Picha za setalaiti za ripota wa Globu ya Jamii zikionesha hali halisi ilivyo muda huu katika sehemu ya tukio la uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya Boeing 737 ya ATCL kupata ajali baada ya kutua leo asubuhi




Ankal Michuzi
picha za ndege Boeing ya ATCL iliyopata ajali
Mwanza leo asubuhi ndo hizi ila nimepiga na simu sababu ni ngumu kwenda kwenye kiwanja
Mdau Eric
(akiwa amekwama airport Mwanza)

HABARI TOKA MWANZA ZINASEMA NDEGE AINA YA BOEING 737 YA ATCL ILIYOKUWA IKITOKEA DAR ASUBUHI HII IMEPATA AJALI NDOGO WAKATI IKITUA KATIKA UWANJA WA MWANZA IKIWA NA ABIRIA 46 HIVI.

HAKUNA ALIYEPATA MADHARA NA
ABIRIA WOTE NA WAFANYAKAZI WAKO SALAMA NA WAMESHAONDOLEWA SEHEMU YA TUKIO.
RIPOTA WA GLOBU YA JAMII ALIE JIJINI MWANZA AMESEMA NDEGE HIYO YENYE NAMBA YA MRUKO TC 100 ILIPATA DHAHAMA HIYO WAKATI ILIPOTUA KWENYE BWAWA KUBWA LA MAJI LILILOTUAMA KWENYE NJIA YA KUTULIA (RUNNAWAY) UWANJANI HAPO KUTOKANA NA MVUA KUBWA INAYONYESHA.

INASEMEKANA MAJI YALIINGIA KWENYE INJINI MOJA AMBAYO IKAZIMIKA NA KUIFANYA NDEGE IACHE NJIA NA KWENDA PEMBENI, BAADA YA KUWA IMEMALIZA UMBALI WA KAMA MITA 1200 TOKA ITUE KWENYE YA UWANJA HUO WENYE UREFU WA MITA 3000. MGUU WA TAIRI LA MBELE ULIKATIKA.
HABARI ZINASEMA UWANJA UMEFUNGWA KWA MUDA, NA KWAMBA KINACHOFANYIKA HIVI SASA NI KUANGALIA NAMNA GANI NDEGE ZINGINE ZITAVYOTUA (DISPLACEMENT) KWANI BOEING HIYO IKO KARIBU KATIKATI YA UWANJA NA PUA YAKE INGALI KWENYE BARABARA YA KUTULIA. HIVYO KAMA NI NDEGE KUBWA ITAKUWA SHIDA KUTUA HAPO HADI ITAPOWEKWA KANDO HIYO BOEING. NDEGE NDOGO ZINAWEZA KUPITA.



























Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. Mkuu tunashukuru kwa kuendeleza libeneke.

    Suala la usalama wa mali na watu halipewa kipaumbele ATCL. Jamani, kutua kwenye dimbwi la maji?? 3km runway is that short for boeng 737??

    Jamaa wanavyoyapenda maji next time ataanza kutua kuanzia pale ziwani.

    ReplyDelete
  2. POLE KWA WOTE WALIKUWEMO KWENYE NDEGE MAANA AJALI YA NDEGE SI MCHEZO, WEWE USIKIE TU.

    HUU NI UZEMBE WA VIONGOZI WA UWANJA WA MWANZA. WATAACHA VIPI MAJI YAFANYE DIBWI KUBWA HAPO UWANJANI.

    VIWANJA VINGI VYA TANZANIA RUNAWAYS ZAKE ZIMECHOKA SANA.

    MAMLAKA HUSIKA ZIFANYE KAZI ZAKE VIZURI KWENYE HILI

    ReplyDelete
  3. POLE SANA KWA WOTE.

    ANYWAY HII INGETAKIWA ITOKEE HAPA DAR TUONE WANANGE RESPOND VIPI KWA MAANA JUZI JUZI TU HAPA WALIWASTUA SANA WATU KWA MAZOEZI YAO

    ReplyDelete
  4. Hii hatari sana. Njia ya kutulia ama kupaa haipaswi kusimamisha maji. vile vile waongoza ndege walipaswa kutambua hilo na kuwaambia waende uwanja mwingine wa karibu ama warudi. Ni hatari, ila ni shukrani kuwa hamna majeruhi.

    ReplyDelete
  5. ndege yenyewe tunayo moja,sasa kama nayo imeharibika,kazi ipo

    ReplyDelete
  6. Nchi yangu Tanzania naipenda lakini...mhhh! Sasa jamani kweli tunanunua ndege alafu hata dibwi uanjani hatuwezi kulikabili. Kwani hivyo viwanja vya ndege vipo vingapi nchini? Kwa kweli ipo sababu ya kuamsha ari ya fikra mpya na uwajibikaji wa kiistarabu.

    ReplyDelete
  7. Tanzania kweli kila kitu ni tunasema ni "MIPANGO YA MUNGU" hata vitu vya kuzuilika kabisa kama hii ajali. Hapo kilipotokea ni kukosekama kwa friction kati ya Tyre and Tarmac due to still water on the lane. Hili ndilo limesababisha brakes kushin
    dwa kufanya kazi na ndege kuseleleka na kukosa "control" Ila kwa bongo watakuambia hajui sababu ni nini hasa na wanaunda timu ya wataalamu(Ulaji baada ya hasara) ili waangalie chanzo cha ajali.

    Mimi kila siku huwa nasema Tanzania inaangamizwa na wanasiasa wanajifanya wao ni kila kitu yaani Maengineer, Madaktari etc. Ukiwapa ushauri wa kuboresha kitu watakuambia hela hakuna fanyafanya tu kwa utaalamu wako ila hela za Kampeni za uchaguzi za kumwaga. Uwanja kama huu ulitakiwa ufungiwe na TCAA kwa usalama wa raia ila bwana mdudu mbaya kabisa kuliko wote katika maendeleo na usalama wa raia ni "SIASA"

    Halafu tunakimbilia kusema ooh imepata "AJALI NDOGO"-hii nayo ni siasa period, AJALI KUBWA IKOJE?. Hii ajali kwa ni kubwa sana kwani nina uhakika japo hakuna loss of life lakini hiyo ndege haitaruka kati ya miezi minne au sita kwa major repair. BONGO na wabongo tuache POLITICS kwenye kila kitu, hata kama mwaka wa "KULA" huu LOL!

    ReplyDelete
  8. kweli mbuzi wa masikini hazai, yaani kaboing ketu kamoja kamevunjwa kaguu kake, kaaz kwelkwel!

    ReplyDelete
  9. NDOMANA TUNASEMA KUOMBA MAZURI YANAKUJA MAZURI UKIOMBA MABAYA UTAPATA MABAYA TUMESEMA UONGO KUANGUKA KWA NDEGE DAR-ES-SALAAM WATU 50 KUFA SASA IMETOKEA AJALI MWANZA BAHATI NZURI HAKUNA ALIYEKUFA. PAZI.

    ReplyDelete
  10. Haya sasa.
    Lile zoezi lao la UTAYARI wamelifanyia Dar ajali imeenda kutokea Mwanza.

    Hivi kweli hilo PIPA lingeshika moto, hiyo FAYA moja tu inayoonekana hapo ingeliweza hilo ZALI kweli?

    Mweeh!

    ReplyDelete
  11. Inasemekana imechukua almost dakika 20 kwa gari la fire kufika airport, gari moja lilikuwa airport halina maji.

    ReplyDelete
  12. Michuzi!!
    Baba baba, unasema hiyo ajali ni ndogo?Hivi mlitaka mpaka watu wapoteze maisha ndio mkubali kuwa ajali ni ajali?
    Kwa huo msemo wa AJALI NDOGO, ina maana mnataka ficha baadhi ya vitu.
    Na hasara usiangalie eti mguu tu ndio umekatika.Angalia kama iingetokea hiyo ajali ndege hiyo ingeingiza kiasi kwa muda woote ambao itakuwa matengenezoni.
    I hope haitaundwa TUME.

    ReplyDelete
  13. Hongera rubani. umefanya kazi nzuri. Ingekuwa Marekani ungeshapewa tuzo.
    Honera sana

    ReplyDelete
  14. Karibuni, sehemu ya tatu ya muvi ya 'Bongo Tambarare'!! Nimewaambia hatuhitaji kuwasumbua professional actors akina Kanumba katika utengenezaji wa muvi hii!!!

    ReplyDelete
  15. JE HAPO MALIPO TSH NGAPI? MANAKE NDEGE HAIJAFIKISHA WATU MAHALA PAKE? ALIYESEMA HIYO AJALI SI NDOGO KAPATIA AJALI NI AJALI SI MPAKA WAUNGUE AU KUFA TUMSHUKURU MWENYEZI KUWAPA UZIMA JAMAA ZETU. WATU WA SHIRIKA LA NDEGE WAPEWE UCHUNGUZI NA KIWANJA CHA MWANZA KIWE KINATIZAMWA KUNA KIPINDI MVUWAI KINYESHA PANAJAA MAJI SI KITOTO. KINDORIPONSINZAGHISAKI WA Sit.

    ReplyDelete
  16. Poleni wahusika.Pamoja kwamba ATCL ni twiga "mnyonge" lakini haina historia ya ajali.Wale jamaa waliokua wanafanya mazoezi ya uokoaji Dar last week ndio walikua wanalichulia...Sasa hapo mizimu imewabipu kua huwa hawajalibiwi.Mazoezi Dar hajali Mwanza wapi naw wapi. nendeni sasa mwanza mkaokoe....LO!

    ReplyDelete
  17. ukiona maji yanatwama kwenye njia ya ndege ujue mkandarasi wa kujenga hiyo njia alikuwa mbabaishaji. yaani hata drainage system hakuwazia, na nnaamini uwanje wa mwanza ulikarabatiwa muda si mrefu.

    sina utaalam wa fizikia ya kutengenza ndege lakini nadhani abiria wana bahati sana mguu wa ndege ulikatika, bila hivyo wangeseleleka mpaka wakagonge kitu kizito na kuikwamisha ndege, na hapondiyo kipimo cha maafa kingeonekana.

    alafu kama sikosei mwaka ule wa el nino boeing nyingine ya ATC ilitiaga nanga pale mwanza. abiria walitelemshwa kwa mashua!!! we eric hebu tutafuite picha maktaba ili watu waone ilikuwaje?

    ReplyDelete
  18. ndege za tanzania zote ni mbovu, mnatia aibu wabongo, madini , benki na mbuga mmeuza bado mnalia njaa ULAYA na USA wawape misaada.VIONGO WA BONGO BWANA , MIYEYU KIBAOOO. UCHIZI HUO HATUJI NYUMBANI BASI.

    ReplyDelete
  19. dimbwi la maji kwenye runway haiwezi kuwa sababu ya hiyo ndege kupata ajali .... ndege inapotua inakuwa kwenye speed ambayo hilo dimbwi haliwezi kufua dafu ... hapo lazima kuna kitu cha msingi kilichosababisha.

    Je, matairi ya hiyo ndege hayana vipara; maana hiyo inaweza ikasababisha ndege kuserereka (kwa sababu kunakuwa hakuna friction ya kutosha kati ya tairi na runway)

    Lakini, nadhani tunahitaji uchunguzi wa kina kuhusu hii second-hand ndege ambayo inalipiwa mamilioni.

    ReplyDelete
  20. Picha za satellite za reporter wa globu ya jamii

    Ankal unatisha, manake umetulieteapicha kbla hata ya ma ripota wa 'mapapa' na 'manyangumi' kufika kwenye tukio.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  21. Poleni mlionusurika katika hiyo ajali.

    Sijui ni waziri wa uchukuzi, sijui miundombinu (wizara nyingi mno, hatuwezi kuzikumbuka) katumaliza. TRL inakufa. Bandari usiseme. ATC nayo kaboeing kake kananyofoka. Ni waziri gani wa miundombinu aliyetengeneza sera zinazotupeleka huku? Wadau naomba kukumbushwa.

    ReplyDelete
  22. US Blogger vipi apate Uraisi na Tanzania hatumuoni kutuwa Hata hapa kwa Ankal tumuone kama kina Mashaka? US Blogger unatuangusha bwana mashabiki wako.

    ReplyDelete
  23. Hapo kweli hata mimi naingiwa na hofu na ubora wa tairi zenyewe zilikuwa katika hali gani maana unaweza kukuta kweli zilikuwa vipara au hata second hand kabisa maana wabongo hatushindwi au zaweza kuwa ni made in Guangzhou, na sikuhizi wamekuwa wabunifu kweli mara utakuta wameandika made in PRC (Peoples Republic of China ila ukijichanganya huchelewi kuambiwa Canada! Kwa jinsi bongo ninavyo ifahamu hakuna kinachoshindikana kwa wenye nazo, si mmeliskia lile sakata la manispaa ya Kinondoni na issue ya matrekta?

    ReplyDelete
  24. HIVI HUU UWANJA SI ULIKUWA UKIFANYIWA MAINTENANCE YA HALI YA JUU JUZI TUU? SIDHANI HATA FIVE YEARS ZIMEISHA!....SASA SIJUI NI NINI KILIKUWA KINAFANYIKA

    JAMANI WATAALAM WAHESHIMU KAZI ZAO NA KUTOA USHAURI KITAALAM, WANASIASA WAACHE KUINGILIA KAZI ZA KITAALAM

    INASIKITISHA KILA SIKU HAO WANASIASA NA WATAALAM WANAENDA NCHI ZILIZOENDELEA KAMA ZA ULAYA NA MAREKANI LAKINI HAWAJARIBU KUIGA YA WENZETU KA WACHINA!

    ReplyDelete
  25. Hiindege haifai tena kwa matumizi ya binadamu. Hivyo msiende kuichomea na kutegemea kurudisha angani. Unajua gari unaweza fix hata likiharibika ni kiasi tu cha kushuka na kuendelea na safari.
    lakini ndege ikigoma huko juu inakuwa ni vilio. Hivyo tukiona Being nyingine inapaa haitakuwa hii

    ReplyDelete
  26. KATIKA UWANJA WA KIA PIA NDEGE YA KLM IMEHARIBIKA KWA KUWA KULIKUWA NA MASHIMO UWANJANI,NDEGE ILIBIDI ISUBIRI MAFUNDI KUTOKA NCHI JIRANI.
    AIBU TENA SKANDALI KUBWA HII ANKALI
    WATU WAWAJIBSHWE KAMA NDIO RUSHWA BASI TUMEKWISHA!!!!!

    ReplyDelete
  27. Kuna tatizo lingine la msingi zaidi ya maji kwenye runway. Mimi binafsi nimeshatuwa mara kibao kwenye runway iliyolowa chepchepe hadi air brakes za ndege zinatifua bonge la wimbi la maji in its wake.

    Kama ingekuwa hivyo wala ndege zisingetumika sehemu kama London na Brazil, ambako mvua ni full time. Na hata biashara ya ndege wala isingekuwepo.

    halafu tusisahau kuwa ndege inapotua, inategemea zaidi air brakes au retrojets kuisimamisha. Matairi yanatumika kiasi, lakini hayana uwezo peke yao kusimamisha ndege.

    Hii ajali ingekuwa ni opportunity ya serikali kuanzisha kitu kama National Transport Safety Board, ambayo ingepewa jukumu la kuchunguza ajali za ndege, mabasi, meli n.k. kwa nia ya kuzuia marudio yake na kupunguza athari ya matukio hayo.

    ReplyDelete
  28. Inawezekana ni hujuma,imesababisha ajali hiyo,kwani juzi tu waongoza ndege walikuwa na migogoro na mwajiri wao juu ya mafao na mambo ya mengine menge,ambayo yawezekana kupunguza moral ya uwajibikaji.

    ReplyDelete
  29. maji hayawezi kuvunja mshikio wa tairi la ndege..engineers na wakaguzi wa ndege inabidi wawekwe kitimoto wajibu waliruhusu vipi iende angani
    I hope investigator wa Boeing wataenda ku-dig root cause of the accident

    ReplyDelete
  30. Ankal, mie nauliza ina maana hizi ndege za ATCL hazina zile ngazi maalum za emergency?mpaka abiria wasubiri nazi ya gari,yaani ankal huwa wanatutsisitiza sana linapotokea jambo kama hili tukimbilie kwenye mlango wa dharura na tukifungua tu hiyo ngazi,ni kama boya fulani hivi linaloteleza kwa hiyo abiria hukaa tu na kwa haraka hufika chini. sumatra nenda haraka angalia hii kabla mathawe hajaitwa na timu yake kuchomea hiyo ndege irudi kazini.unashangaa nini?mbona Gobore(DCM)linachomewa!!!!!!!!!!Bongo tambarare

    ReplyDelete
  31. Si ajabu hii ndege ya kukopi ya mchina

    ReplyDelete
  32. njooni mwanza muone sasa ata uwanja na icho kibanda chake(eti waiting lounge)ilivo kabisa na ndege inapotulia
    kwa ufupi hii ndege ingeenda kupiga break ktk icho kibanda na kuua airport nzima (apa namanisha waiting lounge,offices zote)

    na mwishowe ingezamia ziwani,maana runaway ziko 2 ya nchi kavu-mlimani kabisa na ziwani yani unatua almost juu ya maji
    icho ki-runaway ni nyembamba sana huwezi amini,,,nilishawai semaga umu bloguni huu uwanja sijui wa ndege mwanza ni nini ichi????
    poleni sana wapendwa

    JAMANI

    ReplyDelete
  33. We anony unaemsifia PAILOT me sioni sababu yoyote ya kumsifia ila kinyume chake yeye pailot ndio wa Kwanza kulaumiwa.

    Unaambiwa hata kama umepewa kliarens ya kuruka au kutua na kontol tawa, uamuzi wa mwisho wa kutek akshen ni wa pailot.
    Ni yeye ndio wa kulaumiwa kwa nini alikubali kutua wakati Ranwei ya kutulia imejaa dimbwi la maji?
    Alikuwa na uamuzi wa mwisho wa kukataa kutua kulingana na profeshen yake.

    Nakumbuka niliwahi kupanda ndege moja ya kenya eaweys rubani alipewa kliarensi ya kuruka lakini alikataa kuruka kwani uzito uliokuwa unaonyeshwa kwenye manifesto ulikuwa tofauti na akchuo uzito anaouona kwenye dash bod yake.
    Ndege ilichelewa kuondoka kwa muda wa nusu saa mpaka hilo lilipokuwa verifaid na kuhakikiwa, ndipo alipokubali kuirusha ndege.

    Wa pili wa kulaumiwa ni huyo wa kontrol tawa ya kuongozea ndege-kwa nini alimpa pailot kliarens ya kutua wakati anaona ranwei ya kutulia ina maji?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...