Nyaya na nguzo za umeme zikiwa zimekata denge kuepuka kupita juu ya makaburi yaliyo kando ya barabara kuu kilomita chache toka Iringa ukitokea Mbeya. Kuna hadithi zinasema Tanseco walishindwa kupitisha nyaya hizo juu ya hayo makaburi kwa sababu ambazo awali hazikuwa zinafahamika. Kuna hadithi zingine pia zilidai kwamba ukipiga picha hapo huwa hazitoki
Makaburi hayo kama yanavyoonekana yakiwa kandoni mwa barabara
Katika pitapita zake ankal alibahatika kuwakuta mafundi wa Tanesco wakiwa kazini karibu na eneo hilo. aliposimama na kuwauliza, na baada ya kusitasita kidogo, mmoja wa mafundi hao alijitolea kwa kumwambia ankal kwamba waliepa kupitisha nyaya hizo juu ya makaburi hayo kuepuka gharama ambayo wangepata bila shaka kwa kulipa fidia katika kuyahamisha. Bahati mbaya hapakuwa na mkaazi wa eneo hilo ili kutoa ufafanuzi. Hivyo kama kuna mdau mwenye data tunaomba msaada tutani ili wadau wapate mwanga halisi wa maajabu haya...



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Hilo nikaburi la Chifu Kiyeuyeu kama bado nakumbuka. Niliwahi kusikia kuwa walipitisha umeme hapo current ikawa hai flow kwenda mbele, jamaa walihangaika sana mpaka walipopata uamuzi wa kukwepa ndio ukapita wenye data zaidi tafadhali

    ReplyDelete
  2. lkn mbona pix zako Ankal zimetoka?

    ReplyDelete
  3. Mi ni mwenyeji wa Iringa tena Karibu kabisa na sehemu hiyo (Tosamaganga) niliwahi kumuuliza mzee mmoja kuhusu hilo nikajibiwa kwamba mahali hapo walishindwa kukata mti ambao upo karibu na kaburi la mzee mmoja aliyefariki siku nyingi hapo na lengo la kukata mti huo ni mrefu kwamba ungegusa nyaya lakini sasa walipojaribu kukata zilikuwa zikimwagika (DAMU) wakilazimisha sana basi mti unakuwa mgumu ajabu wakatumia mpaka mbinu ya Greda lakini nalo lilishindwa na wakijaribu kulazimisha watu walikuwa wakipoteza maisha (KUFA) sasa ndo maana serikali ikatoa amri kwamba nyaya zivuke barabara kuepusha balaaaa hilo
    HICHO NDO NILICHOJIBIWA BAADA YA KUULIZA
    Mdau Ughaibuni))))

    ReplyDelete
  4. Mhandisi BarabaraSeptember 05, 2010

    Barabara kuu haina mistari??? Kwa viwango vya barabara, mistari ya kutenganisha njia haiwekwi kwenye vile vibarabara vya majumbani. Sasa hio barabara kuu inafuata viwango vya nchi gani? Angalizo ama ni kwasababu Nchi yetu haina viwango vya barabara.

    ReplyDelete
  5. Hio ni Iringa au Dodoma/singida hivi! Au ndio miti yote imeishawashwa mkaa.

    Jibu la kisayansi ni kwamba Tanesco wanabidi kununua eneo wanalopitisha umeme. Kama wakipisha gridi juu ya makaburi inabidi kununua ardhi hio na kuenda kuzika masalio sehemu nyingine. Sasa kuondokana na bughudha na vitu vingine vya kilugha bora walale mbele.

    Jibu la kizushi........kakobe alionewa pale kanisani kwake. Makaburi yapo ndani ya hifadhi ya barabara hivyo inabidi yaondolewa kwa stahili ya mabango ya kakobe yalivyoondolea na marehemu wailipe Serikali.

    Hio ndio maana Mhandisi hapo juu amesema kuwa Tanzania hatuna viwango kwani hayo makaburi yapo ndani ya "clear zone" kwahio yanahatarisha usalama wa watumiaji wa barabara. Suluhisho ni kuondoa obtacle ambayo hapa ni Kaburi.

    Tunahitaji pia mapinduzi ya miundombinu kama tunavyo hitaji yale ya kilimo, afya, na viwanda nchini kwenu

    ReplyDelete
  6. Mahimbi cirrusSeptember 05, 2010

    Mdau, hayo ni makuburi ya uko wa kiyeyeu alikuwa ni m2 mwenye mizimu mikali mpaka umeme ulikuwa hauwezi kuvuka(means upande wa kwanza kunakuwa na umeme ila waya ukifka upande wa pili baada ya kaburi una luz na hauna moto kabsa) makaburi haya yapo barabasa ya kuelekea mafinga kutoka iringa mjini mkono wa kulia na niupande wa kushoto km unatoka mafnga/mbeya kuja iringa mjini. Haya ndo kakobe aliyo2ahdi kuwa umeme wa tanesco hautawaka km 2 serikali itabaki na mcmamo wake kutokuhamisha njia na kubaki mbele ya kanisa lake, je nae atafanikiwa km marehemu kiyeyeu

    ReplyDelete
  7. WALIHAMISHA NGUZO BAADA YA KUMBIWA GHARAMA KUBWA UHAMISHA MAKABURI. KULUKUWA NA ENGINEER MMOJA AKASEMA BORA TUKA TISHE KUNA KULIKO GHARAMA HIO .HUU NDIO UKWELI. YOTE NI MANENO YA UONGO .TUWE NA AKILI TIMAMU JAMAANI

    ReplyDelete
  8. Ankal Nashukuru kwa kuliweka hili hapa leo,hiyo line ya umeme iliwekwa kama sikosei mwaka 1993/94 kutokea pale ruaha chini kuelekea Tosa,Tanangozi, Ihemi mpaka Ifunda.ni maajabu ambayo nadhani yabidi kutaweka wazi na pengine tukapatqa hata pesa kwa utalii wa kimaajabu yaliyopo nchini mwetu,nakumbuka ilikuwa ni malumbano makubwa sana kati ya mafundi waliobobea wa tanesco na hata kutoka DANIDA wakati huo juu ya ukweli kuwa 33kV au 11kV power line iwe live upande moja na iwe dead upande wa pili bila kizuizi chochote.lakini ukweli ulibaki pale pale kuwa umeme hauvuki upande wa pili waya zikipita juu ya makaburi hayo,haina ubishi wala ligi ya kushindana katika hilo,kama mtu anaona hilo haliwezekani na ni porojo za watu,basi aende pale korogwe mkoani Tanga sehemu inaitwa Makorosi kama ukiwa unaelekea Mombo kutokea Korogwe mkono wa kushoto kuna mawe ambapo mto ruvu wote unaoendesha kinu cha umeme cha Hale unapita katika eneo lisilozidi mita moja na nusu na akajaribu kuruka upande wa pili halafu atatusimulia kitakachompata.yapo mengi la muhimu nadhani ni kuwa positive nayo tujipatie kipato kutokana na hayo,kuna maji moto kule utete,mlima izimbili kule Tabora, mbuyu kule karibu na stesheni ya Mlimba Ifakara n.k

    ReplyDelete
  9. hat mm hadith iyo nilii[ata ivo kila nipitapo napaangalia km utalii tu

    ReplyDelete
  10. Anka Misupu,
    Mimi nilikata nondoz zangu hapo Tosamaganga pia. Hayo makaburi yanamizengwe na Tanesco. Tumekuwa tukielezwa mara nyingi kuwa ukipitisha nyaya hapo juu ya makaburi basi hakuna umeme.kuna imani na ushuhuda fulani wa mambo ya ANCESTORS wa huko Iringa. Ankal next time ukiyapiga picha bila kibali ujue pia kuwa glob ya Jamii itazima kabisa na kutoklwenda hewani;

    Kuwa makini,

    ReplyDelete
  11. Hahhaha watu wengine bwana hata vitu vidogo na muhimu vya nchi yao hawavijui...wewe km mtanzania kweli usiyejua historia ya hayo makaburi ya highway ya Iringa kuelekea makambako basi...Utalii wa nyumabini ni muhimu jamani.

    ReplyDelete
  12. Da asante michuzi nilikuwa nasikiaga sana hyo issue lakin inawezekana ikawa kweli umeme haupiti nani mwenye rea data kuhusu makaburi hayo?

    Its YMCMB aka Teflon Don

    ReplyDelete
  13. Lakini michuzi mbona umepiga picha na imetoka nayaona makaburi vizuri tuu.

    ReplyDelete
  14. Mdau Mahimbi cirrus uelekeo wa hayo makaburi ni kinyume na ulivyosema, makaburi yapo kushoto kama unaelekea Mafinga,Mbeya,Songea nk na yapo kulia kama unatokea sehemu nilizozitaja hapo juu.

    ReplyDelete
  15. Mahimbi cirrusSeptember 06, 2010

    Mdau lipo kulia unapokwenda mbeya ukitoka iringa kwenda mbeya na waliotengeneza barabara ilikuwa ni kampuni ya stealing astard walishndwa kubomoa kaburi hlo kwan lengo ilikuwa kutengeneza barabara kwenda zambia 1967, pale kitengere (wenda) kuna dada ake na marehemu maltin kiyeyeu na pamoja na kuwa na mizmu mikali huyu bwana maltin kiyeyeu alikuwa muumini mzuri wa roman catholic. Mdau kwa maelezo zaidi check.. Mahimbi.cirrus27@gmail.com

    ReplyDelete
  16. daaa iyo noma hata askofu angeenda kutafuta maujuzi kwa hao jamaa

    ReplyDelete
  17. hilo ni kaburi la Chifu Kiyeyeu kabla ya kufika Tanangozi ukitokea Iringa Mjini ilo kaburi lina maajabu mengi hapo umeme ukikatiza juu mbele moto hauendi na si umeme tu bali hata barabara imelikwepa hilo kaburi ndio maana unaona liko karibu sana na barabara ni kwamba greda zilikuwa zilitaka kulibomoa zinakufa na zikitolewa hapo zinawaka, wakandarasi wakaona isiwe tabu wakakwepesha barabara

    kuna mwaka flani lori liliacha njia na kuangukia kaburi hilo na kuharibika vibaya sana ila lilivyonyanyuliwa wakakuta kaburi halina hata mkwaruzo wowote

    hayo ni mambo ya sayansi ya asili wala msibishe wadau. Mimi nimekulia Tanangozi najua historia vizuri ya ilo kaburi na pia hata kama mkitaka kuzika pembeni ya ilo kaburi lazima mfanye maombi na zindiko kwenye kaburi la Kiyeyeu otherwise hapachimbiki kuhusu picha hapana kwani hata mimi niliwahi kupiga picha hapo miaka ya nyuma bila tatizo

    ReplyDelete
  18. Hayo makaburi ni ya Chief Kiyeyeu pamoja na patners wake, chief inasemekana alikuwa na mizimu, ambayo inasemekana ilizuia umeme kupita hapo hapo, tatizo sio fidia wadau fikirieni tanesco miaka hiyo wangeshindwa kulipa, picha zinatoka kama kawa ila Mithupu hujasema kingine hapo kuna bomba la tazama nalo limepiga kona kama nyaya za umeme ina maana makampuni yote mawili yalishindwa kulipa fidia, ni fidia gani inatakiwa kulipa kwa makaburi wakati nyaya zapita juu,

    ReplyDelete
  19. Makaburi yapo kulia kama unakwenda mbeya mdau na kushoto kama unatoka mbeya, mdau naamini umepitiwa

    ReplyDelete
  20. Ukweli lazima utabaki pale pale hiyo sijui fidia sijui mahali pa kuyahamishia tunadanganyami Ankal, Mi si mwenyeji wa Iringa But nimekaa kama miaka Miwili!! Sikuulizia ila nimeambiwa kama kuna maajabu umeme ulishindwa means UMEME ULISHINDWA kupita Juu na TANESCO WALISHINDWA kuyang'oa hayo Makaburi!! Na huo ndio Ukweli!! Iringa Ina mambo mengi Ya Kihstoria! Maeneo Y mwakalenge Kuna Mto Unapita UNDERGROND. Ankal Unaweza ukaitafiti hii nayo ukairusha pia. Thanks

    ReplyDelete
  21. Sasa kama waliamua kuyakwepa makaburi kwa kuyaheshimu,mbona hawakutaka kuheshimu kauli za walio hai waumini wa Kakobe??au sehemu ya makaburi ni bora kuliko hoja za kakobe?basi hata pale Sam Nujoma road wafanye hivo wapige umbo la bakuli?sufuria.Sababu za kakobe ni bora kuliko hayo makaburi.walio hai na wafu kipi bora/cha kudhurika?

    ReplyDelete
  22. ankal ukome kutuona wahehe wanga ivo mbona umeyapiga picha sasa,,,hakuna hadithi kama izo ni ukwepaji wao tu hao tanesco wa kulipa fidia na kununua ardhi hapo

    koma ankal koma kabisa!!
    msg sent

    ReplyDelete
  23. wahehe wanga tu, hata kwetu mbeya huwa wanakuja kutuwangia.

    ReplyDelete
  24. Hizi habari mbona zinatokea leo tungekuwa tunazijua tangu ile siku umeme umekataa ziwekwe kama maajabu ya taifa kitendo cha kukatiza barabara nikwamba ni uoga tu hakuna chochote, we bwana, mtu akisha kufa amekufa hana jipya angekuwa na hizo nguvu za ajabu namna hiyo asingekufa au angefufuka basi,nyie wahehe acheni uongo,mambo ya kichawi yamepitwa na wakati.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...