Matroni wa wodi ya kina mama bi. Haule akimhudumia mtoto na aliyembeba ni Bi Sabina Lyombo mama wa mtoto
Hivi ndivyo kichwa cha mtoto kinavyoonekana

Na Sekela Mwasubila, Ulanga
Mtoto mmoja katika hospitali ya Wilayani Ulanga mkoani Morogoro amezaliwa ubongo ukiwa nje baada ya kukosa ngozi ya kichwa huku akiwa mwenye afya njema.

Akiongea na mwandishi Kaimu Mganga Mkuu (W) Dkt Amani Kombe amesema kuwa tukio hilo lilitokea siku ya jumatatu majira ya saa tatu usiku baada ya mama wa mtoto kujifungua mtoto huyo wa kiume hospitali hapo.

Aliongeza kuwa hali ya mtoto kuzaliwa na kukosa ngozi ya kichwa hutokea wakati wa uumbaji wa viungo mbalimbali vya mwili wa mtoto na hali hiyo huweza kusababishwa na ukosefu wa madini mbalimbali kwa mama wakati wa ujauzito aidha ni tukio la kwanza kutokea katika hospitali hiyo ya wilaya.
Naye mama wa mtoto bi. Silvia Lyombo (20) ambaye ni ujauzito wake wa kwanza alisema kuwa hakupata matatizo yoyote ya kiafya wakati wa ujauzito na alijifungua katika hali ya kawaida mtoto mwenye uzito wa kilo 2.9 na kuwa ananyonya kama kawaida na hana tatizo lolote zaidi ya kukosekana kwa ngozi ya kichwa aidha hakuna dawa zozote ambazo alizitumia katika kipindi chote cha ujauzito wake.

Hata hivyo wataalamu wa hospitali ya wilaya walisema kuwa watampeleka mtoto huyo katika hospitali kubwa mkoani Morogoro kwa uchunguzi zaidi wa nini kifanyike kukabiliana na tatizo la mtoto huyo ambaye hadi sasa yupo hai na afya njema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Kutokana na hali halisi ya maisha yetu hapa Tanzania, mama anahitaji msaada mkubwa sana kumkuza mwanae, hii ndiyo fursa jamani si pingi watu kusponsor umiss au club za michezo n.k, pia tujitahidi kuangalia kiasi flani jamii yetu na kusaidia wanaotegemea msaada toka kwetu.
    Mdau.

    ReplyDelete
  2. Tukio hili uitwa kwa kizungu "deformed at birth or birth defect" huwa inatokana na viungo kutokamilika kukua vizuri wakati wa mimba. Kuna sababu nyingi sana zikiwepo:

    1) Ukosekaji wa madini muhimu wakati wa mimba

    2) Sumu - kwa mfano mekyuri - je mama huyu alikuwa akifanya kazi kwenye migodi ya dhahabu huko Ulanga morogoro? Zile mekyuri zisizo kuwa handled kitaalamu zina madhara kama haya.

    Mekyuri ya wachimba dhamabu kienyeji hawa wakubwa saa nyingine uingia kwenye mfumo wa maji hivyo wanavijiji wa jirani huweza ku-athirika bila kijijua

    3)Sumu - mfano madawa ya mazao kama DDT pia huweza sababisha demormed birth

    4) Sumu - nyingine hutokana na miti shamba, hizo tunaziita dawa za miti shamba, jamani utomvu wa miti mingine ni sumu mbaya, hata uuwa ngombe na tembo pia.

    Sasa sisi watanzania tusimtafute mchawi kwa hili, viongozi wa huko Ulanga wachunguze waweze kufahamu chanzo na kuchukua hatua kuzuia hili lisitokee. Hakuna cha Allah Akbar au Mungu Mkubwa

    Wadau vipi hapo?

    Alex bura, dar

    ReplyDelete
  3. Bongo tambarare lakin bado sonogram hakuna na pia labda hakwenda clinic huyu alipokua mja mzito? Mungu ambriki mwanae asijeakapata infection tu hapo.

    labda nchi za wenzetu zitamchukua huyu na kuurudisha ndani ubongo wake..

    ReplyDelete
  4. Anon wa pili, toa reference tafadhali!

    ReplyDelete
  5. Mungu amsaidie mtoto wa watu

    ReplyDelete
  6. MUNGU WACHA AITWE MUNGU,KITU CHA HARAKA HAPO HOSPITAL WASIMCHELEWESHE WAMPELEKE HARAKA MOROGORO NAPO APITE TU APELEKWE MUHIMBILI MAANA ILE NDIO HOSPITAL YA RUFAA NA INA WATAALAMU WENGI,NA NI RAHISI KUPATA HATA MISAADA KWA HALI NA MALI.ASIJE POTEZA MAISHA MAANA INATAKIWA MALEZI YA HALI YA JUU NA UANGALIZI MKUBWA,
    ANON NO,3(ALEX) UMETOA MIFANO YAKO KITAALAMU ULIONEKANA WA MAANA, LAKINI UMEJISHUSHA HADHI MNO, KUTAMKA HAKUNA ALLAHU AKBAR AU CHA MUNGU MKUBWA!! NAKUSHANGAA SANA INA MAANA HUKO HUKO MGODINI HAKUNA WATOTO WANAOZALIWA SALAMA? NA WANAFANYA KAZI NA VITENDEA KAZI KAMA VYA HUYU ALIEATHIRIKA? ULIELEZA VIZURI LAKINI UMEONYESHA KUWA NI MWANA MPOTEVU UNAHITAJI MAOMBI.

    ReplyDelete
  7. Niliamua kutochangia blog hii baada ya kukwazwa na mwenendo wake wakati wa uchaguzi ila kwa kujenga ngoja niweke ya kwangu.

    Sasa hivi technologia imekuwa sana, Tanzania tunahitaji kuwa na scanner za kisasa jamani, tatizo hili lilitakiwa kujulikana tokea wiki ya 20 na ku-terminate mimba. Mbona huku kwa wenzetu wanaweza kujua mpaka mtoto mwenye mtindio kabla hajazaliwa.

    Tatizo la viongozi wetu wao kila kitu wanakwambia usifananishe na nchi zilizoendelea, wakati vifaa hivyo vinauzwa na havipo ardhini kusema hivi ni vya ardhi ya nchi zilizoendelea tu nchi nyingine havifanyi kazi. Tuwe makini sasa, katika kuboresha huduma za afya.

    Ukweli ni kwamba mtoto huyo anasubiri muda wa kufariki tu hakuna cha ziada maana matibabu yake yanaweza kuwa sawa na gharama za kununua scanner ya kisasa.

    ReplyDelete
  8. mungu amsaidie mama na mtoto yawezekana alijaribu kutoa mimba kwa miti shamba ikashindikana hilo nalo liangaliwe

    ReplyDelete
  9. Jamani acheni kuto comments ambazo zinaumiza wengine. Kwani nyinyi ni nani na mnajua mipango ya Mungu?

    Naamini Mungu ana mipango na kila mmoja wetu hapa duniani. hamuwezi kushangaa alitokaje tumboni kwa mama yake bila kujeruhiwa akiwa njiani? kama Mungu alitaka asiishi asingemwacha atoke salama. Still naamini kuna sababu ya kuja kwake duniani na Mungu atampitisha salama salimini.

    Ni kweli awahishwe katika hospitals kubwa, na wasamaria watakaoweza kusaidia na tusaidie kumsaidia mama huyu. Kuanza kuzungumzia termination na nini wakati kiumbe kimeshafika haiko sawa, hebu jiweke katika miguu ya mama (msichana) huyu.

    nawatakia kila la heri

    ReplyDelete
  10. jamani msimsahau mwenyezi MUNGU huyu mtoto atakuwa kwa uwezo wake aliye muumba hakuna aliye kamilika mtu yeyote anaweza fariki na mtu yeyote anaweza kusavaivu badala mumuombee mnaleta midomo ili??
    naomba wauguzi wampe mapenzi na huduma kadri ya uwezo wao kwani hakuomba kuzariwa vile na kama nchi yetu haina uwezo basi wampeleke hata nchi zenye uwezo huwezi juwa kesho atalifaa vipi taifa letu. yesu ni mwema yesu baba mlinde huyu mtoto akuwe kwa nguvu zako na baba muuba bingu na nchi AMIN

    ReplyDelete
  11. EH mWENYEZI mUNGU UMUANGALIE HUYU MTOTO NA WAZAZI WAKE NA IBARIKI KAZI ZA MIKONO YA WAUGUZI NA MADAKTARI NA WALE WOTE WATAKAOGUSWA KATIKA KUMSAIDIA HUYU MTOTO APONE.JAMANI KAKA MICHUZI HUYU MTOTO ANAHITAJI MSAADA SIO MPAKA HALI IWE MBAYA NDIO WATU WAANZA KUKIMIZANA NA KUCHANGISHANA.KAMA KUNA LOLOTE LA KUFANYIKA LIFANYIKE MAPEMA,MIMI NI MWANAMKE YAANI I FEEL CRYING JUST BY SEEING THESE PICTURES.INASIKITISHA SANA LAKINI MUNGU WETU NI MWEMA ATATENDA MAAJABU NA JITIHADA PIA ZINACHANGIA.MUNGU ASIMAMIE KATIKA HILI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...