
Wachawi 10 wamejitokeza kutengeneza ndumba zitazoiwezesha Taifa Stars kushinda mechi yao na Brazil siku ya Jumatatu katika nesho jipya jijini Dar, mfadhili mkuu wa zamani wa Simba Azim Dewji amesema leo.
Azim kaiambia Globu ya Jamii mchana huu kwamba baada ya kutangaza juzi kwamba atatoa shilingi milioni 10 kwa kila mchawi atayewezesha Taifa Stars ishinde, amepigiwa simu toka kwa watu 10 ambao wamedai wao ni wachawi mahiri na wako tayari kuifanya kazi hiyo.
"Wote walionipigia simu kuwa wako tayari kufanya kazi hiyo nimewaomba wafike ofisi za TFF kesho saa tano asubuhi kuandikishiana mikataba na makubaliano mengine.
"Wamekubali wote nami najiandaa kuwazawadia milioni 10 kila mmoja wao endapo tutawafunga Brazil. Lakini tukifungwa mkataba utakuwa kwamba wote watapigwa picha na sura zao kuoneshwa kwenye vyombo vya habari kuwa ni matapeli..." amesema Azim.
Amesema wazo la kutoa zawadi hiyo limemjia kwa kutaka kudhihirisha kwamba soka si uchawi bali ni mazoezi na mipangilio ya maendeleo ya muda mrefu, hivyo endapo kama Taifa Stars itashinda itajionesha dhahiri kwamba ndumba nangai ipo na inaweza kufanya kazi.
"Mimi siamini uchawi iwe katika soka ama katika maisha ya kawaida yoyote yale. Lakini kuna baadhi yetu tunaamnini sana uchawi, hivyo testi itakuwa hii mechi yetu na Brazil. Tukishinda tutaanza kuamini ndumba na nitawazawadia hao wachawi wataojitokeza.
"Dunia nzima inatambua kwamba Brazil ni timu bora. Ingawa Taifa Stars nayo sio timu ya kubeza lakini kuwafunga mabingwa hao wa mara tano itakuwa si rahisi sana. Hivyo nimeona nitoe changamoto hii ili kudhihirisha kwamba soka sio lelemama linahitaji maandalizi", kasema Azim.
Taifa Stars hivi sasa wanaelekea nchini Rwanda ambako Jumapili watakipiga na timu ya Taifa ya nchi hiyo katika kuwania nafasi ya kucheza kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa nyumbani. Katika gemu lao la kwanza hapa Dar walitoka sare ya 1-1 hivyo inabidi Jumapili washinde.
Taifa Stars watarejea nyumbani Jumatatu alfajiri kwa ndege maalumu ambapo jioni yake watakumbana na Brazil katika mchezo unaotajwa kuwa wa karne.
Mtaishia hivyo hivyo!
ReplyDeleteWenzenu wapiga vita uchawi lakini nyie ndio kwanza mnautangaza na kuuremba. Poleni wabongo poleni!
Hii mechi sijui kama itafanyika.Kwanza hao brazil wameshaingiza timu yao Da? Subirini mtaletewa under 21 brasil wawapige ubaya sio senior brasil.Changa la macho hilooo,pesa kibindoni.hahahahahaha
ReplyDeleteHili ndo tatizo kubwa za timu zetu za Tanzania, ni kuamini mambo ya giza ndo maana hatufiki popote pale tunabakia kudumaa kimichezo kwaajili ya kuamini kwamba kufanya vizuri ni lazima kutumia ndumba! Pole sana timu za Tanzania mtaishia kuchezea ligi za ndani tu mkitoka nje mnagaragazwa kwani uchwai hauvuki bahari! LOL
ReplyDeleteSafi sana!!! Nasubiri kwa hamu picha za matapeli hao zitoke hadharani. this is a good bet: itawadhihirishia washirikina once and for all kuwa uchawi ni bullshit!!!!
ReplyDeleteWe mbigiri acha wazimu wako.
ReplyDeleteMshindwe katika Jina la Yesu Kristo wa Nazareth!
ReplyDeleteHao wachawi wakijitokeza tu na kukiri kuwa kweli ni wachawi na kutoa maelezo ya kazi zao (ndumba walizowahi kufanya), moja kwa moja Mahakamani! Tena pengine hii itapelekea hata kutungwa kwa sheria inayotambua uchawi na ushirikina Tanzania.
Baada ya hapo itakuwa; mtu akianguka na ungo tu, Mahakamani! Misukule ikipatikana tu, aliyewaweka misukule au aliyewaendea kwa mganga wawekwe misukule (watatajana tu, mbele kwa mbele)Mahakamani! Kwa sababu Mi naamini kumuweka mtu msukule ni sawa na FALSE IMPRISONMENT, ambayo mtu unaweza kudai fidia; hivyo ikiongezeka na sheria ya kutambua ushirikina hapo juu yake; IMAKOREA KO SHINGO!
Tena adhabu ya uchawi na ushirikina iwe kubwa kweli kweli, maana hawa watu saa nyingine hadi huua! Sasa murder si murder? Au ni mpaka murder ifanywe na watu kama majambazi ndio iwe murder?
Nahisi hatimae watu watamrejea Muumba wao.
Tukipata ma-snepu ya hao wachawi, tutapata pa kuanzia (Mtatajana wote!).
Anon wa tatu,
ReplyDeleteUmejuwaje kuwa uchawi hauvuki Bahari? Mmnnn, unatutia mashaka.
Tunategemea kukuona siku hiyo mkiwa mnahojiwa na wenzako. LOL! Mtatajana tu siku hiyo, woote. LOL!
na mimi nataka kusaini, na mie ni mchawi, nyie shangaeni , hii ni kamali, hapo kuna potential ya milioni 10, changamkieni hiyo wabongo tujitokeze tuwe kama 50 wachawi mbona jamaa atafilisika ikitokea! things hapen bwana, naomba niarifiwe namna a kujiunga na kundi la watakaochawia, namba za sim za Dewji ziwekwe hapa tupige wachawi wa mbali,,,
ReplyDeleteHao ndio wanaotegemewa kunyanyua kiwango cha soka nchini!!!
ReplyDeleteYaani anatoa offer kwa washirikina!
(US Blogger)
Raifa star watachoka sana. Hiyo game ni back to back.
ReplyDeleteHao wachawi mnaoenda kesho kutia mikataba someni hili,... na nyie mseme mkataba wetu upo chini kama watacheza wachezaji wanaoaminiwa wakikosi chao na chetu....Wakija the second or reseve team mkataba haupo...na kwetu kukiwa kunamajeruhi mkataba haupo....
Mchawi wa mbali wewe loga huku huko. We umeshaambiwa uchawi hauvuki bahari unataka kutwambia nini tena? Aaah haya masihara sasa..kama unajiamini panda pipa haraka haraka nenda huko kesho saa Tano halafu hela yako itarudi na ya nauli na umetajirika tayari...Kama unajua kuloga washinde hela yako si ipo bwana ...kwanini ukae mbali huko
ReplyDeleteHii habari imenifurahisha sana,nimecheka sana.Hivi mpira na uchawii wapi na wapi? Loh Bongo kwa ndumba !!!!teh teh teh hee.
ReplyDeleteNicholas,Netherlands
Uchawi ni imani jamani msiuseme sana hata timu za ulaya zinaloga. Ufaransa walienda Benin kutafuta nmchawi hanjui hilo?. Isipokuwa hauwezi kushinda kama timu yako mbovu kwa kutegemea uchawi.
ReplyDeleteNilikuwa kiongozi ktk timu. Weee acha tu wachezaji hawatii timu kama ujaroga. Ukiwaambia umeroga watacheza na watashinda hata kama uliwafunga herizi za Uongo. Kwa maana nyingine uchawi kama hamasa tu.
Anon. Sat Jun 05, 02:53:00 PM, nakubaliana na wewe kabisa katika wasi wasi ulionao. Ila siri yenyewe kabisa anaijua Tenga, asubiri cha mtema kuni akitupiga changa la macho.
ReplyDeleteHalafu wewe Dewji, unathibitisha kabisa kuwa hayo ndio mambo yenu simba. Sasa nakuagiza ukabidhi hiyo listi ya hao wachawi (wote wahindi, wandengereko etc.) kwa Kakobe, fanya hivyo haraka utakasike.
Kipimo cha uzalendo hicho. Anaenda uwanjani akiamini kabisa timu yake inaenda kufungwa. Watu wengine bwana...
ReplyDeleteMUNGU na amlaani yeye atakayefunga hiyo mikataba na wachawi maana anataka kutuharibia ladha ya soka na sifa yetu kwa ujumla.
ReplyDeleteOH PLEASE, GIVE US A BREAK! HIVI HUONI KUWA TAIFA STARS WAKIWAFUNGA BRAZIL KWA FLUKE SI UTAKUWA UMEWAPANDISHA DAO HAO WACHAWI NA KUWADHIHIRISHIA WATU KUWA UCHAWI UPO?
ReplyDeleteUjinga mtupu...hii kweli habari ya kutangaza??? Nyie kina Michuzi waandishi wa habari hii habari gani?? Tupu kwenye Karne ya 21 sasa ...acheni mambo yasiokuwa na mbele wa nyuma.
ReplyDeleteUS Blogger, I think you missed the point. Anachotaka kuonyesha ni kuwa UCHAWI NI UONGO, na kuwa ni ujuzi, nidhamu na matayarisho ndiyo yatakayoleta ushindi. Kwa sababu hizo Brazil watatufunga na hata wachawi hawawezi kuzuia hilo. You get it? Hebu soma purpose ya offer hiyo. Thanks.
ReplyDeleteNilikua nakauaminaia kumbe nawe.............! Hii ndio hoja gani mzee? Kuwa mbunifu siku nyingine
ReplyDelete