JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIAUZUSHI KUHUSU MADHARA YA MAWASILIANO YA SIMU

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imepata malalamiko kutoka kwa watumiaji wa simu za mkononi kwamba kuna ujumbe unaosambazwa kwamba ukipokea simu utapata madhara.

Mamlaka ya Mawasiliano inapenda kuwahakikishia wananchi kwa ujum;a kwamba taarifa zinazoenezwa ni za uzushi na sio za kweli. Wananchi wanaombwa kupuuza uzushi huo kwa kua hauna ukweli wowote.

Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, kuna tafiti nyingi zimefanyika sehemu nyingi duniani, ambazo zimeonyesha kwamba kiwango cha mawimbi ya mawasiliano hakina madhara kwa afya ya binadamu. Mamlaka inashauri watumiaji wa huduma na wananchi wote kwa ujumla, kuendelea kuwa na imani na teknolojia mpya zikiwemo za mawasiliano ya simu, utangazaji na utumiaji wa kompyuta, ambazo hutumiwa ulimwenguni kote bila kuleta madhara yoyote.

Madhumuni ya Mamlaka ya Mawasiliano na watoa huduma za mawasiliano kwa ujumla ni kuwaletea wananchi wa Tanzania mawasiliano bora kwa kujenga miundombinu, kutoa huduma bora na matumizi mema.

Uzushi unaoenea upuuzwe kwa kuwa hauna ukweli wowote.

Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Sasa Bro michuzi nini maana ya security waliyoisema itakuwepo kipindi line zikisajiliwa?
    Si watafute chanzo(source)ya sms ya kwanza kabisa, maana kiusalama watu wametishiwa maisha yao!
    Hiyo moja...

    Idea nyingine, je tuna uhakika vipi hizi sms za thread(watumie na wengine pia..)Si kutoka kwa hizi kampuni zetu za simu to boost up sales ya siku?

    Mi ni ideas zangu tu ili at least tuwe aware na mambo ya kitaifa against wajinga wachache sana!!

    Ni hayo tu

    The Dreamer!

    ReplyDelete
  2. Pongezi kwa Mamlaka kutoa taarifa hii maana hali ilikuwa ya kutisha. Atafutwe alianzisha meseji hizi na achukuliwe hatua za kusheria kwa kusababisha usumbufu. Mamlaka ya Mawasiliano ihakikishe hali kama hii haitokei tena.

    ReplyDelete
  3. hiyo meseji ya kwanza itafutwe ilipotoka

    ReplyDelete
  4. Ankal lazima tukubali ukweli: sisi Waafrika - ikiwemo TZ - (majority) ni washirikina sana ni rahisi sana kudanganywa. Hii inatokana na (1) ujinga wa kutofahamu kanuni za sayansi; (2) kutokuwa ni imani thabiti ya Mwenyezi Mungu (usidanganyike kuona watu makanisani na misikitini, wakitoka huko wanakwenda kwa 'jujuman'). Niliposikia haya mambo ya simu nilijiambia "haya, mambo ya wachunangozi na waua maalbino yameanza, wajinga ndio waliwao." Tukiendelea hivi, tutazidi kuwachwa nyuma na mabara yote duniani. Tuamkeni, tuachane na ujinga huu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...