Rais Jakaya Kkwete amemteua Dkt. Mwelecele Malecela (pichani) kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa leo na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, uteuzi huo unaanza Desemba 14, 2010.
Dkt. Malecela ana shahada ya juu ya uzamivu ya vimelea vya magonjwa ya binadamu katika fani ya matende na mabusha kutoka chuo kikuu cha London University, Uingereza. Amefanya kazi NIMR kwa miaka 23 sasa na kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkurugenzi na Uratibu na Kukuza utafiti, na amekaimu nafasi ya Mkurugenzi mkuu Nimri toka mwaka 2009

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Ankal, tunampongeza dada yetu Dr. Mwele lakini ningependa kama itawezekana utupatie full CV ya huyu mwana mama. Hakika anastahili hongera.

    ReplyDelete
  2. Nae kasubiri sana kutajwa, hatimaye.

    ReplyDelete
  3. mdau wa mwanzo, ukishapewa cv yake itakusaidia nini katika maisha yako ya baadae? Humjui hakujui, kutaka kujua zaidi ya yaliyoelezwa juu ya huyu bibie ni ushambenga tu!

    ReplyDelete
  4. We annoy wa 3 huna akili hujui kusoma CV ya mtu inakusaidia kupata challenge na kukupa hamasa watu wengine mna uelewa mdogo sana, any way hongera Dr.Mwele, naona wapare wote wa NIMR kwishnei maana taasisi imejaa wapare utafikiri tupo same?

    ReplyDelete
  5. ANONY WA 3 ACHA USHAMBA YANI UMEJIONESHA JINSI ULIVYO KILAZA.CV NI KITU CHA KAWAIDA AMBACHO HUTOA MOTIVATION NA MWANGA KWA WENGINE KATIKA JITIHADA ZA KUPAMBANA NA MAISHA.WASOMI WOTE HUWA TUNAANGALIA CV AU PROFILE ZA WATU WALIOFANIKIWA KATIKA MALENGO YAO AU WALIO KATIKA NAFASI NZURI AS INSPIRATION.LAKINI KWA AKILI YAKO YA MAJUNGU UMEKURUPUKA KAMA KENGE MTONI.HONGERA SANA DR MWELE.

    ReplyDelete
  6. Uliyekuwa unata cv, majibu yako tu yameonyesha ulikuwa na green monster haya Dr Mwele leo kawa mpare, makubwa mbadilishe na dini pia. Wanatolewaga wanaume hapa wameteuliwa lakini husikii watu wakiomba cv.

    ReplyDelete
  7. Hongera Dr Mwele. Kazi njema.

    ReplyDelete
  8. Hongera sana na kila la heri!!

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  9. We anon unayesema wapare waliopo NIMR wamekwisha mshamba mkubwa wee, wapare wameingia na vyeti vyao, Dr. Mwele sio mshamba kama wewe wakujali ukabila yeye anajali uchapaji wa kazi. Nenda shule ukalimike!!

    ReplyDelete
  10. wewe mdau wa Fri Dec 31, 09:35:00 PM na amdau wa Fri Dec 31, 10:53:00 PM,, kama kweli unategemea kusoma cv za watu ndio mnapate motivation basi nyinyi ndio washamba na wenye akili finyu. unless kama bado ndi kwanza mnaanza shule na hamjawa na muelekeo wa nini mnataka kufanya katika maisha yenu! otherwise cv ya mtu sioni itakusaidiaje wewe katika maisha yako ya baadae, na wala sioni ni vipi cv ya mtu itakubadilishia maisha yako. Kinachokubadilishia maisha yako ni determination yako juu ya malengo yako na sio kukaa na kutobolea macho cv za watu

    ReplyDelete
  11. Eh, Ain't she cute?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...