TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UGONJWA WA MAFUA YA NGURUWE

(SWINE INFLUENZA/FLU) 
 
 

Utangulizi 

Mafua ya Nguruwe ni ugonjwa wa njia ya hewa kwa nguruwe unaosababishwa na virusi (type A influenza viruses) ambavyo mara nyingi husababisha mlipuko wa ugonjwa huo kwa nguruwe

Kwa kawaida watu hawapati ugonjwa huo wa mafua ya nguruwe lakini maambukizi kwa binadamu huwa yanatokea. Hata hivyo ilishawahi kuripotiwa kuwepo kwa maambukizi kwa binadamu kati ya mtu na mtu. 

Nchi ambazo ugonjwa huu umeripotiwa 

Kuanzia mwezi Machi mwaka huu hadi sasa, nchi 8 zilizotoa ripoti ya ugonjwa huu kama ifuatavyo:

Mexico – wagonjwa 1,614 (suspected and confirmed) na vifo 106; Marekani – wagonjwa 20 (confirmed); Canada  - wagonjwa 6; New Zealand – wagonjwa 13 (suspected); Spain – wagonjwa 7 (suspected); France – mgonjwa 1 (suspected); Israel – mgonjwa 1 (suspected); na Brazil – mgonjwa 1 (suspected). 
 
 
 

Mafua ya Nguruwe yanavyoambukizwa 

Katika wanyama, kati ya nguruwe na nguruwe ugonjwa huo unaambukiza kwa wanyama kuwa karibu na pia kugusana na kitu chenye virusi vya ugonjwa huo.

Aidha ugonjwa huo unaweza kuambukiza kati ya nguruwe kwa nguruwe, nguruwe kwa binadamu, binadamu kwa nguruwe, na binadamu kwa binadamu. 

Dalili za ugonjwa huu kwa binadamu 

Dalili za ugonjwa wa mafua ya nguruwe kwa binadamu ni sawa na dalili za mafua ya kawaida kwa binadamu pamoja na homa, kukohoa, maumivu ya koo, kukosa hamu ya chakula, maumivu ya mwili, kuumwa kichwa, kutetemeka baridi na mwili kuchoka. Kwa baadhi ya watu huharisha na kutapika. Aidha wagonjwa wengine huzidiwa na kupata vichomi (pneumonia), kushindwa kupumua na kusababisha kifo. 

Dalili za ugonjwa huu kwa nguruwe 

Dalili za ugonjwa kwa nguruwe ni kama ifuatavyo: Homa ya ghafla, mfadhaiko/kuzubaa, kukohoa, mafua, kupiga chafya, kupumua kwa shida, macho kuwa mekundu, na kukataa kula. 

Jinsi virusi vya mafua ya nguruwe vinavyoenea kwa binadamu  

Ugonjwa unaweza kuambukiza kati nguruwe na bindamu kwa kuwa karibu au kumgusa nguruwe mwenye ugonjwa.

Virusi huenea kutoka kwa mtu kwenda kwa mwingine kwa njia ya hewa kwa kukohoa na kupiga chafya; kugusa kitu chenye virusi hivyo na kujigusa mdomo au pua.

Mtu mwenye ugonjwa huo anaweza kuambukiza wengine siku moja kabla ya dalili za ugonjwa kujitokeza hadi siku saba (7) au zaidi baada ya kuwa mgonjwa. Kwa hiyo mtu anaweza kumwambukiza mwingine kabla ya yeye kujua kama anaumwa na wakati akiwa mgonjwa 

Je unaweza kupata ugonjwa wa mafua ya nguruwe kwa kula nyama ya nguruwe? 

Huwezi kupata ugonjwa wa mafua ya nguruwe kwa kula nyama ya nguruwe iliyotayarishwa na kupikwa vizuri (nyuzo joto 100 centigrade). Hata hivyo inatakiwa kuchukua tahadhari wakati wa maandalizi kabla nyama haijapikwa. 

Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa mafua ya nguruwe 

  • Kitu muhimu cha kwanza ni Kunawa mikono vizuri kwa sabuni na maji mara kwa mara
  • Kuepuka kuwa karibu na watu wanaonekana kuwa na dalili za ugonjwa huo
  • Zuia mdomo na pua kwa kitambaa au karatasi laini wakati unapokohoa au kupiga chafya
  • Kuepuka kushika macho, pua na mdomo
  • Kufuata kanuni za afya bora kwa mfano kufanya mazoezi ya viungo, kupumzika vizuri, kula chakula bora, n.k.

Jinsi ya kutambua na kuthibitisha ugonjwa wa mafua ya nguruwe 

Baada ya mtu kuhisihiwa kuwa na ugonjwa, sampuli huweza kuchukuliwa na kuthibitisha katika maabara maalumu. Hapa nchini maabara hiyo ipo katika jengo la Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR/National Influenza Centre).

Tanzania tumejenga uwezo wa kuyatambua  magonjwa kama haya hapa nchini baada ya kuwepo maabara za kisasa za kufanyia uchunguzi. 
 

Tiba ya ugonjwa huu 

Ugonjwa wa mafua ya nguruwe unatibika na kuzuia kwa dawa aina ya Tamiflu au Zanamivir. Hakuna chanjo kwa binadamu. 

Tunawasiliana na Shirika la Afya Duniani hapa nchini ili tuweze kupata dawa za kudhibiti ugonjwa huu. 

Hatua zinazochukuliwa na Wizara 

  • Kutekeleza  mikakati ya kuimarisha ufuatiliaji hasa katika viwanja vya ndege na vituo vya mipakani
  • Kushirikisha wadau husika katika kuchukua tahadhari pamoja na kuzuia kuingia kwa ugonjwa
  • Kuwasiliana na mikoa pamoja na wilaya kuchukua tahadhari
  • Vifaa kinga vipo vya kutosha kwa makundi maalumu ambayo yatahusika kwa karibu iwapo ugonjwa unatokea
 

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii

Tarehe 28 Aprili 2009

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 77 mpaka sasa

  1. Jinsi mnyama huyu anavyoleta balaa. Huyu alitakiwa atumiwe kufukuzia pepo tuu siyo vinginevyo.

    ReplyDelete
  2. Hata kama nyama pikwa haisababishi ugonjwa kwa sababu ya wadudu kufa, kumbuka wadudu huenea wakati wa kuiandaa ikiwa mbichi na ni vigumu kuhakikisha kila mtu aliyeshika nyama gonjwa mbichi amenawa dawa vizuri. Ndipo hapo gonjwa hupata upenyo.

    Ukishika nyama na ukashika sehemu nyengine hata kama si mwili, ukajiosha, kisha ukashika baadaye uananasa.

    Cha msingi wakati huu wa mlipuko watu wakae mbali na mdudu huyu, wale ng'ombe, mbuzi, na kuku nk. vinatosha.

    ReplyDelete
  3. Huu usawa unalazimishwa na asili.

    ReplyDelete
  4. Mmelitambua sasa, kuwa hii mboga huwa inavirusi vibaya,sasa bora kuwateketeza wote, ili tunusurike pia tusivae matambara mdomoni alooo. kila allah alilolikataza lina hekma yake.

    ReplyDelete
  5. Na kitimoto ipigwe stop sasa!!! Watu wataandamana, weeeeeee!! Sio kama DECI!

    ReplyDelete
  6. Hatutarajii komenti za kidini

    ReplyDelete
  7. Watu wakiambiwa nguruwe haramu eti ooohhhhh, hamjui utamu wake. OK sasa tutaona. nguruwe wote watachommwa moto. Sipati picha siku Bongo kitimoto ikipigwa stop! Hivi nyie wachaga mtaishije??

    ReplyDelete
  8. kujikinga..nilidhani wangesema hakuna kula kiti moto..white paper!
    kalini sijaona..kwa iyo ndio kusema wana maana gani??

    ReplyDelete
  9. Nchi za asia ziliuwa kuku, bata, njiwa, kanga, ili kutokomeza konjwa la mafua ya ndege. Sasa hivi itakuwaje?

    ReplyDelete
  10. Ubaya wa nguruwe umetokana na dini. Na ubaya wa kila jambo umetokana na dini. Hivyo si vizuri kupuuza dini hata kama huamini.

    Uzuri, huyu nguruwe aliharamishwa tangu agano la kale (mambo ya walawi 11:3-8), Yesu alifukuza pepo wawaendee nguruwe (ikionyesha ubaya), Kurani imekataza pia (kama agano la kale).

    ReplyDelete
  11. Ukiacha kufuata amri za Mungu, atakulazimisha kwa hekima uzifuate. kakataza mdudu asiliwe, mmekula, katia ugonjwa.

    Kimsingi amri ingetiiwa huu ugonjwa usingekuwepo katu/kamwe.

    ReplyDelete
  12. NautiakasiApril 28, 2009

    Hivi tayari Tanzania mshafanikiwa kupata treatment ya virus??!!!!

    Ha ha ha.. hiki kiumbe hakitibiki mtu wangu! Kinachofabyika hapo ni ku "suppress viral replication" tu.

    ReplyDelete
  13. ukisali kabla ya kula huumwi hata kama mdudu ana virusi.

    ReplyDelete
  14. LAKINIBIBLIA,IMEKATAA.TUKUBALIKUWATUMEKIUKAMAAGIZOYAMUNGU,UZURIALISHATUTAJIAWANYAMAWAKULA IWEJESISI TUVUKEMPAKA? KUSALI HAISAIDII. CHAMSINGITUTII,TULICHOAMBIWA.

    ReplyDelete
  15. wabongo mna-comment za kidini.Sababu eti ni nguruwe.Ingekuwa kuku mngesema Kuku kalaaniwa ndio maana haruki.
    Swine itapita na nguruwe wataendelea kuliwa tu.Hivi vigonjwa vya ajabu vinatokea sana huku majuu na vitapatiwa ufumbuzi .Juzi juzi mboga za majani zimeathirika,Nyama ya ng'ombe iliathirika lakini sasa tunaendelea kula.Msijali sana.Ufumbuzi wa SWINE upo mbioni kupatikana.Chukueni tahadhari tu.

    ReplyDelete
  16. Kazi nzuri sana kwa Serikali kutoa hili tangazo mapema. Nadhani pia tangazo kama hili litapatikana katika vyombo vingine vya habari kama vile magazeti, redio, televisheni nk.
    Sitarajii watu watakao kwenda kinyume na onyo hili warudi wailalamikie serikali. Umefika wakati kila mtu awajibike kwa maamuzi na vitendo vyake mwenyewe, hapo Tanzania itapiga hatua muhimu katika kuelekea kwenye maendeleo.

    ReplyDelete
  17. Mdudu ameingia luba..kitimoto imeingia balaa watu bongo tutatafutana wakipiga marufuku hii kitimoto. Mdudu kaingiaje kwenye kokwa la embe?

    ReplyDelete
  18. anonn wa kwanza kumbuka nguruwe hafukuzi pepo kwa sababu yesu alipokemea wale mapepo yalikuwa yakimtesa yule jamaa yalipomtoka yaliwaingia nguruwe na ndio maana nguruwe anakula chochote kinachokuja mbele yake akiwa anazaa anageuka anakula usipomuwahi unaweza kukuta watoto wote kawamaliza.michu usinibanie asante

    ReplyDelete
  19. ASILI YA UGONJWA HUU HAPO ZAMANI ULITOKANA NA AU ULITOKA KWA WANYAMA AKIWEPO NGURUWE, WANYAMA WOTE WANAWEZA KUWA NA UGONJWA HUU, NI NCHI ZA ULAYA WAKATI HUU MIFUGO YAO MINGI ILIKUWA NGURUWE NDO MAANA WAKAITA MAFUA YA SWINE, NA NDICHO KILIKUWA CHAKULA CHAO KIKUBWA WAKATI HUO, SO NI UGONJWA ILIOANZIA KWA WANYAMA WAKIWEMO NGURUWE. SO BE CAREFULLY WITH THE CHANZO CHA JINA, MNYAMA YOYOTE ANAWEZA KUWA NAO. NA HUU MLIPUKO WA SASA WALA HAUKUTOKANA NA NGURUWE DIRECT. 1918 ULIKUMBA DUNIA NA WAKATI HUO HAKUKUWA NA DAWA, UNITED KINGDOM TU WATU ZAIDI ELFU THELATHINI WALIKUFA, ULIKUJA TENA 1968, UNATIBIKA KIARAHISI KABISA, HASA KWA NCHI HIZI ZA KITAJIRI, AFRIKA TUTAKUFA KAMA UTAKUJA KWA VILE HATUNA MAPESA YA KUNUNULIA DAWA NA WATAALAMU WA KUTOSHA. SO MUSIANZE KUCHANGA UGONJWA NA ULAJI WA NGURUWE.

    ReplyDelete
  20. Sisi tupo Toronto Canada na hatujasikia ugonjwa huu ukiusishwa na kula au kushika nyama ya nguruwe.
    Hii ni aina ya mafua/flu na imeanzia Mexico na kinachosambaa ni mafua hayo; mafua kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine japo yatakuwa yameanzia kwa nguruwe huko Mexico.

    Mafua ya nguruwe kwa kawaida hayaambukizwi kwa watu lakini virusi hivi vimebadilika/mutate kuweza kuingia kwa binadamu na hilo ndilo tatizo lililopo sasa hivi. Nguruwe wengine hawana mafua hayo yaliyoanzia Mexico.

    Tuwe wailewa kama tunavyoeleweshwa na wataalamu (though I am not one of them).

    JJK.

    ReplyDelete
  21. allah ameharamisha maiti yaani mzoga,damu na nyama ya nguruwe tukitaka tusitake hilo halipingiki.

    ReplyDelete
  22. We anon wa April 28, 2009 10:46 PM, kwa nini sasa tule midudu ina mipepo? mpaka leo? mi naoona anon wa mwanzo kafata mafunzo hasa.

    ReplyDelete
  23. Mbigiri;
    imekuuma nini? soma komenti za April 28, 2009 9:17 PM.

    kwani huu ugonjwa ni mara ya kwanza kutokea?

    Mbona kimwi husemi? si zinaa imekatazwaa?

    ReplyDelete
  24. Kumbukeni zile sala "wi aski yu tu blesi ze fudi so zati iti naurishezi awa badiz" Eemen. kabla ya kula.

    Hata kama mdudu ana vidudu vinakufa nyenyewe.

    Maombi huku unapinga maelekezo au kutii maelekezo huku unasali kipi bora sahihi kwa MUNGU?

    ReplyDelete
  25. kama sala zingekuwa zinauwa wadudu wa ugonjwa basi tungesali na kuendelea na zinaa wala ukimwi usingetupata.

    Au tunakubali kwa ukimwi tuu kwa mafua ya chamoto tunaganga?

    ReplyDelete
  26. Kuteketeza na kuangamiza wadudu hawa ndo dawa ili tusiishe na upungufu wa kinga za mafua ya nguluwe.

    ReplyDelete
  27. Mbigiri sikilizia uchungu mwanangu!!

    ReplyDelete
  28. Kuanzia leo naanza kutibu watu wenye pepo kwa kutumia nguruwe. Nikimsogeza tuu pepo woote wanamvaa halafu mtu anakuwa huru. au siyo anon wa April 28, 2009 10:46 PM.

    ReplyDelete
  29. We anon wa April 28, 2009 10:46 PM, unamaanisha nguruwe ni vichaa?

    ReplyDelete
  30. Wkenya kudadeki watayaleta Tanzania makusudi kama hamuamini mtaona.Maana hawa jamaa sijui wana nini yaani watu wa ajabu sana.Lakini hii ni tahadhali tu au ndio tayari amesha patikana yoyote mwenye nayo.Je wafugaji wa nguruwe?

    ReplyDelete
  31. Kivumbi kiko Bongo na Tamiflu za China!!!

    ReplyDelete
  32. Unajua sisi binadamu tunajiangamiza wenyewe, wakati mwingine kwa makusudi,kwenye mavakula, sigara ,pombe. Tunaambiwa nyama kama ya nguruwe ina mafuta mengi, hata kabla ya huo ugonjwa, lakini watu wengine kila siku anaila,tena wengine kiushabiki tu na anaponunulia hana uhakika na upikaji wake.
    Haya sasa gonjwa hilo, watu wanasema ajali kazini, sawa,kama ingekuwa inamuathiri yeye mwenyewe tungesema hewala, lakini inamgusa aliyekuwepo na asiyekuwepo!

    ReplyDelete
  33. acheni udini swine flu blah blah blah na bird flu ni nini? Hata kuna cow mad decease nayo je? ACHENI UDINI

    ReplyDelete
  34. MAGARI YA BONGO YANA LAHANA YANACHINJA WATU KILA SIKU TUACHE KUYATUMIA.

    ReplyDelete
  35. udini eeeeeh!!!

    ivi kipindi kile cha kuto---la (mfun--o) mbona kitomoto hakuzi wateja wanapungua????
    hii nyama safi saaaana na tutakula adi kieleweke,naungana na annons apo;cow-madness,birds flu mbona hamkuita HARAMU SIJUI KITU GANI!!mbona adi leo mwala??watu na raha zetu mafua yataisha na k/moto italiwa kwa kwenda mbele...
    wee unaesema imekatazwa wapi??soma maandiko petro aliposhushiwa mfano wa SHUKA KUUUBWA NA NDANI KUNA KILA AINA YA MNYAMA MWENYE KWATO ASIYE NAZO,MWENYE KUCHEUA,ASIYECHEUA AKAAMBIWA CHINJA ULE,AKASEMA VIMELAANIWA,AKAAMBIWA KILICHOTAKASWA NA MUNGU USISEME HARAMU"

    ni hayo michu bana hii sasa,watu mna udini sana utafikiri mnatekeleza basi iyo dini
    hahahahaaaaaa

    ReplyDelete
  36. Michu...mbona huwaambii wadau watembelee tovuti ya www.harusiyangu.com? Kuna kipande cha forum humo ndani yaani wabongo wanayaweka matatizo ya ndoa kikweli kweli..cheki hii...http://www.harusiyangu.com/forumview.php

    ReplyDelete
  37. Ajabu ni kwamba wote wanaosema haramu ndio hao hao walaji kwa siri. tunawafahamu sana bia na kiti moto kwa kwenda mbele na wanasehemu zao mahali vitu hivyo vinapopatikana. Pia ugonjwa wa nguruwe si kitu cha ajabu TZ miaka michache ulikuja na ukaisha. Magonjwa ya wanyama yako mengi tu kama alivyisema anony mmoja hpo juu lakin watu wengine wanang'nga'ania udin tu. Ati dini imezuia mbona unakula ng'ombe wakati kwa wahindi dini imezuia?

    ReplyDelete
  38. Habari za kuaminika na UK tuna wagonja kama 5, na sasaivi mmoja yupo birmingham na mwingine london wametoka na virus zao mexico. haya je nchini tz wamejiandaaje na kukabiliana nalo??? pse wizara husika ziwe makini hasa na wageni waingiao nchini.
    hapa UK tunashukuru they re very much considerable and hope they gonna tackle the problem soon.
    xx
    nou vag

    ReplyDelete
  39. Mbona Kitimoto inatibu ukimwi. Kuleni tu mbuzi katoliki ni poa tu.

    ReplyDelete
  40. Anayelalamikia udini ndo mdini hasa, kajuaje kama ni udini, yaani watu wasitoe mawazo yao?

    We kama unataka kula mi-mbuzi hiyo iliyokataliwa tangu wakati wa kutoka endelea kivyako. Siyo kutafuta sapoti kutoka kwa watu wasio kula.

    ReplyDelete
  41. We anon wa April 29, 2009 9:58 AM, ukiona mistari miwili katika biblia inapingana katika jambo moja basi ujue mstari mmojawapo haujatoka kwa Mungu. Mungu hajipingi mwenyewe.

    Watu wanaweza kuamini mstari wa zamani zaidi kwa sababu wayahudi wamefanya kazi nzuri kutunza agano.

    Ndo maana hata wasabato wanafata amri hizo.

    ReplyDelete
  42. Ndio, wadini ni hawa wafuatao: watu wasiokunywa pombe, wasiokula nguruwe, wasiozini, n.k. na kuwakataza watu kufanya hivyo.

    Sidhani kama watu hawa ni adui za Mungu.

    ReplyDelete
  43. Yaani watu wawaita wenzo wadini kwa sababu tu hawajawapa sapoti ya kula cheafaya.

    Duniani kuna mambo.

    ReplyDelete
  44. Kama wewe si mdini basi mshetani. vipi hiyo.

    ReplyDelete
  45. hii ni kutoka CNN wanasema kwamba kwa nchi kubwa kama Marekani na uingereza na nyinginezo,chati ifuatayo inaonyesha asilimia ya wakazi ambao wanaweza kutibiwa na madawa yaliyopo katika bohari ya nchi husika.

    (1)Marekani -25%
    (2)Uingereza - 50 %
    (3)Japan -10%
    (4)India - 0.25 % ikumbukwe india ina wakaazi kama bilioni 1 hivi.Sasa asilimia 0.25*1 bilioni= ?

    (5)China - 12 %

    Naishia hapo.Sasa huku Africa sijui kwa sababu nchi ambayo kidogo inajiweza ni Egypt(Misri).

    Tuombe tu isifike huku kwa sababu huko Magerezani,kwenye daladala,mashuleni.sijui itakuaje.

    Mungu ibariki Tz pia Africa.Amen

    ReplyDelete
  46. MICHUZI RUSHA HII USIBINYE HATA KIDOGO ILI WATANZANIA WENZANGU WAZALENDO WAAMKE!MAANA UFISADI TANZANIA UMEZIDI WATU WANATUMIA VYOMBO VYAO VYA HABARI KTK KUTETEA UFISADI WAO.
    ONENI MENGI NA MAFISADI WENZIE WA KIHINDI WANAVYOILA NCHI.
    MICHUZI KAMA NA WEWE SIO KIBARAKA WA MENGI NA HAO WAHINDI UTAIRUSHA HII.
    UKIIBINYIA JUA ATAKAEKUJA KULIPA UTUMBO WAKO NI MTOTO WAKO NA SIO WATOTO WA MENGI NA HAO WAHINDI.

    MAWAZIRI wawili, Sophia Simba na George Mkuchika jana walimshambulia mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi ambaye wiki iliyopita alitangaza majina ya wafanyabiashara watano wenye asili ya Kiasia, akisema ni mafisadi waliokubuhu.

    Simba, ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) na Mkuchika, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo walisema mfanyabiashara huyo wa jijini Dar es salaam "amechemsha".

    Mengi alitangaza majina ya wafanyabiashara hao Alhamisi iliyopita akisema ni kati ya watu wasiozidi 10 ambao alidai wanaifilisi nchi na kutaka wadhibitiwe mapema kabla hawajaitingisha na kuiyumbisha nchi.

    Hata hivyo, Mengi, ambaye alidai katika taarifa yake kuwa juhudi za Rais Jakaya Kikwete zinakwamishwa na watu hao, hakueleza jinsi watano hao wanavyoitafuna nchi zaidi ya kusema kuwa wanatorosha fedha wanazozipata 'kifisadi'.

    Jana, kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam mawaziri hao wawili walitoa kauli za kumshambulia mwenyekiti huyo mtendaji wa makampuni ya IPP, kauli ambazo zinadokeza mtazamo wa serikali katika mjadala unaoendelea wa vita dhidi ya ufisadi na vinara wake.

    Waziri Simba, ambaye wizara yake pia inawajibika katika vita dhidi ya ufisadi, alisema: "Kakosea... watoto wa mjini wanasema kachemsha."

    Simba alitoa msimamo huo jijini Dar es Salaam jana muda mfupi baada ya kufungua semina ya wadau wa vyama vya siasa kuhusu namna ya kuiboresha Sheria ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995.

    Simba alisema Mengi hana mamlaka hayo ya kutaja watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

    Kabla ya kujibu swali kuhusu kitendo cha Mengi, ambaye anamiliki televisheni ya ITV na kituo cha redio cha Radio One Stereo, kutaja majina ya watu hao aliowaita mafisadi papa, Simba alihoji: " Hapa kuna mtu wa ITV?."

    Baadaye alisema: "Sikilizeni, kwanza kitendo alichokifanya Mengi si sahihi, kakosea hawezi kuhukumu watu, mamlaka hayo anatoa wapi?"

    Simba, alisema Mengi amekosea kwa kuwa baadhi ya watu aliowataja wana kesi mahakamani.

    "Anahukumu watu," alisema. "Kuna mtu kama Jeetu (Patel) ana kesi mahakamani (EPA), sasa unapokuja kusema ni fisadi wakati mahakama haijathibitisha, unakuwa na maana gani.

    "Kwanza kwanini awatuhumu wafanyabiashara wenzake tu, ina maana si ana nia mbaya nao."Alisema Mengi amechukua uamuzi huo kama vile serikali, wakati serikali ipo siku zote na imekuwa ikifanya kazi zake kwa umakini kwa kufuata misingi ya sheria.

    "Serikali ipo na inafanya kazi kwa misingi ya sheria, sasa yeye kukaa na kutangaza watu nasema si sahihi kabisa. Mahakama pekee ndiyo inaweza kumtia mtu hatiani, lakini huwezi kuhukumu watu kama hakuna mamlaka."

    Waziri Simba, ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), alisema Mengi hapaswi kutumia vyombo vyake vibaya.

    "Asitumie vyombo vyake kufanya atakavyo yeye. Huwezi kukaa katika chombo chako na kuanza kuhukumu watu. Kila mtu akifanya hivyo itakuaje," alihoji.

    Akiongea na Mwananchi baada ya kupata taarifa za kauli ya Simba, Mengi alisema: "Namuombea kwa Mwenyezi Mungu na kwa maskini wa Tanzania ili wamsamehe kwa sababu hajui anenalo."Mengi hakutaka kuzungumza zaidi kuhusu hatua hiyo ya Mama Simba.

    Naye Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika aliwaambia waandishi wa habari kuwa serikali itamchukulia hatua za kisheria Mengi iwapo itabainika alikiuka taratibu na kanuni za nchi kwa kutangaza majina ya watu anaowatuhumu kwa ufisadi.

    Mkuchika alisema jijini Dar es Salaam jana kwa sasa serikali inafanya uchunguzi juu ya suala hilo na itatumia mikanda ya video pamoja na maelezo ya kimaandishi aliyoyatoa Mengi siku alipokutana na waandishi wa habari.

    "Tumekusudia kupata ule mkanda wa video, pia tusome maelezo yake ya kimaandishi... tukigundua kuna mahala ambapo sheria haikuzingatiwa, (Mengi) atachukuliwa hatua," alisema Mkuchika.

    Mkuchika alisema serikali imepokea malalamiko mengi kutoka kwa watu wengi, wakishutumu hatua iliyochukuliwa na Mengi, ambaye pia anamiliki viwanda vya vinywaji.

    Bila kutaka kuwataja majina, Mkuchika alisema miongoni mwa walalamikaji, wapo walioeleza kuwa vyombo vya habari vya mfanyabiashara huyo havikuwatendea haki watuhumiwa waliotajwa kuwa ni mafisadi wakuu.

    Alisema ni kutokana na vyombo hivyo kuwataja majina watuhumiwa bila ya kuwapa fursa ya kujibu madai dhidi yao.

    Waziri Mkuchika alipotakiwa kueleza siku ambayo uchunguzi huo utakamilika, alijibu wananchi wanapaswa kuwa watulivu kwa sababu serikali ikimaliza kuchunguza, itawatangazia yale waliyobaini.

    Hii ni mara ya pili katika kipindi cha miezi takribani mitatu kwa Mengi kuingia katika mvutano na serikali baada ya kuvutana mapema mwaka huu na Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha kutokana na kutangaza kuwa kuna mipango ya kumfilisi na kumuua.

    Mengi pia amewahi kujikuta katika malumbano na watendaji wa serikali hasa na waziri wa zamani wa nchi, ofisi ya rais (utawala bora), Wilson Masilingi alipotoa tuhuma kuwa suala la utoaji zabuni ya ununuzi wa hoteli ya Kilimanjaro, hivi sasa inajulikana kama Kilimanjaro Kempiski, kulikuwa na kitu alichokiita "mchezo mchafu".

    Suala hilo liliamsha malumbano makali, lakini liliishia hewani.

    Katika tuhuma za wiki iliyopita, Mengi aliwahusisha wafanyabiashara hao watano na kashfa za wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), utoaji zabuni ya ufuaji umeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond Development (LLC) na uuzwaji wa jengo la Mfuko wa Hifadhi ya Taifa ya Jamii (NSSF).

    Mengi, ambaye kituo chake cha televisheni cha ITV kiliwahi kuendesha mchezo mkubwa wa bahati nasibu ya Jackpot Bingo, pia aliitaja Bahati Nasibu kuwa katika tuhuma hizo, pamoja na mradi wa makaa ya mawe wa Mchuchume.

    maoni juu ya mengi:

    mengi kwa muda mrefu amekua akisifika kwa kupenda bifu na watu ambao wanaonekana kutishia maslahi yake binafsi na sio ya taifa.recodi zipo amekua akitumia
    vyombo vyake na kivuli cha uzalendo kutaka kujinufaisha na kukandamiza wenzio.

    mengi na hawa mafisadi wenzie wakiindi wasituyumbishe kwa maslahi yao binafsi,wote hakuna mwenye maslahi na taifa letu.

    amekua akifanya ufisadi mpaka kutumia vyombo vyake vya habari

    ReplyDelete
  47. The facts about Swine Flu.

    Swine flu, which was initially only transmitted from pigs to humans, is now traveling through human to human contact, and is one of the most deadly of the flu viruses.

    9 a.m. Sunday, April 26,
    Centers for Disease Control and Prevention (CDC), USA



    Q: What is Swine Flu?

    A: It is a new strain of flu that consists of a mixture of genetic material from swine, avian and human influenza viruses. This new strain of influenza is not only extremely contagious but also deadly, however, there are flu pandemic preparation measures you can take to ensure you do not get the Swine flu.

    Symptoms include runny nose, muscle aches, lethargy, lack of appetite, fever over 101 and sudden onset. It is difficult to distinguish from other flu types, and does require a diagnosis.


    Q: Can I get it from eating pork or pork products?

    A: According to USDA and the Centers for Disease Control and Prevention, NO. Swine influenza viruses are not transmitted by food so you cannot get swine influenza from eating pork or pork products. Eating properly handled and cooked pork and pork products is safe. Cooking pork to an internal temperature of 160 degrees F kills all viruses. The USDA suggests, as it has in the past, cooking pork and pork products to the proper internal temperature and preventing cross-contamination between raw and cooked food is the key to safety. You should:

    • Wash hands with warm water and soap for at least 20 seconds before and after handling raw pork;

    • Prevent cross-contamination by keeping raw pork away from other foods;

    • After cutting raw meat, wash cutting board, knife, and countertops with hot, soapy water;

    • Sanitize cutting boards by using a solution of 1 tablespoon chlorine bleach in 1 gallon of water;

    • Use a food thermometer to ensure pork has reached the safe internal temperature of at least 160 degrees F to kill food-borne germs that might be present.

    There is also no evidence at this time that the virus is in swine or that touching uncooked pork could infect someone with the virus.


    Q: Can I get it from being around or touching pigs?

    A: The CDC says that the spread of swine flu can occur in two ways — through contact with infected pigs or environments contaminated with swine flu viruses. Through contact with a person with swine flu. Human-to-human spread of swine flu has been documented also and is thought to occur in the same way as seasonal flu. Influenza is thought to spread mainly person-to-person through coughing or sneezing of infected people.

    Q: Is my pet potbelly pig in danger?

    A: There is no evidence at this time that the virus is in U.S. swine. Swine owners should learn the warning signs of swine influenza. Signs of swine flu in pigs can include sudden onset of fever, depression, coughing (barking), discharge from the nose or eyes, sneezing, breathing difficulties, eye redness or inflammation, and going off feed. If your pig is showing any of these signs, call your veterinarian.

    Buy your animals from reputable sources and ensure that you have documentation of your new pet’s origin. Be sure that you get your new animals checked by a veterinarian. Keep your pigs and areas around them clean. If you have been around other animals, make sure that you clean your shoes, clothing, and other items. And don’t forget to wash your hands with warm water and soap for 20 seconds before and after handling your pet.



    Q: Is there a vaccine for humans for this new strain?

    A: The CDC should answer any questions about a vaccine. According to the CDC, there is no vaccine to protect humans from this new variant swine flu. Researchers are not yet sure if antiviral medicines such as Tamiflu or Relenza may remain effective against swine flu, although these antiviral medicines are working against the current strain. The CDC is currently in the process of developing a vaccine to protect against the Swine Flu.


    — Visit www.cdc.gov for more information.

    ReplyDelete
  48. Kama nguruwe kweli ni mchafu au ni hatari kula basi wachina na wajapani wengi wangekufa.

    Siasa ya dini tusilete katika chakula. Kuna ugonjwa katika kila mnyama endapo hatuwachungi vizuri au kutumia usafi tukiwapika. Ng'ombe pia ana madhara yake kama Mad Cow Disease, mbona hatuachi kula mishikaki na steki?

    Wale waislamu wenzangu, hamjawahi kula nguruwe aliyepikwa na wachina, ni mtamu mno na bei chee, ndio maana wachina wanapenda kula nguruwe na kama mkienda katika website ya W.H.O, mtaona kuwa jina hili la Swine Flu hawalitaki kwa kuwa halihusiki na ugonjwa huu asili 100 kwa 100. Linawapotosha watu na linavunja soko la nguruwe duniani na kusababisha watu wazidi kuwa masikini.

    Kula nyama yoyote ili mradi ni safi na inapikwa katika sehemu iliyo safi. Kama kuna vita kesho Tanzania, nyama yote ile watu watakula. Nilipokuwa Croatia, wananchi wao waliniambia kuwa walikula paka na mbwa kulipokuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe huko (nchi ya Yugoslavia iligawanyika kinguvu na ikazaliwa Croatia, Serbia, Montenegro, Slovenia, n.k).

    ReplyDelete
  49. wapendwa nguruwe hajaruhusiwa na Mungu kuliwa mimi nazungumza kimaandiko matakatifu toka kwenye biblia, maana hacheui. mambo ya walawi 11:3,7, kama kakataza asiliwe haiana ubishi hiyo lazma tuwe watii tu tukubali sio unasema unaombea alaf umemaliza. maandiko yanasema ( kila mnyama mwenye kwato na kucheua hao ndio mtakula. kifungu cha 7n inasema na nguruwe kwa sababu yeye anazo kwato lakini hacheui yeye ni najisi kwenu.

    nguruwe ni mchafu na ni najisi ndo maana bwana Yesu wakat anakemea mapepo yatoke kwa yule mtu alikuwa kapagawa na mapepo aliekuwa anaishi makaburini, mapepo yakamsihi Yesu watoke kwa yule mtu lkn waingie kwa nguruwe nae Yesu akawapa ruhusa. marko 5:12-13.

    wandugu usijidanganye kama humkubali Yesu usije weka mfupa wa nguruwe nyumbani kwako ukasema unafukuza mapepo au wachawi ndo unawakaribisha maana wenyewe waliomba hata kwa bwana Yesu waingie kwa nguruwe.

    Mungu tusaidie

    MS GBENNETT

    ReplyDelete
  50. Jamani ndugu zangu tuzingatie usafi hasa kunawa mikono. Pia mchezo wa kuchokoa pua na kushika wenzio ni mwiko. Jamani hizi pua sijui zinawasha maana asilimia 80 inapenda kuchokoa pua. Tafadhalini tujiangalie.

    ReplyDelete
  51. Anon wa April 30, 2009 10:09 AM;

    Watu (waislamu, wasabato, na wayahudi) hawakuacha kula mbuzi wa aina hii eti kwa sababu si tamu, laa hasha, bali kwa sababu Mola wao kawakataza. Na wanataka kutii, basi. Kama utawakejeli kwa utii huu basi utalipwa tuu.

    Pia topfautisha dharura na utashi. Mola haadhibu dharura bali utashi mbaya.

    ReplyDelete
  52. Kiingiacho mwilini si najisi bali kitokacho!
    Ng'ombe ana blucera,ana TB na pia analeta Rift Valley Fever je naye ni najisi?
    Kuku wanaleta mafua ya ndege je nao ni najisi?
    Mbuzi wanasababisha goats je nao ni najisi?
    Samaki pia wana fish fever tunasemaje hapo?
    Tujadili vitu kwa maarifa siyo kwa utashi wa vichwa vyetu!

    ReplyDelete
  53. AnonymousMay 01, 2009

    Anon wa April 30, 2009 10:10 PM, sababu za unajisi si ugonjwa ni biblia (walawi 11:3-8)

    ReplyDelete
  54. AnonymousMay 01, 2009

    Anony April 30, 2009 10:04 PM
    Nakujibu:

    Mimi napinga maswala ya dini katika chakula kama nilivyosema awali.

    Dini ni imani yako, amini au usiamini. Lakini kama nilivyosema, kama Tanzania kutakuwa na njaa kali au vita, nina uhakika kuwa utaacha maswala ya dini na kula nguruwe na kitu chochote mbele yako pamoja na majani na miti ili uishi.

    Mimi Muislamu na siamini kuwa nguruwe ni mnyama mchafu kuliko ng`ombe au mnyama mwingine. Na kama nilivyosema, kama huyu mnyama ni mchafu au ana hatari fulani ukimla basi Wachina na Wajapani wengi wangekufa. Nguruwe analiwa kwa wingi mno huko na hatuoni watu wao wanataabika na magonjwa yanayotokana na nguruwe au Mungu amewaalaani kwa kula hio nyama. Sana sana, naona wao wamejaaliwa kuliko sisi kwa utajiri, akili na maendeleo. Angalia wao wako wapi na sisi toko wapi. Au labda mwenzangu unasubiri utese ukifika ahera.

    Wala nguruwe wametujengea uwanja wa ndege, uwanja wa mpira. treni, na karibu barabara zote za Tanzania.


    Sijamkajeli mtu yoyote, ila ninatumia haki yangu ya kusema kuwa nguruwe ni mnyama kama mwingine yoyote na siamini kama ni mchafu kuliko wengine. Hii ni imani yangu na wewe amini unavyopenda. Tanzania ni huru.

    Shukurani Balozi.

    ReplyDelete
  55. AnonymousMay 01, 2009

    Anon wa May 01, 2009 8:32 AM;

    Utawalaumu saana watii amri za Mungu (waislamu, wasabato na wayahudi) lakini lawama zako hazitafanya wabadilike kwa kuogopa maneno yako. Wanamuogopa Mungu zaidi ya yeyote.

    Hawakusema kuwa hawali kwa sababu nguruwe ni mchafu au mchungu, wanakubali ripoti za utamu wake lakini hawatakula ili wasipate dhambi (wana idadi ya wanyama halali na haramu/najisi). Kama vile sex ilivyo tamu lakini wafuata dini (mapadri na masista) bado hawafanyi, tetea na hiyo sex basi.

    Kimsingi sasa hivi hakuna dharura ya kusababisha ulaji wa nguruwe, wanyama halali hawajaisha wala nguruwe si chakula pekee kilichobaki duniani.

    Kwa zaidi nguruwe huliwa magharibi kwa bei yake kuwa chini kuliko nyama yeyote kutokana na ghrama nafuu za uzalishaji wake. Tanzania, nguruwe ni ghali kuliko nyama zoote na wanaokula hudhani wanatekeleza dini.

    Mwisho, kauli yako haionyeshi kuwa wewe una chembe yeyote ya imani ya dini za kiislamu, kisabato au kiyahudi. Maana watu hao huheshimu dini zao na za wengine na hutegemea heshima pia.

    Mtu asiyefata maelekezo ya dini yake ameikana hata kama bado ana jina. Jina si dini bali lebo.

    ReplyDelete
  56. AnonymousMay 02, 2009

    Anon wa May 01, 2009 8:32 AM;

    Kimsingi huji tofauti ya "uchafu", "hadathi", na "najisi" na katika walawi 11:3-8 imesema msile "vichukizavyo." We unasema "nguruwe anapendeza saana kuliko wanyama woote."

    Ndipo unasema unajisi wa nguruwe unaondolewa kwa kuosha na kusali kabla ya kula? (ile sala ya " blesi ze fudi so zati it naurishezi awa badiz.")

    Teh teh...

    By the way kama wewe ni mwisilamu mbona unapingana na kurani? hata wasio waslamu wanajuwa kurani imekataza ulaji wa mbuzi huyu.

    ReplyDelete
  57. AnonymousMay 02, 2009

    Anony May 01, 2009, 8:26;
    Najibu:

    Kwanza simlaumu au simtukani mtu wala dini yoyote hapa, ila natoa maoni yangu binafsi tu. Si nia yangu kukashifu mtu hapa.

    Pili, Tanzania tuna uhuru sasa wa kimawazo. Natumia uhuru wangu kuelimisha jamii kama ninavyoelewa mimi. Fuata au usifuati mawazo yangu ni juu yako wewe.

    Kufuata sheria za dini yoyote ni wajibu wa mfuatiaji sio jamii. Fuata masharti yote ya dini yako lakini huna uhuru wa kunilazimisha au kuamua kuwa kwa kuwa mimi sifati masharti kadhaa ya dini ya Kiislamu au Kikristo basi nimechapotea na nisiwalaumu wafuasi wa dini wanaosema kuwa wanafuata masharti ya dini.

    Kwanza, hamna binadamu yoyote anayeweza kufuata masharti ya dini yoyote. Sio tu kutokula nguruwe, bali kusali, kutoa riziki asilimia 10% ya mshahara kwa waislamu, kutochukua faida katika benki yako, kuomba Mungu kabla na baada ya kula, kufanya mapenzi, kuingia choo, kuamka na kabla ya kulala, kutopigana, kutotukanana na kadhalika. Sasa, mfuatiaji wa dini ni yule anayeweza kufuata hizi sheria zilizopo katika vutabu vya dini. Huwezi kusema kuwa kwa kuwa huli nguruwe na unasali basi wewe ni Mwislamu au Mkiristo bora.

    Kwa imani yangu, mimi ni binadamu bora kwa kuwa siibi, nawasaidia wenzangu nikiwa na uwezo, nasali kwa muda wangu na nawaangalia familia yangu vizuri bila ya kwenda nje kutafuta wanawake. Swala la nguruwe, pombe na kufunga sifuati na sioni sababu yoyote ya kuifuata.

    Chembe zangu za dini ni bora kuliko hao mapadri unaodai hawapendi mapenzi kwa kuwa sheria hairuhusu ya kikatoliki. Uki google utaona kuwa wiki hii Papa Benedict ameomba msamaha kwa niaba ya mapadri waliowaharibu watoto yatima wa Canada waliosoma chini yao. Mapadri na masista pia wameomba msamaha Marekani kwa kuwashika kwa nguvu watoto wadogo. Rais mmoja wa Marekani ya kusini (jina limenitoka) alikuwa padri miaka mingi kabla ya kugombania uraisi. Wamejitokeza wasichana watatu waliozalishwa na yeye na amekubali. Kwangu binafsi, starehe hii ni muhimu kwa binadamu, na kama huipati basi ni kama akili yako haitafanya kazi vizuri mpaka utakapofika umri fulani na huitaji tena. Ndio maana mapadri na masista wameruhusiwa kuoa na kuolewa katika dini za kikristo nje ya katoliki kama Lutheran na Protestants.

    Kwa kifupi, wewe una haki ya kufuata dini kama unavyojua na mimi pia nina haki ya kufuata ninavyoielewa. lakini Mungu peke yake ndio ana uwezo wa kusema nimekosa au sijakosa sio binadamu mwenzangu hapa duniani. Mimi naheshimu dini zote lakini sifuati sheria ambazo akilini haziingii, kama Luther na wenzake walivyofanya na dini ya ukiristo na kuamua kufuata dini ya kikristo bila ya sheria za kikatoliki.

    Naheshimu maoni yako lakini napinga msemo wako kuwa mimi sina dini kwa kuwa sifuati sheria za dini japokuwa asilimia 99% ya binadamu hawafuati sheria za dini zao kama zinavyosema katika vitabu vyao. Dini sio tu kufuata sheria rahisi bali kuijua na kuisoma kindani. Naamini kuwa kuna binadamu wengi kama mimi na wachache wanaojifanya wanatekeleza sheria za dini kama wewe au wanna siasa za kali za kidini.

    Anony May 02, 2009, 2:31 AM
    Najibu:

    Sijasema kuwa nguruwe anapendeza kuliko wanyama wengine. Nasema kuwa sheria za kukataza kula huyu mnyama hazina msingi. Ni wajibu wako kufuata au kupinga sheria za dini, mimi nimeamua kupinga hii sheria kwa kuwa haingii akilini mwangu. Una haki ya kuniweka katika picha yoyote lakini naamini kuwa kuna binadamu wengi duniani wanaoishi kama mimi kuliko wale wanaojiita wafuataji wa dini lakini wakipinda kona tu basi wanavunja sheria zote kwa kulala nje ya ndoa, kutowaangalia familia zao, kufanya mapenzi na watoto wadogo, kuwapiga wake zao, kuwanyima elimu watoto wa kike,kutotoa riziki, kutosaliau, LAKINI hawali nguruwe kabisa.

    Ni wajibu wetu kama binadamu kupinga sheria zote zinazotupeleka nyuma badala ya kutuendeleza, ziwe za dini au nchi. Sheria ya kukataza kutokula nguruwe ni moja wapo. Kama ina sumu au madhara mwilini basi wengi duniani wangekufa kama nilivyosema awali. Hatuishi miaka ya 1500 tena.

    Shukurani Balozi.

    ReplyDelete
  58. AnonymousMay 02, 2009

    Anon wa May 02, 2009 7:45 AM:

    1. kusema kwako hukusudii kukashifu mtu au dini ni utangulizi kuonyesha unataka kurusha kashfa chini ya kivuli cha uhuru wa kunena, kwa hiyo usiulizwe. Kimsingi kisheria ungekuwa huna nia kama huelewi ukisemacho kwa sababu ya utovu wa akili au bahati mbaya, laa sivyo una nia na maneno yako na unataraji matokeo yake.

    2. kama ungekuwa mwisilamu msomi akam ulivyojiita ungejuwa aya mbili zinazotaja uhuru asili kutoka kwa Mungu, a)hakuna kulazimishana katika dini, b) mwanadamu kapewa utashi(hiari) basi akitaka akosee au apatie katika matendo yake. Kwa hiyo unafanya makosa kusema maelekezo ni sheria.

    3. Una uhuru wa kwenda kinyume na dini yeyote na bado ukajiita mfuasi wa dini hiyo, hamna maelekezo ya kutoa zaka au sadaka (ambayo wewe umeita riziki, teh) 10% ya mshahara kwenye waislamu. Either u r uninformed or missinformed. Lakini kwa nini ung'ang'nie uislamu ambao unaupinga kwa makatazo yake ya nguruwe? kwa nini usiingie dini ambazo zinaruhusu nguruwe na unakuwa umeenda vizuri na kitabu chao, na huna haja ya kutetete ulaji wako kinyume na kitabu? Mi nlifikiri watu huchagua dini zenye maelekezo nafuu ambazo wanaweza kuzifuata.

    3.Ubora wako juu ya wanadamu wengine unategemea vigezo. Vigezo vinaweza kuwa vya Mungu, vya UN, vya OAU, vya serikali, vya marafiki zako nk. fafanua. Pia ukumbuke kujiita bora ni kujikweza na ni kosa. Biblia ikasema ajikwezae atashushwa. Ni mstari gani katika korani au biblia unaosema wewe ni bora kuliko mapadri na masista? Kama hamna mstari basi ujue utaratibu/uhuru wako wa kujiita bora unaweza kutumiwa na watu kukuita si bora.

    4. Umesema una dini, ni kweli, hakuna matu asiye na dini. Watu husema hata kutofuta dini za kiislamu na kikristo nayo ni dini. Hivyo inategemea uelewa wako wa neno dini, mimi nadhani dini ni mfumo wa maisha.

    5. Naona unatumia triki ya "wengi wape" kana kwamba siku ya hukumu Mungu atasema wengi waende paradiso na wachache waende jehanam kama kwenye uchaguzi mkuu. Hapana, Mungu atamlipa kila mtu wema kwa wema na ubaya kwa adhabu. Hata mahakama zetu utaona bila kujali wangapi wamekosea hutiwa magereza.

    6. Umekosea, dini zinaruhusu kumuita mtu aliyekosea mkosaji ikiwa ushahidi upo na dini zinaamrisha mtu aliyekosea aripotiwe panapohusika. Kitu dini zinakataza ni kumhukumu mtu kuwa yeye ataenda jehanamu kwa makosa yake kwani hujui atatubu wakati gani. Kwa hiyo kama mtu akiiba atasemwa mwizi na atapelekwa polisi.

    7. Samahani, sijasema wewe si mwisilamu bali unapinga mambo ambayo waislamu wanasema. Inawezekana we ni dhehebu jipya la kiislamu ambalo linaruhusu nguruwe,pombe, linakataza kufunga, n.k, ni uhuru wako wa kikatiba na ninaheshimu uhuru huu. Ila nadhani wewe hauko katika madhehebu ya kiislamu, kisabato au kiyahudi yanayokataza nguruwe.

    8. Pia inaonyesha exposure yako ya dini ni ndogo. Scholars woote wa dini zoote wanakataza siasa kali lakini wanahimiza wafuasi wasali kupata baraka kwa Mungu. Lakini wewe unaita watu wanaosali kuwa ni siasa kali. Kuna haja gani ya kuwa na dini kama hamna sala, hakuna dini isiyo na sala au sala ndo msingi mkuu wa dini yeyote duniani, ukiacha dini ya kupinga sala.

    8. Uhuru ni msumeno, unamruhusu mtu kuchagua ale au asile nguruwe. Unamruhusu mtu afate au asifate dini. Kwa nini wewe unaona kama wafata dini hawajatumia uhuru wao bali wewe? Kama wewe ulivyo na uhuru wa kuchagua kula mbuzi na wao wana uhuru wa kuchagua kutokula mbuzi na hamna haja ya kushangaa kwa nini wameamua kutokula.

    9. Nafikiri wewe kweli ni mpinzani wa jamii, yaani unawaambia watu wapinge sheria, je wakienda segelea utawatoa wewe. Nafikiri ingekuwa busara kuwaasa watu wafute sheria ili pawe na amani na wasipate matatizo. kimsingi hakuna nchi yeyote duniani isiyo na sheria na si lazima upende sheria lakini kama RAIA MWEMA lazima utii sheria hata usizozipenda.

    ReplyDelete
  59. AnonymousMay 03, 2009

    Anony May 02, 2009, 9:35 PM.

    Ahsante kwa maoni yako na yafatayo ni majibu yangu.

    1. Nategemea madau wengi kama wewe hawataridhika na maoni yangu juu ya ulaji wa nguruwe na dini. Narudia kuwa sio nia yangu kukashifu mtu yoyoye bali kutoa maoni yangu binafsi. Ni uhuru wako kama utaniweka katika kapu la watu wenye akili potovu kwa kuwa unapinga maoni yangu lakini mimi nitakuweka katika kapu la mpingamizi wa maoni yangu tu.

    2. Narudia tena kusema kuwa binadamu na sheria za dini haziendi pamoja. Ukisoma maoni yangu juu utaona kuwa asilimia kubwa ya binadamu hawafuati masharti ya dini sheria kwa sheria. Mara nyingi utakuta na mtu na heshima zake lakini ana wanawake wengi nje ya ndoa na amezalisha watoto haramu. Lakini mtu huyu pia anaswali kila siku na hakosi kwenda Ijumaa. Mtu huyu pia anapinga watoto wake wa kike waende shule zaidi ya sekondari au analazimisha waolewe wakiwa wadogo. Mimi najiuliza na nawauliza wadau hapa. Je, kuna watu wangapi kama hawa katika jamii yetu? Je, kwa nini mtu kama huyu anaonekana bora katika jamii kuliko mtu kama mimi niliye na mke mmoja, sina watoto nje ya ndoa, ninayeheshimu elimu ya watoto na uhuru wa kufanya ndoa wakiwa tayari lakini sifungi na nasali kwa muda wangu? Kama sheria ni msumeno, basi wafuasu wengi wangefeli kwa kuwa wengi wetu hatuwezi kufuata sheria za dini bila ya kuvunja sheria katika maisha yetu ya kila siku (mimi kunyw apombe, wao kuzaa nje).

    3. Karibu kila binadamu anaenda kinyume na sheria za dini kila siku japokuwa hatufikirii sana. Kama unatumia mipira kukinga na magonjwa kama ukimwi au mimba, kutumia vidonge kuzuia mimba, kutosali wakati wa kusali, kupokea faida katika akaunti ya benki yako (interest) na kulala na mwanamke kabla ya ndoa. Yoye hayo unavunja sheria. Kwa kutumia sheria za dini basi karibu wote sisi hatuwezi kujiita wafuasi wa dini.

    3. Naomba ujibu hapa kama unafuata sheria zote za dini yako halafu utakuwa huru iniite utakavyo. Kama unapinga mtu anayekula nguruwe asijiite Mwislamu basi mimi napinga mtu anayelala nje ya ndoa au kuvaa mipira akifanya mapenzi kuwa sio Mwislamu pia kwa kuwa wote tunavunja sheria. Je, kuna wangapi hapa tunatumia mipira au kupanga uzazi kwa vidonge na shindano? Kwa nini hawa ni Waislamu zaidi kuliko yule anayekula nguruwe au asiefunga kama mimi? Inabidi basi wote tutafute dini nyingine kwa kuwa asilimia kubwa ya jamii yetu inavumja sheria za dini kila siku sio tuu kutokula nguruwe.

    4. Mimi siwezi kutumia maneno katika vitabu vya dini kama vile ni sheria msumeno. Tanzania kuna wafuasi wa dini nyingi. Ninafurahi kujua kuwa sheria za dini ya kiislamu hazifuatwi Tanzania. Sheria zao inasema ukiiba basi ukatwe mkono kama wanavyofanya Saudi Arabia. Pili, wanawake wanaokamatwa na wanaume ambao sio waume zao katika vitanda huwa nauawa kwa kutumia mawe. Je, unafikiri hizi sheria ni bora kufuatwa kwa vile ziko katika Kuran? Sijasema kuwa mimi ni bora kuliko mapadri au masista. nimesema kuwa mimi ni bora kuliko padri au sista aliyemharibu mtoto mdogo kwa kumshika kwa nguvu. Sheria za kikatoliki zinasema kuwa wasioe na wafanye kazi ya Mungu tuu. Nasema hii sheria ni kinyume na haja za binadamu na ndio maana kuna wengi wao wamefikishwa mahakamani na kuna Wakiristo wengine ambao wanaruhusiwa kuoa au kuolewa wakiwa mapadri kama Lutherans na Protestants.

    5. Umesema la kweli kabisa kuwa uelewaji wa neno la dini ndio unazingatia kama mimi ni mfuasi au la. Mimi nafuata dini lakini sio kama kipofu. Sifuati sheria ambazo naona sio za karne ya 21. Mimi binafsi najiona kama ni Mwislamu bora kwa kuwa naishi bila ya kuiba, natoa riziki au unaita wewe sadaka nikiwa na uwezo na nawaangalia familia yangu na jamii yangu. Sioni sababu ya kufunga au kutokula nguruwe au kunywa pombe. Siamini kabisa kuwa kuna binadamu duniani aliye na haki ya kusema kuwa navunja sheria za dini au nitaenda motoni au ahera. Hukumu ikija, nitahukumiwa na Mungu sio binadamu mwenzangu duniani. Mpaka hapo, nitaishi kama raia anayependa haki kwa wote, nitawafundisha watoto wangu kuheshimu watu wote, nitawasomesha, nitawaozesha wakiwa tayari kuolewa au kuoa. Sitaenda kutafuta wanawake nje ya ndoa au kuzalisha watoto haramu, sitawapiga mke na watoto wangu. Kama sifuati sheria za kukatana mikono au kufunga au kula nguruwe na kunywa pombe basi Mungu atanihukumu ikifika muda wangu.

    6. Nadhani unakumbanisha sheria za dini na za nchi. Sheria za nchi ukiiba utapelekwa mahakamani na kushtakiwa baada ya polisi kupeleleza na kuleta vithibitisho. Hakimu ataamua hukumu. Halafu utakwenda jela kwa muda kadhaa. Hakuna sheria inayosema usile nguruwe wala kunywa pombe kwa kuwa hatufuati sheria za Kiislamu (Sharia) Tanzania. Ukiangalia sheria za nchi, sijavunja kwa kuwa sijamwibia mtu ila nakunywa pombe. Sasa kama hamna sehemu ya kuripoti kama nimevunja sheria za dini kwa kuwa hatuna sheria za dini ya Kiislamu katika katiba yetu, basi mimi ni mfuasi na raia mwema. Huwezi ukatumia sheria za dini na kunishtaki kuwa mimi si mfuasi wa dini yangu kwa kuwa sijavunja sheria za nchi ambazo ziko juu kuliko sheria za dini katika katiba yetu.

    9. Mimi napinga sheria ambazo hazina nafasi katika karne ya 21. Mimi sina dhehebu jipya wala wafuasi wepya. Ni uhuru wako kuniweka katika picha ya mtu asiyekuweko katika dhehebu la Kiislamu kwa kuwa sifungi au nakunywa pombe. Narudua kuwa hakuna binadamu anayeweza kufuata sheria za dini yoyote bila ya kuvunja sehemu moja au nyingine. Nikitumia logic yako, basi kuna wafuasi wachache tu wanaoweza kujiita waislamu au wakiristo kwa kuwa hawawezi kufuata sheria za dini kama sinavyosema katika Biblia na Kuran.

    Nashukuru kwa muda wako na kupewa nafasi na Balozi kukujibu.

    ReplyDelete
  60. AnonymousMay 03, 2009

    1. Dini ni imani, aidha unayo au huna.

    2. Sheria za dini ya Kikristo na Kiislamu ni kali na za kale. Ndio maana kuna nchi chache tu duniani wanazitumia katika katiba zao.


    3. Mwislamu na Mkiristi haruhusiwi na dini kutumia dawa au kinga kuthibiti mimba. Je, kama unatumia vidonge au kondomu, wewe bado ni mfuasi halali?

    4. Dini yako ikisema kata mkono mtu akiiba lakini sheria ya nchi inasema peleka mwizi segerea baada ya kuhukumiwa. Je, hapa, binadamu si anakiuka sheria za Mungu na kutumia sheria za binadamu? Kwa nini mfuasi anakubali sheria za binadamu kumpeleka segerea lakini anapinga mfuasi akinywa pombe au kula nguruwe?

    5. Sheria za Tanzania zinaruhusu kila mtu kula nguruwe na kunya pombe. Hatufuati sheria za dini. Kwa hivyo, swala la kula nguruwe ni la binafsi sio la kidini. Sheria yetu na katiba yetu sio ya Kidini. Kama tunaishi Iran, Pakistan, Saudi Arabia, Sudan Kaskazini au Afghanistan, basi tutakiuka sheria kama wafuasi wa Kiislamu tukinywa pombe au kula nguruwe.

    6. Kama tunakubali kuwa sheria za Tanzania siko juu kuliko sheria za Biblia au Koran, basi hamna mtu atayeweza kusema kuwa wafuasi wanavunja sheria za dini wakila nguruwe au kama hawaendi kanisani jumapili kwa kuwa sheria zetu sio za Kidini.

    ReplyDelete
  61. AnonymousMay 03, 2009

    Wapendwa tusidanganyane. Kuna wengi wetu hatuelewi yanayofundishwa katika dini zetu na tunashika kile kidooogo tunachoona kinafaa kwetu kuendesha maisha. Unajisi wa vyakula uliongelewa wakati wa Agano la Kale na ulikuwa na sababu (JIFUNZE UELEWE). Wewe si wa agano lile, ni wa Agano Jipya la Bwana Yesu Kristo. UKO HURU. Ukitaka kuelewa soma kitabu cha WAKORINTO (ktk biblia sijui kama vitabu vya kiislam kipo), kitafungua mawazo yako (ila uombe roho akusaidie) na utajijua wewe ni nani. Hili linajitokeza tena hapa, hatujui na hatukubali kuwa hatujui. Soma maelezo au tafuta anayefahamu juu ya Swine Flu ili utoe maoni ya maana, ukikumbuka kuna wengine watajifunza kwa comment yako, usijifunze kwa kusikiliza maneno ya vijiweni. Kama wewe ni wa SHERIA maandiko yanasema FATA YOTE UISHI...Unafanya hivo?

    ReplyDelete
  62. AnonymousMay 03, 2009

    Anon wa May 03, 2009 9:26 AM;

    nimeyasikia majibu yako, na naheshimu uhuru wako, ila hapa hatutakubaliana kamwe kwa hiyo ingekuwa vizuri tukubali kutofautiana (agree to disagree). Hata hivyo unavyoleta hoja hazizingatii pande mbili za shilingi. Kila siku lazima yawepo makundi mawili pinzani katika kila jambo na nahisi hutapinga hilo.
    Hivyo hamna haja ya mijdala mireefu.

    A.1. Wewe si mwendawazimu. Hapo nililenga kuwa ukiwa na akili timamu wakati wa kusema au kutenda basi humaanisha kuwepo na nia ya neno au tendo na matarajio ya matokeo yake. Hata hivyo matumizi yako ya neno "riziki 10%" na "ahera" kunatoa dondoo za wewe dini gani japo ushahidi zaidi unahitajika. Maneno haya yana maana tofauti katika dini tofauti.

    B.2.-6. Kama umesema kitu kimoja tuu. Kimsingi unatumia wafuasi wa dini waliokosea kama mfano wa udhaifu wa dini. Huwezi kulaumu dini kwa makosa ya wafuasi. Kumbuka watu tumepewa utashi au hiari (free will), tuna uwezo wa kuchagua mema na mabaya bila adhabu ya papo. Tofauti yako na wanadini wengine ni kwamba wanatenda dhambi kwa kuteleza na kuitambua dhambi na kutubu na kuomba msamaha kwani Mungu ni msamehevu. Wewe unakataa kutambua dhambi ili usitubu na unataka wengine wawe hivyo. Wale wanojitahidi kufuata maelekezo katika waislamu na wakristo kwako si mfano?

    Na kuwa watu wanatenda dhambi we si wa kwanza kusema kwani Mtume amesema kila mmoja wetu atatenda dhambi kutokana na udhaifu wetu na mbora wetu ni yule anayetubu na kuomba msamaha. Na hivi ndivyo dini zilivyo: watu hujitahidi kufanya mema na wakikosea huomba msamaha na Mungu huwasamehe.


    C. Nakupongeza,kimsingi wewe una mawazo ya ki-Luther kama ulivyojisifu lakini hutaki kufuata kanuni zake. Ulitakiwa kuanzisha na kusajili dhehebu la kiislamu liruhusulo pombe na nguruwe na uje na kurani yako ya karne ya 21 au ufute au ubadili aya katika kurani ya zamani. Unajuwa ndo maana kuna madhehebu mengi, watu wakiona hawakubaliani na mafundisho huanzisha dini au dhehebu jingine kwa amani, hawajaribu kubadili katoliki nzima ifute maelekezo. si unaona kuna biblia mbili tofauti? Kama Luther asingejitoa kimasomaso tungekuwa na katoliki tuu hii leo.

    D. Mimi nakubali wewe ni mwislamu lakini siyo wa madhehebu ya kukataza nguruwe kama wengi wajuwavyo, wewe ni mwenye dhehebu la kimapinduzi lakini unajificha hutaki kutumia uhuru wako wa kikatiba kuleta mapinduzi yako katika jamii kubwa. Vipi utaondoa sheria usizozitaka bila kuanziasha movement? Hapa sajili dhehebu na utahubiri utakavyo kwa kurani yako na hutakuwa na haja ya midahalo na malumbano. Au kama unaogopa kuanzisha dhehebu basi kuna dini nyingi ambazo zinaruhusu nguruwe na pombe kwa nini usijiunge nazo uache kunga'nga'ania wisilamu ambao una kasoro na kukaa unabishana na vitabu vyao na mashehe wao? Chagua dini bora zaidi na uifuate kwa amani na furaha.

    E. Suala la kuwa kuna wafuasi wa kweli wachache katika kila dini ni la kweli, kwa hiyo wewe unashauri tufute dini kabisa ziishe ili pasiwepo na dini kwa sababu jamii kubwa haizikubali katika maisha ya kila siku? Vipi uhuru wa wachache walioamua kufuata? Kimsingi unatakiwa ujuwe Mungu aliahidi hatatuangamiza duniani kwa makosa yetu kama wakati wa Noah, Lot, Moses n.k. Hata walioangamizwa walikuwa wengi zaidi ya waliosalia. Kwa hiyo una uhuru wa kutumia loophole hiyo utakavyo hamna adhabu ya papohapo.

    F. Pia kitu kingine unaweza kuwa hujakipa muda wa ni kwamba dhambi na jinai ni tamu na zina faida ndo maana watu huzifanya. Mfano nguruwe anasifiwa ni mtamu saana, pombe hupoteza mawazo na kuongeza nguvu, zinaa ina ladha na hufanya watu wakatuliza tamaa zao na kuendelea na shughuli nyengine, kuiba hela nyingi bila kukamatwa humgeuza mtu tajiri bila jasho halali, kusema uongo hunufaisha waongo. Kama pasingekuwa na faida katika makosa basi watu wasingefanya na kama pangekuwa na adhabu ya papo. Lakini faida ya makosa ni ndogo kulika hasara zake.

    G. Mwisho, nahisi wewe una kipaji cha uongozi na ushawishi ila hutaki kukitumia. Naona mitazamo kuhusu nguruwe na pombe una uchaguzi kama unataka kusaidia wengi duniani, sanasana watu ambao wanang'ang'ania wislamu huku wakipenda kula nguruwe na pombe. Ni kuanzisha dhehebu jipya la kiislamu amablo litakuwa halina kasoro unazoziona ili kusaidia watu wengi wawe bora, hii itajibu vipengele vyoote vya B-F. La sivyo njia ya amani ni kujiunga na dini amabyo ni bora kuliko wislamu na kushawishi waslamu wengine wajiunge pia, itakuwa ni bora na njia ya amani kuliko kulumbana na mashehe ambao hawatakubali hoja zako tena kificho ukivizia mada tata katika gulobu.

    Kwa wema.

    ReplyDelete
  63. AnonymousMay 04, 2009

    Anon wa May 03, 2009 11:47 AM;

    Habari mpendwa, una mjadala mzuri japo kuna majibu mepesi yasiyohitaji rejea.

    1. Hata kutokuwa na imani ni dini au mfumo wa maisha.

    2. Sheria za dini zipo kwenye jamii zisizo mseto ambazo ni chache duniani na sio kwa sababu ya ukali au ukale.

    3. Sijui kwa wakristo, lakini waislamu hamna mstari wowote unaokataza matumizi ya kondomu au vidonge au upasuaji kwa afya ya uzazi. Kimsingi natural sciences zinakubalika kwa asilimia 100% na zisizokubalika ni kama darwin theory of origins, imani ya dini ni kwamba Adam na Hawa/Eva waliumbwa na ni watu wa mwanzo. Kwenye uislamu hamna kukataza jambo bila mstari, kama hamna mstari ni ruksa kujirusha, hamna baraza la wazee la kutunga sheria.

    4&5. Jibu rahisi baada ya lile la 2. Nchi kama tanzania ni ya mseto na ya kisekula. Hivyo waislamu hutakiwa na dini yao kufuata maelekezo ya dini na pia hutakiwa na serikali kufuata sheria. Mwisilamu mtiifu na raia mwema hufuata maelekezo na sheria kwa ujumla. Kwa sababu sheria za nchi ni laini zaidi ya maelekezo ya dini, na zinaambatana kwa kiwango kikubwa basi mwisilamu hapati taabu yeyote kufuata sheria za nchi. Kwa hiyo, Wanazuoni wamegawanya makosa katika sehemu tatu ambazo adhabu zake zinategemea umemkosea vipi kama ifuatavyo i> mpaka iii>.

    i> Dhambi tuu. Kumkosea Mungu pekee: huu ni uchumaji wa dhambi na asipoomba msamaha ataadhibiwa siku ya hukumu na hamna adhabu kutoka kwenye jamii kwani si jinai. Makosa haya mfano wake ni ushirikina, uchawi, ulevi, zinaa, kula wanyama waliokatazwa, kunyima wanaostahili kusaidiwa, kiburi, ujeuri, kukandamiza wakopaji kwa riba badala ya kuwasaidia wainuke,kuacha kusali, n.k.

    ii> Dhambi na jinai. Kumkosea Mungu na jamii: mtu huchuma dhambi ambazo ataadhibiwa siku ya hukumu asipoomba msamaha. Jamii itamwadhibu kulingana na sheria zinazoendesha jamii. Mfano wizi, ujambazi, ufisadi, dhuluma, ubakaji, ugaidi, uharamia, dawa za kulevya, kuuwa, kupigana, kubagua kwa misingi ya rangi na kabila, n.k.

    iii> Jinai isiyo dhambi. Hii ni kuikosea jamii na mkosaji huadhibiwa kwa mujibu wa sheria za jamii lakini kwa Mungu hana kosa wala haadhibiwi na huenda akazawadiwa kwa Mungu kulingana na kitendo. Makosa haya yako machache Mfano: kupinga ubaguzi Afrika ya kusini serikali ilimfunga Mh. Mandela, watemi wengi waliuliwa na wakoloni kwa kugombea uhuru, ...unaweza kutaja mengi ya hivi.

    6. Kimsingi sheria/katiba ya nchi haifuti maelekezo ya dini bali inatoa uhuru wa kuamua kufuata au kuacha. Ukiamua kula nguruwe kama wewe ni islamu au sababto basi unakuwa umetenda dhambi lakini hamna jinai kama 4&5.i> juu hapo na pia umetumia uhuru wako vizuri. Ukiamua kutii maelekezo ya dini basi hujafanya jinai na umetekeleza uhuru wako na unapata baraka za Mungu. Usiposali hujafanya jinai bali dhambi lakini pia umetumia uhuru wako. Ukisali unakuwa umetumia uhuru wa kikatiba na unapata baraka za Mungu.

    Hitimisho: uhuru ni kitu muhimu kuliko mambo mengi mno.

    ReplyDelete
  64. AnonymousMay 04, 2009

    Anony May 02, 2009, 9:04 PM

    Asante kwa majibu yako. Nakubali kuwa hatutakubaliana katika haya maswala na nimefurahi kuongelea maswala ya dini na wewe. Naomba tu nitoe jibu la mwisho.

    1. Kwanza, sina nia ya kuanzisha dini au dhehebu. Ni maoni yangu tu juu ya jamii na dini.

    2. Nakubali kuwa kuna watu wengi wanajitahidi kufuata dini zao na wanafanya makosa kila siku na wanaomba Mungu awasamehe.

    3. Swala hili hukulijibu: Kuna tofauti gani katika dhambi ya mfuasi anayetumia kondomu au vidonge vya kuzuia mimba na yule anayekula nguruwe au asienda kanisani? Nadhani utakubaliana na mimi kuwa wafuasi Tanzania wanatumia vidonge au Kondomu kupanga uzazi au kuzuia mimba na magonjwa (japokuwa sio 100%). Kama mimi niko katika kundi la mfuasi anayekunywa pombe au kula nguruwe, kwa nini unaona nimepotea zaidi kuliko asimilia kubwa ya wafuasi wanaovunja sheria ya kutozuia kizazi cha Mungu kisiishi?

    4. Kama tunatenda dhambi kila siku basi utakubaliana na mimi kuwa hatuwezi kuwa wafuasi halisi wa dini kwa kuwa tumeshindwa kufuata sheria za dini? Huwezi kujiita mfuasi kama hufuati sheria za dini yako, si ndio? Dini sio tu jina, kuna wajibu lazima ufuate ili uitwe mfuasi.

    5. Mimi sina mawazo ya ki-Luther ila mawazo yangu ni yale ya karne hii ya 21. Sina nia ya kuanzisha dini ila ni mawazo yangu kuwa baadhi ya sheria ya dini yangu hayana msingi kama kutokula nguruwe au kukata watu mikono au kupiga wanawake mawe au kufunga.
    Nadhani utakubaliana na mimi kuwa huwezi kujiita mfuasi kama unavunja sheria za dini kama mimi juu ya swala la nguruwe na pombe. Kwa ujumla, wewe pia si mfuasi kwa kuwa huwezi kufuata sheria za dini yako kamili kama utatumia madawa kuzuia mimba/Kondomu au kutosali au kukubali sheria ya katiba ya nchi badala ya dini yako. Kuomba msamaha kwa Mungu akusamehe kila siku ni vizuri lakini inaonyesha kuwa wewe kama binadamu umeshindwa kufuata sheria za dini yako.

    6. Kama wafuasi wengi, mimi naipenda dini yangu na naifuata kwa furaha na amani. Kama wafuasi wengime wengi, navunja sheria ya dini yangu kila siku kama sisali mara tano au kama sifungi au nikinywa pombe. Tofauti kati yangu na wengine ni kuwa nimechapisha hapa maoni yangu na kujaribu kuelimisha jamii juu ya maswala haya. Si nia yangu kuanzisha dini nyingine inayoruhusu nguruwe na pombe. Kama ni hivyo, basi lazima pia nianzishe dini ya kuto sali sala tano au dini inayoruhusu kuwa na watoto nje ya ndoa au inayoruhusu kutumia kondomu. Sishauri kufuta dini, nashauri tujitokeze na kusema kuwa wengi wetu si wafuasi wa dini kwa kuwa wengi wetu tumeshindwa kufuata sheria za dini kama zinavyosema katika Kuran na Biblia. Utakubaliana na mimi hapa nadhani. Ni rahisi mno kujiita mfuasi lakini ni vigumu mno kufuata sheria za dini yako.

    Natoa shukurani tena kwa kunipa mawazo yako na kupewa nafasi na Balozi hapa. Nia yangu ni moja tu: kuelimisha kwa kujiuliza. Kubali au kataa maoni yangu, hii ni haki yako.

    ReplyDelete
  65. AnonymousMay 04, 2009

    Anon wa May 04, 2009 5:00 AM;

    Bado katika majibu yako ya mwisho (kama kweli)hueleweki kama wewe ni mfuasi au mpinzani wa dini yako.

    6. Kwa nini ung'ang'anie kufuata dini ambayo huwezi kuitekeleza wakati kuna dini nyengine ambazo nyepesi na rahisi, hazina sheria ngumu, zinaruhusu pombe na nguruwe kwa nini usijiunge nazo? Au achana na masuala ya dini utulie zako kama dini zinakukera, kwa nini usumbuke?

    Swali la msingi kama unataka kujibu ni"kwa nini ung'ang'anie uislamu, uislamu una nini hasa kinchokufanya uung'ng'anie, ikiwa unaamrisha mambo usiyoyataka na unakataza mambo uyatakayo? wakati kuna dini nyingi na una hiari ya kutokuwa na dini?"

    Na kama wewe unajitambua kama mvunja amri, kwa nini usiwaache wanaotaka kuifuata ilivyo wafuate? Ni ruksa kuanzisha dini ya kufuata maelekezo utakayo (kukataza kusali, kukataza kufunga, kukataza jema lolote, kuamrisha baya lolote), ila angalia lisikataliwe serikalini kwenye usajili, hamna dini ya kukataza kusali, hasa sala ndio dini. Naona ungeleta maoni ya amani katika jamii.

    Hiyo nia ya kuelimisha unayodai haitafaulu kwa sababu unawaelimisha watu wakatae kitu ambacho wamekikubali. Wanajuwa wamekatazwa nini na wameamuwa kuwa kundini japo wanajuwa dini nyingine nyepesi zipo. Unataka kufundisha ukristo msikitini? Hata mtu akitaka kukataza wakristo(wasio wasabato) kula nguruwe hatofanikiwa katu kwa sababu ya misingi ya dini yao.

    Njia bora ya kuelimisha wafuasi wa dini ni kuwa kiongozi wa dini au kutumia viongozi wao kama serikali ifanyavyo. Lakini ni vigumu kuwaambia unawaelimisha ili wakatae maelekezo ya dini yao. watakwambia elimu hiyo tunayo, tumechagua kufata hivyo.

    Nina uhakika 100% ukisema haya maneno yako msikitini, watakushtaki na utafungwa kwa kosa la kukashifu. Faida iko wapi sasa? Wengine watakupa kipigo kabla polisi hawajafika, na askari watakuongezea, si unajuwa askari wa bongo.

    Na kama unavyosema wengi wameshidnwa kufuata sheria za dini, na kuzifuta dini hizi hutaki, so what? what is your point? Unajenga nini hapa? Yaani nini suluhisho lako, tuzifute au tuziache? Pointi yako ya 4 unakubali ni sahihi wewe kuitwa si mwisilamu au vipi?

    ReplyDelete
  66. AnonymousMay 05, 2009

    Kama walokole wanaweza kuacha pombe na zinaa kwa nini wengine washindwe?

    Japo wanasingizia uongozi wa roho mtakatifu hamna ushahidi wa uongozi huo kwani kupewa paradiso itakuwa hawastahili ikiwa kila kitu wamelazimishwa na huyo roho bila utashi wao. Na wakosaji hawatakiwi waadhibiwe maana hawakutumiwa roho kama ni hivyo.

    Na wakikosea husingizia shetani lakini wao ndo huadhibiwa. Mungu si mwonevu. Ikimaanisha watu wanatakiwa watende mema kwa akili na myoyo yao na wajizuie na mabaya pia.

    Kwa nini wakifanya mema wamsingizia roho na wakifanya mabaya wamsingizia shetani? kimsingi shetani si utetezi na kama roho ndo mtendaji hapatakiwi kuwepo malipo ya paradiso.

    ReplyDelete
  67. AnonymousMay 05, 2009

    Jamaa hapo juu anajuwa islamu ndo dini ya kweli pekee ndo maana anaing'ang'ania.

    Kwa nini aumizwe kichwa na amri asizoweza wakati kuna dini zitampa majibu yote kama ayatakayo?

    ReplyDelete
  68. AnonymousMay 05, 2009

    anony may 03,2009 2:05pm

    unakosea unaposema sisi ni wa agano jipya na mambo ya nguruwe yalisemwa agano la kale. swali kwako mdau mbona kanisani tunatumia vitabu vyote vya agano la kale na jipya? wachungaji au watumishi wanatusomea kitabu cha mwanzo,kutoka,walawi kwanini tusiwe tunahubiriwa tu kwanzia mathayo, luka, matendo peke yake? na amru 10 za Mungu ambazo tunazifata zinasema usiue, usiibe ,usizini,usitamani n.k zimeandikwa kwenye agano la kale na tunazifuata ? baba wa imani ibrahim ,isaka na jakob wameandikwa kwa agano la kale na mbona hata kwenye maombi yetu tunawataja. kutokana na hoja yako watu hawapaswi kukubali hata amri 10 maana ni za kale.ebu tuache tusikumbatie dhambi, kama nguruwe dhambi tukubali tu, hamna mjadala hapo

    MS GBENNETT

    ReplyDelete
  69. AnonymousMay 05, 2009

    Anon wa May 05, 2009 9:40 AM,

    Nachokuunga mkono ni kwamba Mungu habadiliki wkati woote. Ni Mungu aliyeleta maagano yoote kwa mwanadamu, vipi tuchague maagano. Na ukitaka kuona kwamba maagano yote yanatakiwa kufuatwa, mambo ya agano la kale hayakutajwa kwenye agano la nyongeza. Misingi yoote inatokana na agano la kale kuanzia amri 10 na maagizo mengine. Kimsingi yesu hakuja kufuta torati bali kuikamilisha. Watu wanafikiri kukamilisha ni kubadili.

    Watu badala ya kutubu dhambi wanataka Mungu abariki dhambi zao.

    ReplyDelete
  70. AnonymousMay 06, 2009

    Anony May 03,2009, 7:26 PM

    Hujajibu swala langu la tatu: Tofauti kati ya dhambi ya kula nguruwe/ kunywa pombe na kutumia dawa au kondomu kuzuia mimba.

    Hamna tofauti kati yangu na wafuasi wengi wasiofuata sheria nyingi za dini yao lakini kwa nini unaning'ng'ania mimi nijitoe katika dini yangu kwa kuwa sitaki kufuata sheria ya kutokunywa pombe au kutokula nguruwe? Kuna wangapi unaowajua wanaweza kusema kuwa wanatekeleza aamri za dini? Kwa nini hukubali kuwa sheria za dini ni ngumu na za kale na karibu asilimia 100% ya watu wanashindwa kuifuata lakini bado wanajiita wafuasi.

    Ni haki yangu kujiita Mwislamu kama nitakavyo. Mimi, kama wafuasi wengi Tanzania, navunja sheria za dini kila siku. Wewe unasema kuwa nisijitie katika ufuasi wa dini yangu kama siwezi kufuata sheria zake. Ukitimia logic yako, inabidi waislamu karibu wote wajitoe katika dini yao kwa kuwa hawafuati sheria za dini kama kutozaa nje ya ndoa au kutotumia vidonge vya kuzuia mimba au kutumia kondomu. Pia, tunaishi katika sheria ya katiba sio Sharia ya dini.

    Nafahamu kabisa kuwa Tanzania elimu ni duni na bado demokrasia ni changa. kami nilivyosema awali, sina nia ya kuleta dini mpya wala ya kubadilisha watu dini zao. Ni kweli, maoni yangu ni mazito na kama nikizitoa hadharani, huenda nikauawa kama walivyouawa wengine wenye maoni na maswali mazito ya dini huko Ulaya. Si nia yangu kuwaambia watu wakatae maelekezo ya dini bali kujiuliza binafsi kama kuna mfuasi wa kweli duniani kwa kuwa sheria karibuni zote hatuzufuati lakini tunajiita wafuasi. Nina uhakika kama wewe kuwa nitashitakiwa nikitoa maoni haya hadharani kwa kuwa hatuna historia ndefu ya demokrasia nchini na elimu yetu ni changa na haina nafasi kwa watu kama mimi wenye maoni yanayouliza maswali mazito katika dini. Ni rahisi kunifunga mdomo kwa kunipeleka segerea au kuniua lakini kama binadamu hajiulizi, basi si binadamu tena. Kujifanya unafuata kanuni za dini siku ya Ijumaa na mwezi wa Ramadhani tu, wakati mwengine ni starehe tu halafu unaomba kusamehewa na Mungu ni kuwa Mwongo wa hali ya juu.

    Kama mimi sina haki ya kujiita Mwislamu kwa kuwa nakunywa pombe au kula nguruwe, basi wewe kuwezi kujiita mwislamu kama utanihukumu na mkono wako msikitini au kuniua kwa kuwa ni kinyume na sheria za dini. Hamna suluhisho katika swala hili. Watu wote tuna makosa, sio mla nguruwe tu. Kuna wafuasi wachache tu duniani wanaoweza kujiita wafuasi. Tuliobakia ni wafuasi wa jina tu.

    Shukurani.

    ReplyDelete
  71. AnonymousMay 06, 2009

    Anony may 04,2009, 1:16 AM

    Ahsante Mpendwa kwa majibu yako. Kama nikibahatisha kwa kutumia lugha ya jibu lako, nitasema kuwa wewe ni Mwanasheria.

    Yafuatayo ni maoni na majibu yangu:

    1. Sikubaliani kuwa kuzuia mimba kwa kutumia vidonge haikatazwi katika dini ya Kiislamu. Kwa kuwa unazuia kizazi cha Mungu kisiishi na kama unafuata aamri ya Mungu, huwezi kumwingilia katika kazi yake ya Kuumba. Kwa upande wa Wakatoliki, pia wanapinga upangaji wa uzazi kwa kutumia dawa au Kondomu. Labda itakubalika tu kama afya ya binadamu iko katika hatari kama hutazuia mimba kwa dawa (contraceptives) au upasuaji (abortion).

    2. Dhambi ni dhambi endapo unaamini Mungu. Kama huna imani ya dini basi huna la kuogopa mbele ya safari.

    3. Kuna sheria nyingi katika dini ambazo zinasaidia jamii kuishi bora na amani. Sheria kama kuwaangalia wazazi wako vizuri, kutoiba, na kadhalika. Hata sheria za katiba yetu ambayo ni juu kuliko sheria za Biblia au Kuran, zimeundwa na binadamu kwa kutumia mifano mizuri ya kanuni za dini kama kuadhibu wezi na kupima vifungo japokuwa nashukuru hamna kata kata mikono au kupigwa mawe mpaka kufa kama adhabu.

    4. Kwa kuwa demokrasia ni changa Tanzania na elimu ni finyu bado, nadhani utakubaliana nami kuwa mahakama itaangaalia ustawi wa jamii na amani zaidi kuliko kunipa haki ya kuwa na maoni ambayo yanaweza kuharibu amani kama kujaribu kuelimisha wananchi kuwa pengine hamna Mungu au kusema nguruwe si mnyama mchafu kama inavyosemekana katika dini yenu kwa kuwa wananchi wengi wa Asia wanakula kwa wingi na hawafi ghafla wala kupata magonywa ya ajabu kuliko magonjwa ya Ng'ombe kama Mad Cow Disease. Kuelimisha kuwa mnyama yoyote ni mchafu kama haishi katika mazingira masafi wala hapikwi katika mazingira masafi.

    5. Nipo na wewe 100 kwa 100 kuwa uhuru wa mwanadamu ni muhimu kuliko kitu chochote japokuwa mara kwa mara uhuru hunyimwa kama itahadharisha amani ya jamii. Nashukuru tu katiba ya nchi haifuati sheria nzito za dini kwa kuwa mimi binafsi nahisi kuwa kuna binadamu wachache tu duniani wanaoweza kuishi bila ya kuvunja sheria za dini zao kila siku. Pia, ni ukatili kumkata mtu mkono kwa kosa lolote au kupiga mawe mwanamke kwa kuwa amekamatwa na mpenzi wake kabla ya kuolewa.

    Kazi njema.

    ReplyDelete
  72. AnonymousMay 08, 2009

    We Anony may 04,2009, 1:16 AM;

    Katika upenzi wako wa kuongoa kitu kimoja, ni vizuri, wakati ukiendelea kutoa mawazo yako huru yasiyo lazima ukumbuke kuwa raisi mmoja hapa tz alitafsiri uhuru kwa kutumia neno rahisi RUKSA akasema.

    1. Ruksa kula nguruwe kwa atakaye, ikiwa anaamini ni dhambi au siyo.
    2. Ruksa kutokula nguruwe kwa asiyetaka, ikiwa anaamini ni dhambi au siyo.

    3.Na mistari ya dini inasema Mpe Mungu cha Mungu na kaisari mpe cha kaisari.

    Na kwa sababu wewe ni mtu kama ulivyosema katika kauli tofauti hapo juu, hamna tatizo, utakwenda paradiso tuu.

    ReplyDelete
  73. AnonymousMay 08, 2009

    Kauli nzuri ni hii,

    " Ya Mungu mpe Mungu na ya kaisari mpe kaisari"

    Watu wenye dini hufuata dini kumridhisha Mungu na pia hufuata sheria za serikali ili kuridhisha jamii. Na hawachanganyi mambo haya kama mtu mmoja hapo juu anayeshindwa kupambanua kati ya uhuru wa kufuata au kuacha dini.

    Kimsingi huyu ni mfuasi wa dini kadhaa (soma kauli zake) anajitahidi kushambulia dini kadhaa (soma kauli zake pia).

    ReplyDelete
  74. AnonymousMay 08, 2009

    We wa May 06, 2009 1:00 AM;

    Kwa pointi namba 2. unamaanisha watu wasiomwamnini Mungu ndo wasafi na hawana dhambi kabisa. Na kama kuna adhabu basi hawa hawatoadhibiwa? Ok, kila mtu, acheni dini ili mwende paradiso. Na ninyi wafuasi wa dini tukutane jehanam kwenye kuadhibiwa.

    Hii ni kinyume na haionyeshi uhaki wa Mungu.

    Kimsingi postings zako zoote zinaonyesha unataka kubadili chenza liwe chungwa.

    ReplyDelete
  75. AnonymousMay 08, 2009

    Muulize mwanasheria yeyote wa Tz, serikali inatambuwa sheria tatu.
    1)Statutory
    2)Religious (mirathi, ndoa, n.k.)
    3)Customary (mirathi, ndoa, n.k.)

    Utambuzi wa sheria za 2 na 3 haimaanishi utumikaji 100% bali kadhaa zinazotumika katika jamii mseto.

    Mfano, sheria ya kikatiba inapendekeza katika ndo ni mme mmoja mke mmoja. Kwa kuwa hii inafanana na imani ya kikristo, serikali ikaamua kutmbua mitazamo mingine kwa kutoa uhuru kwa waislamu kuoa mpaka wanne na kwa watu wa dini za jadi au wasio na dini kuoa idadi waitakayo.

    Serikali iliamua kuacha masuala ya ndoa kuwa ni urafiki wa kijamii na ikaona haina haja ya kumpangia mtu marafiki wangapi.

    ReplyDelete
  76. AnonymousMay 08, 2009

    Hebu tueleze unang'ang'ania uisalamu wa nini wakati unakataza nguruwe na pombe?

    Kwa nini usiwe mlokole au katoliki vinavyoruhusu?

    ReplyDelete
  77. AnonymousMay 08, 2009

    Ikiwa kuwa kwako mwisilamu ni uhuru wa kuchagua dini uitakayo basi umetumia uhuru wako vizuri lakini hujui kuchagua maana umekumbana na MISSMATCH. Angalia kemia vizuri wakati wa kuchagua, ukipata PERFECT MATCH ndo uamuae.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...