Ze marco Polo

Kaka Michuzi, Habari za siku?
Mimi nashukuru Mungu niko salama na naendelea vyema na shughuli.
Naomba usaidie kuwafikishia ujumbe wapenzi wote wa blogu ya jamii, kuwa mwanablog mwenzao Dr. Imani Hamza Kondo ( kwenye dunia ya ku-blog wananifahamu kama zemarcopolo), ninatangaza nia ya kugombea ubunge wa Morogoro Kusini Mashariki kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu ujao.

Nikiwa kama mwanablog mwenzao, nawaomba tushirikiane kuomba Mungu ili uchaguzi uende vizuri na tufanikiwe kupata matokeo yenye manufaa kwa taifa letu tunalolipenda.

Yeyote atakayehitaji taarifa zaidi basi asisite
kuwasiliana nami moja kwa moja kwa
zemarcpolo@yahoo.co.uk
Nashukuru Sana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2010

    Karibu sana katika uchaguzi, kila la heri,tutaonana Bungeni.

    Nakutakia kila la heri japo kuwa sipo ndani ya Chama chako.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2010

    CCM nooo mimi siko kwenye chama chako.

    But why CCM though?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2010

    KILA LA HERI DR. IMANI WATU ZAKO TUPO KILA KONA ZA DUNIA , DUHH MZEE UONGOZI UMEUNZIA MBALI TANGIA ENZI YA MZUMBE , ILLBOUR ..... YES GO DR. IMANI ...

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2010

    Nakupongeza bloga mwenzangu kwa kuamua kugombea na kutumia haki yako ya kikatiba, kwa kweli ni uamuzi wa busara. Shida niionayo ni moja tu, hicho chama ulichopitia!
    Ninakitilia shaka sana, kiko madarakani miaka karibu 50, lakini mpaka leo jiji la Dar halina uhakika wa maji na umeme, achilia mbali mikoani!
    Sina mengi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2010

    Kila la kheri Dr.!
    Mdau toka Avcilar.

    ReplyDelete
  6. We anonymous hapo juu. Why not CCM? It is the only political party my friend. The rest are only NGOs whose agenda is known to themselves. Unashangaa nini. Zemarco ubunge utapata mheshimiwa.

    ReplyDelete
  7. Zemarcopolo tumekumisi sana katika kublogu, kumbe ulikuwa unapiga jaramba kwa ajili uya uchaguzi. kila la heri sana.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 05, 2010

    Imani, kila la khei mheshimiwa. Hope you will succeed.
    Amani J Kitali.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 05, 2010

    Asanteni sana wote kwa kuungana nasi na kwa changamoto. Mwaipopo, bado tupo pamoja. Mdau wa Avcilar, nimekusoma. salam zao kocamustafapasha. Petro tuendelee kuwa pamoja.
    zemarcopolo...

    ReplyDelete
  10. Kila la heri kiongozi.

    ReplyDelete
  11. Kila la heri kiongozi.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 06, 2010

    Hivi Tz sheria za kuombea ugumbe ni zipi? Hii imekaaje? Simjui huyu mtu wala anakoishi lakini nimeona juzi tu yule Nakaya anachukua form za kugombea Arusha. Je ni halali mtu uende tu kuchukua form mahali usipoishi? Mtu anaishi Dar miaka yote leo unagombea uongozi jimboni Arusha ina maana atahamia kuishi huko au ndio hayo tunayoyaona kila mabunge anaishi Dar na kuwakilisha huko madongo kwinama. Yanayowasibu huko hayajui atakalojua ni kwenda kurecycle kura tena wakati wa uchaguzi unaofuata...

    Watanzania tuamke mjumbe muwakilishi wa kweli ni yule anaishi na wewe na kujua hali halisi ya jimbo lako wengine wanaoishi mbali na kurudi tu kutafuta uchaguzi kupitia nyumba zenu msiwape kura kabisa. Mimi hapa nchi ninayoishi huwezi kugombea kwenye hilo jimbo mpaka uestablish residency for two years

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...