Bw. Amaniel Mahimbo

“NAKUACHIA kibanda chako, nakwenda kwenye nyumba yangu.”

Hayo yalikuwa maneno ya mwisho ambayo Aminiel Mahimbo aliambiwa na mkewe, Josephine Mushumbusi siku alipoachwa na mkewe huyo aliyeamua kwenda kwa mgombea wa urais wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa.

Mahimbo ambaye ni mume halali wa Josephine, (kwa ndoa ya kanisani) alisema anakumbuka kuwa ilikuwa Machi mwaka huu na hakujua mke wake alipokuwa akienda na wala hakuhisi dalili yoyote ya kuwepo kwa mwanamume mwingine katika ndoa yao mpaka siku mwanawe wa kwanza Upendo (7) alipomwambia “baba tunaishi na daddy”.

Akisimulia kisa hicho kilichoanza takribani miezi saba iliyopita, katika mahojiano maalumu na gazeti hili jana, Mahimbo ambaye ndoa yake ilifungwa Agosti 16, 2002 na Mchungaji Lewis Hiza katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Kijitonyama, jijini Dar es Salaam, alisema hakujua kama huyo ‘daddy’, ni Dk. Slaa mpaka siku moja alipoambiwa na mama mkwe wake.


Chanzo na Habari Kamili Nenda Habari Leo
ANGALIZO: MAWAKILI WA BW. MAHIMBO INASEMEKANA WATAFUNGUA KESI MAHAKAMA KUU KUHUSIANA NA UTATA HUU. TUTAWALETEA HABARI ZAIDI KADI ZITAVYOPATIKANA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 107 mpaka sasa

  1. michuzi wewe tunakufahamu vizuri sana

    ReplyDelete
  2. MICHUZI,
    SWALI HUYU MUME ANALOPASWA KUJIULIZA NA KUJIJIBU NI KWA NINI MKE WAKE ALIAMUA KUMUACHA. JAMBO LA PILI LAZIMA TUTOFAUTISHE KATI YA MAISHA BINAFSI YA MTU NA MASWALA YA KIKAZI, WAKATI MWINGINE VITU HIVI WALA HAVIINGILIANI. HII NI MBINU TU YA CCM KUGEUZA MWELEKEO WA MAWAZO YA WANANCHI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU.
    KAMA JAMBO HILI LILITOKEA TANGU MACHI MWAKA HUU, MALALAMIKO KWA NINI YAJE SASA MIEZI 6 BAADAYE?
    TUNATAFUTA RAIS WA NCHI NA WALA SI MUME WA MKE FULANI, KAMA NI HIVYO BASI KILA MGOMBEA AWEKE HADHARNI MAMBO YAKE YA NDOA HALAFU TUONE NANI SAFI.

    ReplyDelete
  3. Mwanamke haji kwako kula na kuzaa tu mkuu.Umeshindwa mfikisha mwenzio sasa walia nini? Umeshindwa mpa kile anachotaka unaleta mazoea kwa ndoa ona sasa umebaki walia.Hii niaibu kwako mkuu ulishindwampa mashine asngekimbia huyo huna mpya

    ReplyDelete
  4. Habari leo ni gazeti la serikali lakini lipo mstari wa mbele katika vita dhidi ya CHADEMA. hilo lipo wazi michuzi, kwani hata wahariri wake wapo kwenye kamati ya kampeni za CCM. Sioni ajabu kulishabikia hili wakati ukweli kuhusu Dk.Slaa na Josephine sisi wadau wengine tunaujua fika. Walianza kwa mke wa zamani wakaona kapangua hoja vizuri kabisa sasa wameleta hili ati kummaliza, wakisema nao waanze kuendesha mashambulizi dhidi ya mgombea wa CCM kweli kutakalika?
    najua utaibania hii comment kwa sababu unafanya kazi serikalini lakini hakuna hoja hapo utaikia watakavyo hit back.

    ReplyDelete
  5. Mwanaume gani huna hata haya kama umeachwa unang'ang'ania nini si uote talaka yaishe. Na wewe michu mbona ya hao wagombea wengine huyatafuti ukayatoa na sisi tunajua mauchafu yao kibaaooo, hasa huyo wa dash dash dash

    ReplyDelete
  6. Suala kuu nafikiri ni watu kusaka umaarufu wa usiokuwa na mpango na kutaka kuona wao ndio wanajua sana kusumbua watu wengine na kuwachafulia majina yao. Anyway kuoana ni makubaliano ya watu wawili na wala hawakulazimishana....... kama kakuacha maaana yake hakupendi,kapata tulizo la moyo wake. Usitake kuumiza akili na vichwa vya watu hapa. Umeachwa tafuta akupendaye usitake kulazimisha kuolewa/kuoa mtu ambaye hakupendi.
    Mdau M.A-Kafanabo

    ReplyDelete
  7. Suala kuu nafikiri ni watu kusaka umaarufu wa usiokuwa na mpango na kutaka kuona wao ndio wanajua sana kusumbua watu wengine na kuwachafulia majina yao. Anyway kuoana ni makubaliano ya watu wawili na wala hawakulazimishana....... kama kakuacha maaana yake hakupendi,kapata tulizo la moyo wake. Usitake kuumiza akili na vichwa vya watu hapa. Umeachwa tafuta akupendaye usitake kulazimisha kuolewa/kuoa mtu ambaye hakupendi.
    Mdau M.A-Kafanabo

    ReplyDelete
  8. Suala kuu nafikiri ni watu kusaka umaarufu wa usiokuwa na mpango na kutaka kuona wao ndio wanajua sana kusumbua watu wengine na kuwachafulia majina yao. Anyway kuoana ni makubaliano ya watu wawili na wala hawakulazimishana....... kama kakuacha maaana yake hakupendi,kapata tulizo la moyo wake. Usitake kuumiza akili na vichwa vya watu hapa. Umeachwa tafuta akupendaye usitake kulazimisha kuolewa/kuoa mtu ambaye hakupendi.
    Mdau M.A-Kafanabo

    ReplyDelete
  9. Kwa hiyo mke wake ana dhamani ya bilioni moja tu? Nipe contact zake aje nimpe vijisent hivyo aache kelele na kutumiwa na CCM

    ReplyDelete
  10. Sasa toka machi mbona hukumfungulia mashitaka ndo unazinduka leo.. ushahongwa na mafisadi wewe huna lolote

    ReplyDelete
  11. Gamaliel- MshauriSeptember 07, 2010

    Kaka Michuzi shukrani.

    Mimi ni CCM damu na ninatoa ushauri wa bure hapa kwamba sisi tubaki katika kueneza SERA ZETU, MIPANGO MIKAKATI YETU NA UBORA WA CHAMA CHETU DHIDI YA VYAMA VINGINE basi. Mbona tunaendelea vyema sana na tumeshapiga honi- pipi?

    Yeyote anayetaka kum attack mpizani yeyote personally afanye mwenyewe na ikibidi sisi tukae mbali kabisa na mambo kama haya maana hayana mshiko na mara nyingi huwa yana-backfire, mark my words!

    Mwenye kulalamika kuibiwa mke aende tu mahakamani na sisi tutasikia kitakachoamuliwa huko.

    ReplyDelete
  12. Jamani huyu jamaa ametumwa ili kumualibishia Dr Slaa,siku zote kakaa kimya kampeni zimeanza oo nimechukuliwa mke wangu basi anamapungufu ndio maana mke kamkimbia subiri watoto wako walelewe watakuja kwako baadae wakikuwa.

    ReplyDelete
  13. hii blog nayo imekuwa blog ya udaku, tuache kujadili mafisadi wanao hujumu nchi, tubaki na kuzungumzia siri za vyumbani mwa watu..tutabaki wadanganyika, kwani we have our priorities really mixed up..

    ReplyDelete
  14. Huyu jamaa anajizalilisha tu, kashindwa kutunza mke, sasa anapiga kelele. Aache wanaoweza kutunza wamiliki. Halafu mwenyewe kaona kapatia kweli kutamka hilo wakati wa Kampeni, sio issue, Mbona hata yule Mshkaji wetu anae kaa pale karibu na Soko la Ferry,(Ankal, hebu nikumbushe nani vile!) pale karibu na Wizara ya Elimu, anao wengi tu wa namna hiyo na hakuna mtu anayepiga kelele!

    ReplyDelete
  15. POLE KAKA ILA UKIMEGEWA NAWE TAFUTA MNYONGE UMEGEE KAKA ! WE MPIGIE TU KURA SLAA SA UTAFANYAJE NDO MKEO KAMPENDA ! ANGEKUWA ANAKUPENDA ANGEBAKI KWAKO KAKA !

    ReplyDelete
  16. Hii habari ina utata. Utaachaje kujua kuwa mkeo ana bwana mwingine mpaka uambiwe na mtoto? Huyu jamaa inaelekea alikuwa hamjali huyo mama na alimtekeleza wakawa hawapo pamoja. Hata mwanafunzi wa primary katika somo la ufahamu atabaini hivyo. Hii ni njama ya ccm pamoja na vikaragosi vyake kumchafua Dr. Slaa kwa sababu maji yamewafika puani. Hilo ni kosa kubwa vipi kuliko mabilioni ya peas yaliyokwapuliwa na ccm? Watanzania tuamke, tufanye uchaguzi wa busara.

    ReplyDelete
  17. Kazi kweli x2 hii ndio bongo bwana, ukiwa juu watu watatafuta kukushusha, mtu yuko radhi awe chongo ili wewe uwe kipofu...Ni kuharibiana kwa kwenda frontttt...

    ReplyDelete
  18. Ona aibu we mwanaume!Unanunuliwa ili ujitukanishe kwa jamii!wanakutumia tu hiki kipindi cha kampeni then utasahaulika faster after election.
    Ukinyang'anywa inabidi utulie tu,mbona wengi tu tunanyang'anywa ila tunapunguza machungu kwa sisi nao kunyang'anya.
    Sasa Dr. Slaa akisha kulipa hiyo fidia inamaana ndio itakua price ya kumuuza mkeo!(Dedication wimbo wa mwana FA)

    ReplyDelete
  19. CCM HUYO !! KAMA MKE KAKUACHA UNATAKA NINI SASA MAYBE ULIKUWA HUMTIMIZII MATAKWA YAKE! TULIZA BALL TAFUTA MWINGINE

    ReplyDelete
  20. ha ha haaa uuuwii!!!

    ReplyDelete
  21. Watu pipoooo!!!loh. we baba sijui hata umehongwa sh. ngapi na jitambi lako hilo. bogas!!hivi sijui mambo ya kinyumba ya viongozi wakuu wa chimwaga yakiwekwa hadharani ikianziwa na mtendaji mkuu patakalika??duh. cjui nijitoe mhanga nikafie jela??Rafu hizi kwenye siasa tume sijui mnaziona??mabere fanya mambo tule kichwa..michuuu

    ReplyDelete
  22. Hi Michuzi

    Nimekuwa nafuatilia makala zako kwenye blog yako, lakini kuna jambo moja linajitokeza, Makala nyingi niza chama Kimoja, Tafadhali tunaomba utende haki kwa wasomaji wako wanataka kujua vyama vingine vinafanya nini Kisiasa,

    Please Strike a Political balance in your articles, to get a balanced audience

    ReplyDelete
  23. Jamani tumuache nayeye Josephine aseme maana hizi Ndoa za siku hizi hizi unaweza kukuta kuna bonge la ishu hapo

    ReplyDelete
  24. Mhhh huyu Mwanaume mimi simuelewi elewi kabisaaaa mhh!

    ReplyDelete
  25. haya sasa First lady huyu mhh! ???

    ReplyDelete
  26. huyu kaishapewa hela na mafisadi....achukue zake time,miaka kumi na tatu ndo anakumbuka ana mke,kisheria huyo sio wake tena!

    ReplyDelete
  27. Duh!!.. Hii kali tunaomba basi umuoji na Dr. Slaa hili halitolee maelezo.
    Au Dr. Jk akubali basi kufanya nae mjadala wa wazi tuyapate majibu hayo live

    ReplyDelete
  28. haya ccm mmeanza ya Agustino Mrema na angelina. Trip hii hatudanganyiki!

    ReplyDelete
  29. HASANTE MICHUZI KWA KULETA HABARI NZURI KWA UMMA, NADHANI HIZI NDO ISUE ZA KUVALIA NJUGA WANANCHI WOTE MAANA KIONGOZI ANATAKIWA AJADIRIWE KWA MISINGI YA MAMBO YAKE BINAFSI MAANA YANAGUSA MASLAHI YA WATANZANIA WOOTE HASA WALIO MASIKINI. ILA CHOOONDECHOOONDE NAWAOMBA WATANZANIA TUSIYAVALIE NJUGA YALE MASWALA YA MEREMETA, RICHMOND,EPA NA DEEP GREEN. HAYO YATALETA MACHAFUKO HAPA NCHINI KWETU, SISI WATANZANIA TULISHAZOEA AMANI.

    michu usiitupe kapuni hii, ni constructive

    ReplyDelete
  30. ishu za hao wakubwa wengine mbona tunazijua... hii ya slaa siyo hoja. liwalo na liwe Slaa mshindi 2010

    ReplyDelete
  31. Mimi sipendezwi na baadhi ya waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo hivyo namna wanavyovitumia kwa manufaa ya Taifa letu. Ni nani asiyejua tabia ya watanzania wengi wakiwemo viongozi wake kwa waume kwenye suala la kuvunja ndoa na kufunga ndoa. Ni viongozi wangapi wana nyumba ndogo au wapenzi nje ya ndoa na leo waandishi hawa wakalibeba la Dr. Slaa kama geni kwao. Ninachoumia ninamna wanavyotumika kusambaza kile kisichomuhimu kwa wakati huu ili watanzania wasiopenda kutafakari na mashuhuri wa kudakia mambo wabadilishwe mawazo yao waliyokuwa nao na badala yake wakalie na kuyumbishwa na hoja ya kuoa na kuolewa kama ndio msitakabali wa Taifa hili katika kuleta maendeleo. nasema hili kwa maana wenzetu leo wanaoana kwa mikataba na halina tatizo katika kuongoza taifa ndio maana nchi zao ni matajiri. kifupi waadishi andikeni hoja za kiuchumi na utawala namna gani viongozi wanaotuomba kura watatupa faraja baada ya kuwa masikini tangu tupate uhuru ikiwemo kudhamini madaktari ,walimu na kilimo kama nchi nyingine zinavyofanya badala ya kuthamini siasa sana ili kuzidisha umaskini katika Taifa LETU.

    ReplyDelete
  32. Wewe anonymous Sep 07,01:43:00PM bogus kabisa. Great minds discuss events, average minds discuss ideas, and small minds like yours discuss people

    ReplyDelete
  33. aahahahahaha, i can now see CCM wananunua kila kitu nowadays, wamenunua magazeti yote isipokuwa Tanzania Daima la Chadema na Mwananchi ambao hawaegamii upande wowote, wamenunua mabango yote huko barabarani, na sasa wamenunua hadi hii blog. du kweli fedha ni nomaaaa!

    Juma

    ReplyDelete
  34. Watanzania wasiwasi kweli...hadi mkeo anaolewa unakuwa huelewi? Ndoa siyo kanisani...ndoa si msikitini...ndoa ni tendo ...sasa kama tendo lilikuwa halifanyiki jawabu lake ni kwamba hakukuwa na ndoa...Kwa mantiki hiyo anayemega saivi ndiyo mwenye ndoa ingawaje bado hawajakwenda kanisani lol... ni mtazamo tu.

    ReplyDelete
  35. mbona coment yangu hujaiweka? au sababu nimesema wewe ccm?

    ReplyDelete
  36. Vituko vya ndoa za wanasiasa duniani ni vingi, Lakini bado wana mvuto kwa umma na wanafanya kweli!!!!!! Kuna wengine hapo Tz wana wake wnegi tuu! na ni watawala wakubwa na wanafanya vema katika nyanja hiyo ya kisiasa! Slaa bado anaweza kuwa kiongozi mzuri. Ukiangalia umri wa watoto wanaotambulishwa kuwa ni wa wakubwa na wake wanaowatambulisha kwa umma kuwa ni wake zao unaelewa tu kuna jambo!

    ReplyDelete
  37. Mambo haya yanaweza yakawa ya ukweli au ni mambo ya kuchafuana katika siasa.

    Suala hili ni zito, lakini kwa nini liibuke wakati wa uchaguzi, na sio hili tu ni mambo mengi tu. Mara huyu sio raia, flani anakimada, Slaa kapora mke na mengine mengi.

    Wagombea, kunamambo mengi sana ya kufanya ktk nchi hii, tunataka kusikia mtayafanyaje. Tupeni sera zenu sio mambo yenu binafsi.
    katika nchi hii katika

    ReplyDelete
  38. Sasa KIKWETE AMELETA NINI?
    Kila analojisifia nalo limeletwa na MKAPA
    ****
    Wananchi tuamke...
    Hawa wasanii wanakopa mahela na hata hayafiki kwa walengwa
    ebu nieleze ni wakulima wangapi wamefaidika na " utapeli wa MAMILIONI YA KIKWETE"???
    Mali za nchi zinatumiwa vibaya.... tukisema tunaambiwa [NENO BAYA]

    1.Ziara kila kukicha, mbona kenya raisi wao KIBAKI ni mzee na Hasafiri lakini misaada wanapata!!! kwani tutaombaomba mpaka lini?
    Hizo pesa za ziara zingejenga shule ama Zahanati ngapi au kusomesha yatiama wangapi?
    2.Juzi kati RIZIWANI KIKWETE kaingiza nchini maziwa feki ya watoto... TUKISEMA wanadai watu wana wivu.
    Wivu wkati watoto wetu wanakufa...
    Tuamke na tuazishe mabadiliko... Hebu tuchague Mgombea wa chama kingine awe Raisi

    ReplyDelete
  39. Hivi kweli katika hali ya kawaida kabisa, kweli mke anaondoka nyumbani toka mwezi wa pili hujui anaishi wapi tena kaondoka na watoto, na hujaenda kuripoti polisi kama ni kweli basi wewe hukuwa mme wa huyo mama na wala si baba ya hao watoto!! Haiingii akilini mke kaondoka nyumbani eti hatua pekee uliyoona ni kwenda kuwaambia wakwe basi? Mchuma janga hula na wakwao angalia, kama mlikubaliana kuachana usiingize fitna hapa!!

    ReplyDelete
  40. HAYA SASA TUACHE KUONGELA MASLAHI YA TAIFA NA TUONGELEE MAISHA BINAFSI KIDOGO.

    LIPUMBA ATUAMBIE MKE WAKE NI NANI?
    JK ATUMBIE ANA WATOTO WANGAPI WA NJE SASA? MAANA HATA IDADI HAJUI.
    JK ATUAMBIE MAMAKE RIDHIWANI NI NANI NA ILIKUWAJE? MAANAKE TUNAJUA SALMA SI MAMAKE.
    JK ATUAMBIE AMESHAFIKISHA WAKE WANGAPI SASA? MAANA KABINT KA WAZIRI WAKE ALIKAKAOA JUZ JUZ KANAPITISHA IDADI YA WAKE4 KWA MUISLAMU SAFI.
    JK ATUAMBIE SAFARI ZA NJE AZOENDA KUSTAREHE NA FEDHA ZETU, ANAFANYA NINI HUKU?? AU TUTOE DATA ZAKEE??
    Quote

    ReplyDelete
  41. HAYA SASA TUACHE KUONGELA MASLAHI YA TAIFA NA TUONGELEE MAISHA BINAFSI KIDOGO.

    LIPUMBA ATUAMBIE MKE WAKE NI NANI?
    JK ATUMBIE ANA WATOTO WANGAPI WA NJE SASA? MAANA HATA IDADI HAJUI.
    JK ATUAMBIE MAMAKE RIDHIWANI NI NANI NA ILIKUWAJE? MAANAKE TUNAJUA SALMA SI MAMAKE.
    JK ATUAMBIE AMESHAFIKISHA WAKE WANGAPI SASA? MAANA KABINT KA WAZIRI WAKE ALIKAKAOA JUZ JUZ KANAPITISHA IDADI YA WAKE4 KWA MUISLAMU SAFI.
    JK ATUAMBIE SAFARI ZA NJE AZOENDA KUSTAREHE NA FEDHA ZETU, ANAFANYA NINI HUKU?? AU TUTOE DATA ZAKEE??
    Quote

    ReplyDelete
  42. Ni siasa tu za kuchafuana matope.sijui kwa nini hawa watu wanashindwa kunadi sera

    Maoni Hayo mambo ya kawaida si ya kushangaa sana kwani mtu ukiwa maarufu haya mambo lzm yakutokee big ni mkubwa yupi au mtu gani maarufu asiye kuwa na kashfa

    ReplyDelete
  43. HAYA SASA TUACHE KUONGELA MASLAHI YA TAIFA NA TUONGELEE MAISHA BINAFSI KIDOGO.

    LIPUMBA ATUAMBIE MKE WAKE NI NANI?
    JK ATUMBIE ANA WATOTO WANGAPI WA NJE SASA? MAANA HATA IDADI HAJUI.
    JK ATUAMBIE MAMAKE RIDHIWANI NI NANI NA ILIKUWAJE? MAANAKE TUNAJUA SALMA SI MAMAKE.
    JK ATUAMBIE AMESHAFIKISHA WAKE WANGAPI SASA? MAANA KABINT KA WAZIRI WAKE ALIKAKAOA JUZ JUZ KANAPITISHA IDADI YA WAKE4 KWA MUISLAMU SAFI.
    JK ATUAMBIE SAFARI ZA NJE AZOENDA KUSTAREHE NA FEDHA ZETU, ANAFANYA NINI HUKU?? AU TUTOE DATA ZAKEE??
    Quote

    ReplyDelete
  44. Kama huyo anayedau ni mke wake kaondoka tangu machi alikuwa wapi kumtafuta tangu kipindi hicho anakuja kuanza kumtafuta sasa hivi. Kwa sheria za kiserikali mtu akiishi naye kwa miezi mitatu tayari ni mke bila hata ya ndoa. sasa hapa naomba wadau mnisaie

    ReplyDelete
  45. Tulia tu ndugu, kama mwanamke ukimpa mapenzi YA NGUVU haondoki namna hiyo hata ingekuwa ameenda JK mwenyewe. Acha ulalamishi wanaume wengi wakishaoa wanalala tu wakifikiri wameshapata sasa ngoja nirare. weee mwenzio jirani yako ana piga maktime na huyo huyo unayemdharau. ABIRIA CHUNGA MZIGO WAKO BABU WEEE MTAIBIWA!

    ReplyDelete
  46. Raha kweli,
    huyu mshikaji kapewa kabilioni tu, kama sio viwili. Alikuwa na njaa mbaya! Ukitaka kujua ana njaa ona anavyobana matumizi kwa simu tatu kiganjani. Kwani nanihii ana simu tatu? moja tu!

    CCM noma, ila hii inaweza geuka kuweni macho. Babu slaa achana na dirty politics, weka sera jamaa naona wana kawasiwasi nchi iutachukua babu. Na josephine atakuwa wako, rahaaa. Mabinti wanagombania wanaona ikulu hiyoo. babu ishia kwa huyo mushumbusi tu. Wakorawaitu wote watakupa kura.ha ha ha! Ngoja nkanye, raha!

    ReplyDelete
  47. katafute wimbo wa bushoke unaitwa mume bwege ndo wewe apo.....toka apaaaa unatuchefua!!!hakutakiiiiii sasa unalazimisha wa nini? ooh nimemuoa sjui nini? mbona mandela alioa na akaacha bila kufungua kesi???njaa zako zitakupeleka jahanam na mungu anakusubiri na mafisadi wako wote wanaokupa hela ya kubadilisha mboga...Toka apaaaa!!!

    ReplyDelete
  48. Tulia tu ndugu, kama mwanamke ukimpa mapenzi YA NGUVU haondoki namna hiyo hata ingekuwa ameenda JK mwenyewe. Acha ulalamishi wanaume wengi wakishaoa wanalala tu wakifikiri wameshapata sasa ngoja nirare. weee mwenzio jirani yako ana piga maktime na huyo huyo unayemdharau. ABIRIA CHUNGA MZIGO WAKO BABU WEEE MTAIBIWA!

    ReplyDelete
  49. ni vitu 2 tofauti,kura yangu ni kwa Dr.Slaa hata akiiba mke wangu sina tatizo nae hata kidogo
    go slaa go

    ReplyDelete
  50. eti 'baba tunaishi na daddy'!! ina maana mlishatengana siku nyingi ulikuwa wapi toka machi leo ndo unakuja kwenye vyombo vya habari.. unatumiwa wewe. wanaokujua wakija na skendo zako...

    ReplyDelete
  51. Shida ya kutokwenda jandoni ndiyo hii.Jitu kubwaa linaongelea mambo ya chumbani kwake kwenye magazeti! Unakauka tuu mambo ya ndani yanaishia ndani, chumba kina kuta nne kaka!!

    ReplyDelete
  52. Labda nianze na kuuliza,baadaya huyu jamaa kuachwa na mkewe alichukua hatua gani?je alitoa taarifa katika vyombo vya sheria,je aliwahi kushiriki khudumia watoto?na je alfanya jitihada za kuhakikisha mkewe anarudu nyumbani baada ya kuondoka na je tokea Mach mpaka ndo ameibuka leo kujua mkewe ameolewa sehemu nyingine?Na kama yote ni ndio je yeye tokea Machi mpaka sasa anaishi na nani?Unajua unaweza kununua kila kitu isipokuwa utu wa mtu,mtu unakubali kununliwa kama andazi?Lakini pia jamani tuanze na vimada vya Viongozi wetu wa chama cha Kijani tuanze hasa na viranja wenyewe!!Ankal usiiibanie hiii....

    ReplyDelete
  53. duh Hii kali! Kura yangu iko pale pale, Dr Slaa, CHADEMA. Jaribuni tena!

    ReplyDelete
  54. Mambo ya ndoa magumu, lakini hayapimi uwezo wa mtu kuongoza, asilimia 99 ya ndoa hazina uaminifu kwa sasa, hata hao wanaoishi katika ndoa mashaka matupu, ndio maana hata Dodoma wakati wa Bunge kunageuka kambi ya makahaba, Kazi ya Slaa katika siasa za Tanzania haitaki tochi, wananchi watumie busara, suala la kupora mke wa mtu lina sehemu za kulishughulikia, sio kwenye sanduku la kura

    ReplyDelete
  55. Maisha binafsi tuachane nayo.tuzingatie sera .yote haya yamejitokeza kwa sababu za kisiasa.Mahimbo alikuwa wapi mke kaondoka na watoto kwa miezi hakujali.Leo Josephine kapata wa kumpenda na kumliwaza na pia kumtunzia watoto ndo unajitokeza.Ndoa ya kanisani kama hakuna upendo wa kweli haina maana.inaonekana Mahimbo hakuwa na penzi kwa mkewe kabisa na alimtekeleza.ss kasikia karibu awe first lady anaanza kichefuchefu.Wapiga kura msitetereke yote ni siasa.kumchafua Dr Slaa.Piga garagaza Slaa ni kiboko cha mafisadi
    2010 HATUDANGANYIKI

    ReplyDelete
  56. Inatia aibu sana mtu aliyeaminiwa na dini anachukua mke wa mtu, hivi we Slaa machangudoa wote wanaojiuza pale Kinondoni hujawaona? Ningekua mimi ningemroga kabisa

    Maselepa
    Kimara Suka

    ReplyDelete
  57. Kaka (Dedication Mwana FA) ukiliwa nawe tafuta mnyonge wako. Kelele wajihaibisha. Huyo mama keshanusa marashi ya first lady, au nawe gombea urahisi labda atabadili fikra. Lakini nakuuliza kaka huyo mama ana nini mpaka unalia hivyo, kilio chako mpaka kinafika kwa Obama. Tulika mpira kaka kwani timu yako haijawahi kufungwa?

    ReplyDelete
  58. Rais gani mhuni anaiba wake za watu? Nilikuwa nimepanga kumpa kura yangu Slaa lakini kwa kitendo hiki cha kifedhuli simpi tena. Kama anatelekeza mke na watoto je sie raia tutapona kweli akipewa nchi? Mungu hamfichi mnafiki humuumbua hapa hapa duniani.

    Kwa vitendo hivi viovu vya Slaa amejimaliza, JK ameshapita kiulaini. Slaa ametusaliti hakuna hata haja ya kupiga kura.

    ReplyDelete
  59. tuwaite ma-presdar wote waliopita kasoro wa awamu ile ya kweusi, kama walikuwawasfi kweli hili la msaidizi wa jiko tehetehete...

    Hii ni janja ya sisiem si mnakumbuka mrema, maalim nao waliambiwaga hivyo hivyo hawana sera hao, si unakumbuka zengwezi kibao kama shule kufunguliwa dis timu ehh...Watanzania amkenisisem hawana jipya wapo madarakan kwa nguvu...kodi zenu ndo hizooo...

    kama kawa misupu weka kapuni

    ReplyDelete
  60. Hivi mtu mzima mwenye akili timamu anawezaje kuita waandishi wa habari na kusema "nimeporwa mke/mume"???

    Huyo Mke itakuwa alishakuona huna akili timamu ndio maana akasepa na Dr...acha kulia lia tafuta mke mwingine.

    (Utu Uzima Dawa)

    Soames,
    Reading,
    UK.

    ReplyDelete
  61. Jamani Watanzania wenzetu, mambo tusiyoyajua, ni kama usiku wa giza! Ya Silaa tumwachie Silaa mwenyewe! Ana mapungufu na yeye kwa vile ni binadamu jamani. Tusiumie bure vichwa kwa undani wao ambao hatuujui. Tanzania ee nakupenda ee

    ReplyDelete
  62. Katika wanaume MBUMBUMBU duniani wewe lazima ni mmoja wao, yaani unanunuliwa ili uweze kujidhalilisha hadharani. Hao wanaokuthamini saizi baada ya uchaguzi hutawaona tena. Mwaka 2005walituambia Sumaye ana Trilioni kumi, lile gazeti lilipokuja kushtakiwa wao walikuwa wanapeta New York, London na kwingineko. Watanzania chaguo mnalo nyie, kama kumchagua Marcopolo (MZUNGUKA DUNIA) wetu ama kuchagua watu wachapa kazi, its ur decision.

    ReplyDelete
  63. mke amekuacha tafuta mwingine angekuona wa maana angebaki na wewe,hata ukishtaki hawezi kukurudia.huwaoni barabarani walivyojaa tafuta mwingine.au huna kazi za kufanya nikakupe kazi ya shamba ukalime ,by mkuki,

    ReplyDelete
  64. Jamani CCM tunataka mtupe sera na mada za maana siyo kujadili mambo personal ya mtu. Kwani Josephine na Dk. Slaa ni watu wa kwanza kufanya hivyo hadi wageuzwe ishu? Mbona nyie mnafanya hata zaidi ya hayo bwana!! Shindaneni kwa sera na siyo kuingiliana mambo binafsi ambayo sisi wananchi hayatunufaishi chochote. Bwana Mahimbo, hukujua kuwa ukisema wa nini kuna wanaosema tutampata lini? umeshindwa kuhudumia jamaa kachukua mzigo kwaiyo acha kulalama ovyo, unajidhalilisha!!! Moi

    ReplyDelete
  65. Nyinyi msiomjua slaa, tuulizeni sisi wenyeji wa Karatu kuhusu tabia yake au nendeni wenyewe Mbulu mkawaulize watu kuhusu tabia yake. Tuhuma nyingi nzito dhidi yake zimeenea kwa miaka mingi. Natumai sasa wahanga watajitokeza kuwafunua macho Watanzania kuhusu waliovaa ngozi ya kondoo kumbe ni....Kama nitapata guarantee kuwa blogu ya jamii haitashtakiwa au kutishwa wanakaratu tuko tayari kuzimwaga tuhuma hizo hapa. Na ndiyo maana 2005, alishinda kwa kura elfu moja TU dhidi ya mtu ambaye hakuwahi kuishi Karatu.

    ReplyDelete
  66. kumekucha sasa mambo ya Anjelika yamerudi,sasa mambo ya thumni kama zamani.

    ReplyDelete
  67. we bwana hakikisha unalipwa hela yako kama ushahidi upo slaa akulipe hela na mke umuuzie.

    ReplyDelete
  68. Kwa kifupi kama wengine mnaona ni ujanja kuchukua mke wa mtu...basi mmepotea kimaadili. Ndoa iko kwenye sheria, sasa huwezi kumuacha mme au mke bila kufata sheria...Slaa hapo amechemsha, ni bora akubali yaishe hilo kosa...ata kama jamaa amelipwa lakini naye Slaa angefata utaratibu kabla ya kudanganya nchi zima kwamba yule ni mke wake wa ndoa..

    ReplyDelete
  69. Slaa ni mchafu, na sio msafi kama alivyotaka tumuone. Ni muongo, hama maadili...mwenye uchu wa madaraka. Mijitu kama hii ukiwapa nguvu ndio utaona undani wao...Chui kwenye ngozi ya kondoo.

    ReplyDelete
  70. Mdau wa 'Kusoma'September 07, 2010

    Mambo ya maisha ya watu ya kibnafsi kama haya yaanzie Ustawi wa jamii na kisha mahakama.

    CCM sisi tuwe mbali kabisa na tuhuma hii. Sisi tuendelee kumwaga sera zetu tu.

    Katika kinyangányiro tukisema haya graph yetu itashuka!

    ReplyDelete
  71. FIRST LADY KIRUKA NJIA hahaha...Slaa na Josephine wote ni vicheche..kesho waingie ikulu siitakua vichekesho. Huyu ni mwongo asiyekua na maadili kabla hajapata madaraka, akipata itakuaje ?

    ReplyDelete
  72. Alichoniuzi Slaa ni kudanganya wananchi kuwa Josephine ni mke wake akijua kabisa sheria za ndoa zinasemaje...HUYU nilikua nimpe kura yangu lakini sitompa, mijitu kama hii ikipata madaraka ndio utaijua ni NYOKA...

    ReplyDelete
  73. ChIcHiem hiyo imebackfire, go back to the bunker. Watu wazima mmewshindwa kuelewa in Tanzanians minds there is a very THICK line btn private life and politics! You have portrayed him as a hero (4 all wrong reasons)! your case is heard but to us its irrelevant. I LOVE TANZANIA I AM VOTING FOR SLAA!

    ReplyDelete
  74. Hii ndio CCM. Hata mtoto wa chekechea anajua kuwa huyu bwana kanunuliwa. Nahisi hata hizo nguo na hiyo simu kapewa na chama twawala. Ni yaleyale ya CCM kumtumia Angelina kumchafua Mrema miaka ya 90.

    ReplyDelete
  75. Ina maana Slaa hakuwana mke siku zote hadi alivyompora huyu bibi Febr mwaka huu? Mbona mzee hivyo? hata haipendezi kama ni kweli. Viongozi wengi ni wahuni lakini hawachukui waka za wenzao. aibu tupu!

    ReplyDelete
  76. Swali la kujiuliza hapa ni: Kwanini sasa? Why now? Nina hakika huyu mheshimiwa hakugundua jana kuwa huyo anayemwita mkewe kwa sasa yupo na Slaa. Nadhani aliyajua haya miezi kadhaa iliyopita. Hapa inaonyesha kuna mkono wa mtu. Kweli siasa mchezo mchafu.

    ReplyDelete
  77. Hamna haja ya kubishana humu kwenye blog!hatujamsikia binti J anasemaje wala DR anasemaje.....hiyo ni chini ya kapeti!!..........BUT ..........UKITAKA WATU WAUJUE HATA UVUNGU WAKO WA SEHEMU NY*TI UNAFANANAJE INGIA KWENYE POLITICS!!!!

    ReplyDelete
  78. inashangaza sana watu wanaomsakama huyu aliyeibiwa baada ya kukemea ushenzi aliyofanya slaa au kwakuwa ni slaa basi ndiyo halali jamani tumrudie mungu alichokifanya slaa ni ushenzi si duniani wala mbinguni, na lazima tukemee vitendo hivi,kweli tunategemea mtu wa tabia hii tumpe nchi,kama amefikia hatua ya kuiba wake za watu ataweza kutunza rasilimali zetu kwa uadilifu?tusidanganyike na maneno yake matamu no way

    ReplyDelete
  79. michuzi acha mambo hayo kwasababu nimekosea kidogo nikasema blog ya ccm basi umebania kweli? basi sirudii tena ingawa inaegemea ccm.

    ReplyDelete
  80. Mahakama Kuu maliza kesi za EPA, IPTL, RADAR, MRAMBA, YONA na Richmond kwanza. Halfu mtaimaliza hii ya huyo mume ubwabwa

    ReplyDelete
  81. Octoba kura kwa slaa

    ReplyDelete
  82. ccm hii imekula kwako hapa sio kanisani huyo jamaa bwege maana haeleweke kwa nini anamshitaki dr ana akika gani kama alijua ni mke wa mtu hiyo kwanza na pili lini mke aligeuka shamba aliache hapo ukirudi utalikuta
    hapa hakuna kitu ndoa matunzo tulisha toka ujima
    kama ujiwezi kwenye ndoa tutakusaidiaje

    ReplyDelete
  83. Hata kama ni kweli, hao wasiopora wake mbona huenda sio viongozi wazuri kama Slaa?

    ReplyDelete
  84. hili jamaa bwege kweli. badala atulie ili baadaye ale yeye analeta domo. muulize mwenzio aliponyanganywa alipewa uwaziri. nawe ungepewa uwaziri. tulia baba. mpigie kura kura huyo.

    ReplyDelete
  85. yaani wachafuzi wanachemka sana. hivi hamjui kuwa wagombea wenye ishu za ngono wanapendwa sana na wapiga kura. angalia South Africa. mshikaji ana wake wangapi na kashfa za kubaka. angalia Zambia yule mshikaji alikuwa vipi. kumbuka uchaguzi uliopita kiongozi wetu alisemwaje.

    nadhani hii ni dalili nzuri za huyu kaka Slaa kushinda. yaani wanasaidia kumtangaza.

    ReplyDelete
  86. EBWANA HII ISSUE ITS JUS' SILLY NA MTU MZIMA MWENYEWE SIJUI MAHIMBO NAYE SI MZIMA MAANA KAMA NI MWENYE AKILI TIMAMU HILI SI SWALA LA KUWEKA HADHARANI MAANA NI AIBU YAKE MWENYEWE NA ISITOSHE JOSPHINE SI KABINTI KA MIAKA CHINI YA 18 HIVYO ALIONDOKA NA SABABU ZAKE....KWA KIFUPI NAOMBA NDUGU WATANZANIA WENZENGU TUAMKE NA TUONE MAMBO VIZURI MAANA HII NI SIASA CHAFU NDO MAANA TUNASEMA POLITICS IS A DIRTY GAME LAKINI KWA WATU WAELEVU BASI WANALITAMBUA HILI...HII NI GAME YA WATU CORRUPT NA KWA KUWA MUME NAYE ANA-AKILI FUPI AMEKUBALI BILA KUJUA NI AIBU...HIVYO WANACHI MSIDANGANYIKE NA MANENO YASIYO YA MAANA,INGEKUWA NI SWALA LA MAANA BASI ALIKUWA ASEME TANGU MWANZO MWANAMKE ALIPOTOKA NA ISITOSHE KWA NINI AMLAZIMISHE KUWA NAYE ILHALI MWANAMKE HAITAJI????GHALAMA GANI KASABABISHIWA KAMA KUPIKIWA SI JOSPHINE ALIKUWA ANAMPIKIA NA KAMA NI KAZI..JOSPHINE HAMFANYII KAZI YEYE...HIVYO HAMNA POINT,ALL I CAN SAY IS THAT WE GOT TO THINK OF CONSTRUCTIVE ISSUES AND NOT THIS CHILDISH ISSUE....MARK YOU DR. SLAA IS EDUCATED ENOUGH PHILOSOPHY...HATA MUDA WA KUANZA KUBISHANA NA HUYO KIJANA MHIMBO HANA KWANI HAKUNA POINT ANAWEZA ONGEA ZAIDI YA KUONGEA PUMBA NA MASHUDU,INAFAA AANZE SHULE....HONESTLY AM SO PISSED OFF WITH HOW P'PLE BACK THERE HANDLE SOME CASES AND PUT THEM IN THE MEDIA!!!...THIS SHOWS HOW PRIMITIVE SOME OF OUR P'PLE ARE AND HOW CORRUPT P'PLE ARE ESPECIALLY IN THE GOVERNMENT...MDAU WA MANCHESTER....

    ReplyDelete
  87. DR SLAA ALIFIKIRI BADO YUKO UMBULU AU KARATU, KULE NA WAMASAI TOFAUTI YAO NI NDUGU TU HATA WANAWAKE WENYEWE WANASEMA "WAMEPEWA BURE WANATOA BURE" HAKUNA CHA MIMI MKE WA MTU WALA MUME WA MTU. HIZO NDIZO TABIA ZA WAMBULU KAMA MLIKUWA HAMZIJUI.

    NA NDIO MAANA HATA ROSE KAMILI HAKUPATA SHIDA KUMTAMBULISHA DR. SLAA KWENYE MKUTANO WA KAMPENI NA ALIWAOMBA WAMBULU WA HANANG WAMPE KURA SHEMEJI YAO NA MKWE WAO, NA WALA HAKUSEMA MPENI KURA MZAZI MWENZANGU, YAANI AKONYESHA KUWA WAMESHAACHANA. HIVYO HUYO ROSE HAWAJAACHANA ILA NI NOMA KUMWEKA KAMA FIRST LADY KWA SABABU ALIKUWA KADA WA CCM MPAKA JUZI TU ALIPOSHINDWA KWENYE KURA ZA MAONI.

    HABARI NDIO HIYO KWETU MBULU HAYO NI KAWAIDA TU! Saitah!

    Ukishajiingiza kwenye siasa na kujifanya wewe ni mtakatifu wakati si mtakatifu ujue utakuja umbuka tu siku moja, hata watu wakimtetea lakini mwenyewe anajua kwenye nafsi yake siri yake yeye na mungu wake na viongozi wake wa kidini kilichomfanya akaondoka huko Baraza la Maaskofu ambako alikuwa na ulaji mkubwa tu! Lakini iko siku nayo hiyo itatoka na zile ndoto zetu zote zitambumburuka. Kwani duniani hakuna siri, siri ni jambo lile ulilolifanya wewe peke yake.

    ReplyDelete
  88. Mahimbo wacha kutia aibu wanaume, wewe umeshindwa kuhudumia familia yako mama akaondoka, kwasababu ulitaka aondoke ndiyo maana hata ujamtafuta tangu March, yaani hukuwa na haja naye sasa kapata pakushika unaanza kuchafua watu kwa utashi wa mafisadi, ulivyokaa mtoto wa kihaya humuwezi wacha wahaya tuoane wenyewe, mama wa kihaya anataka bwana wa kutafuta siyo kama wewe umevaa kinigeria, nakushauri tafuta mke mwingine, wacha kutia aibu.

    ReplyDelete
  89. Ankal hivi tunaanzaga kuvaa viatu kabla ya soksi au? maana nimesahau kibogo...Nadhani unapenda comment kama hizi kwani umebana comment zangu zote leo

    ReplyDelete
  90. Wewe baba hujui hata mila na desturi za kwenu, ndiyo maan mke kakukimbia ungekuwa umefundwa wewe mke ungekuwa nae, unasimu mbili mkononi kwa nini hukuwa unawasilina na mkeo, hizo simu siku zote ulikuwa unawasiliana nanani. Kwanza kabisa unaonekana si mtu hata wa kumpatia mkeo kikombe cha chai. Unajiona wewe ni wewe tu na mke kama vile mfanyakazi wako. Hongera mama umeondoka mapema kwani huyu si mume bali ni balaa. Mama nakutakia mafanikio mema na kura yangu nampigia Dr, Slaa kwani inaelekea yeye anjuwa Mke maana yake ni kitu gani.
    Wewe baba ka chini fikiria jinsi ya kutunza hao watoto, mambo ya kwenda mahakamani na kupigania mtoto wa watu uache, ndowa siyo kwamba mtu awe mtumwa wako huyo ni binadamu na nauhuru wa kwenda na kufanya nachotaka, kwani kama ungekuwa mume wa ukweli mke asingekuacha. Sisi tunasubiri tusikie kwa jirani na rafiki zako wakuumbuwe vyema. Acha watoto wa watu hata ukilipwa hiyo pesa hutakuwa na furaha na labda itakuwa ni pesa ya kunywa pombe na makahaba tu. Kwani kilichomkimbiza mkeo watu wankijuwa. Nenda kwenu uliza wazee wakufunde vizuri next wife asije akakukimbia. Elimu ya jamii ni muhimu kwako wewe baba heshimu wakina mama.

    ReplyDelete
  91. jamani mbona haya si mapya?mwanasiasa maarufu na rais wa kwanza mweusi wa South Africa Mh Nelson Mandela alianza mahusiano na Graca Marcel hata kabla ya kuachana na Winnie ambaye hatimaye baadaye alimuacha na kumuoa Graca, huyu ni Mandela role model duniani sembuse Slaa!! Come oooon!! Michu hata mjipange vipi kumchafua Slaa hatudanganyiki.. people's power!

    ReplyDelete
  92. Pole Bro Amanieli. Sisi tunaokuja tunatambua majaribu yaliyokusibu. Be strong...Mungu atakusaidia na "Dr" Slaa ataadhirika tu.

    ReplyDelete
  93. Anon wa 11:23:00 PM, Wacha ukichaa wako wa kumfananisha Slaa na Mandela. Hamna mtu anataka kumchafua Slaa kwa sababu mambo mabaya aliyoyafanya yanajulikana. Wala hakutumwa na Mungu kama mnavyosambaza. Hafa hafai hafai kabisa. People's power bado iko CCM. Tusiandikie mate wakati wino upo. CCM IMARA!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  94. huyu mwanaume simwelewi kwasababu anasema amefunga ndoa kanisani halafu anaonekana amevaa kiislam, kingine muda wote huo alikuwa wapi mpaka leo ndio anaamua kufungua mashtaka, hii yote ni dalili ya kutaka kumchafulia slaa na umehongwa na ccm. kama ulishindwa kumhudumia acha wengine wamuhudumie.

    ReplyDelete
  95. BWANA MAHIMBO , URIJALI UMEKUSHINDA ,IMEKULA KWAKO.
    TUTAKUCHANGIA BILIONI MBILI UKAE KIMYA NA KUJIUGUZA MAJERAHA!!!!!!

    ReplyDelete
  96. Dat is bullshit Mr . Kama ukuweza kutake care your BIACH let other men help you and stop saying de other man took ur BIACH. Blame your wife for leaving you ,she is adult she knows what she is doing ,she ain't a baby she is grown ass woman let her go they way you used to go

    ReplyDelete
  97. Kosa ni la mke kuto kumweleza Slaa ukweli kama alishaolewa. Yafaa uthibitisho utolewe kuwa Dr. Slaa alikuwa akimfahamu huyo Mahindi na kwamba kwa makusudi aliamua kuchukua mke wake. Otherwise, Mahindi mchemfu kufa mtu!!! Ila hela ina majaribu washikaji, unaweza ukajitoa mhanga kiasi hiki? Alishoniudhi ni kuwaingiza na mabinti zake kwenye matatizo yake, bulshit!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  98. BWANA MAHIMBO acha uzushi.....
    Epuka kutumiwa vibaya na wanasiasa.
    Mimi ni Mwanachama, pia Kada wa CCM lakini jiulize baada ya yule mwanamke kutumiwa kumwangusha Mrema yuko wapi hii leo.
    Utatumiwa na malengo yakikamilika utatupwa kwenye kapu la sahau.
    Pili.... Tukizungumzia Usafi wa Ndoa leo hii ni Kiongozi gani wa Serikali yetu atasimama?
    Binti yangu niliyemzaa 22yr ago nilienda naye Dodoma ... kilichotokea ni aibu maana sio wabunge wala mawaziri waliomtongoza
    Katika mkasa mmoja Binti yangu alimpa Kiongozi mwenzangu namba yangu ambayo natumia kwa mambo ya kifamilia, naye alinipigi na nikatambua sauti akadai amekosea namba, lakini binti yangu aliniambia na HADI LEO HATAKI TENA SIASA.
    NAJIULIZA upepo ukitugeukia itakuwaje.... Rais mawaziri na wabunge ni wanaume wangapi tumewadhulumu ndoa zao???
    TUCHAGUE VIONGOZI WENYE SIFA ZIFUATAZO:
    1.WASIOPENDA RUSHA NA KUENDEKEZA URAFIKI NA DHULUMA
    2.WAOKUWA WASHIRIKINA
    3.WASIO WEZI
    *** Nawasilisha Ndugu Michuzi,
    naomba usibanie

    ReplyDelete
  99. Baba umemechisha, simu mbili na kiti cha enzi eti unapiga vuvuzela eti umeibiwa mkeo. Mbona hulalamiki kutunziwa wanao?

    ReplyDelete
  100. Ndugu umeniaibisha sana mpare mwenzio yaani tumefikia mahala tunawatafuta namna hiyo mbona hizo kwetu kule thio dhetu wajina.Noma sana ona sasa au ndio hivyo utu uzima mambo huko chini nayo yanaenda msobe msobe pole thana thatha twende thuji kwa wadhee basi

    ReplyDelete
  101. Mbona ya Karamagi na mke wa John hamkuyatangaza magazetini ?au kwakuwa John alipozwa na ukuu wa wilaya?
    mdau.

    ReplyDelete
  102. nataka nikueleze hivi hakuna penzi linalonunuliwa kwa pesa hata ukipewa burget nzima ya serikari hakuna penzi ebu acha ushamba wa kutaka kujulikana kupitia vyombo vya habari.by mkuki

    ReplyDelete
  103. Ndio,
    Nimempata Bwana Aminiel, sio mwanamume wa kuaminika. Kwa vile niko Dar naanza mchakato wa kumchukua hata huyo uliye naye. Hawizekani ulalamikie kwenye magezeti,na TV namfuata huyo uliye naye nsjua hutalalamika. Mimi ni mtu wa kawaida sitafuti uraisi.

    Mdau

    ReplyDelete
  104. KWA MUELEKEO WANGU SILAHAa ni mwana CCM damu iweje msomi kama yule anajua mambo kashfa , na anajua akiwa mpinzani atapata mashabiki, kwanini asijiandae mapema kuepusha kashfa hizo? HAPO BONGO HAKUNA UPINZANI DANGANYA TOTO; mdau ITALY

    ReplyDelete
  105. Bwan Mahimbo hata haya huna! Lazima una mapungufu ya kiume au Mr P kawa mvivu! Aibu kweli!

    ReplyDelete
  106. HUYU JAMAA KWELI HAZIMO,YAANI WEWE UNALALAMIKA LEO HII,SIKU ZOTE ULIKUWA WAPI??KWELI WAJINGA NDIO WALIWAO,JUST WANNA DEDICATE U DA SONG ``BADO NIPO NIPO KWANZA`` BY MWANA FA,LABDA UKIUSIKILIZA WIMBO HUU UTATIA AKILI,KAMA UKIONA VIPI MTAFUTE MNYONGE WAKO NA WEWE UMMEGE,CCM HAMNA SERA TUMESHAWAZOEA NA TUMEWACHOKA KWA UFISADI...BIG UP DR SLAA..GO GO GO, ITS A TIME TO WAKE UP WATANZANIA MTALALA HADI LINI???KWELI WATZ MMELOGWA NA ALIYEWALOGA ALISHAKUFA NDIO MAANA MNAZIDI KUCHAGUA CCM TUUU

    ReplyDelete
  107. Mimi sioni tatizo, kama Slaa angekuwa ana mahusihano na mwanaume mwenzie nafikiri ndicho kingefanya kumnyima kura yangu. Hivi hata wewe unayesoma sasa hivi hujawahi kuharibu mahali!!!!!????


    Nkyabo - Bongo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...