Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahimu Lipumba akichukua fomu za kugombea nafasi ya Urais kutoka kwa Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Kinondonio, Mh. Kassim Chogamawano katika ofisi za CUF wilaya ya Temeke jijini Dar leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2010

    Anataka kugombea u-rais tena?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2010

    Huh ama kweli bongo tambarare..!! Inakuwaje mtu amegombea urais mara mbili mfurulizo anashindwa kwa kishindo, anapewa tena nafasi ya kugombea urais huo huo, tena ndani ya chama hicho, ina maana hakuna watu wengine wenye sifa za kugombea urais kwenye hicho chama au ndiyo "privatization and monopolization of leadership" huu?.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2010

    jamani ni anachukua fimu toka kwa katibu wa wilaya ya kinondoni kwenye ofisi za wilaya ya temeke?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2010

    safi sana prof napenda sana watu wasiokata tamaa kama wewe ipo siku utafanikiwa hata prof mwenzio Atter Mills rais wa ghana aligombea vipindi 3 akashindwa akaja kuibuka kidedea kipindi cha nne chapa mwendo baba tuko nyuma yako

    ReplyDelete
  5. Yes my Ripu ripu!wewe ndio pekee uayefaa kuwa raisi wa nchi yetu hao wengine upuuzi mtupu i hope the will understand you and give the post.ni uchaguzi kuwa wa haki tu.Na wewe unaechukia asigombee hukuambiwa umchague ccm ipo pigia hiyo.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2010

    Wewe unayejidai anagombea urahisi mfululizo na kushindwa unajua katiba yao inasema nini???Hebu kaa kimya huko kama hujui kitu nyamaza...Mbona akigombea Ralph Nader hufungui mdomo na kupeperua kizabina zabina hapa...Kuwavunja moyo watu wasiojua mambo waanze kusema tu...

    We fully support you Professor for doing such thing...

    Tunahitaji watu wengi wa kuchallenge CCM...Nchi inayoongozwa na chama kimoja miaka nenda rudi haitaendelea milele...Ni kama ukingship fulani hivi kupasiana uongozi ndani kwa ndani....

    Nakumbuka kabla Kikwete hajawa raisi, Mkapa alikuja hapa NY city na kati ya watu aliokua nao wakati huo alikua kikwete pia. Na pale kwenye mkutano alitwambia huyu ndio atakua kiongozi wenu mwakani. Na wakati huo uchaguzi ulikua hata haujaanza but they already knew the next president...Sigh...Kura zilikua za kuhalalisha tu


    Halafu utume comment yangu kwenye kapu

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 05, 2010

    This is a joke. This man disappeared, we haven't heard much from him for the past five years only to reappear during general election. You don't have my vote. Good Luck!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 06, 2010

    Sasa mtu kama huyo akishaupata Urais kisha kubadilisha mihula ya mtu kuwa Rais kuwa mitatu mtamshangaa kweli?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 06, 2010

    FALSAFA YA FUNGU LA NYONGEZA;
    "FFN": Kawaida wauuza matunda na mboga za majani, uweka fungu la nyongeza. Kwaida ukichunguza fungu hili kwaida tunda au mboga huwa inayo walakini au katika dakika za mwisho kuelekea kwenye pipa la takataka, . Wauza nynya fungu hili uitwa masalo. Wakina Lipumba na Mwenzake Seif hivi sasa wapo katika kundi la "FUNGU LA NYONGEZA. Ndiyo watapata Ruzuku, walau kunganga njaa: Kama kundi la Mrema, na Mbowe: Lakini katika uhalisi wa Siasa hawataleta changamoto inayotakiwa katika Sisa kwa sasa. Tuna Chama tawala ambacho kinfanya madudu, ingawa nacho ni Fungu la "Nyongeza" lakini bado hakijapata changamoto ya watu wenye moyo na kupenda nchi kuweza kufanya mapinduzi ya kweli; Basi sasa SISA zetu wangombeaji ni wengi ni Fungu la Nyongeza; Wapo kwa ajili ya kulinda masalai binafsi au wasiwekwe kwenye Pipa ..... CUF, CHADEMA na vyama vingine wekeni watu Makini katika Nafasi za kuongembea, na si wanganga Njaa! Kweli adui yako mwombee njaaa

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 06, 2010

    Hivi kugombea URAISI NI SIFAAAA? AU ANATAKA PESA ZA KAMPENI TU NJAA KALI.
    DUH ATASHINDWA URAISI TENA ILA ATAFAIDIKA NA PESA ZA KAMPENI YA URAISI YEYE NA CHAMA CHAKE.
    MJINI SHULE,HIYO NDIYO BONGO LAZIMA UTUMIE AKILI KUPATA PESA.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 06, 2010

    Huyu naona hata akipata urais atbadili katiba ili aendelee bado tuuuu,mtu mzima embu ona vibaya waachie vijana sasa

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 06, 2010

    alijisimeaga baba wa taifa huyu jamaa ana moyo kama wa mwendawazimu moyo ucokatata tamaa kweli bongo tz tambarare bwana yaani jamaa uroho umemshika vibaya sana

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 06, 2010

    tumekuchoka mzee

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 06, 2010

    Si kwamba Bongo ni tambarare...bongo tuna matatizo ya Ubongo. What in the world Lipumba is going to offer after losing uncountable times???

    Jamani kwanini vichwa vyetu vimejaa maji hivi..... whether u like it or not, politics is everything..when our politics is messy everything is guaranteed to be screwed..

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 06, 2010

    mwacheni agombee awapunguzie mafisadi kura zao mnaona what happened in uk recently...yeee semeni semeni watu kama hawa watachukua kura za watu wengoi mmoja wapo miye...niheri nitupe humu kwa vile sioni wa kumpa huko kwingine

    profesa hoyeeeee vijana mpoo tupo vijana mpo tupooooo

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 06, 2010

    PROFESOR HONGERA SANA.
    KURA YANGU UNAYO.
    TUNAHITAJI MABADILIKO NA KUPITIA MAARIFA YAKO TUTAFIKA.
    TANZANIA INABURUZWA VYA KUTOSHA.
    PROFESSOR MCHANGO WAKO UNATAMBULIKA KIMATAIFA HIVYO NI IMANI YETU CHINI YA UONGOZI WAKO TANZANIA ITAKUWA NCHI INAYOJITEGEMEA KIUCHUMI.

    HONGERA MWANA UCHUMI PROFESSOR LIPUMBA!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 06, 2010

    Wote mnaopinga Prof kugombea ni simply mnakitu kimoja kinawasumbua. "Mnamwogopa" na wengi wa critic mtakuwa ama CCM au CHADEMA. Wewe unayeongelea philosophy yako ya kwenye ya kinabii Tito ya "FFN" mbona hueleweka?, mi nilidhani philosophy hiyo itakuwa inafanya kazi vizuri zaidi kwa walikuwa madarakani, maana ndiyo walipewa nafasi ya kuziweka sera zao in action, sasa iweje unawalaumu watu ambao ni sidelines?

    Ukweli ni kwamba Lipumba ana mashabiki wengi na wapiga kura wengi kuliko mgombea yeyote yule. Na kama unabisha utaona Dec, Kura zote za CUF ni kura halali zisizo na mizengwe wala manouvrebility ya kuhakikisha ushindi wa kishindo ni lazima. Acheni woga, Halafu unaposema waweke watu makini, hebu toa definition ya mtu makini kwanza kabla ya kuja na msamiati usiouelewa maana yake.

    Prof anayo haki ya kikatiba ya kugombea cheo chochote ambacho chama chake kitamwona anafaa kwa manufaa ya nchi yetu sote na wewe ukiwemo.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 06, 2010

    Sasa washikaji mbona mnamuonea chuki Lipumba tu wakati mkoo kimya kwa kina Malecela,Kingunge na wengine wengi wameyangangania madaraka tokea 60s hadi leo wakati Mh Lipumba yeye anagombania tu au nyie ndio wale wanachama wa Moscow,Russia kudadadeki.

    ReplyDelete
  19. waswahili siku zote wanasema dalili ya mvua ni mawingu na dalili ya kitu kuharibika ni harufu na dalili za mtu muongo zipo nyingi lakini tatu kati ya nyingi zinaweza kukutambulisha uaminifu wa mtu-:(1)mtu anapotoa ahadi lakini asitimize kile alichokiahidi < be carefull with this type of person> (2)mtu alieazima akashindwa kurejesha alichokiazima (3)mtu ambae akizungmza huwa anazungumza uongo.Lipumba anajulikana na wengi kama profesa na maana ya profesa ni mtu mwenye uweledi wa taaluma fulani kwa kiwango cha juu kwa maana nyengine mtu alieelimika sasa kilichomfanya lipumba aelimike kitu gani ikiwa kuna kila dalili yakuwa anaharufu ya udikteta.siamini kama hakuna watanzania wenye uwezo kugombea uraisi lakini lipumba kama dikteta yupotayari afie madarakani hii si dalili nzuri kwa wanakafu na tanzania kwa ujumla tunahitaji watu wenyekuhibiri demokrasi na maendeleo ya nchi kwa vitendo sio blah,blah tupu.chukua mifano ya watu wenye kuielewa demokrasia na kuwajibika kwa misingi ya kidemokrasi-:jk,nyerere alikuwa kiongozi wa chama tawala ccm lakini akamua uanzishwe mfumo wa vyama vingi unafikiri kama angelikuwa lipumba au seif ndio nyerere wangefanya hivyo sifikrii kwa sababu wameshaonyesha kiwango cha kutisha cha uchu wa madaraka-:Algore baada kushindwa uraisi katika ucaguzi uliofanyika 2000,kati yake na bush,uchaguze ambao inasadikika algore ndie mshindi aliamua kukubali matokeo kwa manufaa ya nchi na kuondoa wingu zito la mvutano lilokuwa limetanda na licha ya kuombwa na wanachi pamoja na chama chake agombee uraisi anasema muda wake umeshapita na anaamini kuna watu wenye uwezo zaidi ya yeye na ni kweli, Obama ameonyesha kiwango cha kushangaza cha uongozi,ni mtu mkweli,anajiamini,mchapakazi kiasi kwamba mpaka wapinzani wamebaki wakigombana wenyewe kwa wenyewe.oh,Nataka kumsahau mandela si elezi mengi kuhusu mandela kwani kila mtu anaelewa''who is madiba'' na mwisho tuwaanglie waengerasha nini tumejifunza kutokana na patashika iliotokea katika uchaguzi wao,yuko wapi Gordon brown alie kuwa waziri mkuu wa uengereza kwamanufaa ya nchi nasema tena kwa manufaa ya nchi ameamua kuachana na kupigania kurudi madarakani na usitarajie kumsikia tena anagombea uwaziri mkuu katika chaguzi zinazofuata kama walivyo viongozi wa siasa nchini hasa wale wa vyama vya upizani.MABADILIKO YA DEMOKRASIA YA NCHI FULANI SI LAZIMA CHAMA PINZANI AU KIONGOZI PINZANI ASHIKE MADARAKA YA NCHI NDIO PANOGE BALI MABADILIKO YA KWELI YA KIDEMOKRASIA NI YALE YANAYOTAMBUA NA KUHESHIMU KUWA UONGOZI NI KWA AJILI YA WATU WANAONGOZWA NA NI KWA MASLAHI YA WATU NA KWA MATAKWA YA WATU SIO MTU BINAFSI-XXX

    ReplyDelete
  20. Kalibha KajibhijibhiJune 06, 2010

    Mbona hii ni siiiimpo!
    Hii ndiyo Demokrasia. Yeyote mwenye sifa kwa mujibu wa katiba yao achukuwe fomu.

    Ili awe au asiwe mgombea ni uamuzi wa wapiga kura! sio mchukua fomu!

    Kama atapitishwa wakati hafai basi ni wanachama wapiga kura ndio hawafai na kinyume chake pia ni kweli.

    ReplyDelete
  21. UK Brown baada ya kushindwa uchaguzi ikabidi na kwenye chama chake cha Labour aachie ngazi. Lakini CUF Maalim Seif na Lipumba mmeshindwa mara mbili bado hamuachii ngazi. Hivi CUF hamna watu wengine zaidi ya hao wawili. Hivi Lipumba hajioni kwamba hana mvuto? Kutwa kakalia kuzungumzia wajihi wa JK.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 07, 2010

    mi nadhani tufike mahali tupeane madaraka kwa kuzingatia kigezo cha zama au wakati na mazingira, hivi hawa jamaa wakipewa uongozi wataweza kuongoza kipindi hichi cha dot com!!!????

    jaman fikirieni kabla ya kutenda eehh!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...