January 2010
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akikagua athari za mafuriko yaliyovunja daraja la Gulwe na kakata mawasiliano kati ya Mji wa Mpwawa na eneo la la Kusini la Wilaya hiyo wakati alipotembelea eneao lililoathirika kwa mafuriko katika wilaya hiyo leo. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. James Msekella.
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akitoa maelekezo wakati wa kukakagua athari za mafuriko yaliyovunja daraja la Gulwe na kakata mawasiliano kati ya Mji wa Mpwawa na eneo la la Kusini
la Wilaya hiyo huku Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. James Msekella akimsikiliza kwa makini.
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwapungia wananchi wa eneo hilo
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiangalia athari za mafuriko yaliyovunja daraja la Gulwe na kakata mawasiliano kati ya Mji wa Mpwawa na eneo la la Kusini la Wilaya hiyo. Shoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. James Msekella.





Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Pius Msekwa akiwahutubia vijana jana mjini Dodoma leo juu ya umuhimu wa kushikamana na kujenga umoja wakati wanaelekea katika Uchaguzi Mkuu, mara baada ya kuwasimika Makamanda wa UVCCM wa wilaya zote za Dodoma na Mkoa katika Sherehe zilizofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM Taifa mjini Dodoma.
Makamanda wa CCM wa wilaya na Mkoa wa Dodoma. Toka kulia kwenda shoto ni Mh. Hezekiah Chibunje,huyo ni Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Dodoma, anyefuata ni Mh. Zabein Mhita yeye ni Kamanda wa UVCCM Kondoa Kaskazini, Mh. Job Ndugai, Kamanda wa UVCCM Kongwa na Mh. Laurent Hoya yeye anakuwa Kamanda wa UVCCM Chamwino.



no image
Habari yako kaka michuzi.
mimi ni Sakina. Shida yangu ni kiwanja maeneo ya kitunda au kigamboni, chenye gharama ya shilingi milioni 2 na nusu. Awali nilikuwa nawasiliana na mwenyeji wangu wa huko Dar akawa ananiambia viwanja kwa sasa ni kuanzia mil.5. Lakini nilipata tetesi kuwa sehem nilizozitaja naweza pata kwa bei nafuu kidogo.

Tafadhali wadau, yeyote mwenye kuweza
kunisaidia awasiliane na mimi kwa email yangu;
sakinaabd@yahoo.com
natanguliza shukrani zangu za dhati!
WEKUNDU WA MSIMBAZI SIMBA SC.
KATIKA PICHA RASMI YA MWAKA 2010


Vinara wa ligi kuu ya kandanda ya Vodacom Simba SC leo wamevunja mwiko kwa kuibanjua Toto Africa ya Mwanza bao 2-0 kwenye uwanja wa nyumbani wa vijana hao wa Kishamapendo wa CCM Kirumba na kuendelea kuongoza ligi wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja hadi sasa.
Simba walikuwa hawajawahi kuifunga Toto Africa toka ipande daraja misimu miwili iliyopita, na mchezo wao wa mwisho Simba ilibugia 4-1 walipotia mguu Kirumba mwaka jana. Lakini leo kibao kiligeuka na kukuta wenyeji wakisalimu amri katika mchezo uliojaa visa kiedekede.

Kisa kimojawapo ni Simba kugoma kuingia kwenye chumba chao cha kuvalia kwa madai kwamba walikuta matone kama ya damu yametapakaa kila sehemu chumbani humo. Kwa mujibu wa meneja wa wekundu hao wa msimbazi, Innocent Njovu, walimwita kamisaa na waamuzi ambao baada ya kuona hali hiyo waliwaruhusu wafanye maandalizi yao uwanjani.
Meneja wa uwanja wa Kirumba, John Tegete, ameruka kimanga alipoulizw kuhusu matone hayo yanayosadikiwa kuwa ndumba-nangai, na kusema yeye alichofanya ni kukabidhi funguo kila timu baada ya kuhakikisha viko safi, na kwamba hayo mengine hayamhusu na wala hakuwa na habari nayo.
Hata hivyo gemu lilianza kama ada na Simba walifungua hesabu dakika ya tano ya kipindi cha pili kupitia kwa mshambualiaji wake Mussa Hassan Mgosi ambaye alitumbukiza kimiani goli la kwanza kwa timu yake na la 11 kwake binafsi baada ya kupokea majalo toka kwa Nicco Nyagawa.

Dakika nne baadaye Mgosi alichachafya ngome ya Toto Africa kwa chenga zaa mwili kabla ya kumtangulizia kiungo mshambuliaji Ramadhani Chambo ambaye alikata nyasi kwa shuti kimo cha kuku iliyoenda nyavuni moja kwa moja, baada ya kumpita kipa Mohamed Azizi.

Ushindi huo umeipa Simba pointi 42 dhidi ya 30 za watani wao wa jadi Yanga inayokamata nafasi ya pili. Toto Africa wamezidi kwenda chini kuelekea mstari wa hatari wakiwa na pointi 7 kutoka michezo 14.

Huko Morogoro Mtibwa Sukari wana tam-tam wameendelea kuogelea katika nafasi ya nne kwa kuifunga JKT Ruvu iliyo nnafasi ya tano kwa bao bao 1-0, na kujikita na pointi 25.



Jerry Muro akiingia sentro leo
Akiwa amezingirwa na makachero wa polisi, mwandishi wa TBC Jerry Muro akiwasiliana na ndugu na jamaa baada ya kufikishwa kituo cha kati jijini Dar leo akituhumiwa kupokewa rushwa toka kwa mhasibu mkuu wa zamani wa wilaya ya Bagamoyo, Bw. Michael Wage

Jerry Muro akihojiwa na waandishi wenzie kituo kikuu cha polisi jijini Dar leo ambako anashikiliwa kwa tuhuma za kupokea rushwa ya shilingi milioni 10. Jerry Muro akijiandaa kukabidhi vitu vyake
kwa makachero wa polisi baada ya kufikishwa sentro leo
JERRY MURO MATATANI

Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia Mtangazaji wa Shirika la Habari Tanzania (TBC) Jerry Muro (pichani juu kulia) kwa tuhuma za kudai fedha kwa njia ya vitisho.

Muro anadaiwa kumtisha aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Bagamoyo Michael Wage ambaye hivi karibuni alisimamishwa kazi na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa tuhuma za ubadhilifu pamoja na viongozi wengine wa Halmahauri ya Wilaya Bagamoyo.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo Suleimani Kova alikiri jeshi lake kumshikilia Muro na kuwa alimtishia Wage kuwa yeye ni Ofisa wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kumtaka atoe fedha Sh milioni 10.

“Polisi inamhoji Muro dhidi ya tuhuma hizo na mahojiano yakikamilika taratibu za kisheria zitachukuliwa dhidi yake na maelezo zaidi nitayatoa kesho wakati wa mazungumzo yangu na waandishi wa habari” Kova alisema.

Bingwa huyo wa Tuzo za Uandishi wa Habari 2009 Tanzania alionekana akiwa sentro na mkononi ameshikilia bahasha tatu pamoja na kamera ya Video.

Alipohojiwa na wenzie juu ya kuhusika na tuhuma hizo alikana na kudai kushangazwa kuwekwa chini ya ulinzi kwa madai kuwa alipigiwa simu na mtu kupewa taarifa kuwa kuna kazi katika Hoteli ya City Garden.

“Kaka nilitaarifiwa tu kama ujuavyo kazi zetu kuwa kuna kazi City Garden niakaamua kwenda. Lakini baada ya kufika tu nilishangaa nawekwa chini ya ulinzi na askari kanzu ambao ndiyo walionifikisha kituoni hapa bila ya kunitajia kosa lanmgu. ” alilonga Muro.

Kwa upande wake Wage alidai kuwa mtuhumiwa anatumiwa na watu wengine ambapo juzi alimpandisha katika gari lake na kumfunga pingu kisha kumtaka atoe Sh milioni 10 na kwa kuthibitisha kuwa alikuwa ndani ya gari hilo alidai kuacha miwani yake yenye mikanda myeusi.

Polisi ilipomhoji Muro kama anazo pingu alikiri kumiliki pingu pamoja na bastola ambapo baada upekuzi katika gari lake lenye namba za usajili T 545 BEH polisi walikuta pingu hizo pamoja miwani iliyosemwa na mlalamikaji.

Muro alishinda tuzo ya Mwandishi bora wa mwaka kupitia vipindi vyake vya Televisheni vya "Usiku wa Habari" vinavyorushwa katika kituo cha TBC1 kila siku na kabla ya kuhamia hapo alikuwa kituo cha ITV na aliendesha kipindi cha "Ripoti Maalum".

Miongoni mwa mambo aliyokuwa akirusha katika vipindi hivyo ni pamoja na rushwa, matumizi mabaya ya madaraka pamoja na ukiukwaji wa sheria.

Polisi wamekuwa ni waathirika wakuu katika vipindi hivyo kwani mara mbili amewatoa Polisi Usalama barabarani wakiomba na kupokea rushwa hadharani kutoka kwa madereva wa malori na mabasi ya mikoani.
kikosi cha misri kilichotwaa ubingwa wa afrika mara
ya tatu mfululizo kwa kuifunga ghana
bao 1-0 kwenye fainali huko angola jioni hii
jiji la cairo likizizima kwa nderemo usiku huu
kufuatia ushindi wao dhidi ya ghana
wamisri wakishangilia ushindi
hata ngamia anatabasamu..

SIRI YA MAFANIKIO YA
SOKA YA TIMU YA TAIFA YA MISRI
Kwanza twamshukuru Mungu na pili pongezi nyingi sana kaka Michuzi kwa kutupa nafasi wadau wako wa Globu hii ya Jamii kusema japo bado hatujakabidhiwa rasmini peni na makaratasi katika Maofisi Makubwa katika kuhakikisha mambo yanaenda sawa Nchini Kwetu Tanzania.

Hii tunaileta kwenu wadau Wenzetu kama Hoja ambayo tunaomba ichangiwe na kwa wale ambao wana nafasi Fulani ya kuweza wafika wahusika wa kutekeleza haya tutakayosema wachukue nafasi ya kuwaeleza ili tuzidi kuliendeleza libeneke letu la Tanzania Daima kila kitu kinawezekana.hasa katika swala la soka.

Tukiiangalia siri ya Mafaanikio ya Timu ya Misri Kuna sababu kuu nne naomba nizilete kwenu ili tupate zifahamu na kujifunza na kupitia hizo.
1. Vilabu
2. Uzalendo
3. Kuthaminiwa Wachezaji
4. Kuwa na Viongozi imara na Wajuzi
katika Soka na sikupeana kwa kujuana tu.

Maelezo kwa urefu :
1.Hapa Misri kuna vilabu vingi na imara ambavyo mtakubaliana na sisi kwamba bila ya shaka Ndio Msingi Mkubwa wa kuweza kupatikana Timu bora ya Taifa.

Binaadamu huwa hawatimii lakini kuna mabadiliko makubwa sana hapa. Zamani ilikuwa Wachezaji wa El-Ahly ndio wengi wao wanaunda timu ya taifa lakini sasa hakuna na wao wamejifunza kutoka kwa Mataifa mengine Mchezaji kama Mohammad Nagy Gedo ni wa Timu za kawaida inaitwa Ithad-Sekandari.
Kuwa na vilabu vingi si tija ila katika Vilabu hivyo kunazalika vipaji ambavyo haviandikiki. Hapa Tanzania tuna Ndugu zetu wengi wana vipaji lakini waleaji hakuna Viwanja hakuna na hata kama vipo hata Mipira hakuna inawezekana mpaka kesho Wadogo zetu wanachezea Mipira ya Vitambaa maarufu Cha ndimu.

Hapa Misri Mtoto Mdogo anazoweshwa kupiga gozi sio mpira wa makaratasi baadae akichezea gozi miguu inauma kwa hiyo Mazingira mazuri na ya kisasa.
Ni Moja ya sababu kuu ya kukua soka hapa Nchini Misri.

2.Uzalendo
Wachezaji wote wa timu ya Taifa wanaipenda Nchi yao ndio maana unapowaona uwanjani wanacheza mpira wa kujitoa Muhanga kwa sababu ya kuleta furaha katika Timu yao na Taifa lao kwa Ujumla.

Nasaha
Wachezaji wetu wajifunze Uzalendo na sio Lawama tu Maximo kila Siku kuwa anabadilisha timu bila ya kuangalia sababu. Huenda Nidhamu hakuna na hii inakuja kutokana na kujengeka kwa jeuri Fulani kwa Mchezaji kuwa mimi ni mimi bila ya kulinda maslahi ya kuliletea Heshima Taifa na furaha kwa Watanzania kiuzalendo wa kikweli kweli.
Nidhamu muhimu sana Kaka zangu.

3.Kuthaminiwa Wachezaji
Kama mwanzo tulivyoeleza suala la vilabu kuwa vingi basi tunaomba tuwaeleze kuwa si wingi tu wa vilabu bali vilabu vinawajali sana wachezaji wao. Wenzetu hapa Misri hakuna mgogoro wa Mishahara na wala hutokuta mchezaji anagoma kisa posho kuthaminiwa kwao inafikia kiwango kwamba hupati nafasi kabisa ya kupigana vikumbo na Wachezaji katika Mabasi au hata migahawa ya kahawa.

Wachezaji wao wanajituma sana na watoa nguvu zao zote kwa sababu wanajua kwamba mwisho wao hauna longolongo kwa vilabu. Hakikisha hilo Mdau Kocha wa Timu ya Taifa Maalim Hassan Shehata alikuwa ni Miongoni mwa wachezaji wa timu ya Zamaleik na wengi tu wapo.

Tuwathamini wachezaji wetu ili wajue kwamba hawapotezi muda wao katika hayo wanayoyafanya katika kuliletea Heshima soka la Bongo na Taifa Kwa ujumla. Ni aibu kubwa sana kumkuta Mchezaji mkubwa kama Ngasa,Tegete na Huyo Kocha Maximo eti wanapata nafasi ya kwenda kuuza sura zao katika soko la filamu za Bongo lakini hatuwezi sema sana soko la filamu linalipa sana kuliko Soka.Tuelewane hapo sio matangazo ya dakika mbili tatu.

Inatia uchungu na Masikitiko wachezaji ambao wametoa Mchango mkubwa katika soka la bongo kama kaka Lunyamila,Mwameja n.k kutothaminiwa tena.
Hata thamani ya Muda wao ambao waliutoa katika mchango wa soka la bongo hatuuoni na hatuwajali kabisa leo hata kuwaongopea kuja kuwapa Ndugu zao nasaha,Moyo katika kambi za kimichezo(vilabu)sijui kama inafanywa.
Fani haizeeki,tunawaona si lolote si chochote Ng'oo soka haitaendelea kwa kutowathimini wakongwe hao.

5. Viongozi Imara
Kuwa na Viongozi imara na Wajuzi katika Soka na sio kupeana kwa kujuana tu. Kaka hapa Naomba pazingatiwe sana katika swala kupeana uongozi kiholela Bongo tunaongoza Mtu hata maana ya huo Mpira ajui anapewa Uongozi hapo hatutofika kabisa.

Jamaa huku Wote ambao wanakuwa katika benchi la ufundi ni wajuzi wa soka hakuna kuingiliana katika Sekta ifike kipindi Jamani tubadilike kama Mtu ni Dr. Atulie katika fani yake,mwanamuziki Tulia kwako ila kama unakuja huku katika soka kutoa Mchango wa Mawazo na uwezeshaji wa mambo Fulani karibu sana na sio kukimbilia Madaraka.

Wataanzania pia na tuinuke tuache Usimba na Uyanga tuweke uzalendo mbele! Tuwaandae vijana vyema katika kutangaza soka letu la Bongo na Nchi yetu kwa Ujumla na Serikali vilevile iwekeze katika soka sio Utalii tu soka muhimu sana katika kutangaza taifa sisi tuliokuwa Nchi za nje tunapoona nchi yetu inasafiri kwenda nchingine kucheza soka Tunajisikia raha sana tumechoka kusikia Naigeria,Ghana,Misri Kila siku.

Wadau tusaidiane katika Kupigia debe soka la Tanzania likue zaidi na zaidi.
Tunashukuru sana kwa nafasi hii yapo mengi sana ya Kuandika lakini Naomba Tuiishie hapa.

kwa Maelezo zaidi ya Kiufundi katika soka wasiliana na
wadau wa soka Nchini Misri
Hussein M Afif katika E-mail
husenoo85@yahoo.com
au
Ghalib N Monero. katika E-mail
gmonero@yahoo.com
Imeandikwa kwa mashirikiano ya watu Wawili.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Africa
Hongera Sana Misri kwa Kuchukua
Kombe mara Tatu Mfululizo
Milioniiiiiiiii Mabrouk.

Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Roma

Rome: Jana tarehe 30 Januari, Mjini Rome, Italy, kulikuwa na mkutano mkuu wa Jumuiya ya Watanzania Roma. Mkutano huu ulikuwa na agenda mbili, kwanza ni Kupitisha Katiba ya Jumuiya ya Watanzania Roma, pili kuchagua Viongozi.
Mgeni rasmi kati mkutano huo alikuwa Mh. Salvator Mbilinyi, ofisa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italy ambaye alimuwakilisha Mh. Abeid Aman Karume, balozi wa Tanzania nchini Italia.
Waliochaguliwa kuwa Viongozi ni ndugu Leonce Uwandameno kama mwenyekiti wa Jumuiya, ndugu Erasmus Luhoyo Pindu, kama mwenyekiti Msaidizi, Diana Olotu kama Katibu msaidizi. Katibu na Mweka hazina wamebaki wale wale yaani Katibu Ndugu Andrew Chole Mhella na Mweka Hazina ndugu Awadhi.
Kwa picha na habari zaidi tutembeleeni hapa
MTANGAZAJI WA TBC JERRY MURO (PICHANI) ANASHIKILIWA NA POLISI KATIKA KITUO CHA KATI JIJINI DAR KWA KILE KINACHODAIWA KUNASWA KATIKA MTEGO WA KUPOKEA RUSHWA TOKA KWA MWANANCHI MMOJA WA JIJINI.
MEDANI ZA KIPOLISI ZIMETHIBITISHA KWAMBA JERRY MURO, AMBAYE NI MTUZWA WA MWANDISHI BORA WA TV KWA MWAKA 2009, AMEKAMATWA LEO JIJINI AKIPOKEA SHILINGI MILIONI 10 KABLA MTEGO ALIOWEKEWA HAUJAFYATUKA.
KAMANDA WA POLISI WA KANDA MAALUMU YA DAR AFANDE SELEMANI KOVA ANATARAJIWA KUTOA TAARIFA KAMILI WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA NA GLOBU YA JAMII ITAWALETEA PINDI HABARI MPYA ZITAPOINGIA.
Maafisa wa NMB wakitembezwa shule ya Msingi ya Nyanza kabla ya kutoa misaada ya ujenzi wa madarasa matatu katika shule hiyo.
wanafunzi wa shule hiyo wakijumuika kwenye hafla

Mkuu wa kitengo cha Mahusiano benki ya NMB Shy-Rose Bhanji, akikabidhi sehemu ya msaada wa saruji na mabati kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyanza Bibi Happiness Kimambo, ikiwa ni msaada wa NMB kusaidia sehem ya ujenzi wa madarasa matatu katika shule hiyo.
Mkuu wa kitengo cha Mahusiano benki ya NMB Shy-Rose Bhanji, akikabidhi sehemu ya msaada wa saruji na mabati kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyanza Bibi Happiness Kimambo, ikiwa ni msaada wa NMB kusaidia sehem ya ujenzi wa madarasa matatu katika shule hiyo.


Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano NMB Shy-Rose Bhanji akiongea na walimu na wanafunzi waliofika katika hafla hiyo.





Rais wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN); Mzalendo Sanctus Mtsimbe; akitoa maelezo ya misaada iliyokusanywa katika awamu ya pili ya Kampeni kwa ajili ya kuwasaidia Wahanga wa Mafuriko inayoendeshwa na TPN, Globu ya Jamii na JamiiForums.
Pichani ni misaada mbalimbali ambayo ilikusanywa na Wadau mbalimbali. Mz. Mtsimbe alisema hadi sasa zaidi ya watu 1880 wanachangia katika kampeni ya SMS. Vitu vilivyokabidhiwa ni pamoja na ndoo; magodoro; miswaki na dawa za miswaki; sabuni; vyandarua; mablanketi; maji ya kunywa; Nguo mbalimabli za kike, kiume,watoto, Mataulo, mashati, Suruali; Viatu na Madawa ya chooni vyote vikiwa na dhamani ya TZS Million 5.
Rais wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN); Mzalendo Sanctus Mtsimbe; akitoa maelezo ya misaada iliyokusanywa katika awamu ya pili ya Kampeni kwa ajili ya kuwasaidia Wahanga wa Mafuriko

Mlezi wa TPN Mzalendo Dr. Maua Dfatari (kati) akitoa maelezo kuhusiana na kampeni kwa; Mkurugenzi wa Maafa wa Chama Cha Msalaba Mwekundu Bw. Joseph Kimaryo (Kulia) katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Chama Chama Msalaba Mwekundu, Masaki jijini Dar.

Alisema TPN imefurahi kuwa imetoa changamoto na sasa wadau mbalimbali wanasaidia na kuendesha kampeni kuwasaidia wahanga ingawa ilikuwa ni jambo jema kuunganisha nguvu kwani wote lengo letu ni moja. Aliasa kuwa Muhimu kuliko vyote ni kuhakikisha kuwa misaada inafika kwa walengwa. Kampeni yetu inaendelea kwa kutuma SMS yenye neon TPN kwenda namba 15522.

Mlezi wa TPN Mzalendo Dr. Maua Dfatari (kati) akitoa maelezo kuhusiana na kampeni kwa; Mkurugenzi wa Maafa wa Chama Cha Msalaba Mwekundu Bw. Joseph Kimaryo (Kulia) katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Chama Chama Msalaba Mwekundu. Mzalendo Daftari aliweka wazi kuwa Kampeni yetu ni ya Kukisaidia na Kukiwezesha Chama cha Msalaba Mwekundu Red Cross na haina uhusiano wowote na kampeni ya Red Alert inayoendeshwa na Vodacom.

Alisema TPN imefurahi kuwa imetoa changamoto na sasa wadau mbalimbali wanasaidia na kuendesha kampeni kuwasaidia wahanga ingawa ilikuwa ni jambo jema kuunganisha nguvu kwani wote lengo letu ni moja. Aliasa kuwa Muhimu kuliko vyote ni kuhakikisha kuwa misaada inafika kwa walengwa. Kampeni yetu inaendelea kwa kutuma SMS yenye neon TPN kwenda namba 15522.






Ankal mcheki mama Clinton hapo, yaani hata yeye anavaa kiatu kikubwa kuliko mguu wake, ama kweli duniani kuna majamboz. Uzee nao....
Rais wa Ufaransa mze mzima Sakozy alisevu ngoma..
kisha wakala bonge la pozi
baadae jioni mama alienda bichi kuvua samaki




no image
Mkuu wa Wilaya ya nanihiii, aksante kwa kuendeleza libeneke kwenye globu yako hii ya jamii. Twafurahi sana kwa updates zako za kila dakika, kazi yako inaonekana kaka. Mie nna jambo linanitatiza sana kwenye hii nchi yetu yenye maendeleo ya kasi; naomba niwakilishe kwako kaka.

Unajua siku hizi familia kibao zina usafiri binafsi. Ila nadhani wengine ni limbukeni hasa ukitegemea anataka mwanae apate starehe ambazo yeye hakuzipata wakati anakua. Matokeo yake ni maafa kwa hawa viumbe wasio na hatia. Utaona mzazi akiwa na mwanae kwenye gari halafu hajali kama mtoto amekaa kwa usalama wakati yeye amepiga belt.

Mara nyingi huwa naona watoto wakicheza cheza na kuruka ruka kwenye gari wakati watu wote wazima wakiwa wamefunga mikanda na kuhakikisha usalama wao. Sioni busara iko wapi hapa. Tena utakuta gari inaendeshwa kwa kasi ya ajabu na brake zisizo na mpangilio, sasa yakitokea tusiyoyaombea huyu mtoto anakuwa na hali gani? Nani wa kulaumiwa?

Kwa umakini sana nimefuatilia hawa watu hawazuiwi na traffic na kupigwa faini. Sijui hapa kwetu huku hili ni swala la kawaida? Nadhani umefika wakati tuanze kuliangalia hili jambo upya, maana hivi vigari vyetu visiwe chanzo cha kuwapa wengine majanga, maana mtoto akiwa loose kwenye gari anaweza akaanza kufanya fujo na kumfanya mzazi kusababisha ajali, kitu ambazo kitakuwa ni uzembe wa hali ya juu.
Mie nilikuwa naomba Traffic badala ya kuona ni jambo la kawaida wawapige bao hawa watu tena bila huruma, maana leo asubuhi nimekutana na familia zaidi ya tano zikiwa zinafanya mchezo huo huo. Jamani huu ni ulimbukeni, fikiria kwanza usalama wa watoto kabla ya kufanya mambo haya, au michuzi hawa wameletewa leseni nyumbani nini? Maana sidhani kama kuna shule ambayo haina mkazo kwenye usalama wa abiria na wapita njia.

Hivi Michuzi, Imagine baba au mama amefunga brake ya ghafla, mtoto atakuwa na hali gani? Mie niliyoyaona yanatosha ila naomba wafikishie wadau wapate kuelewa kuwa kama mtu mzima anafunga mkanda kwenye gari iweje mtoto aachwe arukeruke na kutembea kama vile gari imekuwa uwanja wa soka na vilevile gari iko kasi?

Mie noana si ustaarabu. Mkuu wa Wilaya, Mifano iko mingi sana kwa wenzetu wa dunia ya kwanza, traffic akiona mtu anaendesha gari na mtoto hajafungwa mkanda vizuri hilo ni kosa kubwa sana, na adhabu ni kali lakini kwetu wanaangalia na kucheka tu. Mie naomba niwakilishie hili maana inaudhi kwa watu wazima kukosa kufikiria jambo la hatari kama hili especially kwenye mji wenye ajali kila dakika kama daslama.

Nawakilisha

Mdau wa River Between
Mbezi kwa Komba
President Jakaya Mrisho Kikwete speaks during a debate on improving agriculture production to boost food Security during the World Economic forum in last night in Davos . Left is Ms. Ellen Kullman Chair and CEO of of the US based DuPont company and right is Microsoft Founder and Chairman Bill Gates.

President Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with the the Microsoft founder and Chaiman of the Bill and Melinda Gates Foundation, Bill Gates shortly after participating in a debate on improving Food Security held in at Davos Congress Hall on the last day of the session. Microsoft supports the ICT college of the Dodoma University among other projects
President Jakaya Mrisho Kikwete(right) in conmversation with Vietnam Prime Minister Nguyen Tan Dung(centre) and the chariman of the New Delhi Television Roy Prannoy(left) who was also the moderator during the debate on Global Food Security held at Davos Congress Hall.
President Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with World Trade Organisation WTO Director General Pascal Lammy at the Davos Congress hall in Davos last night during the last session of the World Economic Forum held in Davos Switzerland. Photo by Freddy Maro.

Na Mwandishi Maalum, Davos, Uswisi

ILO YAISIFU TANZANIA
KWA UONGOZI BORA NA IMARA
Shirika la Kazi Duniani (ILO) limesema kuwa Tanzania ni mfano mzuri wa nchi yenye uongozi bora na imara, hali iliyoiwezesha nchi hiyo kutoyumbishwa kupita kiasi na msukosuko wa karibuni wa uchumi duniani.

Aidha, Shirika hilo limeipongeza Serikali ya Tanzania kwa kufanikiwa kutengenezaji ajira zaidi ya milioni katika miaka minne ya uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kama ilivyoahidiwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

Mkurugenzi Mkuu wa ILO, Bwana Juan Somavia amesema kuwa ukweli kwamba Tanzania haikuyumba kupita kiasi kutokana na msukosuko wa uchumi dunia ni ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa nchi inasonga mbele kwenye mikono salama.

Bwana Somavia ametoa sifa hizo kwa Tanzania wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo, Jumamosi, Januari 30, 2010, kwenye Hoteli ya Arabella Sheraton Woodhuus, Davos, Uswisi, ambako Rais Kikwete amefikia.

Rais Kikwete pamoja na Bwana Somavia, walikuwa mjini Davos kuhudhuria Mkutano wa 40 wa Taasisi ya Uchumi Duniani ya World Economic Forum (WEF), ambao unamalizika kesho, Jumapili, Januari 31, 2010. Mkutano huo umehudhuriwa na mamia kwa mamia ya wajumbe kutoka sehemu mbali mbali duniani wakiwamo viongozi kutoka zaidi ya nchi 30.

Bwana Somavia amemwambia Rais Kikwete kwenye mazungumzo hayo: “Yako, Mheshimiwa Rais, ni nchi inayosonga mbele, ikiwa haina jambo la kuiyumbisha. Ni nchi iliko kwenye mikono iliyotulia, yenye uongozi bora na imara, ukweli ambao ulijidhihirisha wakati wa msukosuko wa uchumi duniani.”
Viongozi hao wawili wamejadili msukosuko wa uchumi duniani na athari za msukosuko huo kwa nchi mbali mbali na hasa zile zinazoendelea. Msukosuko huo ulilipuka kati ya Oktoba na Novemba, mwaka juzi, 2008, na athari zake zinaendelea kuisumbua dunia hadi leo.
Viongozi hao wamekubaliana kuwa mfumo wa uchumi wa soko, pamoja na manufaa yake makubwa duniani, bado unahitaji aina nzuri ya kuudhibiti mfumo huo, ili kuzuia dunia isiweze kuingia katika matatizo makubwa zaidi ya uchumi.

Kuhusu ajira katika Tanzania, Bwana Somavia ameipongeza Serikali ya Rais Kikwete kwa kuweza kutengeneza ajira zaidi ya milioni moja, kama Chama cha Mapinduzi (CCM) kilivyoahidi katika Ilani ya Uchaguzi wa 2005.

Hata hivyo, Rais Kikwete amemwambia Bwana Somavia kuwa ni bahati mbaya kuwa msukosuko wa uchumi duniani umeifanya Tanzania kupoteza nafasi 47,000 za ajira, lakini akaongeza kuwa ni dhahiri kuwa zipo ajira zaidi zilizojitokeza hasa katika sekta isiyokuwa rasmi katika kipindi hicho cha msukosuko duniani.

Mbali na kukutana na Bwana Somavia, Rais Kikwete pia amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa WEF, Profesa Schwab.

Katika mkutano huo uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Davos cha Congress Centre ambako shughuli za WEF zinaendelea, viongozi hao wamejadili, miongoni mwa mambo mengine, maandalizi ya Mkutano wa WEF-Africa ulipangwa kufanyika mjini Dar Es Salaam mwanzoni mwa Mei, mwaka huu, 2010.

Hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa mkutano huo wa WEF-Africa kufanyika nje ya Jiji la Cape Town la Afrika Kusini ambako miaka yote mkutano huo umefanyika.

Rais Kikwete pia amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani la World Trade Organisation (WTO) kwenye Congress Centre.

Wakati huo huo, Rais Kikwete anatarajiwa kuondoka mjini Davos asubuhi mapema ya leo, Jumapili, Januari 31, 2010, kwenda Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Mwaka huu wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) ulioanza leo, Jumamosi, Januari 30, 2010 mjini humo.

wataalamu wakipima maeneo ya kiwalani katika
mchakato wa upanuzi wa uwanja wa ndege dar
wapimaji wakiendelea na kazi maeneo ya kiwalani
ambapo nyumba zote hizo zitapigwa nyundo
shoto ni ukuta wa uwanja wa ndege wa dar na
kuume ni nyumba ambazo zote zitapigwa nyundo
nyundo inaendelea maeneo haya kupisha upanuzi wa uwanja huo

gwiji la muziki zahir ally zorro akimtambulisha zahir jnr ambaye naye ni moto wa kuotea mbali kama walivyo wakubwa zake banana na maunda. zahir baba kaiambia globu ya jamii kwamba wadau wakae mkao wa kula kwani dogo hivi sasa anapikwa hadi apikike kabla ya kuibuka kivyake

Kaimu Mhariri Mtendaji wa Tanzania Standard Media Newspapers Ltd, Bw. Mkumbwa Ally, akiongea na wafanyakazi wa kampuni hiyo ambayo huchapisha magazeti ya serikali ya Daily News na HabariLeo wakati wa mnuso wa kusherehekea mwaka mpya ulioandaliwa Ijumaa usiku katika hoteli ya New Africa jijini Dar
wadau wa TSN wakisikiliza hotuba kwa makini
Mtu mzima Deo Mushi (kulia) akichati na Mdau Furaha ambaye ni mwakilishi wa biashara wa TSN kanda ya A-TAun
wadau wa TSN wakijichana
Shafii Mpenda (kati) na makamanda wenzie
wawakilishi wa TSN toka kanda zote nchini wakitambulishwa
gwiji la habari aa mahakamani Faustine Kapama (pili kulia) akiwa na mhariri wa michezo Nas Kiliyinga (pili shoto) na wapiganaji wenzao
wataalamu wa teknohama wa TSN wakila raha
masembe tambwe anajinyoosha baada ya msosi wa nguvu na wenzie
Maafisa waandamizi wakiwa mezani pao.
mhariri wa habari wa HabariLeo Mgaya Kingoba na wapiganaji wake
wadau wa TSN wakiendelea kujichana
kila mtu alikuja kapendeza
wataalamu wa usanifu kurasa na wenzao
wazee wa kazi wa uwakala wa matangazo wakijipendelea
"...ah, mi n'shachoka kula anasema bibie nanihii wakati
zena chande akikata mbuga kama hana akili nzuri
ze fulanazzz huwa haichezi mbali kwenye mnuso kama huu..
masaladi time...
libeneke mpaka lyamba...
Deo Mwanambilimbi (shoto) akiongoza The Great Kalunde band kutumbuiza