Kaka Michuzi pole kwa kazi!
Mimi ni kijana wa umri wa miaka 35,nna mpenzi wangu ambaye ameachika mara mbili,yaani ameshaolewa mara mbili na kuachwa.Hivi sasa nnae mimi natarajia pia kumuowa,mimi nnae mke,pindi nikibahatika kumuowa atakua mke wa pili au mke mdogo.Jambo linaloniumiza kichwa ni kwamba hajatulia,yaani ana wanaume wengine nje.
Mara ya mwanzo tulipokutana alinambia yeye ameachika na muda huu hana mwanaume yeyote,nilimuamini kwani ilikua naenda nyumbani kwani bila ya wasiwasi wala woga.Kwa muda wote huo sikuona ishara yoyote mbaya ilikua ananipa penzi motomto.
Baada ya kupita kama kipindi cha mwezi mmoja niliona mabadiliko,mpaka akanambia nikitaka kuonana na yeye nisifika nyumbani kwake kwani wako mama zake wadogo kwa hiyo ilikua tunakutana mbali kidogo na yeye,hata ile tabia ya kunipigia simu kila mara ilikatika kabisa na nikimpigia mimi ilikua hapokei au anakata kabisa inaweza hata zikapita siku mbili hatujawasiliana.
Pindi akiwa na safari zake ndo ananipigia nende nikampakie kwenye gari langu nimpeleke,nilijaribu kumdadisi kwa nini amebadilika,alinambia ameamua tu nanisiwe na shaka kwani yeye bado ananipenda kwa udhati wa moyo wake.
Hali ilizidi kunitia wasiwasi nikaamua kupeleleza ndipo nilipogundua kwamba kumbe kaja bwana wake ambae anaishi UK.Niliumia sana lakini ilibidi nivumilie nilijua iko siku ataondoka tu na nitamueleza duku duku langu.
Siku moja akaniaga kua anakwenda Kenya kwa ajili ya kuwasindikiza mama zake wadogo ambao wanatoka UK wamekuja Zanzibar kwa msiba,Nilimkubalia kwani huko nyuma aliniaga anakwenda Kenya kwa matibabu kumbe ilikua ndio amekwenda kumpokea huyo bwana wake wa UK na pesa ya nauli na matibabu nilimpatia.
Siku ilipofika aliondoka na kuwasindikiza wageni lakini nilijua kika kitu kwamba anamsindikiza huyo bwana wake,ruhusa nikatoa.Alikaa kwa kipindi cha wiki moja Kenya baadae akarejea Zanzibar nilikwenda kumpokea bandarini nikamrejesha nyumbani kwani,lakini kwa kipindi chote hicho hakufahamu kwamba mimi naelewa kila kitu kuhusu yeye..
Zikapita siku mbili ndipo nilipoamua kumueleza kila kitu mwanzo alikataa baadae akakiri kua ni kweli akaomba msamaha nikamsamehe kwa vile ilikua bado nampenda.Tuliendelea kuishi vizuri baada ya kupita mda kama wiki tatu akaniaga tena kua anakwenda tena Kenya kwa ajili ya kumtafutia mdogo wake chuo niliingiwa na wasiwasi kidogo ingawa nilimruhusu baadae nikagundua kua sio kweli.
Niliamua kufanya utafiti wangu tena baada ya kurejea Zanzibar ndipo nilipogungua kwamba ana mwanamme mwengine huko kenya ambae ni kigogo wa KRA.Kama kawaida yake alikataa.Siku moja niliamua kuchukua cm yake nikaona msg za mapenzi kutoka Kenya,moyo uliniuma sana kwa huna moyo huwezi hata kumaliza kusoma msg moja.
Nilimuonesha msg zake akanambia kua huyo jamaa yeye hana mahusiano nae kimapenzi ila amamdanganya tu kwa vile alimuahidi kumtafutia kazi,isitoshe huyo ni kaka wa shoga yake kwa hiyo na yeye ni kama kaka yake.
Na hivi sasa huyu kigogo wameagana anakuja Zanzibar karibuni ingawa yeye ananificha lakini nimeona msg kwenye cm yake ingawa yeye hajui kama mimi najua.Mpaka hivi sasa bado wanaendelea kutumiana msg za mapenzi na huyu bibie kila siku safari za Kenya hazimwishi.
Kaka michuzi naomba wadau wanishauri nifanyeje na mimi bado huyu dada nampenda.
Ahsante,
Mdau Zanzibar