Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgombea Mwenza Dr. Mohamed Gharib Bilal wakisaini tamko la Kisheria linalothibitisha usahihi wa taarifa alizozitoa kwenye fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku Jaji Mkuu Agostino Ramadhani akishuhudia.Tamko hilo lilisainiwa leo asubuhi na kukabidhiwa ofisini kwa Jaji Mkuu jijini Dar es Salaam.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Jaji Mkuu Agostino Ramadhani tamko la kisheria linalothibitisha usahihi wa taarifa alizotoa kwenye fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ofisini kwa Jaji mkuu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Anayeshuhudia kulia ni mgombea mwenza Dr.Mohamed Gharib Bilal.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo amekabidhi Hati ya Idhini(University charter) kwa baadhi ya vyuo na taasisi mbalimbali za elimu ya juu hapa nchini.Pichani Rais Kikwete akimkabidhi Mkuu wa Chuo Cha Mtakatifu Agustino Mwanza Mhashamu Askofu Aloyce Balina hati Idhini kwa chuo kishiriki cha Bugando Weill Medical College kilichopo jijini Mwanza.
(Picha na Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Naomba kuelimishwa, hivi ni wagombea wote wa urais wanakwenda kusaini kwa jaji mkuu au ni CCM peke yake? Kwa kuwa kama ni kwa rais anayemaliza muda inakuwaje kwa huyo Bilal wakati hajapata madaraka?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...