moshi ukionekana toka katikati ya jiji kama alivyoshuhudia mdau arden kitomari
moshi ukifuka toka kambi ya jeshi ya mbagala wakati mabomu yakilipuka na kuzua kizaazaa. hadi inaondoka eneo la tukio dakika kumi zilizopita globu ya jamii imehakikishiwa kwamba moto uliolipuka kwenye ghala ya silaha umeshathibitiwa na kwamba hali ni shwari. taarifa rasmi ya wangapi wamejeruhiwa na hasara gani imepatikana ilikuwa bado kutolewa. maafa pia yalikuwa bado hayajaripotiwa rasmi. askari shupavu wa jeshi la wananchi pamoja na polisi na kikosi cha zimamoto walikuwa wameshaingia kambini ambako masaa matatu yaliyopita ilikuwa ngumu kwani mabomu yalikuwa yakiruka kama hayana akili nzuri. mkuu wa mkoa wa dar mh. william  lukuvi amethibitisha kwamba hali kwa sasa ni shwari na wadau wanaweza kurejea majumbani mwao. majeruhi wengi wamepelekwa hospitali ya temeke wengine muhimbili. idadi kamili haijatolewa wakati globu ya jamii ikiingia hewani, ila habari zinasema  wadau watatu wamepoteza maisha na  takriban 100 wamejeruhiwa. shule ya st. anthony ni mojawapo ya majengo yaliyoathirika kwani vioo vya madirisha karibu yote yamevunjika, na nyumba kibao zimeharibika.
katikati ya jiji wadau maofisini wameambiwa waondoke maghorofani na kuelekea majumbani
penye zali kama hili vibaka hawakosekani. hawa wamedakwa wakisaidia kuanua nguo zilizoachwa nyuma wakati wenye nazo wametoka nduki
wadau wakiangalia mabaki ya mojawapo ya mabomu yaliyoruka umbali wa kilomita nne na kutua sehemu za mbagala kizuiani. ni moja ya takriban ya mabomu 12 yaliyolipuka na kutua uraiani. 
penye soo kama hili inabidi wadau watolewe mkuku. kweli amani mbaya. yaani penye soo watu wanakimbilia kuangalia kulikoni
afande akiomba watu watawanyike kwani sehemu hii si salama
askari wa faya ilibidi watulize boli maana kule kambini kulikuwa hakufikiki 
mtangazaji mzururaji wa clouds 88.4fm bonge akiwasili eneo la tukio huku akirusha mambo laivu
usafiri wa mbagala leo ulikuwa wa TZ 11 tu
wadau wakiwa juu ya daraja la mtoni wakiangalia mambo yanavyoendelea
askari wakilinda lango la kuingilia kambini

wengi ilibidi waunge mkono azimio la arusha kwani hakukuwa na usafiri leo kwenda ama kutoka mbagala

kinabibi wakipiga teke kujisalimisha
kama kawa, badala ya kukimbia wadau wamebaki kung'aa macho. 

kuona video ya mbagala leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. Hili ndilo tatizo la kambi ya jeshi kuwa jirani na makazi ya raia!
    mpaka sasa kambi za vikosi mbali mbali vya jeshi vimezungukwa na makazi ya raia wa kawaida ,ukiachilia mbali kutanuka kwa miji kuongezeka kwa wakazi katika maeneo ya mjini...lakini plan za makambi ya jeshi bado yapo jirani mno na makazi ya raia wa kawaida,na mara nyingi raia ndio wanaopata madhara yatoeapo matukio kama haya! wasi wasi na mashaka lazima yanakuwepo! si hilo tu bali na wanajeshi wenyewe wafanyapo mazoezi ya kijeshi nako kunawafanya raia kuwa na mashaka na wasi wasi unaojenga swali? la kulikoni na bila kupata jibu.inachangia maradhi ya kihakili.Maofisa wa mipiango miji lazima waweke mbali kambi za kijeshi kuepukana na matukio kama haya

    ReplyDelete
  2. Kaka Michuzi na team yako asanteni sana kwa kutuhabarisha. Watanzania pole.Hivi inakuwaje ghala la silaha linakuwa karibu na makazi ya watu,sipati jibu! nchi hii jamani!

    ReplyDelete
  3. mabomu yalikuwa yanaruka kama hayana hakili nzuri, michuzi umenichekesha kidogo mabomu huwa hayana hakili tangiapo na ndiyo maana yakaaminika ktk kuuwa

    polenileni sana kwa wale wote waliokubwa na mkasa huo

    ReplyDelete
  4. Kweli Wabongo naona sasa Amani IMETUKALIA Pabaya!!!!

    Yaani Mmeona kuna milipuko, tena ya Mabomu, + Moshi Unafuka, bado watu Wanakimbilia eneo la tukio kushuhusia!!! Duh. Ingekuwa Marekani hapo au Iraq, pangekuwa Hapatoshi jinsi ambavyo watu wangetimua mbio.

    Mungu Tunusuru.

    ReplyDelete
  5. PETER NALITOLELAApril 29, 2009

    NAJUA HUTAIWEKA LAKINI NI OPENI LETA KWA MICHUZI....HUNA JIPYA
    wewe michuzi umeeanza kuleta umalaya wa comment mbona tumeweka comment nyingi tu hujaweka hata moja. kama unawatu mahawala unawapenda basi wafungulie globu huu mchezo ni wa kitoto bulogu zote duniani zinaluhusu uhuru wa maoni sasa wewe unachuja nini ngoja nikupeleke utamu wakufundishe adabu, wewe mwenyewe ukiambiwa unatakiwa kuweka picha fulani za kiongozi filauni fulani utafulahi? sasa kwa nini unajalibu kuzuia maoni ya wanaume tena wa mbegu? nimekuandikia hii personally kwa sababu najua huna gust za kuiweka humu ila ukisoma ujumbe umepata, kazi kutoa ushuzi tu weka maoni ya wanaume. mashaka akikuandikia unakimbia kwenye mitandao kibao kuiweka hata kama hicho kingeleza cha kwenye kamusi hukijui sasa ya kwetu maoni yenye busara unayakaria matakoni.
    PETER NALITOLELA
    MUZUMBE UNIVERSITY
    MULOGOLO TANZANIA.

    ReplyDelete
  6. dar es salaam bado kuna ujinga wa hali ya juu kwa raia hasa nyakati za matukio ya hatari.kuna wanao kwenda kuzengea kujipatia riziki zao kupitia kwa waathirika,na kuna wanao kwenda kutafuta umbea tu ili wapate cha kusema.
    lakini ukweli nikwamba hili litakuja sikumoja kuwagharimu wahusika maisha!! yaani unasikia mlipuko badala ya kukimbia au kusimama ulipo unakwenda kuangalia nini kinalipuka,au kuchota mafuta kama ni tenker la mafuta au fuel[oil] station imelipuka!! huu ni upungufu wa akili ya kawaida wala sio umaskini! ila ikosiku watakiona kilicho mzuia kuku kukojoa!!
    je ukikuta ni askari amepata ugonjwa wa akili gafla anapiga watu risasi ukajikimbiza kwenda kuangalia si utajikuta nawewe ni muhanga? au ukute ni majambazi wamebanwa kisha ukajiingiza nao wakaamua kukuteka na kukufanya ngao ili wa sevu!! waelimisheni watu kupitia vyombo vya habari waache ujinga!!!
    HUKU HATA KIFURUSHI UKIKIACHA MAHALI HAKIOKOTI MTU,WATATOA TAARIFA KIKOSI CHA USALAMA WAJE KUKIHAKIKISHA KAMA NISALAMA AU LA! sio huko utakuta ndio nafasi ya vichomozi kuokota na kulakona!!

    ReplyDelete
  7. Isije ikawa ufisadi umeingia hadi jeshini,maana bongo kwa ufisadi tunaikaribia Nigeria.

    ReplyDelete
  8. Kuodno kambi za kijeshi toka maeneo raia si suruhisho la kuondoa hatari ya kulipukiwa na mabomu: swali la msingi la kushughulikia ni kuhakikisha kuwa usalama na utunzaji wa siraha hizo; Kwanza maghal ya siraha nzito yapo mbali kulinganisha ni vituo vya mafuta vya Dar E salaam. Pili Kambi za Jeshi Dar Es salaam zimesaidia kupunguza nguvu ya hewa ya CO2, maana toka eneo la mabibo tunapata hewa safi ya mti na misitu ya kambi hiyo, pia huko mbagala, Kibaha, gongo la mboto nk.
    Zaidi duniani hata kwenye miji mikubwa kama New York, silaha zipo tu na hata mitungi ya Nyuklia kama New York kwenye mto wa Hudison- huko Ossining, pia Manhattan project, ambapo bomu la atomic lilitengenezwa. muhimu ni kanuni za usalama wa kutunza siraha hizo.
    Pole wote mabo mmefikwa na dhaham hili.

    ReplyDelete
  9. Wewe anon hapo juu sijui kutoka morogoro huna adabu kabisa. huna sababu ya kumtukana michuzi namna hiyo. Michuzi hujitahidi sana kutoa maoni ya kila mtu. sasa wewe kama unaandika matusi basi ayatoe hivyo hivyo tu. kumbuka hii ni blog ya jamii na sio ze utamu ambako watu hawapigi mswaki wanasema chochote tu. mimi ni mmojawapo wa watoa maoni na kila ninapotuma maoni yangu haichukui muda tayari yanakuwa hewani. MICHUZI UDUMU SANA mzee wa ze fulanaz.

    mwisho, POLENI SANA WOTE MLIOKUMBWA NA DHORUBA LA MABOMU.

    ReplyDelete
  10. rosemery mlekwaApril 30, 2009

    sasa wewe peter nalitolela kama ungependa busara kwa nini unatukana? hata mimi kwa utalatibu wa comments zako nisingeziweka, unaonesha jinsi usivyo kuwa na hekima na akili timamu.

    ReplyDelete
  11. Hiyo ni salamu kwa wanaochokonoa muungano

    ReplyDelete
  12. Huyu Peter Nalitolea hapo juu, sijajua kama ndiye au amejivisha jina lisilo!
    Kwanza ujue kuwa hii blog inasomwa na watu wengi ndani na nje ya nchi wenye hekima zao,kama umejipima na kutambua kuwa mawazo yako na mwelekeo wako haukubaliki katika jamii ya watumiaji wa blog hii basi nenda katume huko kwenye blog zenu za matusi ya nguoni na huko ndiko utakakokutana na wenzako.
    michuzi ujue tu kuwa hii blog yako inaunganisha watu wenye hekima na ni Mungu alikupa maono haya ili kuwaunganisha watu walio mbali na vyombo vingine vya habari kupata taarifa za nchi yetu na kwa kuruhusu watu kama huyu aliyepost hiyo comment hapo juu kutakupunguzia hadhi yako rafiki.
    Zaidi tunakutakia kazi nzuri, na huyo ndugu tumsamehe maana hajui alitendalo.asante.Ni mimi Ndikupasya Malafyale Gwalugano.

    ReplyDelete
  13. anony no 1 wanaofuata kambi za jeshi ni raia na uvamizi holela na sio jeshi,hata airport walioifuata ni raia na pale lugalo walishaanza vamia kwa kweli ni ujinga wetu ndio unaotuponza. haifai kuvamia viwanja kama hujapewa na ardhi na kufuata masterplan, nani alianza jeshi a u shule ya msingi iliyoka ribu na jeshi,tuelimike kikarne ya 21

    ReplyDelete
  14. Peter Nalitolela, unaishi maeneo ya Mzumbe au unasoma Mzumbe??maana icho kiinglishi mie hoi...ulimaanisha guts ya spirit au gust(explosion? aya we nyie ndo wasomi wetu mtakaokuja kutuongoza baadae mtasaini mikataba bila kujua imekusudia nini.
    Nawapa pole watzee wenzangu waliopatwa na janga hili. Mithupu tunahitaji kueleweshwa kwani ni hatari wananchi kukimbilia maeneo ya hatari hasa kwa ishu kama hii ya mabomu.
    Mungu ibariki TZ na wasomi wetu wakina PITA NALITOLELA

    ReplyDelete
  15. poleni wa tz.. na hapo mzumbe university kuna umuhimu wa kuwapiga madent wao somo la nidhamu... peter umetia aibu chuo chako

    ReplyDelete
  16. MIMI NINAMFAHAMU HUYU PETER, NI KIJANA MZURI TU ILA AMECHANGANYIKIWA HIVI SASA NADHANI SABABU YA KUSOMA SANA BILA KUPUMZIKA. PETER HAJUI r NA l ZINATUMIKA MAHALI GANI, HUYU NI MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU; NA KIBAYA KABISA NI PALE ANAPOTUMIA LUGHA YA WENDAWAZIMU KWENYE BLOGU YA JAMII.MIMI NITAJARIBU KUONANA NAYE ILI NIMPE USHAURI NASAHA ARUDI KWENYE MKONDO WA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KAMA NITAWEZA KUUTULIZA WAZIMU WAKE.

    ReplyDelete
  17. SALA MAALUMU,,
    Ee Mola tuepushe na majanga kama haya
    Eee Mola tusaidie watu walioathirika wapone mapema na watulie,na wote waliofiwa uwatie nguvu zako
    Ee Mola wasaidie wote wenye nia njema,askari wetu,watu wa misaada wafanye kazi kwa utu na upendo wakielewa watu wamechanganyikiwa,
    Ee Mola turehemu na midomo yenye kunena maneno ya balaa juu ya Tanzania,
    Ee Mola warejeshe WATOTO wote walopotea majumbani,akina mama wanaomboleza sana km Rahel,
    Ee Mola wape VIONGOZI wa nchi Tz hekima na busara jinsi ya kupanga na kutatua matatizo/majanga km haya na kuwa na miundombinu mizuri,
    Ee Mola wape hekima viongozi wote wa JESHI la Tz jinsi ya kuepusha izi balaa mana tunazisikia tu nchi jirani MITUTU ya bunduki,
    Ee Mola tupe kuelewana kati ya RAIA NA VIONGOZI mana hasira imo ndani ya watu.
    Amen....

    ILI JANGA NI LA PILI KUTOKEA BAADA YA LILE LA GONGO LA MBOTO

    ReplyDelete
  18. Hii inaonesha hatari kubwa ya kuhifadhi makombora (missiles) karibu na makazi ya watu wengi.

    Haya siyo mabomu, bali nia surface-to- air missiles za kutungulia ndege, pia sitashangaa kama kuan surface-to-surface missiles ambazo zaweza kufyatuliwa na mzinga wenye midomo 20, hiyo kuruka kwa mpigo ktk uwanja wa vita.

    Itabidi kupanga mkakati mpya ktk mipango miji kwa kushirikiana na wizara zote husika.

    Poleni wakazi wa DSM

    ReplyDelete
  19. Ninamuda mfupi tu tangu nilipoanza kutuma comment zangu na hakuna hata moja ambayo haijarushwa.

    Nahisi wadau wengi wanaolalamika kutotolewa kwa comment zao labda zinafanana na huyo jamaa hapo juu.

    Tumia busara, sio mitusi kama hiyo hapa sio mahala pake, peleka kule kungine kusikokuwa na mchujo.

    Poleni wana Mbagala.

    ReplyDelete
  20. sasa watu walikuwaje evacuated??
    helicopter,mabasi,malori au ndo kila mtu miguu tu??JAMANI

    sina hamu kabisa,yan mabomu yanaluka makazi ya watu na mengine adi yanadondoka kilometerz??
    yan mtikisiko adi city center??

    naskia wajeshi walikua wanakimbia na mitutu barabarani,raia wacha wachanganyikiwe wakijua TUMEVAMIWA VITA!!wengine wanaweza kuwa waeshapata kichaa sasa,Mungu epusha

    kweeeeli mjeshi unafanya ivo?aya hospitals wauguzi wote nduki,majeruhi wamefika no huduma (pale mbagala health centre)
    elimu ya majanga hatuna wabongo,wala huduma ya kwanza!!
    asante mdau uletuma pichaz

    ReplyDelete
  21. ONA KAMA AO PICHA #3 TOKA JUU
    YANI NDO WANAKODOLEA KABISA IYO MIDUDE

    afu ikilipuka,sijui tunasikitika/tunalia??

    aya ilo bomu kubwa lilishadhibitiwa au uzushi tu???

    mnaboa sana

    ReplyDelete
  22. wee annon unaesema eti city center wavivu tu,ulikuwepo eneo??

    vioo vyote vilikua vinapukutika km havina akili zuri,yale majengo yetu ya Dar.
    yan nasema ivi,siku tetemeko lapita apo city wee utaona maajabu ya musa na farao

    majengo hayajafata kabisa kuhimili matatizo,mitikisiko!!

    kazi ipo na infrastructure za bongo

    ReplyDelete
  23. poleni sana kwa yaliyotokea,
    naungana na anony wa 3:52 AM.
    muhimu ni kufuata sheria za usalama na utunzaji wa silaha mbalimbali,ila ajali huweza kutokea.
    Mazingira ama makambi ya jeshi ni mazuri sana,salama, kuna utaratibu safi na utunzaji wa mazingira ni namba moja! ndiyo sababu popote kambi ilipo,raia watasogea na watajenga tuu! ukiangalia,maeneo yote hayo yalikuwa misitu minene wakati jeshi lilipo establish makambi lakini with time wananchi wamesogea na wengine wamevamia kabisa! wakiambiwa waondoke hawataki na wanaenda hadi mahakamani!
    makambi kuwepo mjini siyo tatizo,maana hata nchi za wenzetu hilo hilo lipo tena wana mambo ya hatari zaidi ya maghala ya silaha!,
    Ila nadhani kuna umuhimu wa
    kuwafundisha watanzania "raia" mbinu za awali za medani na jinsi ya kusaidia na kujisaidia panapotokea balaa lolote.kwa sasa watz wengi bado "bongo lala" -penye hatari sisi tunakimbilia,utayari na kutambua hatari ni karibu na sifuri
    -JKT irudishwe upya kuondoa uzembe unaojionyesha na kuweka watu fiti kwa mujibu(kupiga msasa).
    Tusipojali haya,it will cost us more than we can imagine!
    -waukae

    ReplyDelete
  24. wewe michuzi wewe
    kama hii ni blogu ya jamii kwanini uchuje komment na uchague baadhi za kuweka na zingine si za kuweka au kwazababu komment zinakukosoa wewe
    umeibania komment yangu ile niliyokuambia wewe na waandisha wenzako mnapotosha jamaa kwa kusema vifo ni watu watano wakati mpaka jana saa 2 usiku kuna maiti ishirina zilipatikana kwenye mtoi kule kizinga mbagala

    heshimu taaluma yako wewe unajiaibisha buree wewe na hao vibaraka wenzako wachache

    ReplyDelete
  25. Wewe Mdau umekosa adabu tena adabu hasa hujafundwa ndio sababu unaongea ovyo...Maneno machafu yanakutoka hata hufikirii huna busara hufai kuheshimiwa. Ungekuwa na busara ungemuuliza tuu swali kwani inatosha...Maneno au maswali ya kiungwana yapo mengi tuu na mtu akahisi isia zako (zikamgusa) sio hadi utukane...

    We mdau labda uliandika PUMBA point ndio maana akazichuja..usimlaumu...Pia wapo wengi sana wanaochangia mbona comment zao zinaonekana kwanini wewe zako zisionekane? Labda uliandika kama hivi ulivyoandika bila kuzingatia adabu..Soma hapo juu katika Blog maneno yanayopita imeonya nini...Hii ni blog ya heshima bwana usituletee uchafu ndani ya blog. Kama ni mdomo wako mchafu huko huko...

    Please mdau...Naomba urekebishe kauli zako.

    Mdau H.

    ReplyDelete
  26. Watu wengine bwana....Nyie ndio mafisadi mnafanya uovu then unataka uwe siri...Then inaonekana wakati ukiandika ulikuwa ndio umekurupuka kitandani tena kwa kuamshwa labda na bomu sababu hukuwa unajielewa kabisa...Kama vile hukupiga mswaki??!!!Fufufufu..

    Hk

    ReplyDelete
  27. Hivi wewe anonymous wa apri 29:2009 unajiita Peter na unasoma mzumbe, hv kichwani umetimia?

    Hata ningekuwa mimi nisingeruhusu matahira kuchangia . kwa maoni kama hayo uliyotoa hakuna hakuna yoyote wa kuyaweka hewani.

    Unaharibu sifa ya Mzumbe. na inawezekana we ndio mtuma picha za mzumbe kwenye blog wa wandawazimu wenzako ya utamu.?

    Hii ni blog ya jamii ya watanzania waliostaarabika

    mdau
    k/koo shimoni

    ReplyDelete
  28. MICHUZI, SEMA MAAFA YA MBAGALA SIO "LIBENEKE LA MABOMU" AU SIJUI "SOO HILI." WATU WAMEPOTEZA MAISHA, HESHIMU AJALI KWA LUGHA STAHILI. WEWE NI MWANDISHI WA SIKU NYINGI SANA LAKINI HUPATI CLUE! (ILA KWA KWELI WALE ASKARI WA FAYA "WALIAMUA KUTULIZA BOLI" KABLA YA KUURUKIA MOTO WANACHEKESHA....)

    HALAFU UMEWAMALIZA HAO WANANCHI WALIOKAA "WANANG'AA MACHO BADALA YA KUKIMBIA." WEWE MWENYEWE MBONA ULIKUWA MBELE YAO UNAWAPIGA MANEPU BADALA YA KUKIMBIA?

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 04, 2009

    bwana michuzi mimi naipenda sana blog yako. ninasikitika sana kwa wewe kuweka kwenye hii blog maoni ya matusi kutoka kwa huyo peter nalitolela. hii blog yako wakati wote imejaa maoni ya watu wenye busara kwahiyo tafadhali usiwape nafasi watu kama hao. hawa ni watu wamechanganyikiwa na maisha. peter, you must be very unhappy with your life if not you are on drugs. kama kweli uko university concentrate on your studies na acha kutukana watu.

    ReplyDelete
  30. Aya mabomu ni ajali au kuna mambo mengine tusiyoyajua. Je tulijifunza nini kwa tukio la mbagala au tuseme viongozi wetu walipounda tume za kuchunguza mabomu ya mbagala walipewa maelezo gani. Je maelezo hayo yaliwasaidia nini endapo sasa mambo ya Gongolamboto yanaendelea kutia aibu nchi na kumaliza ndugu zetu. Nani awajibike hapa au kama kawaida inaundwa tume nyingine!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...