Mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM,Dk. Bilal akizungumza na wanachi wa Wilaya ya Nanyumbu baada ya kuingia mpakani mwa wilaya hiyo na Masasi leo
Kamanda wa Chipukizi wa Wilaya ya Masasi, Fatuma Rajab akimvisha skafu Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal alipokuwa akiingia mpakani mwa Wilaya ya Masasi akitokea Wilaya ya Newala leo mchana
Mgobea Mwenza wa urais, Dk. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na wananchi na viongozi wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Masasi, baada ya kuingia mpakani mwa wilaya hiyo na Newala, leo
Baadhi ya makada wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Newala Mkoa wa Mtwara, wakiwa katika magari kwenye msafara wa kumsindikiza Mgombea Mwenza wa nafsi ya urais, Dk Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akitoka Wilaya hiyo kuelekea Wilaya ya Masasi leo asubuhi
wananchi wa Kijiji cha Lukuledi Wilaya ya Masasi Mkoa wa Mtwara, waliojitokeza kumsikiliza mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia na kuwanadi wagombea Ubunge wa Jimbo la Lulindi,Bwanausi Dismas na Mariam Kasembe wa Jimbo la Masasi leo
Wananchi wa Kijiji cha Mangaka Wilaya ya Nanyumbu Mkoa wa Mtwara Jimbo la Nanyumbu, wakimsikiliza mgombea mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Kijiji hicho leo mchana.
(Picha na Muhidin Sufiani)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Polisi mpo wapi? angalia watu mananing'inia katika magari mnawaachia je huu si ushabiki?

    ReplyDelete
  2. TANZANIA MAISHA BORA KWA KILA MTU. WANANCHI HAO WANAONEKANA WAKO VYEMA KABISA NA MAISHA YAO NI MSWAANO KABISA. WATEGEMEE KUENDELEA KUISHI KATIKA HALI HIYO YA MAISHA KWA KUICHAGUA CCM TENA KWANI NDIYO IMEWAFANYA WAWE NA MAISHA YA HALI HIYO TANGU UHURU WA TANGANYIKA MWAKA 1961.

    ReplyDelete
  3. Na mchina naye CCM?

    Hussein Bashe mumesema si raia, mchina Raia?

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  4. MSAADA TUTANI JAMANI, NAOMBA KUFAHAMU NI BLOG GANI IPO INDEPENDENT KATIKA KUTOA HABARI ZA VYAMA VYA SIASA YAANI HAIPENDELEI CHAMA CHOCHOTE, NAHITAJI KUPATA HABARI ZA CHADEMA NINAAMINI KUNAKITU WANAKIFANYA WAKATI HUU SOMEWHERE AMBAKO MICHUZI NA TIMU YAKE HAWAFIKI

    ReplyDelete
  5. we michuzi unaboa sana..wewe ni mdini na mbaguzi na hufai kuwa mpashaji hbr..huwezi ukawa waweka za ccm tu na cuf kidogo tena vile waona cuf sio threat kwa ccm..mbona huweki hata kidogo mambo za chadema..kwakweli nimeamua nikuambie..hatushi namna hiyo..weka na mambo ya chedema...dr slaa amechana sana juzi hujaandika kitu

    ReplyDelete
  6. Bradha mwambieni huyo Kamanda wa Vijana taratibu hapo aangalie asije akamtoa UDHU Mhe. Bilal kwani mwenzie kafunga!

    Mikono hiyo isije ikagusa mwili. Iguse shati tu.
    vinginevyo atamfungulisha mwenzie bure!

    ReplyDelete
  7. WATU WAZEEEEEEEEEEEEEEEE???? MADARAKA KUACHIA HAWATAKI. ANAWAYS, TUTAFIKA TU.

    ReplyDelete
  8. Kwao muhimu juu kuna shati la sisiemu, maisha bora ndio hayo.
    Mungu tusaidie

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...