SERIKALI imeyataka mabenki nchini kupunguza riba ili wateja wakope nayapeleke sehemu kubwa ya mikopo yao katika kilimo ili kuleta maendeleo ya haraka ya uchumi nchini.
Mwito huo ulitolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipozindua tawi la Benki ya Biashara ya Afrika (*Commercial Bank of Africa - CBA*), Barabara ya Nyerere jijini Dar wikiendi hii.
Waziri Mkuu Pinda alisema kuwa Serikali, kwa upande wake, imeiimarisha sektaya fedha na kusababisha Benki za Biashara nchini kuongezeka kutoka 2 mwaka1991 hadi 34 mwaka huu.
Serikali pia imeanzisha Mahakama ya Biashara kushughulikia mashauri yabiashara na pia imerekebisha Sheria ya Ardhi ili kurahisisha mikopo yanyumba, ikiwa ni sehemu ya mabadiliko na uboreshaji wa sekta ya fedha nchini, alisema.
“Tunatarajia kuwa riba katika mabenki zikishuka, mtakopesha wateja wengi nahivyo kupanua wigo wa mikopo kwa sekta binafsi ambazo zitasaidia kukua kwauchumi,” alisema.
Aliongeza: “Kama Benki zetu hazitaweza kutoa mikopo kwenye kilimo,kutarudisha nyuma juhudi za Serikali za kuboresha maisha ya Watanzania nauchumi wa nchi yetu kwa jumla.”
Waziri Mkuu Pinda aliisifu benki ya CBA kwa kurejesha upya mikopo kwa ajiliya ujenzi wa nyumba miaka 15 baada ya kufilisika kwa Benki ya Nyumba (*TanzaniaHousing Bank - THB).*
Mapema, Ofisa Mtendaji Mkuu wa CBA, Bw. Nehemiah Mchechu alisema benki yake ni ya Kitanzania halisi kwa kuwa watendaji wake wote ni Watanzania.
Bw. Mchechu alisema Benki yake itatoa huduma ambazo Watanzania watazifurahiakwa kuwa kaulimbiu ya CBA ni “Benki isiyo na Mfadhaiko” (Stree FreeBanking).
hivi viongozi wetu wanaelewa namna haya mabenk yanafanya kazi? Watapunguzaje riba kwani wao wanafanya kazi ya kanisa? Does PM understand risk involved kukopesha wajasiliamali?
ReplyDeleteTusichanganye siasa na biashara
Namna hii private sector itawaje na ushindani?
hao ndiyo viongozi wetu
HIVI NI MAPENKI AU MABENKI...YAWEZEKANA NIMESAHAU KISWAHILI?
ReplyDeleteWEWE BWANA! NI STRESS FREE BANKING NASIO STREE FREEBANKING.
ReplyDeleteAnita,
ReplyDeleteTuliza boli. Benki za Bongo zina charge riba kubwa kupita kiasi. Kuna watu wanapigwa mpaka 30%. Hiyo ni haki kweli.
Tatizo hapa kwetu Bongo mtu kupata mkopo ni deal. Yaani inakuwa kama si haki ya mteja kupata mkopo.
Namuunga mkono PM. Tunaomba baadae ahamie kwenye kampuni za simu za mikononi. Bei zao nazo ni za kuua mtu.
Anita,
ReplyDeleteNasikitika kuwa labda hujui jinzi gani benki za kitanzania zinatoa mikopo ama ni kuwa na hasira na viongozi wa kitanzania. Mimi mchango wangu kwa hili ni kwamba ninamuunga mkono kabisa waziri mkuu. Benki nyingi za kitanzania hazipo kwa ajili ya kumsaidia mwananchi wa kawaida hasa ukija kwa utoaji wa mkopo. Mfano benki nyingi sana nyumbani zinatoa mikopo kwa riba kati ya asilimia 20 na 25. Mfano ukichukuwa mkopo wa sh.4000,000/= ambao utatakiwa uulipe kwa muda wa miaka mitatu kwa riba ya aslimia 23, basi mpaka unamaliza kulipa mkopo utakuwa umelipa kiasi cha shs.6,800,000/= Riba ya asilimia 23 utakuwa umeilipa benki kiasi cha shs. 2,800,000 ambayo ni sawa na asilimia 70. Mlipajia atakuwa analipa kiasi cha shs.189,000 kwa mwezi. sasa kama huu siyo wizi ni nini? Mfano nchi nyingi zilizoendelea zinatoa mikopo kwa asilimia 4 mpaka 7. Ambao nikichukua mfano huohuo wa hapo juu wa shs. 4,000,000. kawa riba ya asilimia 6 kwa miaka mitatu mpaka mwisho wa mkopo mlipaja atalipa kiasi cha 4,720,000/= ambayo ni ongezeko la shs. 720,000/= sawa na asilimia 18.Mlipajia atalipa kiasi cha shs.132,000 kwa mwezi. Sasa ukiangalia ni nani anaumia????
sio MAPENKI NI MABENKI
ReplyDeletekwani base rate ni ngapi???!!
ReplyDeleteSijawahi kusikia Benki Kuu wanatamka base rate...maana hapa UK tunajua ni 0.5% na US is even lower, Japan ilikuwa 0% kwa muda mrefu ..Ya kwetu ni ngapi??
Does it matter????!!
Na pia Tanzania hutegemea zaidi mauzo ya amana za serikali(treasury bills) katika kuweka riba kwa njia ya soko, hivyo kwa kuwa serikali ilikuwa inatoa riba kubwa hadi 15% mapenki yakaona bora yaikopeshe Sirikali kuliko mtaani maana wasiwasi wa kutokulipwa ni kidogo.
baadae nafikiri mwaka mmoja tu hivi umepita serikali ikaamua kupunguza kukopa kwa mabenki ili watafute wateja wao hivyo ile rate yao ikashuka hadi karibu na 10%(mara ya mwisho nilipocheki).
Hivyo kama serikali kwa kupitia benki kuu inatoa riba kubwa hivyo unategemea mlalahoi atachajiwa ngapi?? Si tunasemaga serikali haiishiwi?!!(sio kweli lakini...uliza Argentina,nk)
Sasa Mzee Pinda aache siasa akae na wahusika wauangalie mfumo mzima wa riba na aone ni jinsi gani unaweza kurekebishwa kitaalamu si kwa maombi( sio kwa Mkwera hapa)