Mwandishi habari wa siku nyingi Hamidu Bisanga (shoto) hatunaye tena. Hamidu, aliyejulikana zaidi kama Hambi, amefariki jana katika ajali ya gari akiwa anaelekea nyumbani kwake oysterbay mtaa wa Chisiza, karibu na iliyokuwa La Dorce Vita. Mipango ya mazishi inafanywa hapo nyumbani kwake na anatarajiwa kuzikwa kesho saa saba mchana makaburi ya Kisutu.

Hambi aliwahi kufanya kazi kwa muda mrefu Daily News akiwa mhariri wa habari kabla ya kujiunga na shirika la maendeleo (NDC), na baadaye kuhamia kampuni ya BayPort. Alikuwa pia mwanachama wa klabu za michezo za  SingaSinga ya relwe gerezani na Brake Point ya kijitonyama.

Katika picha hapo juu ni Februari 11, 2009 ambapo anaonekana Kamanda wa mkoa maalumu wa Kipolisi wa Dar es Salaam Afande Suleiman Kova akipokea traksuti 22 alizokabidhiwa na meneja wa masoko na uhusiano wa kampuni ya Bayport Hamidu Bisanga ikiwa ni msaada wa kampuni hiyo kwa timu ya polsi inayoshiriki michuano ya klabu bingwa netiboli kwa nchi za afrika mashariki na ya kati huko zenji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. haiyaaaa

    ReplyDelete
  2. Inna lillaah wa inna illaah rajiun. I cannot express my grieve over the loss of such a wonderful man.

    ReplyDelete
  3. Habari hii ni ya kusikitisha sana kwa jamii na wanahabari.

    Katika siku za karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la ajali nchini Tanzania. Kila mwezi tumekuwa tukishuhudia ajali kubwa zaidi ya moja ambazo zinaua wetu wengi.

    Kuna haja ya kufanya tathmini ya kina kuhusu vyanzo vya ajali nchini ili kubaini tatizo ni nini. Ili liende sambamba na kufanya mapitio ya utoaji wa leseni kwa magari na madereva na vile vile kuimairisha sheria za barabarani na kuzisimamia ipasavyo.

    Mwisho, napenda kutoa pole kwa ndugu za Hamidu Bisanga na jamii ya wanahabari

    Mdau
    Faustine
    http://drfaustine.blogspot.com/

    ReplyDelete
  4. Poleni sana ndugu zetu waandishi wa habari kumpoteza mwenzenu wa pili katika muda mfupi.

    Nitamkumbuka Mzee Hamidu alivyokuwa kweli ni mtu wa watu, mcheshi, mwenye moyo wa upendo, na mwenye kujua mambo mengi sana, na hasa historia yote ya Tanzania kwa undani kabisa.

    Tafadhali ufikishe salamu za rambirambi kwa familia yake kutoka kwa wadau wa Blog ya Jamii.

    ReplyDelete
  5. WATOA HABARI MSIWE WAVIVU WA KUTAFUTA HABARI KAMILI KABLA YA KUZITOA, TRENI IMEPATA AJALI CHAKUSHANGAZA HATUAMBIWI TRENI YA ABIRIA ILIKUWA IKITOKA WAPI KWANI HILI NDILO MUHIMU ZAIDI KULIKO IDADI YA WALIOKUFA. SASA MSIBA WA HAMIDU UNAFANYIKA OSTABEI KARIBU NA LA DORCE VITA, NIJUAVYO HUKO KUNA MITAA MINGI TU NAYO INA MAJINA, SIJUI KAMA KUNA GHARAMA ZA ZIADA KUTUJULISHA MTAA! NAIPA POLE SANA FAMILIA YAKE NA MARAFIKI WOTE.

    ReplyDelete
  6. Mwenyezi Mungu amrehemu mzee Bisanga na awape nguvu familia yake za kukabiliana na wakati huu wa majonzi. Alikuwa akifanya mambo yake bila kusumbuana na mtu!!

    ReplyDelete
  7. MR MICHUZI HESHIMA YAKO,
    NAOMBA NITOE DUKUDUKU LANGU JAPO HALITAFANYIWA KAZI.
    1. TANZANIA HAIDHAMINI RAIA WAKE KWANI TUNAPOTELEWA NA WATU WENGI SANA KWA UZEMBE WA BARABARANI
    WATU WANAENDESHA MAGARI KIHOLERA TU BILA LESENI AU HUHONGA WAHUSIKA NA KUPEWA LESENI AMBAZO HAWAJAZIFANYIA MAFUNZO.

    2. KWANINI NAILAUMU SERIKALI
    MATRAFIKI HAWAFANYI KAZI BALI NI KUKUSANYA PESA TU KWA RAIA ANAYEONEKANA NA KOSA BARABARANI TENA WANAZITIA MFUKONI MWAO HIVYO HAWATOI ELIMU KTK RAIA KUWA WAPI WAENDESHE KASI NA WAPI WAENDESHE POLEPOLE

    3. KAMA MMESHINDWA KUENDESHA NCHI NA WATU WAKE BASI NYINYI WAHUSIKA WOTE MJIUDHURU ACHIENI WENGINE NCHI HIYO SIO KULETA UZEMBE KTK MAISHA YA WATU

    POLENI WAFIWA NIMESIKITIKA SANA

    ReplyDelete
  8. Mdau, OmanMarch 30, 2009

    Mdau, je ni kweli Sheikh Yahya Hussein kafariki au story tu za watu? Maana kama ni kweli, basi huku arabuni watalia sana maana jamaa wanamind ndagu vibaya

    ReplyDelete
  9. Innalillahi waina ilaihi rajiun (Hakika yeye ametangulia nasi huko ndo marejeo yetu) Poleni ndugu zangu, Allah awape moyo wa stahamili katika kipindi hiki kigumu haswa cha msiba wa kushtukiza, kwakweli inauma, poleni ndugu zangu.

    ReplyDelete
  10. Innalillah wa inna illaihy rajiun!!
    Poleni sana ndugu wa marehemu na watanzania wote, kwani tumempoteza mtu mzuri sana!
    Jamani tunaweza kabisa kupunguza ajali Tanzania lakini matatizo ni serikali ambayo haijui jinsi gani ya kuanza kufanya hivyo. Hakuna utaalamu wa kutosha, hakuna rekodi za vyanzo vya ajali n.k. Hili ni janga la taifa, nguvu zote na misaada mingi tunaelekeza kupambana na Ukimwi na Malaria, lakini sijasikia hata siku moja serikali imetenga kiasi kadhaa cha bajeti kupunguza ajali barabarani.
    Tutangojea mpaka lini? Tumepoteza wabunge, ndugu na majamaa!! Jamani tuamkeni!!
    Ninakuja bongo...lazima kieleweke!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...