Buriani. Prof.Ken Edwards (Joshua Mkhululi)

Mungu akulaze pema peponi.
22 January 1945 - 18-March-2009

Wengi wameguswa na msiba huu wa marehemu Prof.Ken Edwards maarufu pia kwa jina la Kaka Joshua Mkhululi,Mwana wa Afrika halisi aliyezaliwa jamaika 22-January 1945 na kufariki Arusha,Tanzania 18-March 2009.

Marehemu Prof Ken Edwards atakumbukwa daima milele kwa mchango wake mkubwa katika jamii ya watanzania na wafrika wenziwe kwa ujumla,kuanzia elimu ya juu mpaka katika maisha ya kawaida ya jamii ya watanzania,ambayo Prof.Ken alijichanganya na kujumuhika.


Prof.Ken Edwards alikuja Tanazania 1976 na kujiunga katika tahasisi ya elimu ya juu kabisa CHUO KIKUU CHA DAR-ES-SALAAM,ikimbukwe katika miaka hiyo ya 1976 nchi hilikuwa katika uhaba mkubwa wa mahitaji ya mwanadamu kama vile vyakula mchele,unga na sukaari ulipatikana madukani kwa foleni! Prof.Ken alikubali kuwa pamoja na watanzania akiamini kabisa kuwa Tanzania na Afrika ni kwao katika ardhi walikotoka mababu zake
miaka 500 hiliyopita,ambao walichukuliwa katika bishara ya utumwa.


Kipindi hicho chote kugumu kwa watanzania prof.ken alishea mda wake kwa kuwa pamoja na watanzania na juhudi zake ziliweza kuanzishwa duka la ushirika la wafanyakazi wa chuo kikuu cha UDSM ambako yeye mwenyewe alikubali kuacha usomi wake! na kusimama dukani pale UDSM na kuhakikisha kuwa kila moja anapata jaapo kilo ya sukari na unga! hili liliwashangaza wengi! Proffessor kushea maisha ya kawaidana watu wa maisha ya chini!

Proffessor Ken Edwards ! Msomi alikuwa pamoja na watu wasio wasomi!
na kula nao Ugali na Mchicha



Prof.Ken Edwards !Mwanamichezo
Prof.Ken akuishia hapo bali alikuwa na moyo wa upendo kwa watanzania na wafrika kwa ujumla ! alitumia mda wake mwingi wa ziada kwa kushiriki kaatika maendeleo ya jamii na alijua wazi KANDANDA ni mchezo unawaunanisha wanadamu wengi bila kujua tofouti zao ziwe za kikabila,dini,koo n.k,linapofikia swala la jamii na michezo Prof:Ken anauweka pembeni usomi na uprofesa wake na anarudi chini kushea na wafrika wenziwe na matunda yake !alianzisha timu ya mpira (Kandanda) ya Vijana wa KUNDUCHI MTONGANI wakati huo Kunduchi hakukuwa na majengo yaliyo sasa bali kulikuwa USWAHILINI,Prof.Ken alikubalika na Vijana na wazee wote wa Kunduchi na kule ni Maarufu kwa jina la Kaka Ken(brother Ken)
au Kaka Mkhululi.

Prof.Ken na UAFRIKA
unapokuja katika swala la uafrika hapa ndipo utagundua kuwa Kaka Ken au Brother Mkhululi Alikuwa ana upendo wa Afrika na kuwapenda wa afrika wenzie zaidi ya wafrika,hapa ndipo palipo mfanya Prof.Ken Edwards kufikia jina la Kaka Joshua Mkhululi,kwani alikuwa anaamini kabisa katika moyo wake wote kuwa kama si biashara haramu ya utumwa iliwafanya babu zake kupelekwa utumwani visiwani Karibeani,yeye angezaliwa Dar,au Arusha,Kama si Kigoma na Dodoma,labda Kilwa,Lindi au Mtwara na Penginepo Mwanza!

Swala hili la UAFRIKA ndilo liliomfanya Kaka Ken au Joshua Mkhululi kuja Tanzania kutumia elimu yake! kuchangia maendeleo katika ARDHI ambayo ni asili yake na aliamini kuwa AFRIKA NI KWAO,kwani ELIMU YAKE ingemweza kufanya kazi na kuishi mahala popote duniani,lakini alikubali KURUDI NYUMBANI,TANZANIA,na Afrika kwa Ujumla.


Mchango wa Prof.Ken kuanzia UDSM kama Proffessor! Kunduchi kama mwanakijiji na Baba Mwanzilishi wa timu ya kandanda ya vijana,Kariakoo kama rafiki na mbwiga wa Ras, ARUSHA kama Mzazi Mwanzilishi wa ESAMI! ambako aliishi na Familia yake Mke na watoto!

Prof.Ken alikuwa mstari wa mbele kwa kuwapa changa moto WASOMI NA WATAALAMU wenye hasili ya Kiafrika ambao wamezaliwa nje ya bara la afrika kurudi nyumbani kuja kuchangia maendeleo ya ardhi waliotoka mababu zao AFRIKA.

Mwisho Kabisa tunatoa pole kwa familia ya marehemu Prof.Ken Edwards pamoja na wote walioguswa na msiba huu. Maelezo ya hapo juu yanatambulisha mchache aliyochangia Prof.Ken Edwards katika maisha ya kawaida lakini yapo mengi.
Kuanzia Arusha,Dar-Es-Salaam,Tanzania.
Accra,Ghana,Mbabane,Swaziland na kungineko.
Ukalale Pema Peponi Prof.Keneth Edwards aka Joshua Mkhululi,Ulizaliwa Ugenini Jamaika umefia Nyumbani ,Arusha ,Tanzania,Afrika.Wewe ni shujaa na Mwafrika wa kweli uliyejitoa muhanga kwa kuchangia elimu yako na usomi na utalaamu wako wa Afrika Upendo wako kwa bara hili la Afrika! utakuwepo
Daima Milele na Milele
JAH RASTAFARI!

NB:
Shukurani Kaka Makunja kwa picha na machache

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Hi!hiii!
    jamani kumbe baba wa watu prof.ken
    kafanya mengi hadi kwa walala hoi!inasikitisha sana kuona mtu muhimu kama huyu alinyimwa uraia!
    na watu mafisadi wasiokubali kujichanganya na wabongo wanapewa uraia na matokea yake waujumu uchumi wa taifa????????????????

    ReplyDelete
  2. te!te! kumbe prof.Ken alijichanganya ki sawa sawa!
    maelezo ya hapo juu yanaonyesha kuwa alikuwa mtu mwenye upendo na kujikubali kuwa yeye ni mmatumbi aliyezaliwa jamaika na karudi kwao bongo!
    tena inaonekana kwa kiasi kikubwa mchango wake haukuwa kwa matawi ya juu ya wasomi wenziwe tu,bali baada ya kazi alijichanganya katika jamii ya wafrika wenziwe
    sasa vipi?tena mtu kama huyu alinyimwa uraia ???? na kuna watu hata uswahilini hawautaki wala kujichanganya hawataki!
    istoshe pengine hata kiswahili awajui lakini baada ya miaka sita kuishi bongo tayari nao raia???

    ReplyDelete
  3. ah! kumbe marehem! alikuwa mtu wa watu!sio mtu wa kila jioni kuwa katika viwanja vikubwa ?bali alikuwa na walala hoi?
    naona maelezo ya hapo juu yanamchambua alikuwa mtu wa aina gani?
    Sasa hapa kulikuwa na kikwazo gani kuhusu uraia wa tanzania?

    ReplyDelete
  4. jamani! wanaharakati wanajuana,
    huu kweli msiba mzito,naoa hiyo picha ni alipokuwa bado kijana kijana,kweli picha ni kumbu kumbu.
    kaka bwana Kichwa Ngumu aka kaka brother Makunja,shukurani kwa kushea picha ya marehemu na jamii

    ReplyDelete
  5. sikuwa nimemfahamu kabla mpaka pale nilipopewa habari za kifo chake kutoka kwa Baba T Rasta wa kweli wa East Africa tv,
    inasikitisha kuona majabali yakianguka bila kupewa hadhi yaliyostahili halafu hadhi inabaki kwa manyang'au yasiyo hata na haya,hivi tujiulize ni bora kuwa na raia fisadi?nyang'au?fisimaji?kibaraka?

    amefanya aliyostahiki kufanya duniani,

    apumzike kwa amani!

    ReplyDelete
  6. watanzania bado tupo usingizini,
    kwa kutujua nani? muhimu kwetu,
    mtu kama huyu marehemu Prof.Ken yaani taifa alikujua kabisa limepata bahati ua zawadi,matokeo yake heti uraia ananyimwa! na mafisadi wanapewa.inawezekana hata baadhi ya wasomi walipita mikononi mwake ambao sasa wapo katika nafasi za juu nao walikuwa vipofi wa kutokujali masilai ya taifa badala yake wanatoa uraia kwa mafisadi

    ReplyDelete
  7. ,We mkuu wa wilaya vp wewe
    Kwani kula ugali na mchicha ndio umaskini hebu jiamini wewe katika nchi yako na jivunie kile kilicho asili nyumbani kwako mchicha ,ugali ndio vyakula asili kwa tanzania na afrika mashariki huwezi kwenda ujerumani au cuba ukakuta watu wanakula mchichi hii ni kwasababu aupatikani kule na sio moja ya asili ya vyakula vyao ni sawa na huku pia huwezi kukuta watu wanakula nodless au yum kwasababu si vyakula vya hapa na si asili yake
    so next time unapondika hapa na watu wasome jaribu kuwa makini kidogo mambo mengine ni lack of confidence michuzi
    eti msomi alikuwa akijichanganya na walalahoi kula ugali na mchicha kwani kuna nyumba gani au familia gani ya kitanzania ambayo hawali kabisa ugali wala mchicha
    kuwa smart mdau proud of what u have got in your country
    ni hayo tu maoni yangu vyovyote huyakubali au usiyakubali lakini ujumbe nimekufikishia hata usipoiweka hii comment lakini powa kwa wewe mlengwa imeshakufikia
    mdau wa ukweli
    Stoke,Ukerewe

    ReplyDelete
  8. NAICHUKIA TANZANIA

    ReplyDelete
  9. Serikali ya tanzania imemuua huyu, kwasababu ilimnyima passport na akashindwa kwenda kutibiwa nje. Labda vyanzo vya kuaminika vitupe maelezo tofauti na niliyosoma hapa kwa michuzi, hivi ndivyo mimi ninavyoelewa.

    ReplyDelete
  10. Sasa huo ndio uwe mfano wa kuigwa, sio mkimuona mtu ana rasta , basi mtampa sifa zote mbaya,mvuta bangi,kichaa, chizi, ajasoma.
    Usichague kitabu kwa kuangalia ukurasa wa mbele, soma kwanza ujue kama kina story nzuri.
    Prof. Eward alikua rasta na anasifa zote za usomi.watanzania acheni kasuba zenu.
    Tutakua na wewe daima,

    ReplyDelete
  11. He's a great man, no doubt, Ras Josh. Last of a dying (if not already long dead) breed! Nakumbuka nilikuwa nikimwona sana miaka ya 80s akikatiza mitaani ya Posta Dar kwenye jua kali la saa 8 wakati nikitoka shule. Alikuwa akipenda sana kuvinjari sehemu za YMCA. Ras Josh na Ras Kwutenge Sokoni enzi hizo walikuwa major figures na kuheshimika sana kwenye rasta community Tanzania nzima.

    ReplyDelete
  12. "marehemu alikuwa mtu mzuri sana". mie sifa zangu nazitaka sasa hivi.

    ReplyDelete
  13. Hi mich

    mazisha ya prof ndio yamepita tayari, maziko yalifanyika majira ya saa tisa na nusu mchana. kabla ya mazishi ulitolewa wasifu mbalimbali wa kuenzi kazi alizofanya professor mkululi. kati ya waliotoa wasifu ni pamoja na dean wa kitivo cika hutuba cha biashara mlimani (udsm)mama huyu hakupendezea katika hotuba yake kwa kile alichoonyesha kwenda kukosoa hutuba ya mtoto wa marehemu aliyotoa na kuanza kurekebisha hata na wale waliotangulia kuongea hakupendeza na alionyesha kukera watu wengi mno na pia alionyesha matambo yasiyokuwa na msingi kwa kutafsiri zaidi ni kama vile alitamani yeye ndio angekuwa dean wa kwanza kitivo cha biashara any way tumalize ya huyu bi mkubwa kwa sasa na aliyeonekana kuvutia na kuongea maneno ya busara ni mhs. Reginald Mengi, ambaye aliongea maneno mafupi na ya faraja kwa wafiwa alisema kama mtu amekuazima ngo'mbe wake wa maziwa ukaa naye kwa muda wote unaetaka wewe, mtu yule akaja kuchukua ngo'mbe wake utachukia?? akautafsiri mfano huu kwa kusema kama mungu amewapa professor kwa miaka 64, leo akaamua kumchukua basi msilalamike sana, kwa kweli maneno haya yalileta faraja kubwa mno kwa wafiwa pamoja na waliokwenda kuzika baada ya hotuba hii zilifuata hotuba nyingine ikiwemo ya Baba mkwe wa professor ambae aliomba na kuasa kwa kuwa prof ameifanyia Tanzania mambo yaliyomengi mazuri basi anaomba mashirika yote ambayo ameyafanyia kazi yawajali watoto wa marehamu pamoja na kuwaendeleza kielemu. Kumalizika kwa hotuba hizi kulifuatiwa na kile kichokua kizikto zaidi ambacho ni kuuaga ni mwili wa marehemu, kabla ya kuuaga mwili huu ilifanyika sala nzito ya imanai ya kirasta, sala hii iliongozwa na orhodox priest ambaye ilibidi afuatwe Nairobi kutokana na kutokuwepo na priest huyu wa ki orthodox hapa nchini, ulikuwa ni wakati mzuri sana kuweza kujifunza mambo mengine yanavyokwenda. Ilikuwa sala nzuri na yenye hisia nzito na kwa mbali kulikuwa na midundo ya ngoma. kulikuwa na huzuni lakini huzuni zote zilipoozwa na hali ya ushwari ilionyeshwa ulionyeshw na marastafari. Kwa kweli msiba huu uliudhuriwa na watu very sensible hapakuwa na watu wasenegnyaji na wasio na imani na hata wasengenyaji wangekuwepo wangeongea nini cha ajabu kuhusu profesa zaidi ya kujifunza na kukubali mchango wake mkubwa.kiuhalali kilikuwa kilio na somo kwa wakati mmoja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...