Polisi jijini Dar wamemtia mbaroni Katibu Muhtasi wa Ubalozi wa Canada, Jean Touchatte(48) kwa tuhuma za kuwatemea mate askari wa Usalama barabarani na Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)

Touchatte anatuhumiwa kumshambulia askari wa usalama barabarani aliyekuwa akiongoza magari katika eneo la Banana wilaya ya Ilala.

Kaimu kamanda wa kanda hiyo, Charles Kenyela, amesema, mtumishi huyo wa ubalozi anadaiwa kufanya makosa hayo Desemba 9 saa 8.45 mchana wakati askari huyo namba E 1653, Koplo Samson akiwa kazini maeneo hayo.

Kwa mujibu wa Kenyela, wakati akiendelea kuyaruhusu magari yanayotokea Ukonga kwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Touchatte alifika eneo hilo akiwa anaendesha gari lenye namba za usajili T 17 CD 178 Toyota Land Cruiser Prado mali ya Ubalozi wa Canada.

Amesema, mtuhumiwa huyo alikuwa anatoka Ukonga kwenda uwanja wa ndege, ghafla alipunguza mwendo, akafungua kioo cha gari lake na kumtemea mate askari huyo.

Kenyela amedai kuwa,kitendo hicho kiliwashangaza wengi walioshuhudia,na kwamba sababu ya kufanya hivyo haikufahamika, hivyo polisi wa doria walipewa taarifa ili kulifuatilia gari hilo.

“Askari wetu walianza kufuatilia kwa nyuma gari hilo na walipofika barabara ya Nyerere karibu na Kamata gari hilo lilikamatwa na kupelekwa moja kwa moja hadi makao makuu ya polisi Trafic Kanda Maalum ya Dar es Salaam na kuwekwa chini ya ulinzi” amesema.

Kwa mujibu wa Kenyela, wakati mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa,waandishi wa habari akiwemo Jerry Muro(29) wa TBC walifika kituoni hapo, wakitaka kufahamu nini kilichotokea ndipo mtuhumiwa huyo akamtemea mate sehemu ya chini ya kidevu chake na kusambaa katika flana aliyokuwa amevaa.

Muro alifungua jalada la shambulio CD/IR/4818/2009, na kwa mujibu wa Kenyela, mtuhumiw alipohojiwa hakuwa tayari kujibu wala kutoa maelezo yake kwa madai kwamba mpaka balozi wake awepo.

Vielelezo vya tukio hilo vimehifadhiwa polisi Kati na kwamba maelezo mengine zaidi juuu ya tukio hilo yatatolewa na Inspekta Jenerali wa Polisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 47 mpaka sasa

  1. hiii too much kwa kweli!!1 yaani makaburu wanathubutu kufanya mambo ya kiaaajabu kiasi hicho kuwatemea mate watu mishi wa umma.traffic na mwana habari.tunaomba jama huyo adhibitiwe afuu badaee anapewa masaa 24 kuondoka nchi ili iwe fundisho kwa makaburu wengine ambao wanafikra ka za huyo mwehu

    mdauu jpn

    ReplyDelete
  2. Nilinyaka audio ya hii habari wakati Inspekta na bw. Muro walipokuwa wakizungumza na BBC Swahili, mtu anaweza kuisikiliza Afisa ubalozi amtemea mate mwandishi...(bofya hapa kusikiliza)

    ReplyDelete
  3. PETER NALITOLELADecember 11, 2009

    MIMI SIYO MJINGA, MIMI NI MTU MAKINI SANA, ILA NINA SWALI, HIVI NASIKIA KWAMBA HASHEEM THABEET NA YOHANNA MASHAKA WANAPOKUJAGA TANZANIA WANACHEZEWA NGOMA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA EAPOTI YA MJKN YA DAR? NA PIA KUPOKELEWA NA MAWAZIRI WA UCHUMI NA MICHEZO?? SASA MIMI MAARUFU KWENYE MASWALA YA UTABIRI WA HALI YA HEWA NDO NITAPOKELEWA NA NANI? NAFIKIRI HII ITAKUNA NI HESHIMA KUBWA SANA KWA HAWA WANAMUZUMBE WALIOBOBEA KATIKA FANI YA NBA NA WALLSTREET. HAWA NI MALI YA MUZUMBE UNIVESITI YA CHUO KIKUU CHA KULE MOLOGOLO AMBAO NI LAZIMA TUJIVUNIE, KUHUSU HUYU MAMA WA KUTEMA MATE, MIMI NAMPA PONGEZI KWA MAANA HAWA MATRAFIKI NI MAFISADI SANA MPAKA MTU UNATAMANI KUWAMWAGIA MKOJO SIYO TU KUWATEMEA MATE. YANAUDHI SANA, KILA SIKU HATA WAKIKUONA NA KABAJAJI KAKO WANATAKA KITU KIDOGO. DADA AU MAMA WA CANADA HONGELA SANA KWA KAZI NZULI YA KUMTEMEA YANGE YANGE MATE,PAAAA

    ReplyDelete
  4. "Polisi jijini Dar wamemtia mbaroni Katibu Muhtasi wa Ubalozi wa Canada, Jean Touchatte(48) kwa tuhuma za kuwatemea mate askari wa Usalama barabarani na Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)"

    Jamani waandishi wa habari muwe mnaandika vizuri sasa haieleweki huyu katibu muhtasi ni canada wapi. ungemalizia kuwa ubalozini wa canada nchini(Tanzania).

    Mimi naona sawa tu watemewe mate wamezidi hawa trafiki. Kila kukicha wanataka Rushwa tu.

    Halafu kama huyu ni mwanadiplomasia basi hakuna kitu kitakachotokea kwani atakuwa na kinga ya kidiplomasia (Diplomatic Immunity) zaidi kinachoweza tokea ni kurudishwa kwao mwisho wa mchezo.
    Ni mimi mwana Diplomatz

    ReplyDelete
  5. michuzi uwe unaweka wazi mana unatuacha na maswali mengi.1.mtuhumiwa yuko rumade au yuko nje kwa dhamana?.2.afande alietemewa mate alimfanyia nini mtuhumiwa mpaka akafanyiwa hivyo? mwisho naomba naomba haki itendeke.

    ReplyDelete
  6. WHEN I SAY I DON'T LIKE WHITE PIPO, THIS IS EXACTLY WHAT I MEAN. YAANI WANAONA MTU MWEUSI ETI ANANUKA NA NDO MAANA KAMTEMEA MATE. KWANZA MNGEMCHUKUA TU MZEGA MZEGA MKAMBWAGE MSITUNI NDO ANGEJUA MKATE NI KITAFUNIO CHA CHAI ASUBUHI SIYO DINNER! yeye hapo anajiona eti ananukia kumbe matapishi tu

    ReplyDelete
  7. si wangempiga vibao tu kimyakimya huyu

    ReplyDelete
  8. Maisha ya Bongo ni balaa.. lazima wazungu wageuke machizi.
    Hii si bure.. lazima kuna longolongo ilitembea then jamaa akaamua kuuvua UZALENDO.
    Kila kitu ufanyacho Bongo watu wanataka waku-enginie ili watengeneze ULAJI.
    Sasa ikishakuwa too much ndo hapo unapoanza ku-faya mimate kwa kila anayekatiza pua yake mbele yako.
    Tanzania yetu oyeee...!!!

    ReplyDelete
  9. Huyo mkoloni inaonekana hasira zake si za kutoa maneno kumtukana mtu isipokuwa utumia mate kuonyesha kwamba ana hasira. hashiri. Nimeipenda hiyo!

    ReplyDelete
  10. Hii haina tofauti na wanajeshi waliopiga traffic police pale ubungo hapo hatujui nini kiendelea na hao kina rigwaride lakini najua huyu kwa sababu ni mzungu is big deal lakini they are all assault charges na pia we need to investigate what was the probable cause things like like alcohol/drugs or self defense may be involved and not making assumptions and jumping to the conclusion.
    Mdau mzawa

    ReplyDelete
  11. hapo wala hakuna kesi

    huyo uchizi umemuanza

    nawashukuru MUNGU hakusababisha ajali barabarani

    ReplyDelete
  12. huyu jamaa apewe adhabu ya kutosha na arudishwe kwao huko canada.yaani amenitia hasira hiyo ni dharau sana,ingekuwa ni mwafrica nchini kwao nadhani anagefungwa haraka sana.

    ReplyDelete
  13. KWASABABU HUYO NI MTU MWEUPE NADHANI HAYO MTAKAA MTAYAMALIZA TUU MAANA HAWA WATU WANATUPELEKAPELEKA KISHENZI. VIPI LILE SWALA LA MZUNGU ALIYEKAMATWA AKIIBA KWENYE ATM KWA FOJALI? AU NAYE WALIKAA CHINI WAKAYAMALIZA KIMYAKIMYA? NAIPENDA SANA TANZANIA MAANA HAKUNA LISILO WEZEKANA

    ReplyDelete
  14. kusema kweli matrafiki wetu wana maudhi sana huyo mzungu si kichaa hadi amtemee mate kuna namna tuu ati alifungua kioo na kumtemea mate bila sababu haiingii kwa oblangata kuna kitu tu kwa wajeshi wanapowakong'oli ni kwasababu gani zaidi ya maudhi yaliyopitiliza?? mambo ya barabarani bongo yanachefua sana hata yule mhishimiwa alipomtwanga mtu risasi ni kwa ajili ya maudhi ya kiwango cha juu watu wengine wana hasira za papo kwa paop kama black mamba!

    ReplyDelete
  15. Anon wa Friday Dec 11 03:07 (Mwanadiplomatz) umeona wapi kinga ya kibalozi inatumiwa bila kuambatanishwa na wajibu? Hata kama ana kinga ya kibalozi haimaanishi kuwa asifuate sheria za nchi husika. Na kibaya zaidi alikuwa ndani ya gari yenye usajili wa kibalozi

    ReplyDelete
  16. YAANI NIMEKASIRIKA MPAKA SINA CHA KUANDIKA!

    ReplyDelete
  17. Nimesoma maoni ya wengi hapa, ila lets not place the incidence under the umbrella of race and color issue. We must assess the content of a verdict.
    Sometimes, traffic corpse enforce hanger. Foreinsic examination must be done well to realize the cause, and bring him/her to law and order.

    ReplyDelete
  18. Nimesoma maoni ya wengi hapa, ila lets not place the incidence under the umbrella of race and color issue. We must assess the content of a verdict.
    Sometimes, traffic corpse enforce hanger. Foreinsic examination must be done well to realize the cause, and bring him/her to law and order.

    ReplyDelete
  19. Shauri ya kuombaomba misaada ya Wazungu kila siku ndio maana wanatudharau. Ndio maana baba wa taifa alisema "Ujamaa na KUJITEGEMEA". Mtu hudharauliwi bila ya sababu.

    ReplyDelete
  20. Duuh!, naona baadhi ya wadau wana hasira na askari huyo wa barabarani mpaka wanashindwa kusona aya inayoeleza kuwa hata mwanahabari naye alitwaga matezz na "diplomat" wakati akiuliza kulikoni. Lazima huyo mzungu alitafuna tambuu au ugolo. Utatemaje mate namna hiyo na hivi, kinga (immunity)ilishindwa kuzuia mate kufyatuka namna hiyo.

    ReplyDelete
  21. HIVI NI SAHIHI KWA MWANDISHI WA HABARI KUMUHOJI MTUHUMIWA NDANI YA KITUO CHA POLISI?

    ReplyDelete
  22. unapoambiwa tembea uone haimaanishi kuwa uingie mitaani !
    wewe mdau PETER NALITOLELA bwege sana na comment yako ! huna uzalendo kabisa wewe. ninaimani ya asilimia mia wewe hujakutana na vitendo vya kibaguzi vya hawa jamaa nchi za wenzetu! mimi ni mmoja wao, kutemewa mate ni kawaida sana kwa hawa jamaa huku kwao, na ukishtaki polisi wanakutoa mkuku, sasa nataka nione polisi wanyumbani watamuachia ama kumdhibiti, RACIST tu huyo mtu hana lolote.
    tena analeta ubaguzi home wallahi ninge mtia midole ...... ya macho ! shenzi sana!
    na wabongo tuwe na uzalendo.
    Mdau No 5 !

    ReplyDelete
  23. Aaaaaaahhhh, kwa kweli hii sasa too much, yaani waafrica tumedharaulika kiasi cha kufikia hatua ya kutemewa mate? Mbona tunadahalilishwa jamani???? Yaania huyu mwanamke ni dharau gani kufikia hatua ya kutemea watu mate?

    Mie nafikiri kuna umuhimu wa watu wakubwa wahusika (hasa waziri wa mabo ya ndani) kuchukua hatua, hasa ni kumfukuza huyu mzugu aende kwao.

    Lakini si ajabu ukiona huyu mwana izaya akaendelea kuishi hapa na kufaudi nchi yetu, hebu tuoneshe kuwa na sisi ni watu na ustaarabu na heshma jamani..Hi ni dharau sana.

    ReplyDelete
  24. well done mzungu alichoshwa na mayeni ya traffic police, jamaa anawai airport halafu wanamletea za kulete! sometimes police dar wanachosha!

    ReplyDelete
  25. Ingawa sijapata taarifa kamili kuhusu tukio lenyewe, inasikitisha kuona mtu, tena mfanyakazi wa ubalozi, ambaye anapaswa kuwakilisha nchi yake vizuri, anafanya mambo ya aibu na udhalilishaji kama hayo tena kwa watumishi wa serikali!!

    Kwa kuwa polisi wana taarifa za tukio hilo, tuache sheria ifuate mkondo wake. Ubalozi wa Canada unapaswa kufuatilia suala hilo na kumchukulia hatua mfanyakazi huyo. Michuzi, fuatilia suala hilo tujue mwisho wake.

    ReplyDelete
  26. michuzi maraffic wetu jamani wanapenda rushwa na traffic anapokusimamisha sio kwamba anataka kukueleza na kukusaidia ila anataka akukandamize, mimi nahisi wakuu waingilie kati, inafika mahala mtu anaweza kufikishwa akafanya kitu asichostahili, kwa kweli wanakera na ni wana roho mbaya.
    lipo jambo wanahisi watu huwadharua na hiyo inawasabibishia wasiwe na onfidence zao zipo kesi wanazichukua kama njia ya kuadhibu.

    jana sijui ile barabara ya lebanon watu hutumia kukicha yupo traffic alimuharis dada mmoja na siku zote wanaoharisiwa barabara ni na matrafic ni wanawake, sijui niji tatizo ni nadra kumkuta mwanaume amekuwa harrased, na huyo dada wa jana tunasikia yuko segerea, but yule rafic hakuwa na haki wala sababu za msingi htakidogo aliamura magari yanarudi reverse kwenye main roda, njia ambayo kila asubuhi huona watu uitumia na matrafic wanaruhusu.
    senaruio kama hii mtu kama huwezi kujua haki yako si unaishia , mimi natoa wito kwa DPP, na wakuu wenyewe tushirikiane mno, maana wanapowapeleka kituoni hukutana na wengine ambao kwanza hawataki kuwasikiliza wanalotaka ni kuwapeleka watu segerea mimi sidhanisheri ndio ilivyo kuna haki za msingi.

    traffic kweli wabadilike, we need changes, otherwise watu hawatisha kurevenge kwa visa wanavyofanyiwa.

    imagine huyo msichana wa jana, yeye ndio aliombwa apelekwe kituoni na alikuwa na kila sababu, na tulishuhudi aunambiwa yuko segerea na aliwekwa mahabusu jamani sheria haki za watanzania?

    ReplyDelete
  27. watu wengine hamna cha kusema,yani mnaona hilo tendo ni halali kwa kuwa tu matrafiki walishawaudhi katika namna moja au nyingine????
    Hamwezi kuwa sawa,usisahau utu wako kwa msala kama huu ambao unapita tu huyo traffic na mwandishi kama wanadamu wengine wanastahili heshima katika utu wao.Kitendo hixho kinapaswa kulaaniwa bila kujali ni nani kakifanya...
    Tusijisahau hivyo tukaoendeshwa na chuki maana bado tuna ufahamu kama kitendo ni kibaya lazima tukilaani kwa kauli moja.

    ReplyDelete
  28. KELAND PRIMARY SCHOOLDecember 11, 2009

    Asijutetee kuwa ana kinga ya ubalozi.Ile kinga haifanyikazi katika makosa ya kipuuzi kama hayo hayo, sheria na ichukue mkondo wake

    ReplyDelete
  29. PETER NALITOLELADecember 11, 2009

    NYINYI WATU MKOMAGE KUNIITA SINA AKILI.NINA DEGREE YA UCHUMI KUTUMA MUZUMBE CGUO KIKUU CHA UNIVESITI MBONA HICHO NI CHA MTOTO, INGEKUWA MIMI NINGEMTUMIA HUYO TRAFIKI HAJA KUBWA KWA MAANA NI MAFISADI SANA, YAANI BONGE LA MMAVI NINGEMTUPIA KICHWANI, ILI LIWALO NA LIWE KARAGABAU SANA HAO MATARAFIKI. MSIMUHUKUMU MUZNGU WA WATU BURE, PENGINE ALIPEWA SIJUI HAUNA FIRE EXTINGUISHER AU TAKATAKA ZINGINE, SI UNAJUA TENA

    ReplyDelete
  30. Au ni mja mzito nini? so anasikia kichefu chefu mara kwa mara ndo maana ana tema mate ovyo ovyo!!!!!

    ReplyDelete
  31. nanukuu "jerry muro (29" kwanini umri wake au ni namba yake???

    mh ila sijui sana yan uyu afisa kapata kichaa tu aanze tema mate???au ndo zile tabia za polisi wetu barabarani??

    hakuna kesi apo,jamaa atapeta tu

    ReplyDelete
  32. kwani ile ISHU ya wajeshi kumtwanga traffic pale ubungo ilifikia wapi???ilimalizwaje?

    kama mdau apo juu pliz wanasheria mtufafanulie mwandishi wa habari ana ruksa kuingia polisi na kumhoji mtuhumiwa kirahisi ivo?tena mtuhumiwa akiwa wa kinga ya "kidiplomasia????????????????

    mbona kawaida sana hii,bongo ubabe ubabe

    kazi kwelikweli

    ReplyDelete
  33. Kwa kisa hiki ninamkumbuka Waziri mkuu wa Singapore Mr Lee Kwan Yeu(Minister Mentor)Bahati mbaya sikumbuki mwaka aliwahi kushikilia adhabu ya VIBOKO kwa askari mmoja wa USA alibaka ndani ya Singapore pamoja na kuwa Rais wa USA kwa wakati huo Mr Bush alimuombea lakini alitandikwa mikwaju bila kujali anatoka wapi kwa hiyo kwa kosa hilo raia huyo ahukumiwe na kuadhibiwa kama wengine.

    ReplyDelete
  34. maaskari wa tanzania hawana ethics jamani kusema ukweli, wanaitaji training ya kurespect others, pindi unapotaka kuheshimiwa uheshimu na wengune.

    ReplyDelete
  35. Nimesoma comments hapo juu, na baadhi y magazeti yalioandika issue hii.Kwa mtu makini yeyote atajua kuwa magazeti yoote yako biased.Yameandika kutemewa mate kwa polisi bila kusema chanzo kilikuwa nini?Haiingii akilini kwamba Jean aitoka huko atokako, akamkuta askari wa kitanzania pale akamtemea tu mate na kuondoka.You guys you need to think deep.
    Mimi naishi Canada, na kama ingekuwa hao watu ni wabaguzi kiasi hicho hapa kusingekalika.
    Na si kila alichosema huyo polisi wenu ni sahihi au kweli.Na ndio maana nawahakikishia japo itawauma kuwa huyo jamaa hatafanywa kitu.na huyo polisi wenu'mla rushwa' moto wake atauona toka kwa bosi wake.
    Kuhusu mwandishi wa habari, ni sheria ipi inamruhusu kumhoji mtu ambaye yuko polisi, tena chini ya ulinzi?Au kwa kuwa alikuwa MZUNGU?
    Acheni kutoa maoni ya kutetea ujinga hata kama inawauma.
    Michuzi hata kama usipotoa maoni haya mimi ujumbe nimeufikisha ,hata ukisoma wewe inatosha.

    ReplyDelete
  36. MIMI NAONA SUALA HILI LINAKUZWA TU KWA SABABU MHUSIKA NI MWEUPE. HAYA MAMBO KWA SISI WASWAHILI YANATOKEA KARIBU KILA SIKU.

    HEBU FIKIRIA MHUSIKA ANGEKUWA DADA WA KISWAHILI SECRETARI NDIYO ANAWATEMEA HAO JAMAA MATE WANGEFIKISHANA POLICE? KWELI? UNAMTUKANA AU MNATUKANANA YANAISHA AU KUZUSHA VITA YA MATE.

    LABDA KWA YULE ASKARI KWAKE INGEKUWA NGUMU KIDOGO LAKINI MURO ALITAKIWA KUTEMEA MATE NA YEYE TENA DOUBLE DOUBLE AND THEN YANAISHA, EASY!

    ReplyDelete
  37. Kaka Michuzi,
    On a Fair Note: Wanadiplomasia hawaruhusiwi kabisa kufanya kitendo kama hicho, nomatter what happen.Hii ni kinyume kabisa na misingi ya kazi zao duniani kote. Kwa kitendo hiki nadhani mhusika angekuwa ameshakamata Pipa kurudi kwao Canada. Jamani Wizara ya Mambo ya Nje na Ubalozi wenyewe wanalifahamu hili fika. Halihitaji maswali mengi wala uchunguzi wowote:

    Nasikitika sana mtumishi wa Ubalozi wa nchi kama Canada amekuwa USELESS kiasi hiki.

    ReplyDelete
  38. NAAMINI KABISA HUYO MZUNGU SIYO KICHAA KUMTEMEA MATE POLISI ILA HAKUPASWA KUFANYA HIVYO. POLISI WETU TUNAJUA WANAMATATIZO SANA, INAWEZEKANA ALIZUIA MAGARI YANAYOTOKA UPPANDE GARI LA MZUNGU LILIPOKUWA KWA MUDA MREFU BILA SABABU MAALUM. HAYO NIMESHAYAONA SANA BONGO NDIYO MAANA MZUNGU AKAINGIA HASIRA. MZUNGU KUFANYA HIVYO SIYO HAKI NA SERIKALI ITOE TAMKO ALAFU POLISI NAO WAJIREKEBISHE

    ReplyDelete
  39. Tanzania kuna mchezo mbaya wa kuabudu wazungu na kuona na miungu midogo! Hao wanaowaabudu waje hapa USA wawaone mitaani wananuka na wanaomba omba hela hata kwa sisi weusi! Nawaambia wakifika Afrika wanaishi maisha mazuri kweli kweli kuliko kwao.

    Nakumbuka nilivyokuwa Daily News mweusi alifungwa miezi sita kwa kumtemea mate polisi. Msishangae kusikia huyo mzungu amerudishwa Canada kwa psychiatric treatment. Mzungu binadamu kama mweusi.

    ReplyDelete
  40. HAWEZI KUMTEMEA MATE BILA SABABU, LAZIMA KULIKUWA NA MTAFARUKU KABLA YA KUMTEMEA MATE, KUNA KINGA ZA KIBALOZI, NA HIZI KINGA ZIMEWEKWA KWA KOSA LOLOTE LILE KWANI KOSA NI KOSA TU SO HUWEZI KUSEMA KOSA HILI KINGA YAKE HAITAMSAIDIA, ITAMSAIDIA TU NA HALITATOKEA LOLOTE KWAKE NA KAMA POLISI NA NCHI ITAMFANYA LOLOTE HUYO BASI LAZIMA KUTATOKA TAMKO TOKA CANADA, NA HUU UMASIKINI WETU, HATUTADHUBUTU KUMFANYA LOLOTE SANA SANA KUTUPOZA LABDA UBALOZI WA CANADA UNAWEZA KUAMUA KUMRUDISHA NYUMBANI ILI KUTUPOZA. MWISHO MATATIZO YA BARABARA BONGO YANATOKANA NA UBOVU WA MIUNDO MBINU YETU, KWANA BARABARA KAMA ZA MJINI DAR ZINATAKIWA ZOTE ZIWE PANA ZA KUTOSHA NA KAMA IKIWEZEKANA ZIWE ZOTE ANGALAU NA LANE MBILI MBILI KUOELEKEA UPANDE MMOJA NA KWENYE JUNCTION ZOTE KUWE NA TRAFFIC LIGHTS BADALA YA KUSIMAMA ASKARI, TUACHANE KABISA NA MCHEZO HUU WA KUSIMAMISHA ASKARI TUTUMIE TAA NA KUWE NA ALAMA ZA WAZI ZA KUELEWEKA ZA BARABARANI NA HAYA MATATIZO YOTE YATAISHA, NA SI WAZUNGU WOTE NI WABAGUZI, NI NCHI MOJA TU AMBAYO WATANAZANIA MNATAKA KWENDA KUISHA AU KUSOMA AMBAYO NI NZURI HIVI SASA DUNIANI NI CANADA NA WATU POA NA WAKARIMU SANA

    ReplyDelete
  41. Hayo matezzzz si bure ni ama hasira ya rushwa au makampuni yao ya madini

    ReplyDelete
  42. PETER NALITOLELADecember 12, 2009

    BUREKING NYUUUZIII KUMBE WALE TIRAFIKI WA BALABALANI HAWAKUTEMEWA MATE KUMBE WAMEPIGWA DENDA MUDOMONI SASA HUYO MAMA WA KANADA AKASIKIA HALUFU AKATEMA MATE KURIKO KYAMEZA SASA POLISI WA TILAFIKI WAMEKASILIKA MNO SANA ETI KAWAZALAU KWA KUTEMA MATE. KWA NINI MUTU HIWE RAZIMA KUNYONYA MATE HATA KAMA YANANUKA UDENDA? MIMI NAHURIZA HIRI SWARI KWANINI HUMEZE MATE YA UDENDA KAMA YANANUKA?

    ReplyDelete
  43. naungangana na mdau wa canada watu tunaishi hapa na hakuna ubaguzi wa aina yoyote kama nifoleni bank ni kwa wote hamna ubaguzi huku ni raha tu sema libaridi limekaza mwendo hivyo huyo mzungu kumtemea polisi mate lazima walichafuana tuu sio bure matrafiki mnauzi saaana hata pale magomeni kuna dereva alimnyuka trafiki makofi ya ys haja yeye alikuwa anaruhusu magari ya pande zingine na upande wao akawa anawalia ngumu jamaa uzalendo ukamshinda akamuwasha makofi na huo mchezo matrafiki wanao saana wa kuzuia magari ya upande mmoja muda mrefu hata kama hakuna mkuu aayepita huwa mnakera kwa hiyo mkichapwa vumilieni manake watu nao wanavumilia maudhi yenu kila kukicha
    mdau canada

    ReplyDelete
  44. Kwa kweli hili jambo huyu ofisa wa ubalozi
    alilofanya sio zuri na linatia hasira
    sana,lakin kuna msemo usemao HASIRA HASARA sis
    watanzania hapo kinachotakiwa tusichukue maamuz ya
    hasira ambayo yanaweza kuathiri maslai ya nchi
    kwa ajili ya mambo madogomadogo.
    Hawa wacanada walianza kutupa misaada toka enzi za nyerere
    Miaka ya 1965 na wanaendelea kumimina misaada hadi leo
    Check http://www.tanzania.go.tz/foreignaffairs.html#CANADA:
    Kwa hiyo kwa maoni yangu kwa ajili ya maslai ya taifa ukizingatia
    Sisi ni masikin kweli nabado tunaitaji misaada,KWA
    AJILI YA MASLAI YA TAIFA na sio kwa maslai ya mtu mmojammoja inabidi asamehewe,wadau
    najua mtakasirika lakin ni umasikin unatuponza.

    ReplyDelete
  45. poa sana angemtemea makohozi kabisa wamezidi mbona wajeshi wana wakon'goli kwa sana tuu??? jamani hawa matrafiki waoneni tu na nguo nyeupe roho zao ni kutu sana hawana utu kikosa kidogo tu cha kueleweshana kwao ni big ishu hadi kieleweke (mlungula aka rushwa) utadhani wao malaika hawana kweli hawana utu hata punje wakiwa kwa road wnawaza tu kukamua bila kutumia hirizi komeshweni sawasawa hadi mtie akili

    ReplyDelete
  46. ndugu zangu watanzania tuamuke kidogo katika kutetea au kuzungumzia jambo, lets wait and see why this muzungu amemtemea mate traffic, but in short i wish one day i will knock one of those traffic police. first they dont use common sence, unajua mungu alimuumba mwanadamu na kumpa akili ya kuweze kuitumia, nitakueleza matraffic wetu wanavyofanya, barabara ya nyerere kutoka mjini saa 5 asubuhi mpaka saa 11 jioni ni barabara hiyo moja tu ambayo wasafiri wote wa ndege wanaitumia sasa una kuta taa zinafanya kazi lakini traffic anaamua kurahisisha kazi (kama wawo wanavyojua) anaongoza magari yote yanayotoka bandarini kwenda buguruni kwa karibu saa nzima anasahau kuna watu wanakwenda airport kuwahi ndege. one day i was traveling and wanted to carry my car and walk...... it’s so bad . kwani kazi ya hizi traffic lights ni nini? i wish traffic could be there just to assist.... mzungu aliweke taa zifanye kazi ndio maana wanatutemea mate kwa kujua hatujui matumizi ya taa. leo pale ubungo nimekaa kwa saa moja kutoka barabara ya mandela kwenda mwenge, and when you hoot to them et unawapa hasira so hawaruhusu kabisa, sasa hiyo ni nini? jingine kwa nini serikari haiweki hizi traffic light za solar? kama ilivy tazara na sinza bamaga? wezetu ulaya wanafanyaje tuzaribu basi hata kucopy mifano ya wenzetu..... agalia barabara zilivyotengenezwa kienyeji mradi watazania wajue kuna barabara mpya. Mzee makufuli alivuja nyumba za buguruni and mwenge ili barabara ijengwe with at least 4 lean but what they did wakarudishia zile zile barabara mbili and kuweka mitaro mikubwa kwa ajili ya kuuwa watu. any way in short let’s wait and see whay mzungu alimtemea mate askari....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...