emma akisaidiwa kwenda chooni
emma akisubiri kuingizwa chooni

Mdau wetu haya ndio mazingira anayoishi kijana Emanuel Urio, Aliezaliwa jijini Mwanza akiwa na ulemavu wa kukosa mikono na miguu.
Emanuel anaweza kujiendeleza na mambo mengi endapo atapata msaada kutoka kwako.Mdau wewe umempa nini Mungu kukuleta duniani bila kasoro yoyote? MSAIDIE EMA NA MUNGU ATAKUONGEZEA.
Kitu ambacho Ema anachukia ni kukaa barabarani akiomba msaada,anapenda sana kusoma, kuchora, kuimba na mambo mengine meengi.Namba zake za simu ya mkononi ni,
+255 757 839 674
picha na habari zingine

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. kaka michuzi inabidi tumshukuru mungu kwa kila jambo mungu anamaajabu yake kweli mtu anaishi kwa kufanya kazi unaweza kujiuliza vipi anafanya kazi lakini kwa mungu ilo ni dogo sana.

    ReplyDelete
  2. jamani wadau wenzangu tumsaidieni huyu kijana kwani kutoa ni moyo si utajiri
    hebu fikilia aliyemuumba yeye ndiye muumba wetu sote

    ReplyDelete
  3. Serikali inatakiwa iuze gari moja la mbunge impe hela.

    ReplyDelete
  4. Badala ya kumsaidia mlemavu mmoja mmoja ni bora tungeshinikiza policy change huko serikali ili watu wa aina hii wasaidiwe kwa ujumla wao cause naona hapa ni wale wanaobahatika kupata fursa ya kutoka katika blog na news sites nyingine ndio watasaidiwa ila tukiwa na petition kama ilivyofanyika kwa albino, walemavu wote watasaidiwa.

    ReplyDelete
  5. hujafa hujaumbika, Sisi tuliyo wazima wa afya yatupasa kupiga goti na kumshukuru mungu kwa kila jambo na kila tunapopata wakati ni kushukuru kwani si kwamba ni wema sna mpaka tuwe salama.

    ReplyDelete
  6. mwenyezi mungu ametuumba tofauti lakini sote tuna haki sawa mbele yake. umejaliwa mikono yenye nguvu na miguu yenye nguvu jiulize kwani wewe una nini hadi ukapendelewa kuwa hivyo, na huyu alikosa nini hadi akawa hivi. kama umeumbwa ukiwa kamili na bado uko kamili hadi sasa basi ni wajibu wako wewe na mimi kuwasaidia wasio kamili kama huyu bwana. tuwasaidie na kuwaombea furaha ndugu zetu walemavu

    ReplyDelete
  7. SASA TUNATAKIWA TUSAIDIE NINI? EBU TUFAFANULIE KIDOGO. PAMOJA NA HILO MIMI BINAFSI NAONA SERIKALI KWA UPANDE WA USTAWI WA JAMII HUWA WANAFANYA NINI NI SEMINA NA KUJILUNDIKIA MISHAHARA MIKUBWA TU. SISIWALIPA KODI TUNALIPA KODI NI PAMOJA NA KODI YETU ITUMIKE KWA WATU KAMA HAWA WANATAKIWA KUWEKWA PAMOJA NA KUHUDUMIWA HADI SIKU ZAO ZA MWISHO HAPA DUNIANI WAJENGEWE HOME CARE CENTRE IWE NA KILA KITU IKIWA PAMOJA NA DAKITARI, NURSE NA WAHUDUMU WA KUWANGALIA KWA GHARAMA YA PESAYETU YA KODI/TAX

    ReplyDelete
  8. HAPO NASHAURI INGETENGENEZWA SEHEMU YA YA KUWATUNZA HAO WATU KAMA CARE WAHUDUMIWE HAPO.

    ReplyDelete
  9. huyu msela yuko fiti sana, yaani anauwezo wa kufanya vitu vingi sana kama kuandika msg kwenye simu, kuandika kawaida, na kadhalika, ila tatizo anamind ulabu na milupo! Aache hizo!

    ReplyDelete
  10. Walemavu kama hawa wanahitaji msaada wa kudumu wa mahitaji yao na vifaa vya kuwasaidia kuishi siku hadi siku. Hili ni jukumu la serikali kufanya hivyo. Namshukuru mdau aliyeleta hii picha ambayo imeamsha hisia zetu na kutufanya tufikirie zaidi na kutafuta njia za kusaidia walemavu.

    ReplyDelete
  11. Namuunga mkono mdau Francis wa trh 8.9.09, 12.27 am. Ni vigumu kusaidia mtu mmoja mmoja kwa kuwa wengi hawawezi kupata fursa ya kuonekana ktk blog. tunatakiwa kushinikiza serikali iwe na sera ya kusaidia watu kama hawa na kuwe na utaratibu wa kuwatambua. Nadhani kwa kuanzia mfuko wa majimbo ambao umepigiwa sana kelele utoe kiasi kwa ajili hii kwa kuwa ni rahisi wabunge kuwajua walemavu ktk majimbo yao.

    ReplyDelete
  12. Wswahili wa michuzi ndio origino-maneno meeeeeengi,kutoa hamna. Kwanini usitoe ndio baadae ukamwaga maneno yako kibao?

    ReplyDelete
  13. Wadau wa Michuzi waswahili kweli kweli,maneno meeeeeeeeeeeeengi kutoa hamna. Kwanini msitoe halafu maneno baadae.

    ReplyDelete
  14. Naomba kufafanuliwa anawezaje kuchora bila mikono na miguu! afu kuna mdau hapo juu kasema ana uwezo wa kuandika meseji kwa simu na kuandika kawaida, how is it possible? Naomba ufafanuzi

    ReplyDelete
  15. wadau wenzangu serikali MAANAYAKE NI SIRI KALI AU WIZI MTUPU HAWA WATU WAPO TOKA MIAKA TANZANIA INAPATA UHURU KWA WAKAAZI WA MWANZA MTAMKUMBUKA MZUNGU MMOJA HIVI SASA NI MAREHEMU KEREMENT ALIKUWA ANAKAA NAO WALEMAVU ALIWAJENGEA SEMUMU KUNAITWA BUJORA
    NINAMAANA GANI BASI YAANI MPAKA MTU WA NCHI NYINGINE ANAONA ILA VIONGOZI WAO HAWAONI HATA PAKIWEKWA CENTER ITAKUWA NI KAMA SEHEMU YA KUWATESEA TU KWANI VIONGOZI WETU WALIO WENGI HAWANA UTU ILA NI UCHU MTUPU HIVYO LABDA WAWE WANAWAPA KIPATO KWA KILA MWEZI WAJISAIDIE HUKO MAKWAO KULIKO WAKARUNDIKWE SEHEMU MMOJA NA KUANZA KULISHWA MAHARAGE YALIYOOZA NA MAFISADI.

    ReplyDelete
  16. Francis we umeongea. Na si walemavu tu, kuna shida mbalimbali hapa nyumbani.

    ReplyDelete
  17. huku marekani na ulaya watu kama hawa ndio wanajadiliwa bungeni jinsi ya kuwasasaidia lakini sisi wabunge wetu wamejaa ushabiki wa dini zao wakati kusaidia watu kama hawa ndio dini safi hivyo tunaomba wabunge badala ya mijadala ya dini wajadili hil ok

    ReplyDelete
  18. nampa pole mdau mwenyeulemavu pamoja na watu wanaomsaidia, kitu kinachonisumbua ni kwa nini wametuletea picha za chooni? ina uhusiano gani na kuomba msaada, pili raisi alipokuwa huku california alituonya tusijihushe na utatuaji wa matatizo ya matibabu, mashule pamoja na muindo mbinu kwa sababu hiyo ni kazi ya serikali, mi nafikiri tuchangie gharama za kuwapeleka watu kama hawa na wengineo kwenye ukumbi wa bunge kikao kijacho ili wabunge watatua matatizo ya kweli ya watu wao na sio kubishania vitu vya kijinga

    ReplyDelete
  19. Mimi siamini kama ulemavu ni sababu ya kuwa ombaomba. Kwa maoni yangu, naona kuwa wazazi wote wenye watoto walemavu ombaomba washtakiwe kwa kutowapa matunzoi sahihi watoto wao, kwani walemavu wote wanwpopelekwa shule husomeshwa na serikali bure. Mifano ipo mingi sana kwani kuna hata kipofu mwenye PhD ambaye asingepewa fulsa angekuwa Morogoro road/biib titi junction akiomba omba

    ReplyDelete
  20. KAMA SERIKALI INA BILIONI 19 YA KUTENGA KWENYE BAJETI KWA AJILI YA CHAI KWENYE WIZARA ZAO BASI PIA INA HELA YA KUJENGA NYUMBA ZA KUWALEA WALEMAVU NA HIO ITASAIDIA KUTOA AJIRA KWA WATU PIA WATAKAO FANYA KAZI KWENYE NYUMBA HIZO.NA NINA HUAKIKA WATAPATA MISAADA KWENYE KITENGO HICHO.KILA SIKU SERIKALI HAINA PESA LAKINI UKWELI HELA ZIPO NYINGI SEMA VIONGOZI HAWANA AKILI YA KUPANGA MAMBO NA MWISHO WAKE ZINA FUJWA TU.MAMBO YA KUONGOZA NCHI KIJANJA JANJA YAMEPITWA NA WAKATI HAYO WATU INABIDI WAONGOZE NCH NA KUONESHA JAMBO LIPI WAMELETA JIPYA LIMESAIDIA KWENYE JAMII.
    HAIWEZEKANI HELA YA KUIBIWA NA MAFISADI HIWEPO LAKINI HELA KUSAIDIA WALEMAVU AU WANAFUNZI WAPATE MADAWATI HISIWEPO HUO NI UONGO NA WIZI MKUBWA.
    naomba usibanie hii comment michuzi kama kweli una jali walemavu wa nchi yetu.MDA UMEFIKA SERIKALI HIFANYE KAZI KUWASAIDIA WANANCHI NA SIO KUWATUPA TU.

    ReplyDelete
  21. kwanza kabisa nielekeze pole zangu kwa huyu bwana,na kwa wale wote wanaoshiriki ktk utunzaji wake.
    pili nichukue fursa hii kufuta dhana ambayo watu wengi wamesema hapo juu kwamba mungu ndiye alimuumba hivi,hii ni kumfanya huyo muumbaji kuwa ni dhalimu na mwenye upendeleo kwa baadhi ya watu,hivyo si kweli kuwa mungu anaumba watu walemavu,ila kuna sababau zinazoweza kupelekea mtu kuzaliwa na ulemavu kama hzi hapa chini:-
    1.mja mzito kuugua surua,au baadhi ya magonjwa mengine wakati mimba ingali changa wakati viungo ndipo vinaanza kujitengeneza na havija kamilika.
    2.matumizi ya baadhi ya madawa kwa mfano aspirini n.k wakati wa mimba changa.
    3.mionzi kama ya nuclear(nyuklia),x-rays na aina nyingine wakati wa mimba changa,au kama itatokea miali ya nyuklia kumuathiri mtu yeyote yeye hatapata ulemavu,ila vizazi vyake vinaweza kuathirika kwa kurithi madhara.
    sasa wanao msingizia muumbaji kuwa ndiye kamuumba akiwa mlemavu,si ajabu ndio wakwanza kutokwenda kupata chanjo,au tiba wanaposhauriwa,au pengine ndi wakwanza kujifanya madaktari wa kujitibu kwa kununua madawa kama aspirini madukani na mengineyoo ilimradi ilimradi du walisha ona mtu anadalili kama za ugonjwa wao na katibiwa kwa dawa hizo basi nao bila kutafuta msaada na ushauri wa daktari aliyesomea tiba wanaanza kujitibu.kumbe hajui hata kama ni mjamzito wa mimba changa au la!

    mdau.

    ReplyDelete
  22. michuzi naomba usipuuzie maoni yangu,mimi naomba kama inawezekana tumjengee choo cha ndani,mimi sijui mazingira ya hapo wanapo ishi ila kama akipata choo cha kukaa itakuwa nafuu sana kwakwe pamoja na familia nzima.
    sijui kama unaweza kuwasliana nao mimi naomba tulivalie njugu hili swala ili huyu kaka apate msaada.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...