezo wa kuendesha na kumaliza kesi fasta namna hiyo! Au kwa sababu inamhusu Rais mstaafu??!!

    kuna watu wana kesi hakimu ana kila kitu mezani ushahidi, mashahidi nk. lakini kesi zao zina miaka kibao haziishi na kibaya zaidi wanaendelea kuwa rumande mtu amekaa rumande miaka 4 akifuhukukumiwa anafungwa miaka miwili ukijumlisha 6!!!!

    ReplyDelete
  37. Mwinyi inabidi afahamu alichokiongea si sahihi kwa mtazamo wa kiislamu, I do know why he said so. But still time is there he can correct what he had messed up before his soul got snatched from his body. He should know punishment of hereafter doesn't resemble one year. And those who are trying to sell the words of God for little pleasure of this world God is gonna show them how much his words cost.

    ReplyDelete
  38. Nyie mnaouliza kwa nini hii kesi imekwenda haraka. jibu ni kwamba: NI KWA SABABU MSHTAKIWA AMEKIRI KOSA. hizo kesi ambazo mnaona zinacheleweshwa huwa ni sababu washtakiwa wamekana makosa yao na ndo maana kesi huwa inaahirishwa kwa uchunguzi zaidi.

    ReplyDelete
  39. safi sana sheikh ebrahim,at least umetenda jema...ujumbe umefika kwa hawa wahalalisha ngono....ungemzaba na shavu la kulia haikutosha!!

    ReplyDelete
  40. Nyie mnayemtetea Huyo kijana mtaona atakapotoka...tutamwinda kila mahali na sisi tumuwashe vibao! na zaidi ni kwamba hatapata kazi sehemu yeyote ili ajute kosa lake! na hatasamehewa hadi atakapoonja mauti!! Kumpiga Mzee ni kosa kubwa kwa maadili ya sisi waafrika!! Kondom tumeweka pembeni na sasa tuko sambamba na huyo kijana!!! atatueleza kilichomfanya anyenyue mkono kumpiga kibao mzee wetu!!! Mimi simo kwenye mambo ya Dini wala Kondomu mimi nitakula naye sahani moja huyo Dogo!!Weka pembeni adhabu ya mahakama weka pembeni alichosema Mzee wetu kuhusu matumizi ya Kondom, weka pembeni Dini inasema nini...turudi kwenye jamii yetu...inaruhusu kumpiga kibao mzee?? hiyoni dharau ya hali ya juu na dogo utaipata fresh ukitoka jela!!Hatutanii

    ReplyDelete
  41. adhabu aliyopewa ni ndogo sana ukilinganisha na kosa alilotenda,it doesn't matter mzee ruksa alikuwa anaongelea nini..ndio maana u need to make choices, aidha kukaa na kusikiliza au kuondoka na kwenda msikitini,.huwezi kukurupuka na kumpiga mtu yeyote kwa kutoa mawazo yake mahali popote ni kosa kisheria na nchi yetu haina dini.

    ReplyDelete
  42. kama kukiri ndio sababu kuharakisha kesi yako mahakamani basi huyu bwana kakiri katika hali isiyo sahihi. kama aliweza kupata kibano mbele ya camera, basi nyuma ya pazia ilikuwaje?

    ReplyDelete
  43. mzee rukhsa tunaamini ya kuwa wewe ni ndugu yetu katika uislamu na kama kweli umemsamehe huyu kijana basi tumia ukubwa wako umtowe ustaadh katika adhabu hii.

    ReplyDelete
  44. unacho amini wewe si lazima waislam woote waamini, au dini zoote zikubali.

    kama dini mnaijua sana nendeni mkapatanishe sunni na shia wasiuane kila siku. Msituletee chuki ktk jamii.

    shika imani yako, lakini usihukumu asiye amini sawa na wewe .

    ReplyDelete
  45. Apelekwe Mirembe Hospitali, karibu na Gereza la Isanga pale Dodoma, kwa kuangaliwa zaidi akili yake, inawezekana akaendelea kuwapiga vibao hata wafungwa wenzake, kwani inaelekea ana farijika kila anapotoa duku duku lake kwa njia ya mateso kwa wengine. ni ugonjwa unaotibika...

    ReplyDelete
  46. niliona vibaya sana kusoma hii habari juu ya mzee wa watu kupigwa kofi. kama huyu kijana ni mgonjwa apelekwe kumuona daktari na sio kumpeleka jela. huyu kijana akipelekwa jela serikali haitamtendea haki. ugonjwa wake unaweza kushuhulikiwa na daktari mtaalam wa magonjwa ya akili kabla ya ugonjwa wake haujawa mkubwa. in fact haina haja ya kumpeleka kwenye hospital ya vichaa. huyu anatakiwa kutibiwa hapo muhimbili. jamani tusimlaumu mgonjwa kwasababu hakuna mtu anataka ugonjwa. tukumbuke ugonjwa unaweza kumpata mtu yeyote.

    ReplyDelete
  47. Ndugu zangu waislamu makaa mkijua kwamba Tanzania haifuati sharia kwahiyo kama hukubaliani na mawazo ya watu wengine its ok lakini kaa ukujua kwamba ukimpiga mtu utahukumiwa na sheria za nchi na sio za dini its simple very simple dini ni dini na serikali ni serikali nynyi mnomtetea huyu kijana its ok he did his thing so he need to pay his deed and that is jail and good luck for him and if you dont like the term he got then kaishi Sauidi arabia wanfuata sheria au Sudan ok

    ReplyDelete
  48. Kwa vyovyote vile Messege send and delivered mwinyi next time utajaribu kupanga vizuri maneno yako yaendane na sehemu na hafla yenyewe sio kila ulipo unamwaga upupu, ujue unawawasha waunini wenzio.

    Simlaumu sana kijana labda hiyo ni njia yake ya kuonyesha msisitizo na hata ukiangalia kofi lenyewe alimpiga kinyenyekevu sio kwa jazba ya kutaka kumjeruhi, ni kiasi cha kumaanisha tu kuwa watu hawahamasishwi zina pale walitegemea kuambiwa na kukumbushwa waache zina sio waendelee kwa kutumia kondom, hata makanisani bado mapadre na wachungaji wanakataza zina hawasemi mutunie kondom.

    TAKBIR...

    ReplyDelete
  49. BIG UP KIJANA UMEFUDHU KATAKA IMANI.
    Kuzuiya munkari Waislamu tumeagizwa, unapoona mukari umetokea kwanza ni kuzuia kwa mkono, ukishindwa zuia kwa kusema basi ukishindwa kabisa, nyamaza na kunyamza ni imani dhaifu kuliko zote.

    TAKBIRRRRRRRRRRRR.....!

    ReplyDelete
  50. M zee Mwinyi pole kwa kofi na kamtoe mtoto kwani alishampiga shetani aliyekuzinga, na bila shaka utakuwa makini. viongozi wengine mpate fundisho sio muongee mtakavyo, mafikiri watu hawana kazi ya kufanya wakiwaazima masikio yao?

    ReplyDelete
  51. Mahakama imetoa hukumu isiyo sahihi.Kwanza ilitakiwa kusubiri ripoti ya kitalamu juu ya afya ya mtuhumiwa ili itoe hukumu,Pili kama serikali yetu inayojifanya kuwa mstari wa mbele kuwahukumu raia haraka haraka kwa sababu tu ya maslahi yao,je wale polisi waliomshambulia mtuhumiwa kwa mateke na mangumi wamechukuliwa hatua gani?Je hiyo sheria inayotolewa na mahakama inawaruhusu watuhumiwa kupigwa na kuteswa kwa hali hiyo?Ibrahim amepiga kofi lakini polisi wamempiga hadi na mateke,Je huu ndio uadilifu wa mahakama zetu?Mzee Mwinyi amekosa busara na ameyaharibu maadili ya mtanzania.Ni kweli serikali yetu haina dini lakini watanzania wanadini na imani zao ambapo viongozi wa nchi wanatakiwa kuziheshimu.Hakuna dini hata moja inayowaamrisha wafuasi wake wafanye ngono.Akiwa kiongozi anayeheshimika,alitakiwa kutumia nafasi yake hiyo kukataza kabisaaa zinaa kwani hilo ndio jambo la msingi katika maadili ya muafrika.Nani yupo tayari DADA AU MAMA yake wafanyiwe kitendo hicho kichafu cha kuziniwa?Nani yupo tayari kuona mwanafamilia yake akiteseka kwa UKIMWI?Ukweli ni kwamba hakuna..Kuhimiza matumizi ya kondom ni kumaanisha tuendelee kuyanufaisha hayo makampuni uchwara pamoja na watoa matangazo wao huku watanzania tukiendelea kuteseka na kufa kwa Ukimwi asubuhi na jioni...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...