Habari bro Michuzi na wadau,
Katiba ya nchi tayari inapatikana katika
tovuti ya Wizara ya Katiba na Sheria
Samahani kwa usumbufu wowote uliotokea, kwa vile ndiyo kwanza na Wizara imeingia katika Libeneke hili.
Tunaendelea kujiweka sawa kadri siku zinavyoendelea.
Mambo mengi tu mazuri yataendelea kuongezwa katika Tovuti hiyo.
Ahsanteni kwa maoni,
Mdau Geofrey Chami

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Safari bado ni ndefu. Nilijaribu jana na hata leo. Ujumbe ni ule ule kama unavyosomeka hapa chini...
    *****************************
    Server not found

    Firefox can't find the server at www.sheria.go.tz.

    * Check the address for typing errors such as
    ww.example.com instead of
    www.example.com

    * If you are unable to load any pages, check your computer's network
    connection.

    * If your computer or network is protected by a firewall or proxy, make sure
    that Firefox is permitted to access the Web.

    *************

    ReplyDelete
  2. Michuzi kuna nyuzzzzzzzzz Jimbo katoliki SAME limepata askofu mpya
    leo mchana

    ReplyDelete
  3. hahahhaha aanze na housegirl wake hahahah na houseboy wake mimi wangu akidai hiyo nitamuomba nimrudishe home kwao tu kwa usalama duh!

    kesho naona watu watazima redio, tv na hawatanunua magazeti maana madada home watakuwa busy kutafuta haki zao poleni wenye ma housegirl na houseboy

    ReplyDelete
  4. Michuzi.. hawa watu bado wana matatizo; Katiba waliyoiweka kwenye tovuti yao ina ibara hadi ya 46 tu!!!

    ReplyDelete
  5. Jamani, mbona inafunguka tena vizuri tu na Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania iliyotajwa hapo inapatikana bila shida yeyote? Labda kompyuta yako ndiyo inamatatizo ama server.

    Saa zingine tuwe tunapongeza hatua za maboresho zinapofanyika. Hivyo, wewe anonymous Fri Apr 30, 01:42:00 PM si kweli kwamba website hiyo haifunguki.

    Mimi tena siko Tanzania lakini nimeweza kufungua bila matatizo kabisa.

    ReplyDelete
  6. Toka mwanzo hadi sehemu ya pili, katiba bado inazungumzia ya Ujamaa na Kujitegemea na syndrome ya Chama (nikiwa na maana ya CCM)!

    Katiba ama uozo usiotakikana kurekebishwa au tufanyayo leo ni yetu tu kinyume cha katiba?

    What a blatant violation of katiba!

    ReplyDelete
  7. Pat-MagazetiMay 01, 2010

    Mimi binafsi nimesoma Katiba ya Tanzania.Inachukuwa zaidi ya masaa mawili mpaka matatu hivi. Kuna vipengele kadhaa lazima wizara ya sheria inatakiwa ibadili. Juu ya Rais wa Serikali ya Jamhuri atalipwa mshahara.Katiba siyo wazi na hakuna mshahara. Pili Attorney General ni Mbunge.Mimi ninaona hii ni conflict of interest juu ya bunge na serikali na waziri wa sheria. Tatu, kama ni mbunge na anaingia kwenye cabinet meeting na hana haki ya kupiga kura to me it does not make any sense. Nne, baadhi tu ya mawaziri wadongo wanaruhusiwa kuingia kwenye cabinet meeting.Mimi ninaona hii ni kosa la kubagua baadhi ya mawaziri wadogo. Haya ni baadhi tu mambo mengi yanatakiwa kuangaliwa upya na kwa undani sana.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 01, 2010

    Binafsi napongeza hatua ya kuwa na hii tovuti japo sina hakika sana na ufanisi wake siku za mbele. Najua mambo yenu Serikali ni yale yale kama zilivyotovuti nyingi za Wizara na Halmashauri, hii nayo anona itakuwa ikitupa mambo ya zamani na ambayo hayatusaidii wananchi. Tunataka mboreshe kazi zenu jamani tena hii Wizara ndi nyeti,lakini siku zote imekuwa nyuma kwa mengi. Hata tovuti ya Mahakama Hakuna, uwezim kupata kesi update za Mahakama zetu, huwezi kupata sheria zote za nchi katika juzuhu update nk.

    Pili ebu mwangalie vizuri sina hakika sana iwapo ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ina tovuti ukienda kwenye link ambayo inaelekeza Attorney General Chambers http://www.agc.go.tz/.

    Unakutana na ofisi ya Mwanasheria Mkuu Zaanzibar...Werema, hii ni aibu! yaani Zanzibar wamepiga hatua kubwa kuliko Bara mpaka wana tovuti makini??.

    Hii ofisi ya AG imevurunda katika mengi, ni wakati sasa wa kujirekebisha na kuweza kuwafikia wadau wake hata kwa kuwa na tovuti ya kutujulisha yale yanayoendelea.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 01, 2010

    NIMESIKITIKA SANA, NIMEHUZUNIKA SANA SANA NA WELOCOME NOTE YA HII TIVUTI... INASOMEKA:

    Welcome to the Website of The Ministry of Constitutional Affairs and Justice where you can read and download the constitution of the United Republic of Tanzania of 1977 in Kiswahili and English language.

    iNAENDELEA:

    The President issued a Notice on assignment of Ministerial Responsibilities (Instruments) vide Government Notice No.20 of February, 2008. This assignment of responsibilities and functions was a creation of the second Cabinet in the Fourth Phase Government. In that functional and structural change, the Ministry of Constitutional Affairs and Justice was separated from the Attorney General's Office.

    The Attorney General's Office is now an Independent Department like the Law Reform Commission; Human Rights and Good Governance Commission; Judiciary and Judiciary Service Commission. All these Independent Departments continue to be serviced by the MoCAJ on all policy issues including Laws Regulations in accordance with existing laws and practices

    MAONI:

    PENGINE MUWE WABUNIFU WA MANENO UNAYOTUMIA KWENYE HIZI TOVUTI JAMANI, HIVI HII TOVUTI YA KISWAHILI AU KINGEREZA??

    jE, NIA LENGO LA TOVUTI NI SAIDIA KUPATA KATIBA YA URT YA KISWAHILI TU AU KINGINE???

    KUNA LINKS NYINGINE ZIMEWEKWA HATA HAZINA TOVUTI KAMA DPP, AGC NK. KWA NINI IPO HIVI??

    HAKUNA HATA TAARIFA MAKINI KATIKA KILA KIELEKEZO, JE, NANYI MMEANZA KWA USINGIZI KAMA ZILIVYO TOVUTI ZA WIZARA NYINGINE ??.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 01, 2010

    Naona mdau Chami na watu wa Wizarani hawakuwa makini katika kufanya design ya hii tovuti hasa kujua mahitaji ya watakaotembelea tovuti (user requirements), shughuli za Wizara pamoja na kukusanya taarifa (content development). Yaliyomo kwenye tovuti ni mambo ya kawaida mno. Hii ni Wizara nyeti sana ambayo ilitakiwa kuwa na a very interactive Web Portal badala ya website ya kawaida kabisa kama hii ambayo haina taarifa za kutosha. Hii sliding pictures kubwa chini ya barner imekula nafasi kubwa ambayo ingetumika kuweka taarifa zaidi. Jamani kuweni serious ili nasi huku nje tutembee kifua mbele. Hata hivyo mna muda wa kufanya marekebisho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...