Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya watanzania wanaosomama kwenye Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala wakati alipozungumza na watanzania waishio Uganda kwenuye Ubalozi wa Tanzania Mjini Kampala leo.Waziri Mkuu, Mizengo Pindana Mkewe Tunu wakisalimiana na baadhi ya watanzania waishio nchini Uganda kabla ya kuzungumza nao kwenye ubalozi wa Tanzani Mjini Kampala leo.
Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda akizungumza katika Mkutano kati ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kulia) na Watanzania waishio nchini Uganda uliofanyika kwenye ubalozi wa Tanzania Mjini Kampala leo. Kushoto ni Mke wa Kaimu Balozi wa Tanzani nchini Uganda, Naomi Ndatta.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hiyo kanga yenye picha sura ya Mwalimu inaonyesha jinsi mlivyompenda.

    ReplyDelete
  2. kuna Dada mmoja hapo kafurahi kupita kiasi naona aliota usiku ukutano wake na waziri mkuu

    ReplyDelete
  3. Cheka basi angalau kidogo Pinda, watu wanakuchekea we umenuna,utajizeesha mapema,we subili.

    ReplyDelete
  4. 'Vipi? Mambo Freshi?

    ReplyDelete
  5. Wanafunzi wa ki-tanzania Uganda nilitegemea watauliza maswali ya msingi na sio ya bandari ya Bagamoyo. Hata ikiwa swali linahusu banadari, basi wangelipaswa kuhoji kwanini serikali iingie kwenye mpango wa kujenga bandari nyingine badala wakati zilizopo hazifanyi kazi kwa kiwango kinachotakiwa?
    Pia, licha ya watanzania 600,000 (nina wasiwasi na takwimu hii, nadhani ni 60,000) kwa nini hakuna benki ya Tanzania yenye matawi Uganda wakati wateja tayari wapo hasa wazazi wanaotuma ada kwa wanafunzi.
    Pia, je Pinda anafahamu kuwa Shilingi ya kitanzania haipokelewa na vyombo vya fedha vya Uganda?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...