sehemu ya magomeni mapipa jijini dar enzi za mwalimu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Tunaomba utuwekee picha mpya ya hii sehemu enzi ya Jakaya Kikwete.

    ReplyDelete
  2. Bwana Michuzi hapa utakuwa unakosea.Hizi si enzi za Mwalimu.Mwalimu alikuta hali hii toka kwa wakoloni na yeye ndio kafanya uchafuzi mpaka Manzese ,Mburahati, Mwananyamala Kisiwani ,Kinondoni ,Kimara nk Hizi ni baadhi ya muda Nyerere kuingia madarakani haya maeneo yalianza kuchafuka kukawa hakuna mifereji ya maji machafu(Drainage system) hakuna plan za barabara wala nyumba ujenzi holela chini ya Uongozi wa Waziri wa kazi ambaye alikuwa chini ya Uongozi wa Mwalim.
    Ndugu yenu
    Mnyapala Wa Jela ya Butimba enzi za Mwalim

    ReplyDelete
  3. Uliyeomba tuwekewe picha mpya ya sehemu hiohio nakupa hongera.

    Tuangalie maendeleo toka siku hizo.

    I guess watu watalia wakiona picha mpya

    ReplyDelete
  4. Ilikua imejengeka kufuata plan siyo holela kama leo

    ReplyDelete
  5. Hiyo sio plan ya Nyerere, hizo nyumba unazoziona hapo zilijengwa na wakoloni, kulikuwa na barabara za lami na taa usiku lakini Nyerere hakutoa hela za ukarabati.

    ReplyDelete
  6. Kuna ukweli kuwa WAKOLONI WALIJALI MIPANGO MIJI KULIKO WAZALENDO.
    Hakuna ubishi kuwa hapa unaona mji ulivyotakiwa kuwa, sasa hivi ni kinyaaa.
    Labda kwenye maongezi yajayo, mheshimiwa Rais atutafsirie maana ya neno MAENDELEO maana naona "kila kitu" chema chazidi kuporomoka

    ReplyDelete
  7. Chacha WamburaSeptember 24, 2009

    Kwenu ma-anony wote mlopinga sentensi ya 'Enzi za MWalimu'. Kwa mawazo yangu ya kikurya ni kuwa tuangalie picha hiyo katika enzi za mwanzo mwanzo wa utawala wa mwalimu na tuilinganishe na hali ilivo sasa kuanzia wasaidizi wa mwalimu walipoanza kuboronga.

    Nadhani tutakuwa tunakosa point tukisema tu enzi za mwalimu kwa kumaanisha kuwa yeye ndo alofanya hayo.

    Nanunua wazo la kutuwekea migo mgo ya sasa ili tuijadili

    ReplyDelete
  8. kwa kwei nyerrere kachangia vitu vingi saana kudorora sijui kwa nini wanamfagilia kiivyo watu hadi wanamaliza chuo kikuu na ukanumba sababu ya nyerere na ujamaa ushuzz

    ReplyDelete
  9. Sasa Mbowe akisema hali ya sasa afadhali enzi ya Ukoloni mbona mnamtukana..!!???

    Enzi hizo barabara zilikuwa safi, maji safi, elimu bomba, matibabu bomba, usafiri ndio kabisa barabara na reli mpaka mashambani, viwanda vinazalisha kama kawaida...leo kiko wapi; 90% ya watumishi wa umma ni majambazi..!!

    ReplyDelete
  10. KWA WALE WASIO NA MAKENGEZA WANAONA NYINGI YA NYUMBA HIZO ZILIJENGW2A NA SHIRIKA LA NYUMBA BAADA YA UHURU NDIYO SABABU UKIZIANGALIA UNAONA ZINAFANANA. NYUMBA HIZI ZILIJENGWA CHINI YA MPANGO AMBAO MWENYE NYUMBA YA MITI ANAKUBALIANA NA NHC WNAMJENGEA KISHA ANALIPA KILA MWEZI KIDOGOKIDOGO MPAKA DENI LITAKAPOKWISHA, HUO ULIKUWA NI MPANGO MZURI SANA NA HAUTARUDI TENA KWANI VYAMA VYA SIASA HAVIONI UMUHIMU WA KUWA NA SERA ZA MAKAZI!

    ReplyDelete
  11. Ni kweli ni enzi za Mwalimu alipopata fedha toka serikali ya Ujerumani kusafisha - 'Magomeni Makuti' yaani nyumba nyingi zilikuwa wa makuti eneo lote la Magomeni. Ndio maana kuna kajisehemu Magomeni Makuti mpaka leo hii kutokana na hali ilivyokuwa baada ya Uhuru wa Tanganyika.

    Shirika la Nyumba walipewa tenda hiyo 'kusafisha' na pesa zingine za Ujerumani zikajenga Chuo Kikuu Mlimani.

    Mdau
    Mtoto wa Mujini

    ReplyDelete
  12. Kama Milton Keynes vile

    ReplyDelete
  13. Bro Michu, mtazamo wangu ni kuwa maendeleo yapo! na bado hisia zangu zinanituma niamini kuwa wadau wanaokandia kuwa hakuna maendeleo Migo migo, naomba warudi walikokuwa [nina maana walikozaliwa] sababu wao ndiyo haswa wanaoharibu Migo migo. Wao ndiyo chanzo kikubwa cha uharibifu wa Migo. Tena utakuta wao ndiyo wa kwanza kuomba kujenda kiholela stoo bubu, maghorofa, na pengine wengine hata bila kupata vibali halafu sasa wanataka kumlaumu Mwalimu bure. Idadi ya watu inaongezeka, ona wanavyozaana, hawana hata habari na nyota ya kijani!. Hebu jiulize enzi ya Migo migo iliyopo pichani watu waliokuwa wakiishi Dar walikuwa wangapi na sasa kuna watu wangapi! Wizi mtupu, Wapemba kibao, Wapare kibao, Wanyakyusa kibao, Wafipa tele, Wahaya kibao mnoo, Wachaga utadhani hapa ndiyo kwao, walau Wakwere walikuwapo kidogo [kaka yangu Phil, enzi za mtaa wa Kibondo], Wachina wanaacha kwenda kupanda mlima Kilimanjaro wanakuja Migomigo, Kariakoo, Sinza!, wizi mtupu.

    ReplyDelete
  14. mheshimiwa kweli mawazo ya watu yanafanana . mimi nilipoona picha ya zamani nikasema nitakuwa mtu wa kwanza kuomba picha mpya lakini wapo walionishinda hongera Tunaomba utuwekee picha mpya ya hii sehemu

    ReplyDelete
  15. yaani kama hazingewaondoa wakoloni mapema ....nchi hii ingekuwa bomba sana Mwl. aliwai sana kuwatimua wakoloni.....

    ReplyDelete
  16. Ni kweli Mwalimu kwa namna fulani alitufanye tudorore kiuchumi, lakini mimi sikubali kuwa ni sababu ya kuwafukuza wakoloni mapema,tukiangalia Zimbabwe yaliyotokea, wakoloni walikaa wakawekeza nakukifanya kila kitu chao!
    Alichokosea Mzee wetu ni kung'ang'ania siasa za Kijamaa, na wakati huo kulikuwa na vita ile vita ya Wajamaa na Mabebari. Na wajamaa ilibidi wajitolee hata kidogo walichonacho kuwasaidia wasio-nacho, wakati mabebari kila mtu anajituma kivyake.
    Uhuru ulikuwa na umuhimu wake lakini baada ya uhuru tulitakiwa tuwe kama Kenya, tusibanwe na sera za mataifa ya Kijamaa, tuwe kotekote.
    Utaratibu wa ujenzi na mipango miji umepotoshwa na mafisadi wetu wenyewe.

    ReplyDelete
  17. ILIKUWA BOMBA, MWALIMU HAD A VISION, WACHOYO WALIMKATISHA TAMAA TU NA UCHOYO WAO

    ReplyDelete
  18. NI UBISHI TU WA CHUKI NYUMBA HIZO ZILIJENGWA NA NATIONAL HOUSING CORPORATION MARA TU BAADA YA UHURU EARLY 1961 HAKUKUWA NA SHIRIKA HILO WAKATI WA MKOLONI NA MKATA ULIKUWA NI KWAMA WALE WOTE WALIOKUWA NA NYUMBA ZA MBAVU ZA MPYA WALIJENGEWA NYUMBA NA NHC NA KUWA WALIKUWA WANALIPA KILA MWENZI HADI GHARAMA YA NYUMBA INAPOKWISHA INAKUWA YAKE 100% NYUMBA KAMA HIZI ZILIKUWEPO SONGEA MFARANYAKI NJIA YA KUELEKEA MBINGA, HAPO DAR, ILALA, MAGOMENI, TEMEKE NA MIKOA MINGINE PIA, ACHA UBISHI USIO NA SABABU. NYERERE WAS A GREAT LEADER WITH VISION.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...