Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa Ridhiwan Kikwete, akimvisha joho Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa Shy-Rose Bhanji ikiwa ni ishara ya kumsimika rasmi kama Naibu Kamanda wa Vijana Kata ya Kijitonyama jijini DSM jana.
Naibu Kamanda wa Vijana Shy-Rose Bhanji akiteta jambo na mgeni rasmi, Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa Ridhiwan Kikwete

Mwenyekiti wa Vijana Kata ya Kijitonyama Ismail Mwenda, akipokea sehemu ya mipira 50 kutoka kwa Mgeni rasmi Ridhiwani Kikwete kwa ajili ya kusaidia timu za soka kwa matawi 9 ya Kata ya Kijitonyama. Mipira hiyo ilitolewa na Kamanda wa Kata ya Kijitonyama Tony Ngombale Mwiru (kulia) na Naibu Kamanda wa Shy-Rose Bhanji ili timu za vijana wa Kata hiyo.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Kusimikwa?? ama kweli kiswahili kinabadilika kila kukicha!!! jamani maana halisi ya neno hili hata sijui nianzie wapi, haya jamani yangu mimi macho!!!!

    ReplyDelete
  2. Hongera Shyrose kwa kusimikwa na Ridhwani.

    ReplyDelete
  3. Hongera sana mama Shyroz maana umetoka mbali umehangaika sana kupata recognisheni na sasa angalau unaona a light at ze end of ze tunnel . nadhani sasa utafikiriwa hata ubunge wa viti maalum au kuteuliwa .

    ReplyDelete
  4. Shyrose hataishia kwenye ubunge tu, bali naweza kutabiri kwamba ataukwaa unaibu waziri .... mwingine ni Imelda Mwamanga; watch this space!

    ReplyDelete
  5. Like Father like Son, Ridhiwani Kikwete, Tony Ngombale Mwiru

    ReplyDelete
  6. Swali: Nimeona wanachama mbali mbali wakisimikwa na wanachama wenzao labda wenye wadhifa fulani ktk chama, je katika mfumo wa uongozi wa CCM ni nani mwenye mamlaka ya kusimika nani?

    ReplyDelete
  7. AMA KWELI NCHI HII YA KURITJIANA< VIZAZI NA VIZAZI??
    ANGALIA MAJINA HAYO JAMA

    YETU MACHO

    ReplyDelete
  8. Udumu ufalme,Tanzania Bara na Visiwani!

    ReplyDelete
  9. Shyrose,
    Katu usikubali kuambiwa kuwa HUWEZI...UNAWEZA!!!!!

    ReplyDelete
  10. NINA COMENT YANGU NDEEEFU SANA KUHUSIANA NA RIDHIWAN KIKWETE LAKINI KUTOKA NA KWAMBA NINA UHAKIKA MICHUZI ATAIBANIA SINA HAJA YA KUPOTEZA MDA WANGU. MICHUZI UBADIRIKE MAANA NIMEPOTEZA IMANI NA WEWE KUMBUKA KWAMBA WATU WANAHAKI YA KUSEMA WATAKALO ILI MRADI HALIVUNJI SHERIA ZA NCHI.

    ReplyDelete
  11. Kaka Michuzi! mbona hujabandika maoni yangu niliyoandika jana kuhusu hao vijana waliopeku na ndala zilizochakaa wakimusapoti SHY ROSE. Bandika hiyo kwani siyo haki kuoneana hivyo.
    Lini viongozi wetu na viongozi watalajiwa watawajali wapiga kula wao.

    ReplyDelete
  12. Sis Shyrose, Sisi tunaokufahamu na tuliowahi kufanya kazi na wewe kwa karibu au mbali tunakupa pongezi za dhati. Endelea na uchapakazi na commitment yako na tunamuomba Mungu Muumba akupe kila la heri. Your bro J. Ngowi.

    ReplyDelete
  13. Mwaka huu sijui yetu macho.....yaani waTZ wanafikiria siasa ndo mambo yote

    ReplyDelete
  14. MICHUZI ANABANA COMMENTS ZA WATU KWA SABABU HII PICHA KAWEKA KUPIGIA DEBE NA KUMTANGAZA HUU DADA HIVYO COMMENTS ZOTE ZA MRENGO WA KUSHOTO ANAWEKA KAPUNI.

    ReplyDelete
  15. hongera dada shyrose tuko nyuma yako

    ReplyDelete
  16. shyroz sasa ugombee ubunge wa jimbo karibu kawe

    ReplyDelete
  17. mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, shyrose tunamkubali kwa sababu ni mchapakazi. Hongera Kamanda. Ushauri wangu kwako shyrose na kamanda tony na wengine waliosimikwa ni kwamba saidieni vijana na isiwe tu ni njia ya kutimiza azma yenu. Tutawapima kwa yale mtayofanya na kama pia hamfai pia tutawakataa ila kwa leo tunawatakia kila heri

    ReplyDelete
  18. dada shyrose kwanza hongera sana kwa kusimikwa unaibu kamanda. pili nataka nikwambie nimekuwa nafuatilia harakati zako sana na ukweli kutoka moyoni mwangu huwa unanifurahisha sana na jinsi usivyokata tamaa bado nakumbuka ushindani mkali sana pale dodoma ulipochuana nafasi ya UNEC na Mhe Londa na hatimaye ukashindwa kwa kura moja! mtoto wa kike huchoki kupambana, kiukweli unakubalika. Endelea na moyo huwa wa ujasiri na iko siku utafika. ni hayo tu

    ReplyDelete
  19. Michuzi kaka hata kama CCM imekufikisha hapo, basi zuga kidogo, post baadhi ya comments za wat, kila mtu mtaani anaongelea hii tabia yako sasa, wabongo wameshashtukia

    ReplyDelete
  20. Ubunge mbona keshapata? Yaani hapo piga ua mwakani yuko mjengoni tena kwa ule wa kuteuliwa bila kuvuja jasho....

    ReplyDelete
  21. ridhwani uko juuuuuuuuu

    ReplyDelete
  22. MICHUZI KUNA NAMNA UNANICHEFUA SANA MAANA NIMETOA KUMENTI KAMA MBILI HIVI NAIPA LIVE FAMILIA YA KIKWETE KUPITIA ridhiwan(HERUFI NDOGO. LAKINI HUZIPOST WEE SI UWEKE TUU UNAOGOPA NINI MAANA HATA WAKIKUFUATA SI HUO NI MTAZAMO WANGU. EBANAEE NAWEWE NIWALEWALE NGOJA NIACHANE NAWEWE

    ReplyDelete
  23. comment zangu zote huyu jamaa anazipiga chini nimeamini kuwa na wewe ni wale wale na kuanzia leo sina mpango tena na hii blog ya wapiga debe wa ccm

    na mwenyewe ni kada na ni usalama wa taifa endelea kubana na hakuna faida kuweka glob hapa kama unabana

    ReplyDelete
  24. HONGERA Shy Rose! Keep up the good work!

    ReplyDelete
  25. SIASA IMEKUWA KIPATIA RUZUKU TUNAJUWA.JITAHIDINI MTAFANIKIWA..HIVI HAWAWANAOINGIA SIASA WAMESOMEA SIASA AU NDIO KURITHISHANA MATAJI???

    KIASI WAIOGOPE DUAL CITIZENSHIP......

    ReplyDelete
  26. hivi baba yako akiwa mwanasiasa lazima na wewe au ukoo mzima muwe hivyo. ona aibu we Ridhiwan tafuta kazi nyingine na si mkumbo kwa baba.
    lazima tukutose tu,we angaika uko mara mjumbe wa nec mara sijui nininini lakin mwisho wa siku tutakuchinjia baharini. ALAAA!!! MNADHANI HII NCHI NI YA KIFALME

    ReplyDelete
  27. hongera shyroz kwa kusimikwa na ridhwan

    ReplyDelete
  28. kaka michuzi asante kwa kutuhabarisha blog ya jamii iko juu asikwambie mtu kitu hongela dada kwa kusimikwa na riziwani. sasa fanya kazi watu wasipate la kuongea

    ReplyDelete
  29. kaza buti dada 2010 ni mwaka wako

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...