Home
Unlabelled
Mabere Marando ajiunga na CHADEMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Atakuwa anafuata yale mahera aliyotoa Mzee Sabodo juzi!!! hihihi
ReplyDeleteCHADEMA KIMESHAKUWA CHAMA MBADALA
ReplyDeletekula tano kaka, na bado wanakuja mpaka kieleweke
ReplyDeleteHuu ni Umalaya na Uchangudoa wa Siasa....hawa watu hawana misimamo kwahiyo hivyo vyama haviwezi kukomaa...leo TLP, kesho CCM, another day CMJ...sasa mbona ni vurugu? Halafu huyo Mabere Marando mbona kaongezeka hivyo kalikuwa kamekaukiana....kuna nini? Lazima kuna ulaji mahali tena wa CCM....
ReplyDeleteWawaaaa!! Hongera Mabere Nyaucho Marando.
ReplyDeleteSafiiiiiiiii sana hiyoo!!
CHADEMA tusonga kwa sana.
CCMafisadi...presha inapanda presha inashuka!! tutawashika pabaya mwaka huu.
Hii imekaa vizuri
ReplyDeleteSasa JK na wanzako tunataka mdahalo mwaka huu. sio mnakimbia kimbia tu kila mwaka.
Kama mnajiamini na mko safi mbele za waTZ na wanachama wenu..msikmbie mdahalo.
Mambo si hayo. na bado kuna wengine wanafuata. Huraa Marando!!
ReplyDeleteChonde chonde Silaa na wenzako, mkataeni huyo jamaa anakuja kuwavuruga huko kama alivyoivuruga NCCR-Mageuzi. Hilo ni pandikizi la mimiem.
ReplyDeleteMdau
Mbezi Louis
Hongera sana mzee Marando kwa uamuzi mzuri. Tunahitaji wasomi wanaoongozwa na fikra zao, sio kukumbatia habari za CCM kwa ajili ya maslahi. Mtu anayechagua kujiunga na upinzani katika hali hii ya ukandamizaji kutoka chama tawala, ninamhesabu kama mtu mwenye uchungu na nchi, na hali ya watanzania, bila kuweka mbele maslahi yake binafsi, kama wengi wanaoshabikia mfumo wa chama tawala.
ReplyDeletehawa watu ndo wanachafua vyama vya upinzani wakisha tozwa uko CCM kugombea huongozi wana jiunga chadema. miaka yote mlikuwa wapi adi leo siku ya uchaguzi ndo mnakimbilia chadema !!
ReplyDeleteI GUESS ANAKWENDA KUWA MGOMBEA MWENZA
ReplyDeletewachanga ni wezi tu !!akuna cha chadema wala nini hapo hanalake analo tafuta !!
ReplyDeletekaribu saaana kwenye chama halisi cha WATANZANIA, lakini plz usije ukaleta malumbano na kuua chama..!
ReplyDeleteALL IN ALL ITS A WISE DECISION ..KARIBU
braza mabe wewe ungerudi CCM tu, huko hamna mpango.
ReplyDeleteMzee wa Mizengwe, na Kuharibu anataka kuwaharibia na CHADEMA sasa!!
ReplyDeleteUuuuuuwiiii!!! Sasa CHADEMA basi!!!! hawa jamaa ndio walioiua NCCR wakati ikiwa kwenye "peak" ...leo CHADEMA tena inajitangazia na kujichimbia Kaburi.
ReplyDeletePole sana CHADEMA.
CHADEMA mpepoteza kabisa mwelekeo, hivi Hamumjui Marando? Huyu Mtetea dhuluma dhidi ya watoto na aliyeua upinzani wa kweli Tanzania kupitia NCCR Mageuzi? AAAGHRRR!
ReplyDeletemaoni yangu, CHADEMA wasimpe cheo shochote cha juu huyu jamaa kwani kazi yake ni kutibuatibua mambo huko upinzani
ReplyDeleteMichuzi usiwe unabania komenti zenye faida kwa wananchi.
Huyu naye ni "political prostitute"...this has nothing to do with haki ya kikatiba...haiwezekani kila kukicha mtu ana-switch tu kutoka hapa kwenda kule!
ReplyDeleteDawa ni moja tu kwa Chadema kuweka maombi yake ya uanachama pending mpaka baada ya uchaguzi...
What happened to Mabere? Mbona kabadilika ivi. Wala sikumjua kuwa ni yeye.
ReplyDeleteAlafu bado tu anrukaruka from one party to another.Si arusi tu kwenye chama cha washikaji CCM. Kwa mzee wakutabasamu
CHADEMA kuweni waangalifu sana na huyu jamaa, ndiye muuaji mkuu wa vyama vinavyokuwa tishio kwa CCM. Kumbukeni alivyoitenda NCCR yake hadi sasa imebakia kuwa chama cha Buguruni kwa Mnyamani tu!
ReplyDeletesafi sana homeboy hilo ndo chama dume lenye watu makin km wewe. hapo ndo pake homeboy
ReplyDeletewe anony 4:05 acha uzushi.angeenda CCMafisadi ungesema hayo uyasemayo?? Marando welcome to CHADEMA chama halisi cha watz
ReplyDeleteHuyo jamaa ni Shesna...jiangalieni wana Chadema
ReplyDeleteHivi mnasema Marando aliua NCCR, lakini hamjui kuwa NCCR ipo kwa sababu yake? Yeye ndiyi mwanzilishi.
ReplyDeleteHamkumbuki kwamba alijivua uenyekiti na kumpa Mrema ambaye alikuwa nyota ya kisiasa wakati ule? Nani angekubali kujivua madaraka kirahisi namna ile hapo Tanzania?
Tatu, msisahau kwamba NCCR wenyewe walimtema kwenye nafasi za uongozi katika uchaguzi wa kidemokrasia na akaishia kuwa mwanachama wa kawaida huku NCCR ikifa yenyewe?
Mnyonge mnyongeni lakini haki mpeni. Akina Mbatia wenyewe ndiyo walimtoa Marando kwenye duru za chama ili wakiendeshe kama NGO. Acheni kusema bila kuwa na data.
Ana haki kuhamia chama chochote kwa maslahi ya nchi na hata yake mwenyewe.
Michuzi weka hii.
wewe uliyeandika wachaga wezi acha kukurupuka kama hujui majina ya wachaga uliza kwanza ndipo utoe maoni, mabere sio mchaga anatoka Mara,. next time do your reseach before u put u're comment. pumbafu we.
ReplyDeleteWangejitokeza wengineo kama akina Dr. Mwakyembe na Anne Kilango-Malecela kuhamia CHADEMA, mbona ingekuwa INRI! Imekwisha! Yaani akina fulani fulani wangekuwa 'marehemu' haswa!
ReplyDeleteWallah, na wengine tungeunga tella (Trailer), japo kwa ujumbe wa nyumba kumi tu.
Karibu CHADEMA.
ReplyDeleteThis time mpaka kieleweke.
Mwaka huu tunamchukua hadi Kikwete.
Ndio kwanza mechi haijaanza.
MUNGU IBARIKI CHADEMA
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
CCM wakati wa cheza ngoma za mdundiko na mdumange inafikia ukingoni.Chadema ina watu makini wasio na mzaaa mzaaa kama CCM.Tumechoka na-mambo ya kimzaa mzaa ndani ya CCM IT'S TIME FOR CHANGE IN TANZANIA POLITICS.CCM imekaa madarakani miaka 49 almost nusu karne,ni wakati wa kuwapisha wengine.
ReplyDeleteWakati umefika kwa upinzani kua-chana na siasa za kibinafsi na kumsapoti mgombea moja kutoka kambi ya upinzani.
HONGERA SLAA
Kuwa na vyama vingi vya siasa tungeacha nyuma kidogo. Kama watu wanataka maendeleo tanzania wangejiunga na chama hiki tu na vingine vidogo dogo viachwe ili kiwe na watu wengi either uwe CCM au CHADEMA. Kwei upinzania ungekua mmakali. Baada ya miaka kadhaa watu wakishajua utamu wa competition ndio viundwe vingine. Bila hivyo hatuna nguvu kabisa ya kuiengua CCM regardless of who is joining and who is not.....
ReplyDeletewengine wataongezeka....ngoja kura za maoni ziishe tu mwisho wa july huko CCM....ubunge deal!....sidhani kama ni wote wana dhamira nyingine zaidi ya kutaka kuingia mjengoni!
ReplyDeleteBongo bana always go opposite mf, Mpira badala ya kusaidia vilabu vidogo viwe vikubwa sisi tunadhamini SIMBA na YANGA tu,Siasa Badala ya Kusapoti CUF ilete challenge kwa CCM sie ndio tunajiunga na CHADEMA. Huku ni kuua upinzani na kufanya CCM kuchukua madaraka easy. AND I KNOW THIS PEOPLE LIKE MABERE THEY KNOW WHAT THEY ARE DOING.
ReplyDeleteWatanzania wenzangu,hii ni blog ya jamii inayoendeshwa na mtu(Issa),tueitumie vizuri basi katika kuleta changamoto za maendeleo ktk jamii yetu.Mtu anapost comment bila kujiuliza amepost nini...bila kuwa na data na umakini kwa yale aliyoyaandika.
ReplyDeleteSwala la Adv. Marando kuhamia CHADEMA ni swala la kawaida katika siasa,sasa kusema maneno ya ovyo ovyo tuu katika hili mimi kwangu naona sio sawa.
Hongera Marando na Hongera Chadema,cha muhimu ni kujitaidi kufanya yale ambayo watanzania wengi wanayategemea na kuyasimamia,tusiwe wabinafsi na wapenda kujilimbikizia mali na madaraka,bali tutumie akili zetu kuendeleza rasirimali zetu na kuzitumia kwa maendeleo ya wote,tusiangalie Chama zaidi,tuangalie uwezo,CHADEMA ni chama chenye watu wenye uwezo na ninaamini kitayaanzisha mabadiliko ya kweli ndani ya nchi hii.CCM na serikali yake kimeshindwa mengi zaidi kuliko kilichoyaweza....kama serikali haina kipaumbele katika bajeti zake miaka yote,hakuna muujiza utakaotokea na kuleta maendeleo katika nchi yetu.
Kwa pamoja tunaweza,tutimize wajibu wetu.
Watu woooooooote WENYE AKILI tunajua Mabere Marando analetwa KUVUIRUGA CHADEMA na kuhakikisha HAIWI TISHIO kwa CCM.
ReplyDeleteKama ndani ya chadema kuna wajinga, basi watamruhusu aingie kwenye vikao vyao, na huo utakuwa mwanzo wa mwisho wa CHADEMA.
CIA & KGB Joint Team Director, Washington
Huyu jamaa amepandikizwa Chadema. Marando kama vile alivyofanikiwa kukivuruga NCCR pia atakivuruga CHADEMA. Watch this space...in 3 years' time!!!!!
ReplyDeleteMimi binafsi simwamini mtu yoyote aliyehama vyama mara tatu kwa miaka 15!!! Mhh, kuna kitu ambacho si sawa hapa.
ReplyDeletejoint team director wa washington, nakubaliana na wewe. ni wajinga tu ambao hawajifunzi kutokana na historia. ni muhimu kwa chama chochote kujua historia ya watu maarufu wanaojiunga nao na kujua vitu walivvyovifanya huko nyuma kuua vyama vya upinzani walivyovipitia. au labda chadema wana mkakati wa kumzuia asifanye damage aliyoifanya nccr ambacho kilikuwa chama imara zaidi ya chadema.
ReplyDeleteMimi binafsi naamini CHADEMA wamejipanga vyema ili kukabiliana na yeyote yule mwenye nia ya kujiunga na chama hiki ili kukisambaratisha. Anakaribishwa saaaaaaaaaana tu kama anania chanya; ila nina hakika kuwa kama anania hasi basi hatachukua mda hapa.. lazima atatimuliwa.
ReplyDeleteMungu ibariki CHADEMA, Ibariki Tanzania. ( a member frm Arusha ).