MAREHEMU DJ EDDY SALLY

Eddy Sally alifariki dunia tarehe 28 july 2009 jijini Dar na kuzikwa kesho yake shambani kwao Mkuranga, Kisiju, Mkoa wa Pwani. Ni mwaka mmoja sasa toka atutoke. Eddy, unakumbukwa na watoto wako Jafary, Adam Mwambile Jnr na Chichi (zainab) pamoja na wajukuu zako Alana-leah, Joyce na Adam, mzazi mwenzake Joyce Mangula dada na kaka zako bila kusahau ndugu jamaa na marafiki tele uliowaachia ukiwa.

Eddy alikuwa musician toka miaka ya 60's akiwa na bendi ya Tonic. Aliwahi kupiga drums na kuimba siku James Brown alipotembelea Afrika Mashariki. Aliendelea kuwa Dj ikuanzia miaka ya 70 mpaka alipostaafu katikatia ya miaka ya 80's.
Eddy Sally pia amecheza kama muigizaji katika filamu kadhaa miaka 90's akiwa kama Dk. Moshi katika filamu ya 'Maangamizi - the acient one ' pamoja na Barabra. Aliendesha Night Club huko Lusaka, Zambia, iitwayo Club africa 2000" miaka ya 70's kabla ya kurejea nchini na kuanzisha Em Three Disco akiwa na DJ Jerry Francis.
Baadaye akawa anafanya biashara ya vifaa vya kuzimia moto na kampuni yake ya ADjef Intergrated mtaa wa Lumumba jijini Dar kabla mauti hayajamkumba.
MOLA AILAZE PAHALA PEMA ROHO YA MAREHEMU EDDY SALLY
-AMINA Eddy Sally akipiga drums katika bendi ya The Tonics miaka ya 70
Eddy Sally na rafikie uwanja wa Independence, Lusaka, Zambia
DJ Eddy Sally akitumbuiza Msasani Beach Club enzi hizo
DJ Eddy Sally akiwa katika hafla jijini Dar
Eddy Sally (wa pili kuume) na maafisa wenzie wa kampuni ya vifaa vya kuzimia moto walipomtembelea Rais wa Zanzibar Wakati huo, Dk. Salmin Amour, Ikulu, Zenji






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Mwangalie katika sinema Maangamizi the Ancient One jinsi anavyowasumbua Dr. Asira na na Dr. Odhiambo. Marehemu Eddy Sally alifika mpaka Hollywood maana Maangamizi ilikuwa sinema ya kwanza kutoka Tanzania kuwa katika mashindano ya Oscars (Foreign Language). Alichangamsha set wakati tunapiga sinema huko Bagamoyo mwaka 1994.

    Rest in Eternal Peace Eddy Sally!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 28, 2010

    EDDY SALLY ALIFARIKI! HE WAS ONE OF MY BEST DJ IN TANZANIA I REMEMBER HIM WHEN I WAS VERY YOUNG IN DAR HE WAS VERY SMART GUY AND HANDSOME BOY VERY FLAMBOYANT GUY. MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 28, 2010

    mungu amrehemu.ila kwenye kumbukumbu hiyo tunaisomaje.sabiniz,themaniniz na tisiniz???? wajameni.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 28, 2010

    SISI WATOTO WA MAGOMENI MWEMBECHAI,TUNAMKUMBUKA KAKA YETU KWA UCHESHI,UKARIMU NA USHAURI ALIOKUWA ANATUPA SIKU ZOTE NAMKUBUKA ALIWAHI KUTUAMBIA BORA UWE BONGE LA BRAZAMENI WAVITU VIKALI,MADEBE DARASANI KWA SANA(ELIMU)KULIKO GANGWE MTU WA MANGO TREE MASKANI ADUI WA MGAMBO.
    FROM SISTERS&BROTHERS KIMAMBA FRESH
    JUMPING JUMPING NO POSITION,VUMBI NEVER PARFIUM KIBAO.
    R.I.P. BROTHER SALLY(BABA JEFF)

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 28, 2010

    Namkumbuka DJ Eddy Sally pale Selander Bridge club alipokuwa DJ anatupigia Disco toto mchana weekends alikuwa anaupenda sana wimbo wa Kool & the Gang wa "Let's Go Dancing".....oooohlahlahlah... Pia namkumbuka na akiwa na gari lake la Fiat saloon!!.
    RIP

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 28, 2010

    Nilikua naishi SEA VIEW, nyuma ya sasa COURT YARD HOTEL(PROTEA)DJ Eddy Sally alikua anapiga Disco hapo.....hakuna DJ wa TZ anaweza kufikia uwezo wake, jamaa alikua anatoa show ya nguvu. anauwezo wa kucheza, kuongea na kuhamasisha hadhira. Nilikua mdogo hivyo sikua naingia Disco lake ila tuliku tunaangalia kutokea juu Ghofani kwetu....pale nyuma ya SEA VIEW au Court Yard kuna magorofa ya Relwe ndio tulikua tunaishi hapo.....BENDI ya BARKEYS (akina KAPINGA, JOHN MHINA, PEPE na wengineo) ilianzishiwa eneo hilo, kwa sasa ndio The TANZANITE....nimekumbuka mengi sana ....mungu amrehemu!
    Mwachikobe AK

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 28, 2010

    Eddy RIP. Mimi ni mzee wa miaka 60 namkumbuka Eddy alikuwa The Tonics ya DSM (wakati nasoma sekondari 1960's). The Tonics walihamia Arusha mwaka 1968 ambapo walikuwa mpaka 1973 an 1974. Hiyo picha ya kwanza inaelekea ilipigwa Arusha kati ya 1968 mpaka 1970 (nikikumbuka hiyo ndiyo ilikuwa sare yao kabla ya kuanza uniform za mashatia ya ukosi (collars kubwa) na vizibau na suruali za bell-bottoms za maua maua. Mola amuweke peama. Amin.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 29, 2010

    Tunakukumbuka sana jirani zako sinzakumekucha.alikuwa ni mtu wa watu,mcheshi,mchangamfu na mpole.R.I.P Brother Sally.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 29, 2010

    Hiyo picha ya pili wakiwa Uwanja wa Independence inanikumbusha utotoni miaka ya sabini. marehemu baba yangu mdogo alikuwa akivaa hivyo hivyo; miwani, kisbau, kifulana cha ndani ya shati, suruali bana kati lakini chini mwaga tu, na hizo laizoni. Mungu awalaze mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 29, 2010

    Hiyo picha ya pili wakiwa Uwanja wa Independence, MA-BITOZ WA ENZI ZILE. SAFI SANA.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 29, 2010

    mwachikobe inaelekea unaijua sana tanzanite wewe..ukiacha kina john muhina,pepe,kapinga kuna kina sticks,marehemu kizibo jina halisi william,kina kanisa,yona na wengine

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...