Asaalam Aleykum Kaka Michuzi na Wadau
wote wa Globu ya Jamii popote pale duniani

Kwanza nawaombea Ramadhani Mubaraka wote waliojaaliwa kufunga na ambao hawakujaaliwa.
Sisi ndugu zenu wa hapa Leeds, U.K tumeandaa muhadhara rasmi kwa ajili ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhan na pia futari ya pamoja siku ya tarehe 21.08.2010;
Muhadhara utafanyika katika ukumbi wa Intercontinental Mill 3, uliopo Mabgate Mill,
Macaulay street,
LS9 7BZ,
LEEDS;
Kuanzia saa 7.00 mchana hadi
saa 12.00jioni (13.00pm - 18.00pm).

WAHADHIR ni Ustaadhi SALUM HATIB kutoka LONDON na wenzake.

Futari ya pamoja itakuwa katika ukumbi wa Ebor Garden kuanzia saa 2.00 usiku hadi saa 4.00 usiku

Kwa upendo mkubwa na moyo mkunjufu Leeds Swahihi Community inawakaribisha WADAU WOTE kwenye MUHADHARA na FUTARI
Ima ima msikose wake kwa waume, hasa wewe kaka MICHUZI

Waandaaji ni : LEEDS SWAHILI COMMUNITY

Allah atujaalie Ibada kamilifu, Upendo, Afya, Ushirikiano na Subra katika kila lenye Kheri dunia na Akhera, Inshaalah! ;
Allah aijalie GLOBO yetu hii iwe ya kheri na kiunganisho cha upendo. Inshaalah !

Asalaam Aleykum, Wabirah Tawfiq

M/kiti; Aran Rashid na wajumbe Sheikh Mahir Mzishi na Ust. Ridhiwan

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Natumai hiyo haitaishia tu kwenye mfungo wa Ramadhani pekee!

    ReplyDelete
  2. Natumai na umbeya utakuwa haupo maana sie mabachelor hatuji huko kuepukana na umbeya.

    ReplyDelete
  3. A.A
    Naona jumuiya mashaallah mnaendeleza mambo ya kheri.
    Dr.Mahir safari hii usikose inshaallah,
    Salaam wote,na Ramadhan Kareem!

    Othman

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...