Nimepokea kwa huzuni sana matokeo ya kidato cha nne kwa watahiniwa waliofanya Mtihani mwaka 2009.
Licha ya kuwa ufaulu umeshuka kwa asilimia 11.2 ila ukiangalia kwa makini takwimu hizo ni za kuhuzunisha na nimeshidwa kujua ni nani hasa wa kupewa lawama au kuwajibika kutokana na haya matokeo maana ni aibu kwa nchi yetu ya Tanzania.

Watahiniwa 339,925 walifanya
mtihani huo na matokeo ni kama ifuatavyo:
Ukiangalia takwimu hizo unaona katika kila watahiniwa 100 watahiniwa 17 ndiyo wenye angalau daraja la kwanza hadi la tatu ambao kwa uzoefu ndiyo wenye nafasi ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano na cha sita.

Watahiniwa 82 katika kila watahiniwa 100 wamepata daraja na nne na sifuri. Mbaya zaidi ni kuwa zaidi wa watahiniwa 65,708 ndiyo wamepata daraja la sifuri yaani hao ni kwa mwaka mmoja tu. Tanzania tumetengeneza watanzania 65,708 wenye sifuri hii inasikitisha sana yani hawa wote hawata pata vyeti na elimu yao ya kidato cha nne na jinsi elimu yetu ilivyo hao wote hawana ujuzi wowote labda kusema wataenda wakajiajiri sehemu hiyo ni hakuna.

Watanzania wenzangu tatizo ni nini hasa maana takwimu hizi ni za kutisha na kusikitisha na huu ndo ujenzi wa Tanzania au ndo wapi tunaelekea?

Mdau wa Elimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 56 mpaka sasa

  1. Naamini zile shule za kata zenye walimu walioenda mafunzo miezi chini ya mitatu ndo zimeleta huu mchango wa matokeo ya form 4 na form 2. Nashangaa wanasingizia wingi wa vitabu wakati wanua fika wingi wa shule majengo bila walimu au walimu wasio na sifa ya ualimu. Kila kata iwe na shule walimu je? Hii ndo tahadhari ambayo iliongelewa lakini ikabezwa na wanasiasa.

    ReplyDelete
  2. Thats crazy
    This is one of the reasons why people liki Kova aka "ELECTRONIKI" can go on the media and talk "PUMBA" because they think the majority of the population do not understand what the hell they are listening to anyway. Its sad. If we keep on playing our children will trail behind every nation in East Africa and we will become the future heaven ya Makaburu."Poor Tanzania"

    ReplyDelete
  3. Bongo Tambarare!!!daa zero zaidi ya 60,000!!Maghembe,Mahiza na Kabaka bado wapo tu wizarani!!

    ReplyDelete
  4. Div IV sio mwisho wa dunia jamani.

    ReplyDelete
  5. sijawaigi binafsi kufuatilia majibu ya wanafunzi,lakini,kwa sasa nimeangalia kidogo,kazi naona ipo.

    Nadhani system nzima ya elimu inabidi ibadilishwe.
    MImi kipindi changu,nilipata olevel 1.8 nilikuwa pale kibaha,na a,level 1.4.
    hata kwa miaka hiyo,kiwango cha watu kufeli nadhani hakikuwa kibaya hivi.

    Tatizo naloliona ni kwamba Tanzania wanafunzi wanasoma mambo magumu sana,na ambayo hayatusaidii,siku hizi nimeambiwa wanasoma mambo magumu zaidi,for what?

    Mimi ni mwanafunzi wa PhD kwa sasa,na vitu ambavyo nilivisoma Tanzania,naanza kuvielewa sasa,mind you Im 25years,sasa kama vitu hivyo vinafundishwa kwa mwanafunzi wa miaka 13-15,it makes no sense.
    Tunatumia Elimu ya Mkoloni,ambayo hata yeye nchini kwake haitumii kwa sasa.
    Its terrible,lakini nadhani makosa si ya NECTA,Waalimu,zaidi ni Wizara
    Ukizingatia hata sisi tulifundishwa na walimu ambao hawakuwa dip kama walivyo wa sasa,wametoka sijui vyuoni.

    ReplyDelete
  6. My Two CentsFebruary 08, 2010

    This is simply a case of the blind leading the blind.


    Na kweli matokeo yanasikitisha lakini kusema kweli hayashangazi. Tanzania tumezoea ku-cram na sio kuelewa hasa kinachofundishwa. Nakumbuka nilivokuwa nasoma Tanzania from the end of primary school to the middle of secondary school kweli nilijitahidi kuelewa kinachofundishwa but you reach a certain point when you realize hata mwalimu haelewi anachokifundisha. So you just try and memorize your notes hoping it will make sense to the person marking your exam!

    Kitu ambacho sikielewi ni kwanini wanafunzi wanafundishwa kwa kiswahili from kindergarden to grade 7 halafu baada ya hapo ni kiingereza all the way? This isn't fair and it doesn't make sense. I think you need to teach in ONE language from beginning to end. Chagua moja, kiingereza au kiswahili.

    Serekali, invest in the future. Better teachers, better learning environments, better results.

    ReplyDelete
  7. Mimi ni Mwalimu na nimesoma Tz mpaka University na sasa nafundisha nje ya nchi. Tatizo kubwa la Tz si kwamba wanafunzi wote wasiofaulu vizuri ni Mambumbumbu; "Hata kidogo". Tatizo ni Mshahara mdogo sana wanaolipwa waalimu wanaopajiriwa, hasa kwenye shule za serikali. Hapo nyuma miaka ya 80 na 90 waalimu walikuwa wanapofuzu masomo ya Chuo Kikuu na Vyuo vya ualimu walikwenda kufundisha mashuleni walikutumwa ila walikuwa wanajishikiza na kazi za ziada kama kufundisha masomo ya jioni na kuuza majarida ya Kielimu (Academic Pamphlets) kwa wanafunzi waliokuwa wakiwafundisha humo humo mashuleni. Unakuta Mwalimu ana-ripoti kazini asubunhi halafu kiguu na njia kwenda kuuza majarida hayo hapo shuleni na shule za jirani. Nilipofuzu masomo yangu ya UDSM nikafanya uchunguzi wa haraka na kugumdua kuwa sasa hivi waalimu wengi wanapomaliza vyuoni hubadili profession zao baada ya hapo na utawakuta wanafanya kazi tofauti kabisa na ualimu. Pia nikasikia sasa unaweza ukamaliza Kidato cha sita ukafundisha hata mpaka Kidato cha nne kinyemela. Na hata kama hukusomea ualimu naweza kupata kazi ya kufundisha shuleni iwapo tu ulisoma ukamaliza chuo Kikuu au chuo chochote kinachotambulika. Nimeshaona waalimu wengi tu wanafundisha mashuleni na hawakufuzu vyuoni kama waalimu na badala yake walifuzu kama Ma-engineers n.k. na baada ya kutafuta kazi bila mafanikio unakuta wanapata ajira kwenda kufundisha mashuleni hasa kwenye shule za binafsi )Private Schools). Hatuweza kufaulisha kwa namna hii! Tunahitaji kuwalipa waalimu vema kwanza ili mwalimu apate MOTISHA na kufanya kazi kwa bidii. Haya ndio maoni yangu.

    ReplyDelete
  8. Mdau wa Elimu umeleta hoja muhimu sana. Waziri wa Elimu aje atoe maelezo yake na atueleze tatizo liko wapi na anampango gani wa kuboresha elimu Tanzania. Kama hana jipya, ajiuzulu haraka sana.

    ReplyDelete
  9. Unashangaa nini, kwani wewe mgeni na Tanzania?? Haina haja ya kusumbuana kuulizana ulizana hapa, kawaulize walimu wanayo majibu - kikoliko

    ReplyDelete
  10. KWA MAONI YANGU, KUNA SABABU KUU TATU ZA MATOKEO MABAYA YA MITIHANI KWA VIJANA/WANAFUNZI WETU.

    KWANZA, nafikiria kwamba baraza la mitihani limefanikiwa kuziba mianya ya wizi wa mitihani au kuvuja kwa mitihani. Hatujasikia mwaka jana kutokea kwa tatizo hili kwa kiasi kikubwa kama ilivyokuwa miaka ya huko nyuma. Yawezekana kuwa ufauru mzuri wa wanafunzi hapo nyuma, ulioenda sambamba na tuhuma za kuvuja kwa mitihani,haukuwa halisi. Na kama hivi ndivyo, basi tulipongeze baraza la mitihani kwa kuziba mianya.

    PILI, shule nyingi za kata zilizotapakaa kila mahala hazijajengewa miundombinu ya kuziwezesha kuandaa na kutoa wanafunzi bora wenye uelewa wa kutosha, na wenye uwezo wa kujibu mitihani. Kwa mfano, shule hizi za kata hazina walimu, hazina vitabu,zipo vijijini kusikokuwa na umeme wa wanafunzi kujisomea,hazina mabweni, pamoja na vikwazo vingine, vinachangia matokeo mabaya. Ni vigumu klutarajia elimu bora na wanafunzi bora katika shule za namna hii. Na ndiyo maana shule zenye miundombinu bora, hasa za kiseminari, zina matokeo bora zaidi kuliko za serikali.

    TATU, siku hizi hakuna utamaduni wa kusoma vitabu. Kuna jitihada kubwa za wanafunzi kusoma ili wafauru mitihani. Hali hii imechangiwa na mfumo uliojitokeza kuanzia miaka ya 90 ambapo waaandishi wa vitabu walivamia soko la elimu kwa kuandika vitabu vya maswali na majibu.Vitabu hivi ndiyo chanzo cha ufahamu kwa watoto wengi! Vinawashawishi wanafunzi kusoma maswali na majibu yaliyoandaliwa na waandishi. Wanafunzi hawa hawana uwezo tena wa kufikiri. Ni kukariri tu. Au, vitabu hivi vimeandikwa kama notisi za mwalimu awapazo wanafunzi kama mwongozo. Siyo aina ya vitabu vya kuwafikirisha wanafunzi. Wanafunzi wanaotegemea vitabu hivi, hawana uwezo wa kuchanganua maswali kwa akili yao. Wanakaa kwenye chumba cha mtihani wakifikiri mwandishi gani aliwahi kujibu swali hili. Ni janga la taifa.

    ReplyDelete
  11. Tatizo ni hili, Serikali haina mpango wa kuzigharamia na kuziendesha hizi shule zimebaki za walala hoi. Viongizi wa serikali, watendaji wake na watu wenye uwezo wanawapeleka watoto wao shele za pårivate ambazo zinafanya vizuri. Ilivyo sasa kama wewe hunauwezo, wanao wataishi zero na four.Hii ni mwanzo na bado mbambo yatakuwa mabaya zaidi.

    ReplyDelete
  12. kuna waalimu wanaitwa vodafasta walipelekwa vyuoni wakafundishwa miezi 2 then wakaajiliwa ili kuokoa jahazi sasa ndio matokeo ya kupenda vitu vya rahisi mwalimu hajaiva mwanafunzi hajaiva sisi tuliozoea jiji tunaita ngoma droo serikali yetu ibadilike waziri wa elimu ni profesa aibu sana hii 20% tu ndio wamefauru!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  13. system yote ya elimu tanzania inatakiwa kubadilisha, maana masomo kwanza magumu beyond ufahamu wa wanafunzi kwa muda huo, yako zaidi kwa nadharia kuliko vitendo na mitihani ndio utakoma kama kukomoana vile. pia sioni kama ni fair kwamba miaka minne yote ya mwanafunzi inakuja kupimwa kwa mitihani ya mwisho ambayo yote unaifanya kwa week moja au mbili tu kama ikitokea unaweek mbaya au unaumwa you are done. kwa ushauri wangu hizi final results zingekua accumulation za mitihani yote uliyofanya since ulipokuwa form one yaani kama incase labda moko umefanya vizuri na final not so good at least utakuwa somewhere katikati instead of failing at all. Walimu pia waangalie namna ya kufundisha wawe na topic ambazo ni practical na zinarelate na real life situations au wanafunzi watakuja kukabiliana nazo in near future sio kufundisha kimtihani tihani tu. mwalimu wangu wa Biology alikuwa anafundisha watu kufaulu mtihani watu wakawa busy kumemorize maswali kuliko kuelewa mambo at the end of day wengi walifail.
    mwisho serikali lazima iangalie hili swala kwamba wanafunzi wote wanalalamika elimu ngumu na ukiwa mwanafunzi bongo huna life nyingine zaidi ya buku, ukitoka school tuition ukitoka tuition kwenda kusongolika na washikaji kwenye mageto ni hivyo ndivyo ilivyo all yeal long. why?

    ReplyDelete
  14. Hii batch ndio wale wa darasa la saba 2005. Mwaka huo asilimia 62 kati watihaniwa laki saba walifaulu. Kwahiyo mwaka huo kuna kama vijana 300,000 walioachwa nyuma (waliofeli). Sasa basi, wale waliofaulu na kuendelea na O level, mwaka huu kati yao wengine ndio wameachwa nyuma, na hawa ndio laki mbili waliopata daraja la 4 na 0 mwaka huu. Ukijumlisha hawa wa kidata cha nne mwaka 2009, na wenzao wa darasa la saba 2005 waliofeli, jumla tuna kama vijana kama laki 700,000 nchini kwa sasa ambao system ya elimu ya Tanzania imewashinda.

    Kinadharia tunaweza kusema kuna vijana Laki Saba wenye umri kati ya 17-19 ambao academically ni Failures. This is easily 2% of Tanzania's population. Sasa, kila mwaka tukiwa tunafelisha wanafunzi, baada ya miaka kumi, nchi yetu inatuwa inazidi kuwa ni nchi ya wasio na elimu ya kutosha. Kwahiyo nadhani nchi yetu haiko makini. Hatuangalii mbele kabisa. Mitaala inabadilishwa kila mara. Cha msingi ni ku'enforce teaching English kuanzia darasa la kwanza. Then tutaondoa hii kasumba.

    ReplyDelete
  15. Haya ni matokeo ya wizara na idara za serkali kutokuwa na dira ya kufikia malengo yanayotakiwa katika kazi zao. Hivi kweli ule usemi wa elimu ndio ufunguo tutautekeleza.Sijui kama tutapata hayo maendeleo kama hali ndo hiyo.

    Mkuu wa nchi anayo kazi kubwa sana ya kuongoza viongozi mbumbumbu kwa kila wizara na idara. Kila sehemu unayo kanyaga ni uozo mtupu. Na cha kushangaza zaidi ni kwamba viongozi hao wanaoharibu ndo bado wanaendelea kupewa nafasi ya kutema sumu ya kutowajibika.

    Viongozi wanachokijua ni kuharibu na kubomoa misingi yote ya maendelea. Hawana dira na niwabinafsi,wanajua kula pesa za serikali bila ya jasho. Hawana tofauti na wendawazimu ambaye hajui anchokifanya na hana malengo.

    Matokeo yake ndo hayo. Tusishangae hao walio felishwa ukakuta wanapadikizwa kwenye nafasi kubwa na kuanza kufichwa kwenye kuoo mbali mbali za serkali. Leo wanaharibu ukoo wa elimu na idara zake,kesho anapelekwa ukoo wa afya. Atatembezwa koo zote na baada ya kuhabu kote anapelekwa ofisi ya mkuu wa nchi.

    Hii niaibu jamani ifikie mahali viongozi wanaposhindwa kufikia malengo ya kazi zao kwa manufaa ya nchi wanyongwe. Adhabu hiyo inawahusu pia mafisadi. Inaudhi viongozi wanajifanya hawaoni na kuleta kelo kwa watumishi na kuendelea kukumbatiwa kwenye wizara na idara ukafikiri wamezaliwa huko.

    ReplyDelete
  16. Ndugu wadau wa blog ya jamii naandika maoni haya nikiwa na hasira sana!
    Tatizo la kutofaulu kwa vijana lipo wazi kabisa ikiwa mdau wa Elimu mwenyewe hajui hata kujumlisha idadi ya watahiniwa unategemea wanafunzi watafaulu.

    Ukiangalia idadi ya watahiniwa aliyotaja mdau wa elimu ni 339,925 ila ukijumlisha idadi ya watahiniwa katika safuwima ya pili (column ya pili) ya jedwali unapata 239,031 hao wengine kawapelaka wapi? na hizo asilimia sijui kazipata wapi jamani? Hii ni hatari kweli kweli. Unategemea mtu kama huyu ameingia darasani kufundisha wanafunzi si wataandika majibu ya uongo. Hii ndo sababu kubwa ya wanafunzi kutofaulu mitihani yao. Hiyo ndo bongo, chai tupu!
    Ankal usinibanie comments zangu.

    Mdau Udsm

    ReplyDelete
  17. ELIMU YA TANZANIA NI UOZO MTUPU HAIJAKAA KUMCHANGAMSHA MWANAFUNZI Akae kujiendeleza vizuri kimasomo.Mimi nilipata daraja la tatu kidato cha nne na sita lakini sasa hivi ni injinia mzuri tu tena kwenye kampuni kubwa ya hapa marekani,ni maajabu manake nilikuwa sitegemewi kufika popote.
    mdau
    duniayetukubwa.blogspot.com

    ReplyDelete
  18. Within a few years ALL the decent jobs are going to be taken over by Kenyans, Ugandans etc. The poor Tanzanian will be left behind until the so called leaders wake up and smell the coffee!!

    ReplyDelete
  19. ni kwamba mmeamua kuwaisha fulz dei ama niaje?
    mbona nikijumlisha idadi ya wenye I-III + wenye IV + wenye O jibu haliji 339925 lakini bado hizo asilimia zaleta 100%?
    au na mie ndio wale wale?

    ReplyDelete
  20. Inakuwaje mtu anapata division 0 na 4-ina maana amegomea masomo ama inakuwaje?

    ReplyDelete
  21. PURE SYSTEM FAILURE, ...VERY SAD INDEED. I call for some people such as the responsible minister to be held accountable, infact the minister the minister should be fired. Hi ina madhara makubwa kwa nchi in the long run, its bigger than EPA, Richmond and the like. The scary thing is we haven't hear any drastic changes planned, which means situation will remain as is in the next few years. This is the future workforce/human capital of Tanzania, they deserve to be treated better than this, wake up Mr. President PLEASE...!!!

    ReplyDelete
  22. Wabongo bwana mnajifanya kama hamjui! Huu ni mkakati kamambe wa nambari wani kutengeneza vizazi vya wapiga kura waliopevuka ili taifa letu changa (dogo) liweze kupata chakula chenye lishe na kukua haraka. Sasa hivi kuna mifumo miwili ya elimu: unaotengeneza wapiga kura wenye akili pevu na unaotengeneza wapigiwa kura wenye akili pevu.
    Ankal, siku hizi umekuwa mbogo kweli, mtu akitaja nambari wani basi unambinyia gizani! ukichukua fomu nami nitarejea huko kukupa kura yangu!!!!!!
    Mlalahoi
    Kwa mfuga mafisadi

    ReplyDelete
  23. Kuna masuala mawili, kuelimisha na kufaulisha. Kwa bahati mbaya tumefeli katika yote mawili. Wanafunzi hawafaulu na wanapata elimu nzuri ya ufisadi. Mtu shuleni alikuwa anaiba mitihani unadhani atakoma akiwa mlipa kodi? Akitoka hapo anafanya mazabe anadanganya ana PhD, anaingia bungeni, anakamata uwaziri akijiita dokta na kuingia mikataba ya ufisadi.
    Tumeshaanza kushughulikia hili tatizo. Tutagawanya majimbo na kuongeza uwakilishi wa wananchi bungeni ili kutatua matatizo yao ya elimu, maji, nk.
    *^(%^&#$#!

    ReplyDelete
  24. Mbona hizo number hazibalance lakini? Kwa haraka tu 44 + 130 + 46 = 240 na wewe umesema wamefanya mtihani ni 339. Ina maana hao laki moja wako wapi? Nadhani huyo liyetoa hizo data naye alipata Div 0

    ReplyDelete
  25. KILIMO KWANZA!!!

    ReplyDelete
  26. ANKAL NANIHII

    NIMESIKITIKA SANA KUONA NDUGU ZANGU WATANZANIA WAKIKURUPUKA KUTOA MAONI; TENA KWA JAZBA PASI NA KUANGALIA MASUALA YA MSINGI?

    HAO 65708 SIO ASILIMIA 27.4 YA 339925, BALI NI ASILIMIA 27.4 YA 239031. SASA LA MSINGI, ILI KUPATA USAHIHI WA TAKWIMU; NINGEOMBA MKUU WA LIBENEKE NA NANIHII UTUPATIE IDADI HALISI YA WALIOFANYA MTIHANI NA WALIOPATA DARAJA 0 NA 4.

    BAADA YA HAPO TUTAENDELEA NA MJADALA NA MAONI.

    BINAFSI YANGU, HUWA NAKEREKA NIKIONA WANAFUNZI WANAFELI; LAKINI NAKEREKA ZAIDI WADAU WAKIKURUPUKA KUSHUSHA MANONDO MAZITO PASI NA KUHAKIKI TAKWIMU

    ReplyDelete
  27. Hii inaonyesha wizara ya elimu imefanikiwa kuthibiti uvujaji wa mitihani, ujue wanafunzi wengi walikuwa wanategemea kununua mitihani mtahani sasa hivi hawaipati tena kwahiyo wanatumia akili zao wenyewe na hayo ndo matokeo halisi ya mitihani kwani wanafunzi wametumia akili zao wenyewe. Kwa vile serikali imefanikiwa kudhibiti uvujaji wa mitihani sasa ifanye mabadiliko katika system nzima ya ufundishaji na namna ya kutunga mitihani.
    Ndugu watanzania msilalamike na wala sio kosa la walimu ukweli ni kwamba wanafunzi wengi walikuwa wanapata mitihani ya kununua ndo maana shule nyingi zilikuwa zinafaulisha hasa za mijini.
    Mdau wa Damu

    ReplyDelete
  28. Kidumu Chama Cha Mapinduzi

    ReplyDelete
  29. Politics aside! We have a problem and we need to fix it now!!!!!!!!!

    These results speaks volumes of our system failures. What can we be proud of??????????? Kila kitu sisi ni ujanja ujanja tu na haya ndiyo matokeo yake.

    Hii ishu nik kubwa mno na ikiwezekana kunahitajika say a spesho forum only kwa ajili ya msuala ya elimu ya nchi yetu. Tumwage hoja humo na kisha tuangalie namna ya kuimplement!!!!

    ReplyDelete
  30. WANAFUNZI HAWAELEWI KI-ENGLISH,THATS A BOTTOM LINE,DONT GO AROUND THE BUSH HUNTING FOR THE WICH,IF THESE PUPILS WERE TAUGHT IN SWAHILI AS FROM VIDUDU THRU STD VII AND ALL THE WAY TO FORMS IV AND VI RESPECTIVELY,NO DOUBT THEY WOULD HAVE AN IMPRESSIVE RESULTS.OUR TEACHERS HARDLY SPEAK ENGLISH,HOW COULD THEY GIVE IT ALL TO THE KIDS?IT WILL TAKE US ABOUT 100 YRS IF WE GET SERIOUS NOW TO FIX OUR BROKEN EDUCATION SYSTEM AS WE WILL NEED TO TRAIN AND GET COMPETATIVE TEACHERS AND THEN START GIVING BACK TO STUDENTS.WE NEED TO MAKE A DECISION NOW WHETHER TO USE ENGLISH OR SWAHILI AS A MEANS OF INSTRUCTION,THE DECISION HAS TO BE ONE LANGUAGE FROM KINDERGARTEN TO HIGHER LEARNING INSTITUTIONS RATHER THAN TO CONTINUE MISLEADING AND CONFUSING OUR KIDS

    ReplyDelete
  31. Walimu wa fodafasta hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  32. This is serious. Mdau amesahau kutoa walioiba mitihani ili tubaki na idadi ya waliostahili kuitwa wamefaulu.
    Na hao waliofeli ndio watapelekwa kusomea ualimu ili waje kufundisha wadogo zao. Je tatizo litapungua au litaongezeka?

    ReplyDelete
  33. Nyie mnaosema kuna tofauti ktk namba. Labda kuna idadi kubwa ambao hawakufanya mtihani, au mitihani yao ilifutwa kutokana na sababu kama kutolipa fee, au kuibia majibu

    ReplyDelete
  34. KWELI KABISA KILIMO KWANZA ELIMU BAABDAE. WALOFELI WOOTE WASHIKE MAJEMBE WAKALIME...

    ReplyDelete
  35. Mimi wazo langu ni moja tu:

    Walimu wana haki ya kukataa kufundisha. Ningependa wanafunzi wote wapate div 0. Sababu ni hii:
    Mwalimu wa primary aliyeamishwa toka shule moja kwenda nyingine akidai fedha za uhamisho apewi mpaka anakata tamaa. Mbunge yuko Dodoma anapata allowance yake per day ambayo inakarabia mshahara wa mwalimu wa primary kwa mwezi!

    Huyo Mbunge hiyo allowance anapata hata kabla ya kudai! Sasa huyu mwalimu atatoa wapi nguvu ya kufundisha jamani? MIMI naona haya matokeo ni ushindi kwa walimu wote watanzania kwani kilio chao kimesikika.

    ReplyDelete
  36. Matokeo haya yanasikitisha sanana yanafaa kuitwa janga la kitaifa. Maotkeo ya darasa la saba na Form Two yalikuwa mabaya. Haya ya Form four ni mwendelezo wa trend hii. Tunajenga Taifa la wajinga, inabidi tuchukue hatua za haraka kunusuru hawa vijana wetu. Kwa maelezo zaidi ya nini kifanyike: Soma http://drfaustine.blogspot.com/2010/02/building-nation-of-fools-decline-in.html#links

    Mdau
    Faustine

    ReplyDelete
  37. MIMI NI MWALIMU JAMANI... MISHAHARA YETU MIDOGOOO, HATUWEZI ETI KUHANGAIKIA WATOTO WA WATU WAKATI WA KWETU HATUWAPI HATA MATUMIZI YA KILA SIKU. WITO KWA SERIKALI WAONGEZE MISHAHARA TUTAFUNDISHA, LA HAMUONGEZI ENDELEENI KUFYATUA VODA FASTA ZENU WAFUNDISHE. SERIKALI AMKENI TUONGEZEENI MISHAHARA TUFUNDISHE TAIFA LA KESHO

    ReplyDelete
  38. Kamuulize mkulu nadhani atakupa jibu sahihi...

    ReplyDelete
  39. leo sina la kuongea kwa mara ya 1 bloguni

    shocked!!! 0,IV???

    ReplyDelete
  40. mdau udsm 2:34 am ivi kweli eee?

    hahahaaaaa yani ninacheka apa kwa kituko hiki kaaazi ipo!!!

    ReplyDelete
  41. mbona mnawachangamkia sana walimu?? hapa kuna uzembe wa wanafunzi pia,mi mwenyewe nilikuwa mzembe lakini walimu walikuwa fresh 2,any way ILA SA HIVI NAJUTA.

    ReplyDelete
  42. AHAHHAHA KAZI KUKAAA BUNGENI AND TALK ABOUT UFISADI N OL THAT ILI MRADI TUU>>>U DONT EVEN TALK OF THINKS LIKE EDUCATION HEALTH SYSTEMS NO MORE VITU MUHIMU..wakulaumiwa its the all goverment system walimu well pia lakini if the goverment was so seriouse wasengeku walimu feki..EDUCATION IS KEY OF LIFE N KAMA TUSHA KUWA NAYO CARELESS NOW MTAONA

    ReplyDelete
  43. Im wondering why people are so suprised by these results!! You rip what u saw! we built a crippling education system just as we have built so many other systems by politising them without looking onto a bigger picture! Everything is politised!! Even health care issues!!Its not our kids faults, these are the results of what we have have built!!

    ReplyDelete
  44. Ni rahisi mno. Kuna aina mbili za elimu. ELIMU BORA na BORA ELIMU, kinachotolewa mashuleni sasa hivi ni BORA ELIMU.Its a plain fact and paining one.

    ReplyDelete
  45. MDAU WA ELIMUFebruary 08, 2010

    Hizo takwimu nilizitoa kwenye magazeti na ni baada ya kutafuta Idadi sahihi kwenye tovuti ya Wizara na pia Baraza la mitihani na kwa bahati mbaya sikupata takwimu(hazipo/hazijaweka).
    Ila idadi ni hiyo kwa mujibu wa magazeti yafuatayo Tanzania Daima,Habari leo,Daily news na Mwananchi.
    Naomba tujadili hoja, matokeo ni hayo na hayata badilika.

    ReplyDelete
  46. kwakeli inasikitisha sana elimu majibu ni mabaya sio siri labda ningependa tanzania yetu wabadili mfumo wa elimu waone itakuwaje!!!loh maana aibu!!lakini nasikitika mtu anafundishwa kiswahili elimu ya chini akuienda sec ni kingereza mmh kwakweli mimi nilivyokuwa nasoma nilikuwa naklem darasani nilikuwa sisomi kwa kuelewa lugha ilikuwa inanitatiza jamani maana nilikuwa simuelewi mwalim kutokana na lugha loh na pia walimu wangeongezwa mishahara wangekuwa na moyo wa kufundisha mpaka tunaelewa mishahara yao ni midogo ndo maana watoto wanabuluzwa tu darasani loh sio mchezo bongo na maisha ya sasa bila elimu ni sawa na hakuna watoto someni jamani elimu ni mkomboziiiiiii eeeh!!!!

    ReplyDelete
  47. siasa bongo zimezidi, wamefuta mitihani ya kidato cha pili ili wanafunzi wasirudie kidato kwasababu wanajua wengi watafeli na madarasa hayatatosha kwamaana kidato cha pili kitakuwa na wanafunzi wengi kuliko uwezo wa vyumba vya madarasa

    hili ni trela subirini watakapohitimu hao wasio na sifa ya kuingia kidato cha 3 watapomaliza.

    KILIMO KWANZA ILIWALENGA NA HAWA VIJANA.. sasa tatizo mashamba! anyway watalima mashamba ya wakorea

    ReplyDelete
  48. Focus ktk kujenga shule na kusomesha watoto iko kwenye quantity sio quality. hio ndio sababu kubwa ya matokea mabaya kila kukicha. Kumbuka pia mtihani wa form four pekee yake sio kipimo kizuri cha uelewa wa watoto!

    ReplyDelete
  49. innalillahi wainna ilayhi rajiuun bro mithupu huo msiba mkubwa

    ReplyDelete
  50. Kweli huu ni msiba kwa taifa, lakini kuna mambo ya kuyatazama kwanza:

    Moja:

    Uhalisia wa takwimu kabla hatujaendelea

    Pili:

    Hakuna haja ya kuilaumu serikali pekee hapa hali kuna watu wamepata Division one na wanafundishwa na hao hao walimu mnaowaita vodafasta, pili wanasoma shule hizo hizo mnazodai hazina miundo mbinu ya kumfanya mtu afaulu. Ni kweli serikali inachangia lakini frankly speaking, wanafunzi ni wavivu na hawasomi na wazazi/walezi tupo busy kutafuta pesa na kutoa muda mdogo sana katika fuatilia maendeleo ya mwanafunzi (unaondoka home majogoo unarudi usiku wa manane). Hivi mnajua how hard to get zero kama mtu unasoma, tena actually kuingia tu darasani na ukamsikiliza mwalimu you just can't fail to have 30% on only two subjects out of 7 or 8 or 9 or 10 subjects.

    Personally, kama nina mwanafunzi ninakaa naye na kapata zero, nadhani natakiwa kuwa wa kwanza kulaumiwa kwa kutofuatilia maendeleo ya huyo mwanafunzi.

    So let us start on ourself, students themselves then go to the government.

    ReplyDelete
  51. kwanza wanaotoa maoni kwa jazba huo ni ulimbokeni..kama mtu ametoa matokea haimaanishi yeye ndiye aliyechapisha..pili nataka kustress kuwwa kufeli mtihani wa darasani si kufeli kimaisha...kwahiyo nashangaa watu wanapotoa kejeli zao..ukienda baraza lamitihani ndio utajuwa uzembe wa usahishaji wa mitihan....

    ReplyDelete
  52. Walimu hawana sifa na wenye sifa hawana vigezo. Period! Mdau aliyezungumzia swala la mishahara kiduchu amemaliza kila kitu. This is insane. Inakuwaje tuko tayari kumlipa mbunge mamilioni ya hela ilihali waalimu wetu wanalipwa chini $200 kwa mwezi. Hivi kama taifa, tunafahamu vipaumbele vyetu kweli? Mbunge (say Yusufu Makamba au Lekule Laizer) ana faida gani sasa kulinganisha na mwalimu? Malipo wanayopata wabunge ingekuwa ndiyo wanayopata waalimu, then matokeo yasingekuwa haya na tungenyeka taifa lililoimara. It's so annoying!

    ReplyDelete
  53. wanataka kuimba bongo flava na kutafuta madili ya haraka haraka ya kutengeneza mamilioni

    ReplyDelete
  54. Watu tunataka watoto wafaulu lakini hakuna anaewajali walimu, kazi yao hawaioni, pesa zao hawalipwi miezi inapita mingi tu, mishahara yenyewe midogo ukilinganisha na kazi mtu anaingia asubuhi anafundisha session mbili, lakini malipo dhaifu tu...
    Walimu wengi wanajua vitu sana.. tena wazuri tu. Nimeshuhudi walimu kadhaa wazuri mnoo katika masomo yao wakishindwa uvumilivu na kuamua kujiendeleza katika fani zingine na sasa hawafundishi tena... Hadi inasikitisha. Sasa tumepoteza walimu wa ngapi kwa njia hio? Tuwajali walimu na maslahi yao mambo yatabadilika tu.

    ReplyDelete
  55. Je kwa matokeo kama haya waziri muhusika kwanini asiwajibike???????

    Majidai yake yote kwanini asijiuzuru????

    XYZ

    ReplyDelete
  56. Haa jamani angalieni mapoint yenu...nnimepita asubuhi katika shule moja ya wazazi Tegeta watoto wanaoungua na jua kama vile wanaoana nje kila kinachoendelea watazingatia kweli wanachofundishwa? shule haina uzio, badirisha hayana top au shater, nondo tu watauwa makini katika kusoma kweli??

    wakaguzi wa elimu wako wapi... mnapita kwenye hizi shule kweli??
    unategemea watoto watafaulu kweli hivi...nadhani tunacheza na nguvu kazi iliyojengwa kwa nguvu miaka arobaini iliyo pita...

    xyz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...