UCHAFUZI WA MAZINGIRA NORTH MARA

Ndugu zangu watanzania, kila binadamua ameumbwa na haki sawa. Tumeumbwa kupendana na kuishi kwa furaha na amani. Haijalishi masikini au tajiri, haki za msingi za kibinadamu hazitambui nafasi ya mtu katika jamii. Wote tuna haki sawa ya kuishi maisha yenye afya furaha na amani.
Kwa minajili hiyo hatuwezi kuukana na kuchelea ukweli kwa faida ya kitambo, Uwoga na tama vimefunika macho yetu wanajamii kwa ujumla pamoja na viongozi wetu kiasi kwamba mazingira yetu yanaharibiwa, na hata wanajamii wenzetu wanakufa pasipo sauti za kulaani vitendo hivyo viovu

Katika muda wa wiki moja na nusu, nimepokea jumla ya emails 39 kutoka kwa watanzania mbali mbali wakinisihi kutafuta mbinu ya kuwasaidia ndugu zetu wilayani Tarime ambao wanahathirika na magonjwa ya ajabu ambayo yanatokana na uchafuzi wa Mazingira.
Kusema kweli, picha zinazotoka huko, zinatisha na binadamu yeyote mwenye akili timamu au hutu kamwe hawezi kunyamaza. Kama wengi wenu mnavyofahamu, binafsi sina nguvu wala madaraka ya aina yoyote katika nchi yetu, ila kutokana na sauti za wengi, nimeamua kuwaandikieni ili tujadili kwa pamoja namna au jinsi tunavyoweza kushirikiana kama watanzania ili kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa matatizo yetu

Hatuwezi tena kuwategemea wanasiasa wetu, kwani wametusaliti. Baadhi ya wanaharakati waliokuwa mstari wa mbele kutetea wanyonge, wamegeuka kuwa makada wa mashirika ya kigeni yanayochafua mazingira yetu. Yupo mmoja ambaye majuzi tu aliweza kutamka wazi kwamba Taasisi za kitanzania ziweze kununua hisa za makampuni Fulani huko Uingereza huku wananchi na wamiliki wa mali zinazofanyiwa biashara huko Uingereza wanakufa. Hatuwezi tena kuwaamini viongozi kama hawa; muda umefika kwetu sisi kutafakari hatima yetu wenyewe

Nawaombeni wenye ushahidi wa aina yoyote kutuma ili tuweze kuvifikisha kwenye vyombo husika nchini Canada (Canadian Senate) na pia katika taasisi ya dunia ya haki za binadamu. Lazima tuwe tayari kujitoa mhanga katika kukupigania haki zetu za msingi. Y
aliyotokea Balluchistan, Chile na New Guinea yanatokea Tanzania. Ikibidi sheria za kimataifa kuhusu “ mauaji ya alahiki” zitumike kuvileta makampuni yanayo waua wananchi wetu mbele ya sheria. Maisha yetu siyo ramisi. Ingawa wengi wetu ni masikini, lakini haki zetu za kibinadamu ni vitu ambavyo lazima tuwe tayari kuvipigania kwa nguvu zetu zote na kwa njia zote zile chini ya uongozi wa kisheria.

Tanzania, ndio moja ya taifa pekee duniani ambayo wananchi wake wanauwawa, na viongozi wake (wasaliti) wakabaki kimya. Lazima tuondokane na adui yetu uoga ili tuweze kushinda unyanyasaji unaofanywa na mashirika haya yanayotuchafulia mazingira na kuhatarisha maisha yetu. Hatuwezi kuwa waoga na kisha tukajiita binadamu na wazalendo.
Kwani binadamu ambaye hayupo tayari kufa kw akutetea haki yake, hana maana ya kuishi. Hawa waathirika hawana hatia, dhambiyao kubwa ni kuzaliwa masikini kwenye jimbo lenye madini mengi. Ikiwa serikali yetu haitatusikiliza, basi Stephen Harper, itabidi atusikilize ila hatuwezi kunyamaza tena, dunia lazima isikie ukatili wanaofanyiwa ndugu zetu wa Tarime na kwingineko

Mtanzania Mungu Ibariki Tanzania
John Mashaka
mashaka.john@yahoo.com

Fuata hizo links hapo chini
http://udadisi.blogspot.com/2010/03/call-for-action-in-north-mara-gold-mine.html

http://allan.lissner.net/category/someone-elses-treasure-tanzania/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 46 mpaka sasa

  1. Nabii mteule, yohana johni mashaka, kalibu sana kwenye uwanja wa fisi wa Barrick goldi. martin luther king wa tanzania, sisi tuko nyuma yako, kama ni mawe mura tutabathema baresyo. thiga niche mura, vitha ni vitha. hii baricki inabidi ipondwe

    ReplyDelete
  2. mr RAIS 2015, mimi kula yangu unapata, hata ikibidi nitembee miguu kutoka malekani kuja kupiga kula Tanzania, nitakuja.

    Unafaa sana kwa kuwa jasiri na mtu mwenye hutu.

    ReplyDelete
  3. Nabii, good job well done.
    This is an example, yaani mashaka ni mfano wa kuigwa kweli.
    ngoja na mimi niimbe mashaka juu, juu juu zaidi

    ReplyDelete
  4. Mimi nilisemaga tangu mwanzo kwamba watu wenye hutu ni wachache. Wenye roho safi ni zero. JOHN MASHAKA, MIMI NATOA TANGAZO RASMI kwamba NIKO TAYARI KUWA MKE WA PILI. Sitaki mahari wala posa NITAKUJA BURE. Kwanza family yangu ndio itakayotoa mahari kwako. SIJUI WAKURYA WANAWEZA KUPOKEA MAHARI TOKA KWA MWANAMKE. Kabila letu hatujali, name niko tayari kuwa mke wa pili

    ReplyDelete
  5. BARRICK WATIMUE ZAO, HATUWATAKI HAPA TANZANIA, FAIDA YAO NI NINI ZAIDI YA MASHIMO WANAYOTUACHIA? WENYE MALI MASIKINI, ANAOKUFA KWA MAGONJWA YA AJABU. BARICK OUT OF TANZANIA, HAKUNA CHA SIRI TENA HATUWATAKI

    ReplyDelete
  6. kuuliza so ujinga,, hivi joni mashaka ndio DIASPORA AU NDO MAANA YAKE NI NINI?

    ReplyDelete
  7. Muosha Wazee H-townMarch 23, 2010

    John Mashaka, my hero. You have started a new movement of the people that will fight for our rights. We do not want Barrick in Tanzania, and you have become the face of common man’s struggle. We have you and Thank you! It's inspiring to see indigenous resistance against Corporate Crime - indeed, against this single Criminal entiry, Barrick Gold - spanning the whole globe, from the Western Shoshone lands to Tanzania and New Guinea.
    How disgusting, this giant Corporate Mafia unit killing and exploiting methodically, and using the same method of displacing native communities, polluting and exploiting systematically without any sense of social justice or ecological sanity.John Mashaka, we want you to be the president of Tanzania in 2015. People like Zitto are money hungry who have been pocketed and have lost their voices now Barrick Puppets. We want you to lead the new breed of leaders, to hell with Barrick. Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  8. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. John mashaka kusema kweli ndiye Martin Luther king Jr. Wa kitanzania siku za husoni. Kaka hongera kwa jitihada zako za kulikoa jamiii letu, taifa letu tukufu linawahitaji wakina john mashaka zaidi. HILI swala la mauhaji ya barick linaogopwa na wanasiasa. waliokuwa wanapiga kelele kama zitto kabwe tayari maeshapewa vijisenti siku hizi kimya, kwani barrick imehslowanisha viganja vyao, kw ahiyo wanaogopa kusema, mtume

    ReplyDelete
  9. mashaka gereza la segerea halina vitanda

    ReplyDelete
  10. BARRICK Gold Corp is fuming over allegations presented at Canadian Parliamentary hearing that its security guards at the Porgera gold mine in Papua New Guinea were involved in gang-raping local women on numerous occasions. A parliamentary committee in Canada is collecting information to support a private members' bill to empower its foreign affairs and trade ministries to impose strict community obligation and social responsibility guidelines on Canadian companies operating overseas.Barrick responded immediately, saying it was alarmed by the "extra-ordinary and extremely serious allegations" that its guards may have been involved in sexual assault on women. It said there were no such cases of sexual assaults since it took over the mine in 2006.A human rights lawyer, Sarah Knuckey, who claimed to have been to Porgera and spoke to local people told the hearing that: "Numerous accounts of rapes show a similar pattern."The guards, usually in a group of five or more, find a woman while they are patrolling on or near mine property. They take turns threatening, beating and raping her."In a number of cases, women reported to me being forced to chew and swallow condoms used by guards during the rape," Knuckey said.Barrick spokesman Vince Borg flatly denied the allegations and said such actions would have been the subject of a full investigation by Barrick's subsidiary in PNG.Knuckey is a lawyer at the centre for human rights at New York University School of Law. She testified recently at the Commons foreign affairs committee examining a proposal to toughen scrutiny of the operations of Canadian mining and resource companies overseas."We are alarmed by the extraordinary and extremely serious accusation that security personnel working at the Porgera mine may have sexually assaulted local Porgeran women," Borg said in a statement."To our knowledge, there have been no cases of sexual assault reported to mine management involving PJV security personnel while on duty, since Barrick acquired its interest in the mine in 2006. "Barrick and PJV would encourage anyone who has information related to a serious crime of this or any other nature to report it immediately to (Papua New Guinea) authorities in order for it to be properly investigated and receive due process under the law," Borg said. According to websites of some of the Canadian media, if the private member's bill is passed, it would break new ground internationally. Canada is home to many of the world's largest multinational mining and metals firms, and the bill is believed to be a first-ever attempt to e exercise control over companies operating abroad.If passed, it would empower the trade and foreign affairs ministers to produce a set of corporate social responsibility standards for Canada's resource firms. The guidelines would be based on international human rights conventions and rights and environmental norms set out by the World Bank.

    ReplyDelete
  11. sasa mbona mashaka kiswahili chake kizuri tu, au anaogopa waosha vinya ndo maana anatumia kimombo kigumuuuuu tiiiiii

    ReplyDelete
  12. US-BloggerMarch 23, 2010

    US-Blogger
    Hakuna kampuni nzuri Tanzania kama Barrick. Mashaka ana hasira kwa sababu alitaka kazi ya kuwa CEO wa Barrick akanyimwa kazi. Akaenda ikulu ili kikwete apewe uwaziri kikwete kampiga chini sasa hivi anajifanya anawapenda watu wa Tarime

    Bwana hizi ni fixi za nabii, hakuna kitu kama uchafuzi wa mazingira North Mara. Mashaka hapa kachemka, mashaka muongo.Mimi nilienda North Mara lakini hakuna tatizo lolote.

    Anataka tu apewe waziri mkuu 2010 ili mwaka 2015 awe Rais. Watanzania tumekuwa wajanja, mashaka ndio wale wamarekani wajanja, ambao wakipigwa kete wanaleta mizenwe.

    Unaona Iran imewashinda, sasa wanazunguka dunia nzima kupiga kelele sanctions sanctions. Msihangae, mashaka anajaribu kupigia kampuni la kimarekani kuchukua ujimbaji madini north Mara. Wadau hii ni uongo wa mashaka

    Us-blogger

    ReplyDelete
  13. MASHAKA JUU JUU JUU ZAIDI
    CCM JUU, JUU, JUU ZAIDI
    UKONGA JUU, JUU JUU ZAIDI
    baliki zii, zii, zii kabisa

    ReplyDelete
  14. Mashaka hapati ubunge, yeye atapata tu ubalozi wa nyumba kumi kule shirati. ameenda utegi sasa hivi kufanya kamepni kumng'oa sarungi. haya tusubiri tuone

    ReplyDelete
  15. mashaka lovrers, and blind followers. Tatizo ni jina mashaka watu wakishaliona vurugu vinaanza kwenye hii bulogu tukufu. Lakini hapa nampongeza mkuu kwa kuwea hii mada. Pengine mafisadi watasikia vilio vya wanyonge waweze kubadilika kimawazo.

    ReplyDelete
  16. SIELEWI KAMA RAIS WETU ANAFAHAMU ILI AU LA. NA KAMA ANAFAHAMU ANAWEZAKE KUKAA KIMYA BILA YA KUSEMA LOLOTE. INAHITAJI ROHO NGUMU KWELI KWELI KUFICHA MAOVU YA WACHACHE, WAKATI UNAONGOZA WENGI WENYE SHIDA

    ReplyDelete
  17. RAIS,
    MH… NABII YOHANA MASHAKA WA 2015
    Kidumu chama cha Mashaka,
    Kidumu

    ReplyDelete
  18. nabii mtakatifu mtume yohana john mashaka,mimi nakuomba kitu kimoja, barabara za kinyelezi na segerea ni mbaya sana, tunaomba uvitengeneze kama mbunge wa ukonga ili tuweze kukupigia kura kwenye bunge tukufu. Hospitari ya temeke nayo hakuna vitanda, watu wanalala wawili wawili na dawa pia hawawezi kupata. au unataka na wewe tukelepeke kwenye D-League ya walstreet

    ReplyDelete
  19. kwikwi haaaaaaaaaa Zito kabwe alikuja kwa mbwembwe after kupewa vijidola kimyaaaaaaaaaaaaa, jamani madogo hatutaki longolongo na siasa njaaa kieleweke lazima yaani kitu spidi mia nane mafisadi jamani ibeni vya mwisho mwisho tunakuja kuwashika, mara mapanga shaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  20. Mashaka hongera sana kwa ujasiri wako, Tanzania nahitaji mashaka wanne tu, matokeo yake ni maendeleo. Kazi nzuri mkuu, ila usinisahau mwaka 2015. Mimi nitakuwa mlinzi wa maswal ya chakula ikulu

    ReplyDelete
  21. Wanaotaka kufuatilia zaidi anayosema Mashaka wanaweza kuangalia tovuti hii hapa.

    ReplyDelete
  22. florian rweyemamuMarch 23, 2010

    sasa ndugu zangu mbona mnaandika pumba tupu. Mimi nilidhani tunaotoa maoni tungekuja na 'facts' za kuhusu hali ilivyo huko Mara badala ya kumpigia debe au kumponda huyo Mashaka. Yeye amekiri kuwa hana taarifa kamili ya kinachojiri huko Mara. Sasa andikeni 'facts' na siyo ushabiki. Mmoja mpaka anaandika kwamba yuko tayari kuwa mke wa pili. Tupo makini kweli au?

    ReplyDelete
  23. US BLOGGER HACHA UTANI, NINA WASI WASI KAMA UNA PhD. UNFANYA MCHEZO NA MAISHA YA WATU. HIVI HUKUONA PICHA CHA WATU WALIOKUWA NA NGOZI KAMA CHATU KWA KUONGA MAJI YALIYOCHAFULIA NA HUYO BARRICK, NA WATU WANAKUFA.

    ReplyDelete
  24. mashaka, watu kama wewe hawaendi mbali kwenye jamii ya kitanzania. watanzania wanafiki wenye wivu na wenye roho mbaya. serikali inalijua tatizo wilayani tarime lakine tumbo zao hazijali wanaougua na kuumia. hii inauma sana kuwaona wazee na watoto wanakufa hivhi hivi taratibu, haki ya nani!

    ReplyDelete
  25. Mashaka ameelezea kuwa amepata e mail nyingi za hayo malalamiko na yeye ametoa muongozo na kusisitiza picha na maelezo zaidi yanahitajika ili hili suala lifikishwe kunakohusika. Mimi na wewe hatuelewi taratibu basi tusikatishe tamaa wanaojitolea kwa ajili ya nchi hii. Mnaoponda hamjafikwa ingetokea mlangoni kwako ungechangia.Tusiweke utani kwenye issue serious kama hizi. Hongera Mashaka.Mmesahau kesi ya wazungu wa Barrick nalivyowalazimisha mbwa wa.... ndugu zetu. Hivi vitu vinauma jamani.

    ReplyDelete
  26. US Blogger sijakuelewa, badala ya kujadili hayo magonjwa ya ndugu zetu huko North Mara wewe unaanza kumchambua Mashaka??? Unadhani Watanzania ni wapumbavu??? Unadhani tutaacha kusikiliza mambo ya maana kusaidia wenzetu na kujenga nchi yetu kikweli na kukuunga mkono kwa kutaka kuleta mabishano ya maneno kwa kumu-attack Mashaka pesonally? Atake kazi anyimwe, aombe uwaziri akose who cares man? The truth ni kwamba ndugu zetu, watanzania wenzetu wanaumia na mangonjwa yasioyoeleweka na sidhani kama nchi ipo tayari kufungua kitengo cha uchunguzi kwa magonjwa haya na picha tumeziona ziadi ya wiki hebu pitia blogu mbali mbali za watanzania yaani utadhani ni cancer ya ngozi! Halafu wewe unatuliletea kashfa kwa Mashaka ambaye ndio anaonekana kukerwa na hili mpaka ameweza kuandika mail kwa Michuzi kuhusu hili wakati wengine tumeona hizo picha na bado tumekaa kimya sijui ni uoga... sijui tuna nini Watanzania!

    Angalia wenzetu wa Botswana, migodi labda ina capacity ndogo kuzidi migodi yetu lakini wana faida sana na mikataba wanayofanya ktk migodi yao, watoto wao wanasomeshwa shule za ukweli tena sio wale watoto top of the class hapana wanatoa chance kwa wanafunzi wote sio upendeleo kwa wale wenye akili tu wachache yaani zaidi ya maelfu ya watoto wa Kibotswana wanapata scholarships USA, Canada, UK, Australia you name it tena ni full board scholarships. Barrick Gold Mine inatupa nini watanzania???

    Tumechoka uonevu huu tumechoka...

    -Mwana.

    ReplyDelete
  27. Mimi binafsi nimeangalia picha ya mama ni kama mama yangu,ya mtoto ni kama mtoto wangu,na sasa nashindwa kuangalia mara ya pili kwa uchungu wa jinsi wanavyoteseka.
    Kwa kweli sijui tuna majitu gani yanayotuongoza hayana uchungu na jamii wanayoiongoza,nashangaa kuna watu wanaleta utani wa Kaka John aliomba kazi akakataliwa?wewe kama ni mtanzania ingebidi hata kama umeajiliwa na hao barrick usimame na kutetea hao ndigu zetu wa tarime.

    Nasema hii sio ndugu zetu wa tarime tu itaenda na kwenu maana tuna,Geita,Buzwagi,Burlahuru,tulawaka kakola na kwingine kote kwenye madini kama unafurahia ndugu zako nao watafikiwa na athali hizi tunakula samaki wa ziwa victoria na zaidi itakufikia na wewe.Hebi tuungane kuwasaidia ndugu zetu.

    John Mashaka tuko nyuma yako onyesha njia.

    ReplyDelete
  28. MnyalukoloMarch 23, 2010

    Thank you Professor Mbele for that link. US Blogger - get a life! If you don't have anything positive or otherwise to say then please just shut the hell up!!

    John Mashaka, another site with damaging photographs is http://michuzijr.blogspot.com/2010/03/call-for-action-in-north-mara-gold-mine.html#comments

    Also here: http://udadisi.blogspot.com/

    Sadly, as with a lot of stuff going on, our government seems tongue-tied and unable to do shit!! Remmy Ongala alisema long time ago "Ukienda Kilimanjaro (hotel) utawakuta. Wake zao wazuri kama malaika, watoto wao wanasoma Ulaya,...." Tutafika kweli?

    ReplyDelete
  29. MliakuvanaMarch 23, 2010

    John Mashaka, labda hii itasaidia kushed mwanga zaidi kuhusu hili swala: http://vijanafm.blogspot.com/2010/03/uharibifu-wa-mazingira-mara-kaskazini.html

    Keep on fighting on!

    ReplyDelete
  30. Mashaka, hii hapa nyingine: http://drfaustine.blogspot.com/2010/02/when-government-take-side-with.html

    ReplyDelete
  31. Kwanza mkoa wa Mara huwa hawathamini maisha yao . Kuuana kila siku. Bora Barrick iwasaidie. Sisi tunataka kizazi hiki kiishe tu.

    Kilimo kwanzaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  32. mume wa us bloggerMarch 23, 2010

    us blogger hacha ujinga. hauwezi kujilinganisha na nabii, nabii yuko juu zaidi yako. nani mwingine mwenye ubavu wa kulizungumzia hili swala na kuweka jina lake??? kumbaf

    ReplyDelete
  33. dhambi za barrickMarch 23, 2010

    A man who is on the council of the prestigious Woodrow Wilson International Center for Scholars is part of an alleged racket in cahoots with a Toronto-based international gold giant that has reportedly resulted in billions of dollars of losses to Baluchistan.

    The man in question is a Pakistani businessman named Muslim Lakhani, who was a polo buddy of Pakistan president Asif Ali Zardari, then got involved with the Musharaf regime that unleashed a bloody military operation against the Baluch and was point-man of Barrick Gold Corporation in Pakistan.

    Lakhani is a non-Baluch and locals complain they are being denied jobs at the Barrick Gold Corporation project at Reko Diq in Baluchistan.

    Lakhani, who arrived in the US a couple of years ago, is on the council of the Woodrow Wilson International Center for Scholars in Washington DC. He contributed $82,000 to the Obama election campaign last year.

    S"We have seen similar reports from Peru and Guatemala," said London-based Baluch resistance hero Hyrbyiar Marri, 41. He said this shows how corruption money made in oppressed countries are then used to buy influence and prestige in the civilized West.

    "The world must know about the loot and plunder going on in Occupied Baluchistan," Marri said.

    Interestingly, Lakhani got involved with the gold and copper in Baluchistan under patronage of the coup leader General Pervez Musharraf regime, which started the worst military operation against the Baluch people. At the time when the former dictator was engaged in a brutal military operation, Lakhani was showering praise on the Musharraf regime.

    [The last four years of the Musharraf government at the federal and provincial level have been unprecedented in terms of support for the project," says Lakhani.

    There has been widespread anguish in Baluchistan over how Lakhani, just because of his contacts with the former Musharraf regime, managed to give the short end of the stick to the Baluch people.

    Critics say that the government in Islamabad blundered by selling what may be the world's biggest untapped copper and gold deposits, worth over $100 billion, to foreign mining firms at a throwaway price, to the disservice of the people of the country's most backward province and economy


    The Baluch are observing black day on Pakistan's independence as their Texas-sized homeland was annexed against their wishes on March 27, 1948 by Pakistan army.


    The DC-based American Friends of Baluchistan is calling upon international auditors to see how Lakhani and Barrick Gold Corporation joined hands in what Pakistani media reports suggest was one of the biggest white-collar crimes in Pakistan's history.

    The AFB is also demanding 100 percent of jobs for Baluch locals and have condemned a Barrick Gold manager, a retired Pakistani Colonel named Sher Khan, who sent an email in defense of Pakistani intelligence officials crimes against humanity in Baluchistan.

    In spring, Pakistani intelligence officials had tortured and killed three Baluch activists Ghulam Mohammed Baloch, Lala Munir Baloch and Sher Mohammed Baloch who were fighting for Baluchistan's independence.

    Since Pakistan is a rogue state, after the killing of the three by the Pakistani intelligence the Pakistani federal government said it was clueless about the killers and interior minister Rehman Malik announced a reward for information about the killers.
    In spring this year, another US think-tank World Affairs Council of Western Michigan had invited former Pakistani dictator General Pervez Musharraf to speak at its annual event while the Middle East Institute, led by former US ambassador Pakistan Wendy Chamberlin had offered a job to the Pakistani dictator.

    The Baluch in Canada are also planning massive protests against Barrick Gold Corporation in Toronto.

    ReplyDelete
  34. mashaka kazi nzuri sana kwa kuwa mstari wa mbele kutetea haki za wanyonge, hachana na us blogger. anatamani kuwa kama wewe amechoka kuosha wazee huko aliko ndo maana kelele zake ni wivu za kike tu

    ReplyDelete
  35. mimi najuaga mashaka kiswahili hakipandi vizuri. akiongea utadhani kazungu fulani. pengine mtu kamatafsiria hii makala

    ReplyDelete
  36. Anon @ Tue Mar 23, 12:11:00 PM

    Ndio, sio jipya, lakini hujiulizi kwanini vyombo vya habari vimekuwa kimya sana kwenye jambo hili?

    Michuzi alipata hizi habari, lakini labda alikuwa "busy".

    Mimi kama mwana-blog, nashukuru tu kwa kuwa hizi habari sasa zitakuwa zimewafikia na kuwafumbua macho watu wengi! Tuamke Wabongo...Tujifunze wenzetu wa Ivory Coast walifanya nini!

    ReplyDelete
  37. Dawa ya Tanzania ni mashaka Watano tu!!!!!!!!

    ReplyDelete
  38. John Mashaka amasisha Tanzania , tunajua utakuwa rais Hilo siyo hoja

    ReplyDelete
  39. Nampendea mashaka kitu kimoja, anajua namna ya kuwafanya watu wafikiri

    ReplyDelete
  40. WEWE US BLOGGER KTK MUONEKANO WA HARAKA HARAKA NDIO WALEWALE MWANACHAMA WA THE UTAMU, KAMA UNAHOJA JITOE JINA KAMILI NA UTEMBELEE TANGANYIKA KAMA NABII MASHAKA TUTAKUELEWA ZAIDI YA HAPO FUTA MIGUU INGIA KITANDANI ULALE. WALUME WAKILONGA WE KUNA NAZI. ASANTE MICHUZI NIFIKISHIE UJUMBE , USIFANYE KAMA UNIFANYIAVO.

    ReplyDelete
  41. Ukisoma maoni mengi unaona watu wanaongea blah blah lakini kuna maoni mazuri pia(yanayoonyesha vitendo vya hizi kampuni nchi nyingine)...jamani tuache kuwa WATANZANIA WA JANA WA KUMUACHIA YOTE MUNGU na kubaki kusononeka tu...tunahitaji POSITIVE ACTION na ndicho kitu Mashaka anachokifanya,sasa badala ya kuleta USHAHIDI tunaanza kutoa maoni ya ajabu ajabu wakati watanzania wenzetu wanaangamia huu ni UPUMBAVU...tafadhali kama kuna mwenye ushahidi zaidi ya hizo picha kama vile watu wa mazingira au waliopima maji au ushahidi wowote wenye nguvu wa kuweza kuwaconvict hawa wahalifu basi asaidie ili tuwaokoe watanzania wenzetu...Bob Marley alisema waweza wafanya watu wote wajinga kwa muda fulani lakini huwezi wafanya watu wote wajinga kila wakati...ndugu zangu watanzania tusiendelee kufanywa wajinga kila wakati na kunyanyaswa katika nchi yetu...Mwenyezi Mungu
    awasaidie na kuwalinda wote wanaopigania haki na atusaidie kuondoa UMIMI na UBINAFSI Tanzania.

    ReplyDelete
  42. ILI TU-appreciate what Mashaka is saying, please visit the following site:http://udadisi.blogspot,com/20/10/03/call-for-action-in-north-mara-gold-mine.html

    ReplyDelete
  43. Unayeuliza Lugha anazoelewa mashaka ni kama aifuatavyo kwa mfuatano:
    1. Kijaruo - vuzuri sana
    2. Kiswahili - wastani
    3. Kiingereza - Vibaya (isipokuwa kile cha kunakiri kazi za Wasomi)

    ReplyDelete
  44. Kwa wale wanaotaka kusoma ripoti ya uchambuzi wa kina uliofanywa November 2009:

    http://vijanafm.blogspot.com/2010/03/uchafuzi-wa-mazingira-geita-na-mara.html

    ReplyDelete
  45. jon mashaka, wewe hauna mpinzani, i salute you man. you are my hero

    ReplyDelete
  46. Unayeuliza kama John mashaka ndio diaspora umenichekesha sana!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...