baadhi ya wanafunzi wa sekondari ya kibasila wakipepea wenzao waliopoteza fahamu baada ya mpambano na polisi walipoziba barabara kushinikiza usalama baada ya mwenzao kugongwa na gari
wanafunzi wakipepea wenzao
waliozidiwa wakiwahishwa hospitali
vilio vilitawala shuleni hapo
mwanafunzi aliyezidiwa akipelekwa hospital
gari la wagonjwa likichukua waliozidiwa
askari wa jiji wakiondosha jiwe lililowekwa barabarani na wanafunzi hao kuzuia magari yasipite

Picha na habari na
Ripota wa Globu ya Jamii, Chang'ombe
POLISI wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam leo wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kibasila waliokuwa wamefunga barabara ya Mandela na Chang’ombe kwa kutumia mawe makubwa yaliyokuwa kandokando ya barabara hizo.

Kikosi hicho chenye askari 11 walilazimika kutumia mabomu ya machozi kutokana na wanafunzi hao zaidi ya 200 wa Sekondari hiyo kupinga hatua ya kugongwa kwa mwananafunzi mwenzao Emmanuel Mapande.

Tukio hilo limettokea leo majira ya saa 3:30 asubuhi, kwenye makutano ya barabara hizo zilizopo karibu na kituo cha Polisi cha Chan’gombe.

Tanzania Daima lilikuweko kwenye eneo hilo baada ya kupata taarifa kutoka kwa baadhi ya askari kufuatiwa kugongwa mwanafunzi hiyo na basi la abiria aina ya Toyota Coaster ambalo lilitoweka baada ya kufanyika kwa tukio hilo, hata hivyo namba zake badi hajizafahamika bado.

Tanzania Daima lilishuhudia kiongozi wa askari hao akiwaamrisha askari kutumia mabomu zaidi kwa wanafunzi hao kutokana na kukaidi kuondoka eneo la barabara huku wakizuia magari kuendelea na safari, mengine kuvunjwa vioo.

“Tutumia mabomu ya machozi wanafunzi hawa wanakaidi amri ya Polisi, basi na sisi tunatumia nguvu kuwaondoa” alisema Kiongozi huyo.

Amri hiyo iliwafanya askari wenye silaha hizo kurusha mabomu hadi kwenye eneo la shule ya sekondari hiyo, huku wanafunzi hao wakijibu mashambulizi kwa kuwarushia mawe kwa askari hao.

Hata hivyo walionekana wanafunzi hao wakitokwa na machozi kutokana na madhara ya mabomu hayo na wengine ambao idadi yao haijafahamika mara moja wamekimbizwa kwenye hospitali ya Temeke kwa matibabu zaidi.

Walikimbizwa hospitali ni;Agatha Kivuvyro, Yusta Herman, Fani Abdul, Kuruthum Athanas, Jackline Gades na Mary Richard.

Wengine ni pamoja na Janeth Kagoa, Anet Kiyogoa na Mary Shao wote wa kidato cha nne na tano.

Baadhi ya wanafunzi waliiambia Tanzania Daima kuwa, mwanafunzi huyo wa kidato cha sita, aligongwa majira ya asubuhi wakati akivuka barabara akitokea shuleni.

“Amegongwa wakati akitoka maeneo ya shule kuelekea nje, hata hivyo ilikuwa ni makusidi ya dereva kwani yeye (dereva), anafahamu kuwa barabara hii inatengenezwa kwa sasa” alidai mwanafunzi huyo ambaye hakitaka kujata jina lake.

Wakizungumza leo wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo waliziomba mamlaka zinazohusika kuweka taa za kuongozea magari ili kupunguza ajali katika eneo hilo ambalo pia ni maarufu kama "machinjioni"







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. poleni wadogo zetu jamani serikali ya mafisadi inaendeshwa kifisadi

    ReplyDelete
  2. hivi mabomu ndo ufumbuzi. yaani hamfanyi kazi mpaka watoto wawaamshe?

    "hata sisi tulisoma hapohapo" hkuna mlifeli!!

    ReplyDelete
  3. Hivi Polisi anawezaje kupiga wanafunzi wa kike kiasi hiki na asifikishwe kwenye sheria?

    Only in Tanzania.

    NE,
    Reading, UK.

    ReplyDelete
  4. Nadhani Serikali inatakiwa kuweka 'zebra crossing' pale ambapo kuna shule na kuna barabara inapita. Lakini hata hivyo, ni kazi bure, kwani hizo 'zebra crossing' nazo haziheshimiwi kabisa, madreva wakiona watu wanapita wao ndo kwanza wanaongeza spidi, huwa nashindwa kuelewa wanakuwa na maana gani, ambapo 'pedestrian' ndo anakuwa ana haki. Cha msingi zingewekwa 'traffic lights' at least hizo zinaheshimiwa kidogo. Poleni sana watoto kwa msukosuko uliowapata natumai kutokana na msimamo wenu Serikali itachukua hatua ya kutekeleza ombi lenu. Pia wale wote ambao wameumia nawaombea kwa Mungu awasaidie wapone haraka.

    ReplyDelete
  5. tueleze hali ya mwanafunzi aliyegongwa

    ReplyDelete
  6. Hii ni aibu kubwa isiyo ya kifani.
    Ukweli ni kwamba usalama wa wanaotembea hauko tena.
    Watoto washule sikuhizi hawaheshimiwi kabisa, tena wanaonekana kama bugudha.

    Watoto wa shule ni taifa la kesho, kitendo walicho fanya ni cha kuheshimika na kuchukuliwa kwa nguvu zote na serikali na sio kupuuzwa.
    Barabara ya Kibasila, Upanga ni mfano mmoja unaosikitisha. hakuna sehemu ya kutembea, watoto wa shule na wanainchi hutembea kwa kubahatisha tu. Sehemu ndogo iliyoko, inajazwa na magari yaliyo paki, sasa usalama uko wapi???
    Hakuna mtu hatammoja aliyejitokeza kugombania haki ya wananchi na watoto wetu hawa wa Shule.
    Wameamua kuchukua hatua yao wenyewe, leo maisha yao yako hatarini, sasa jamani tumkimbilie NANI?? MEYA UNALAKUSEMA???? NA UTASEMA NINI????

    ReplyDelete
  7. what a shame Dar Es salaam - Police are protecting themselves and the criminals instead of protecting the school kids - Tanzania is dwindling more everyday - there are no policies to protect the children especially school children - no rules of engagement and the culprit will go kill another person and of coz get away with it - This govt is shameful - you sign human rights declarations yet there are no human rights if children are treated like crap - I feel sorry for all children - but more sorry for school children who have noone to protect their basic human rights - what am I saying "rights" in Tanzania? its like speaking chinese in Kilosa! Shame on the Police and all those who Did not come out and help these school children!

    ReplyDelete
  8. Hili tatizo linaanzia mbali. Wananchi wengi tunasifia "maendeleo" ya barabara kubwa zinazojengwa miji mikuu kama Dar na Arusha na wingi wa magari mazuri mazuri na mengi ya kisasa yenye magurudumu makubwa na viyoyozi ndani. Njia hizi za lami zimejengwa vizuri na kuna sehemu za watu kupita vivukio vya punda milia (zebra crossing) ambavyo haviheshimiwi kabisa na madereva.
    Ukija kwa madereva wa vipanya na mabasi ndiyo wako chini kabisa ya orodha ya raia wanaoheshimu raia wenzao. Hapa matatizo mengi. Kuna haya "maendeleo" ambayo Mwalimu Nyerere aliyaita "maendeleo ya vitu" na "si ya utu"; halafu kuna binadamu wanaokabidhiwa mashine huku fahamu zao hazipambanui kati ya mashine kuwa mtumwa wa mwanadamu au mwanadamu mtumwa wa mashine. Ukija kwa sisi wenyewe raia tunaotembea kwa miguu (pedestrians) utagundua tabia ya Kizungu inayoanza kuingia Tanzania.
    Na nimeshaongelea hili mara kadhaa katika safu zangu. Tunaanza kuiga tabia za kutopisha magari; tukitembea katikati ya barabara kama tuko sebuleni. Kwahiyo matatizo ni mengi na utatuzi wake ndiyo huo wa mkono wa sheria wa polisi kuwatimba na kuwadunda watoto wadogo kwa mabom ya machozi. Pale askari usalama na wanajeshi wanapoanza kutesa raia ni mwanzo wa ghasia tupu nchini.
    Na hawa askari nao si kiini cha tatizo maana wao ni mkono tu wa wenye nchi. Tatizo liko huko darini...
    Halafu ajabu wananchi wengi tumekaa kimya. Kama alivyosema dadangu mmoja ingekuwa ni wasichana walioshinda urembo au kukaa nusu uchi wapambe wangekuwa wanakutumia maoni tele kushangilia, Michuzi.

    ReplyDelete
  9. jamani kwanini asikari wetu wa bongo wanapeda sana kutumia nguvu kuliko busara hata kwa watoto pia shame on you people who are in power

    ReplyDelete
  10. Kama hii shule ingekuwa iko maeneo ya osterbay ingeshawekewa matuta maana watoto wa vigogo wanasoma huko lakini huku kwetu mtoni kwa mtoni kwa mzizi ali no body cares kama michael jackson alivyoimba kwenye wimbo wake akisema THEY DONT CARE ABOUT US

    ReplyDelete
  11. Its about time...hao mafisadi wasiopoangalia maslahi ya wananchi ...ndio mwanzo huo. Itaanzia kwa wanafunzi na kuishia kwa raia mitaani...Kama hawafungui macho sasa na kuwork for the people of Tanzania.....chungu kinachemka

    Ni aibu sana wao kumeheana nchi na kusahau raia wao kabisa. Kodi ilipwe na vitu visieleweke. Hapo machinjioni toka nikisoma miaka hiyo palikua panajegwa tu....Nakumbuka sana hayo maeneo...AGHHH

    ReplyDelete
  12. Hakuna kisingizio chochote ambacho kinatoa ruksa ya kutwanga watoto au in this case wanafunzi. kuna njia na ngazi za kisheria ambazo zingeweza kutatua malalamiko ya wanafunzi bila kupigwa na polisi, kuanzia kwa Waalimu hadi kwa wanaohusika na usalama wa barabarani na usalama wa wanafunzi but!......machinjioni pako vile vile tokea sie vijana wa zamani tuko shuleni, kwa hivo hii inaonyesha wazi kuwa miaka kumi ijayo machinjioni patakua hivi hivi na idadi ya wanafunzi pamoja na wavuka njia wengine itaongezeka. Kuridi kwenye swala la Polisi kutumia nguvu na mabomu ya mchozi, virungu na bakora kwa watoto binafsi sidhani kama ni sawa, tumeyaona haya enzi za Soweto na Sharperville hakuna haja ya kuridia historia mbovu tena. Wanafunzi bado ni watoto na akili zao bado zinakua sisi watu wazima inabidi tuwaonyeshe mifano kwa kuwalinda kwa kurekebisha waombi yao...I hope I did not offend no one but afte I saw the pictures it kinda hit me in the head and so I really think that there was a pieceful and ligal way to deal with this kinda situation, that's why Police go to training so they can have better judgement when time comes to deal with situations like this and other.
    God Bless Bongo.

    ReplyDelete
  13. HUO NI UTUMIAJI WA NGUVU ZA ZIADA KWA KUWAKABILI WATOTO WADOGO TU AMBAO WANGEWEZA KUTULIZWA KWA MANENO YA BUSARA TU, THAT IS NO LEADERSHIP, NI UNGOZI WA KIDIKTETA. TUNAOMBA KITU KAMA HIKI KISIRUDIWE TENA JAMANI NA YULE ALIYETOWA AMRI YA KUTUMIKA MABOMU ANATAKIWA KUWAJIBIKA.

    ReplyDelete
  14. Naona kuna siku hii nchi itageuka na watu watajichukulia sheria mkononi kwa kila kitu. Sababu ni uongozi finyuuuuuuu.

    ReplyDelete
  15. Poleni wanafunzi wenzangu. Hiyo ndo serikali isiyojali usalama wa wanafunzi. Sehemu zote za shule inabidi speed limit iwe enforced na adhabu kali ichukuliwe kwa dereva yoyote atakayepita hiyo speed limit. Adhabu kama fine pamoja na kifungo, na siyo fine peke yake. Lakini kwa sababu serikali yetu ni ya mafisadi, badi watajali maslahi yao kwanza badala ya wananchi. Kila mara Rais wetu anakuja huku marekani kuomba msaada, inadibi atulie huko kusafisha kwanza serikali ndo sisi watanzania wa nje tutamsaidia kuijenga. Lakini ka hali ya sasa sitoi msaada wangu ng'o!

    ReplyDelete
  16. Waziri wa mambo ya ndani Lawrence Masha si umeishi Marekani wewe? Je uko Marekani wana utaratibu gani kwenye barabara zinazopita karibia na mashule? Sasa kuna ugumu gani wa kulitekeleza suala hili uko bongo? Hivi hata suala hili ndugu Masha unahitaji kuelezwa kwenye Michuzi blog ndio ulifanyie kazi? Duh!!!!! Ama kweli siasa inaondolea watu common sense..

    ReplyDelete
  17. Maskini, vitoto vyenyewe vidoogo ndo vipambane na polisi hivi. Polisi muwe na aibu, kuna mengi makubwa mnatakiwa kuyafanya sio vita na vitoto kama hivi!!
    Mdau wa P&T

    ReplyDelete
  18. WADOGO ZANGU HONGERA SANA KWA UJASIRI WENU NACHOWASHAURI SUBIRINI RAIS AKITOKA ULAYA MUANDAE MAANDAMANO YA AMANI MKAONGEE NAYE IKULU, MUOMBE YAWEKWE MATUTA TENA MAKUBWA KUPUNGUZA KASI YA MWENDO WA MAGARI. HAWA ASKARI WATAWAUMIZA BURE NA HAKUNA KINACHOTENDEKA. POLENI.

    ReplyDelete
  19. wee nendeni mwanza mkaone jinsi watu wanavoshindana na magari barabarani

    yani mtu anatembea katikati ya barabara bila woga na baskeli ndo balaa lingine,,,yani mwanza magari yanapisha watu barabarani tena kwenye mataa kabisaaa

    iringa wanaheshimu sana zebra pale mjini nilishangaa sana gari inasimama kuangalia km raia anavuka

    iko kazi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...