video ya sehemu ya maneno yaliyotamkwa na spika wa Jamhuri ya Muungano Mh. Samwel Sitta muda si mrefu uliopita. kunradhi picha si ya ubora wa juu ila sauti ni mswano
Home
Unlabelled
spika samwel sitta awaondoloea uvivu anaowaita maadui zake
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Huyu sasa anasahau majukumu yake yeye ni spika wa wabunge sio wa wananchi sio kila kinachooandikwa kwenye internet ni uzushi mengine ya kweli.asisahau ule uhuru wa vyombo vya habari na wala asije kutunga sheria zake
ReplyDeleteHabari ndio hiyo ndugu spika
huo ndio uwazi na uwajibishaji. ukiwa msafi uhandamwi. mbona hawajamsema Pinda au Shein? kwa nini wakuseme wewe? tujibu. Pikipiki wapi na wapi na uchaguzi? Ya richmond na epa yalianza hivi hivi na ukayabeza eti yanatoka kwenye internet. matokeo yake kila mtu anajua sina haja ya kuelezea. Bunge likuundie TUME.
ReplyDeleteJamani, kama speaker yuko terrorised kiasi hicho, nani yuko salama? Usalama wa taifa wako wapi mpaka mkuu wa muhimili wa pili wa serikali anakuwa na woga kiasi hicho?
ReplyDeleteKaka Asante kwa kutupa hint hii muhimu. Nafikiri ni habari njema sana hasa kwa watanzania wa leo, kupata maelezo yenye usahihi kuhusu maneno ambayo yanavumishwa hasa kipindi hiki. Kwa wale wana-blog ambao wako nje ya Tz wanaweza wasielewe sana hali halisi kwa sasa, ila kwa wazoefu wanaweza kufahamu kuwa tunakaribia kipindi cha uchaguzi mkuu mwakani (2010). Kwa kawaida wanasiasa ambao hawajatulia huwa wanatumia muda mwingi kuchafua wenzao ili yeye aonekane safi... Lakini ukweli anayemchafua mwenzake kwa uongo, huyo ndio mchafu zaidi... Ombi langu tuwe macho sana... Watanzania tuna akili sana ya kuona na kuamua..tuzitumie hizo kuweza kuchagua mchele safi na chuya tutupe shimoni...
ReplyDeleteNsa
Hongera sana muheshimiwa, sasa mambo yameiva, si uwataje tu au uwapeleke polisi, kwa nini ulinde hivyo , si kuna vyombo husika, jamani viongozi wetu, tunawaomba muwe wazi; kama wanakuonea wivu we kuwa wazi na wawajibishe badala ya kutoa vitisho. Watanzania tuwe macho kwa kila kinachosemwa mwaka kesho ni uchaguzi. AU unasemaje? lazima tuwapige maswali kuhusu hizo habari wanazo toa, Il tujue ukweli.
ReplyDeleteMichuzi sikujua nilitolee wapi dukuduku langu. ila nadhani sasa kuna baadhi ya mambo inabidi kama ni ushamba basi tupunguze kidogo. Hivi kumkabidhi Waziri Mkuu ripoti ya hujuma za Ubungo ikiwa imefungwa kama zawadi ya harusi ni ulimbukeni au ndio fasheni? Manake nimebaki hoi, kwa tafsiri ya harakaharka ni kwamba wamempa Waziri Mkuu zawadi akajipongeze! Huu ni uhuni na haswa ofisi inayoshughulikia masuala ya matumizi ya umma huu ni ubadhirifu usio wa lazima (kama kuna wa lazima)
ReplyDeletehongera ziwafikie wana vyombo vya habari kwakutuhabarisha, mtambue kama alivyosema unonymous wa mwisho watanganyika sasa ni watanzania waliofunua ubongo, vyovyote watakavyo jitetea, shughuli palepale tumechoka na danganya toto. politcs! 2010 kazi kweli kweli!!!
ReplyDeleteANONY WA 12:40, WATZ WALIONJE WAPO INFORMED SANA KULIKO WALIO TZ HASA ISHU HIZO ZA SIASA. WANAFUATILIA SANA KWANI WANAVYANZO VINGI SANA, NA WANAKATISHWA TAMAA NA TABIA ZA VIONGOZI WETU KUUMA NA KUPULIZA. KWA NINI SPIKA ASISEME SIO KWELI, NA AJITETEE KWA USHAHIDI. MSUMARI WA MOTO UMEINGIA KUMOYO HASAAAA.
ReplyDeleteNAOMBA KUWASILISHA MITHUPU,HII IMETULIA, HATA YA RAIA MWEMA NAYO YA MEREMETA WATASEMA NI INTERNET STORY. MITHUPU NAWE JIANGALIE KWANI NAWE UNAMILIKI CHO CHA UTOAJI MAONI NA UPASHANAJI HABARI.
Mmmh! Mzee mzima mambo yamemfika mpaka anasema ulinzi alionao hautoshi?
ReplyDeletePambana usitumie jukwaa hilo kwa maslahi binafsi.
Huu ni uhuni. Ana uhakika gani kwamba atakuwa spika? Je anajua kama chama chake kitashinda? Mimi kwa kweli naona hii ni kuwakejeli watanzania wote!! Demokrasia ya kweli iko wapi iwapo hata spika atakuwa kama dikiteta? Naomba kutoa hoja!!!
ReplyDeleteMichu,
ReplyDeleteWeka hiyo atiko ya mwananchi iliyotoka ikisema "JK akana RICHMOND". Ningependa tuijadili.
Naomba kutoa hoja
six anaomba aongezewe ulinzi kwa pesa za nani? walipakodi? jamani hivi jasho la mtamzania limekuwa la kuchezewa hivi? cha msingi hapo ajibu shutuma juu jake na ajibu kwa vithibitisho na mamlaka husika zichukue hatua sio tu kukaa kimywa ama kushabikia. inafikia sasa watanzania tuache kuteteana na kuweka ukewli bayana na tutafute jia sahihi za kutatua matatizo yetu! kama tutaendelea kuleana na kuteteana na kuona kama hayatuhusu kunasiku tutalia na kusaga meno na kukumbuka nyakati hizi. jamani tubadili tanzania kwa kizazi kijacho bila kujali hadhi ya kiongozi wala mali. mzee six sema ukweli usiwe na jaziba na kutumia mic zinazolipiwa kodi na walala hoi kutishia watu na kujigamba! ni wakati wa ukweli sasa
ReplyDeletechief oderee
mfalme wa kitaa
Nachoweza kusema huyu,Spika Mnafiki,wakati anaandikwa Lowasa na wengine na m,agazei hayo hayo makini yalionekana mazuri sasa yanamgusa yeye anayapa sura ya uadui ili Watanzania wasiyaamini,wote viongozi wa CCM wachafu na X PM alisema wakati anaachngia nagi hatobaki mtu na hakika mtakwisha na mtamalizana wenyewe.Watanzania tukumbuke Spika huyo huyo alimbambika mtu tuhuma za uongo za uchawi Bungeni.mimi nasema waende zao na hafai kuwa Spika ni mroho wa madaraka na mtaka sifa tu.
ReplyDeletekuongezewa ulinzi pia ni ufisadi,watu waachekufanya kazi za kujenga taifa wakae wakikulinda wewe mtu mmoja ndani ya watanzania wangapi,na inaonekana wewe tu ndo una maadui siyo,wataje basi hao maadui wako ili uwe na ulinzi wa kutosha kwa kuwakazia macho
ReplyDeleteKaka Michuzi ninashukuru kwa hii habari,kweli mambo bado kabisa Tanzania.
ReplyDeleteHow comes the speaker of the house of representatives is terrified and seeks additional security.Why do I think he does not feel safe?
From what i know, some of the qualities of speaker are integrity which is straightforwardness and honesty in all his professional duties.Conducting house proceedings.
He is supposed to be objective meaning he should not allow bias( "Tutashinda uchaguzi na nitakuwa speaker") and conflicts of interests.It seems from his words,he allowed bias presumably unfair favouring some people hence conflicts.
The speaker has got to be independent which will avoid threats such as familiarity,and advocacy to one strong side( majority) hence rendering his obligation prone to attack then conflicts.Therefore he is fearing for his life.
Thus why Mr Michuzi,from my incomplete leadership issues article,i stressed responses from executives to be scrutinized effectively and people to debate.
I do not wish to compare TZ to UK but the above fundamental issues ought to be observed in houses where there are opposition to policies.Internal party issues and external.UK has another speaker after the expulsion of the other due to incompetence,bias,poor judgement on MP expenses skendo.
So Mr Sitta has right to seek protection and I suggest,he should counter forces by observing fundamental principles of the house.From his words,Clearly,he is bias,unprofessional and advocating to one side.
His deputy, as well,has same problems for being pro government for self interest knowingly that the general election is on horizon by protecting budget scrutiny by profihibiting nosy questions that are likely to stir up proper contention of issues.
So kaka michuzi,it is vividly seen how political issues are undertaken in our country such that politicians are fearing for their lives.
I could write endlessly on these issues and seek debate as I did on leadership issues article.Could I send you Part II?Anyway let others comment.Later
Mdau ( John ) UK
HAYA NDIO MAMBO YA KUPOST KWAI NI YA KITAIFA NASIO KUTUPOSTIA MASHATI YA KIJANI KWENYE BLOG YETU YA JAMII.
ReplyDeleteKwa kweli nimesoma hizo article kuhusu 6 na naona tangu alipoingia madarakani amekuwa akiiongoza ofisi ya bunge kidikteta. Lakini mimi lazima nataangukia kwenye upande wa habari zinazotoka kwa maana bado sijaona maaendeleo yetu sisi wantanzania na mapesa yanatumika tu mabilioni kwa manufaa ya nani???
ReplyDeleteyaani hiyo nyumba ni ya kuongelea mambo hayo. mbona anaweka hoja zake sehemu ngumu kujadiliwa na wengine. halafu ulinzi wa nini? mwanzoni nilimwona wa maana sana kumbe hamna kitu. hivi kweli watanzania tunachezewa kiasi hiki.
ReplyDeletenaombeni kuuliza. check and balance kwa wabunge ni wapi? tofauti na sheria zao ambazo mahakama inaweza kucheki? nadhani kuna mwanya hapo ndo maana wanafanya watakavyo.
Mimi nasema huyu Spika ameanza kufanya Kampeni,tena anatumia jukwaa la Bunge,ningependa jambo hilo likomeshwe kabisa,kama kuna mtu huko anamuohofia kapeleka pikipiki na yeye awapelekee gari kwanza Watanzania tumechoka kuongozwa na watu masikini kama yeye anaeganga njaa!!,ohho unachafuliwa,unatungiwa,sisi tunajua nyinyi wote humo mna makundi na kila kundi lina magazeti yake.wewe Spika huwezi kusemwa hata siku moja katika magazeti ya Mzee Mengi kwa kuwa ndiyo kambi yako.
ReplyDeleteLakini magazeti hayo hayo kila siku yanataja mahisimu wenu kwa majina mabaya ya wezi,wahujuhumuna mafisadi kama vile hawana familia ndugu na jamaa wanaowaheshimu.
Kuna Bwege mwingine aliwahi kutumia Bunge kuombea magazeti ya Bwana wake matangazo kwa Serikali sasa sisi siyo mafala tukomomeni kabisa.
Acha magazeti yaandike wote ninyi humo ndani,mmezidi kubana habari tupate uapnde mmoja tu ya watu wasiyo na magazeti na nyinyi wenye magazeti tusipate upuuzi wenu.
huo ndio uwazi na uwajibishaji. ukiwa msafi uhandamwi. mbona hawajamsema Pinda au Shein? kwa nini wakuseme wewe? tujibu. Pikipiki wapi na wapi na uchaguzi? Ya richmond na epa yalianza hivi hivi na ukayabeza eti yanatoka kwenye internet. matokeo yake kila mtu anajua sina haja ya kuelezea. Bunge likuundie TUME
ReplyDeleteMICHUZI NAONA UMEKUA SASA!!! NAONA TARATIIBU NAWE UNAANZA KUBADILIKA. UNAANZA KUWA NA AKILI SASA!!! SAFI SANA, YALE MAMBO YA UCCM CCM TU NAONA UNAANZA KUYAWEKA KANDO BAADA YA WATU WENYE AKILI ZAO KUANZA KUIPONDA BLOG YAKO!!! HIVYO NDIVYO UNAVYOTAKIWA KUWA KWANI TANZANIA YETU ITAJENGWA NA SOTE UKIWAMO WEWE. WEWE UKIWA WA AJABUAJABU LEO WAKATI UNAANZA KUZEEKA UJUE UNAWAANDALIA NCHI MBOVU WANAO!!! THE TRUE MEANING OF BLOG YA JAMII NDO HII SASA. SIO ZAMANI MAONI YAKIWA CRITICAL TU UNAYATIA KAPUNI!!!
ReplyDeleteUMEONA KATIKA MAONI 18 YA MWANZO KARIBIA 96% YA MAONI WAMEMPONDA SPIKA NA HOJA ZAKE. YEYE ANA UHAKIKA GANI KUWA NI LAZIMA ATASHINDA UCHAGUZI KAMA SIO YALEYALE MABAVU NA NGUVU ZA DOLA WANAZOTUMIAGA CCM KUPOLA KULA ZA WATANZANIA!!!!
WAJUE MWISHO UPO NA UNAKARIBIA!!
Mdau kutoka BIDII Forum + JF
GA,USA
A third world country in a G8 media spin. With recent 'Fibre optic' internet boost in TZ this entails to more exposure of our govt leaders 'ufisadis' and I trust this would be in wananchi's favour. Developed countries would be exposed to 'ufisadi' prevailing in TZ and foreign funded projects would be closely monitored by the donors to the benefit of the intended recipients as opposed to the fisadi leaders hence the intended civilians continue to suffer.
ReplyDeleteI commend the technological advancement in our country, Radio and TV stations have somewhat failed to shed more light on issues relating to our govt leaders due some strict rules set by 'them' so as to protect their interests to the eyes of the general public in favor of winning votes during general election.
But time has come for our leaders to be 'striped' out in 'black and white' and the general public need to be alerted of the truth behind the people they've elected lest we end up developing individuals rather than developing the country as a whole. Internet rules, fibre optic optimise the connection and let the world know the truth...
Mungu Ibariki Tz.
huyu mtu hatufai toka aingie yeye bunge limekuwa la majungu, makundi na lisiloelewa. Bunge sasa limekuwa kama nyumba ya majungu tu lakini mbona wakati wa msekwa kulikuwa hakuna hv vitu bunge lilikuwa na heshima yake anazungumzia maadui zake yeye c alichekelea wakati kina lowassa wanaondolewa kwenye madaraka akaacha hadi safari ya nje aliyokuwa naye ili awepo kwenye kikao cha kujadili ripoti ya richmond siku hazigandi mzee, yeye anataka kumkosoa kila mtu kwani yeye ni msafi. Uchaguzi wenyewe alitumia pesa nyingi sana yeye na mwenzie salim ahmed salim ilimradi akishinda akaibomoe serikali ya kikwete na kwa kiasi kikubwa kafanikiwa lakini sasa ndi mwish wake.naomba kuwasilisha hoja
ReplyDeleteKuna mambo matatu yaliyonigusa katika maneno ya spika:
ReplyDelete1. Ametumia maneno "maadui zangu". Japo wahenga walisema Adui Mpende, kwa kawaida wanadamu huenda kinyume. Uadui wa Mmatumbi kwa Mmatumbi hauliletei taifa letu manufaa yoyote!
2. Amesema wabaya wake "wako Dar es Salaam wanamsikiliza". Inaashiria kwamba anawafahamu hao watu ambao anawaita wazushi. Kama kweli kuna watu wanaoleta uzushi na kitendo chao ni kinyume cha sheria kuna vyombo vya dola vinatetea haki za kila mwananchi. Natumai spika amevipa vyombo vya dola taarifa na ombi lake la ulinzi kwa Waziri Mkuu linamaanisha kwamba angependa Waziri Mkuu atambue kwamba vyombo vya wizara ya mambo ya ndani vimepewa kazi.
3. Ni kama amejihakikishia Uspika kama asipokumbwa na mambo yaliyo nje ya uwezo wa kibinadamu. Haya ni mambo ambayo Watanzania hawataki kuyasikia ya uongozi kuwa utawala wa kisultani. Kibaya zaidi wanapoenda watu Urambo na kusaidia kuleta maendeleo wanaonekana ni maadui wa Spika wanaotaka kuchukua kiti chake. Kile kiti sio chake, ni cha Watanzania. Kazi ya kuchochea harakati za maendeleo ya Urambo sio mpaka uwe mbunge tu, hata ukiwa Mtanzania mwenye nia na uwezo wa kufanya japo jambo dogo, uwepo wa mbunge haupaswi kukuzuia. Kina Mashaka waogope kutoa misaada kwenye hospitali kwa ajili ya kumwogopa mbunge ataelewaje???? Tutakuwa hatufiki!!!
Nilidhani SPIKA anachaguliwa, Kumbe kuna wengine wakiwa hai tu washakuwa maspika??? eti Mungu akiniweka HAI NTAENDELEA KUWA SPIKA...Huu ni ubaradhuli uliopita mipaka. SPIKA anasupport rushwa kwa kusema wakipewa PIKI PIKI wanaongezewa uchumi na kuondoa Umasikini??
ReplyDeleteNyie mnaomponda spika inaonyesha ni kiasi gani hamjui siasa za nchi hii. Huyu ni spika wa kwanza kuruhusu mjadala wa kuiadhiri serikali kwa rushwa na kufanya waziri mkuu ajiuzulu. Spika wa kwanza kuruhusu marais wastaafu waelezwe ukweli bungeni kutokana na walivyotuibia. Mafisadi sasa hivi hawana raha sababu anaruhusu mijadala kwa kina kuliko spika yeyote aliyewahi kutokea nchi hii. sasa ukizingatia amewabania mafisadi ulaji, hivi ni kitu cha kushangza kuona hizo tuhuma za maji taka mitandaoni. Ana mapungufu ndio, lakini kwani nani hana?
ReplyDeleteRipoti ya CAG ambaye ofisi yake ina mamlaka ya ukaguzi na wataalamu wa hali ya juu wa auditing, wameipa ofisi ya spika clean report ya matumizi kwa mwaka ulioisha. Vitabu vipo in order.
Sasa huko kukaa kwenu ulaya na kudhania habari za mtandao niza kuzichukulia jumla, mungeanza na wamarekani wanaosema Obama ni rais batili sababu alizaliwa kenya na kwenye internet hizo habari zimejaa...Mnasemaje?
Acheni ujinga wa kudandia kila stori na kuimeza nzimanzima kama chatu, mkishaimeza ndo mnakua kama mazezeta sasa, mafisadi wanawang'ong'a!
Watu wanapanga foleni sinza kuchukua bahasha za kuja kuwasafisha mafisadi na nyie wengine mdandania treni kwa mbele kama mandondocha.
Michuzi usinibanie comment wapuuzi wanaibiwa nchi yao huku wanajiona halafu yanabaki ushabiki tu.
Nimeandika makala fupi kuhusu kuandamwa kwa spika. Nimejaribu kuuliza maswali ambayo ikiwa Spika ataweza kuyajibu kunaweza kuleta mwanga juu ya nini kinachoendelea. Inapatikana hapa: http://drfaustine.blogspot.com/2009/07/ya-spika-wa-bunge.html#links
ReplyDeleteMdau
Faustine
MIMI NAFIKIRI KUNA KITU HAMJAKIELEWA AMBACHO AMEONGEA 6,NI KWAMBA KAOMBA ULINZI KWA MKUU,NI KWAMBA ULINZI ALOOMBA NI KUHUSU UCHAGUZI UJAO KUTOKA SERIKALINI WAKUWEZA KUMUWEKA TENA MADARAKANI NAFIKIRI MIMI NDIO ALICHOOMBA HICHO.MAANA KAMA ULINZI ANAO TAYARI,NINI ANATAKA KAMA SIO KULINDWA KTK UCHAGUZI?.NAWAKILISHA!
ReplyDeleteHAKUNA VITU VIPYA .TUWE WAWAZI UCHAGUZI KARIBU KUPAKANA MATOPE,KASHIFA NA SIASA CHAFU NDO MUDA WAKE HUU...SIX ULIHAMA KUNDI,AMBALO LILIKUWEKA HAPO..WANATAKA KITI CHAO...BLOG IWE
ReplyDeleteHURU SIO GREEN TU...
TANGANYIKA MZALENDO
Vita ni Vita Mr Sitta, Pambana ndo sihasa hiyo uliyataka mwenyewe, kwani ulimaliza mkataba Pal uwekezaji au mbio zako za kutaka makubwa, Ukubwa jaaa la taka unalalamika vipi? achia uspika na ubunge kama kuna mtu atakufuata urambo ukiwa unalima Tumbaku yako na kula michembe
ReplyDeleteNAUNGANA NA ANONYMOUS WA 11:29 KWAMBA WATANZANIA TUWE TUNAJARIBU KUCHAMBUA HOJA WA KUANGALIA PANDE ZOTE MBILI! SIKATAI SIX ANAMAPUNGUFU YAKE! LAKINI HATA SIKU MOJA SITA HAWEZI KUFANANISHWA NA MSEKWA! HUWEZI KUSEMA SIX NI DIKTETA KULIKO ALIVYOKUWA MSEKWA NA WENGI TUNALIJUA HILI! NI UKWELI USIOPINGIKA KUWA TUKIWEKA SIASA PEMBENI NI SPIKA WA KWANZA AMBAE AMELIFANYA ANGALAU BUNGE LIWEZE KUWAJIBIKA! NDIO TUNAWEZA TUKASEMA KUTOKANA NA MAKUNDI LAKINI SISI KAMA WANANCHI TUNACHOANGALIA NI MATOKEO! TUMEONA ANGALAU SASA HATA BAADHI YA WABUNGE WENYE UJASIRI WANAONGEZEKA! TOFAUTI ZA ENZI ZILE NI ALIKUWA MZINDAKAYA NA NJERU KASAKA TU! MIMI NIKIASHA PEMBENI MAPUNGUFU YA SIX LAZIMA NIKUBALI BUNGE LIMEBADILIKA ACHILIA MBALI MAKUNDI, MITANDAO, U-CCM NA UKANDA! NAPENDA KUSEMA TUTAFIKA TU
ReplyDeletekaka asante kwa habari hii mimi nimeona waraka wenyewe kusema ni mbaya kwa wafanyakazi wote wa bunge si spika peke yake lakini baadhi ya maandishi ni uzushi mtupu hayana ukweli ndani yake alafu hakuna adress ya mwandikaji bali ni mambo ya kutunga na mengine ni kweli lakini nafikiri ni kwasababu ya 2010 uchaguzi kama keli anajihami aweke adress na ninani au ni akina na nani kaka michuzi mimi sio mtalaam sana wa computer ila naomba utuwekee hapa uwanjani kila mtu asome ili aone mambo yalivyo ya kungaunga ni hayo tu.
ReplyDeleteHii kauli ya maadui wangu na kutaka aondoke katika cheo alichonacho iliwahi kuitoa Lowasa katika sakata la Richmond. Hivyo kama spika ni msafi basi iundwe kamati itafiti jaombo hili kisha iwajulishe watanzania. Asifanye mambo ya ajabu, wengine wakituhumiwa huwekwa ndani chini ya ulinzi ili wasikimbie, yeye baada ya kutuhumiwa anataka alindwe. Awekwe rumande kama wangine na habari hii ifanyiwe kazi asitufanyie ujanja.
ReplyDeleteHoja hujibiwa kwa hoja...spika aache kuleta longolongo. Tuhuma zimeandika majina na namba za magari husika. Badala ya kujibu tuhuma anaingiza mambo ya kampeni za uchaguzi ujao. Kama anaona yanayodaiwa si halali, basi ajitoe kimasomaso kupangua kila tuhuma na si porojo. Inawezekana usemi wa Lowassa kuwa "hakuna kiongozi aliye msafi" ni sahihi.
ReplyDeletespika anatoa ajira za kidini hivi karibuni ajira wapewe wakristu watupu bungeni toka NYEGEZI.
ReplyDelete