mdau pernille wa libeneke la http://pernille.typepad.com leo mchana alijikuta amekwama kwenye bonge la foleni sehemu za mkata, kiasi cha kilomita 7o hivi toka segera katika njia ya kuelekea tanga na arusha, baada ya wananchi wa hapo kufunga barabara kushinikiza mwenyekiti wao aondolewa madarakani kwa tuhuma za ufisadi. inasemekana mwenyekiti huyo alizuia mfanyabiashara mmoja wa maji ya kunywa na kumruhusu mwingine ambapo wa kwanza alikuwa anauza kwa shilingo 300/- na huyu wa mwenyekiti alikuwa akidai sh. 500. wakazuia barabara ili kufikisha ujumbe.
polisi walipofika ilibidi wafyatue risasi hewani kuutawanya umati wa watu ambao waliweza kuzuia barabara kwa zaidi ya masaa mawili. hatimaye muafaka ukafikkiwa na mweney kuuza maji bei chee akaruhusiwa kuendelea na biashara, na hatma ya mwenyekiti bado haijulikani
juu na chini ni tenka la maji ya bei poa ambalo linalakiwa kwa chereko na vifijo
















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. safi sana stand up for your rights

    ReplyDelete
  2. Namna hii maendeleo yatakuja! Hongereni sana wananchi kwa kudai haki zenu bila woga. Lakini wajameni, maji sh. 300 Kijijini?!!

    ReplyDelete
  3. We have been independent for 45+yrs and still water and electricity is a problem ............. what a shame.

    ReplyDelete
  4. This shows that the villagers are well organised, so why dont they go a step further.
    There are plenty of able bodied men who am sure can dig a well and then collect money and buy a well-head hand pump, and that will solve their problems Aluta Continua
    wakatabahu

    ReplyDelete
  5. any revolution start in small pace and then get bigger and bigger. siku moja watanzania tutajiuliza kwanini tulichelewa kutatua matatizo yetu kwa kushinikiza. kama umelala serikali will never wake you up. mapinduzi yanaanzia kijijini ni ajabu.

    ReplyDelete
  6. HII NI VIZURI SANA. KUNA WAZEE WA VIJIJI PALE ARUSHA SEHEMU ZA OLOSIVA SAKINA AMBAO WAMEKUA WAKITUMIA MAJI WALIYO PATA KWA MISAADA YA NJE KUPITIA SERIKALI KAMA VITEGA UCHUMI VYAO. UKITAKA KUYAPATA HAYO MAJI NYUMBANI KWAKO LAZIMA UTOE HONGO KUBWA. UFISADI MTUPU. I HOPE SERIKALI ITACHUNGUZA HILI JAMBO. WENGINE TUNAOGOPA KUTOA HII SIRI ILI TUSINYIMWE MAJI. KUNA WATU WASIO JIWEZA WANATESEKA SANA KWA KUKOSA HATA MAJI YA KUNYWA. MJI WA ARUSHA UNAHITAJI KUKUA KWAHIYO WANGECHUKUA SEHEMU KAMA HIZO. ITAKUAJE HAWA WAKUU WA ARUMERU WANAKATAA KUTOA SEHEMU KAMA HIZO WAKATI SERIKALI NDIYO YENYE KU OWN THE LAND.

    ReplyDelete
  7. Kuchimba kisima ni 3,000,000TSH .chenye uwezo wa kuhudumia wanakijiji wote,Lakini serikali inanunua gari la Mbunge kwa 40million TSH ,wakati atukioni wanachokifanya.

    ReplyDelete
  8. Kumbe uhuni waweza kusaidia MARA NYINGINE!

    ReplyDelete
  9. watanania wengi wanateseka kwa kukosa maji. serikali ina takiwa kulishuhulia hili jambo kwa bidii kubwa. hapa mjini arusha maji ni shida sana. michuzi hiyo habari hapo kuhusu maji sehemu za sakina tafadhali ipeleke kwenye magazeti ya arusha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...