Profesa John Mbele

Ankal nimeona hoja hii ya haja ya Profesa John Mbele very interesting
ku-'share' na wadau ktk blogu ya kimataifa Blogu ya Jamii
Hoja ya Profesa Joseph Mbele kama nilivyo 'Qoute' toka KwanzaJamii:
Mdau A-Taun
---------------------------
'''Mwenyekiti

Hoja zangu zitaingiaje vichwani mwa watu wenye akili finyu, wasiojiamini, ambao hata kujitambulisha hawajitambulishi?

Ufinyu wa mawazo unajitokeza hapo watu wanapodhani kuwa kazi ya kujenga nchi ni ya rais, wanapokaa vijiweni na kungojea Kikwete afanikishe malengo ya Taifa. Ukiachilia mbali akina mama huko vijijini ambao wanafanya kazi sana, na baadhi ya watu mijini, mamilioni ya Watanzania wanakaa vijiweni wakisogoa badala ya kufanya kazi.

Watanzania wengi wanakaa vijiweni, kwenye baa, kwenye sherehe, badala ya kuwajibika kazini. Hata maofisi yameshakuwa vijiwe. Ni nchi gani inayoweza kusonga mbele na wananchi wa aina hiyo, hata kama kiongozi ni makini sana? Ufinyu wa mawazo ndio unawafanya watu wasione hilo, na badala yake wawe wanamshambulia rais. Jishambulieni pia nyinyi wenyewe.

Sasa pamoja na ufinyu huo, hao ndio wanaodai kuwa wataweza kushindana katika dunia hii wakishapata uraia wa nchi mbili. Mtashindana na nani kama ni waoga namna hiyo, msiojiamini? Mpewe hata uraia wa nchi kumi, mwone kama mtaiweza dunia hii inayohitaji elimu, maarifa na ujuzi.

Inafahamika wazi, na imefahamika kwa miaka mingi, kuwa waTanzania wanapata shida hata kujieleza. Lugha inawashinda, iwe ni ki-Swahili au ki-Ingereza. Vyuoni, inabidi mwalimu anapofundisha atumie maneno ya ki-Ingereza na kiSwahili, kwani lugha ya kufundishia, yaani ki-Ingereza, haifahamiki vizuri. Na bado watu mnaamini kuwa, pamoja na uzembe wote huu, mkipata uraia wa nchi mbili mtaweza kushindana ulimwenguni.

Huku Marekani, kuna nafasi za kufundisha ki-Swahili katika vyuo mbali mbali. Ajabu ni kuwa wa-Kenya ndio wengi wanaochukua nafasi hizo. Watanzania bado wako vijiweni, hawasikii la mtu.

Daima nimewaambia wa-Tanzania kuwa tujizatiti kielimu, na tujielimishe kweli. Na ninajaribu kutoa mchango wangu kwa upande huo. Sio siri, hata vitabu nimewawekea huko huko Tanzania. Lakini wa-Tanzania ndio hao, maneno na maringo yasiyo na maana. Shuleni wanatafuta dezo, na wengine wanaghushi vyeti. Wako wanaodhani watafanikiwa kwa kutumia ngozi za binadamu, viungo vya albino, bahati nasibu za makampuni ya simu au bia, uraia wa nchi mbili, na kadhalika.

Huku ni kujidanganya. Inabidi Watanzania mtambue kuwa leo kinachoongelewa ni uchumi unaoendeshwa na ujuzi, elimu, na maarifa. kwa kiIngereza wanaita “knowledge economy.” Tujitazititi kielimu. Bila kujizatiti namna hiyo, hata mkipata uraia wa nchi kumi haitawasaidia, kwani mtashindana na watu wa dunia yote waliojizatiti ipasavyo.

Nitakuja Tanzania mwaka huu kuendesha warsha, na ratiba mtaipata. Njooni tukutane, kama mnajiamini. Lakini vile vile, njooni tuelimishane, kama mnataka kujiandaa kweli kwa ushindani wa dunia hii ya utandawazi. Warsha moja imeshapangwa tayari. Itafanyika Arusha Community Center, tarehe 3 Julai, kuanzia saa 4 asubuhi.''

kutembelea libeneke la Prof. John Mbele

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 76 mpaka sasa

  1. Prof. ana pwennti nzuri lakini kwa kuwalaumu waTz waliko Tz kwa kudai uraia wa nchi mbili ni kuwaonea, kwani wanaoomba kupewa uraia wa nchi mbili kwa asilimia kubwa ni waTz waliko nje ya Tz.

    Zaidi yahilo nadhani Prof. kasema ukweli usiopingika,

    ReplyDelete
  2. Wow! Wow! Professa

    Aste Aste Apna Siko, Chote Chote Rhooonaaa!

    Uraia wa nchi mbili ? Nini hasa ubaya wake ? Mbona unarusha Maneno tu! in generalizing what has already been proven to differ your views that; negatively portraying the advantages of dual citizenship.


    Profesa, kuna ubaya gani wanangu kupata uraia wa nchi mbili, JE kuna ubaya gani sisi kupata uraia wa nchi mbili achilia mbali ya hayo zaidi ya hayo ya SENENE kwenye maji, kama anavyoongea Michuzi.

    ETI MSOMI? mwenye kutegemewa kuchambua mambo ?


    Profesa.."Diaspora wa kitanzania nchini marekani wamepeleka fedha za kigeni nchini Tanzania, kwa muda mwaka mmoja tu 2009, kuliko kilichopatikana kwa muda wa miaka kumi katika madini kwa muda wa miaka 10 iliyopita ukichanganya"

    So Who is the real JEWEL here profesa?

    ReplyDelete
  3. Mzee Mbele, heshima yako mzee wangu!
    Nakuheshimu sana na ninakubali kuwa waTz tunatakiwa kujichambua kwanza wenyewe. Lakini, anayestahili kupata uraia wa nchi mbili si yule tu aliyekwenda shule ya kubobea, mchango wa taifa unaweza kuletwa hata na wale wasio soma kwani wanafanya kazi nyingine ambazo zinawapa kipato kizuri tu; kwa kipato hicho wanaweza kuwachangia hao mama zetu wa vijijini na kuwaondolea ugumu wa maisha ya kila siku ... maji ya bomba, mafunzo juu ya chakula bora, magari ya usafiri, nk. Halafu, NI HAKI YA KIMSINGI KWA KILA RAIA!!

    ReplyDelete
  4. Prof a little bit despaired but with good reason, he has given it all and we don't seem changing.

    No doubt, he's got a very strong case. A lot of pieces to put together, I guess. So how do we move forward??

    ReplyDelete
  5. Mmetoa points nzuri,wadau. Professa mzima anatoa hoja za darasa la saba. Tanzania haiko nyuma kwa sababu wanataka dual citizenship, ni kwa sababu ya uongozi. Ni kweli kuna uzembe mwingi, lakini kuwanyima watu uraia wa nchi mbili sio solution. Uraia wa nchi mbili unahusu nini mambo ya rushwa, umeme wa mgao, maji yasiyotoka, shule mbovu na incompentence ya viongozi?

    Sishangai sana; kwa sababu hizo ndio hoja za Tanzanian intellectuals. Wakati wa zile enzi za kupanga foleni ya unga, sukari na vyakula vinginevyo, Professor mmoja Mtanzani aliyekaa Marekani kwa muda mrefu, alisikika akisema kuwa, "Watu wanalalamika njaa, njaa! Kwani lazima kula ugali, si mnaweza kula mihogo tu?"

    ReplyDelete
  6. Truth is paramount for civilised society, speaking truth like this Man and behaving accordingly within those bounderies of truth determines how your neighbours and fellow citizens perceive you. Tell you what expecting to see stupid ideas from some people who will vent their anger and some to make us lough. Professor write to champion truth. Tuamke wadanganyika.

    Mdau Nansio.

    ReplyDelete
  7. Haya masuala mawili sio mutually exclusive. Ni kweli elimu ndio nguzo ya kutuwezesha kushindana katika ulimwengu wa sasa lakini Profesa ameizungumzia kama elimu sijui niiite ya darasani ya kusoma mpaka chuo kikuu...
    Vipi na elimu za watu kama Haruna Moshi ambaye anaongea 'fluent football' lakini Kiingereza chake sio kizuri? Uraia wa nchi mbili haungemfungulia milango ya kucheza ligi nyingine za ulaya bila kuchukua nafasi za wachezaji wa nje ya Ulaya?

    ReplyDelete
  8. Professor ameandika upupu tuu, hamna lolote jipya alilosema. Yeye anajaribu kutibu symptoms badala ya ugonjwa wenyewe. Serikali yetu imeshindwa kutengeneza mazingira yatakayowafanya watanzania wajikwamue!

    Sio kwamba watu wanataka Kikwete awape pesa; bali, wanataka serikali itakayoondoa vizingiti - rushwa na urasimu. Mbona huyo Prof. hajawatukana wamarekani wwanaompinga Obama kila siku kwenye Tea Party Movt, jee nao ni wavivu wa kufikiri?

    Rushwa kila sehemu , halafu huyu Professa anaisifia serikali! Nenda bandarini, nenda mahakamani , nenda wizarani matatizo ni yale yale. Prof. Mbele must understand that the government has a major role to play in bringing positive changes to our country. Tanzanians are not whiners, as professor would like to potray; nonetheless, they want their elected officials to become part and parcel of the solution to their problems.

    ReplyDelete
  9. ooooh jamani wabeba mabox mshirikishe profesa mkileta makontena bongo,mnamuacha na vitabu tu haipendezi!

    ReplyDelete
  10. Maoni ya profesa tunayaheshimu. nitatoa maoni yangu katika hoja mbili, tatu hivi:
    1. "mamilioni ya Watanzania wanakaa vijiweni wakisogoa badala ya kufanya kazi". SI KWELI, ninafikiri hizo ni fikira tu za profesa. Unafikiri pesa zinazofisadiwa na kuendesha anasa za wateule zinatoka wapi? wafadhili wanachangia si zaidi ya 40% ya bajeti ya serikali. 60% inatoka kwa watanzania walipa kodi. Kusema mamilioni yamekaa kijiweni ni matusi.

    2. Kwa vile makala yako inakazia ulichokiita "knowledge economy", kwa maoni yangu hiyo "knowledge economy" haidondoki kutoka hewani kama mvua, bali inatengenezwa - na hilo ndilo mojawapo ya majukumu ya viongozi ikiwa ni pamoja na rais. Kama Rais Kikwete hajatumia mamlaka aliyopewa kuleta mageuzi ya "knowledge economy" tumnsifie kwa lipi kuwa ni kiongozi bora? "knowledge economy" italetwa na wakulima wa Mbinga???? Huo ndio uongozi tunaozungumzia - kufanya maamuzi mazito vinginevyo kama huwezi usikimbilie Ikulu!!!!!

    3. uwezo wa kushiriki katika ushindani wa dunia ya utandawazi hautapatikana kwa njia ya warsha iwe ni Prof Mbele au ya Rais JK au UN, bali kwa UONGOZI kuchukua maamuzi mazito kuleta mageuzi katika mfumo wa elimu. Bado mfumo wetu unaongozwa na misingi tuliyoirithi kutoka kwa wakoloni kama ulivyo mfumo wa utawala mzima wa nchi. Nani alaumiwe: mamilioni ya watanzania au wateule wetu?

    Nimalizie kwa kusema kuwa ningekutarajia profesa uzungumzie masuala ya kimuundo na kimuundombinu (structural issues) na haya uliyoandika ukawaachia akina Mhe Yusuf Makamba & Co.
    Mlalahoi
    Kwa mfuga mafisadi

    ReplyDelete
  11. Huyu profesa amechemsha; hakuna uhusiano wowote kati ya uraia wa nchi mbili na hiyo anayoita knowledge economy!!

    ReplyDelete
  12. Kweli mtu unaweza ukasoma sana lakini usielimike. Ningekudadavua hapa wewe unayejiita profesa lakini najuu hili jukwaa maoni hayatatolewa. Aliyeileta hii habari (ambaye ninahisi ni Mjengwa) anatakiwa amwambie profesa wake aende Jamii forums akutane na maneno yake. Kwenye hoja yake ameanza kwa kuita watu wanaakili finyu hii ni kashfa na kuonyesha uwezo mdogo wa kufikiri na kutojiamini kama yueye anavyodai wa Tanzania walivyo. Pili swala la uraia lina maslahi mengi mno ambayo asie nao hawezi pata. Yeye mwenyewe ama aliomba kibali cha kufanya kazi (working VISA) au ni mkazi wa kudumu (permanent Resident) au pengine ameshachukua uraia kabisa sasa wenzie wakitaka uraia wa pili ambayo ni hatua ya juu zaidi kuliko hiyo status aliyonayo tatizo linatoka wapi? Profesa mambo yote yanaanzia kwenye familia hebu angalia kwako kama yako sawa ndio uje utukane watu kuwa wana ufinyu wa mawazo. aaaaggggrhh!!!!!!

    ReplyDelete
  13. Prof. Mbele naona unapigia pande unga wako hapo Kuanzia July 3rd...kwi kwi kwi. Ila ujasirimali ndio wenye. Mbona nasikia wewe Prof. Mbele umechukua uraia wa marekani?

    ReplyDelete
  14. Professor I will be able to see your point if you could tell us how to go forward! Please tell us the truth, I guess you should have your own problems with the DIASPORAs! If you don't mind, can you please tell me if your books (those books you have written) are for sale or not?
    Let us be open!!!!!

    ReplyDelete
  15. Anonymous wa Feb 8, 09: 02: 00, taratibu ndugu yangu, embu punguza jazba ili uelewe ujumbe wa Prof. Mbele. Muhimu sio suala la dual citizenship- la muhimu hapo ni kuipa elimu kipaumbele na kuacha ubabaishaki kwenye masuala ya ujenzi wa Taifa.
    Prof anchaoongelea hapo ni ukweli isiopinga, haswa kwa Watanzania waliopo nje, na ambao suala la elimu wameliweka kando. Katika dunia ya leo, ambayo imekuwa kama kijiji, tukiendelea na mfumo huu, basi majirani zetu, hosusani Kenya na Uganda ndio watakaokula kuku kwa mrija.
    Utamaduni wametupa utamaduni wa kuheshimu elimu.

    ReplyDelete
  16. Kwanza kwa kutoa hoja juu ya vikwazo vinavyomrudisha mtz nyuma kimaendeleo napenda kumpongeza. Pili nitachangia hoja 2 3 kuhusiana na mada hii. Lakini kabla ya kutoa hoja zangu nitatanguliza maoni yangu .
    Ni rahisi sana kwa mkazi wa nje ya nchi kunena eti watz wanapenda kupiga stori tu na wanategemea msaada kutoka kwa walionacho.
    Je wasema chochote hawahawa laiti wangeamka siku mmoja na kushinda na watu vijiweni wangeweza kugunda mengine. Kwa mfano kwa mfumo wa sasa unaosimamiwe na viongozi wa sasa hautoi fursa ya ajira. Kwa hiyo mtu huyu angetumia nafasi yake ya exposure kurudi tz na kuomba nafasi ya kuongoza tz na watu wake kujinasua kwenye mtego wa ujinga. Angeweza japo kuhakisha sheria za ardhi, kodi, na elimu zinabadilishwa kwa kasi zaidi. Pia huyu jamaa kama angeshinda vijiweni angejua kuwa hata kama options za kujiendeleza zinge kuwa nyingi za kumwaga, wadau bado watakuwa na wakati mgumu wa kuchagua kwa sababu mfumo wa uliopo sasa unatoa nafasi kwa chaguo moja tu. Yaani unatakiwa uwe unajulikana na unatakiwa kukubali kutoa chochote. Tatu, watanzania wanao shinda kijiweni wengi wao wanafanya hivyo kwa sababu hakuna umeme ofisini, foleni ya magari, na nauli za usafiri hazina mvuto wa kulipa. Na mwisho ilikumaliza hoja zangu nasema hivi kushinda kijeweni inafaida zaida kuliko kutoka jasho na kupoteza mtaji na muda ili usikae kijiweni.

    ReplyDelete
  17. huyo ni prof maji marefu nini mbonahaeleweki kama mjumbe aliyesema hapo juu hakuna uhusiano kati ya dual citizenship na tulipofika sasa hapa tanzania,anasema maendeleo yataletwa na watanzania wenyewe lakini kama raisi ana ruhusu mikataba ya wizi wa madini halafu,ana nyanyanya watanzania migoni (ie tanzanite merarani)halafu anawapa wageni,we prof unataka hao wachimbaji wadogo waende wapi kama sio vijiweni,jiulize kwanini wanakaa vijiweni sio kulaumu watanzania,kwa asilia binadamu wanapenda kufanyakazi,kazi ni heshima,hakuna mtu asiyependa kufanya kazi,wewe naona umeongea off point kabisa,mimi naamini maendeleo yanaletwa na viongozi kuwahamasisha wananchi ndo maana tunachagua viongozi,bila hivyo kila mtu angekuwa anafanya lake bila planning,kwa hiyo viongozi wapaswa watumie mamlaka tuliyowapa watunze rasilimali zetu,wahakikishe hazifujwi na mapato yanayopatikana yapelekwe kwa wanachi kama elimu,afya ,ajira na mengine mengi,kutokujua kiingereza sio hoja kwenye maendeleo kama tutaweza kutumia kiswahili chetu kwenye kupata maarifa kama science na teknologia inatosha tu,kuna nchi kibao wanatumia lugha zao kama china japan,korea na wameendelea vizuri tu,kwa hiyo nafikiri hao viongozi wetu ndo wabovu wanatupeleka kupaya

    ReplyDelete
  18. Fundi_mangungoFebruary 09, 2010

    Huyu ni Professor wa kiswahili, I wonder anajifanya anaijuwa siasa na uchumi! Ni miongoni mwa wale wanaodhani kujipendekeza sana kwa Kikwete basi huenda wakapata hata ubunge wa kuteuliwa!!! Nna mashaka na u professor wake! Na daima ntaendelea kuwa hivyo! Uwezo wake wakufikiri na kujenga hoja hauna tofauti na Baba yangu alieshia darasa la nne la mkoloni! Of coz sikutegemea kuskia mchango wa maana kuhusu uchumi kutoka kwa Professor wa Mofimu, virai, viima na viarifu (kiswahili), lakini nlitegemea angalau anyamaze au afunguwe blog afundishe watanzania kiswahili! Unapopiga kelele watanzania wanapiga soga wakati huna statistical data na wewe kama Professor si aibu hiyo, unatofauti gani na hao unaowalaumu (wapiga soga)...uliozungumza ni mazungumzo ya maandazi tu! Tanzania ina hasara sana kama ina Professors wa aina hii! Na kama huu ndo u prossor, mungu mie usinijaalie kamwe kuwa professor!

    ReplyDelete
  19. Prof hata mfanye kazi vipi kama hamna good GOVERNANCE itakuwa ni vigumu kuwa na maendeleo. Na hili sio tatizo la TZ peke yake bali ni afrika na nchi za dunia ya tatu kwa ujumla.
    Rushwa na ufisadi wa Viongozi wetu ni tatizo kubwa katika tawala zetu. Hope uko aware na kesi mbalimbali za recently kuhusiana na matumizi mabaya ya fedha za Umma ambazo wala hazitapatiwa ufumbuzi mojawapo kubwa ya former Governor. Kesi hizi ambazo wala hakuna watakaowajibishwa ni za miaka tu ya karibuni lakini tatizo hili limekuwapo muda mrefu especially baada tu ya kipindi cha Mwalimu.
    Wewe ni Prof nilitegemea utaelewa kwanini vijana huishia vijiweni. Inaanzia kwenye maandalizi shule na elimu duni inayotolewa kuwaandaa na maisha ya baadaye either kwa kuajiriwa au kujiajiri kama ni ufundi, kilimo, uvuvi, nk.
    Serekali kushindwa kuandaa vyanzo na mazingira mazuri ya ajira na uwezekeshaji. Kitu tu kama kuwa na barabara nzuri kuna rahisisha uwekezaji, Reli, Umeme, Maji, Simu nk.
    Ufanisi wa kazi kwenye taasisi za serekali kama TRA, kwani ukusanyaji kodi ndio pato la serekali. Kwa kifupi tu matumizi mazuri ya fedha na mipango mizuri ya maendeleo yana nafasi kubwa katika kuendeleza nchi.
    Wananchi nao wana nafasi kubwa katika maendeleo na nina imani kubwa kama watanzania wakipata nafasi ya kuwa na nyenzo wanafanya kweli. Mfano ni majumba au biashara zinavyofunguliwa watu wanapopata nafasi.
    Saa nyingine kukaa vijiweni, starehe au hata kunywa ni katika kupunguza stress za maisha. Wanasema mkaa bure sio sawa na mtembea bure maanake mtembea bure anaweza kuokota.
    Nategemea katika workshop zako utalenga kwenye kiini cha matatizo na sio kwenye matatizo yenyewe mfano kwanini hamjui kiingereza. Kwani mfumo wa elimu ya TZ hauujui? Research again “kwanini vijana hukaa vijiweni” nini nafasi ya serekali/viongozi na nini nafasi ya wananchi/wazazi.
    Please also refer to the following BOT Governor’s case, BOT’s Twin Towers, Kiwira Tan Power Resources, BAE, TANESCO’s Richmond, Mramba and Yona case, Parking na mradi wa mabasi Dar, na mengineyo mengi, wakati unawalaumu vijana.

    ReplyDelete
  20. PROFESA AMEFULIA huyu!!!!!umri umekwenda anatafuta pa kutokea.....kwikwikwikwi.

    ReplyDelete
  21. huyu ni profesa wa wapi kwanza? mbona hata makala yake haina mpangilio wa kiprofesa? halafu mada zinajichanganya. nchi imeharibiwa na uongozi mbovu na wasomi wasio tumia taaluma zao ipasavyo. wote mlipewa degree halafu mkapelekwa chuo cha CCM Kivukoni wapewa ujinga... acheni hizo mabadiliko ya kidunia lazima myakubali. Hata hao wafadhili wana urai wa nchi mbili itakuwa Tanzania?

    ReplyDelete
  22. Stay away from this MAN. His essay, simply put.....is mind stalling.
    Cha-pombe

    ReplyDelete
  23. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  24. Ngoja niandike kiswahili ili hata wasio na fursa ya kusoma ama kuandika kingereza waweze kunielewa. Hapa Prof. ametoa maoni yake kama Joseph Mbele na si vinginevyo. Hii ni fani yake ya uandishi na anaweza kuandika chochote anajosikia yeye. Hii ni ruksa kabisa. Basi mimi nilikuwa na haya machache ya kuuliza na kama Joseph Mbele atapata nafasi ningeomba atujibie ili na sisi tusikuwa na elimu au wazifa kama wake tuweze kufahamu.

    1: Serikali inaongozwa na nani? na nani anayetakiwa aweke miongozo iliyo bora ili wale waliovijiweni waweze kupata fursa ya kujiendeleza, wawe wamesoma au hawajasoma?

    2: Ni nchi gani watu walioendelea bila ya watu kukaa kwenye mabaa, kwenda kwenye sherehe bila ya hivyo kweli uchumi wetu ungeweza kwenda mbele?. Ingekuwa vipi kwenye viwanda vya bia na vinywaji laini Joseph Mbele? si vingefungwa watu wangapi wangekuja kuongeza idadi hapa kijiweni? Je wale wanajiajili wenyewe na kuanzisha biashara binafsi za huduma kwenye masherehe wakale wapi Joseph Mbele au wale waajiliwa wao ambao kwa mtazamo wako ni hawana elimu kabisa si wangetukaba humu njiani?

    3: Kama serikali haijaweka misingi mizuri ya lugha unadhani watanzania wanaweza kuja tu na kufundisha kiswahili? Nimeona kwenye profile yako unasema unapenda sana kufanya utafiti embu fanya utafiti ufahamu ni waingereza wangapi hawajui kuzumza Kiingereza? Na pale Uingereza hawazungumzi lugha nyingine yoyote zaidi ya Kiingereza. Hili sasa namwachia Prof. J. Mbele na si Joseph Mbele?

    4:Kuna watanzania wangapi wako nje ya nchi na wanauwezo mkubwa wa kuwekeza nyumbani na kuwapatia watanzania wenzao ajira, ila kwakuwa wanauraia wa nchi nyingine kwanini warudi nyumbani kwao wahudumiwe kama wageni? Kama ukitaka hilo nitakutajia kwa majina sawa Joseph Mbele.

    5: Na nchi ili iendelee ni lazima kuwe na matabaka kwenye elimu, uwezo wa kifedha na madaraka. Kama si hivyo itakuwa ni migogoro tu na kutakuwa hakuna anayeshindwa kushushwa chini matokeo yake matunda yanakuwa hafifu. Lakini lazima nchi iwe na watu wanaojua kusoma na kuandika na si lazima wafanye uliyofanya wewe. Badala tuweke elimu ya msingi na sekondari bure mnatoa. na si kutoa mabilioni ya shilingi kujenga nyumba ya kulala mtu mmoja halafu serikali inatangaza kila mwanafunzi aje na dawati lake na ada. Kwani kabla hajachaguliwa kwenye ile nyadhifa alikuwa analala nje? Kwanini msimwongezee ulinzi wa kutosha pale alipokuwa anaishi ili hizo fweza zikatumike pale zinapohitajika zaidi kwenye elimu ya msingi na sekondari?

    6: Nimeona kwenye blogu yako inaonesha uko Marekani nahisi ndipo unapoishi. Kwanini usirudi nyumbani Tanzania kwenye serikali safi,viongozi bora na yenye kujali wachangia uchumi wa nchi na kuwalipa mafao bora. Uliona nini Marekani kilichobora kuliko Tanzania? Usiseme umeitwa kufundisha unaweza kabisa ukawa kwako Lindi na kufundisha kutumia teknolojia si kuna ule waya umeshazambazwa Tanzania nzima?

    7: Joseph Mbele mwisho ningependa kujua wewe ni Prof wa mtaala upi hasa? Umeshanya jambo lipi la kipekee la kuendeleza taifa letu kwa juhudi zako mwenyewe bila msaada wa serikali ya Tanzania? Pia kama ulikuwa unafundisha Chuo Kikuu cha Tanzania kipi kilichokuondoa wakati bado taifa linahitaji wasomi walio wazawa?


    Mdau Mkweli

    ReplyDelete
  25. PROFESA BONGO HAKUNA AJIRA ULITAKA WATU WAKABEBE JEMBE WAKAVUNJE MSITU WAANZE KILIMO CHA MKONO?IAMBIE SERIKALI IACHE KUKARABATI MAJENGO KWA MABILIONI NA KUGAWANA MASHANGINGI YA MAMILIONI MIA MIA BADALA YAKE HIZO PESA ZINGETUMIKA KUWAELIMISHA WANANCHI NA PIA KUTENGENEZA AJIRA JAPO KWA WABONGO KADHAA ...HIVI KWANINI MAPROFESA WENGI HOJA ZAO ZINAKUWAGA NI HOHEHAHE..HAWAKO REALISTIC MTU HANA KAZI ULITAKA AJIFUNGIE CHUMBANI ALALE BWANA PROFESA???

    ReplyDelete
  26. Nitajitahidi nifike kwenye kwenye warsha Arusja, tena ni kipindi kizuri cha kuzunguka mbugani.

    Profesa sante kwa changamoto.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  27. professor ,
    before this article wewe ulikuwa mmoja kati ya wanataaluma ninao wakubali sana ,lakini umenishangaza unapokuwa against mawazo ya watu!! unapoandika article watu wana haki ya kupingana nayo ama kukubali lakini unavyolaumu ujuzi wa lugha au marekani wakenya wanavyochukua kazi za kufundisha kiswahili,MIMI NINA SWALI MOJA KWAKO WEWE HAPA MINNESOTA UMEWAHI KUMSAIDIA NANI AU KUTOA TAARIFA KWA UMOJA SOCIETY NAMNA YA KUPATA HIZO KAZI??? AU UNAAMUA KULAUMU TU ?wewe kama una ambition zako za kuwa mwanasiasa au kikwete akuone unamtetea,wape nafasi watu ya kutoa maoni yao.Hata wakiweka majina itakusaidia nini??

    ReplyDelete
  28. SWING THE DOOR OPEN AND LET ALL CON ARTISTS COME AND DO THEIR THING.

    ReplyDelete
  29. Hbari wadu na pia hesima yako Mzee Mbele,

    Mimi sijafuatilia habari za nyumbani kwa ukaribu sana. Ila hoja hii imenigusa na ningependa kuchangia machache. Mzee Mbele ameongea mengi katika hoja yake. Ila mimi ningependa kutoa kipaumbele katika eneo moja tu la hoja hii. Kama kuna mtu awe kiongozi wa nchi au mwakilishi wa jamii ya wa-Tanzania amotoa ksisingizio kuwa Daul Citizenship kuwa ndio chanzo cha ukosefu wa self esteem na elimu kwa ajili ya kushindana duniani, then nadhani mtu huyo atukosea na anapotosha jamii. Kwani mimi sidhani kama Dual Citizenship pekee inaweza kujenga kujiamini overnight. Ila kama mtoaji hoja hiyo alitaka koungelea Daul Citizenship kama platform ya kuruhusu wa-Tanzania kuwa na wigo mpana zaidi wa kujitafutia maisha, then nakubaliana naye kwa asilimai 9.99999% asilimia moja nakaa nayo mwenyewe.

    Kwako Mzee Mbele, asante sana kwa kuwa mkweli kuhusu tabia ya uvivu makaziani. Maana kuna watu wanakwenda lunch masaa manne, au kwenda kwenye warsha-makongamano-semina-trainig etc kila wiki. Tuache uvivu jamani. Njooni huku mjifunze. Huku watu wanalipwa kwa saa. Nenda lunch masaa manne utakuta barua yako mezani.

    Asanteni

    Mdau toka Stdney Australia.

    ReplyDelete
  30. DUH YAANI NIMESOMA TOKA MWANZO MPAKA MWISHO NMEONA KWELI WALIOANDIKA WOTE NI WATANZANIA, SIJUI TATIZO NINI?
    NI WAGUMU KUELEWA,HAWATAAKI KUAMBIWA WALA KUKUBALI UKWELI
    ALAFU ETI TUNATAKA MAENDELEO HAHAHAHAHAH NI SAWA KABISA NA KUTAKA KUJENNGA GOROFA HEWANI

    ReplyDelete
  31. MAONI YA WADAU SAFI SANA INAONEKANA WA-TZ WANAUELEWA MKUBWA KULIKO HUYU PROF. WA MOFIMU NA MASHAIRI YA SHABAN ROBERT ANAVYOFIKIRIA.WATANZANIA WA LEO PROF SIO WALE WA MIAKA YA 80'S WANAUELEWA MKUBWA,UPROFESSOR UNAWEZA KUWA NAO NDIO BUT INAONEKANA UMESHINDWA KABISA KUTOA HOJA YA MSINGI KUHUSU MATATIZO YA MTANZANIA LEO NA ULICHOHARIBU KABISA NI KUWA-DEFEND POLITICIANS.NEVER TRUST POLITICIANS COZ THEY WILL DO ANYTHING TO WIN THE WADANGANYIKA BALLOTS

    ReplyDelete
  32. Profesa Mbele na ndugu zetu wengine ambao mko US na sehemu nyingine nje ya Tz, mkiona fursa za kazi mfano kufundisha Kiswahili huko mlipo jaribuni kutoa links kwenye blog kama hii ili watz wajaribu.

    Nadhani wenzetu majirani wanafanikiwa kwa kupeana habari.

    ReplyDelete
  33. Jamani, mimi niliwahi kumsikia huyu mzee mwaka 2004 akisifiwa na Mtanzania mwenzetu mmoja kwamba huwa anakwenda Tanzania na rundo la vitabu. Pia alimsifia kuwa ni mwalimu wa Kiingereza hapa Marekani. Mimi, nakiri kabisa, kwamba sikujua kuwa huyu mzee ni mtu wa ajabu namna hii. Nashangaa hata uprofesa wake wa nini wakati hajui wapi aweke herufi kubwa na wapi aweke "hyphen" kwenye maneno yake.

    Cha ajabu ni kwamba huyu ni mwandishi sijui wa vitabu na pia mwalimu wa lugha, lakini hajui hata jinsi ya kuandika neno "Kiswahili."

    Ni ajabu na kweli kwamba anachanganya mambo mengi yasiyo na uhusiano kwenye mjadala mmoja bila mbele (kama lilivyo jina lake) wala nyuma. Wanaokaa na kupiga soga ni Watanzania walioko Tanzania ambao hawajadai uraia wa nchi mbili, sasa analaumu nini? Watanzania walioko nje hakuna hata mmoja anayepiga soga na si wote wanaodai uraia wa nchi. Kimsingi hakuna Mtanzania aliyedai uraia huo, kama atafuatilia. Kuna ubaya gani kwanza kama watu wakidai?

    Hii ni fedheha kwamba mtu anayejiita profesa anashindwa hata kupanga hoja zake. Nina hakika huyu mtu hayuko kwenye chuo cha maana hapa Marekani.

    Nimevunjika moyo kabisa na huyu mzee. Siwezi kamwe kujisumbua akili zangu kumuwaza huyu mzee. Hii ni aibu kwetu Watanzania. Eti Profesa mzima hawezi kuchanganua mambo na kujieleza, halafu analaumu nini sasa?

    Ama kweli Tanzania ni nchi ya dunia ya tatu; mpaka akili nazo?

    Tuna kazi.

    ReplyDelete
  34. Hao ndo wasomi wetu bwana,wanakurupuka tu,naona hapo lengo lake kubwa ni kumtetea Kikwete na serikali yake.Sidhani kama watanzani wanashinda vijiweni kama unavyofkiri,maisha ni magumu watu wanaamka saa 10 alfajiri kuwahi makazini.

    Pr. Mbele waulize watz wenzako wanaojua mambo,mtu unaende kulipia kodi hutapewa TIN hadi utoe chochote,then unaita watu wana mawazo finyu.Mzee acha kabisa.

    ReplyDelete
  35. PROFESA UMEWASHAMBULIA WANANCHI WA KAWAIDA KWA KUKAA VIJIWENI LAKINI MBONA UMEWAACHA WABUNGE WALIOKIGEUZA KIKAO KIKUU CHA NCHI KUWA KIJIWE CHA POROJO. NENDA RUDI BUNGE HUKUTANA MARA NNE HIVI KWA MWAKA LAKINI CHA AJABU HAKUNA CHOCHOTE CHA MAANA KINACHOENDELEA NDANI YA BUNGE HILO ZAIDI YA POROJO NA VITISHO VISIVYO NA UFUMBUZI, HAWA NDIO WABUNGE WETU WANAOTAKIWA KUANDAA MWELEKEO WA MAENDELEO YA NCHI SASA WA CHINI WATAKUWAJE? TANZANIA NI NCHI PEKEE KATIKA AFRIKA MASHARIKI NA KATI INAYODUMAA KIMAENDELEO NA KUSTAWI KWENYE MALALAMIKO YASIYO NA MSINGI.

    ReplyDelete
  36. KUNA BAADHI YA WADAU NAFIKIRI HAWAJAMPATA VIZURI PROF, ANACHOJARIBU KUONGEA YEYE NI UVIVU TULIONAO WATANZANIA NA HIYO NDIO MAIN POINT ILIYOPELEKEA HADI KUONGEA MAMBO YA KUTAKA URAIA WA NCHI MBILI....JAMANI HAMJUI KULINK ISSUES AU MNAJUSTFY UWEPO WENU NJE?

    ReplyDelete
  37. Jamani, kwani Prof. kaongea kuhusu uraia wa nchi mbili pekee? Mbona watu hawazungumzii mambo mengine? watanzania kushindwa kufundisha kiswahili katika vyou vikuu vya nje, poor education etc.

    ReplyDelete
  38. MIMI KWA KWELI KUNA POINT ZA PROFESSOR NZURI NA KUNA POINT ZINATAKIWA KUCHUNGUZWA.

    KWANZA KICHWA NDIO KIONGOZI WA MWILI NA SIYO MWILI KIONGOZI WA KICHWA HIVYO VIONGOZI NI MUHIMU SANA KATIKA KULETA MAENDELEO AMA WANANCHI WAO WANAKUWA SUPPORTIVE ONLY.

    PILI NI MUHIMU WANANCHI PIA WACHAGUE VIONGOZI WANAOWEZA KULETA MAENDELEAO NA SIYO SABABU YA KUHONGWA KIPESA MAANA VIONGOZI WANAWEKWA NA WANANCHI.

    TATUO SERIKALI NI MUHIMU ITENDE HAKI KWA KUBADILISHA KATIBA YA NCHI NA KUFUATA MFANO MZURI WA SASA ULIOKO NI WA AMERIKA TUKIATAKA TUSITAKE AMERICA NI MFANO MZURI DUNIANI HASA MFUMO WA SERIKALI NA UCHAGUZI. PIA KUNA SEHEMU FULANI HATA AMERIKA INATAKIWA KUFANYIWA MAREKEBISHO LAKINI SEHEMU KUBWA YA SHERIA ZAO NI NZURI MAANA VIONGOZI WENGI HUCHAGULIWA NA WABUGE AU WANANCHI NA RAISI KAZI YAKE NI KUTEUA JINA LAKINI FINAL SAY NI WAWAKILISHI WA WANANCHI AMABO BUNGE AU WANANCHI WENYEWE.

    NNE RAISI KATIKA KATIBA YA SASA YA TANZANIA KAPEWA NGUVU SANA NA HIVYO RAISI NI BANADAMU KAMA MTU YOYOTE ANAYO MARAFIKI HIVYO KWA KUWA SHERIA SIYO NZURI KUMCHUNGA YEYE NA WANANCHI ANAJIKUTA ANAMCHAGUA KIONGOZI SIYO KWA SIFA BALI KWA URAFI AU UNDUGU.

    TANO TUKIFUATA MANENO YA HAYATI BABA WA TAIFA KUWA KIONGOZI ASIWE NA BABA, MAMA, RAFIKI NA ADUI HAPO TUTAENDELEA MAANA UKISHAKUWA NA HAYO VIGUMU KUFANYA CHOCHOTE MAANA UNAKUWA UNATAWALIWA NA HAO.

    ReplyDelete
  39. Napendekeza Profesa akasome kitabu kinaitwa "Masaibu wa boboa". Kitamfumbua ajue nini hasa is the core of the problems Tanzania is facing now and where we actually dropped the ball.

    ReplyDelete
  40. Zungu Wa MbiziFebruary 09, 2010

    Nimekuwa nikisomasoma makala za Profesa Mbele pale Kwanza Jamii kwa muda mrefu sasa. Ninasikitika sana kuona anavyoshindwa kupambanua mambo yanayohusu jamii.Siku zote amekuwa kinara wa kumtetea JK bila kueleza cha maana alichokifanya....Na hii hoja ya hapo juu ndio kabisa imenifanya hata mimi nianze kuhoji kuhusu Uprofesa wake...dunia ya sasa imebadirika sana tofauti na ile ya miaka ya 70 au 80,inapaswa aelewe kuhusu hilo...Nimeanza kupata mashaka kuwa uhenda huyu profesa ni kibaraka wa uozo uliopo katika serikali ya Tanzania!!

    ReplyDelete
  41. Ukitaka kujua watanzania jinsi tulivyo angalia maoni mengi katika mada hii, baada ya kujadili hoja zilizotolewa na profesa wameanza kumjadili yeye mwenyewe, na hapa ndio nakumbuka usemi ule maarufu kwa kimombo
    “Great minds discuss ideas; Average minds discuss events; Small minds discuss people.” -Eleanor Roosevelt

    ukweli ni kwamba utamaduni wa kusoma vitabu na kukaa kujadili hoja za maana haupo kwa watanzania wengi itakushangaza hata kwa wale wanaoitwa wasomi jinsi wasivyokuwa na muda kabisa wa kusoma vitabu lakini cha ajabu muda wa kukaa baa kunywa pombe na nyama choma haukosekani karibia kila siku, matamasha ya pombe yamejaa kila mahali kila mwisho wa wiki lakini jaribu kufanya utafiti kama kuna matamasha ya watu kusoma vitabu kama utapata ni moja au mawili kwa mwaka mzima, na ukijaribu kwenda kuangalia mahudhurio unaweza ukatoa machozi.hauwezi ukachangia na kujadili hoja zilizoibuliwa na profesa kama magazeti unayojua kusoma ni magazeti ya udaku, na ukiwasha runinga unachoangalia ni miziki na ukijitahidi sana ligi ya uingereza pekee, utaishia tu kusema profesa amefulia, kwa sababu hicho ndicho kilichojaa katika kichwa chako. kama wakenya tu hapa karibu wanatupeleka puta kiasi hiki, Tanzanite iko kwetu lakini wao, wanaongoza kwa mauzo,Mlima kilianjaro wanatangaza kuwa uko kwao, kazi za tingatinga tunasikia wakenya wanazichangamkia, wakati tingatinga ni mtanzania na kadhalika, tunaweza kushindana na mataifa yote duniani katika ulimwengu ambao unakuwa ni kama kijiji kimoja? Jambo la kushukuru ni kwamba wapo watanzania wachache ambao wanaliona hili na kulifanyia kazi,kwa kuwa siku zote mabadiliko yanaanza na mtu mmoja.

    ReplyDelete
  42. Hii makala haikuanzia hapa ni mwendelezo wa makala aliyoitoa mwanzo na hapo Prof alikuwa anajibu hoja ya mtu aliyesema kuwa watanzania walioko nje wanashindwa kuwekeza TZ kwa sababu ya kukosa dual citizenship, wakati sio ukweli tatizo hapo ni mitaji. Hilo moja.

    Pili amezungumzia utendaji kazi wa watanzania hasa katika mashirika na ofisi za serikali kuwa umejaa ubabaishaji. Nani anapinga hapa? Nani hajui utendaji wetu wa kazi ulivyo ukiwatoa wale wanaofanya kazi kwenye kampuni binafsi.

    Na majority walomshambulia Prof ni hao hao culprits wameumwa na ukweli uliosemwa hapo, ni mara ngapi unakwenda ofisini uhudumiwe badala yake unakuta mtu wa kukuhudumia yuko busy na simu? Au anablogu.

    NI WANGAPI HUMU WANABLOG BAADA YA SAA ZA KAZI UKITOA WATZ WANAOISHI NJE WENYE ACCESS NA INTERNET 24 HOURS? HIVI SI NDIO VIJIWE VYENYEWE HIVI? SASA MNABISHA NINI?

    Mswahili

    ReplyDelete
  43. Profesa!! Kushambulia wananchi ni sawa, lakini Ungeanzia Juu Kwanza au sio. Huko juu kunahitachi ukarabati usio wakawaida KUMEOZA!!

    Tungekuunga mkona asilimia 100 kama ungeanzia Juu, au una ajenda yako na wewe??

    Rudi nyumbani uishi na sisi, tunahitaji utaalamu wako, uungane mikono bega kwa bega na waalimu wenzako, kwa maendeleo ya kesho, usitupigie TARUMBETA TU, rudi nyumbani utuonyeshe mfano, tupigane vita ya ujinga, kwanzia Juu kwanza.

    Ahsante.

    ReplyDelete
  44. mimi nilishaacha kusoma article za prof mbele siku nyingi sana, huyu jamaa siku zote yeye huwa ni mwamvuli wa JK, nadhani hata yeye ameona ambavyo inakuwa ngumu kumtetea JK na utawala wake na ndio maana wengi hawajamuelewa ktutokana na kuruka ruka ukweli halisi

    tanzania tunachokihitaji ni mazingira bora ya kazi kutuwezesha kusonga mbele ambayo yapo nje ya uwezo wetu(external factors) ambayo yapo chini ya serikali na mwananchi hana la kufanya, mf kilimo,bei ya mazao kupangwa na serikali,
    rushwa,mfumuko wa bei nk

    ReplyDelete
  45. MADELA WA-MADILUFebruary 09, 2010

    Professor Mbele, Heshima mbele mkuu mwenzangu.
    Kama una nia ya kutumwagia matusi sisi akina MADELA WA- MADILU njoo pale kwenye jamvi.

    Wote tuko hapa Marekani tunaganga njaa, shule tumepiga kisawasawa lakini si wote shule zetu zinafanana na kufundisha kiswahili

    Hesabu za majoka (Calculus)na Ngeli wapi na wapi???

    mambo uloongelea(ukiondoa matusi) yanaweza kuwa na ukweli mwingi yakijadiliwa kwa kina katika umoja wake. Kwa kujadili kiujumla jumla na kimchanganyiko kwa namna yako umeshangaza umma na pengine hata kuupumbaza. Kwa mfano Hata hao Wakenya unaotukoga nao wamekumbatia Uraia wa nchi mbili,na sababu za kuukumbatia si kuharakisha maendeleo ya Kenya kisa gani kutuzodoa sisi Watanzania hasa tuishiyo Marekanani ikiwa ni pamoja na wewe mwenyewe??

    Kuficha majina,Wengine tunaficha majina kwa sababu Baba na Mama zetu ni watumishi ya serikali, hivyo usongo tuutoao hapo JamiiForum utawaathiri wazazi wetu kuliko ukweli kwamba tunaficha nyuso zetu.
    Kwanza Internet siyo siri.
    Pili, tunajificha au hatujifichi je hoja zetu ni makini?
    Kwa nini umeamua kupambana na nyuso zetu na siyo hoja zetu?

    Pamoja na kuweka uso wako wote na mawani hadharani bado woga haujakutoka. Unajipendekeza kwenye system kijumla jumla huku ukiweka lensi za mbao machoni na kutoa nusu ukweli huku ukimaanisha ni ukweli ulokamilika kwamba matatizo ya Tanzania ni uvivu wa wananchi; na si ubathirifu na Ufisadi wa viongozi wetu unaolindwa kwa taratibu mazoea na ukiukwaji wa sheria na haki za binadamu.

    Kama kweli wewe ni bingwa wa hoja bila matusi tafadhari tuonane pale JamiiForum, huko hapendwi professor wala umaarufu wake. Inapendwa hoja tu.

    ReplyDelete
  46. Lakini hii mada ya uraia wa nchi mbili si tulishaijadili na nilitoa wazo la "diaspora visa" ambalo halikupingwa kwa hoja?

    Kama mtanzania yeyote wa nje ya Tanzania atapata "diaspora visa" yeye pamoja na familia yake; na kama hii visa itampa haki zote ambazo anazipata mtanzania aliye tanzania, sasa uraia wa nchi mbili wa nini tena? Kuna kitu gani kingine unachokitaka kwa kutumia passport ya Tanzania ambacho huwezi kukipata kwa kutumia "diaspora visa"?

    Lengo la "diaspora visa" ni kuzuia wasiokuwa watanzania (wazungu) kujifanya watanzania ili kuihujumu nchi.

    Narudia. Mimi binafsi siyo mshabiki wa uraia wa nchi mbili kwa kuogopa kwamba wazungu pia watauchukua uraia wa Bongo, na nilitoa mfano wa kibera kenya na wazungu. Mzungu mmoja kenya (mkenya/muingereza) anamiliki ekari 48,000 za ardhi ya kenya analima kunde kuwauzia asda, tesco na wall-mart; wakati wakikuyu milioni moja wanaishi katika eneo lenye ukubwa wa sawa na viwanja sita vya mpira.

    Amgalieni ardhi wanazomiliki wazungu, Kenya, Zimbabwe, Namibia, Botswana, South Afrika; na nchi zingine za afrika zenye wazungu.

    Mimi binafsi nawaogopa wazungu, kama historia yetu na wazungu inavyoonyesha, hii tamaa ya uraia wa nchi itawatengezea watoto wetu wa vizazi vijavyo mapigano kama yaleyale waliyopigana akini oliver thambo na walter sisulu.

    Tuache kujifikiria sisi wenyewe na tuanze kuifikiria nchi; kama mdau mmoja hapo juu aliposema "kuna ubaya gani kwa watoto wangu kuwa na uraia wa nchi mbili?" Jee umewahi kujiuliza kwamba kuna uzuri gani kwa Tanzania kuwa na watanzania ambao "their first loyalty" siyo Tanzania?

    Mdau, Scotland

    ReplyDelete
  47. Mdau wa Scotland,

    Nakubaliana na wewe kuwa wananchi wa Kiafrika lazima wapewe ardhi nao pia walime. Lakini kwa bahati mbaya, kuna matatizo madogo madogo ambayo yanamyima Mwafrika kusaidia uchumi wa nchi yake na mwenyewe vile vile:

    1. Elimu. Kama huna elimu ya ulimaji wa kisasa huwezi kuzalisha kwa wingi. Wanakijiji wengi wanazalisha kidogo na wanakula kidogo. Kuuza kwa wingi inatakiwa elimu na fedha.

    2. Gharama za ukulima. Tena tunarudia katika fedha na umasikini pia. Hata kama utammpa ardhi kubwa Mwafrika, mazao yataoza kwa kuwa usafiri ni mgumu. Tanzania haizalishi kwa wingi kwa kuwa siasa za Ujamaa umempa kila mwanakijiji ardhi ya kulima. Kuuza mazao kwa wingi nje inatakiwa tajiri amiliki ardhi kubwa. Kama Watanzania hawapo tayari kuwapa watu ardhi kwa wingi, basi hatuwezi kulima kwa wingi, hatuna uwezo.

    3. Ufisadi. Kumpa Mwafrika ardhi haimalizi njaa. Mugabe kawapokonya ardhi wazungu lakini kawapa ndugu zake na mawaziri wake. Sasa tunaona Zimbabwe imetoka katika nchi inayozalisha na kuingia katika umasikini na waZimbabwe kukimbia Afrika Kusini kufanya kazi. Ardhi ambaye mzungu alikuwa anamiliki sasa imekaa na kuoza.

    Mimi binafsi pia sipendelei wageni wamiliki ardhi yetu, lakini katika miaka ya sasa, hatuwezi kuwanyima. Hasa kama tutaingia katika WTO na umoja kamili wa EAC. Pia, ni bora kwa ardhi itumike na watu kidogo lakini nchi inalishwa na serikali inapata mapato ya fedha za kigeni kuliko ardhi wapewe wanakijiji masikini ambao hawana uwezo wa kulima kwa wingi na kutumia ulimaji wa kisasa kutokana na elimu yao ndogo.

    Pia, tusikimbilie sana katika kilimo kujafuta utajiri, kwa kuwa mazao hayana soko sana kuliko uzalishaji wa magari, mashine mbalimbali za viwanda na kadhalika. Hamna hata nchi moja inayozalisha mazao kwa wingi mno na kutajirika.

    Mbongo

    ReplyDelete
  48. Jamani kumbe mtu akisoma mpaka akafikia ni klass ahead anafutika mawazo. Sasa hoja ya uraia wa nchi mbili inasaidiaje aconomi tekinologi edukation elimu. Anataka kutuambia hao waliopata maendeleo ni kwa ajili ya hiyo Duo cetezenshepu. Profesa naona uende ukanyoe ndefu zako kwanza kabla ya yote. Huna dola.....

    ReplyDelete
  49. kama mdau alivyosema hapo juu profesa anaongelea symptoms badala ya kuangalia kwanza chanzo cha ugonjwa. Kama hawa ndio maprofesa wetu ambao upeo wao wakuelewa unawaonyesha kuwa hakuna matatizo kwenye leadership ila ni wananchi wenyewe, basi kazi ni kubwa sana.

    Profesa hauna tofauti na yule waziri fulani aliyesema watanzania wanapenda kutumia pesa zao kwenye sherehe etc badala ya kuzitumia kununua madawati na kujenga visima vya maji! Kama ndio hivyo sijui responsibilities za serikali zitakuwa ndio zipi..

    Pia sijaona sababu ya wewe kuingiza hoja ya uraia wa nchi mbili kama the main theme ya hii article ilikuwa ni uzembe, uvivu, kukaa vijiweni, kutokujiamini, pamoja na uwezo mdogo wa akili na elimu. uraia wa nchi mbili tayari unawahusu sana watu ambao wako nje au waliopata nafasi ya kukaa nje na tayari wana uraia wa hizo nchi, na ningependa kufikiri kwamba mpaka wameweza kupata uraia wa hayo mataifa makubwa ni kwamba wameshughulika kidogo. watu hao tayari wanashindana na watu wa mataifa mbalimbali huko nje waliko. Pia ni asilimia ndogo sana ukilinganisha na audience unayotaka ku-target. Hata hivyo simaanishi kuwa watu walioko nje ni bora kiupeo au kielimu kuliko wengine.
    Kwa hiyo profesa kama wewe audience yako ni watu walioko nchini (e.g. kama itakavyokuwa julai 3 Arusha), please drop issue ya uraia wa nchi mbili. Kwani hii ni debate nyingine kabisa. Halafu profesa tatizo lingine ni jinsi un avyotumia lugha kuchambua hoja. Naelewa lugha inaweza kuwa ngumu hata kama ni lugha yako ya kuzaliwa (hata wewe mwenyewe unayakubali hayo). Kwa kipimo chako cha elimu profesa ungetakiwa uepuke na maneno kama 'akili finyu'

    Hata hivyo kuna mambo ambayo umesema hapo profesa ambayo yana ukweli ndani yake na inabidi yashughulikiwe. Tatizo ni jinsi ulivyoipanga hoja na pia mtazamo wako kuhusu leadership ya nchi.

    Tafaddali profesa haya ni maoni tu, usije ukasema watanzania hawapendi kuambiwa ukweli.

    k

    ReplyDelete
  50. Fundi_mangungo una matatizo...mbona unadharau sana wataalamu wa Kiswahili. Kwa vile ni Kiswahili? Kwa vile ni lugha? Kwako wewe Mchumi, Mathematician au MD ndiyo msomi. Nimeshaona wote hao na wengi wao ni "wajinga" kabisa katika mambo ya dunia.

    Prof. Mbele hawezi kutoa maoni yake kwa vile ni Profesa wa Kiingereza?

    Watanzania HATUTAENDELEA!!!!!

    ReplyDelete
  51. HII INAHUZUNISHA!!!!!!!

    ReplyDelete
  52. Hapa kwa Michuzi pia unaweza kuchukulia kwamba ni Kijiweni. Mahali tunapokuatana kubadilishana mawazo, kupeana taarifa, gossiping kucheka au kulia. Tofauti tu hatukutani physically. Vijiwe viko vya aina tofauti mfano kile cha the utamu kilichofungiwa kitazungumzia mambo yake. Hapa kuna heshima. Hivyo kama ulikuwa hujui karibu kijiweni.

    ReplyDelete
  53. "You can be a fool even you go to school".May Allah bless Tanzania

    Mjusi

    ReplyDelete
  54. Napendekeza usifanye semina au workshop maanake uko so much out of reality. Na ideas zako itakuwa ni kupotosha vijana.

    ReplyDelete
  55. Prof, Kuhn-Tucker conditions unazijua wewe?? super and submodularity je?? je vipi kuhusu maximum principle na calculas of variations (CV). niambie unawezaje kujua iwapo a twice differentaible function ni concave au ni convex!! baada ya hapo naomba u-state transversality condition ya Infinite Horizons model!! Ukimaliza hapo nieleze matumizi na umuhimu wa ARCH and GARCH models especially as applied to high frequency financial data, kabla ya kumalizia na maelezo kuhusu procedures zilivyo katika ku-conduct augument dickey fuller test (ADF) na short comings zake.
    Ahsante

    ReplyDelete
  56. mimi nataka niulize watu wanaoshabikia dual citizenship swali moja, whats the big deal about it? mimi nimekuwa naishi uingereza kwa muda wa miaka 15 na nasafiri sana tu kwenda nyumbani Tanzania, katika miaka hiyo 15 sijaona umuhimu wa kuukana uraia wangu wa Tanzania. sasa hawa diaspora wanaotaka urai wa nchi mbili watueleze kwanza kuna umuhimu upi sana wakuchukua urai wa nchi wanazoishi sasa na pili kwanini wameukana uraia wao wa kiTanzania? wakishatueleza hayo then ndio twende tuangalie faida za kuwa na huo urai wa nchi mbili. mdau mmoja kaongea kuhusu watoto wake, navyojuwa mimi ni kuwa watoto under 16 wanaweza kuwa na urai wa nchi mbili mpaka hapo watakapo kuwa matured kisheria kuamua urai upi wa kuufata. ieleweke hapa kwamba mie nachotaka ni kujuwa sababu kuu zinazotufanya sisi watanzania tutake urai wa kitanzania na wa nchi nyingine ni kwa sababu zipi?

    ReplyDelete
  57. je wachina nao tuwape urai wa kibongo pia? maana wanaingia kwa fujo bongo, mpaka uswahilini wapo. Mwalimu aliona mbali kukataa mambo haya, tupitishe sheria ya uraia huo halafu tuwe tayari kuwa na rais mwenye asili ya kichina, kikongo, kizungu na asili yeyote ile 2025. tupo tayari wabongo kwa hilo ama tunaangalia upande mmoja tu wa shilingi jama?

    ReplyDelete
  58. Nanukuu.....
    Prof, Kuhn-Tucker conditions unazijua wewe?? super and submodularity je?? je vipi kuhusu maximum principle na calculas of variations (CV). niambie unawezaje kujua iwapo a twice differentaible function ni concave au ni convex!! baada ya hapo naomba u-state transversality condition ya Infinite Horizons model!! Ukimaliza hapo nieleze matumizi na umuhimu wa ARCH and GARCH models especially as applied to high frequency financial data, kabla ya kumalizia na maelezo kuhusu procedures zilivyo katika ku-conduct augument dickey fuller test (ADF) na short comings zake.
    Ahsante
    ====================

    Huyu naye ni walewale mbumbumbu walioenda shule lakini hawajaelimika. Hata kama unayajua haya madudu SO WHAT? Yanamsaidia nani? Ninyi ndio hawa hawa kwa kutumia mafomyula yenu haya mnakwenda huko mnatamba eti uchumi umepanda kwa asilimia 6 wakati maisha ya wananchi yanazidi kudidimia. Kila mtu hapa akianza kuweka ma-jargon ya taaluma yake tutafika? Huu ni upuuzi wa kiwango cha juu kabisa....

    ReplyDelete
  59. jamani ningemuomba profesa aarudie kuandika nakala kama hii kwa makini..cheo cha uprofesa yeye anayaamini aliyoandika..kwahiyo asilaumiwa...ana preach what he believes.na kama kuna wanafunzi basi unahaki yakumkosoa.profesa ningependa kukufahamisha kitu..inawezkana marker pen umezoea kushika..lakini ni hivi...kila unayemuona investor basi kuna vitu muhimu anaviangalia kabla ya kutia mono wake kwenye "mtungi". stability and security...mambo ya dual citezenship na mambo yako soo deep kiasi umakini unatakikana.kwenye hayo kuna advantages n disadvantages...na sio yote utafaidika...KWAKUMALZIA NINGEPENDA KUSTRESS YA KUWA..VIONGOZI WETU WA TZ WANAOGOPA SANA JAMBO HILI KWANI NDIO LLITAKALOWAKOSESHA RAHA SANA KWENYE UFISADI WAO..KIVIPI???...TO BE CONTINUED.......

    ReplyDelete
  60. Jamani wote nyie na profesa wenu Tisa, kumi ni huyo anoni wa Tue 07:14 p.m haha ha ha kweli humu kwenye hii blog kuna watu tofautitofauti na mawazo tofauti. wewe anoni ni hayo madude yamekupindisha kichwa umeamua uwatese watu hapa au?? kwikwikwikwi koh koh koh!!! ni kwa mtu aliyesoma sana advanced economic analysis courses tu ndo atayaelewa hayo vinginevyo watu hawatajua umeongea nini hahahahaha, aisee umeniacha mdomo wazi na umenikumbusha mbali sana shule hiyo ya uchumi tulipigwa pale london school of economics kwenye advanced mathematics for economists na time series econometrics ilikuwa hali ngumu, hayo madude uliyoyaweka hapo hayafai, leo profesa akisoma maswali yako na degree zake za kiswahili atabaki akiona nyota tu. mh nimecheka sana leo wewe kiboko. unasoma wapi au umeshamaliza?? na wewe ulipita LSE au? pole sana kama bado unayasoma hayo manondo mie nashukuru nilipita salama na sasa nakula bata tu nyumbani tz.

    ReplyDelete
  61. profesa ameongea pointi nyingi,moja ya maana nyingi pumba!!!!
    Kwanza inaonekana prof ni mgeni kwenye nchi yake(kama bado ana uraia wa Tanzania yetu), kama angekuwa mwanajeshi ningesema ni raia anaesubiri taarifa za magazeti ya serikali kuhusu kinachotokea vitani na sio foot soldier anaeona hali halisi, anajua kidogo sana kuhusu kinachoendelea ardhini.
    1. Nilitegemea kama Profesa atoe statistical datas, wangapi wapo vijiweni, wangapi wakulima, wangapi wefanyakazi wa ofisini, wangapi watawala kwa asilimia.
    2. Atuambie average income ya segment za watu hao hapo juu, ili tuweze jua watu asilimia ngapi ni wazalishaji Tanzania.Maana bila hizo data huwezi sema majority wanakaa vijiweni kwa facts zipi?
    3. Pia aongelee matumizi ya wafanyakazi wa serikali na posho wanazolipana ni asilimia ngapi ya pato la taifa kutoka nje na ndani ya nchi. Na vipi linatuathiri, bila kusahau kwamba asilimia kubwa za ofisi za serikali ni watumiaji na sio wazalishaji katika pato la taifa.
    4.Atoe suluhisho la rushwa,urasimu,ufujaji wa mali za umma n.k bila kuihusisha serikali kama ambavyo anaelekea kusema kwamba serikali na rais si suluhisho la haya matatizo.

    Hayo ni machache yapo mengi ya kufanyia tafiti.Na ndio maana ya uprofesa, si kutoa mitazamo isiyojengwa na facts zozote.

    Conclusion:Profesa inaonekana una majibu rahisi kwenye matatizo magumu, vitabu vimepindisha analytical skills zako badala ya kuzisharpen, welcome to the real world.

    Jambo pekee la maana uliloongea ni kwamba ofisi za umma kuna uzembe na uvivu mwingi japo si zote,lakini hiyo haimaanishi ni watanzania wote kwa ujumla wao.

    Computer Analyst

    ReplyDelete
  62. Haya KaMichuzi naona oni langu umelibania, Naona nilichemsha sana, lakini ni ukweli unaujua sana au sio?!!!

    ReplyDelete
  63. Mdau wa Scotland,

    Some of us missed the original information about “diaspora visa”.
    Can you elaborate on how this “diaspora visa” would work?
    What are the pro and con arguments for and against “diaspora visa”?

    Mdau, USA

    ReplyDelete
  64. wanaoshabikia uraia wa nchi mbili wa nini? mtu ukiwa nchi za nje kiuhalali unaukanaje uraia wako wa awali,wapigania uhuru waliokuwa nchini wengine walikaa miaka mingi, hawakuomba uraia nchi mbili hao waliokuwa wanawataabisha huko nchini kwao wengi walikuwa ni raia nchi mbili, tuangalie wanayotaabika nayo Zimbabwe,Namibia na South Africa hata jirani zetu Kenya, uraia wa nchi ni pamoja na kuwa na haki ya kumiliki na kujivunia ardhi na raslimali za nchi hiyo

    ReplyDelete
  65. KWANZA NAKUPONGEZA PROFF KWA MAWAZO YAKO MAZURI SANA.ILA HILI TANZANIA ISONGE MBELE ,TUNAOMBA RAIS HAWE WAZI ,NA AKEMEA NA KUKAMATA WANAOHUJUMU UCHUMI NA KUWANDOA NA KUWAWEKA KWENYE KTK OFISI ZA SERIKALI WATU WANAOLETA MAENDELEO,SIO WATU WANAOJIFANYA WAFALME.WANANCHI WANATAKA WAONE KUWA HAKUNA FISADI NA HUTAMTETEA MTU HATA MMOJA HATA KAMA NI RAFIKI YAKO NA MWISHONI WATANZANIA ,TUSIKAE VIJIWENI ,TUANGALIA MFANO KWA VIONGOZI WETU NA KUFANYA KAZI KWA BIDII.NA TUWE NA VIKAO KUONA NANI HAFAI NA TUSISHABIKIE MTU FISADI KWA USHABIKI TU.TUMSIFU MTU KAMA ANAFANAYA MAZURI NA TUMLAUMU NA KUMTOA KWENYE WAZIFA WAKE MTU KAMA AMEFANYA KOSA.SASA HIVI TUWEENDE KWA KASI KWANI TUPO NYUMA SANA.UTAONA RAIS ANACHEKA NA MTU AMBAYE HATA YEYE ANAJUA AMEFANYA KOSA SASA UNAFIKIRI HIYO INALETA PICHA GANI KWA WATANZANIA.?MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  66. Professor nakubaliana na wewe kwamba watanzania tuna ufinyu wa mawazo na hiyo inajionyesha wazi kwenye mambo mengi, angalia mfano wa viongozi mafisadi bado tunazidi kuwapigia kura ili waendelee kutuongoza, ila kitu ambacho umeshindwa kueleza nini kimesababisha huu ufinyu wa mawazo, sababu ni nyingi sana na kama wewe ni professor wa ukweli basi bila shaka utakuwa unazijua, ila ulichofanya wewe ni sawa na kuwalaumu watoto ambao wametelekezwa na wazazi badala ya kuwalaumu wazazi waliotelekeza watoto. Mdau Mfulukutwa

    ReplyDelete
  67. Naona unknown wa saa 7:14 amesahau kunywa SSRI zake. Nimecheka sana, mpaka watu wanadhani na mimi nimechanganyikiwa!

    ReplyDelete
  68. Mdau wa USA; "diaspora visa" ni kitu ambacho mpaka sasa hivi hakipo. Ni wazo nililolipendekeza kama njia mbadala "alternative solution" kwa uraia wa nchi mbili. Ni kitu ambacho serikali inaweza kukianzisha ili kuwapa wananchi wa nje "diaspora" urahisi wa kuchangia maendeleo ya nyumbani.

    Ili uipate visa hii, inakubidi uwe umezaliwa Bongo, au wazazi wako wawe wamezaliwa bongo. Visa hii iwe na nguvu za kumpa "diaspora" anapokuwa tanzania haki zote anazozipata mtanzania aliye tanzania.

    Pro:
    1. Itazuia watu kama Karl Peters kujifanya wabongo ili waweze kuihujumu bongo kwa manufaa ya nchi zao za kweli.
    2. Itaondoa sababu ya kutaka uraia wa nchi mbili.


    con: Hakuna

    Mdau, Scotland

    ReplyDelete
  69. HUTU PROFESA ANASHINDWA KABISA MASKINI YA MUNGU KUJUA KUWA KWA NCHI ZA KIAFRIKA AMABAZO HAZINA DEMOKRASIA KAMA HAPA KWETU UIMARA WA RAISI WA NCHI UNACHANGIA SANA MAENDELEO YA NCHI TENA KWA ASILIMIA ZAIDI YA TISINI (90%). KAMA RAISI HAWEZI WEKA WATU WA MAANA WENYE UCHUNGU NA NCHI NA KULEALEA MAMBO YA RUSHWA,WIZI,KUFANYIZIANA NA UFISADI HATA MFANYE KAZI VIPI MTAWANUFAISHA WACHACHE TUU NA HAMTAONA MANUFAA. HAKUNA MTU ANGEPENDA MAMBO YA URAIA WA NCHI MBILI KAMA HALI INGEKUWA INAVUTIA TANZANIA.
    Mzozaji

    ReplyDelete
  70. WATZ TUWE WASTAARABU BASI KWA TAALUMA ZA WENZETU. KUMPONDA MTU KWA VILE AMESOMEA LUGHA, IT DOESN'T MAKE AT ALL.

    NAPENDA NIAMINI KWAMBA WATU WA AINA HIYO NI WANAFUNZI AMBAO BADO WANAENDELEA NA MASOMO BUT THAT CAN'T BE AN EXCUSE. JIFUNZENI KUJENGA HOJA ITAKUSAIDIA WEWE MWENYEWE HAPO UNAPOSOMA AU UNAPOFANYIA KAZI.

    KUSOMEA LUGHA HAIMAANISHI KWAMBA MHUSIKA LABDA NI KILAZA AU ANA UWEZO MDOGO WA KUELEWA, IT'S A CHOICE.

    WATZ HAWATAKI KUWA THINKERS, PEOPLE JUMP ON THINGS. I WANT TO BELIVE THAT THIS BEHAVIOUR IS EXTENDED TO THEIR WORKING PLACES, SHAME!!

    HEBU ANGALIA COMMENTS HAPO JUU ZAIDI YA NUSU NI WATU AMBAO WAMECHEMSHA!! THEY DIDN'T UNDERLINE THE ISSUES DISCUSSED BY THE PROF.

    NDUGU ZANGU, TUNAFULIA VIBAYAAA!!

    ReplyDelete
  71. MNH!WATU BWANA!

    KUSOMA HAMUWEZI?HT PICHA PIA HAMUONI?ITS SIMPLE...

    HUO MUDA MNAOPIGA KELELE KUHUSU DUAL CITIZENSHIP..BLAH! BLAH!....ALICHO-SUGEST..UNGEELEKEZWA KWENYE JITIHADA BINAFSI,KUJIKOMBOA NA UMASIKINI!,,UKIWA NA URAIA HATA WA NCHI KUMI,KM HUNA ELIMU ITAKAYOKUWEZESHA KUPATA KAZI NA KIPATO KIZURI,,,HUO URAIA UNABAKI KNY MAKARATASI TUUU...HAUNA FAIDA KWAKO!..PERIOD!!....NIKIWA KM MPIGA BOX MSTAAFU..I KNOW WHAT YOU MEAN PROFESSOR!..NIMEKUJA HAPA 'BOXINI' SIX YEARS AGO,NIKAJIKITA KNY MABOKSI...KAMA HUO MUDA NINGEULEKEZA KNY SHULE SASA HV NINGEKUWA MBALI SANA!....SASA NIKIPATA HIO DUAL CITIZENSHIP ITANISAIDIA NINI,AU ITASAIDIA NINI NCHI YANGU KAMA SINA SHULE????..ON THE OTHERHAND,NIKISOMA NINA UHAKIKA WA KUPATA KAZI NZURI ITAKAYONIWEZESHA MIMI NA FAMILIA YANGU..TUISHI COMFORTABLE...NA PIA NIKISEMA NIRUDI NYUMBANI,PIA NITA-TRANSFER SKILLS/KNOWLEDGE...AMBAZO PAMOJA NA MAMBO MENGINE ZINGEWEZA KU-BOAST HIO ECONOMY YA TANZANIA...

    SIJAPENDA PROF,ALIVYOPAINT PICTURE HAPA WA-TZ NI WATU WA KUKAA VIJIWENI,SABABU I KNOW FOR A FACT KAMA SIO SERIKALI YETU KUTOKUWA NA MIUNDOMBINU THABITI,THEN LABDA MAJORITY...WASINGEISHIA KNY HIVYO VIJIWE!!!...NAJUA WATU KIBAO NA TAALUMA ZAO..AMBAO WANASOTA,,,DAY IN DAY OUT,HIIVI HAO WAKISOTA BAADA YA MUDA WAKAISHIA VIJIWENI..UTAWALAUMU???WAMEPENDA KUKAA AMA THE WHOLE SYSTEM IMEWA-FAIL??
    AT THE SAME TIME SIE WA-TZ NI WATU WAVIVUUUU!...LAZIMA TUSEME UKWELI!..UKIENDA NJE YA NCHI HASA HUKU UGHAIBUNI NDIO UTAJUA NINI MAANA YA KUFANYA KAZI!,TO SUSTAIN A LIVING...YOU HAVE TO WORK MONDAY TO FRIDAY,8 HOURS A DAY...WANGAPI WANAFANYA HIVI??WATU WAPO MAOFISINI KAMA HAWAPO VILE!?...NIMEONA PIA MTU ANAKUWA ENTITLED 28 DAYS ONLY AS HOLIDAY A YEAR!...NA PIA RETIREMENT AGE NI65YRS,BASICALLY YOU HAVE TO WORK 33 YRS..SO THAT YOU QUALIFY FOR BASIC STATE PENSION...JAMANI TUNAKIMBILIA NCHI ZA WATU,ZINA MAENDELEO HAYAKUJA KUTOKA HEWANI PEOPLE WORKED HARD FOR IT!!!!!....WE STILL NEED GOOD GOVERNANCE THOUGH!...UNDERSTANDABLY WATU WAKAISHIA...KUTUSI HUYU PROF,HUWEZI UZA UTUMBO AFU UOGOPE MAINZI ATII?...HUWEZI KUMKUMBATIA KIKWETE NA SERIKALI YAKE WHATSOEVER!!...JAMANI..MADUDU YA UTENDAJI WAO HAYABEBEKI!,YEYOTE ANAYEJARIBU KUYAKUMBATIA..ATAISHIA KUTUKANWA TUU HAPA KNY BLOG YA JAMII...!!HUWEZI KUANDAA WARSHA,AMA KUWASUKUMA WATU VIJANA WAJITUME MAKAZINI,WAKATWE KODI YA NGUVU IISHIE KWA WATU WACHACHE...NO!!IF WE REALLY WANT A CHANGE IN OUR COUNTRY,LETS GET RID OF THIS GOVERNMENT FIRST!!

    PROF,UMEANZA MAKALA YAKO KWA KEJELI/LUGHA ZA MITAANI..IN MY POINT OF VIEW...YOU DESERVE HAYA MANENO YA KEJELI NA OTHER GARBAGE THAT WERE THROWN AT YOU!
    if you want to be treated as grown up person/msomi,,then act LIKE ONE!!!

    wewe uliyesoma LSE please please naomba tuwasiliane kny hii email:jmalcomeee@yahoo.com...please kuna jambo nataka kukuuliza!

    ReplyDelete
  72. kila mata apa nilipo watu uniangalia na kushangaa nachocheka asa nn?labda nina mtindio wa ubongo ivi....kumbe ni viroja za comments blogu/globu ya jamii...

    kikatiba once umedeclare uraia tuseme wa siberia,AUTOMATICALLY umeukana uraia wa Tanzania (someni katiba ya nchi nimesahau tu kile kipendele)au rejeeni mazungumzo ya TBC1 na waziri membe na timu zima.

    hahahhaaaaa

    ReplyDelete
  73. PROF. ACHA BLA BLAH.......KARIBU KIJIWENI HAPA NAPO MBONA KIJIWE.....HAPA KWA MICHUZI KIWENI PROF. MUDA MWINGI TU TUNAPIGA POROJO HAPA KAMA KAWA !!!!!

    ReplyDelete
  74. Pro shule imepanda lakini mambo yake bwana, angalia resume yake
    http://www.stolaf.edu/people/mbele/resume2.html

    ReplyDelete
  75. JAMANI HUYU PROFESA SIO MJINGA KAMA MNAVYOONA NYINYI...ANA AKILI ZAKE..LAKINI MARA NYINGI WATU WALIOSOMA HUKA NA TECHNICK KAMA HIZI ZA KUCHOMEKEA.. MIMI NICHOSHANGA NA NIMESHANGAZWA SANA NAJAMAA MMOJA HAPO JUU YUKO MIAKA 15 ULAYA HAJUI THAMANI YA KUWA NA RAIA MBILI..HAWA NDIO WALE WANAOONGEZA IDADI LONDON..HATA UKIKAA MIAKA HAMSINI BURE TUU...UNASUBIRI BLOG IKUPE DARASA..KWIKWI

    ReplyDelete
  76. Nashukuru kwa mada yako Prof Mbele.
    Mimi ninatofautina na wewe hapa.
    1.Shule si ya kila mtu, maana uwezo wa kusoma hauko kwa akila mtu.Vipaji kama mziki,michezo na mambo mengine ni moja ya mambo yanayoleta ongozeko la uchumi.

    2.Dual citizenship ni jambo zuri wala sio baya.Nafikiri lengo sio kushindana na ulimwengu,ila kusaidia inchi na watu wake.

    3.Watanzania wengi waliohuku wamekuja kusoma na siku hizi wankuja kusoma masters.THEY ARE SMARTER ALREDAY..!

    4.Hao wakenya wanafundisha kwakuwa they are eligible to teach,sio kila mtu mwenye kujua kiswahili he/she is eligible to teach.Kuna viingilio fulani unahitajiwa kuwa navyo.

    5.Mwisho,NAOMBA USEME UKWELI KUWA UNAUZA VITABU VYAKO NA UNAMAPNGO WA KURUDI BONGO UNATAFUTA SHUNGULI YA KUFANYA.

    Mimi ni mtanzania niko hapa USA na nafikiri kuwa hapa kuna faida nyingi,lakini pia kuna hasara zake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...