Bosi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akiongea leo na wanahabari juu ya libeneke la bei za vocha za simu za mkononi ambapo ghafla tu wauzaji walianza kupandisha bei kwa kuongeza shilingi 100 kwa kisingizio cha kodi
Bei ya Vocha za muda
wa maongezi za Voda wala hazijapanda

Dar es Salaam July 6, 2009:
Kampuni ya simu za mkononi, Vodacom Tanzania, haijapandisha bei za vocha za muda wa maongezi kwa wateja wa jumla na hivyo bei sokoni haitakiwi kupanda.

Akuzingumza Jijini mchana huu, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano cha Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba alisema kilichotokea ni kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imebadilisha mfumo wa wa ukusanyaji wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ambao umesababisha badiliko dogo katika gharama za usambazaji kwa wateja wa jumla.

Alisema mabadiliko hayo ya mfumo wa ukusanyaji wa kodi hayatakiwi kuleta mabadiliko katika bei ya uuzajiwa vocha sokoni.

Mwanvita alitoa ufafanuzi huo kufuatia hatua ya baadhi ya wauzaji wa rejareja wa vocha za muda wa maongezi kupandisha bei ya vocha hizo kwa kati ya shilingi 100 na 200, mathalani vocha ya Sh,1000 inauzwa kwa bei ya shilingi 1200, Sh.2000 inauzwa kwa Sh.2200. Sh.5000, inauzwa kwa Sh.5200 au zaidi.

“Kubadilika kwa mfumo wa ukusanyaji wa kodi ya ongezeko la thamani hakupaswi kubadilisha bei kwa wauzaji wa rejareja, natoa wito kwa wauzaji hao kuacha kupandisha bei ya vocha hizo kwani mabadiliko madogo ya kodi yaliyofanywa hayana madhara kwao,” alisema.


Mwanvita.Alifafanua kwamba Vodacom hivi sasa inakutakana na wauzaji wa jumla wa vocha ili kuhakikisha kwamba bei za vocha zinabaki na thamani kama zinavyotakiwa sokoni, yaani vocha ya 1,000 inauzwa kwa 1,000 na si vinginevyo.
Baadhi ya wateja wa Vodacom wamekuwa wakilalamika kufuatia kupanda huko kwa bei kwa madai kwamba hakuna tangazo lolote la Vodacom lilowataarifu mabadiliko hayo ya bei na kwamba kupanda huko kunawaumiza.
Vodacom Tanzania ndiyo mtandao unaoongoza hapa Tanzania ukiwa na wateja zaidi ya milioni 6 na ukiwa umesambaa nchini nzima.
Imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano
Mwamvita Makamba
Kwa niaba ya Vodacom Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 06, 2009

    JAMANI JAMANI. HUYU MTOTO MIMI NAPELEKA POSA KWA MZEE MAKAMBA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 06, 2009

    Hapo hamjatusaidi KITU WATEJA WENU kwasababu tukienda kununua hizo vocha wanadai mbona sukari tunapandisha bei hamlalamiki, sisi tunauza hivyo ili tupate faida, KUTOKANA NA JINSI TULIVYONUNUA. Kwaminajili hiyo anakupa hiari ya kununua au kuacha, wewe unashida ya haraka na vocha ufanyeje?
    Ingefaa muanze kuchukua hatua za kuwabana wauzaji kuwa atakayepandisha mtamfutia leseni,na tumeni watu wenu wasibishe hili, kila duka wamepandisha,hii ni ajabu, wamekutana lini nakukubaliana hili!
    M3

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 06, 2009

    mhhh toto la kisambaa limependeza si mchezo vp yupo single au kesha kamatwa

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 06, 2009

    Wabongo kwa wizi tunapenda sana kuibiana kifalafala mi simu yangu nilifunga kwa hasira siku mbili zilizopita, baadae nikaona ujinga huu ngoja niende nao sawa nikaenda duka la jumla na mie nikanunua vocha za mia 5 za alfu 10, kwa Tsh.9800 nikudishiwa chenji Tsh.200/= mzee dah nikaona yes, nikaamini jamaa wamepandisha bei na sio siri vocha kwa faida ya sh.10/= hailipi wala nini. Ila swali jingine Michuzi bei halali ya soda ni shilingi ngapi maana mi najua halali ni Tsh.350/= lakii twauziwa Tsh.400/= hadi jero na PEPSI & COCACOLA wako kimya tu ka mafala wala hawaweki matangazo ya bei. Shukrani kwa TBL hakika wao wanamjali mteja maana wameamua kuweka bango kabisa kilimanjaro na nk bei ni Tsh.1300 safi!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 06, 2009

    Bongo bwana yaani VAT inashuka kwa 2% bei zinapanda kwa 10%. CCM hoyeee!
    Hakika kila Watanzania 100 basi 99 ni ama white collar or blue collar thieves! Kama unabisha uliza Busanda na Biharamulo watakwambia

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 07, 2009

    Honesty a picture is worth a thousand words and also a picture can make you or break you.....Wow!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 07, 2009

    AL..LAHAULA..MBAVU SINAA...BINTI WA MAKAMBA.."..DNA.." YANINI SASA HAPA KUPOTEZA FEDHA TU...

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 07, 2009

    MKE WA MTU HUYO , TENA MUMEWE NI MDHUNGU ! MLIE TUU........... !

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 08, 2009

    Kwa kuchangia tu nilitaka kumwambia mdau anon wa 08.41 pm . watu wameuliza je yupo single au ameolewa? kwa utumbo unajibu ni mke wa mtu TENA NI MDHUNGU kwa hiyo wewe unaona kuolewa na mzungu ni big deal au sio ? amka Sister (kimtazamo yaonyesha wewe ni demu) toa ufinyu wa mawazo .ungesema ni mke wa mtu ingetosha sana .wacha kuwakweza wazungu wakati tulioko huku tunawaona ni kama nguruwe tu (samahani kutumia lugha hiyo) inaonyesha kabisa nyinyi ndio wale mnaotupa Mila na Tamaduni zenu na mkaona kila afanyalo mzungu ndio la kufuatwa .
    mdau Zee la Bandari Leicester -UK.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 08, 2009

    mdada mzuri lakini mmmh

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 08, 2009

    wasemalo ni kweli sana ZEE LA BANDARI..kuolewa na mzungu wala si dili...wazungu nao waweza kuwa watu wazuri na wabaya pia..kama waswaili wetu. huyu dada ni mtoto wa mkubwa, kapata kazi ya maana, na sasa kaolewa na mzungu (kwa nnavyo mjua ni inglishspiking tu..)..kila kitu kina uzuri na ubaya wake. hata cent ina vipande viwili..

    Hs

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 08, 2009

    ebu mwacheni Mrs wa watu...

    ila jamani vocha zinatusumbua sana mtaani,sii muwajie uku na kuwapa marufuku ya kufutiwa leseni za mauzo ayo??

    sio unaongea ooo hawatakiwi!so what

    soda wamebandika coca ktk visibi na mabango yao yale ya nguo bei shs400/-

    njooni mtaani muone,kama annon apo avosema,wanunua vocha za jumla basi

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 08, 2009

    Wewe mdau wa 12:37 zeze la bandari Leicester tena acha tabia ya kukaa unakashifu watu humu wakati hujui mtu kwani mimi kusema mdhungu ndio nini labda wewe ndio unawaona big deal hao wazee unaowatawaza tena naomba usinichefue kabisa kusema eti nimesema hivyo naonesha ni mwanamke this has nothing to do with my gender huo usexist wako peleka huko huko kwani nikiwa mwanamke ndio unitukane na huo ufinyu wako wa fikira. It was just a comment na sikuwa na maana yeyote na hiyo comment nilijisikia tuu kusema hivyo sasa wewe nani mpaka unipangie niandike nini kama unaona ishu basi kaa pembeni kaka tena taadabu kuvamia vamia watuu eti ooh uko Ulaya , Ulaya Leicester? hebu nenda kwa mwalimu hamisi hapo kaode hako kasahani kako ka "biriani" sijui ule ukae chini unywee maji utulie mana naona una njaa tuu wewe umetoka kufuta wazee saa hizi uko hooi unataka kuvamia vamia watu humu ! HAbari ndio NDio acha kujishaua eti ooh Zee la Bandari Leisecetr -UK so what ? signature ndeeeeefu kwani ulaya unakaa peke yako umeambiwa ? na hao wazungu ni rangi tuu ya ngozi and when I said it I meant NOTHING by it except wewe na njaa zako ndio unataka kuanzisgha ISHU. Na kwa taarifa yako tuu nikurekebishe mimi sifati mila za kizungu , nimeolewa na mweusi mwenzangu na wanangu nawakuza kiutamaduni wangu , na vilevile mimi sio mbaguzi wa rangi na wala mfinyu wa fikra kama wewe kwa kiasi cha kumuita mzungu Nguruwe kwani yeye na rangi yake ni binadamu kama mimi . Wewe mtu akikuita Nyani hapo ulipo utakubali ? sasa kwa nini ukashifu wenzako kiasi hizo ? Jamani mko ulaya basi fanyenyei hata hivi vifree course shule muhimu wewe si mkimbizi hebu nenda kafanye Free courses ufunguke mawazo > Mnafiki kujitia unakuona mzungu nguruwe wakati unakaa nchini kwake so unafanya nini tena jamani kwenye hili banda la nguruwe ? si urudi kwenu ? acha Dharau kabisa nakwambia tena usinichefue. ..... .ohooo hebu mimi niende zangu lunch saa hizi watu wenye kazi zetu za kujiajiri hapa ulaya sio watumwa haoooo tuna uwezo wa kuandika emails hata mchana kweupe sio wewe unaongoja mpaka masaaa sita ya usiku ukirudi kupindwa ndio ukae kwenye email kuandika pumba badala ya kulala unamnyima na mkeo ujumba na kwanza wewe inaelekea huna hata mwanamke anaekutaka kwa hizo dharau zako ndio mana umejaa stress za ulaya na hii credit crunch sijui imekucrunch , ama unachukua jobseeker allowance wamekukatia nini ? stress zimekujaa na ndio mana kimekuuma mimi kusema dada yetu huyo binti makamba kaolewa na mdhungu mana wewe huna hata mwanamke wa kukuuliza hali.....! Kaka Mithupu samahani Mkuu mimi sijawahi kukashifu mtu humu lakini huyu mdau kaniudhi sana kwa hiyo this is personal only me and him to this mdau naomba haya majibu yapate kuona mwanga ili ayapate na kama atajibu bring it on! .

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...