Hapa ni maeneo ya Tanga Kabla ya Kufika Mto Wapi,
Kuna ujenzi wa Barabara Unaoendelea.
Ndugu Watanzania,
Hivi majuzi nilikuwa nikisafiri kutoka mikoa ya kaskazini kuja Dar es Salaam. Kabla ya kufika mto wami, nililazimika kusimamisha gari na kutoa kamera kwa ajili ya hizi taswira. Siwezi kusema mengi ila wewe mwenye uamue, je hii ni ajira au ni mporomoko wa kimaadili. Hii ni ndani ya Tanzania, kwenye barabara kuu, na katika siku ya wiki ambapo hawa watoto wangekuwa darasani. Je, ni nani wa kulaumiwa...
Mungu Ibariki Tanzania
John Mashaka
Watoto Wakiwa Kwenye Heka Heka za Kutafuta maisha........ndani ya Tanzania
Pengine Wao wanaweza kuelezea walikuwa wakifanya nini, ikiwa wahusika au waajiri wao watabadilisha lugha
Bila Shaka Picha taswira inajielezea,
Watoto tena Umri wa Shule wakifanya kazi...




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 54 mpaka sasa

  1. Mr John, that's a tip of an iceberg!!

    Wakienda shule wanakula mizinga, wanaona afadhali waanze mapema kuwa wajasiliamali!!

    Unatoa ushauri gani!!

    ReplyDelete
  2. Inasikitisha!!, lakini John Mashaka, kutafuta wa kumlaumu hapa kwa Michuzi wakati watoto weneyewe ulikuwa nao ina maanisha nini? Wa kulaumiwa angempata kwa haki ikiwa ungevuta subira na kuwauliza hao watoto wenyewe, wako hapo kwa sababu zipi, na kama wametumwa, na nani? Sidhani kama hao ni waajiriwa wa hiyo kampuni, huenda wametumwa na wazazi wao, au wametoroka shule kutafuta hela ya pipi!

    ReplyDelete
  3. Bwana John, asante kwa picha, zanasikitisha lakini ndio hali halisi ilivyo Tanzania nzima. Hatutaondokana na ajira kwa watoto mpaka lindi la umasikini na ujinga uliopo ututoke. Imagine ungekuwa wewe katika umri huo huna wa kukupa chakula, malazi ni ya shida, mavazi ndo usiseme, na zaidi sana huna wa kukuonyesha njia ya shule na kukununulia uniform. Hakuna altenative isipokuwa kujishughulisha.

    By the way, hawa watoto walikuruhusu kuwapiga picha? Walijua kwamba utazitumia namna hii taswira zao? Angalizo ni kwamba always tuheshimu haki za watoto hata kama ni yatima, masikini na hawana wa kuwatetea.

    ReplyDelete
  4. MASHAKA:
    Nashukuru kwa picha yako, lakini huu ni ushuhuda mwingine kuwa kichwa chako ni matope.

    Nafikiri hujui kwa nini ajira za watoto zinashamiri na ajira hizi ni matokeo ya viashiria gani katika jamii.

    Mtu ataendaje shule wakati umasikini umeshamiri nyumbani? wewe unafikiri hao walipenda kuwa hapo?

    Usijidai mjuaji, wewe kama una dhamira zako za kisiasa basi ziweke wazi, unaweza tuambia uliyoifanyia jamii ya watanzania kuongoza mwamko wa jamii kupambana na matatizo haya?

    Wewe ndugu yangu mimi nakuona kichefuchefu tu? malumbao yako na US Blogger ni utoto mwingine ambao watanzania hawataki kuuona.

    Come out in a very constructive way, and genuine people will join you. Malumbano ya kijinga na habari za uchochezi zisizo na kichwa wala miguu haya kusaidia wewe au jamii ya Tanzania.

    Kama kweli wewe ni msomi na uliyeelimika, ungetueleza baada ya kuyaona hayo umefikiria nini na unafikiri watanzania wakuunge mkono kivipi.

    Wasalaam.

    Andrea - UK

    ReplyDelete
  5. NASEMA KUWA KUNA BOMU KUBWA LA NYUKILIA TUNALITEGA WENYEWE.HAWA WATOTO UNTEGEMEA NINI?.WATU WENGI WANAPENDA KUSEMA KUWA,WEWE NDUGU YANGU ANGALIA FAMILIA YAKO TU.ACHANA NA HAO WATOTO.KWA KWELI KITAKACHO TOKEA HAPO BAADAYE NA TENA SIO MUDA MREFU NI KUWA HAWA WATOTO WATAKUWA HAWANA LA KUFANYA,NA WATAKUWA WANANYANYASHWA NA WALE AMBAO SASA HIVI HAPO SHULE.HAWA WATOTO WATAKUWA WANA NJAA,MAISHA MABOVU.SASA WATATAFUTA MBINU YA KUWEZA KUJIKWAMUA KUTOKA KWA WENYE NEEMA.SASA UTAONA KIDNAPPING INATOKEA ILI WAPATE PESA.KAMA INAVYOTOKEA BRAZIL HIVI SASA.KAMA KUNA MTU ANA PESA NYINGI ,WATAJITAHIDI KUMTEKA ILI WAPATE PESA[MILLIONS OF MONEY].SASA SUBIRINI HILI BOMU.WATANZANIA TUSIMAME SASA KILA MTOTO NI KIJANA WETU NA PENGINE ATAKUWA RAIS HAPO BAADAYE.HATA KAMA HAJASOMA UTASHANGAA ANAKUWA RAIS .KWANI IDD AMIN ALITOKEA WAPI.NA WASOMI WALIKUWEPO PALE?
    ASANTE SANA MASHAKA KWA UJUMBE HUU.MUNGU IBARIKI TANZANIA.TANZANIA LAZIMA ITABADILIKA KWA LOLOTE LILE ,WATU WENYE BUSARA TUMEONA LAZIMA TUIBADILISHE.HATA KAMA MAFISADI WATANGANGANIA.
    MDAU WASHINGTON DC

    ReplyDelete
  6. Ndugu Mashaka mswala ya dual citizenship yanakushinda sasa unataka kuwaharibia hao watoto kula yao. kama hutaki watafute mkate wao unataka wafanye nini?

    Kama watoto hao wako hapo saa hizo muda wa shule hufikirii kuna tatizo zaidi ya wao kuwapo hapo? hufikirii wao wasipofaya hivo wanaeza kufa njaa? Nafirkiri ingalikuw ani nyema ukaandika chanza unachofikiri cha matatizo yanayowakabili watoto hao, au angalua ungewauliza ni nini kimewasibu labda kwa nmana hiyo ungepata fursa ya kujua zaidi na kuandika kwa uzuri zaidi kuliko kupachika picha zao hapa bila hata huruma na tena bila idhini yao na bila kuwalipa bila shaka.

    ReplyDelete
  7. Inasikitisha sana lakini bado unahitaji kuishi. Ushauri ambao mimi nimejipatia ni kwamba ukitaka usipatwe na shinikizo la damu au ugonjwa wa moyo, yaangalie matukio ya Tanzania kama filamu ya hollywood kama sio nollywood - na hiyo ni kuanzia ikulu kupitia bungeni na mahakamani hadi hapo mtaani unopoona watoto wananyimwa haki yao. Wote waigizaji kama Kanumba! Hawa watoto ni malaika wasiojua kama kuna fisadi wala mpiganaji dhidi ya fisadi lakini angalia huo ukatili wanaofanyiwa!!!Na kwa taarifa yako mbunge wa eneo hilo atarejea oktoba na kuomba kura na atapewa nyingi tu na wazazi wa hao watoto, ccm watapata ushindi wa kishindo, na ukisema Jk hafai wanakukata mapanga!!! Sasa kwa nini usiingalie bongo kama filamu!!!!
    Mlalahoi
    Kwa mfuga mafisadi

    ReplyDelete
  8. Acha uzoba wewe...sasa unashangaa nini wakati hiyo ni hali halisi??! Ukisikia Okonkwo ndio hawa wanaenda tu darasani kusoma kisha wakirudi wanaanza kushangaa ndugu zao.
    Kwanza huhitaji kwenda mbali kuona hivi hii ni hali ya kawaida Tanzania na nchi nyingi za aina yetu. Sasa wewe kwa usomi wako na muono wako ungetoa mawazo sio kushangaa SASA ukeshashangaa ndio wataenda shule??!
    Wewe unafikiri wenzetu walizaliwa wote wakienda shule?! Usidanganywe na Wazungu walikofikia nao wametoka mbali.
    Mzawa

    ReplyDelete
  9. mmmh
    ndo tatizo la serikali za watanzania bro we have to work and change the country . . . . . . kaka angu
    all the best
    sai

    ReplyDelete
  10. inasikitisha sana hata mimi niliwahi kula mzigo nikiwa mdogo kama hao hizo ndiyo nchi zetu ILA NINAHASIRA SANA HIVI SASA NINAMIAKA 35 SIJAWAHI KUPIGA KULA HATA SIKU MOJA NA SIWAPENDI WANA SIASA WOTE NAWAOMBEA DUWA WAPOFUKE MACHO WOTE ILI WAACHE KUFISADI

    ReplyDelete
  11. WANASIASA HAWATAIONJA PEPO HATA KIDOGO

    ReplyDelete
  12. we john mashaka unalete tu story humu azina kichwa wala miguu...watoto wanaoteseka sio tanzania tu...nenda mumbay india utapata picha zaidi....sasa unataka tufanye nini????jakaya kikwete anaishi hapo na kila siku anawaona hawa watoto...labda wasiliana nae.
    mdau money uk.

    ReplyDelete
  13. @John Mashaka.. Mkandarasi hajawaajiri watoto hao, wapo kuzoa zoa cement ili wakauze! Nafikiri viongozi wa Ward au kijiji waulizwe kwanini watoto hawaendi shule!

    ReplyDelete
  14. Haya mambo ni kawaida hapa Tanzania. Viongozi wakienda nje au hata wakiwa ndani ya nchi kiswahili kizuri as if kama hakuna matatizo makubwa! E bwana mimi ninashindwa kuelewa hii nchi inakwenda wapi? labda tuwaachie wajerumani warudi waanze kutupiga viboko ndio tutaelewa tunakwenda wapi. Mungu tubariki sisi tusio kuwa nacho.
    Mgombeaji mtalajiwa 2010

    ReplyDelete
  15. hawana uchaguzi maana:
    1. nenda shule ukirudi ulale njaa ili kesho usiende tena
    2. kafanye kazi ule ili upate nguvu za kufanya kazi kesho

    wazazi hawana lawama maana nao ni maskini wanashindwa kutunza watotowao.

    wa kulaumiwa: SIRIKALI.

    ReplyDelete
  16. DEVASTATION.NO COMMENT
    KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI NA ZIHESHIMIWE SERA SAHIHI ZA CCM

    ReplyDelete
  17. Watu wanaona mbali. Kama hawa watoto wangeenda shule wazazi wao wangelazimika kulipa ada kuwasomesha mpaka sekondari za kata. Kule wangezungusha. Hela ingekuwa imepotea bure. Mbadala wake ni kuanza kutinga mzigo mapema. Badala ya kupoteza hela wanaingiza hela kwa sasa huku wakiandaliwa kuwa manamba wa wawekezaji na EAC. Ili kuwahakikishia usalama wao tunaongeza majimbo ya uchaguzi ili kuwaongezea uwakilishi.

    ReplyDelete
  18. viongozi watasema wao hawana habari..watakuwa na habari kama hizi mpaka wakati wa uchaguzi unapokaribia kujipendkeza kwa rai..kwa viongozi kujuwa umuhimu wa watoto hawa ni wachache sana wengi wanaona sawa..ukienda kwenye majumba yao wao ndio wakwanza kuwaajiri wafanyakazi wadogo na wengine kuwapa mimba...na kuwatelekeza...tabia hii inanikera sana. mimi bwana mashaka kila mwaka napita upande wakaskazini kwa mwaka mara mbili lakini halii hii ni kawaida huko...jee pesa za misaada zinafanya nini? au wanataka zaidi funds...come on...tuwache kuyaendekeza matumbo yetu sana...nakutojali vizazi vya baadae...

    ReplyDelete
  19. Tanzanians love John mashaka so much. It is like evere bodi want to go to bed widh im. Amewrka picha wengie wameanza usememe na majungu. Mashaka hoyeeeeeeeee, haya vulugu na zianze

    ReplyDelete
  20. Ukiangalia picha hizo utaona kuwa hawa si waajiriwa kampuni ya ujenzi wa barabara. Wanaokoteza chochote kinachoweza kuwapatia fedha. Ungeenda shuleni au kwa viongozi wa eneo hilo .
    Kama ambavyo ungefanya ukiwa Marekani

    ReplyDelete
  21. nimesoma maoni ya wadau wengi hapo juu,kinachosikitisha ni kwamba watu wanauliza:-
    1.UNASHANGAA NINI?
    2.SIO TATIZO LA TANZANIA TU!
    3.SASA WAFANYE NINI?
    4.WAKIPEKWA SEKONDARI ZA KATA WATAZUNGUSHA,SI BORA WAANZE MAPEMA?
    5.WAZAZI WAO NI MASKINI WAMESHINDWA KUWATUNZA,SASA WAFANYE NINI?
    mimi binafsi hii inanipa picha halisi ya UPEO wa jamii yetu katika kutizama mambo.
    nijuavyo nikwamba jambo linapoletwa mbele ya hadhara linalenga kuamsha ari ya kulitazama katika mtizamo tofauti na uliozoa kulitazama kila siku.sasa kama watu wenye uwezo wa ku-access i-net wanafikia kuwa na mtizamo hafifu kiasi hiki,je wale walioko katika mazingira ambayo hata ku search ktk i-net hawawezi wanamtizamo gani wa mambo?
    wakati umefika ambapo inapaswa tujifunze kufikiri kabla hujasema chochote au kutenda. na hili ndilo liliifanya ulaya kuanza hatua za kupiga hatua,japo lilijitokeza katika kipindi cha mapigano na wengi waliitumia kama gia ya kukwepa kwenda kupigana,maana ulikuwa ukitambuliwa kama mwana philosofia(a great thinker) una epushwa kupelekwa vitani. kupitia njia hiyo watu wengi walijenga tabia ya critical thinking na kila mmoja aka shape namna ya kufikiri kama ambayo sasa kwa hapo tanzania kuna wimbi ka kila kijana mdogo kutaka awe MSANII,au mabinti wanataka awe MODEL,miss XWYZ n.k
    hadi jamii iwe na mwamko wa kutizama mambo sio kwa njia waliyozoea kuyatizama,bali kujiuliza maswali kama vile:
    1.nini chanzo cha jambo hili?ni nguvu za asili au ni matokeo ya binadamu kutenda kitu flani?
    2.je liko ndani ya uwezo wangu kulitatua au wa mtu ninaye mfahamu?
    3.nisipo litatua mimi je kuna anayefikiri kulitatua?je mtizamo wake unafanana na wangu au unatofautiana?je upi ni bora?
    tutambue wazungu pia walikuwa katika hali ngumu hivihivi,lakini kupitia great thinkers walijenga tabia ya kujenga idea,kuzijaribu na kuziprove practically,kupima matokeo yake hasi na chanya kwa jamii,na hadi leo wanaendeleza utamaduni huohuo wa kufikiri.
    kwetu sisi tumejenga tabia ya kutofikiri kabla ya kutenda,na matokeo yake tunasubiri kulaumu na kusema si tatizo langu nahivyo kutegemea kuwa kuna mtu flani ndiye anapaswa kufanya au kulifikiria na sio wewe.
    KWA MFANO;-
    1.mzazi anaona jukumu lake yeye ni kuzaa tu watoto,lakini sio jukumu lake kuhakikisha kuwa watoto hao wanapata maisha bora tangu afya,lishe,mavazi,malazi,elimu,starehe n.k hadi watakapo anza kujitegemea wenyewe wakiwa na msingi wa kusimama.matokeo yake unakuta mzazi ana wake 4,ana watoto 20,hana nyumba bora ya kuishi,watoto hawawezi kwenda shule,na mambo muhimu niliyotaja hapo juu,ila anaona ni haki yake kuilaumu serikali au ndugu mwenye uwezo ktk familia kwa kutomsaidia.
    UKWELI NIKWAMBA VICHWA VYA WENGI WALIO KTK UNDERDEVELOPED COUNTRIES VINASHIDA KUBWA SANA na ndiyo chanzo cha kutobadilika kimaendeleo.haijalishi ni WATAWALA au WATAWALIWA wengi ni tabu tupu.
    MFANO 2:
    Ukitolewa msaada unaolenga kubadili hali za maisha,unaishia kuwa miss used au miss alocated.unatumika kujinufaisha kwa wachache,kilichokusudiwa kubadilika hakibadiliki.kinabaki kilivyo.
    -ukianzishwa mradi wa kusaidia jamii unageuzwa na watendaji kuwa sehemu ya kujinufaisha wao,mfano badala ya fedha iliyotengwa kuwafikia walengwa kwa wakati ili ifanye kilichokusudiwa,wataibana ktk fixed account zao miezi au miaka,kipindi hicho kilichokusudiwa hakifanyiki.
    hapa pia inaingia tatizo la kutokuwa serious na TIME(watu wanapenda kupoteza muda,kufanya jambo lisilo stahili kwa muda husika).
    ninamengi ya kuzungumza lakini yataishia kwenda nje ya maada,lengo ni kuonyesha nini shida hasa tuliyo nayo inayopekea taabu tunazoziona katika jamii zetu kuto tatulika na kuendelea na mzunguko dumu wa kujirudia shida zilezile miaka nenda miaka rudi vizazi hadi vizazi.

    ReplyDelete
  22. wapili ulietoa maoni wewe kwa kifupupi tu tunakuosoma laivu, kama john ambaye simjui wala sitaki kumjua saaaana naona kafanya kitu flani kinacho eleweka ata kama ii isingekua bongo tu pekeyake asa wewe umefanya nini zaidi ya kumponda tu na kumuonea wivu kwa sababu watu wanampenda. ndo maana wengine hatujitokezi aina ya izo picha tunazo tunapiga kila tunapotembelea bongo ila tunajuz wabongo ni porojo mtupu ata mtu skija kwa ajili ya maendeleo, nilitegemea mtakua wengi tu kama nyie nilivyo soma story tu, eatu na upeo mdogo wa kufikiri, pole sana na kaa ukijua nyie nda sababu atufiki tunakokwenda. aisee pole sana, na haturudi ada mbadirike, uku tumesoma na tunakuja fia uku uku, atuwasaidiii ata kidogo mtafia porini mkisafisha kokoto. bora iwe ivyo kuliko kupingwa sana na mtz mwenzako wakati unataka kumsaidia yeye. tulio wakatieni tamaa tuko wengi kuliko mnavyo zania, tunatema yai si kisenge tumeamua kuishi uku na tumewatemeni nyie kwa upumbavu wenu na sio nyie mmetutema sisi, kumbukeni ilo. sio mnaongea tu wengine wameshindia pumba midomo inanuka na raisi mnae aaaaah. poleni wandugu wa zamani, kuna ukoo mi naujua wa mazengo mi nawajua saivi wote wako ulaya bongo limebaki jina tu, we unafikiri kwanini kama sio wapumbavu kama nyie, na akina mkwawa nao wakiondoka mtakaaga mnawasoma ktk vitaabu tu. aisee poleni.

    ReplyDelete
  23. Una consent ya kuwapiga hao watoto picha kutoka kwa wazazi wao? kwa muonekano tu uliwapiga picha kwa mbali ukiwa ndani ya gari kama vile unapiga picha twiga au pundamilia mbugani. It is very very unethical, angalau basi usingetoa sura zao. Umasikini wao hauwaondolei haki yao ya msingi ya privacy! Umewadhalilisha hao watoto kwa kuweka picha zao hapo. ngetafuta mbinu nyingine, na kisheria ungeomba ruhusa kwa wazazi wao wakakubali uwapige picha na uzitumie kwa mambo yako kwa sababu kwa umri walio nao hawawezi kutoa consent.

    Tatizo lipo kweli lakini njia uliyotumia si sahihi, na ajira kwa watoto ni kosa, hata kama hawajajiriwa na mkandarasi, huyo anayewatuma kukusanya kifusi ana makosa. Lakini makosa yao hayahalalishi kosa ulilolifanya, umeabuse hao watoto ingekuwa uko UK ungeshtakiwa ukizingatia umri wa watoto wenyewe.

    Hivi hizi shule zenu mmesomea wapi nyie vijana!

    ReplyDelete
  24. Munaomtukana John kuwemo wastaarabu kidogo.

    Kwanini tunashindwa kutofautiana bila ya kufarakana.

    John, hii nchi bwana itakuumiza kichwa na ushahidi ninao.

    Wewe unawaonea huruma wakati utafiti unasema wa-Tanzania 75% wameridhika na hali ya nchi na wanataka Serikali iliyopo iendelee kupeta. Subiri uchaguzi mwaka huu, wajanja wa propoganda wanaweza kuvuta 80% ya kura za ndio.

    John, naomba nikupe usia muhimu na utanikumbuka-matatizo ya watanzania yanasababishwa na wananchi wenyewe.

    ReplyDelete
  25. Mashaka nashangaa umeyaona huko Tanga, ila kama unakaa DSM, haya mambo ya watoto kutumikishwa kazini yako maeneo ya Boko, Bunju, Mbagala, Kisarawe.

    Nchi yetu tunalalamika na serikali kusema hawana mapesa, lakini ukiangalia kila kidogo tulichonacho kingeweza kupunguza makali yote haya ya maisha kama vile ya ;
    Umeme
    Maji
    Ustawi wa jamii
    Elimu
    Afya
    Barabara na ma "flyover pia!" bila kusahau sehemu za kupita watembea barabarani maana ajali zimezidi, bila kusahau kufukia na kuweka mifuniko kwenye mifereji
    Nyumba za walalahoi

    Ila ukiwauliza watasema hela, ila wao wanasomesha watoto nje, wanatibiwa nje, wana magari na nyumba tele, akaunti zao za benki zina "visenti"

    Na sie hatutafumbua macho, tutazidi kuwapigia kura!

    ReplyDelete
  26. Mnaona dispora , kazi ni ku point fingers! we si umekulia kijijini wewe? na maisha si unayajua ? leo hii kuwa diaspora ndio mmhhh pua juu juu

    ReplyDelete
  27. ukitaka kujua watanzania wana wivu
    1. weka jina la john mashaka
    2. hasheem thabeet
    3. steve kanumba
    Aki ya nani mashaka anwafanya watu wapige mayowe kwenye computer na wivu aisee hii kali
    Kidumu chama cha Mashaka
    Kidumu

    ReplyDelete
  28. Ajabu US blogger anamtetea mashaka, baada ya kumponda???

    ReplyDelete
  29. nyie watu mbuzi kweli. mashaka anawaonea hurumna lakini vichwa vyenu vinavyojua kila kitu haviishi kukoment pumba. mtakufa masikini

    ReplyDelete
  30. Mashaka, wewe kama ujasoma historia ya jamaa zako wa Amerika, kila Taifa linapitia mlolongo huo. Kumbuka "the Gilded Age" (1877-1900). Watoto ndio waliokuwa wakifanya kazi viwandani, migodini etc. Mpaka kipindi cha "the Progressive Era"(1900-1917) wakati wa maraisi Theodore Roosevelt na Woodrow Wilson ndipo sheria zikapita za kuzuia watoto kutokufanya kazi na kupiga marufuku kunywa pombe ("the Prohibition Era").

    Sasa kama unataka kuwa mtatuzi wa masuala haya unaingia ulingoni kisiasa na kupambana nayo kwani, masuala ya kijamii na uchumi yanahitaji political power itakayokuwezesha kuwashawishi wanajamii waone madhara na faida ya kubadilisha muelekeo kwa yale yanayotendeka ndani ya jamii.

    Mdau US.

    ReplyDelete
  31. COMMENT AMBAYO NIMEIPENDA KULIKO YOTE NI YA US-BLOGGER KUM SUPPORT NABII YOHANNA MASHAKA. HUU NDIO UKOMAVU WA KISIASA. US BLOGGER AMEFIKA HATUA YA KUMTETEA KIBOKO YAKE

    US BLOGER, SIYO KWAMBA WANAMCHUKIA MASHAKA, LA HASHA. MASHAKA ANAPENDWA MNO, NI WACHACHE NDIO WANAOMUONEA WIVU KWA MAANA MASHAKA AMEWAACHA KARNE MBILI NYUMA

    MASHAKA ANA AKILI BUSARA NA HEKIMA NI MTU WA KUFIKILIA MBALI. KWA HIYO WAO KUJADILI ANAYOYASEMA WAO WANAMJADILI WAKITAMANI WAO KAMA YEYE. MIMI MSHAKA NAMFAGILIA NA NITAZIDI KUMFAGILIA

    ReplyDelete
  32. @aNONY Mon Feb 22, 06:53:00 PM
    hivi kusema kweli wewe na mashaka nani kichwa ni matope?
    mimi kama mfuasi wa mashaka siwezi kukubali uona mbuzi kama wee akimtukana nabii wetu, kwenda zako huko ukichoka na boxi dandia meli rudi nyumbani kwenu ukachunge ng'ombe. mashaka anatufundisha na kututabiria yajayo. huyu ndiye rais wetu kwa hiyo TOA USENENE WAKO mwache mashaka wetu na kipenzi chetu, endelea na ufisadi wako na akili yako finyu. akili ya mashaka ni nyingi hata uchukue kijiji chenu chote hawamfikii, habali ndo hiyo

    ReplyDelete
  33. HUYU NI JOHN MASHAKA FEKI,,, JOHN MASHAKA WA UKWELI YUKO WALSTRITI YULE HAJI TANZANIA KABISA. ANAKULA TU KUKU NA MAYAI YAKE

    ReplyDelete
  34. mashaka picha zinajielezea, na wenye akili na wataelewa, mashaka wanaokupenda ni wengi kuliko hii mitoto myenye wivu

    ReplyDelete
  35. Watanzania bwana,mnashindwa kuwatukana mafisadi mnamtukana John Mashaka .Yeye hapa kataka watu wajadili ni nini kifanyike,kweli Tz ni kichwa cha mwenda wazimu,mijitu ina wivu kweli kweli.

    ReplyDelete
  36. John Mashaka you did well in exposing the bottom of our country....who do we blame? of course ourselves...and shame on us all that we can not provide to our children...30 to 40 years ago that was not the case...BTW I am sure you asked for their consent before taking their photograph...Mr. Mashaka you have my vote,...Good Luck...Mdau Canada

    ReplyDelete
  37. Asante kwa picha sio nzuri kimaadili,maana kwanza hukutaka uulize kulikoni? Taswira hao watoto hawajaajiriwa,hapo kuna gari ya saruji ilianguka hao watoto wakiwa na mama zao wanazoa huo udongo wakakandikie vibanda vyao, pili siku hiyo ni jumamosi kulikuwa ni mapumziko,tatu wewe kama mzalendo una nia gani na Taifa lako mwenyewe?

    ReplyDelete
  38. bw mashaka unajifanya unajua unatafuta umaarufu kwa nguvu child labour ni tatizo la dunia nzima c tanzania pekee so usijshauwe

    ReplyDelete
  39. US Blogger yaani uko sawa kabisa "matatizo ya watanzania yanasababishwa na wananchi wenyewe". Hii ni nukuu kali ya wiki.

    Nimekukubali ndugu yangu.

    Kazi njema.

    ReplyDelete
  40. Bwana US Blogger, you are very right, na nakubaliana na wewe nimeshangaa sana kusikia eti watanzania asilimia 75 wameridhika na hali ya Utawala uliopo madarakani. NI KWELI KABISA KWAMBA MATATIZO YOTE YANALETWA NA SISI WATANZANIA WENYEWE HATUNA WA KUMLAUMU. Yaani kusupport uongozi ulioko madarakani sasa hivi na hali ilivyo hapa nchini ni ushahidi tosha kwamba watanzania wenyewe tunajitakia hali hii iloyopo nchini kwetu. Tanzania jinsi tuijuavyo!

    ReplyDelete
  41. JOHN NAPATA PICHA HAYA MAMBO YANAVYOKUUMIZA NA UKIYAFUATILIA YATAKUUMIZA SANA. MIMI NIPO BONGO NA SIJAWAHI TOKA HAPA BONGO NILIISHA ACHA KUFUATILIA MAMBO YA KIBONGO NIMEAMUA NIWE NAANGALIA MAMBO YANGU TUU. SITAKI KUFAHAMU SIJUI KUNA UCHAGUZI, SIJUI LEO BUNGENI KIMEZUNGUMZWA NINI NINACHOKIFANYA NAAMKA ASUBUHI NAFUNGUA KAOFISI KANGU NAFANYA BIASHARA ZANGU TAARIFA YA HABARI IKIANZA MASUALA YA VIONGOZI WA NCHI NASWICHI MZIKI THEN NITARUDI KUSIKILIZA MATUKIO MENGINE, IKITOKEA KIONGOZI WA NCHI ANAHUTUBIA SIMSIKILIZI ILIMRADI TUU NISAHAU TUU MAMBO YANAYOENDELEA NCHINI KWANGU, NA MASUALA YA KAMA NA KWEPA KODI AU LA NAOMBA NISIONGELEE HAPA MAANA.... HASA UKICHUKULIA MTAZAMO WANGU KUHUSIANA NA KODI NINAYOTOA.

    KWA KUFANYA HIVI IMENISAIDIA SAAANA MAISHA YANGU YAMEKUWA MATAMU SANA WIKIENDI NAENDA NA KAFAMILIA KANGU BEACH SITAKI KUJUA MAMBO YA WATU WENGINE WANAISHI VIPI MAANA NTARUDI KULE KULE OOOOOH! SERIKALI HAIONI WATU WANATESEKA OOOOH! SERIKALI IKO WAPI WAJAWAZITO WANAFARIKI HOSPTALINI WAKIWA HATA HAWAJAHUDUMIWA JAPO WAMEKUWEPO HAPO MASAA KADHAA. KUNA MTU HUMU KANIBOA SANA KANIJURISHA BILA YEYE KUJUA KWAMBA MWAKA HUU KUNA UCHAGUZI MKUU SIJAPENDA.

    ReplyDelete
  42. Hivi ni lazima kila mtu a comment?? maana comments nyingine za kijinga kweli wengi wao nadhani ni wafuasi wa zeutamu (RIP)

    ReplyDelete
  43. """Kabla ya Kufika Mto Wapi""" then unasema """Kabla ya Kufika Mto Wapi""" Lipi ni sahihi? nijuavyo mimi kabla ya kufika mto wami toka tanga kuma lami sasa ujenzi unafanyika wapi au lami ya zamani wameitoa na wanaweka mpya?

    ReplyDelete
  44. nilitoa comment hapo juu,na ningependa ku summarize kwa kusema kwamba tatizo kubwa tulilo nalo mataifa maskini linaanza na:-
    1.MTU KUKOSA ELIMU THABITI anakuwa na upeo mdogo wa kufikiri,kupanga,kutenda,kupima matokeo(individual level)
    2.kukosekana UPEO nilio utaja hapo juu kuna pelekea FAMILIA KUKOSA MWELEKEO,kuwa fukara na isiyo jiweza KIUCHUMI n.k( Family level)
    3.ukijumuisha FAMILIA KADHAA zenyenye matatizo yanayo karibiana au kufanana unapata JAMII(community)iliyo athirika na tatizo la aina moja(COMMUNITY LEVEL)
    4.ukiziunganisha jamii mbalimbali toka maeneo kadhaa unajikuta unapata TAIFA LENYE AINA FLANI YA KUNDI KUBWA LA WATU WENYE SHIDA ZINAZO FANANA( taifa maskini)
    nirahisi kusolve tatizo kuanzia ktk grass roots,yaani individual level,kuliko linapokuwa limefikia community level au natinal level maana linakuwa ni GIANT PROBLEM.
    EDUCATE THE PEOPLE,THEY WILL BE IN THE POSITION TO TACLE THEIR PROBLEMS BY USING THEIR BRAIN.
    lakini itambulike kuwa kumtawala mtu asiye na elimu ni rahisi,ila kumuongoza ni igumu sana!na kumuongoza mtu aliye elimika ni rahisi,lakini kumtawala ni vigumu sana maana anajuwa nini haki yake,wajibu wake na mipaka yake.
    Mdau

    ReplyDelete
  45. hii mijitu mijinga dawa yao ni john mashaka tu. huyu kijana mimi nimefali in love na yeye kusema kweli

    ReplyDelete
  46. wewe mzee mshamba unafilter maoni why?

    ReplyDelete
  47. Toba jamani wabongo wakishaenda ng'ambo wanajisahau!! lol..wanajiona wajuaji wa kila kitu, wanajiona wasomi, wanajiona wao ndo wao, hata utoe mada nzuri na ya maana vp wanakuona fala... wakati asilimia 95 ya hao wabongo waishio ng'ambo ni wabeba mabox...
    ushauri wangu kwenu nyie mafala rudini nchini kwenu mje kula bata acheni kuuza magazeti, kubeba mabox, shoe shiner, kuogesha vizee, etc... HESHIMU NA UHESHIMIWE!!!

    ReplyDelete
  48. Shule mnazotaka waende hazina waalimu, watoto hawana cha kufanya.Gazrti la leo lina habari ya shule ya Rufiji yenye mwalimu mmoja kwa masomo yote!

    ReplyDelete
  49. Hamna kitu hapo mtaumiza vichwa vyenu buure!! hebu leteni picha za maana bwana. mikoa yoote hiyo uliyokatiza hamna taswiraz ya maana!!

    Mdau wa Pajazzz+titizzz

    ReplyDelete
  50. we michuzi fala...unachagua coment za kuweka..choco.

    ReplyDelete
  51. Kupewa uhuru wakutoa maoni hamaanishi umepewa uhuru wa kuonesha upumbavu wako au ujinga wako.

    ndugu zangu watanzania tumieni vizuri uhuru wenu wa kutoa maoni na kama unaona huna cha kuchangia basi bora uendelee na shughuli zingine au kwenye post nyingine kwani ziko nyingi sana.

    nimesoma comments nyingi humu ni utumbo mtupu watu wameandika japo swala lenyewe ni zito na watu wangeweza kuja na mawazo mazuri tu.


    karibuni kuficha ujinga wenu ndugu zangu saa nyingine wengi wenu watu wazima tu kwa vile mna mda wa kupoteza ndio mnatumia kuandika upumbavu humu.karibuni kujiheshimu na kuheshimu uhuru wa maoni hata kama hamjulikani kimajina,maoni yenu yanaonesha wazi maisha yenu.

    ReplyDelete
  52. Hili US Blogger lina akili sana.

    ReplyDelete
  53. Kaka aliepost muda Tue Feb 23, 12:18:00 AM, sikujua kama bado tuna pumba kama nyie unatofauti gnin na hao watoto uliandika kuwa watapata zero. Sina mengi ya kuandika kama umeenda shule naomba urudi shule. Umeandika maelezo mengi na umejicontradict sana. Simjui John Mashaka. Lakini wewe kaka rudi shule tu umeandika pumba kama mzazi wako akiiona hiyo na amekulipia shule basi atadai ada yake. Poor presentation and poor analysis.
    Nimeona kuna watu wanamshutumu John Mashaka anajipendekeza, lini sisi watanzania tutatoka kwenye fumbo la maisha? Badala ya kukaa chini na kujiuliza kwanini Mashaka kaandika hivyo unaanza kutukana
    Poor Tanzanians.

    ReplyDelete
  54. to be fair! naomba utoe na maoni ya kimpumbavu unayoyaita tuone hao watanzania wapumbumbavu wanasemaje, na hiyo uite column ya wapumbumbavu. sidhani kama watanzania ni wapumbavu kiasi hicho. acha jamii ijudge yapi ni maoni ya maana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...