Kiongozi wa Marian Healing Faith Centre cha River Side, Ubungo jijini Dar, Fr. Nkwera akisalimiana na viongozi wakati wa sherehe hizo mwezi juni mwaka jana
mama Maria Nyerere akimwagilia mti ambao ameupanda katika viwanja vya Kanisa la Namugonga nchini Uganda nje kidogo ya jiji la Kampala. hii ilikuwa Juni mwaka jana
Rais Museveni akimkaribisha Mama Maria Nyerere shereheni huko Namugogo. Chini akimwagilia mti alioupanda kama kumbukumbu ya siku hii

Na Paulo Malimbo wa
Globu ya Jamii, Namugogo,
Hizi ni baadhi ya picha za mchakato wa kumuombea baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere kuwa mwenyeheri na baadaye kuwa Mtakatifu. Kisheria na tofauti na ilivyoripotiwa awali, mtu hawezi kuwa mtakatifu kabla hujawa mwenyeheri.


Rais Yoweri Museven wa Uganda alisema kuanzia sasa (last year 2009) kila June mosi itakuwa siku ya kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ili aje kutangazwa kuwa Mwenyeheri na hatimaye kuwa mtakatifu.



Hivyo hajatangazwa kuwa mtakatifu na mtu yeyote hapa Duniani. Kilichopo hivi sasa na ambacho pia kitakuwepo Jumanne ambayo ni June mosi katika Kanisa la Namugongo nchini Uganda na ambapo marais mbalimbali wanatarajia kuhudhuria, kama siyo wawakilishi wao, Ibada hiyo ni kuomba mchakato wa kumfanya baba wa Taifa kuwa Mwenye heri na hatimaye Mtakatifu.


Familia ya Mwalimu Nyerere imeondoka Tarehe 28 kwenda kuhudhuria misa hiyo ambayo itafanyika June mosi na baadaye ibada kubwa ya hija ambayo itafanyika hapo hapo Namugongo. Namugongo ni eneo la hija ambalo lilitumika kuwatesa mashahidi wa Uganda 22 ambao waliuawa kwa kuchomwa moto na kukatwakatwa mapanga.


Kwa sasa maelfu kwa maelfu ya watu wamekuwa wakienda katika eneo hilo ili kuhiji wakitokea Ulaya, Kenya, Rome, Tanzania, Sudan, Rwanda, Burundi, Congo na kwingineko duniani. Wale walioko katika mikoa ya karibu nchini Uganda pamoja na nchi jirani za Rwanda na Kenya wamekuwa wakienda eneo kwa kutembea kwa miguu kutokea nchini mwao.


Mama Maria Nyerere yuko Namugongo akiwa ni sehemu ya wanahija ambaye ameongozana na wanamaombi wa kituo cha Marian Healing Faith Centre cha River. Aliyeanzisha mchakato wa kumuombea Baba wa Taifa kuwa Mwenye heri na hatimaye kuwa Mtakatifu ni askofu wa Jimbo Kuu la Musoma.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2010

    Huyu m7 ni mnafki, anatumia jina la nyerere kama ngazi ya kuwa rais wa afrika mashariki, watanzania hatudanganyiki

    ReplyDelete
  2. Namtakia kila la heri Mwalimu. Ni heshima ya pekee kwa nchi yetu kuwa na mtanzania katika mchakato wa kuwa mtakatifu.

    Mdau
    Faustine
    http://drfaustine.blogspot.com/

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 31, 2010

    Blog ya Jamii Hoyeeeee? Asante kwa kuripoti habari za utakatifu wa Nyerere. Si mlitangaza juzi kuwa Nyerere atatajwa mtakatifu Kampala mwezi wa Juni mwanzoni?. Sasa imekuwaje tena au na mafisadi nao wameingilia hiyo process? Michuzi tueleze kwa sababu tunawaogopa sana hawa mafisadi siku hizi

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 31, 2010

    issa usinibanie hiyo msg yangu ya awali pls. thnks

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 01, 2010

    mimi ni mkristo na pia nampenda na kumuheshimu hayati baba wa taifa but hili swala la kufanywa mtakatifu linanitatiza kabisa. kwa kipi cha kitakatifu au cha ajabu sana alichofanya jamani? mbona mnataka kuutia doa ukristo sasa. am very sorry kama nitawakwaza but utakatifu nooo, haliingii akilini kabisa,

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 01, 2010

    Petition for Beatification, then later Canonization. So Nyerere has to be beatified then if he deserve he will be canonized. Tuendelee kumwombea ili tuweze kushuhudia au kuthibitisha miujiza yake itakayopelekea kutangazwa mtakatifu. Jamani inafanyika Uganda sio kwa sababu ya Yoweri Museveni hapana,ni kwa sababu Uganda kuna historia ya wafia dini(Uganda Martyrs) ambao kati ya mwaka 1885-1887 waliuawa kwa kuchomwa moto wakitetea imani yao ya Ukatoliki na Anglikan. Kati ya hao mashahidi 25 alikuwapo Mtanzania mmoja aliyeitwa John Maria Muzeeyi ambaye aliuawa kwa kukatwa kichwa na sehemu kilipodondokea hadi leo kuna chemchemu ya maji ikiwa imetengeneza rammani ya Tanzania , chemchem hiyo wakazi wa jirani hutumia maji hao kunywa na kama dawa ya magonjwa mbalimbali. Pope Benedict wa XV ndiye aliyewatangaza wafia dini hao kuwa wenye heri(Beatified) mwaka 1920 na baadaye mwaka 1964 Papa Paul VI aliwatangaza watakatifu.So wakatoliki wengi toka sehemu malimbali Duniani huenda kufanya hijja kila mwaka hasa mwishoni mwa mei na mwanzoni mwa juni.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 01, 2010

    Bigg upp to all Ugandans. We've been & we'll always be friends. With EAC we'll learn Kiganda & you guyz learn just Swahili. Don worry if each one of us cant "English is there. These are things to write not PUMBAVU KENYAN who is interfearing people internal affairs.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 01, 2010

    KAAZI KWELI KWELI

    HONGERA PEKEE KWA YULE RAIS ALIEINGIA MADARAKANI NA KUTANGAZA KUWA WATU WASITUMIE JINA LA MTUKUFU RAIS PINDI WATAKAPOMTAJA JINA

    KWANI HAMNA MTAKATIFU WALA MTUKUFU AMABE ATAKAEJIPA MWENYEWE AU KUPEWA NA WATU UTUKUFU HUO

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 01, 2010

    Hakuna sababu ya kufikiria mengi juu ya mchakacho wa kumfanya Julius Kambarage Nyerere kuwa mtakatifu, ila ni dhima ya kanisa kwa mwanakanisa anapokuwa na mwelekeo wa maisha unaokuwa mfano mzuri wa kuigwa na wengine. Hivyo ridhaa ya Mungu kama ataridhia hivyo inabaki katika kumbukumbu ya maisha ya kila siku katika kanisa na wengine kuiga mfano wake wa maisha .
    Hata wanamichezo hupewa kipa umbele wale manju kuwa mfano wa kuigwa na wengine wanaofuata, sasa iweze watu tushangae hayo?

    Kanisa katoliki lina utaratibu maalum katika hayo na lazimna kuwepo jopo linalokubali na linalopinga na huhitimishwa kwa Mungu anayeweza toa ufunulio wa pekee wa kumwonyesha mtarajiwa kuwa ni mtakatifu.

    Ndio maana huanzia na zoezi la kwanza la beautification (kufanywa mwenye heri) hatua ambayo tunaisubiri na kuomba Mungu mdhihirishe hilo. Baada ya hapo ndio ushuhuda zaidi unahitajika ili awe Canonized (kuwa mtakatifu).

    Kwa mantiki hiyo kuna kanuni na sheria za kanisa zinazofuatwa, na kuna wengi wamefanyiwa hayo hawajatangazwa na kuna wanaotangazwa. Na pengine huchukua miaka mingi sana.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 01, 2010

    Jamani it seems wengi hawajui package ya Presidency. Nyerere did so many good things to many. He also did so many bad things to others. In those days he said is for the benefit of many. For example, he created and trained freedom fighters. To them he was a hero, but to those who faced bombs and bullets saw him as a bad person. The fact remains, he did hut few in the process of komboa wengi.

    Tanzania is one of the few countries that created concentration camps and put its citizens. This happened when he was president. He misplaced thousands of people in Bassotu and created a wheat farms, he never cared about where those people would go. Those who resisted were shot and their cows hit by cars. S good number of women were raped. Others were sent to concentration camps. In one of the events, a teenager was forced to have sex with his mom. All these happened following his orders. He did nothing to stop and the farms became operational. When citizens went to court and won against the government, he fired the judge, put another judge and the government won.

    Now you tell me he is what???? Mtakatifuu???? Give me a break!!!!

    There are so many bad stories about him. One could argue that he had to do those things because of his position as a president. I agree. But he then loose the credibility of becoming a saint, because of his position, as a president.

    I think he should be left to rest in peace.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 01, 2010

    Dummies! Did he put people on detention? Did he kill? Doesn't mean if is one or many? Do you know how many life he screwed? Ask Kassanga Tumbo, Kassela Bantu, Oscar Kambona etc. His inner circle said about him? USIOMBE NYERERE AKAKUSHOA KIDOLE. Watakatifu never done any of that. So this will never go anywhere besides Uganda where M7 wanna 15 minutes of fame using his name.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...