Kikundi cha kucheza cha watoto wa
hapa Marekani kiitwacho Taratibu
Shughuli ya kuadhimisha miaka mitano ya Shina huko Lanham Maryland ilifanyika wikiendi iliyopita na ilifunguliwa na Abbas Missana kutoka Ubalozi wa Tanzania. Halafu kufuatiwa na hotuba ya kipawa cha Elimu na mchungaji Rochelle Durant. Na sala iliotolewa na Mchungaji Thomas Obrien wa kanisa la Kilutheri la Good Samaritan.

Waziri wa Kazi, Vijana na Wanawake wa Zanzibar Mh. Asha Abdullah Juma (shoto) wakiwa na Bi Jessica Mushala wanzilishi

Nacho kikundi cha kucheza cha watoto wa hapa Marekani kiitwacho Taratibu kilitoa burudani murua ya nyimbo za Kiswahili, Kizulu na Kiingereza na uchezaji stadi iliyofuatiwa na hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa maendeleo ya kazi, Vijana, Wanawake na Watoto wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Asha Abdullah Juma ambaye alitoa hotuba ndefu ila kwa kifupi alielezea kuhusu changamoto za wizara yake na malengo ya wizara hiyo kusaidia kupunguza,ufanyaji kazi wa watoto,lengo la kupunguza umasikini na kusisitiza kuwa elimu inaweza kusaidia kupunguza matatizo Afrika na pia alizungumzia juu ya mpango wao wa maendeleo wa Millenia.
Waziri Asha Abdallah Juma akiwa na maafisa Ubalozi Abbasi
Missana (kulia) na Suleiman Saleh(shoto).

Waziri Asha Abdullah Juma akiwa na Sunday Shomari wa VOA na afisa wa Ubalozi DC, Suleiman Saleh

Waziri huyo alielezea mapambano dhidi ya Ukimwi na vifo vya watoto ambapo alisisimua nywele za watu ukumbini humo alipotoa takwimu kuwa watoto wengi katika maeneo ya vijijini hawafikishi umri wa miaka mitano nchini kwake kwa kupoteza maisha halikadhalika aligusia ushindi wa kisiwa chao kutokomeza Malaria.


Alitoa takwimu mbali mbali mojawapo ikiwa 36% ya watanzania wanaishi kwenye umasikini mkubwa. Alielezea mipango ya maendeleo huko Zanzibar na kushukuru taasisi kama Shina zinazosaidia maendeleo ya wananchi wao na kutaka wengine waige mfano wao.

www.shaininc.org



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. naona Sunday shomari umenyuka pamba si mchezo,ukishuka kwa wala vumbi lazima wakuone tofauti na watajua tuu huishi wanapoishi wao,maana shower la maji ya moto kila siku na mashampoo shampoo na body washes lazima utakate tuu

    ReplyDelete
  2. Massoud Abiola, OHIOOctober 23, 2009

    Sunday mdoigo wangu, jihadhari na watu wazima, we haya weeee!!!

    ReplyDelete
  3. huyu Bi jessica Mushala ana uhusiano na Karl Mushala? namtafuta huyu mdau nilikuwa nae Tambaza 1996...
    mjoseph@yahoo.com

    ReplyDelete
  4. Sunday, alwayz handsome!

    ReplyDelete
  5. MATUMBO YA FROZEN FOOD UTAYAJUWA TU, MIKATE KWA MAHARAGE YA KOPO, NA MIKUKU ILIYOCHINJWA MWAKA JUZI

    ReplyDelete
  6. wee michuzi wee mbona nishai sana comment zangu mara nyingi unazibania au wewe blog yako hii ni ya serikali umefadhiliwa nao wewe vipi nishai sana wewe..
    basi na hii pia tia kapuni nishai sana wewe lakini sikulaumu si ulikuwa unafanya kazi serikalini wewe katika magazeti yao wewe ndo maana umepanda chati kwa kupigwa jeki na serikalini...

    basi na hii bania..

    laki kusema kweli huyu waziri bi ashaa ana roho mbaya sana tena sana mwache aritaye..nafasi kila leo anataka kwenda majuu peke yake nisha sana wewe na yeye pia

    bania comment hii pia..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...