Mdau Zablon Mgonja ambaye ni mwalimu wa Kiswahili akiwa na madenti wake huko Madison, Wisconsin. Hawa wote wanakuja Bongo kuedelea kusoma Kiswahili na kushiriki katika miradi mbalimbali ya jamii. Mdau pia anakuja rasmi January 8 kuwaandalia utaratibu
Mkuu katika hali ya kuendeleza Libeneke la Kiswahili huko Marekani, darasa hili lilichaguliwa kuwa la mfano kwa waalimu wanaofundisha lugha za kigeni. Walitumia vigezo vya namna ya utumiaji wa zana za kufundishia, na kutumia lugha lengwa bila kutumia lugha asili ya wanafunzi. Yaani kama unafundisha Kiswahili basi unafundisha kwa kiswahili bila kutumia kingereza, na kama unafundisha Kingereza kwa waswahili basi unatumia Kingereza bila hata Kiswahili. Walirekodi video na wameweka mtandaoni. Hapa bado ipo kwa majaribio lakini itawekwa kwenye mtaala wa vyuo mbalimbali hapa Marekani ili walimu watumie kama mfano.
Mdau Zablon anamshukuru Mungu kwa hilo shavu.

Unaweza kuiona video yenyewe hapa
http://media.nflc.org/NCOLCTL-IC.mp4

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Mdau (mfundisha Kiswahili) kazi nzuri endeleza "libeneke", muulize Michuzi tafsiri ya "libeneke" endapo wanfunzi wako watakuuliza nini maana ya neno hilo

    ReplyDelete
  2. Safi sana kaka naona kazi nzuri sana. nimeangalia video yote... hongera sana

    ReplyDelete
  3. Asante sana mdau mfundisha Kiswahili. Unaendeleza utamaduni wetu na kulitangaza vyema taifa letu la Tanzania. Mungu akubariki!

    ReplyDelete
  4. Haya tena kila mtu na namna yake ya kuzamia;kuna anayefunga ndoa na mzungu azamie Ulaya na kuna anayejifunza Kiswahili azamie Bongo!!Kazi...!

    ReplyDelete
  5. sawa kabisa fundisha wazungu wote kimatumbi hadi obama tunataka dunia nzima ijue kimatumbi

    ReplyDelete
  6. safi sana fundisha wazungu wote kimatumbi hadi obama tunataka dunia nzima ijue kimatumbi

    ReplyDelete
  7. Hongera,

    Lakini kufundisha Kiswahili kwa Kiswahili sio utaalamu peke yake bali ni motivation ya wanafunzi. Yaani wanafunzi kukitaka hicho Kiswahili.Hapo ulipo Madison kuna Chuo kinakipa nguvu Kiswahili. Lakini ungekuwa unafundisha katika vyuo ambavyo havikipi Kiswahili nguvu basi ungegonga mwamba.Wanafunzi wangekimbia mmoja mmoja.
    Lakini kufundisha Kiswahili kwa Kiswahili sio uchawi. Mimi nakumbuka nilisoma Kispanish na mwalimu alikuwa anatoka Cuba na hakuwa anajua Kiingereza. Na ilikuwa poa sana. Hakuwa akitumia teknolojia yoyote isipokuwa kitabu chake tu. Lakini wanafunzi wote walikuwa wanataka hiyo lugha.

    ReplyDelete
  8. Huyu mwalimu apewe sifa tele! Ni matumaini yangu Baraza la Kiswahili Tanzania litamsaidia mwalimu huyu kwa mawazo, silabasi na pia vitendea kazi kama vitabu nakadhalika ili mtaalamu huyu aendeleze "libeneke" hapa Marekani.
    Wazungu hawa wasiishie hapa, wasome riwaya, wajue tungo, wajue ngeli zote n.k. Ni hayo tu kwa leo.

    ReplyDelete
  9. ww ndio mwanaume kweli hii ndio kazi decent majuu,sio mtu ana degree Dr anauza wadoli dukani,kuchamba vizee

    kuna kazi za maana waweza fanya na ukaishi kwa raha tu,sema wabongo wengi wavivu sana kujishughulisha na kazi za maana km ualimu na unesi

    ReplyDelete
  10. Hongera Zablon, Mungu akujalie ufanikiwe zaidi. Nadhani hii inafaa hata kutumika hapa kwetu kwenye kufundishia kiingereza...

    Storge!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...