Home
Unlabelled
polisi waokoa mtuhumiwa wa wizi asibanikwe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Jamani Watanzania, kwa nini tunawachoma binadamu wenzetu, mbona wezi wa EPA. tunawapigia makofi.
ReplyDeleteHongera polisi kwa kuokoa maisha ya kijana huyu. hizi ni njaa na umaskini uliosababishwa na CCM.
Tusijichukulie sheria mkononi. sio juzi wafanyabiashara watano wameuwawa huko kanda ya ziwa kwa kudhaniwa ni majambazi.
sasa hizi tabia sio nzuri, tunawauwa ndugu zetu kwa kesi za kijinga kama simu, kipochi n.k wakina R....m na wenzao tunawaacha na kuwaita mashujaa.
Heko kamanda kova. ongeza bidii upambane na wanojichukulia sheria mkonon.
mdau
K/Koo Shimoni.
aaah jamani wa Tanzania,nadhani kabisa mtu wa kuchoma moto ni Fisadi huyu ni njaa iliyosababishwa na mafisadi ndo inamfanya atake kuchomwa Hebu kuweni wastaarabu na wenye akili timamu sasa.kamata Fisadi papa Choma au fisadi Nyangumi sio hawa vibaka.
ReplyDeleteMichuzi sasa hebu tuonyeshe Fisadi akipewa kibano ya vibaka acha Kwanza tupumzike au yule anaenunua Shahada za upigaji kura ndo inatakiwa wachomwe
ReplyDeleteHuyo askari aliyemuokoa mwizi ni True Hero. Nuyu ni Tanzania One!
ReplyDeleteMuangalie jinsi alivyokuwa anajichukua kwa uhakika na ukakamavu. Utulivu wake na self controll ya hali ya juu aliyoonesha ni mfano wa kuigwa.
Aksante Kijana. You have made my day.
At least he gets someone to thank for being alive - other than God, of course...
ReplyDeleteI am seriously sometime wonder, why we are such terrifically hostile towards the pocket pickers, in such a way we are exceedingly going far to torch a fellow human on FIRE, while the vingunge wa chama, wabadhirifu ktk vitengo vya serikali, nk are getting away lightly, in matter of facts, we do see them as the BEST OF WAJANJA, and we do sometime honor them in doing that!
ReplyDeleteWhile they deserve pretty much capital punishment, for put this petty thief on desperate situations,
Here is my point,
Billions stolen, could be used to put people back to work,
New technical schools,
New business expansion around countries,
get rid of government bureacrat for small business...
New and enhancing Hospitals na nk.
Why we dont talk them on the same level, as this kibaka, they(vingunge) cause us more incremental harm to us and the comming generations for years to come....and we dont do justice by inflicting a such harsh punishment, including death to be precise.
duh havi... mwenyenzi mungu yupo!
ReplyDeleteumenifanya niangushe chozi kwa huzuni kubwa,,,asa izo comments zako ktk kila picha....
ReplyDeletejaman aya maisha sijui niseme nini iki kinachofanya watu wapate shida ivi?ETI WADAU
uyu kijana hajapenda kuwa ivo angepata opportunity km sie kupata shule na kazi au kujiajiri angekua km sie tu wenye izo nafasi
i wish ingekua umetoa angalizo.
anyway
Watu wanaiva tu ndani ya jua kali Bongo, nyama chomaaa..!!, du sheria mkononi. Mi chichemi ukiwaacha wanakuua, ukichoma unavunja sheria. kama huyu jamaaa kesho atakua mtaani anatafuta wabaya wake.
ReplyDeletejamani jamani jamani,hapa sasa ndio uzalendo huwa unanishinda kwa nini watu wanakuwa wakatili hivi?hii ni aibu kwa nini huyo mtu asipelekwe polisi?,binadamu mnakuwa na roho ya mnyama!.kwa nini tumhukumu mwenzetu,wakati wote safari ni moja kana kwamba nyie ambao hamjaiba hamna dhambi na hamtakufa!
ReplyDeletePicha nzuri sana, maelezo safi sana...mpangilio super!! kama movie vile!! habari picha bomba kabisa!! tunataka mambo kama haya!! siyo maelezo na text nyiiiiiingi pila picha!!
ReplyDeleteDuh eee banaaa..ehh...hii kali...sijui kama jamaa atakuja iba tena!
ReplyDeleteMUNGU MKUBWA JAMANI KWELI KUIBIWA KUBAYA LAKINI SI TUFIKILI PINDI TUNAPOTOA ADHABU SIDUMISHI WIZI BALI KUMCHOMA MUHARIFU KWA MOTO NAMNA HIYO SI UBINADAMU JAPO WIZI NAO SI UBINADAMU.MIMI SI UNGI MKONO ADHABU YA MOTO KWA KOSA LA KUIBIWA SIMU,BINADAMU TUNASAHAU SOTE NI WAHARIFU MBELE YA MUNGU KAMA UKUIBA BASI KUNA KOSA LENGINE UMELIFANYA
ReplyDeleteJAMANI UKO NYUMBANI TUSIWABANIKE NDUGU ZETU TUWAFIKISHE MBELE YA SHERIA
Huyu Dogo ni mwizi mkubwa mitaa ya Kinondoni, jamaa walikosea wamemwaga diseli hapo ingekua petroli tungepata ndafu saaafi.
ReplyDeleteHawa wazee muda mwingine wanazingua,wanambeba kisha wanaenda kumuachia kwani ushahidi hawana dogo akifika mahakani anaachiwa!Kiboko yao moto tu
It is excellent!!! Ata vibaka wengine wakiona nathani kidogo moyo utaenda pwaaaaa!!! Ila jamaa aliewasha kiberiti atakuwa na roha ngumu yani ya kinyama. Kumbanika binadmu mwenzio kama kiti moto!!!
ReplyDeleteAta askari wangemuachia aende zake tu, ilo litakuwa fundisho tosha.
Wangesubili aungue kidogo ili askilizie utamu wa kubanikwa
Kaka Michuzi hiyo habari kwa Picha imetulia ila inasikitisha.Binadamu wamekuwa kama "wanyama wa mwituni" iweje umchome moto binadamu mwenzio kwa maslahi madogo ya kidunia? Sitaki kujua alichoiba, kwani hata kama aliiba nini lakini kufikiria kumchoma moto ni ujinga na upuuzi usioingia akilini kwa mtu mwenye busara,bado tuna kazi kubwa ya kuelemishana kuhusu haki ya kimsingi ya kuishi.Hongera sana POLISI kwa kumuokoa huyo kijana.
ReplyDeleteTHE
KOP
CANADA
kaka ahsante kwa up date za bongo
ReplyDeletelakini kaka hawa jamaa wanakera sana tena sana kama hujawahi kuhibiwa ndoo unaona huruma lakini mimi sina huruma hata kidogo yalishawahi kunikumba kaka. napenda sana blogg ya jamii kwa sababu ina taharifa tofauti, wengine kucopy na kupest.
Wizi ni wa aina yoyote ni mbaya naukemea, vibaka wa kawaida ambao hawaatarishi maisha ya mtu wanastahili mkon'goto ili wajifunze na sio kutoa uhai wao kama haojamaa walivyotaka kumuuwa kwa moto.
ReplyDeletekitendo walichotaka kufanya cha kuuwa ni kibaya zaidi ya huyo mwizi alivyofanya, sisi ni binadamu tumepewa uwezo wa kupambanuwa.
angelikuwa jambazi ambaye alikuwa na nia ya kutoa roho ya mtu ningeafiki kabisa achomwe moto. ila inaonekana alikuwa ni kibaka tu.
je nyinyi mafisadi mnaoiba pesa za walalahoi serikarini mpigwe kiberiti?????
Huyu kama ataiba tena,kalaaniwa. Lakini hata hivyo nani ksema mwizi achomwe moto, hiyo hukumu mumeipata wapi? Mwizi mkateni mkono,na wewe unayemkata mkono uhakikishe hujawahi kuiba! Nani ambaye hajawahii kuiba, fikiria unavyokwepa kulipa hela kwenye daladala,unavyopiga chabo nk.
ReplyDeleteKitu nilichojifunza,kama adhabu kali zitakuwepo, uhalifu utapungua saana, lakini kama kuna uchochoro wa kukwepa hizo adhabu, sidhani makosa kama wizi, rushwa na ndugu zake utaisha!
M3
Mzee hapa naona umechemsha, hivi ubinadamu uko wapi jamani? mtu kaiba nini mpaka apate hili pigo la aina hii, mimi nilidhani mambo haya yalishaisha enzi hizo kumbe bado yanaendelea?
ReplyDeleteThe photos are too too graphic man, i know you have to show them for everybody to see, but to be honest, for some of us, it is difficult to actually look at them even for a single second. I know people will say that they are there to be seen. Unless otherwise the guy has killed or tried to kill someone.
P.E.D
inaelekea huyu jamaa ni member wa CCM (pls mean what i mean "Chama Cha Mafisadi" not otherwise)... mbona gali lililokuja kumchukua lin limefunikwa bendera ya GREEN? any way kwa mtu asiyewahi kujeruhiwa na vibaka atamuonea huruma utamsikia aah mbona mafisadi hawachomwi moto? wee bwana wee hawa vibaka wakikuingilia usiku lazima wakucharange na mapanga, visu, nondo, spoko,.... hawa sio watu kabisa... ukikamata choma moto kumpeleka police ni kupoteza mda
ReplyDeletechezo kamili yaani mleta habari kwa picha umekamilisha movie lote hiyo ndo dawa yao
ReplyDeletehii ni sheria ya dini gani?
ReplyDeleteHuu ni unyama kujichukulia sheria mikononi na kutoa hukumu ya kifo kwa vibaka. Inatuondolea ile kujisifia eti watanzania tu watu wazuri sana mbele ya mataifa mengine. Je unafahamu kuna nchi nyingine hata kuchinja kuku ni kosa, considered animal brutality?
ReplyDeleteInajulikana wazi vibaka ni watu wanaosumbua na mara nyingi wakifikishwa polisi au mahakamani huwa wanaachiliwa. Lakini hai justify wananchi kujichukulia sheria mikononi na kutoa hukumu ya kifo kwa kuchoma mtu moto.
Kumbuka huyu ni mwanadamu kama mimi na wewe ana wazazi ndugu na jamaa zake. Ni kosa kwa shughuli anazofanya lakini huyu pia angeweza kuwa ndugu yako ungejisikiaje kumuona katika hali hiyo? Ugumu wa maisha unatufanya wote mwizi na wananchi kuwa wanyama. Pia maafa ya sheria za mikononi kama hizi watu anaweza kuwa na chuki binafsi na wewe wakasingizia tu mwizi. Swali la mwisho je alikuwa na silaha na alidhuru mtu yoyote kwa maana ya jambazi? Serekali ingechukua hatua kali kwa wananchi kama hawa wanaojichukulia hatua mikononi.
Jamani mimi ni mwanamume, nipo majuu shuleni. Machozi yamenitoka kwa huruma kwa sababu, kijana huyu amekuwa mwizi akitafuta namna ya-ku-survive, na ameishia kuchomwa anachomwa moto. Wakati huo huo mafisadi wenye pesa za kufuru, za wizi ambazo hawajui hata namna ya kuzitumia wanaendelea kula maisha ya raha. Mafisadi hao hao ndiyo waliosababisha indirectly kijana huyu awe mwizi. Jamani hii kweli inauma sana. Kijana huyu angepata shule na ajira pengine asingekuwa mwizi. Jamani hii ni simanzi kubwa. Tusiliangalie suala hili juu juu, tuliangalie kwa undani. Tunajenga jamii ya namna gani???? This is "Unbearable to look Shame of the Nation........."
ReplyDeleteKWA HAKIKA HII STORY NI YA HUZUNI SANA, KILICHINISHANGAZA HAPA, KWA NINI IMEANDIKWA KAMA VILE NI MCHEZO WA KUIGIZA? KUMBUKA MICHUZI HAPA UNAZUNGUMZIA MAISHA YA MTU YALIYOOKOKA JUST KWA TUNDU LA SINDANO BRO!! NA UKIANGALIA KIMSINGI HUENDA ALIKUWA ANATAKA KUPATA HELA YA KULA TU, WEZI WAZURI WENYE MAMILIONI HATA SIKU 1 HUTASIKIA WAMECHOMWA MOTO AU KUPIGWA MITAANI, UTASIKIA STORY TU KWENYE VYOMBO VYA HABARI NA KESI HUISHIA HIVYO HIVYO TU!! JAMII SASA HAINA BUDI KUBADILISHA MTAZAMO, NA HABARI KAMA HII IWE NA UZITO WAKE, HATA MNYAMA HUTHAMINIWA IJE KUWA BINADAM??
ReplyDeleteTatizo la wa-tz wanaonea wezi wa kuku walioiba Mabilion bado wanatesa mtaani. Wangemfania fisadi mmoja hivyo wote wangejisalimisha na kurudisha mabilioni yote. Tu ashumu hiyo ni catalyst na warning kwa Mafisadi.
ReplyDeleteThese pictures have broken my heart. If you have a son, and imagine the "system" has transformed you son into this, by denying him good education and employment..... This is unbearable pain and grief down to the nerves.
ReplyDeleteHebu tufikiri kwa undani na kujiuliza, Jee ni nani wa kulaumiwa???
Kijana, Mzazi au Taifa?
Amshukuru sana mungu kwa kuwa nae kwani alikuwa amesha kufa.Kumbukeni Mungu yupo kila mahali na anatulinda kwake wote tuna haki hata wezi.
ReplyDeletesheria ya DINI GANI????
ReplyDeletewee annon acha kuchokoa watu umu
ila jibu ninalo,sema nachelea ugomvi umu bloguni
hahahahahahahhaha
hamjawahi kuibiwa!!
ReplyDeletengojeni
Bro michu... story imetulia.. imepangiliwa vyema.. nampa hongera jamaa aliyefanyakazi hii.. yaani habari imeeleweka vizuri sana japokuwa ni ya kusikitisha.. namna hii ya utoaji habari ndio hasa tunahitaji
ReplyDeleteNyie mtabaki mnaandika wee kwenye internet kuwa wakuchomwa ni mafisadi...Hao mnaowapa ujumbe huo, ni asilimia ndogo sana they are aware of the impact and implications za mafisadi! Hata wakijibizana kwenye ma-tv yao, wao wanaona kama a playfull drama. Mbaya wake yeye ni yule aliyemkwapulia elfu tano yake iliyokuwa kibindoni aliyokuwa anaenda kufanya maarifa ya kupeleka mboga nyumbani kwa familia yake.....hayo ya mafisadi mhangaike nayo wenyewe kwa kuwa yeye hayamsaidii kwa lolote.
ReplyDeleteNyie mtabaki mnaandika wee kwenye internet kuwa wakuchomwa ni mafisadi...Hao mnaowapa ujumbe huo, ni asilimia ndogo sana they are aware of the impact and implications za mafisadi! Hata wakijibizana kwenye ma-tv yao, wao wanaona kama a playfull drama. Mbaya wake yeye ni yule aliyemkwapulia elfu tano yake iliyokuwa kibindoni aliyokuwa anaenda kufanya maarifa ya kupeleka mboga nyumbani kwa familia yake.....hayo ya mafisadi mhangaike nayo wenyewe kwa kuwa yeye hayamsaidii kwa lolote.
ReplyDeleteunamwibia masikini unategemea nini?
ReplyDeleteKWA PICHA HIZI , TANZANIA=ANIMAL KINGDOM
ReplyDeleteJamani tusiwalaumu wananchi kwa nchi kujichukulia sheria, Serikali yenyewe imeshindwa kuchukua sheria mafisadi na kuhalalisha mauji kwa kusema ukimkuta mtu anafanya kosa muhukumu hapo hapo(Rejea mauji ya albino). Sasa unatarajia hukumu ya wananchi wasiokuwa na jela iwe nini?, ni kuua tu.
ReplyDeleteSometimes hata polisi huwa wanalalamika wakimkuta mtuhumiwa bado mzima utasikia aaah kumbe bado mlikuwa hamjamaliza kazi, wanatusumbua sana hawa.
Serikali itambua kuwa njia pekee ya kumaliza wizi ni kwa wananchi kuwa ajira za uhakika, sasa watu wachache wanaimaliza nchi huku wakipewa ulinzi na UWT pamoja na polisi majumbani kwao na kuacha wengi tukiwa hoi na kuamua kuibiana hata vidogo tulivyo navyo na kuvipata kwa mbine Inatia hasira sana.
Mi nazani watu huwa munasomaga habari kuwa watu wanaibiwa kwenye foleni za magari? Hawa vibaka wanatusumbua sana, wanatuibia hata kodgo tulicho nacho, sisi masikini kama wao, ila wao hawataki kubeba zege kama sisi. Fikiria nimetoka kubebe zege, halafu unaniibia helfa tatu niliyopata, nimepigika siku mzima, kweli nitakuacha?
ReplyDeleteHawa wa EPA kwa kuwa hatuna uwezo nao, siku yao ipo nao tutawatia moto, akina MABUTU na IDD AMINI nao arobaini zao si zilifika?
Kwahiyo wale wanaiba kidogo ambacho mimi nimepiga na zege tukimpata moto. Hao MAPAPA nao siku zao zikifika nao MOTO. Munakumbuka yule jamaa wa Royal Bank of Scotland, waingereza hawakuchukua hasira MIKONI? au mwatusema sisi tu, hawa tunauwezo wakukamata, ndio maana tunawapa kipigo. Ngoja uibiwe na hawa jamaa, mwenyewe utaunga na sisi.
huu ni unyamamuliopita kiwango kwanini watu wanependa kujichukulia sheria mikonnoni.
ReplyDeletehivi jeshi letu la polisi kazi yake ni nini? weel naweza kuelewa ni kwani nini watu wanajichulia sheria ni sababu ya polisi kushindwa kufanya kazi yao.lkn hata hivyo sio ndio sababu ya kujichukulia sheria hizo za kinyama
kama kweli mambo haya wana yafanya kwa kuwachoma watu ambao maybe wanaiba kutoka na ugumu wa maisha ambayo serikali yao haifanyi chochote kuwasaidia watu hawa mimi nafikiri wangewachoma kwanza mafisadi wote kwanza ambao they walking in the streets freely kungekuwa hakuna huu upuuzi unaondelea nchini kwetu yaani inasikitisha
sijui sisi tuenda wapi maana naona baadala ya kwenda mbele sisi tunarudi nyuma.
THIS IS AGAINST HUMAN RIGHT!!!!!!!!!!
Askari mkakamavu sana huyu.
ReplyDeleteKakuta wananchi wenye jazba wanamchoma mtu huku wakiwa wamebadilika na kuwa wanyama kabisa. Wengine wanamchomachoma kwa kijiti huyo mwizi na karibu wote wanapiga makelele. Kweli ni mazingira ya kutisha.
Lakini angalia alivyoweza kumchomoa kibaka kwenye moto. Nadhani wale wananchi walipigwa na butwaa.
HAKUNA MTU ALIYE JUU YA SHERIA. HAPA KUNA KOSA KUBWA SANA. MICHUZI AMEWAPA POLISI 'EVIDENCE' ZA MTU ANAYETAKA KUUWA KWA KUKUSUDIA, TENA MBELE YA UMATI WA WATU! POLISI WA TANZANIA WAPO WAPI? MBONA WANANCHI WANAJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA HAKUNA ANAYEWAGUSA? MUNGU IBARIKI TANZANIA.
ReplyDeletekama mwizi "kibaka" kaiba ni halali kuchomwa ilikutokeza vvibaka, ili mradi tu amekamatwa live anaiba.
ReplyDeleteMichuzi,
ReplyDeleteMimi nina maswali mawili, je ni wewe uliyepiga hii picha? Na je nini wewe uliyeandika kichwa cha habari na maelezo ya picha zote?
Kama ni wewe uliyefanya hivyo nakusifu kwa uandishi wa habari kwani umeripoti habari kama ilivyo lakini pia aibu kwako kwani umeripoti kama ni kitu cha kushangalia. Anagalia kitangulizi cha picha “polisi waokoa mtuhumiwa wa wizi asibanikwe”. Mtu unabanika nyama ya kuchoma unayotegemea kula baadaye. Kilichokuwa kinatokea pale ni mauaji na ni wajibu wenu waandishi wa habari kuaza kuelimisha wananchi.
Mpiga picha ameweza kuonyesha mkono wa mtu anayewasha kiberiti lakini hajachukua picha ya uso wake. Mpiga picha kapoteza nafasi nzuri ya kutoa mfano kwa jamii kwani hiyo sura ya mchoma moto ingeweza wekwa kwenye magazeti na vyombo husika vimchukulie hatua muuaji huyo…
Na mwisho naomba usome vielelezo vya kila picha na uniambie ni ujumbe gani unatumwa..
…kibiriti kinapigwa
….moto lipu!
….moto unakolea watu wanasepa
….askari kanzu anawahi kusevu ngoma
….jamaa anachoropoka
….haya bwana... twende umeshasevu...
…..mchezo kwisha!!!
Inamaana kumchoma mu Tanzania ni Mchezo?
Kama nilivyosema mwanzo kutupa hii habari ni jambo zuri kushangilia kilichotokea ni aibu!! Naamini si wewe uliyeandika hii stori na ningependa uwaelimishe waliokosea!!
ingekuwa picha ya mtu akibaka, polisi wangemkamata.lakini pale anapoamua kuua mtu mwingine, polisi wanakaa kimya. hii ndiyo hali halisi ya Tanzania. iba mabilioni unaweza kuendelea kutembea mitaani, jaribu kuiba buku, unaukumiwa kifo... hahaha. kila kosa na adhabu yake...
ReplyDeletejaman me roho inauma, alf bado kuna mijitu inatoa comment za kiushabiki, angekuwa nduguyo je?????huyo shda zinamsumbua unatakiwa ukimkamata unatafuta cha kumsahidia co kum kill, inayotoa Comment mingne ni mijizi ktk ndoa za watu na nyie mchomwe........kwakwel my day imekuwa ya very kuumia roho.
ReplyDeleteIts Neyma
Na huyo mpiga picha naye ana roho ngumu kweli (Nadhani siyo wewe Michuzi). Yaani mtu anaungua moto, yeye anampiga picha badala ya kumuokoa (ili apate haki yake kwenye vyombo vya haki)
ReplyDeleteHizi ni frustration za watu tu! Vitu kama bili za umeme kuwa juu, kukosa maji wiki, ada za shule kudaiwa, ishu za kazini, ufisadi uliokithiri, bei za bidhaa kupanda, jua kali. Yote hayo yanaleta frustration katika maisha ya mbongo kila siku. Akitokea kibaka, basi hasira zote zinamwishia yeye. That's the reality!
ReplyDeletemtoto
Nijikuta katika mtihani mgumu. Nafundisha hapa Marekani na pamoja na kuwafundisha, nawapigia debe waje Tanzania wajionee tulivyo nchi nzuri, ya amani, mshikamano na kadhalika.
ReplyDeleteKwa kuona picha na taarifa hizi za leo, ni sherti nitafakari. Hao wanafunzi wanapokuwa Tanzania wanakatiza mitaa hiyo hiyo. Sijui niache hizi ngonjera za kuisifia Tanzania? Kuna ukweli gani katika kuisifia Tanzania, wakati waTanzania wanafurahia kuwachoma moto binadamu wenzao kama inavyoonekana kwenye hizo picha? Halafu jumlisha na mauaji ya albino. Ngonjera zangu zina mantiki kweli?
Halafu, mitaani humo wako hata watoto wadogo. Nao wanashuhudia mambo hayo ya kutisha. Je, hawaathiriki kisaikolojia? Na je, wanakua wakiwa na mtazamo gani kuhusu uhai wa binadamu?
Mungu isamehe Tanzania!
ah michuzi siamini kama nawe una ngumu na mbaya kiasi hicho. roho yako ni ngumu sana. yani mtu anawekea majani we upo tu, wanamwagia dizeli wewe upo tu umekomaa na kamera yako, wanatoa kiberiti wewe upo tu na kamera yako, wanawasha moto kumchoma binadamu mwenzako yani wewe upo tu umekomaa na kamera yako. kwa hiyo ulikuwa unafurahia?? kwa hiyo polisi wasingetokea ungetuletea hadi picha za jinsi kiumbe huyu akikata roho??? nimesikitika sana. nilitegemea ungetuletea picha za hadi pale wanamwagia dizeli kisha ukatuambia wadau gemu liliishia hapa sababu mimi michuzi ngoma ilinishinda nikaamua kuingilia kati!!!
ReplyDeleteanyway ahsante kwa picha, lakini!!! mh
Mdau, CA,USA
Viongozi wa serikali wanasema kwa kutamba kuwa Tanzania kuna amani...hii ni amani? Tanzania hakuna amani kabisa. Maisha ya wananchi yamekosa amani: umaskini, maradhi, ujinga etc. Wanaona kwa macho yao kuwa hawana nguvu ya kubadilisha mfumo wa maisha yao, matokeo ni kutolea hasira zao kwa hao vibaka wanaokwapua mitaani. Hii ni ishara ya wakati. Ishara ya wakati ambayo hao viongozi wetu kama wana macho yakuona, waangalie; kama wana masikio ya kusikia, wasikie. Hii ni ishara ya wakati kuwa amani hakuna na moto unatokota kichinichini na unakaribia juu. Ukija kulipuka matokeo yake yatakuwa mabaya sana kwa nchi nzima. Sina haja ya kutoa mifano kwani mifano inatisha...ilitokea nchi za jirani, na wenyewe tulijionea. Tanzania ni nchi ya amani...la hasha. Haya mwaya, endeleeni kufisadi nchi,kupanda mashangingi na kujiita waheshimiwa huku wananchi wanateseka, lakini msije mkasema hamkuambiwa
ReplyDeleteYa
ReplyDeleteRabana twaomba samahani
I really shed a tear when I downloaded and enlarged the first picture and saw the fear written all over poor boys face
What was the MOB thinking of
Barbeque
Ndafu
Ama mishikaki
Aib Aib Aib
Wakatabahu
habari imetulia ! amepata dozi yake na hiyo ndiyo hali halisi wala hakuna kuremba-ndiyo bongo halisi.
ReplyDeleteWewe Injinia hapo juu naona hupo dar na huijui kwa sasa,kwavile wewe injinia naelewa,
you can be in dar but maeneo poa!-unakula vyako tu,hongera na pole kwa raha!
Kama wengi mnadhani huko mliko,iwe nje ama wapi i don't care..mpo shwari,hapa mambo ndiyo hayo wala hatulaumiani,shangaeni kwavile hamna mjualo-mkija bongo ninyi dar hata kwa miguu hamtembei,ndani ya vimkoko vyenu full kiyoyozi mnalalamikia jua!mmechanga vidola ama viyuro nk. mnajiachia tu.poa lakini hamjajui yanayojiri! muwe makini kuna kupigwa ngeta,ukiachiwa kwishney...
Hapo mmepewa hali halisi tu na hakuna cha oooh "human rights" wala nini,mnazijua nyie ama mnadanganyika na huko mliko-ninahisi hamjaona hata watu wakienda kuzikwa na mmesahau kabisa-mko peponi eeh? bure!
mambo yenu safi tuacheni tunaovuja jasho kweli tusulubishane maana hata wahusika huko juu
hawana mpango nasi-"sasa kila mtu ale jasho lake"-
vibaka kama wanaweza wakaibe huko zinapotoka pesa....
mwendo mdundo!
Personally i don have issues with the pictures . The act itself is morrally disturbing ,to say the least.At the same time,i msut say whatever it is that has happened does not surprise me.Given these economically and politically critical times,it will only get better from here.Guarantee.
ReplyDeleteThese pictures on the other hand are nothing but a reflection of the desperation that is sweeping scores of ordinary folks.With these pictures,as appaling as they might be they are clearly indicating some degree of media freedom.That's my perspective .Uncensored and uncut tell it as it is,ofcourse with a twist of aesthetics.The bottom of the issue here is that Michuzi has done a great job.He's acomplished his task.delivery,no sugar coating,uncensored and uncut.Obviously in any society it may please some and ofcourse disgust others.My complements go to Michuzi on this.There is nothing that i like a great narrative photographic work.Ofcourse the theme may not necessariry be interesting.But the photographic skills displayed here wont pass without my complements,Kudos to Michuzi.great work
Sasaman
KAMA WEZI WA EPA NA MAFISADI WENGINE WANGECHOMWA BADALA YA KUITWA WAHESHIMIWA TUSINGEFIKA HAPA. NINI CHANZO CHA WEZI HAWA KAMA SIO HAO MAFISADI LEO TUNAWACHOMA WALALA HOI WENZETU NA KUWAPIGIA MAKOFI MAFISADI> AMA KWELI HATUTAFIKA.
ReplyDeleteVibaka na wezi wanaotusumbua huku mitaani waendelee kuchomwa moto tu.
ReplyDeleteAnayewatetea ni yule ambaye hajawahi kuibiwa.
Mimi waliniingilia home siku moja na kukomba laptop, TV, microwave cooker na pesa taslim Tshs 200,000 (bahati nzuri kiasi kikubwa naweka benki) ... lakini vitu vyangu ... hususani laptop ... ambayo kwangu ni kama ofisi ikiwa na deal kibao ... iliniuma sana.
Nilitamani ningekuwa na dawa niwageuze wote mandondocha hapo hapo kisha niwatie kiberiti.
HIVYO CHOMENI MOTO TU. WATU WANAOJIFANYA WANAJUA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU NDOJA SIKU WAKIPORWA AU WAKIVAMIWA NYUMBANI NA KUSAFISHWA NDIO WATAELEWA TUNACHOONGEA HAPA.
Na by the way, watu wanaoishi ughaibuni ambako sheria kweli zinafanya kazi (yaani vibaka hawahongi Polisi na kutoka kesho yake) hawawezi kuelewa kadhia ya hawa vibaka.
Michuzi
ReplyDeleteHii habari imeiripoti kiushabiki sana kauli ya "Mchezo Kwisha" imenisikitisha sana. Haya ni maisha ya binadamu, huyo aliyeokolewa ni binadamu kama mimi na wewe. Tuwe imani kwenye maisha ya binadamu wenzetu.
looooh..., inawezekana huyu mjomba ameiba hindi la kuchoma tuu. hivi ni kweli maisha ya mtanzania hayana thamani kiasi hiki?
ReplyDeleteNdugu wanainchi!!TAARIFA NYETI INASEMA NCHI YETU INAONGOZA KWA UKIUKAJI WA HAKI ZA BINADAMU KTK BARA LA AFRIKA!! IKIFUATIWA NA AFRIKA YA KUSINI.Watu wa chache( VIGILANTE)msijichukulie sheria mikononi! Japo Mwizi ni mwizi ata kama kaiba Vitumbua!Unaposikia yowe la Mwizi jambo la kwanza nikuangalia kweli keba na ushaidi upo pili kitu alichoiba kina thamani gani???ubinadamu(hekima) kwanini kaiba?Kama kweli una uchungu(MUUNGWANA) simama naye mtuhumiwa mahakamani toa ushaidi wa kweli mpaka afungwe.Swawabu zako utazipata kesho.
ReplyDeleteNitakupa mifano mitatu
1.Kuna Vilante Afrika yakusini(Mapoko matamanga)au Chui mwitu Sheria zao (a)Ukimwiba mwana chama wao,wakikukama anatakiwa urejeshe mali ulizo iba (b)ktk wizi uki uwa na wewe unauliwa
2.Nchi za kiarabu wanakitu wanaita Sharia (a)ukiiba kitu kinachozidi Dola 200 za U.S.A unakatwa mkono mmoja.(b)chini ya dolla 200 za U.S.A unapigwa bakora (c)ktk wizi ukiua naye unauliwa
3.Vigilante wa TZA mtu akiiba chapati,saa ya mkononi ya kichina,akiiba kipochi chenye 500Tz shillingi kwanza mkongoto wa nguvu,kisha anachomwa moto!!ANAULIWA!! kweli hii ni haki??
Naomba serikari irejee toka likizoni,kitambo siku za nyuma walikuwepo vijilante i)sungusungu ii)Watu walio hisi wenzao(Vibibi venye macho mekundu) wananchi wakawaua shinyanga lakini walishughurikiwa ipasavyo.Serikali inangoja nini???HII NI AIBU KUBWA KWA NCHI YENYE MAADILI KAMA TANZANIA.
KIPI ALICHOIBA AU ALICHOTAKA KUIBA KINACHOWEZA KULINGANISHW NA THAMANI YA MAISHA YAK!!!????!!!---MUOGOPENI MUNGU, FIKIRIA KAMA HUYO ANGEKUWA ANAEKUHUSU AU KUMFAHAMU TU, UNGEPENDA HATA KUANGALIA KWELII,
ReplyDeleteUHAI WA MTU JAMANI!!! WALIOHUSIKA WAKATUBU MUNGU ATAWASAMEHE. TUBARIKI BABA MUNGU.
Wadau Bongo!! mnaoibiwa pesa zenu,simu zenu,cheni zenu n.k. poleni sana,Nazingatia vitu vyenu vina thamani mmevitolea jasho kuvipata,Mnayo haki ya msingi kukasirikia wizi!Mimi siyo naunga mkono Wizi,Naomba mfikirie mara mbili!vitu mtu anavyoibiwa vinathamani yake na roho ya Binadamu?? Mwenzako?hata mimi bongo nilizawa niliishi niliibiwa.Fikirieni kwa makini suala hili Adhabu mnayoitoa ya kumchoma Mtu MOTO,Mpaka AFE inalingana na kosa alilofanya?Wa bongo tunakasumba moja mbaya ya kuiga mambo!kufuata mkumbo!Kama hiyo ni fashion huko Bongo hiyo kali imezidi kipimo!!!???basi isiwe kiingiacho mjini .....Ilianza kidogo kidogo Sasa imekuwa ugonjwa sugu,kwani kwenye picha Ninamwona Dada mmoja Anaonekana kama Muungwana amevaa kaunda suti au (suluali)Afananikabisa kushabikia Maasi.
ReplyDeleteKuuwa vibaka nje ya mkondo wa sheria ni ufisadi na inabidi ukemewe.
ReplyDeleteUtamaduni huu ukiendelea vibaka watakuwa wanawageuzia wanaowaibia hapo ndio mutaona ubaya wa mob justice.
Ole wenu Mnaotanguliza wenzenu kuzimu,kwa visingizio vya pesa, simu n.k.Siku ya siku ikifika msije mkajibu kesi!!sitaki kujaji napenda kuuliza,dini dani inakubali kuua???wanaokufa ni viumbe wa mwenyezi Mungu.Naomba kama mnaadhabu nyingine mnaoweza kumpa mwizi,mpeni siyo kumuuwa,Nawaombeni tafadharini mrudishe mioyo yenu nyuma,punguzeni hasira,Gadhabu!jifunzeni kusamehe.Wapeni nafasi nyingine wanaweza kubadilika.
ReplyDeleteOle wenu Mnaotanguliza wenzenu kuzimu,kwa visingizio vya pesa, simu n.k.Siku ya siku ikifika msije mkajibu kesi!!sitaki kujaji napenda kuuliza,dini dani inakubali kuua???wanaokufa ni viumbe wa mwenyezi Mungu.Naomba kama mnaadhabu nyingine mnaoweza kumpa mwizi,mpeni siyo kumuuwa,Nawaombeni tafadharini mrudishe mioyo yenu nyuma,punguzeni hasira,Gadhabu!jifunzeni kusamehe.Wapeni nafasi nyingine wanaweza kubadilika.
ReplyDeleteHii story inafundisha vizuri sana. Naona tunalaumu system tu kwani huyo aliemwibia hayuko kwenye hii system? Yeye kapata vipi mpaka mwizi aweze kuiba - kila mtu anahangaika na sote tutavuna tulichopanda jamani eeeeeh.
ReplyDeletejamani inahuzunisha lakini hawa jamaa wamezidi ukiona hivyo hajapata pesa ya kuvuta ya unga ndio akili inamtuma aibe jamaa ana umri mrefu kweli yani akipona hapo bora atubu aache kabisa
ReplyDeleteHUKU MBAGALA KWA WAHANGA WAMBOMU, VIBAKA WATUIBIA VITU VYA MISAADA JAMANI, HAWA WATU HAWANA HATA HURUMA.
ReplyDeleteKAMA SERIKALI IMESHINDWA KUTUJALI WOTE, LAKINI WAO WANAONA KWANINI WASIENDA KUIBA HUKO KWA MAFISADI PAPA, WAO WANAKUJA KUTUIBIA SISI TULIO NA KIDOGO, KAMA WAO WANAUCHUNGU WAKAWAIBIE MAFISADI PAP, SIO SISI WALALAHOI, NDIO MAANA TUNAWACHOMA MOTO, ILI WASIRUDIE, MAANA WOTE TUNAPIGIKA, SIO WAO TU WANAPIGIKA.
Kweli bongo tambarare lakini hii hapo kweli siu ungwana ..actually i appreciate some views and opinions of most of wadauzi here and its proves that Tanzanian we are still humanity nation doesnt matter where we are.
ReplyDeleteTambarare tunayo ambiwa kwenye blog kama ni hivyo duuuuu ipo kazi but the sad thing is to see the (kibaka) huyu jamani sio mwizi , mwizi hawezi kuwa mchuvu kiasi hicho huyu ni kibaka wa mtaani anatafuta hela ya kununua sembe na fungu la dagaa ili aweze kupata usingizi jioni.
Majambazi wanakwenda na gari ,wana machine-guy zao na SMG ambazo wanazipata wapi??????????? jibu analo wahusika wa home affairs na JW silaha kama hizo zinanunuliwa kwa fedha ya kigeni na zinaingia nchi kwa contract how comes zinakuja kuwa owned na wahuaji wanatelekeza amani ya nchi yetu, hao watu waliokusanya kuni kumchoma kibaka nafikiri wangelijioganizi na kuwauliza wahusika nafikiri ingelileta amani kidogo kuliko kuangaika na mtu ambaye maisha tayari yameisha mchuma na nyie kiushabiki mnataka kumwashia kiberiti. Watanzania kama hatutaacha kuchanganya mambo kati ya KUTEKELEZA au KUWAJIBIKA basi nchi yet haina future ...maana majority ya viongozi wetu wanatekeleza instead of kuwajibika which is bad signal.Nusu ya wakazi wa miji mikubwa hawana kazi and the government is aware but no any reaction as results watu wameamua kuingia mtaani matokeo yake tunaanza kuchomana moto adharani watoto wadogo wanaangalia what they learn from us myself i dont have an answer..but iam sure tunaandaa taifa la kesho lenye asili ya ukatili na unyama((((Mbona hatujiulizi kwanini wakati wa Mwalimu vibaka walikuwa hawachomwi moto na hawakuwa wengi kama hivi leo na jibu ni kwamba Nyerere aliweka sheria ya kutojichukulia madaraka mikononi..serikali na vyombo vyake walikuwa wanawajibika siyo kama leo inatekeleza matokeo yake ndiyo hayo.)))))........sijuhi watu wanao shabikia mambo kama hayo lakini in general iam so worry with destiny of my country....
MDAU WA KAMACHUMU
Mnaohangaika na hizo sheria za mafisadi kalaga bahao...
ReplyDeleteHao wakibambwa wachomwe tu hakuna msamaha kwani hawana wema hao, ukikaa vibaya wanakutumbua jicho. Sina hamu nao hao binadamu.
MNAO WATETEA HAO BINADAMU HAMJAWAHITENDENDEWA UNYAMA. NILIINGILIWA NAKUIBIWA VITU KADHAA VYA NDANI, NA WALITAKA KUMBAKA KIJANA WANGU WAKIUME NA KUFANYA UHARIBIFU MKUBWA KATIKA NYUMBKUA YANGU. MAJIRANI WALIMUOKOA KIJANA NA KUANZIA SIKU HIYO KIJANA ALIAMUA KURUDI KIJIJINI AKIOGOPA KUWA WATARUDI TENA. WAKITOKEA TENA AMA ZAO AMA ZANGU.
MANAOSEMA WACHOMWE MAFISADI NA SIO WEZI, MNADHANI NIRAHISI KUYACHOMA HAYO MAFISADI? MIZIZI IMEENDA MBALI SANA NA HATA MOTO WA PETROL HAUWEZI KOLEA KWAO JINSI WALIVYO WAGUMU.
MCHANGIAJI.
SASA NAAMINI HAKUNA WATU HATARI BARANI AFRIKA KAMA WATANZANIA. NI WATU WANAFIKI SANA WANAJIFANYA WANAAMANI NA DEMOKRASIA KULIKO WENGINE, KUMBE WANAFIKI WAKUBWA DUNIANI.
ReplyDeleteKWANZA WANAUUA WENZAO ETI TU KWASABABU NI ALBINO, NA PIA WANACHOMA WENZAO KWA MOTO BILA CHEMBE YA HURUMA YA KIBINADAMU,
WAKATI WANGETAKIWA KUTUMIA VYOMBO VYA DOLA KUDHIBITI WAHALIFU, WAPI UTAWALA WA SHERIA????
HIVI KWELI SISI NI CIVILIZED SOCIETY? WATU WANAONEKANA WANACHEKA WAKATI MTO ANAOCHOMWA SABABU KAIBA TU KITU KIDOGO BADALA YA KUMPELEKA POLISI. KWANINI WASIWAKAMATE BASI PIA HAO WA EPA NK?
NIMELIA BAADA YA KUONA UNYAMA HUU, NA KUTAMBUA HASA UNDANI WA MTU ANAYEJIITA MTANZANIA HUKU AKIONA WENZAO KAMA RWANDA , SOMALI NK KUWA WAKATILI ZAIDI YAO.
MUNGU WAREHEMEMU, WASIJE WAKAWA KAMA MARARISAYO
NIMESOMA MAONI MENGI JUU TA SAKATA LA KIBAKA HUYO
ReplyDeleteJE KUNA MTU YEYOTE ANAWEZA KUTOA USHUHUDA WA KUVAMIWA NA KIBAKA / VIBAKA POPOTE PALE?
haki ya mwizi ni adhabu lakini uyu jamaa anapo pita mtaani kwenye baa zetu za nje na kukuta wafanyakazi wa TRA wanakunywa bia adi wanamwaga wakati yeye siku ya pili ajala na kazi ana uanategemea atafanya nini zaidi ya kumsubili jamaa hao hao ili kuwaibia kinabidi tanzania tuanzie kuwa coma jamaa wanaop ibia serikali
ReplyDeleteduu hivi mawazo gani yalikuwa kichwani mwa huyo kibaka alivyojikuta anamwagiwa dieasel,kafunikwa na kuni alafu kiberiti kikawashwa?lazima amshukuru Mungu otherwise.........
ReplyDeleteJAMANI WADAU KUUA NI DHAMBI LAKINI KAMA UMEWAHI KUIBIWA - UKIONA MWIZI ANACHOMWA MOTO BINAFSI NINGETOA PESA YA PETROL WA SIO KIBIRITI. JAMANI WAMENIRUDISHA NYUMA NAOMBA MUELEWA HIVYO.
ReplyDeleteWadau...
ReplyDeleteKWANZA NIWAFAHAMISHE HUYU JAMAA ALIFARIKI DUNIA JANA KATIKA KITUO CHA POLISI OYSTERBAY.
inasikitisha,ila kwa wanaojiuliza ilikuwaje na aliiba nini nikuwa,kijana huyu aliruka ukuta akaingia ndani ya nyumba moja iliyopo maeneo ya msasani drive in,karibu kabisa na ubalozi wa marekani na karibu sana na kituo cha polisi oysterbay,
Alichoiba ni TV,wakati akiwa katika jitihada za kumpasia mwenzake ndipo binti anayefanya kazi za nyumbani akawashtukia na kupiga kelele za mwizi mwizi mwizi,wakati huo ilikuwa majira ya kati ya saa tano na sita mchana,mara umati ukajaa kumfukuzia na kumpiga,alijitahidi kuokoa maisha yake kwa kupanda mpaka juu ya ghorofa lingine bila ngazi!! na kujificha kwenye tanki,kwa kiwewe akatoka humo,akaaanza kuwarushia mawe watu waliokuwa chini wakipiga na mawe hayohayo,baadae vijana wengine walipanda na wakamrusha toka juu ya ghorofa mpaka chini...hapo nguvu zikapungua ,damu zinamtoka kila mahali..ndipo wakamuashia moto..na baadae kuokolewa na polisi...lakini alikuja kufa baadae.
Inasikitisha saana mtu kupoteza maisha kwa maumivu makali ilhali wanadamu wengine wakikuzomea...fikiria kukata roho kwa namna hiyoo,kila mtu angependa akate roho huku mashehe au wachungaji au mapadri wakimuombea na sio ukitukanwa na kulaaniwa.
inasikitisha kijana huyu kauwawa kwa sababu ya TV na radio na dvd inavyosemekena aliiba siku za nyuma..ilhali wale wezi wakikweli kweli mapapa na manyangumi wakiabudiwa na jamii hi hi kama Mungu watu,
Tanzania tufike mahali sheria iheshimiwe na ifanye kazi kama inavyostahili,mamlaka za usalama acheni kushirikiana na wezi,wapeni nafasi za kuhukumiwa mahakamai na wakienda jela huko wasiende tu kufua ngua za maafisa magereza bali wakafundishwe,maafisa magereza acheni biashara za kuuzia wafungwa sigara na bangi....wanazidi kuharibika baada ya kifungo.
Nawafikiria wazazi waliomzaa kijana huyu nini yalikuwa matarajio yao baada ya kuzaliwa ,na yeye wakati anakuwa aliwaza nini kama maisha yake...mwisho wake haukuwa mzuri...na jambo hili si lakushabikiwa.INASIKITISHA
WIZI DUNIANI SI WEMA
Mwanajamii DADA TMM
mauaji ya vikongwe,mauaji ya albino,wachuna ngozi, mauaji ya vibaka n.k Tanzania, mpaka lini???hii ni karne ya 21 haya mambo bado yapo tu???na bado watu wanafurahia na kuchekelea(kama huyo jamaa kwenye picha!!AIBU AIBU KUBWA! KWA TAIFA!
ReplyDeleteHAO WATU WALIOTOA COMMENT HUMU BADO HAWAJA IBIWA NA KUJERUHIWA NA VIBAKA, hAO VIBAKA SIO WATU NI KATILI SANA SANA, NYIYNYI WOTE MKISHA IBIWA NEXT TIME MTATOA COMMENT TOFAUTI, DAWA YAO MOTO TUU
ReplyDeleteNasikitika kusikia Mtuhumiwa ameuwawa kinyama.Kwa mujibu wa Dada TMM.Naomba kamanda wa polisi ajiuzulu kuonesha mfano bora wa kupinga kitendo hicho cha kinyama!!!kilichotokea hapo Drive inn,kwasababu mbili kubwa
ReplyDelete1.Drive inn ni karibu sana na kituo cha osterbay polisi wangeweza kuwai kuokoa maisha ya mtuhumiwa
2.Ninafikiria kelele na vurufu zote ubalozi wa marekani ulisikia na kupiga simu polisi
*aliyepiga picha anaweza kutoa ushaidi mahakamani kwa wahusika ikawa mfano.Hayo ni maoni yangu ktk kukomesha hali hii.sijui Wadau mnafikiria nini ktk kukomesha unyama na ukatili unaoendelea nchini????.
Nakubaliana na anons wa:
ReplyDeleteMay 15, 2009 6:30 PM
na May 16, 2009 11:05 AM
Naheshimu uhuru wa kutoa maoni wa wale wote wanaotetea vibaka wasichomwe moto ... lakini nashawishika kuamini hawajawahi kusafishwa bado.
Subirini siku wakiwasafisha ndio mtaelewa.
JAMANI JAMANI ETI NAIBIWA HALAFU NAKAA KIMYA HATA KELELE SIPIGI KWASABABU NIMEIBIWA TV/DVD?
ReplyDeleteWAKATI NIMEVIPATA KWA JASHO? TENA KWA MKOPO, HAPO SIKUELEWENI NDUGU WACHANGIAJI MLIOSEMA HUYO MWIZI HAKUSTAILI.
ETI TUWASAKE HAO MAFISADI PAPA.. MASIKINI SIE TUTAWAKUTA WAPI? TUNAPOTEZA MUDA MUDA WETU.
KILA MTU ATAFUTE ANGALAU KIJIKAZI CHAKUMPATIA MKATE WA KILA SIKU, SIO WOTE HADI TUAJILIWE...
TUTANGOJA HADI LINI HAO MAPAPA WATUACHIE NAFASI HUKO MAOFISINI?
MDAU!!!HAPO JUU UNAYESEMA BADO HAWAJAIBIWA SI KWELI.HAKUNA MTANZANIA AMBAYE AJAIBIWA KILA SIKU MABILIONI YA PESA YANAIBIWA NA MAFISADI UNAJUA NI PESA ZA NANI?? SIKILIZA KUNA MSEMO UNASEMA MWIZI AKIIBIWA ...............
ReplyDelete*MCHUMI MMOJA ALISEMA WATANZANIA WOTE NI WEZI,MSHAHARA WA KIMA CHA CHINI Tsh 60,000 HAOWEZI KUFANYA UISHI, AU MISHAHARA ILIYOKUWEPO BONGO HAIFANANI NA MALI WATU WALIZONAZO KWA HIYO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINGINE WIZI UNAENDELEA...
TUSIHUKUMIANE KIBAKA AKIKUPITIA MSUBIRI BINAMU YAKE AKIJA OFISINI KWAKO UTAMWONESHA!!!!
Utafutwe ufumbuzi wa kudumu kuhusu vibaka. Ni vibaya kuua vibaka, lakini nao ni wauaji wakubwa. Mfano tu walimchoma visu na kumuua mtoto wa kaka yangu na kumuibia simu. Kibaka kama huyo nikimfuma nimfanye nini? Ni 9mm tu.
ReplyDeleteMTU YEYOTE AMBAE HAJAWAHI KUIBA KATIKA MAISHA YAKE AWASHE KIBIRITI CHA KWANZA,LA SIVYO ANYAMAZE.YAANI SISI WAAFRIKA NI AIBU TUPU,WENZETU WANATUONA NA KUSEMA SISI BADO"PRIMITIVE".ZIPO SHERIA ZA KUFUATA HATA KAMA MTU KAIBA;SASA IKITOKEA KWAMBA MTU HUYO HAKUIBA NA BAHATI MBAYA KISHA KUFA?.TANZANIA WAKE UP!
ReplyDeleteWADAU BONGO!!! PUNGUZENI HASIRA,BONGO IMEBADILIKA NA NYINYI MBADILIKE!KULINGANA NA HALI HALISI YA KUPANDA KWA MAISHA. WADAU MME OVER REACT KWELI JUA LINAWAKA KWA KILA MTU,KWELI VIBAKA NI WA BAYA LAKINI ANGALIA UPANDE WAPILI WA SHILINGI:UKIJIKUTA UPO AFRIKA KUSINI,AU BRAZIL LEO UMEIKANYAGA MIWAYA YAO VIBAKA WA HUKO UTAKUBALI AU UTAJUTA KUZALIWA!, VIBAKA(WANATUMIA SILAHA)KUIBA SIMU,CHENI,VIPOCHI n.k TENA ,MWIZI HAWEZI KUUIBIA BILA KUKUJERUi AU KUUWA.MIMI NILIULIZA KWANINI WANAFANYA HIVYO JIBU:AKIKUACHA KESHO UTAMKUMBUKA UTAMTOLEA USHAIDI MAHAKAMANI ATAFUNGWA. MWIZI WA HUKO HAKUNA KITU ANAOGOPA KAMA JELA AKIFUNGWA ATAKOSA KUVUTA YALE MAMBO YAO.SASA NAOGOPA KAMA VIBAKA HAO WAKIANZA KUTUMIA SILAHA
ReplyDeleteKWA KUJUA NI KUFA AU KUPONA ITAKUWA MBAYA SANA.Mfano:NILIENDA ULAYA NILIKUTA MATANGAZO YA AJABU AJABU KANISANI KUNA POCHI INA FEDHA MTU YEYOTE ALIYEDONDOSHA AMWONE PADRI!!!!PIA KUNA WALETI INA PESA IPO POLISI KWA MTU YEYOTE ALIYEPOTEZA,!!!! NILISHANGAA SANA
NIKAGUNDUA WIZI NI HALI NGUMU.MTU KUSAHAU MZIGO WAKE KWENYE BUS, NA KWENDA KUUFUATILIA BAADA YA SIKU TATU,NA ATAUKUTA KAMA ALIVYO UACHA NI JAMBO LA KAWAIDA TU ULAYA.**
Please people, be a little human, to burn that person its like your burning your own fresh. Yah, economy is very tough thats why people like him they still existing in our country and all around the world. Why don't you go and burn those people EPA, and all BOT members who took you there in a first place? eehh? Wengine mnattetea kwa sababu baba zenu ndiyo viongozi wa EPA na wamekuwa msimamo wa mbele kuiba na kurudisha wanainchi nyuma.Wengine wanaficha UFISADI wao kwa kupaki hata magari walionunua kwa wizi wa pesa za EPA kwa majirani zao MBEZI tunawajua na tutawataja majin muda ukifika, Hao mafisadi ndiyo wasaidie hao vibaka kuwapa mitajiya biashara waone kama wataiba. Tena natamani kama vibaka wanasoma hii Blog waende kwa nyumaba za hao mafisadi kwanza.
ReplyDeletewewe unaesema kuwa sisi hatukuibiwa umjinga mno. wengi tumeibiwa na inauma sana, lakini hutuna roho za ujahili kama wewe. katika dunia hii hakuna mtu mwenye haki ya kujichukulia sheria mikononi mwake na hakuna mwenye haki ya kumuadhibu mwenziwe bila nje sheria za nchi. kaa ukijua kama ulikuwemo katika waliompiga huyu jamaa basi wewe ni muuaji tu na kwa nchi nyengine mgelisakwa na kufikishwa mbele ya sheria.
ReplyDeleteBINADAMU MUOGOPENI MUNGU,KUTOA ROHO YA MTU KWA SABABU YEYOTE ILE NI KUJIHALALALISHIA JEHANAMU YA MOTO!MUNGU ANATUAMURU TUSIHUKUMU ILE NASISI TUSIJE HUKUMIWA,HUWEZI KULINGANISHA THAMANI YA UHAI WA BINADAMU KWA SIMU,PESA,AU MALI YEYOTE ILE,KWANI UKIFA HIVYO VITU UTAZIKWA NAVYO?SI WATAFAIDI WENGINE VILE VILE JAPO SI VIBAKA.MWIZI ANAPOKAMATWA JAMANI CHONDE CHONDE TUMPELEKE KWENYE VYOMBO VYA SHERIA WAO WENYEWE WAHANGAIKE NAYE,LAKINI KAMWE USITOE ROHO YA MTU,KWA AJILI YA MALI.HIVI HAMJUI HIYO DAMU YAKE ITAKULILIA KILA SIKU YA MAISHA YAKO,NA DHAMBI ZAKE ZOTE HAPA DUNIANI ZINAHAMIA KWAKO-NA UTAJIBU SIKU YA MWISHO?BASI KAFUNGUENI KITABU KITAKATIFU CHA MUNGU UPATE UFUNUO.
ReplyDeletekwa nchi nyingine kama usa watu waruhusiwa kumiliki gun asingefika mbali maana wako nazo ndani kulinda familia zao na mali zao,hao vibaka ni wakatili sana na wanaweza hata kukutoa roho,hiyo adhabu iendelee kutolewa na wananchi mpaka jeshi la polisi na vyombo husika viwe bora,anayeiba auliwe pindi anapokamatwa live
ReplyDeleteMICHUZI KAKA YANGU MIMI SIKU NYINGI SIJATOWA MAWAZO YANGU YA KISHUJAA.. NAWASHANGAA SANA HAWA WATU WANAO LALAMIKA ETI TANZANIA HATUNA AMANI AMA TUNA KIUKA HAKI ZA BINADAMU. MBONA HAWAONGEI KUHUSU HUKO IRAQ, AFGHANISTAN PALESTINA AMBAKO WATU WANA VAA MABOMU NA KWENDA KUJILIPUA KWENYE MIKUSANYIKO YA WATU. MBONA HAWASEMI WASOMALI WANAO UA WATU HUKO BAHARINI MBONA HAWASEMI KINA MUGABE WANAO UWA WATU WANAOWAPINGA. HII NI KAWAIDA HUYU BWANA KAMA ANAOGOPA MOTO BASI ANGEACHA KUWA KIBAKA!! HATA MIMI MSOMI WA MUZUMBE KIBAKA AKINIIBIYA NITAMUCHOMAGA NA MOTO. INA BOA SANA KUISHI KAMA KIBAKA, HII NI POA SANA CHOMENI KILA SIKU MPAKA WAKOMAGE, NAWAKILISHA
ReplyDeleteukiuliza kaiba nini utaambiwa kaiba saa ya mkononi au simu ya mkononi au kofia ya kichwani!!!he is not diserve that kipigoring.
ReplyDeleteKweli WTZ wengine hamnazo.....Mnateteha na kuwaonea huruma hawa vibaka......kudadadeki acheni wauawe wamezidi hawa.Hata hao mafisadi hawajakaa kwenye site za kuchomwa moto.....waje hii mitaa waone.
ReplyDeleteMdau, Mchukia Vibaka na wezi
tatizo sio wizi ulivyoshamiri tanzania, tatizo lilopo ni kwa wananchi kuona kuwa n haki yao kuua vibaka. pia tatizo ni "the sytem" kutoelinda jamii dhidi ya vibaka na kushindwa kuielimisha jamii kuwa kufanyiwa kosa hakukuhalalishia wewe kuchukua sheria mikononi mwako.
ReplyDeleteMimi nimeshaibiwa sana hapa USA kwenye apartment niliyokua nakaa....ilikua inside job lakini huku kama huna ushahidi basi tena....ni miaka kama saba lakini kila siku nikifikiria vitu vyangu walivyochukua roho inaniuma sana.....ila hii picha leo imeniliza. Those are just materials things jamani...wanaoiba sio kuwa wanatajirika ...wakikuibia ndio unapata nguvu za kufanya kazi zaidi na unanunua more updated things....tumwachie Mwenyenzi Mungu awapunish mwenyewe. Tutakuja kuchomwa hata tusio wezi siku moja
ReplyDeleteNimeshatoa maoni hapo juu, lakini baada ya kusoma maoni ya wengine, nimeona nirudi ukumbini.
ReplyDeleteWako wanaosema kuwa tunaopinga kuuawa vibaka tunafanya hivyo kwa sababu hatujaibiwa. Sijui ya wengine, ila mimi nilishaibiwa. Kwa mfano, baada ya kuanza kazi, mwaka 1976, nilifanikiwa kununua vitu kadhaa vya nyumbani. Wezi walikuja wakaondoka na jiko la gesi na vitu vingine. Pamoja na kuwa walikuwa wamenirudisha nyuma, nisingekubali wauawe huko mitaani. Siku nyingine wakati nahangaika kupanda dala dala pale Buguruni, kibaka alikwapua saa yangu akatokomea nayo gizani. Siku nyingine, pale Posta Mpya Dar, niliibiwa dola 100. Je, kama hao wezi wangefukuzwa na kushikwa, ningekubali wauawe? Hapana. Thamani ya maisha ya binadamu ni kubwa; haielezeki.
Kama wezi hawathamini mali na maisha ya wenzao, mim siko tayari kuwa kama wao, yaani nisithamini mali au maisha ya binadamu wengine. Ni muhimu kuzingatia mambo mema, ikiwemo kutumia sheria. Mungu mwenyewe anataka tufuate amri zake daima.
Kama watu wanasisitiza kuwa wezi wauawe, basi naomba kuwapa jambo walitafakari. Nimeona kwenye baa wanywaji au walevi wakijaribu na pengine kufanikiwa kuingia mitini bila kulipa bili. Hao ni wezi, na wanamtia hasara mhudumu au mwenye baa. Sasa je, wahudumu wa baa wapige kelele za "mwizi" halafu hao wezi wakamatwe na kuchomwa moto? Kama ni sahihi kuwachoma wezi moto, mnakubali utaratibu huu utumike pia baa? Na kama haikubaiki, ni kwa nini? Ni wezi wepi wanaostahili kuchomwa moto na wepi hawastahili?
UGHAIBUNI HASA UK WANATAMANI KUTIA MTU MKONONI KAMA HIVI LAKINI WAPI. KUNA MZUNGU ANATAKA KUJA HUKO KUWAANGUKIA WEZI. HUKU MWIZI ANALINDWA KAMA MALI ALIOIBA ANA HAKI NAYO!
ReplyDeleteSijui lini wa TZ tutabadilika. Mzungu akija toka holiwood akitengeneza documentary na kuonyesha huu ukatili lazima atashinda tuzo za oska.. serikali itaingilia kati na kusema tunaonewa kwamba sio kweli.
ReplyDeleteHawa watu ni sawa na wale wanaoua maalbino ...roho zao zinanuka damu za watu kila siku. Kama mtu anaweza kuthubutu kumtia binadamu mwenzake kibiriti kwa kosa la kuiba shilingi elfu tano haitakuwa tatizo kukata mkono wa albino na kuuza.
Mungu tuepushe na usaidie kuondoa ukatili iliojaa ndani ya mioyo ya watu ...
Hii mada moto sana.
ReplyDeleteMbona wezi wakiua mtu hakuna anayeshtuka na kulaani kwa nguvu zote.
Just think about it.
Eti mwizi au rijambazi likiua kinaonekana ni kitu cha kawaida.
After all, rijambazi si ndio kazi yake kuua watu.
Ila raia sio kazi yetu kuua wezi na majambazi.
Kaaazi kweli kweli!
kwa kweli wezi wauwawe kabisa mimi nalaani kabisa wauwawe .nikiwa na maana yangu kwamba wezi hawana huruma hata kidogo wameniulia baba yangu bila huruma na mimi sono sababu ya wao kutokuliwa wafe kabisa ingekuwepo kwnye tukio nisingekubali wamuokoe kabisa mwizi ni mbaya sana .hao mafisadi wao wanaiba kwa kutumia kalamu hawajamjeruhi mtu au kuuwa mtu bora wao
ReplyDeleteanayemuonea huyo kbaka huruma hawajawah kumfka
hivyo asubiri yatakavyomfika atajua uchungu wake siku hiyo
mimi wakuletwa
Watu wanafikiri ni mazuri wanayoyafanya lakini kumbukeni mbele ya haki sijui mtajitetea nini tendo la kuua binadamu mwenzako ni dhambi tena hasa ukizingatia kosa lake ni wizi tu.
ReplyDeleteWatu wanabidi kuelimishwa kuhusu sheria za nchi na sio kuchuka hatua mikononi.Je kama huyo mtu sio mwizi na imetokea bahati mbaya kabambikizwa kama ni mwizi na watu wameshachukua hatua mikononi na kumuua.Haki ipo wapi?
Mjusi
Hivi hawa wananchi ni dini gani? mbona sheria za dini yao kali hivi?
ReplyDeleteJe aliyeua mtamfanya nini?
UKWELI HALISI WA TANZANIA.MIMI NAFAHAMU WALIO WENGI WAZEE WETU SERIKALINI NI WEZI JE TUWAUWE?SABABU MISHAHARA YAO HAIZIDI LAKI TANO ILE MIJUMBA WALIOJENGA MBEZI ,MIKOCHENI ,MBWENI NA NK,PESA WAMEETOA WAPI?SHERIA YA WEZI TUWAFIKISHE KUNAKO USIKA MPAKA USHAIDI KWA UKUMU.KUNA WAJINGA WENGINE WANAFIRI UKISOMA NDO UNAKUWA SI MWIZI,KWANGU MIMI MWIZI NI MWIZI UWE UMEPEWA DHAMANA SERIKALINI AU UMEIBA HINDI;KAMA TUNAJUA KUPIGA MBONA ATUENDI MAOFISINI TUKAWACHOLOPOE WEZI, WAKUBWA?TUJIULIZE TUMEFANYA NYINYI KWA WEZI WA RADA,RICHMOND,KWANGU NADHANI WAPIGAJI WAKUBWA NI WENZANGU NA MIMI WA MLO MMOJA,wake up wewe mdanganyika
ReplyDelete