Juu na chini ni Kinyago chetu hicho ambacho kiliibwa na watu wasiojulikana katika ofisi za wizara ya Maliasili na Utalii na baadaye kupatikana nchini Uswisi kwa msaada wa Polisi wa kimataifa (Interpol) na kurejeshwa nyumbani hivi karibuni.
Handsome boy
Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga (kushoto) akipokea kinyago cha kimakonde kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Ladislaus Komba. Kinyago hicho ambacho ni urithi wa sanaa ya nchi yetu kiliibwa na watu wasiojulikana katika ofisi za wizara ya Maliasili na Utalii na kuja kupatikana nchini Uswisi kwa msaada wa Polisi wa kimataifa (Interpol). Hafla hiyo imefanyika leo katika Makumbusho ya Taifa yaliyopo katika mtaa wa Shaban Robert jijini Dar



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2010

    huu ni upuuzi kweli sasa kinyago kimeibiwa wizarani hapo wizarani hakuna ulinzi?mbili hao waliokamatwa nacho walitoa tamko gani?wakati kinasafirishwa kama ni kwa njia ya anga,maji au barabara je hakuna ukaguzi wa mizigo?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2010

    Hakikuibwa wala nini kuna jamaa mmoja alipiga hela fastafasta

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 12, 2010

    mchangiaji wa mwazo kwa nini hujiulizi wewe mwenyewe kwanza ni nini umeandika, jee umesoma habari yote? au ndio kila kitokeacho tanzania ni kichekesho?

    imewekwa wazi kuwa walioiba hawajulikani lakini wewe kichwa maji unataka kujua waliokamatwa nacho wanasema nini? sasa kama wangelikuwa wamekamatwa si ingelikuwa wanajulikana hapo? duhhhh! ama kweli akili ni nywele!!! toba yarabi.

    ReplyDelete
  4. NdumbaNangaeKamosingaMay 12, 2010

    Michuzi ukibania komenti yangu nitakuroga kwa kugeuza upande wa nje wa sura yako uwe ndani na wandani uwe nje.

    Nina maswali mawili ya msingi

    (a) Kinyago hiki ni sura ya nani? Maana nikangalia kwa mbali naona sura ya binadamu nikiangalia kwa ukaribu ni mbwa kwisha kazi. Swali la nyongeza; Tz tunafaidika vipi na sura ya mbwa-mtu huyu?

    (b) Ashakhum si matusi, Anko supu mbona kinyago hiki kwambaali kinafanana na picha ya mtu aliyevaa shati la pundamilia iliyo kulia juu kwa blog yako. Swali la nyongeza, Je una mafikirio gani endapo kinyago hiki tukikivalisha the fulanaz na kufanya kiwe nembo (logo) ya blog hii?

    Utanisamehe, kitimoto kisichoiva vizuri na laga vinasumbua sana mpangilio wa mawazo ya kufyatua keyboards

    ReplyDelete
  5. Mume Wangu, Mikanjuni TangaMay 12, 2010

    Kinafaa sana kuwanyamazisha watoto wanaopenda kulialia ovyo.
    Teh Teh Teh!!!!

    ReplyDelete
  6. Matari, New Albany - OhioMay 12, 2010

    Hiki kinyago kimefanana sana na Mjomba wangu yule msanii maarufu

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 12, 2010

    nakubaliana na anon wote hapo!kweli kama kiliibwa walokamatwa nacho kwa niniwasishikwe?haki vitu vingine vinatia hasira!!!!!upuuzi mtupu bora hata wasingefanya show ya kukipokea wangapoikea tu kimya kimya!!dili hilo mtu alishakula hela yake fastafasta kweli hapo!!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 12, 2010

    ha ha haaa uuuwiiiii bongo kuna ishu kali acheni tu!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 12, 2010

    Kiasi gani cha pesa kimetumika katika makabidhiano ya kinyago "kilichoibwa" kutokana na uzembe?

    Mzee wa busara.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 13, 2010

    Teh teh teh teh! haki ya nani! kwenye hii blog kuna watu wamedata ni hakuna tena! kiti moto kisichoiva na......! utulivu sifuri!

    ReplyDelete
  11. Pangu Pakavu Hali NgumuMay 13, 2010

    Ukweli ni kwamba kinyago hiki kiibiwa kwa msaada mkubwa wa wafanyakazi wa Maliasili(Makumbusho)mwaka 1984 na kuuzwa kwa TX ambaye naye alikiuza kwa mnada huko Uswisi na wakakiweka katika Makumbusho yao.Ila gharama iliyotumika kukuleta kinyago hicho ya ujumbe wawatu zaidi ya 10 kwa siku 14 na sherhe za kukikabidhi huku ikioneshwa kwamba kiliibiwa kwa uzembe ni AIBU ya mwaka na wala sio ushujaa.Pia mijusi iliyoko Ujerumani kwa nini isiletwe kwa gharama zozote hapa nchini mbona TZ inapoteza fedha nyingi kwa ziara za Wkuu wa nchi na wappambe wao bila manufaa yeyote?

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 13, 2010

    Sisi watanzania ni wa ajabu sana yaani tunakaa kushabikia kurejeshwa kwa kinyago kilichoibwa, vipi kuhusu yule mjusi aliepo Ujerumani ambae angeweza kuwa na manufaa zaidi.
    Halafu tujiulize ni rasilimali nyingi kiasi gani inayoibiwa hapa kwetu kuanzia Madini,Ardhi,Fedha n.k ingefaa na hivi vyote virudishwe.
    Jamani amkeni (TUSIWE WAVIVU WA KUFIKIRI)

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 13, 2010

    Haya makabidhiano nayo yalitaka sherehe?

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 13, 2010

    HONGERA MH.SHAMSA KWA KUWEZESHA KINYAGO CHETU KURUDI JAPO KILI OVERSTAY,HIVI KILE KICHWA CHA SHUJAA WA WAHEHE MKWAWA KILICHOPELEKWA UJERUMANI VIPI HABARI ZAKE?KILISHAREJESHWA AMA BADO?NA VYURA WETU WA KIHANSI NAO JE?WAMEREJEA TOKA MAREKANI?NA ARUSHA KUNA KITU WAZUNGU WALIKICHUKUA JAPO SIKUMBUKI NI KITU GANI WANAOFAHAMU MSAADA TUTANI,JE KIRIRUDI?

    sayz mwajiri mkuu

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 13, 2010

    Watanzania tunachekesha sana, who cares kuhusu hicho kinyago?? kuanzia huyo waziri anayechekelea, prezdaa mpaka mkulima wa chini kabisaaa. By the way, kimerudishwa sio kwa juhudi zetu hata tone, ni hao hao wazungu ndo wamepiga kelele na sisi tukaonyesha tunajali. Na huko kujali kumekuja kisa tu kuna vi-allowance vitapatikana kwenye kukirudisha etc. Nishachoka mimi...

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 13, 2010

    KINYAGO HIKI KILIUZWA KAMA AMBAVYO VILIVYOUZWA VITU VINGINE TOKA MAKUMBUSHO YA TAIFA NA HAUKUNA AHTUA ZOZOTE ZILIZOCHUKULIWA KWA WAHUSIKA.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 13, 2010

    kiswahili kimenipita kuna wadau wameongela mijusi? ni mijusi gani hii na ina faida gani kwa tanzania?

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 13, 2010

    Hivi hiki kinyago kama kingebaki huko huko kulikuwa na hasara gani??? Maana nafikiri gharama za kukichonga kwa wachonga vinyago pale Mwenge au Bagamoyo ni kama shilingi laki moja na ushee, hivi ni kweli hakuna kabisa kabisa watu wengine wa kuchonga vinyago mithili ya hicho au kilikuwa na alama pekee ambazo tusingeweza kupata kinyago kingine kinachofanana na hicho!! Sikatai kwamba ni urithi, lakini hatujaambiwa ni watu wangapi hasa waliokwenda USWIZI kukichukua na wametumia shilingi ngapi kukileta BONGOLAND, pia isije ikawa hakikuwa kwenye luggage allowance...!!! Teh. Teh. Teh.

    NB(Michuzi naomba uwape wadau wa blog hii taswira ya uharibifu wa bababara ya kwenda Arusha kutokea Dar hasa maeneo ya Korogwe mpaka Mombo n.k., kama mgongo wako si imara kwa sasa usipite barabara hii)


    Nkyabo

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 13, 2010

    jamani tz kuna mambo, sasaa hicho kinyago jamani ndo kinarudi na kufanyiwa sherehe ? na msimlaumu huyo aliyeuliza kwanini hajakamatwa aliyekiiba mkamwambia hana akili , anazo akili kwani hicho kinyago hao waliokirudisha walikiokota huko ulaya ? si wamekikuta sehemu then aulizwe yule kakipata wapi , KAMA HUKU BONGO UNAISAIDIA POLISI (UKIWA RUMANDE )

    ReplyDelete
  20. Halafu na hizo GLOVUZ walizovaa mikononi ni kwa ajili gani?

    Sasa kama kinyago ni kichafu au kinatia kinyaa walikirudishia nini sasa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...