- Benki kuu ya Tanzania imetoa toleo jipya la noti za shs 500, 1000, 2000, 10,000. Noti hizi zitaingizwa katika mzunguko tarehe 1 Januari 2011. Noti za zamani bado ni fedha halali na zina thamani sawa na zile mpya. Zitaendelea kutumika na kuwepo katika mzunguko sambamba na hili toleo jipya la noti mpaka hapo hizo za zamani zitakapotoweka taratibu na hatimaye kwisha kabisa kwenye mzunguko. Hivyo basi, wananchi wanashauriwa kuendelea kuzipokea na kuzitumia noti za zamani bila shaka au wasiwasi wowote kuhusu uhalali wake hadi hapo zitakapokwisha na kutoweka kabisa katika mzunguko. Vilevile ieleweke kuwa hakutakuwa na ubadilishaji wa kupeleka noti za zamani benki na kutaka kupewa mpya.
- Toleo hili la noti mpya lina taswira inayozingatia mandeleo ya uchumi na jamii. Tumefanya mabadiliko kidogo katika toleo jipya kwa kuweka picha za waasisi wa taifa letu. Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anaonekana kwenye noti ya shilingi elfu moja na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume kwenye noti ya shilingi mia tano. Noti tatu zilizosalia yaani elfu mbili, elfu tano na elfu kumi zitaendelea kuwa na picha za wanyama pori ambao wanapatikana kwa wingi kwenye hifadhi na mbuga zetu za wanyama. Hata hivyo, kutokana na kupunguza ukubwa wa noti hizi mpya tumeweka picha za vichwa vya wanyama hao badala ya wanyama wazima kama ilivyo kwenye noti za zamani.
- Ili kupambana na uhalifu wa kughushi na kuongeza muda wa noti hizi kukaa katika mzunguko kwa muda mrefu kabla ya kuchakaa, toleo hili limeongezewa ubora kwa kuweka alama maalum mpya za usalama na kutumia taaluma mpya ya kuziimarisha. Alama mbali mbali za usalama zimeboreshwa na kwa mara ya kwanza kabisa alama ya “motion” ambayo ni rahisi sana kutambulika kwa macho imetumika katika noti hizi. Ili kuelimisha wananchi kuhusu alama za usalama zinazotambulisha uhalali wa noti zetu, tumetoa matangazo na vipeperushi ambavyo vitasambazwa sehemu mbali mbali za nchi. Taarifa ya alama za usalama za noti pia zipo kwenye tovuti ya Benki Kuu kwa anwani www.bot-tz.org
- Ni muhimu kwa umma kufahamu alama za usalama ili uweze kutofautisha noti halali na bandia kwa urahisi. Hata hivyo Benki Kuu inapenda kutahadharisha watu wawe waangalifu na kuzichunguza noti zote wanazopokea hasa kwenye giza ili kuhakikisha kwamba ni noti halali. Uchunguzi ufanywe kwa noti zote zilizopo kwenye mzunguko pamoja na za zamani. Endapo wana mashaka warejee kwenye mabango na vipeperushi vilivyotolewa na Benki Kuu au tawi lolote la Benki Kuu.
Gavana
Benki Kuu ya Tanzania
Naomba kufahamu hivi sisi watanzania hatuwezi tengeneza/design noti ambayo itakuwa bora na imara na ina picha ambayo tunaitaka. Na itumike kwa muda mrefu sana!!!
ReplyDeleteMbona kila leo tunabadili noti, ukiangalia nchi nyingine zilizoendelea ni nadra sana kufanya mabadiliko ya noti kama sisi....
Je haya mabadiliko yanafanyika kwa manufaa binafsi nini?. na hata huko bank kuu sina uhakika kama stock ya hizi noti wanazotaka kuzitoa imeisha (yaani ambazo ni mpya kabisa ila ndio hazitaingizwa kwenye mzunguko kuanzia january 1, 2010)
Nafikiri ingekuwa bora kama sisi watanzania tungekuwa concerned na hela yetu kushuka thamani!!! nadhani hapo tungekuwa tunafikiria cha maana zaidi....
Hakuna jipya hapo.haya kaka MICHUZI na hii ibanie.Hahahaa jana Gavana kanifurahisha sana kwenye HOTUBA yake pale aliposema EURO ya UINGEREZA...Wajameni UINGEREZA wanatumia 'EURO' ama 'POUND'Nielewesheni wajameni maana mimi ni mgeni maeneo haya!!!
ReplyDeletehizi siasa, yaani wamemweka karume leo walikuwa wapi siku zoote?
ReplyDeletemafuta nini?
nyinyi hamjui maana ya serikali kubadilisha pesa ni kuhahakikisha wale mafisadi walioficha mabilioni ya pesa kwenye masimtank yao majumbani mwao wanayatoa , hapo serikali imewakomesha mafisadi woote walioficha pesa , sasa kazi kwao ...
ReplyDeletemdau
dar
Fisadi anaficha dolla wewee
ReplyDeletewe unafikiri,fisadi gani mjinga kiasi hicho mpaka afiche hayo makaratasi.
Minaona tunapelekwa pelekwa tu, wananchi libidi tuhusishwe kwenye swala kama hili na tutoe maoni yetu kabla uhamuzi haujafanyika,
siyo kupelekwa pelekwa tu.
Kati ya wote waliochangia hapo juu na nikipewa nafasi nimpate mshindi mwenye maoni mazuri ya ukweli basi ni Anony wa Sun Dec 19, 09:21:00 AM.
ReplyDeleteNi kweli watanzania wengi wana pesa na wamezificha aidha nchini Tanzania au nje ya nchi.Ili hizo pesa zirudi basi mbinu ya kuwafanya wazirudishe ni kubadilisha fedha.