Jiji la Dar usiku wa kuamkia leo liliripuka baada ya timu ya Inter Milan kuifunga Bayern Munich magoli 2-0 katika mchezo wa fainali ya Mabingwa Ulaya kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid, Hispania.
Furaha ilikuwa zaidi kwenye ukumbi wa Arcade Mikocheni ambao kampuni ya Mabibo Wines Beer and Spirits ambao ni waagizaji pekeee wa bia ya Heineken walipoandaa hafla maalum kwa wapenzi wa soka kuangalia mechi hiyo ya fainali.
Kabla ya mpira kuanza majira ya saa 3:30 usiku, mashabiki walikuwa wakitambiana kila upande ukijinadi kushinda mechi hiyo mhumi na kubwa katika soka kwa upande wa vilabu duniani.
Hata hivyo ilionekana wapenzi wa Inter Milan walikuwa wengi zaidi ukumbini baada ya mshehereshaji (MC) wa shughuli hiyo, Ephraim Kibonde alipoanza kutaja majina ya wachezaji wa timu zote mbili.
Ukumbi ulilipuka zaidi pale Kibonde alipotaja majina ya Samuel Etoo,mchezaji kutoka Cameroon anayeichezea timu ya Inter Milan na pia alipotaja jina la kocha wa timu hiyo Jose ‘Special One’Mourinho .
Etoo ambaye wapenzi wengi wa soka jijini Dar es Salaam wamempachika jina ‘shemeji’ alikuwa ni kivutio kikubwa kwa washabiki hao.
Shabiki mmoja ambaye alikuwa amevalia jezi ya Inter Milan na akiwa na tarumbeta la kushangilia mfano wa Vuvuzela ya Afrika Kusini alisema kuwa kilichokuwa kinamsukuma kuipenda zaidi timu hiyo ya Italia ni kutokana na Etoo kunyanyaswa na kocha wa Barcelona alipoamua kumuuza mwaka jana licha ya kiwango chake kuwa cha juu.
Hata hivyo, mashabiki wa Bayern Munich waliokuwa wakidai kuwa timu hiyo ya Ujerumani ingeshinda, walinywea baada ya Diego Milito kufunga magoli mawili peke yake.
Usiku huo pia ulipambwa na wasanii wengi kama vile bendi ya FM Academia, Lady Jay Dee na bendi yake ya Machozi, mshindi wa tuzo tatu za Kilimanjaro Awards, Diamond, Wanne Star na wasanii kutoka Tanzania House of Talents (THT).
Zawadi mbalimbali kama vile fulana,bia za Heineken na kofia pia zilitolewa kwa watu waliofurika katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Mabibo Wines and Spirits Jerome Rugemalira alisema kuwa kampuni yake inafuraha kuweza kuwa pamoja na wanywaji wa bia ya Heineken katika tukio muhimu kama hilo.
“Huu ni mwanzo tu wa kuwaleta pamoja wapenzi wa mpira wa miguu hapa Tanzania na wanywaji wa bia ya Heineken”, alisema.
Alisema kuwa kampuni yake ina mpango wa kuandaa hafla kama hiyo mikoani siku za baadae.
Bia ya Heineken ni mmoja wa wadhamini wakuu wa Kombe la Klabu Bingwa Ulaya.
Wacha bongo iitwe bongo.
ReplyDeleteunbelievable!
ReplyDeleteYAANI NYINYI NI WAKEREKETWA KULIKO WAITALIANO WENYEWE...KWELI BONGO KAMA MTONI....LOL
ReplyDeletemaajabu na aibu kubwa. Hivi hizo timu zetu tunazisapoti kama tunavyofanya kwa hizi za kigeni????
ReplyDeleteAma kweli mtumwa daima atabakia mtumwa hata akombolewe vipi.
Wenzetu wenye mafanikio katika timu zao huwezi kukuta hata siku moja wanapapatikia timu za kigeni, wao wanathamini vyao hata iwe vipi. Mfano UK, waingereza hawana time ya kushabikia timu za nje na ndio maana wanafanikiwa. Ukikuta watu wanashabikia sana timu za kigeni UK utakuta ni haohao weusi kutoka Afrika.
Ama kweli ni mtumwa ni mtumwa tu hadi kufa!
Nyinyi waTZ hao Intermilan hata wanajua kwamba kuna nchi inaitwa Tanzania?
ReplyDeleteMusijipendekeze kwao bure!
ni furaha tu kuliko timu ya taifa ikishinda,bongo kweli raha sana
ReplyDeleteHivi Bongo kuna mashabiki wa Inter Milan kweli? Au watu wameamua kujifariji baada ya timu zote za England kuangukia pua?
ReplyDeleteHovyooooooooooooooooooooo !!!!!
ReplyDeleteDar wanashangilia nini sasa; sisi kweli ni washamba sana. Mbona wazungu huko kwao ulaya hawajawahi kuuonekana wakishangilia ushindi wa timu yoyote ya Tanzania.
ReplyDeleteNilikuwa sina lengo la kutoa maoni, lakini maoni mengi yaliyotangulia yamenikera.
ReplyDeleteWengi wanasema ni ushamba/utumwa kushangilia timu za nje, kwa hapa.. Inter Milan.
Binafsi sidhani kama ni tatizo, kwa maelezo yafuatayo.
1, Mpira hauna mipaka, na hauna lugha. Watu wengi wanaopenda mpira, wanapenda kuona viwango vilivyo bora, hivyo UEFA Champions League, Ligi za nchi za Ulaya (Uingereza, Italia, Hispania, Ujerumani) ni Nzuri. Na sasa Kombe la Dunia linakuja wapenzi wengi wataburudika.
2, Upatikanaji. Kombe kama UEFA Champions League linaonyeshwa kwenye Tv. Hivyo ni rahisi kwa washabiki kufuatilia na kujenga mapenzi na timu au wachezaji au hata makocha
3, Human nature. Ni kawaida kwa binadamu kuchagua upande. Hata kama kutakuwa na timu mbili zinacheza, hata kama huzijua.. moja kwa moja utachagua timu ya kushabikia.. iwe kwa sababu ya rangi za jezi, au wachezaji wanavyocheza ama chochote..
Kwa sababu hizo tatu, ni kawaida na sahihi kwa mtu yoyote anayependa kiwango, kuwa mshabiki wa timu fulani,,.. hata kwa muda.
Kuhusu ushamba au ukoloni..
Sina hakika kwa nini watoa maoni wamechagua mpira.. wakati naamini kuna waTanzania wengi tu ambao wanaangalia Isindigo, na hizi Tamthilia nyingine za saa 4 usiku.. tena wanafuatilia kwa makini. Tatizo liko wapi, ni kupenda vitu vizuri.
Uwezo.
Watu wenye kuona channel mbali mbali, wanaweza kujenga ushabiki wa kina katika filamu/tamthilia/michezo mbali mbali. Kuna kipindi 24 na Prison Break zilikuwa zinanunuliwa kama njugu, ni viwango tu.
Wapo wanaopenda mpira wa kikapu, lazima watashangilia NBA kwani ndio ligi ya juu kabisa, na mifano inaendelea.
Mwisho
Kama mnataka watu wa nje, washangilie ama wafuatilie michezo yetu, ni rahisi. Tuwe na michezo mizuri, halafu tuifanye iweze kuonekana kiDunia.. wataipenda tu.
Michezo ni global
Kupenda vitu vyenye viwango, ni raha na kawaida
Maisha mafupi, waache raia wafurahie wanachopenda..
Mdau mwenye miwani picha ya kwanza what's wrong with your trouser's zip
ReplyDeletekwendeni huko sasa mnataka tuishangilie taifa stars kwa makombe yapi?? acheni unafiki ndo maana wakati wa world cup uwanja unajaa ina maana washabiki woote wanatokea sehemu hizo timu zinapotokea?? mpira una raha yake bwana na hauna mipaka haki ya nani nimefurahiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii inter kuwanyuka hao wajerumani wasingeitoa manuu tungebeba hilo kombe laivuuuuuuuuu safi sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa mnaokereka kunyweni chibuku mdumishe mila na desturi mvae na magome ya miti manake nguo zililetwa na wazungu nyambaff hamjui msemalo ovyo ni nyinyi msiojua maana ya soka raha ya mpira ushindi babu eeh kama timu yetu haishindi tushangilie hewa na timu zipo??
ReplyDeleteWe Mdau hapo juu unaoutetea huo ujinga ni hivi:-
ReplyDelete1. Kupenda/kushabikia timu ya nje kunaruhusiwa lakini si kwa kiwango kama kilichooneshwa hapo juu cha mabendi, vuvuzela, kualikwa watu na mijezi yao yaani ni shughuli maalum. Kuonyesha upendo ushabiki kwa kutia chumvi zaidi inageuka ulimbukeni na kutothamini vya kwako.
2. Ndio maana hizo Isidingo etc unazosema watu wanaangalia majumbani hawaendi kwenye mabaa mabendi kutumbuiza kuangalia Isidingo.
3. Hapa UK kwa sababu kulikuwa hakuna timu ya UK iliyokuwa fainali watu waliangalia mechi majumbani tu na wachache kwenye ma-pub hata Skysports 3D ilionyeshwa kwenye pub chache ku-compare mechi ya Man U na Chelsea last month.Hiyo yote ni kwa sababu wanapenda vya kwao.
4. Tukiendekeza huo utumwa mamboleo timu zetu hazitafikia viwango vya juu, kwani support kutakuwa hakuna, vizazi vijavyo navyo vitafuata mkondo huohuo.
Tatizo unahitaji kutoka kuja Ulaya sio kutembea ishi kidogo ndio utajua hawa jamaa kwa nini wameendelea ni pamoja na uzaledo wa kupenda vya kwao, sio kwenye michezo tu hata bidhaa madukani wanaangalia British produce nk.
we unaejiita mdau wa uk ungetumia jina lako kamili mnafiki wee kwa nini unatumia kivuli cha uk kama na wewe hujalewa mambo ya ulaya?? nyani haoni kundule acha ufala wewe na aliekwambia kila mtoa comment humu ndani anaishi bongo nani?? unakaa uk ya vichochoroni unajiona uko marekani njoo viwanja vya ukweli ati uk ovyooo ufala umekujaa sina la zaidi tembea uone uk tuu ndo unajionaaaa na bado tutashabikia timu za ulaya kwa raha zetu kama kinakuuma meza wembe
ReplyDeletemdau nyc
ati penda vya kwenu nyoo vya kwetu vimefulia rushwa majungu no maendeleo rudi bongo uje uviendeleze badala ya kuleta pumba zako
ReplyDeletemdau kandahar
Watanzania ni vilaza kweli kweli, ndiyo maana Kenya wanataka waichukue Tanzania hii kwa kivuli cha jumuia ya afrika ya mashariki kwa sababu wanajua tulivyo vilaza wanaoshabikia kila kilicho cha nje na kudharau cha kwetu. Leo hii wakenya wanaheshimiwa kwetu hapa Tanzania na kupewa kazi za maana kuliko watanzania kwa sababu hii hii ya kushabiklia kila kilicho cha nje; watanzania hawawezi kupewa kazi ya maana kenya wakati kuna wakenya pale.
ReplyDeleteMdau wa Mon May 24, 03:39:00 AM
ReplyDeleteUsipoteze mistari muhimu, achana na "waliojilipua" wanaokuja kujifunzia Uzalendo humu!
Kooote na kupanda midege unaona kushangilia soka ndo kukosa uzalendo!