














Habari Kamili
Mlimbwende Iluminata James kutoka mkoani Mwanza leo usiku ametwaa taji la Miss Universe Tanzania kwa mwaka 2009 na kujikatia tiketi ya kuliwakilisha taifa katika michuano ya dunia itakayofanyika baadaye mwaka huu katika visiwa vya Bahamas.
Iluminata ambaye anampokea taji hiyo mwanadada nyota katika fani ya mitindo nchini Miriam Odemba alifanikiwa kutwaa taji hilo baada ya kuwashinda walimbwende wenzake 19 ambao nao walikuwa wakichuana vikali kuwania taji hilo.
Shindano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es Salaam , mbali ya mashabiki wa masuala ya ulimbwende kupata burudani ya kuonyeshwa mavazi na miondoko ya ‘catwalk’ kutoka kwa washiriki 20 pia walikongwa nyoyo zao na burudani safi ya muziki kutoka kwa msanii nyota wa Bongofleva , Ambwene Yesaya ‘Mzee wa Comercial’ , mwanadada Wahuu kutoka Kenya anayetamba na wimbo wa ‘Sweet love’.
K abla ya hapo bendi ya Diamond Musica chini ya Allaine Mulumba ilikuja na wimbo wao maarufu wa ‘Mapenzi kitu gani’ na kufuatiwa na sebene la uhakika na burudani hiyo ilihitimishwa na ngoma za utamaduni kutoka kikundi cha Albino Revolution Cultural Troope.
Mbali na Iluminata washindi wengine katika fainali hizo za Miss Universe Tanzania ambazo zilihusisha warembo kutoka mikoa mitano ya Tanzania , Arusha , Mwanza , Dodoma , Morogoro na Dar es Salaam walikuwa ni Evelyne Almasi ambaye alichukua nafasi ya pili na hivyo kujipatia nafasi ya kushiriki kwenye shindano la Miss Earth.
Mwanadada Hidaya Maeda ambaye alishinda nafasi ya tatu katika kinyang’anyiro hicho, yeye ataliwakilisha taifa katika shindano la Miss International baadaye mwaka huu, na nafasi ya nne ilikwenda kwenye Zeinab Kianda na Gisela Tarimo alinyakua nafasi ya tano.
Miss Universe Tanzania 2009 mbali ya kujipatia tiketi ya kushiriki kwenye shindano la dunia pia alizawadiwa Sh milioni tatu , nafasi ya kusoma kozi ya lugha ya kifaransa kwa mwaka mmoja katika kituo cha Alliance Francaise pamoja na kupatiwa vipodozi vyenye thamani ya Sh 500,000 na duka la Shear Illusion .
Majaji wa shindano hilo walikuwa ni pamoja na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Al Sharyamaa Kwegyabir , mwanamuziki John Kitime,Masoud Kipanya , Mbunifu wa mavazi Ally Rhemtullah, Maria Sarungi Tsehai , Amit Patel kutoka kwa wadhamini wa shindano hilo kampuni ya Samsung ambao waliongozwa na jaji mkuu Rosie Motene kutoka Afrika Kusini ambaye ni Muigizaji nyota na Mtangazaji wa kituo cha Studio 53.
jamani mishel obama ndiye anayetoa zawadi au ni macho yangu.
ReplyDeletemadau!!
huyo miss sarungi simjui. lakini nampongeza kwa kufanikisha hii miss universe tz...well done next time get some big names from africa 'n outside africa as judges. well done again.
ReplyDeleteSasa huyu Maria ana hangaika nini nyuma ya ma jaji au alikua anataka kuhakikisha mtu wake ana chaguliwa?
ReplyDeleteAi leti picha nzuri bibibie , maana kama umeandaa mashindano kwa level ya kimataifa unatakiwa kuwaachia majaji wawe huru ,bila kupita pita kuongea nao , maana tuna kua na uhakika wamesha pewa semina kabla ya show , so hawaitaji msaada wowote siku ya show wa kuelekezwa .
Siwezi piga picha eti Donald Trump ana pita pita nyuma ya ma jaji na kuongea nao siku ya show.
IBRA BUKENYA aka KYAKALONGO NAKUONA IN WHITE BIG UP MWANA
ReplyDeleteam agreed with da guy hapo juu..haipendezi kuingilia kazi ya majaji..next tym maria jifunze kutulia kitini or uwe jaji mwenyewe kama unashindwa kutulia.othrwz kitu kipo bomba
ReplyDeletelabda anataka kujua wamefikia wapi, atoe updates, kwa wageni, IM JUST SAYING......Maana nimeona kama alikuwa na mikrofoni pia, I dnt know....labda kuna sababu ya msingi yuko hapo nyuma kwa majaji ...
ReplyDeleteNaomba kuuliza huyu MARY SARUNGI, ndie yule aliesoma Zanaki miaka ya 90, SHOMBE hivi, au majina tu, baba ake nadhani alikuwa Profesa, au majina tu yanafanana?.
ReplyDeleteVinywaji vilikuwa bure nini...Maana huyo mkorea yupo BWAAAAAAAAAAXXXX!!!!
ReplyDeleteMdau, 8:11am
ReplyDeleteYea, Maria went to Zanaki in late 80's I think, that's her, Mzee Sarungi used to be Waziri wa afya pia, if you remember well. Maria has changed a lot, she looks even more pretty.
acha kubania hoja za watu zenye maana hawa mamisss nao wamezidi kwa tabia mbaya watu tunaandika halafu unatubania poa
ReplyDeleteAsante Mdau-Zanaki Product, kwa info, kwa kweli amebadilika sana ndo maana nilikuwa sielewi vizuri,kama ni yeye au macho yangu,asante.nakumbuka wakati anamaliza shulemi ndo nilikuwa naanza form one.thanks.She is cool.
ReplyDeleteKwa wadau wa Zanaki kapo juu. mnacho zungumza ndio nilikuwa nakiwaza .
ReplyDeleteNinapenda kusema katika watu wano zeeka vizuri mmoja wapo ni huyu Maria Sarungi
Kwakweli mtakubaliana na mimi haswa kwa wanao mjua hapo zamani ni tofauti na sasa ,tena ka kiasi kukibwa sana , yani ni amekuwa mdada na amependeza zaidi kupita zamani.
Na nani naweza hisi siku moja Maria ata shughulika na urembo na kuweza kufanikisha vizuri ?
Maria nimesoma naye Oysterbay Primary school ,alikwua madarasa matatu mbele yangu na alikwua na Siter wake anaitwa Verocica ambaye ndio tulikuwa tuna muona mzuri kupita maelezo .
Hongera sana Maria ,kazi nzuri na unazidi kuwa mrembo .
JAMANI KWA TAARIFA YENU WOTE HUYO MSHINDI WA PILI ANAITWA EVERLYNE AMASI NA SIO ALMASI,
ReplyDeleteKAKA MICHUZI REKEBISHA HILO KAMA UTAWEZA.
huyu maria sarungi yuko na mwenzie wamefanana sana, alafu mmoja ndio alikuwa pale zanaki tena alikuwa dada mkuu, waliosoma naye wanasema alikuwa mnoko sana na walidhani atakuja kufanya kazi wizara ya mambo ya ndani kumbe yuko kwenye fani ya urembo.
ReplyDeletekeep it up mrembo!
jamani natafuta mchumba sasa huyu dada mwana wa sarungi vipi!!
ReplyDeleteMdau wa 8:16pm
ReplyDeleteKama sijakosea, I think ameolewa but, she's very pretty.