Ndugu wapendwa,

Story ifuatayo ni ya kweli maana imenitokea mimi binafsi jana tarehe 11/11/2009. Najua kwa kiasi fulani itakuwa inaninizalilisha kwa kutokuwa makini lakini naona ni vyema niwashirikishe rafiki zangu ili msije mkatapeliwa kama mimi na wengine wengi wameshatapeliwa kama vile ndugu yake Galeba, laiti Galeba angeweza kutuelezea yaliyomsibu ndugu yake labda na mimi ningeweza kuepuka utapeli huu. Kinchosikitisha matapeli wenyewe ni watu wanaotufahamu vizuri.
-----------------------------------------------
Mnamo muda wa saa tano asubuhi nikiwa nyumbani (nipo likizo) nikapokea simu nisiyoifahamu kutoka kwa mtu ambaye alijitambulisha ananifahamu, na kwa jinsi alivyonitaja kwa jina na career background details zangu sikuwa na shaka kwamba hanifahamu. Mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo:

TAPELI: Mr. Alex Matovu habari za siku nyingi.
Mimi: Nzuri
Tapeli: Vipi bado unafanya kazi Blue Financial Services?
Mimi: Hapana, nani mwenzangu?
Tapeli: John, nilikuwa nafanya kazi Wizara ya elimu, na uliwahi kunisaidia nikapata mkopo, ila kwa sasa nipo World food programme, Kigoma kama Chief supplies officer.
Mimi: okay sasa nikusaidie nini John (ukweli nikwamba sikumkumbuka ila kwa kuwa tulikuwa tunatoa mikopo kwa wafanyakazi wa serikali, siku jiuliza sana , after all alikuwa hajasema anachotaka)

Tapeli: Sasa nina issue naomba unisikilize kwa makini, kama unavyofahamu WFP tunatoamisaada ya vyakula hivyo tuna maghala makubwa ya kuhifaadhi chakula, hivyo ili kuhakikisha vyakula haviharibiki huwa tuna weka presavative inayoitwa Damoline Liquid solution made in Sweeden, hii inapatikana MSD na kwa licensed dealers kama Mohamedi Enterprises. Kwahiyo tuli float tender mwaka jana na supplier aliyeshinda tulikubaliana anipe 10% lakini baada ya ku supply hayo madawa akanidhulumu na kunitisha kuwa iwapo nitamdai hiyo 10% angeniripoti kwa mabosi wangu. Kwa hiyo sikuwa na cha kumfanya bali kusubiri contract yake iishe alafu nimtafute supplier mwingine. Sasa ndio nikaona nikupigie ndugu yangu maana nakujua wewe hii kazi utaweza kuifanya ukizingatia unalipwa cash on delivery!

NOTE: nimeshawahi ku deal na supplies officer wengi hivyo sikuwa na doubt yeyote, bali nikaona hii is just another deal kama ambazo nimeshawahi kufanya successfully.

Mimi: Okay sasa unataka nifanye je?

Tapeli: Unachotakiwa kufanya ni kwenda MSD umuone Dr. Shija, huyu ndiye mkuu wa hapo na ndiye aliyekuwa supplier wetu wa zamani aliye ni dhulumu, sasa kwa kuwa sitaki kumpa kazi tena, wewe uende ujifanye unaulizia hiyo liquid solution, na u negotiate ujue atakuuzia shillingi ngapi. Kwahiyo nakutumia simu yake mpigie muongee akupe quotation, alafu akisha kupa bei nipigie ili nikuelekeze cha kufanya.

Basi wandugu nikampigia dr. shija, mwanzoni shija ana hesitate kuzungumza na mimi aki pretend kuwa hapendi kuongea na strangers na akataka kujua namba yake nimeipataje, sasa kwa kuwa siwezi kumwambia ukweli kuhusu aliyenipa namba yake, ikabidi na mimi niwe muongo kwa muda, nika pretend kuwa mimi ni mkulima na nahitaji hiyo presavative kwa ajili ya maghala yangu yaliyopo arusha. Basi akawa na imani na kukiri kuwa anayo stock yakutosha, na hiyo liquid inauzwa kwa pair ya chupa mbili zenye ujazo wa 1000mls, kila pair ni 1.2m. Sasa angalia nilivyoingia katika mtego, baada ya kunipa bei ni kaomba punguzo na akasema atauza kwa 1million.

Nikafanya kama nilivyoelekezwa na John wa WFP kuwa baada ya kupata bei nimjulishe nilivyomjulisha akasema kinachofuata ni kuwa mimi nitauza kwa USD. 1700, na tofauti kwa maana ya faida tutagawana, hivyo nisubiri aniunganishe kwa bosi wake for further final details.

Basi wandugu kama mnavyonijua katika issue za fwedha, nikachukua calculator ya simu ili nijue deal ina shillingi ngapi, hela zilivyokuwa nyingi hata calculator iligoma, maana WFP wanahitaji 50 pairs @ usd 1700, mimi nanunua kila pair kwa 1million ambayo ni kama usd 770 hivyo difference usd 930 x 50 pairs = USD 46500, ALAFU tunagawana pasu pasu. Guys you can imagine what was going on in my head!

Basi kweli muda si mrefu nikapigiwa simu na huyo bosi wake ambaye ni mzungu na mazungumzo yalikua kama ifuatavyo:

MZUNGU: This is Mr. Scheinder from WFP, are you the new supplier?
MIMI: YES
MZUNGU: Do you have enough stock of Damoline Liquid solution, we are looking for 50 pairs?
MIMI: Yes I have sufficeint stock
Mzungu: what is your price per pair?
Mimi:$1700
Mzungu: ahaaaaaaaa thats a very good price, do you want to be paid in dollars or TZS
MIMI: Dollar of course, you how how unstable the local currency is ( Hapo tena na mimi nataka kuonyesha kuwa ni International businessman)
Mzungu: No problem, we have enough dollars, you want to be paid cash or by cheque?
Mimi:Cash
Mzungu: Okay no problem, now listen very carefully mr. new supplier we need this liquid urgently possibly today, and since you have said you have enough
stock we are taking off this morning from Kigoma coming to Dar, please arrange for the transport to take us to Movenpick, we will pay usd. 200 for your fuel, but most importantly make sure you bring one pair of the sample with you.
Mimi: No problem at all I have been in this business for quite sometime now you can be sure everthing will be fine.

Masikini bila kujua nimeingizwa kingi, nikachukua cheque book, nikaandika cash withdraw 1million ili nikanunue sample yakwenda kuwaonyesha wateja wangu. Baada ya kutoka bank nikampigia dr. shija ili aniuzie hiyo sample, akasema kwa sasa ametoka ofisini ila sample anazo katika gari na alikuwa anaelekea Mwananyamala hosp, then Magomeni alafu Muhimbili, hivyo tukutane Magomeni hosp. Yaani jinsi nilivykuwa naendesha gari basi hata kama ni mashindano ningeweza kushinda, basi mimi mbio mpaka magomeni hosp namsubiri dr. shija. Nikampigia akasema yupo ndani hospitalini na yupo na mabosi wake asingeweza kutoka ila anamtuma kijana wake nimpe hizo fedha na yeye anipe hizo dawa, kweli ikawa hivyo kijana akaja akaingia kwenye gari nikamwambie anipe hizo sample kwanza nikazisoma ziko exactly kama WFP wanavyotaka! NIKAKABIDHI HELA 1 MILLION. Bila hata aibu yule kijana akaniomba 50,000/= nikamwambie asijali maana deal kubwa itakamilishwa saa nane.

Kwa kuwa wageni wangu walishaniambia niwaaandalie usafiri, nikampigia dreva tax wangu aje airport saa nane, nikamuuliza bei kutoka airport mpaka movenpick ni ngapi akasema 25,000 nikamwambia usijali ntakupa 50,000/=!!!!!!!!!!!!! (kumbuka mimi ntalipwa usd 200 ya usafiri).

Basi mimi mbio nikaenda airport terminal one kusubiri ndege ya WFP ili tumalize biashara, nilipofika kuulizia reception nikaambiwa hakuna kitu cha namna hiyo na mimi ni mtu wa 10 kutapeliwa, basi tena nikajirudia kimya kimya. Nikaenda kula chefs pride nikamsimulia jamaa mmoja yaliyonisibu, kabla sijamaliza akasema hata ndugu yake ametapeliwa wiki iliyopita, nikampigia Galeba akasema yeye jamaa yake alipigwa 3.5m last week.

Taarifa nilizonazo mpaka nikuwa hii ni network ya wahaya na mpaka sasa ni wahaya wengi wameishaibiwa ukilinganisha na makabila mengine.

So guys thats my story for yesterday!

Foward to everyone you know.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 75 mpaka sasa

  1. Ina maana ya kwamba huyu doctor Shija ndio kagawana hizo pesa na tapeli? naomba kuelimishwa maana wengine vichwa vizito.

    ReplyDelete
  2. Hakiyamungu nakwambia, huu mkenge mtu yeyote lazima angeuingia..hata uwe msomi vipi...shukrani kwa kutuhabarisha mdau na pole kwa yaliyokusibu.

    ReplyDelete
  3. I am speechless! Na nakupa pole kwa yaliyokusibu na kukushukuru kuweza kutujulisha manake hilo ni fundisho tosha kwa wengi.

    ReplyDelete
  4. Pole sana bro. Nashukuru kutujulisha, kwa kweli huu mkenge yeyote yule anaweza kuingia.

    ReplyDelete
  5. Alex pole sana kaka. kama mdau hapo juu alivyosema, huu mkenge mtu yeyote angeweza kuuingia. Tunashukuru pia kwa kututoa tongotongo kwa kushare hii kitu, Mungu atakubariki kwa hilo. POLE SANA KAKA, MAPAMBANO YANAENDELEA.

    Gordon chiggs

    ReplyDelete
  6. Hii ni sanaa ambayo imekuwa ikijirudia-rudia miaka nenda miaka rudi. Na kama watu hawatajiwekea priciples za maisha hii sanaa itaendelea kuishi kwa miaka mingi ijayo.

    Kitu cha kwanza tuondoe TAMAA katika nyoyo zetu. Once TAMAA ikiwa mbali na sisi basi tutakuwa tumejiweka mbali na majanga kama haya.

    Pili, any deal ya kutengeneza pesa nyingi bila ya efforts zinazolingana na wingi wa pesa, jiulize maswali mengi, ikibidi jiepushe nayo.

    Mwisho hakuna pesa inayoweza kuja kirahisi...kila mara jiulize na ikibidi share taarifa za awali na mtu unayemuamini...usifanye siri!!!!!

    ReplyDelete
  7. MAZEE HAWA WALINISUMBUWA LAST MONTH!
    KWA BAHATI NZURI HAWAKUFANIKIWA KWANGU, NILIWAITIA MWIZI WAMEKIMBIA. WANA MZUNGU MMOJA ALIYOCHOKA CHOKA, NINAZO NAMBA ZAO ZA SIMU BADO!

    ReplyDelete
  8. it sounded too honest to be involved from the beginning.at that time,it probably was....

    ReplyDelete
  9. POLE SANA, LAKINI KWA SASA WENGI WAJANJA WANAMBINU ZA KILA AINA.MIMI WIKI MBILI ZILIZOPITA SIMU ILINIOKOA KIAJABU NILISAHAU SIMU KWENYE NYUMBANI NIKAGEUZA KURUDI KURUDIA SIMU,KUFIKA NYUMBANI NAKUTA KUNA GARI LIMEPAKI NYUMBANI ETI WAMETUMWA NA MIMI MWENYE NYUMBA KUTENGENEZA FRIDGE NILITETEMEKA UKIANGALIA NJEMBA ZENYEWE HAZIKOSI KUWA NA CHA MOTO WAKAJIONDOKEA KIMYA KIMYA,KUWENI MACHO ACHENI MAAGIZO NYUMBANI ASITOE AU ASIRUHUSU MTU KUINGIA NYUMBANI BILA RUHUSA YA MAMA AU BABA MWENYE NYUMBA WAJANJA WENGI SASA!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  10. OOOHHH my god!! this is just bad!Matapeli sasa hivi wamezundua mbinu mpya na tafauti za kujiingizia pesa, especially ndugu zetu walio njee wametokea kuamini kila mtu! sio kila mvaa joho ni padre ndugu zangu wa majuu-TANZANIA TAMBARARE hata Yesu akishuka watamuibia vile vile, so please be careful and do not trust everything and anything..HILI NI FUNDISHO LA KUTOSHA HASWAAAA..POLE SANA WEWE ULIYEIBIWA MWENZIO SAA HIZI ANAFANYA SHEREHE NA MAHELA YAKO!! DUUUUU!

    ReplyDelete
  11. Sioni kwa nini uonekane mtego ambao anaweza kuingia mtu yeyote. Kuna vitu viwili hapa vinakosekana - uadilifu na busara na nafikiri vingekuwepo ulitakiwa umkatie simu katikati ya maelezo yake kabla ya maelezo yako:

    Mimi: Okay sasa unataka nifanye je?

    ReplyDelete
  12. Pole sana. ndugu, nimesikitika sana kwa yaliyokupata.
    Ila tatizo kubwa hapa ni tamaa ya hela za haraka haraka.
    Kwa upande wangu naona huu mtego unaweza kumkumba yeyote kwa mazingira haya ya kwetu, ambayo kila mtu anataka kutoka hata kwa kumwua albino.
    mimi sikulaumu moja kwa moja kuwa kuna kauzembe ulifanya, ila yakupasa kuwa makini sana katika mazingira haya ya sasa, na watz tuache kale kauzembe ketu kakuamini miradi ya wazungu, ukisikia mzungu tu, unaona dili. haya ndio marichmond. wapo hapa mjini na laptop tu. wanashinda internet cafe. wamegundua tz ni mahali pakuchuma.
    Tunahitaji elimu kuelimisha watanzania. Kila siku watu wanatapeliwa tena wengi ila hawasemi. nashukuru kwa wewe uliyejitokeza kutufumbua macho, tuwe makini.Ufisadi unouona sasa hapa nchini ni tamaa, hawa jamaa nao wanatapeliwa kwa njia isiyo rasmi.

    POLE SANA NDUGU.

    ReplyDelete
  13. Pole mdau Alex kwa mkasa ulikufika, hii ngoma inahitaji kutengenezewa movie kwa kweli. Mazingira ya huo utapeli yalikuwa yamepangwa vizuri ila pia kama alivyotangulia kusema anonymous wa Wed Nov 18, 10:41:00 AM inabidi tupunguze tamaa. Yani kutapeliwa kupo ila hapa katika hii simulizi inaonesha hukuwa na wasi wasi kabisa kwamba hii ingeweza kuwa scam. Siku zote pesa nyingi kama hizo unapaswa kuwa na mashaka japo kidogo. Tuache hizi tabia za kuishi kuchangamkia dili na turidhike na tunachokipata, katika hii simulizi inaonesha wewe mdau huna maisha magumu, ila bado roho yako haijakinai unafukuzia utajiri.

    Hao matapeli walikuwa na advantage kwako, ni wazi wanakufahamu vizuri kitabia, yani mtu wa mitikasi kama wasemavyo vijana hivyo ilikuwa vigumu kuwakwepa. Ushauri wangu nabidi tuwe makini na hizi biashara za kufanyia mtaani ndio madhara yake, siku zote kwenye transaction kubwa unapaswa kuwa na leverage zidi ya unae deal nae ili kuepuka mambo kama haya. Kwa mfano ulipaswa kwenda airport na kuonana nao kabla kununua hiyo chemical, hapo sasa huna lakufanya nikushkuru tu. By the way hii biashara ya sim registration imefikia wapi? si ndio lengo lake ni kutusaidia na mikasa kama hii? ungejaribu kufuatilia hizo namba au hawajaregister namba za watumiaji wote?

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  14. Jamani tamaa tamaa tamaa - pole sana ndugu yangu. Lakini pamoja na hayo yote it is just a matter of common sense - NAFAKA itahifadhiwaje na MAJI (LIQUID) - POLE SANA TU. Mimi walinikosa kosa maana niliuliza nafaka na maji wapi na wapi - nikakatiwa simu sikuwasikia tena

    ReplyDelete
  15. Mimi ndiye niliyekutapeli kwa kuwa una misifa sana kule mtaani na kigari chako cha used. Na una bahati tulikupunguzia dau dogo, tungekuambia kubwa ungeweza ukaanza kusumbua. Hiyo inatutosha kwa kuanzia na ikupe fundisho kidogo.

    Na wewe Michuzi dawa yako iko jikoni kwa kuanzia tunaanza kuipa lile litishirt lako kwanza ili ukiwa unaenda kulalamika watu wasikujue kama ni wewe. Halafu tunahamia kwenye hiyo camera na kuendelea.

    ReplyDelete
  16. This is true story !!I was also approached in the same manner after the con men read my contact Mobile No. from busness shop at Sinza kwa Remmy. After hesitating about procument arrangement I queered them about WFP procurement- Why should they make cash purchase??. That was all, they disappeared. One said he lives at Vingunguti.

    ReplyDelete
  17. Anti- PhariseesNovember 18, 2009

    Si Dr. Shija unamfahamu na yupo MSD?

    Maswali:
    1.Je kweli hiyo dawa (sample) inauzwa kwa bei hiyo? Quotation za MSD na hata Pharmaceutical shops kibao zinaweza kukupa hilo bila jasho.

    2. Je siku hizi MSD wanauza tu madawa yao kwa watu binafsi ambao hawajaandikishwa kupata huduma toka kwao, kama vile mahospitali na vituo vya afya?

    3. Ulipewa stakabadhi au ndo ilikuwa kuaminiana tu na mwendo wa kununua bidhaa za magaa.

    Kama majibu ya maswali yote ni hapana kula sahani moja na Dr. Shija maana huyu kaamua kukuua kimasomaso sasa na wewe muue hivyo hivyo maana ana wakubwa zake na kwa evidence ya alichokifanya anaweza kupoteza hiyo kazi yake.

    Binafsi namfahamu mtu kwa jina la John alikuwa akifanya kazi WFP Dar sasa ameshahama anafanya na shirika moja la Kimarekani lakini nadhani si yeye maana sijawahi kusikia kuwa ni tapeli hata siku moja na ninamwamini sana ingawa kibinadamu huwezi kumtetea mtu 100% hapa duniani. Na kama kweli nia ilikuwa kukutapeli basi hasingetumia jina lake halisi.

    Nakusaidia yafuatayo kama mmoja alivyosema hapa:

    Jitahidi ufanye biashara ya haki utabarikiwa sana. Maana hata kama si kutapeliwa tayari wewe unaonekana kuwa una mazoea ya kufanya biashara ya kificho ambayo hata kodi pengine hulipi na hivyo wewe umeshalitapeli TAIFA na kukaidi maelekezo ya bosi wetu aliye mkuu ambaye ni MOLA. Sasa yaliyokukuta kama ni kweli (maana huu pia waweza kuwa ni utunzi tu au habari ambayo umetupa nusu nusu bila kuweka kwa uwazi ukweli wote) ni gharama tu ya malipo ya kazi ya mikono yako. Yaani hakuna kazi yeyote halali ya faida kiasi hicho kwa muda huo kwa kiasi cha kazi uliyokuwa umepewa. Vinginevyo hata watengeneza hayo madawa wenyewe wa Sweden wangeacha kazi yao na kuingia kufanya hiyo kazi dakika hiyo!!!!!

    Pili ingawa wengi wanasema kuwa yeyote angeingia mkenge si kweli inategemeana na jinsi ulivyozoea kufanya kazi au biashara yako na pia kiwango cha uelewa wako.

    Kweli Mzungu na WFP atafute supplier asiyejulikana wakati anajua kuwa anaweza kuwasiliana moja kwa moja na MSD. Mashirika yanayoanza na majina ya 'W' (World) yana taratibu zake nzuri zilizokuwa established kitambo on Finance and Materials Management na tendering ni za wazi kwa kufuata taratibu zote zilizowekwa hivyo binafsi nisingekubaliana na tender hiyo ya WFP bila kuifanyia uchunguzi wangu wa ABC kibinafsi. Tatizo ni hili kwamba kama ulizoea kazi za hivyo basi huwezi kujiuliza na hivyo huwezi kulaumu yeyote.

    Tunashukuru kwa hii story lakini pia nashukuru kama utageuka leo na kuokoka kijamii.
    Ubarikiwe sana.

    ReplyDelete
  18. ACHA TAMAA. WEWE MWENYEWE TAPELI KWA SABABU ULITAKA HELA ZA RUSHWA. HIKI NDICHO KINACHOFANYIKA HATA SERIKALINI. WEWE UNAJUA PESA ZA KUENDESHA WFP ZINATOKA WAPI? HIZI NI HELA ZA WALIPA KODI WA NCHI FULANI. SASA KWANINI USHIRIKI KUZITUMIA VIBAYA KWA KUUZA KITU BEI YA JUU KULIKO YA SOKO.

    KUMBUKA UKITENDA DHAMBI ADHABU YAKO IPO HAPA HAPA DUNIANI.
    WEWE ULILIPWA HAPO HAPO.

    NA IWE FUNDISHO KWAKO NA WENGINE ILI WATENDE MEMA HAPA DUNIANI. FANYA BIASHARA ZAKO ZA HALALI NA UISHI KWA KIPATO HALALI

    ReplyDelete
  19. Tamaa ndo iliyokuponza bro. kwa akili ya kawaida tena kwa msomi kama wewe huwezi kufikiria kwamba WFP as an international and reputable organisation wafanye biashara kwa njia ya simu? tena masuala ya procurement bila kufuata procedures? mbaya zaidi unaambiwa utapewa hela ya mafuta kwa ajili ya kuwapeak from airport wakati WFP HQ ni dar es salaam na kama walikuwa wanakuja kwa official issue wangefanya arrangements na HQ.

    vile vile bro, hukujiuliza iweje afisa wa MSD atembee na dawa kwenye gari wakati ni mali ya shirika? je hukujiuliza iwapo unatoa pesa kununua sample halafu wateja wako wakaikataa itakuwaje huku umeshainunua kwa gharama kubwa? je ulipewa risiti uliponunua sample hiyo? BRO. NEXT TIME AKILI KUMKICHWA NA ACHA TAMAA YA UTAJIRI WA HARAKA HARAKA

    ReplyDelete
  20. Jamaa hakuwa makini kabisa...angeweza kufika MSD physically na kuonana na huyo jamaa anayeitwa shija...FYI HAKUNA KITU KAMA NEGOTIATION MSD KATIKA BEI NA SI KILA MTU ANAUZIWA DAWA NA VIFAA TIBA HAPA BALI HOSPITALI ZA SERIKAL NA ZA MASHIRIKA YA DINI......POLE LAKINI KILA KI2 2FANYE KWA UMAKINI WA HALI YA JUU UGUMU WA MAISHA USI2FANYE KUKURUPUKA NA KUSABABISHA MATATIZO

    ReplyDelete
  21. Bora huyo.

    Mi Arusha niliwahi kuibiwaga na demu mmoja wa kutoka kenya.

    Nimezuka nae chumbani, alikuwa mtanashati kweli huwezi kuamini, tunakunywa kumbe kaniwekea madawa ya kulevya.

    Nakuja kuamka kesho yake asubuhi ni saa 4.30 keshakimbia na Tsh. 1.7m, US $ 1,300 Laptop na kamera.

    Nikaona aibu nikaa kimya tu bora uhai wangu kaniachia.

    ReplyDelete
  22. kwa hiyo na wewe ni muhaya au

    sioni ajabu vitu vingi huwa vinaanzia kwa wahaya vikiingia nchini kwetu kwa mara ya kwanza...nayo 419 scam inaingia itawamaliza wahaya wote kwanza...

    greedy imekuponza...mnapata hela zenu kifisadi sana ndio maana hata hamuoni uchungu na kuwaza ...kweli $1000 nimpe houseboy tu wala simjui ...fast money inawaponza

    ReplyDelete
  23. Kila mtu anaota kuwa milionea! kumbuka ni ngumu! Utaelewanaje na mtu dili la mihela kama hiyo bila kumfahamu? Angalau hata kuonana ana kwa ana?

    Ndo yamewaliza wengi huku ulaya watu wananunua nyumba na viwanja katika net na wanalipa cash, at the end no kiwanja no nyumba wanabaki kushikana mashati lakini sinema ndo ishakwisha.


    Fanaya reserch kwanza sio kukurupuka na biashara kichaa. Bongo kila mtu anataka kutoka.

    ReplyDelete
  24. This is a wake up call fellas, hapa marekani wakati bubble la nyumba halija pasuka watu walikuwa wananunua nyumba leo hata mwaka haujaisha unaiuza unapata faida hadi dolla laki na zaidi sasa wale wale watu wanachukua ile hela waliyopata wanaenda kununua manyumba zaidi.Lile li bubble lilopokuja kupasuka wakakutwa hajaziuza hizo nyumba guess what happened,ni madeni madeni na wengine wamepagawa hadi wanakimbia nnchi na kurudi africa na laiti kama ile hela wangeitunza wangekuwa matajiri na watu tuliokuwa waoga sasa hivi ndo tuna peta kwa kwenda mbele with good credit(wao bila sisi 3) so the bottom line tuwe wazito wa kukimbilia mambo makubwa maishani let them come by themselves,hakuna haraka ktk maamuzi mfano huyu bwana alex ange omba more time to consider that offer il aongee na watu wake wa karibu pengine angeshituliwa mapema,yaani wewe jiulize who make all that money about 50 grand us dollar in couple of hours c'mon man. Huhitaji kuwa proffesa kujuwa huu ni wizi lakini pole sana ndugu alex next time kumbuka msemo usemao wajinga ndio waliwao!!

    ReplyDelete
  25. Jamani jamani hii story ni yakweli kabisa, hata sisi yalitukuta lakini tuliwashtukia waliposema tumplekee boss wao mzungu anakaa White Sands Hotel wakiwa na kaka mmoja wa kikenya. Sisi tuliambiwa hiyo chemical inapatikana Shellys Pharmaceutical LTD. This is very true story sisi wenyewe tulichanganyikiwa tuliona ni zali la mentali so guys be aware.

    ReplyDelete
  26. pole sana kaka. Mimi nilishasikia huu mchezo, sasa iliponitokea niliwaweka kati wa walisema wanataka mzigo tuonane Muhimbili. Nilipowaweka sawa nilienda polisi kuriport na nikapewa watu. Tulifanikiwa kumkamata mmoja na niliwaomba polisi nimetake risk kwa faida ya wengine ambao wametapeliwa na walichukulie serious kupangua hiyo chain. Nitaifiatilia tena hiyo kesi polisi. Ila naomba wakereketwa wengine tuungane tuharibu huo mtandao. kaka Michuzi naomba ufuatilie hiyo kesi nitakupa jina la askari anayeshughulikia

    ReplyDelete
  27. Pole sana ndugu yangu na hongera kwa kuwa jasiri wa kusimulia.Matapeli kama hawa wapo wengi na kijiwe chao ni mwananyamala hospt,magomeni hospt mimi walishakuja kunishawishi kwa kuna tender ya kufundisha wazungu lakini mimi niliwashtukia pale waliponiambia ni tution fees kubwa sana. ninachowashauri ndugu za tuwapeleke hawa watu police.

    ReplyDelete
  28. hahha hahahaha ACHA TAMAA YA UTAJIRI WA HARAKA HARAKA.MIMI WALINITOKEA KWA STAIL KAMA HIYO HIYO ILA NILIMKAMATA MIMI WALINIPELEKA SINZA MAPAMBANO CINEMA YAKE HAIKUA NDOGO NILIWATIA MIKONONI WAWILI ILA MMOJA AKAKIMBIA ALIE BAKI TUKAPIGA SANA TUKAPELEKA POLISI OSTARBAY. UNACHOTAKIWA KUFANYA NEXT TIME USIMSIKILIZE MTU USIE MJUA KWA MUDA MREFU

    ReplyDelete
  29. Mshikaji wangu mmoja alinielezea kuhusu hiyo deal nikajaribu kumweleza anatapeliwa akaniona namfanyia roho ya kwanini. Sasa anajuta yeye kapigwa millioni tano

    ReplyDelete
  30. Pole sana! Ushauri wa bure ni kuwa usiwe na tamaa ya kupata vingi kwa haraka na tena bila ya kuvitokea jasho. Hii habari yako inaonyesha jinsi wengi wetu tunavyopenda kutumia njia za mkato kutafuta pesa. Kisicho halali hakiliki!

    ReplyDelete
  31. acheni tamaa jamani mtaibiwa sana na hao matapeli mkiwakamata dawayake ni kuwambie wakalie chupa tu. wenyewe wataacha

    ReplyDelete
  32. Anyway usajili wa simu utapunguza matukio kama haya.

    ReplyDelete
  33. pole sana bro...watu wengi wanaingizwa mkenge na matapeli ambao siku hizi wameongezeka kwa kasi ya ajabu na wanatumia akili nyingi sana, si kitu cha kustaajabu jinsi walivyoweza kukudanganya maana wanajua wanachokifanya. utapeli mwingine unafanywa online ambapo siku hizi watu wanatuma email as if zinatoka yahoo wakidai kuwa wanataka kupunguza emails ambazo hazitumiki kwa muda mrefu, hivyo basi unachotakiwa ni kutuma yahoo ID yako na password yako, ukilogwa ukaingia mkenge, unakuwa umewapa access kwenye email yako, wanaingia na kubadilisha password yako na kuanza kuwatumia watu walioko kwenye contact list yako kuwa umepata matatizo na unahitaji msaada wa fedha haraka sana.
    si rahisi kabisa kugundua kama watu hao ni matapeli, binafsi nimepokea such email na tena ina warning kwamba within 24 hours usiporeply watafunga account yako.
    Be careful guyz...gud day

    ReplyDelete
  34. Mmh! mimi nashangaa kweli! hivi unawezaje kufanya na mtu deal la mamilioni bila hata kumuona kwa macho, kwa simu tu? au hata bila kufanya uchunguzi kidogo kuhusiana na biashara yenyewe?. masuala yanayohusisha mamilioni ya fedha kama hayo hata siku moja siwezi kufanya kwa kupewa maagizo tu ya simu.
    Pole sana lakini kama ungefikiria kidogo na kutumia akili badala ya tamaa usingetepeliwa.
    Ahsante sana umewafungua watu macho.

    ReplyDelete
  35. Am very impressed with this kind of new quick money making business. For how long Tanzanians will worship and like a quick money? Well done for the inventors of this business. Always you have to know how to gain the right money on the right way. Once again well done. Don't let the fools, fool you. Get what is right for you.

    ReplyDelete
  36. Kuna mdau hapo juu anapendekeza kula sahani Moja na Dr. Shija. Kama ambavyo wameweza kupata jina na nmba zako za simu bila kukuomba huoni kama wanaweza pia kupata jina la mfanyakazi yeyote wa MSD bila idhini yake? Unaweza ukaona huyo Dr. Shija hata hajui kama jina lake limeshtumiaka kupoteza na kumake 1000,000 kwa siku moja tu!

    ReplyDelete
  37. Pole sana kaka! Hapa hujidhalilisha ila umesaidia wengi! Hata kama ni mimi ningeingia mkenge the deal is too close to the truth! Huwezi fikiria mara mbili when something like this happens!
    Thanks for your story

    ReplyDelete
  38. Kumbuka wale jamaa wa wenye basi walotapeli watu miaka ya themanini! Nahisi ni wale wale na style yao imebadilika kidogo. Please deal na mtu unayemuona kwa dunia ya leo TZ. Tukwepe utajiri wa haraka haraka.

    ReplyDelete
  39. WELL DONE!!!!!!

    SASA UMEKUJA HUKU ILI TUKUSAIDIAJE, TOKA LINI ULIFIKIRI MAISHA YANA NJIA YA MKATO?

    HAMTAKI KUFANYA KAZI ZA HALALI, MNATEGESHEATEGESHEA TU, SASA HUKO MNAKOTEGESHA KUNA MAPROFESSA.

    ONA SASA WAMEKAMATA NYETI, HIYO PESA SI INGETOSHA KUWASAIDIA WAZAZI WAKO WALAU WAKALA VIZURI KWA MWAKA MZIMA?

    HIVI HILI DEAL LINGEITIKA UNGERUDI KWA MICHUZI WEWE? SI UNGEKIMBILIA CMC kuvuta VOGUE

    KWELI WAJINGA NDO WALIWAO.

    TABU NI KUWA KILA MTU ANATAKA KUTOKA KAMA IDDI JANGUO, NA MATOKEO YAKE NDO MNAINGIA MIKENGE.

    ReplyDelete
  40. NAONA WENGI HAWAJAELEWA, WANAMLAUMU JAMAA BURE WAKATI MTU YEYOTE ANAWEZA NASA TU. YEYE NI BIZMAN NA MJINI UJANJA HATA SERIKALINI WANAFANYA HIVYO.
    NA KUHUSU DR. SHIJA NI KUWA EITHER NI MTU WA KUFIKIRIKA AU YUPO LAKINI JAMAA ALIDILI NA MTU MWINGINE ALIYEJIFANYA NI DR SHIJA. NA MWISHO MLITAKIWA KUMSHUKURU KWA KUWAELEZEA YALIYOMKUTA ILI WENGINE WASINASE KWENYE MTEGO HUU, LAKINI TANZANIANS BEING TANZANIANS MNAUA TU.

    ReplyDelete
  41. bongo kila mtu fisadi, shortcut zitatuponza jamani.
    naona Wed Nov 18, 01:06:00 PM hapo juu hajelewa maana ya chezo la kihaya ni nini

    sasa jamani tushirikiane kutatua tatizo hili maana limepevuka haswa,japo tumbane mmmoja tu na tumuhukumu wenyewe, huu ni upuuzi..

    ReplyDelete
  42. Guys I know this might sound crazy, but I think this is good. Even in computer world Hackers ndio wanazileta kazi za computer securities.May be these types of scams will slow down the selfishness of Officials, especially public officials.The number one rule in procument business is Integrity, atleast in the first world countries anyway.
    and that is my four cents!!!!!

    ReplyDelete
  43. Wewe ni mwizi. Umezoea kufisadi kwa 10%. Na unasitahili kabisa kutapeliwa kama vile ambavyo ulitaka kuifisadi WFP. Ubaya ulipwa kwa ubaya.

    ReplyDelete
  44. Wabongo kwa madili, nimechoka. Nawaambia watu kufanya biashara halali, kuandikisha kampuni, lipa kodi, ukichukua mkopo rudisha ili ulale usingizi mzuri kila siku, watu wananiona mimi siyo mjanja. Kama kuna utapeli kama huu Bongo kwa nini filamu zetu bado siyo nzuri? Anyway, mdau pole. Naona hii ni Bongo version of Ashton Kutcher's Punk'ed!

    ReplyDelete
  45. Huu ni ukurasa mfupi wa Nigerian movie Masters starring Nkem Owoh and Kanayo O Kanayo. Hao wameiga hawa matapeli wa Kinaijeria ambao wamecheza katika movie hiyo na hata kucheza music video "I GO CHOP YOUR DOLLAR".

    Mjihadhari na Scammers, wako kila pembe ya jamii siyo Wahaya tu.

    ReplyDelete
  46. Unajua kwa nchi kama yetu miujiza kama hiyo ipo kwa hiyo wakikupigia jaribu inaweza ikawa kweli maana hata wale walio pata za EPA ilikua hivyo hivyo na wengine sasa ni mabilionea. Bongo matombola mengi ndio utajili wetu wengi!!!!!!

    ReplyDelete
  47. Ushauri mwingine ni kwamba .. hatat wazungu kuna matapeli .. manake Bongo sometimes mtu akiona deal inamuhusisha mzungu tu anaamini kwa kudhani wazungu hawatapeli.. nao wezi,waongo, majambazi nk .. kuna kina Madoff nk .. sasa sio tu mtu anaongea kiingereza basi .. utasikia ..ahaha hata mzungu yumo .. ahahah pole jammaa yangu

    ReplyDelete
  48. Hii ni kweli. Naamini ni mchezo kutoka Magomeni. Walinipigia na ni exactly kama Alex alivyoandika. Niligoogle na sikupata kitu walichotaka nikajua ni kamba. Jamaa waliingia na gia ya kunijua katika Chama pale Magomeni.

    ReplyDelete
  49. Pole sana ndugu yangu. Sorry, hivi ulimpa huyo kijana cash au ni cheque? Kama ni cheque kwa nini usingeenda Bank ukawaambia wa-stop-pishe hiyo payment?

    ReplyDelete
  50. TAMAA NA UJINGA USIO NA MPAKA. KILA SIKU MNAPIGA KELELE UFISADI SASA KAMA WEWE ULIYETAPILIWA SIO FISADI NI NINI? MTU ANAKWAMBIA WAZI WAZI BIASHARA YA 10% NA WAKATI UNAJUA WAZI KUWA HUO NI UFISADI NA UNAKUBALI KUFANYA UPUUZI HUO. NADHANI WANGEKULIZA KAMA 10M HIVI NDIO MNGEKOMA NA TABIA ZENU ZA DEAL ZA 10%. KAZI KUWAPIGIA KELELE WANASIASA WAKATI NYIE UFISADI UMEWAJAA WACHA WAWALIZE NI HAKI YENU.

    KWANZA KAMA NI WFP INAKUWAJE MTU ANAKUPA TENDA KIENYEJI TU UNAKUBALI? TENDA SI INATANGAZWA? KISHA UNABID, BAADA YA KUNUNUA TENDER DOCUMENT, HALAFU UNASUBIRI MATOKEO NA UKISHAPATA WANAKUPA MKATABA AMBAO WAO WFP AU YEYOTE YULE MWENYE TENDA ANASAINI NA WEWE UNASAINI TENA BAADA YA BEI YAKO KUKUBALIWA NA KUKAMILSHA MASHARTI MENGINE KAMA TECHNICAL SPECIFICATION.

    SASA HII TENDA YENU YA MITAANI NI YA AINA GANI? HAMNA HATA AIBU KUTUELEZEA JINSI MLIVYO NA TAMAA NA UFISADI ULIOKITHIRI. FUATENI SHERIA MUONE KAMA MTAUMIA

    ReplyDelete
  51. huo mchongo upo Ki-West Africa mtupu.
    ukiondoa TAMAA,pia upeo wa kuona mbali hakuna.NGOJA waNigeria wakupigie cm wakueleze wanataka uhifadhi mihela yao ktk akaunti yako.i bet u won't hesitate 2 think twice.

    wale wenye TAMAA pekee ndio wanaoweza kuingika ktk MOTO huo na sio kila m2.

    ReplyDelete
  52. Pole sana kaka Alex, ila napenda kuwapongeza hao jamaa walikufanyia hivi as inaonyesha wewe ni mjamaa ila shetwani la kifisadi lilishaanza kukuteka.
    wewe ni mjamaa kwa maana umeamua kuanika masihabu yako, ukijua kuna watu watakucheka, ili wengine wasiingie kwenye mkenge huo.
    Sasa basi coz usharudi kundini, endelea kuwa kondoo mzuri wa ujamaa, na baki humuhumu, achana na roho ya kifisadi!

    ReplyDelete
  53. Always mashabiki wanajua kucheza kuliko walioko uwanjani.
    Tunalugha nzuri ya kukosoa na kujifanya tunajua
    truth is mtego ni mtego tu na ikikutokea hata uwe na PhD unanasa tu.
    Kaka waosha vinywa na wajuaji watakucheka ila mimi nakupa pole na thanks ku-share nasi kwa lengo la kuokoa wengine
    Kila mtu ana dream ya utajiri so ni vita ama kupata ama kupoteza
    Thanks man

    ReplyDelete
  54. utatoaje pesa kijinga kijinga babu????tamaaa hiyo.kalaga bao.
    mdau money uk.

    ReplyDelete
  55. hapa nakiri na ujanja wangu wote naona kama ningeingizwa mjini tuu,bora umetuambia...next time kabla ya kufanya deal ya pesa na watu demand mfanyie ofisini kwao na lazima legal document ziwe involved na ungeweza kupiga simu WFP kuulizia moja kwa moja

    ReplyDelete
  56. BIJA MPOLA HIYO: LAKINI WAFANYAKAZI KATIKAM KAMPUNI HIYO SI WAHAYA PEKE YAO WAPO MAKABILA MBALI MBALI: TAMAA NA KUKOSA UDADISI NDO MATOKEO YAKE HAYO; PIA MZUNGU BINJA MPOLA NI MZEE WA KIPARE! NA SECRETARY NI MCHANGA, MLIZI MMAKONDE;

    ReplyDelete
  57. NAFIKIRI UNGEKUWA MAKINI KIDOGO TU USINGETAPELIWA KITOTO NAMNA HIO,HUYO TAPELI ALIKUELEZA TOKA MWANZO KUWA HIYO NI TENDA KWA HIYO ISINGEWEZEKANE DEAL YA TENDER IFANYIKE KWENYE SIMU FOR FEW HRS.NAFIKIRI HUKUWA MAKINI,PERIOD,KWA MAANA TENDER INA-PROCESS YAKE HATA KAMA INATOLEWA KWA RUSHWA BUT STILL IT HAS TO UNDER GO SOME PROCEDURES KAMA 1.KUOMBA KUSSUPLY 2.UNAJIBIWA KAMA UME-WIN HIYO TENDA.SASA WW KWA TAMAA YA PESA HUKUFIKIRIA KABISA AND WHAT WAS IN YOUR MIND WAS TO GET THE MONEY THAT WAS PROMISED.TANZANIA MMZOEA SANA DEAL CHAFU KILA MTU ANATAKA KUWA MILIONEA KWA KUIBA,RUSHWA AMA KUDHULUMU.MIMI SIKUPI POLE KABISA NA HILO LIWE FUNDISHO KWA WOTE WANAOPENDA VITENDO VYA RUSHWA.
    FANYENI KAZI VIJANA HIZO PESA ZA RUSHWA NI DHAMBI TU WILL NOT GET YOU ANYWHERE

    NA WADAU WANAOULIZA KUHUSU DR.SHIJA NI KWAMBA HAKUNA CHA DR SHIJA WALA NINI HUYO NI IMPERSONATION TU ILI KUWAINGIZA WAJINGA MKENGE.

    N.B.NI LINI SAMPLE IKAUZWA????

    ReplyDelete
  58. Obviously I simpasize with you for the loss...However,
    Mzee ulivyoandika inaonekana akili yako ni timamu na U know what you doing, pamoja na hayo nafikiri tamaa kidogo ilikuzidi nguvu.
    Yaani experience yote ya kazi uliyosema umesahau shirika kubwa kama WFP hawatafanya deal bogus kama za kwako.
    On top of that, how in the hell would someone who you can barely remember give you such a damn good deal and not his family member or close friend...c'mon man.....
    I am guessing this time the common sense just didn't make sense ahhh..
    Nxt time utatapeliwa mke...

    ReplyDelete
  59. Pole sana kaka,

    ReplyDelete
  60. Kaka mithupu yaani mimi nikisikiaga matukio kama haya kwanza nakimbilia kusoma mawazo mbalimbali ya wadau.Nakwambia blog ya jamii inaburudisha sana kwa kusikia mawazo ya wadau.Kama katika tukio hili anoni aliyesema kwamba ndiye yeye kafanya hivyo, kwakweli ni msanii mzuri.Nawengine wametoa mafundisho mazuri kabisa.Nawapongeza sana wote walioshiriki.Kuna mmoja amesema kwamba tusiwe tunawaabudu wazungu kwa kudhani ndio wastaarabu,wenye fedha,na masifa kedekede hii ni kwasababu tulioko hapa ughaibuni wapo wazungu ndiyo wanaotuoshea magari,wanaporishi viatu vyetu n.k
    Pia kale katabia ka kutoshare info..ni ugonjwa mkubwa kwa watanzania.Anataka kwanza ajaribu pekeyake kisha akijakuingia mkenge ankaa kimya kwa haibu.Haya tena hii imenionyesha kwamba watu wengi wana mamilioni huko nyumbani.Je hizi hela zinatoka wapi?mbona sipati jibu? nikweli kwamba watu wanafanya kazi tatu au mbili?
    Na jamaa kasema eti ni wahaya sijui kama akina nshomile hawa wanaweza kukamatika maana wao ni wabunifu, na ikisha expire wanaaza nyingine.Nikipata namba yao nitawaomba wawaibie wote wala rushwa.Every profit is theft discuss Rwega

    ReplyDelete
  61. Nilikuwa natafuta gari hapa US, jamaa wakataka kunichapa na hii nikawastukia, nikawa dk 3 mbele yao. Kuweni makini sana hasa mnaogiza magari japan, waNigeria wameshakujua Japan

    Hi,
    Thank you for your email. The Altima is in immaculate condition, meticulously maintained and hasn't been involved in any accident...I do have the title , clear, under my name.
    The car has 20,000 miles VIN# 1N4AL21E47N439660.
    I'm an US Air Force Col. currently stationed in UK and the car is here with me. It was bought in the US and shipped to Europe, but it was never registered here, is still registered in the US.
    It is still available for sale if interested, price as stated in the ad $4,300. There will be no extra or hidden taxes for you to pay since the car is still registered in US. Shipping will be $900, I can ship it anywhere in US.
    In case you decide not to keep the car I'm responsible for shipping back costs. As I'm unable to travel in the near future and I don't have anyone back home to help me with the sale I decided to sell this car through eBay or craigslist. Our transaction will be entirely through eBay Motors and we both will be covered.
    Let me know if you are still interested.
    Regards!!!

    2007 Nissan Altima 2.5 SL
    Vehicle title: Clear
    Body type: Sedan
    Engine: 2.5L L4 SFI DOHC 16V
    Exterior color: Red
    Transmission: Automatic
    Fuel type: Gasoline

    You can find more pics at:
    http://picasaweb.google.com/teresaoverton77/Altima?authkey=Gv1sRgCPrp6dy_3Ov1bw&feat=directlink


    Col. Teresa Overton

    ReplyDelete
  62. Iweje mnunuzi akuelekeze na mtu wa kwenda kwake kununua na kukupa namba yake ya simu usishtukie? You were supposed to go to MSD and ask for DR. Shija which am sure asingekuwepo mtu kama huyo na ungeshtukia!!

    ReplyDelete
  63. hahaha pole sana sasa juzi me na mtu wangu wa karibu tu nusu tuingie mkenge hivo hivo ulivotuelezea hadi mzungu na airport walipochemka ni kutuambia tutoe hela me n ma friend tuna akili zaki MERU money comes n stays there haitoki kikenge ivo...
    so tukamwambia either we split the cost ya kuchukua sample au no deal mwishoni wakatutukana kwamba hatuwezi deals n stuff tukacheka

    ReplyDelete
  64. hii kitu imemtokea kaka angu mwezi uliopita same thing yani huyo huyo mtu na yeye yuko kigoma yani kila kitu hvyo hivyo sema yeye alimbana akamwamabia kuna watu wanauziwaga business card za watu kwaio anakuwa anajua wats ur position at work na your full name.

    ReplyDelete
  65. acheni tu wadau siku ya kutapeliwa sijui kwa nini mtu unakuwa zuzu ni kama nyani tu siku ya kufa miti yote huteleza msimlaumu mwenzenu kama ni madili asilimia 99 ya watu wanayacheza sana tuu ukizingatia christmas is around the corner jamaa akaona aichangamkie dili ili mambo yaende mswano lol pole ndugu yangu watu na akili zao wengi tuu weshalizwa hapa sio kurusha madongo tu ni kujifunza na kuwa makini kwani mie zamaaani niliingizwa mkenge pale nje ya ips kuna majamaa nilibadili dola mia mbili na pesa nikahesabu mwenyewe noti za elfu tano tano lol usiku wa balaa ni pale nilipotaka kununua kitu nilipofungua pochi nilikumbana na noti za mia mbili mia mbili nyiiiiiingi nusu nizimie haikuingia akilini zile noti za elfu tano tano ziliyeyuka vipi nikabaki na vile vinoti vichafu vya mia mbili mia mbili ambavyo baadaye serikali ilikujaga kubadilisha noti acheni tu bongo chuo kikuu

    ReplyDelete
  66. Tamaa ilimponza fisi.
    Kuna vitu vingine hata havileti maana. WFP wana maghala kiasi gani? Unataka kuniambia 1000ml@100 ni tosha kudhibiti uharibifu wa chakula chao? "Preservatives" huwa zinawekwa kwenye vyakula vilivyo majimaji au vyenye unyevunyevu mwingi k.m. Nyama.
    WFP wanahifadhi nafaka kama watamwagia hayo madawa kwa kifupi hicho chakula kitakuwa hakifai kwa matumizi ya binadamu kama sio viumbe hai. Kama ungetafakari kabla ya kurukia hii habari wala usingeibiwa kumbuka "if its too good to be true then it is, walk away". Wewe ulitaka kuwaibia hao wanaotoa msaada na badala yake ukaibiwa wewe hiyo ni safi kabisa na ukome. Ujue kuwa wizi haufai. Fanya biashara halali na utafanikiwa lasivyo utaibiwa sana tuu kwa sababu hapa mjini tunapenda watu kama nyinyi wa kijiji.

    ReplyDelete
  67. duhh! yaani mkasa wako ni kama movie moja ya wapopo ameact nkem yule aliyeact usofia in london, sikumbuki jina la hiyo movie ila inaelezea jinsi 419 inavyoendeshwa na kuna sehemu walitapeli kuhusiana kabisa na huo mkasa wako. pole sana ndugu kama ukipata kuona hiyo movie utajifunza mengi kuhusiana na jisi wanavyoweza kutapeli, i'm sure wapopo wana hand on it maana wamejazana bongo,

    ReplyDelete
  68. KWANZA POLE SANA NDUGU YANGU KWA KUTAPELIWA NA KARIBU BONGO DASLAAM NA HONGERA KWA KUWEKA WAZI HILI WENGI WAJUE KAMTINDO HAKO KA UTAPELI KALIKO INGIA BONGO.


    PAMOJA NA KUKUPA POLE LAKINI KUNA VITU KADHAA VYA WAZI KABISA AMBAVYO KAMA UKIWEKA MBALI TAMAA YA KUTENGENEZA MSHIKO WA CHAPCHAP KWA JASHO DOGO [ka DECI] UNGEWEZA KUSHTUKIA, HII HAINA TOFAUTI NA MA JUNK EMAILS AMBAYO TUMEKUWA TUKIYAPATA KILA UCHAO TOKA KWA WASIOKATA TAMAA YA KUTUIBIA,


    VITU KAMA MTU USIYEMFAAMU VYEMA KUKUTAFUTA NA KUKUPA DILI YA HELA USAWA HUU SI KITU CHA KAWAIDA LAZIMA KA KENGELE KALIE KA WE NI WA MACHALE.

    PILI, HAKUNA SHIRIKA LOLOTE LA KIMATAIFA LINALOFANYA BIASHARA KIHOLELA NAMNA HIYO TENA KWA CASH!!! HAKUNA KITU KA HICHO NDUGU YANGU.

    TATU, WOTE HAO ULIKUWA WAWASILIANA NA KWA SIMU TU, JE HAIKUKUINGIA AKILINI AU KUSHTUKA JAPO KIDUCHU KUWA DILI LA MILIONI HAMSINI ZA KIBONGO LAWEZA FANYWA HIVYO KWELI??

    POLE SANA.

    bongopix

    ReplyDelete
  69. Duuh!hapa nimecheka sana sina mbavu.

    hii lakini inatokea bongo tu. Ingekuwa kwa wabeba boksi basi mazungumzo yangekuwa kama yafuatavyo:

    Tapeli: Unajua sijui ten percent na kadhalika.

    Mbeba boksi: Mimi ni muajiriwa wa kubeba boksi,sina ujuzi wa biashara wala si fani yangu,je una maboksi nije kukubebea?gharama zangu ni shilingi kumi kwa saa!

    Tapeli: Unajua ten percent,quotation nakadhalika.

    Mbeba boksi: Sasa ni kipi huelewi?mimi ni mbeba boksi na wala si mfanyabiashara,una maboksi mangapi nikubebee?quotation yangu ni shilingi kumi kwa saa.

    Tapeli:basi isiwe tabu mtu mwenye huna lolote mbeba boksi tu!

    Mbeba boksi: Ni nini hujaelewa?si ndo nshakwambia mimi mbeba boksi?

    Tapeli: Kwaheri,fala tu wewe.

    ReplyDelete
  70. Pole rafiki yangu.

    Mimi walinijaribu na bidhaa ilikuwa dhahabu lakini kwa kuwa mimi ni mtoto wa mjini nilimchukua mmoja wao chooni pale Monevpick wakati huo ilikuwa inaitwa Sheraton na kumtolea bastola na kumwambia anipe kila kilichokuwa mfukoni kwake ili iwe fidia wa kupoteza muda wangu.

    Niliondoka na kama sh50,000 zake nikaenda kuzitoa sadaka.

    ReplyDelete
  71. jamani japo na taama yake lakini amewafaamisha kwahiyo ametufaamisha,
    mimi binafsi nakupa hongera sana kwa kutuhabarisha habari hiyo ya utapeli, mimi binafsi nakusifu hasa, mwanaume kutafuta hela, na hiyo ni kama biashara kuna kupata faida na kupata hasara,

    ReplyDelete
  72. Da hiyo story ya wed. imenifurahisha sana, imenikumbusha mbali sana. Michuzi lakini unaharibu kazi za watu maana hizo ni dili zetu lakini sie tuwekua tukizifanya Botswana, Namibia na South Afrika. Tena jamaa kakosea alitakiwa ahusishe polisi hapo yaani anapotoka Magomeni hospital tu anakutana na pila na wanamrukia kinomanoma nao wanakwalua mkwanja. Sie tushawaingiza kingi wacongomani kwenye dili za diamond alafu tunarukiwa wote na wazee na tunakwenda ndani kisha mkongomani anaachiwa kwa kukosa ushahidi na kwa jinsi alivyotuamini anahonga hela ili tutolewe tunatoka na yeye anarudi mikono mitupu sie hao kiulaini tunaenda kuskuma mzigo na askali wetu. Tukija bongo ni bata kwa kwenda mbele! nb dont try this there is thin line btn being alive and dead!

    ReplyDelete
  73. IGNORANCY, STRAIGHT IGNORANCE.....NOTHING COMES IN SILVER SPOON OR PLATE OR WHATEVER..MAYBE THIS IS A LESSON LEARNED FOR YOU..WATANZANIA WACHENI KUPENDA EASY MONEY, WORK YOUR ASS OFF FOR IT..THE WHOLE SITUATION IS WRAPPED UP IN ERRORS.HOW COULD YOU NOT BE SMART ENOYGH TO KNOW THAT IT WAS TOO GOOD TO BE TRUE. i AM GLAD UMETAPELIWA BECAUSE YOU LIED TOO IN THIS GAMBLE. LESSON 2, BE HONEST TO YOURSELF AND TO OTHER

    ReplyDelete
  74. Jamani nashukuruni sana wote kwa maoni mliyoyatoa hapo juu, hawa matapeli wanaojifanya wanatafuta hiyo dawa wapo,na mimi leo hii wamekuwa wakinipigia simu tangu saa tano asubuhi,na nimeendelea kuwasiliana nao hadi naandika message hii. Mimi wameniambia wako kempinski hotel,wengine wawili wako kigoma na dokta nimeambiwa anaitwa dokta Haji. Sasa kwakuwa mimi nimeshawahi kusomea cyber crime law haikuchukua muda kuwashtukia na kuendelea kucheza nao kama vile ndo naingia mkenge. Hadi sasa bado nawasubiri waendelee nione tunaishia wapi

    ReplyDelete
  75. Siyo kweli ndugu yangu mimi nmchga na nilikutana na kitu kama hicho miaka mi 5 iliyopita allmost nitapeliwe hivo hivo but nlistukia ishu the way mambo yalivyo kuwa yana rahisishwa coz walitaka 1milion na ckuwa nayo bac yule jamaa alinipunguzia hadi kufika laki 5 pia nikawa cna akataka hadi kunikopesha coz nlikuwa na laki3. Hawa jamaa wanakutapeli kutokana na mzingira yaliyo kuzunguka kwa mfano mimi aliniambia alimleta mdogo ake shuleni umbwe secondary sasa kutokana na ukarim nlio uonesha kwao ndio maana ameamua kunipa huo mchongo kama kulipa fadhila! Wajanja sanahawa jamaa na wamejamilika kila idara sema mimi zengwe lilianza pale nikipotaka kwenda kwenye ofisi zao kuifata hiyo dawa wakagoma kwa kigezo wameenda lunch so watamtuma kijana nikutane nae mawenzi hospital, nashujuru mungu kwa kunipa akili ya kujiongeza so nilienda kwenye bohari la dawa za mimea kuiulizia wakaniambia hakuna kitu kama hicho thanx god 4that coz hela yenyewe nlimkopa mtu nusu ila kuna ndugu yangu alininyima laki2 kukamilisha hiyo 5 nilipanga kumuonesha jeuri yapesa nikirudi pamoja na kumuahidi aliyenikopesha kuwa nikirudi breki ya kwanza ni kwenda kupata masanga na kitimoto hahaaaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...