Samuel Andrew Mbwana a.k.a Braton
nikiwa mitamboni Backyard Records
Hii ni kwa wasanii wote wanao fanya music wa aina mbali mbali wenye kueleweka na kuleta maana, kueleweka na wenye maadili kwa watanzania wote.

Nimeona nitoe offer hii ili mradi wasanii wapate nafasi ya kutosha katika kuelimisha jamii kuhusu uchaguzi wa amani, faida ya kupiga kura na kuelimisha jamii kuhusu viongozi wanao tufaa katika jamii.

Naomba wasanii wajitokeze ili elimu na ujumbe ufike kwa jamii. Wasanii wa mikoani wanaweza kupiga simu au kuandika barua pepe kwanza ili kuwapa booking kabla kwa kuwaondolea usumbufu wa kusubiria ratiba. Hii isiwe kwa wasanii kupata nafasi ya kumuimba kiongozi flani au mtu flani hatufai hapana sina dhumuni la kutengeneza nyimbo kwa ajili ya chama flani au kiongozi flani kwa jina lake.

Vile vile ipo nafasi ya vyama vinavyo pigania haki, katiba na uratibu wa uchaguzi kuwapa nafasi pekee ya kurecord chochote kuhusu uchaguzi kama matangazo, michezo au hata nyimbo tenzi na ngonjera zinazo husu uchaguzi.

Offer hii ni kuanzia tarehe 01June2010 hadi 01August2010, ila wasanii wajiandae vya kutosha kwani sina lengo la kumfundisha watu au mtu kutaka kujaribu kuimba tu kwa sababu amesikia ipo nafasi ya kurecod bure. HPANA! Naomba nafasi hii iwe kwa wasanii wanaojua kuimba na wenye mazoezi ya kutosha na wawe na nyimbo zilizoandaliwa kwa ufundi zaidi ambazo zitapata nafasi katika media zote.

Backyard Records inawajali watanzania na ndio maana tumeamua kutoa nafasi hii wakati muwafaka ambao watanzania wanahitaji elimu na hamasa kuhusu uchaguzi. Tupo Magomeni Moroko hoteli Mchinga A. Street barabara ya Kawawa na Uzuri Road.
simu +255713888779
Wenu
Samuel Andrew Mbwana (Braton)
Producer Backyard Records.
Braton akiwa na QJ na Kibe studio za Backyard Records

Braton (kati) akiwa studio na Nas G (shoto) na Darkmaster


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2010

    Vipi Bai yupo ?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2010

    dah una uzalendo wa kweli katika kuhamasisha uchaguzi na imani utafanikiwa kwani ni mfano mzuri sana katika jamii mtanzania halisi
    HONGERA.....
    mdau napoli italia

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2010

    Big up!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 29, 2010

    Nikiwapa $12,000 mutaweza kunitengenezea nyimbo 5 kwa ajili ya kampeni yangu?

    Wenyewe mutatafuta muimbaji na mengine.Nyimbo 3 ziwe katika style ya Bongo flavor na 2 iwe katika style ya rusha roho.

    Yaani mufanye kila kitu from A-Z, mimi nawakabidhi mikwanja na nyinyi munanipa mziki pamoja na hatimiliki zinakuwa zangu.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 29, 2010

    misifa dot com!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2010

    Sat MAY 29,03:42:00AM
    Kiswahili chakushinda alafu unatuletea ubishoo wako kampeni yangu...MUTAWEZA, MUNANIPA cha wapi hicho Lindi au Ntwara he he he contact si katoa au unatuletea ujivuni wako na kodi zetu? shame on u

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 29, 2010

    Burton safi sana. Umenikumbusha Usagara. Keep it up

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 29, 2010

    Hao vijana wahuni tu. Hakuna lolote!! Nawafahamu sana. Vifaa vyenyewe walivyopiga navyo picha wameazima. Halafu leo hoo tunarekodi nyimbo za kampeni bure. Acheni kuzengua watu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 30, 2010

    wewe UB BLOGGER kumbe ule uchaa wako bado haujakuisha!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...