Nakaaya Sumari akihurubia katika harakati zake za jamii

Na Woinde Shizza
wa Globu ya Jamii

WAKATI vuguvugu la uchaguzi mkuu likiendelea kushika kasi nchini mwanamuziki wa maarufu wa kizazi kipya nchini,Nakaaya Sumari ameamua kujitosa katika kinyang”anyiro cha kuwania ubunge wa viti maalumu mkoani Arusha kupitia chama cha demokarisia na maendeleo(Chadema) kwa kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo mjini Arusha.

Nakaaya ambaye ni katibu mhamasishaji wa baraza la vijana wa Chadema wilayani Arusha alichukua fomu ya kuwania kiti hicho juzi katika ofisi za chama hicho zilizopo maneeo ya Esso jengo la Meru Plaza mjini Arusha.

Akiwa ameongozana na mwenyekiti wa vijana wa Chadema wilaya ya Arsuha.Exaud Mamuya sanjari na katibu wa vijana,Arnold Kamnde,mgombea huyo alichukua fomu ya kuwania kiti hicho majira ya saa 3;30 asubuhi katika ofisi hizo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kuwania kiti hicho Nakaaya alisema ya kuwa binafsi anahisi ya kuwa nafasi ya yeye kuwa mwakilishi wa wanawake wa mkoa wa Arusha katika bunge la jamhuri nchini kupitia chadema mkoani Arusha umewadia.

Nakaaya alisema ya kuwa lengo kubwa lililomsukuma kuwania nafasi hiyo ni kutokana na uchungu alionao hususani mateso wanayopata wakinamama katika masusla ya afya ya uzazi katika huku akihaidi kusimamia masula ya afya ya uzazi kwa wakianamama nchini.

“nahisi muda umefika wa kutenda ninayoyahubiri siku zote,nataka nikasimamie matatizo ya uzazi kwa wakinamama hili linanipa uchungu katika maisha yangu siku zote”

“nataka nikawawakilishe wnawake wa mkoa wa Arusha kupitia chama changu nina imani nitashinda nafasi hii kwasababu ninajiamini, hivyo naomba mniunge mkono wanawake’alisema Nakaaya

Awali akimkabidhi fomu ya kuwania nafsi hiyo katibu wa Chadema wilayani Arusha,Bakari Kasembe aliwataka wanawake wote wa mkoa wa Arusha kupitia chama hicho kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi hiyo.

Kasembe alisistiza ya kuwa awali chama chao hakikuwa na uwakilishi wa kiti hicho mkoani Arusha katika bunge la jamhuri nchini lakini wakati huu wamejipanga kutoa viti vitatu na kiti cha ubunge wa Arusha mjini.

Tayari joto la kuwania nafasi ya ubunge wa viti maalumu mkoani Arusha kupitia chama hicho limeanza kushika kasi ambapo hadi sasa tayari wagombea wawili wameshajitokeza kuwania kiti hicho ambao ni Magreth Olotu na Joyce Muya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2010

    I dont think this is a good idea to her, she does have that charisma. She better concentrate, use that energy and resourses on musick industry. Jicho alompiga huyo dada aliyekaa hapo linaeleza kila kitu.

    All in all, Gudluck.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2010

    Duh!!!!! na mimi nagombea

    ReplyDelete
  3. Kwa mara ya kwanza mbunge atatoa album.

    bajeti ndani ya album featuring Rais.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 29, 2010

    Anony hapo juu umesema kweli tupu! ili kwenda bungeni lazima uwe na nia ya kusaidia watu, na sio kupeleka usanii mjengoni!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 29, 2010

    NAKUSIFU SANA DADA.WEWE UMEONYESHA UKWELI.UMEONYESHA SIO MNAFIKI.WENGINE WAMEVAA NGUO ZA CHAMA FULANI KWA UNAFIKI ILA WEWE UNAPENDA KWELI KUSAIDIA WANANCHI.SIO WASANII WENGINE NI PESA INAWASUMBUA WALA SIO KUWAONYESHA WATU UKWELI KAMA NI CHAMA KIPI SASA HIVI NI ANGALAU.MUNGU AKUBARIKI DADA.
    MDAU USA

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2010

    Big up dada keep on usihofu kitu mungu yu nawe hadi mwisho

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 29, 2010

    ooh politician this politician that kumbe na yeye humo humo, dada imba nyimbo siasa hazikufai

    ReplyDelete
  8. yellowbone babyMay 29, 2010

    naakaya, hongera sana, mpenzi,,, yaani nimefoli in love na wewe, na us bloga, namchukia mashaka sana, yaani simpendi kweli, na akiingia tu kwenye siasa, tunaanzisha ka blogu ketu kumtoa nishai, hana adabu, mami umependeza kama kawa, endelea, tu ubunge utapata, siyo tupo, nikija bongo tukutane level 8 kmempinsiki. kila la kheri

    yellobone baby (h-towni)

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 29, 2010

    mpaka sasa tumewasikia wadau wawili hapa wanagombea ubunge mwaka huu, US Bloga na Nakaaya.

    Tunamsubiri na Mashaka ajitangaze.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 29, 2010

    makubwaaaaa
    najutaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 29, 2010

    AMINIAAAAAAAAAAAA@ NKAYA UR FRIEND UNGEEND CCM UNGENIUDHI

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 29, 2010

    Sawa kabisa na hongera sana!
    Lakini ujuwe kabisa NIDO bungeni mwiko!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 29, 2010

    A way to Go...Congratulations

    Lazima tuwaondoe mafisadi wote...lakini jina la baba kama naye alikua mmoja wa wafisadi au...Hili jina sijui nimelisikia wapi vile

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 30, 2010

    badilisha na mavazi dada. siasa na ujana haviendani.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 30, 2010

    nadhani inabidi abadili namna anavyovaa, kuonyesha kifua chake namna hiyo haitomsaidia kwa watu kuwa yuko serious, na unless anataka kujipatia hicho kitu kwa kutumia her sexuality, she better cover up a bit.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 30, 2010

    ah hha "Miss Politician" ah ahah kaazi kweli kweli!

    Mama sasa hilo nyonyo bungeni jamani!

    I wish you the best, but remember your song and live it!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 30, 2010

    thanks nakaya for your spirit keep it up ili iwe changamoto for young girls who need change in this lovely country ambayo imekuwa hijacked na mizee isiyochoka na mawazo yao ambayo yamelala ukifanikiwa mama nitakuomba jambo moja tu pls usafiri wa wanafunzi jibu litoke wapi? shule nyingi za kata zimefunguliwa lakini hajafikiri hao watoto wataenda vipi shule.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 31, 2010

    All the best.

    Tutakutana Bungeni Mola akipenda.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 31, 2010

    this is ridiculous ,we ANONY WA HTOWN , how can you even say I hate MASHAKA DO YOU HAVE ANY CLUE OF HOW AND WHAT HE DOES FOR THOSE IN NEED, YOU ARE BEYOND IGNORANCE,AND REALLY CANT EVEN BLAME YOUR EMPTY BRAIN.WHAT HAVE YOU PERSONALLY DONE TO MAKE THE WORLD A BETTER PLACE???????????

    FREE KNOWLEDGE: a word HATE should be omitted in your vocabs it reflects such shallowness in you character

    YOU AS A WOMAN HAS AN OBLIGATION TO APPLAUSE ANY WOMAN ESP. BLACK WHO STANDS UP FOR SOMETHING POSITIVE. IT IS HOW WE AS WOMEN TODAY GOT TO WORK OUTSIDES OUR HOMES,GOT TO SIT IN OFFICES,UNIVERSITIES---. AND GOT OUR NEEDS REPRESENTED AS CITIZENS AS OPPOSE TO 2ND CLASS CITIZENS. YOU HAVE TO KNOW THE HISTORY TO APPRECIATE THE PRESENT.

    NAKAYA, I KNOW IT IS INSIDE YOU,KEEP UP THE GOOD HEAD,WHEN POSSIBLE FIND TIME TO ATTAIN MORE KNOWLEDGE I HAVE LISTENED TO YOU BEFORE, YOU ARE WELL ROUNDED JUST BUILD FROM IT WE ALL NEED MORE,
    YOU WILL DO WONDERS.
    LOVE T.T.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 31, 2010

    Hayo ma-apple vp mheshimiwa!? jifunze basi kukaa kiheshimiwa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...