TAARIFA YA HABARI YA TBC1 LEO
Viongozi wa CHADEMA kwenye
maandamano leo huko Arusha


HABARI ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE,INARIPOTI KWAMBA NAE KATIBU MKUU WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDEOE (CHADEMA),DR. WILBROAD SLAA PAMOJA NA MBUNGE WA JIMBO LA MOSHI MJINI, MH. PHILEMON NDESAMBURO WAMEKAMATWA NA POLISI MKOANI ARUSHA USIKU HUU KWA MADAI KUWA NA WAO WAMECHOCHEA VURUGU ZILIZOTOKEA LEO MKOANI HUMO.

VIONGOZI HAO WAMEUNGANA NA VIONGOZI WENGINE WALIOKAMATWA MAPEMA LEO KUTOKANA VURUGU ZILIZOTOKEA WAKATI WA MAANDAMANO YALIYOKUWA YAKIFANYIKA MKOANI ARUSHA LEO.

VIONGOZI WA CHAMA HICHO WALIOTIWA MBARONI HADI HIZI SASA NI MWENYEKITI WA CHAMA HICHO,MH. FREEMAN MBOWE,KATIBU MKUU WA CHAMA HICHO,DR. WILLBROAD SLAA,MBUNGE WA JIMBO LA ARUSHA,MH. GODBLESS LEMA PAMOJA NA MBUNGE WA JIMBO LA MOSHI MJINI,MH. PHILEMON NDESAMBURO.

HABARI KAMILI NENDA HABARI LEO
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. Vurugu wapi watu wanadai haki yao nyie mnatumia dola kuwazuia!!

    ReplyDelete
  2. Chadema mie ni shabiki wenu mkubwa, lakini kuna mambo mnayoyafanya hayana maana. mnawapeleka wananchi kibao haswa wa hali ya chini kwenye matatizo badala ya kuwasaidia. Wameumizwa leo nyie mtaenda kujitibu wao watabaki kuhangaikia hela za matibabu. CCM wajanja wanatumia udhaifu wenu kufanya mabadiliko majimboni mwao( mfano Mh Makalla, kapeleka maji jimboni kwake, mawaziri wanafanya kazi kwa kishindo) N.K. sasa nyie sijaona hata badiliko mlilofanya toka mpate hizo nafasi zenu zaidi ya kubwabwaja na kutafuta mvunjiko wa amani kinguvu. SASA HICHO NDICHO TULICHO WACHAGULIA????? Fanyeni kazi acheni kubabaisha na kuchukua mishahara bure. bunge lipo pelekeni hoja. sio kila siku kampeni. TUMEWACHOKA SASA. NA KURA BORA TUWAPIGIE HAO HAO CCM. TATIZO LENU NYIE MNATAKA KUKIMBIA WAKATI HATA KUKAA HAMJAANZA. wenzetu wako mbali. Fanyeni mabaliko ya ukweli kwa wananchi waliowachagua na mtafika mnapotaka.ME NAWAONEA HURUMA WANANCHI MAANA KUMBUKENI ARUSHA NI MJI WA KITALII NA KUNA WANANCHI WANATEGEMEA KULA KUPITIA UTALII, LEO MNAENDA KUSABABISHA VURUGU AMBAZO MLISHAKATAZWA.
    MDAU MAREKANI

    ReplyDelete
  3. Do we have any government at all in Tanzania?! Kama watu wanaandamana bila kufanya vurugu ni kwanini wanawekwa jela?? Kama watu wanaandamana na vitambaa vyeupe ina maana ni maandamano ya amani, sasa kwanini wapigwe virungu? I would like to hear from CCM leaders, if they are truly our leaders.

    ReplyDelete
  4. wakati cuf tulipokuwa wapinzani wa juu tuliitwa wadini kwa kuandamana, sasa leo hii chadema vipi nyie tuwaite chama cha ukiristo na ukilimanjaro? maana viongozi wenu wote wakilimanjaro na wakiristo. jamani tanzania siasa bado ni ya kibaguzi bora hiyo ccm ina mchanganyiko.
    mungu ibariki tz. michuzi a.k.a ankali usiibanie hii
    maisha utani , holland

    ReplyDelete
  5. Wewe Mdau wa Marekani acha pumba bana!!!!! Hata mimi nipo Marekani, na wala sina mawazo finyu kama yako. Wananchi wenye uchungu na nchi yetu, ambao wengi pia ni wanyonge wamewachagua CHADEMA kwa ajili ya kuwaletea maendeleo. Ila lazima utambue kuwa maendeleo hayo hayatokuja kama mabadiliko kadhaa hayatofanyika, ikiwemo mabadiliko ya Katiba, ambayo ni sheria mama. Sasa huo ndio msingi wa madai ya CHADEMA, na mimi sio walichokosea, kinachotakiwa ni CCM kuwasikiliza, kwani wana wakilisha kilio cha wananchi wengi. TUMECHOKA KUONA NCHI YETU INAENDESHWA KIIMLA KILA KUKICHA....HAKI IKO WAPI????

    ReplyDelete
  6. Sawa mawazo yako yanaona naongea pumba, lakini katiba wanayotaka si Mh raisi kashakubali?, sasa wewe unaongelea katiba gani? sasa uchungu na nchi ndio kuwapeleka watu na watoto kwenda kuandamana na kuvamia kituo cha polisi. fatilia habari vizuri kabla haujatoa hoja zako. na hatupo mashindanoni,kila mtu anauchungu na nchi lakini sio kwa staili ya kuandamana, tunaongea fact, wananchi wamewachagua wao kuwawakilishia bungeni malalamiko yao,chukua mfano wa kugomea hutuba ya rais si ndio chanzo cha mpaka kupelekea rais kufikiria kukubali kubadilisha katiba. kwahiyo chadema kwa miaka yote mitano shughuli itakuwa kudai katiba? na shughuli za maendeleo majimboni mwao afanye nani? hiyo ndio hoja yangu ya msingi. lakini wewe unadandia tu hoja bila yakuwa na uhakika wa unachoongea na kutukana watu.

    ReplyDelete
  7. Mdau soma habari vizuri, kabla haujatukana watu wanaakili finyu. samahani bwana michuzi naomba mueleweshe mdau maandamano ya leo ya chadema yalikuwa yanahusu nini. maana kashikilia katiba, wakati hiyo iko njiani kubadilishwa na watu tumeshasau. sasa sijui mwenye mawazo finyu ni nani?

    ReplyDelete
  8. HUYO MDAU WA MAREKANI WAPI .ANAKAA HUKO TANDIKA.TOA MATOPE YAKO KWENYE MACHO YAKO SAWA.AU KALALE HUKO.MIMI NI MDAU TOKA MAREKANI.NATAKA NIPIGIE SIMU NIKUTOE NISHAI BASI.
    MDAU WA KWELI
    TOKA MAREKANI

    ReplyDelete
  9. Poa mdau wa marekani wa ukweli nashukuru. basi naomba post namba yako nikupigie au weka email address yako.then tupate kuwasiliana na kurekebishana.

    ReplyDelete
  10. siwaelewi kwani maandamano ni nin na je kuandamana ni kosa??sijui we unasema mshabiki mkubwa wa chadema sidhani maana ungeelewa wanachoandamana hungesema hayo usifikiri wale woote akili hawana na hao unaosema wa hali ya chini nani kakwambia hawajui wanachofanya,tukubali tu ccm na dola yake wanafanya makosa makubwa kutumia nguvu na kuzuia maandamano swali hivi wangewaacha wakalinda tu polisi yangetokea yalo tokea.sipendi kuongelea na kujali maslahi ya chama bali unaangalia kweli jeshi la polisi na serikali yake wakatumia busara nchi hii watu wake ni wastaarabu kupita mfano atakaye haribu hii nchi na watawala wenyewe na dola zake

    ReplyDelete
  11. We unayejiita mdau marekani, Jaribu kuwa na ushirikiano mzuri na akili zako unapotoa comments humu. Unasema suala la katiba mmeshasahau, na nani ?? labda wewe na mkeo au mmeo..maana sijui jinsia yako! Utasemaje tumeshau wakat katiba mpya haijapatikana. PANUA ufahamu wako ,elewa alichosema Rais ni kupoza spidi ya madai ya katiba tu. anadai kuunda tume,tume ngapi zmeshaunda na mapendekezo kutupwa kapuni?? Kwa watu walio seriose na hili huunda Kamati ya kubadiri katiba na siyo tume.kama kenya walivyofanya. Sisi hatutaki hiyo tume ya kisanii tunataka kamati huru ya kubadiri katiba, na hizi ni rasharasha tu hatuchoki wal kusahau kama akili zako mpaka kieleweke.

    Pia, elewa kwamba CHADEMA walitoa taarifa ya maandamai mwezi mmoja kabla, Kwa nini serikali iasiandae ulizi wa kuwalinda wakiandama ?? badala yake wanazuia masaa 12 kabla ya mmandamano?? kwanini Jeshi litumie siraha za moto kwa raia wasio na hatia wala silaha yoyote mkononi?? kwanini wapige mabomu watu wanaotimiza haki yao kikatiba??

    Chanzo cha matatizo yoote ni uchu wa madaraka wa wanasiiem wenyewe na si CHADEMA. Wamechakachua kweny urais na maadhi ya majimbo ya Ubung na udiwani mwaka jana, hawajaridhika!! Sasa wamheami kwenye umeya..wamefanya uhuni uhuni tu kumweka meya wa Arusha. Then unatak wati wasiandamane , Y? kama wanaitakia nnchi hii amani waache kuiba haki za watu kwa nguvu, waache viongz halali wawe viongozi. narudi tena AMANII YA NCHI HII INAONDOLEWA NA SERIKALI WENYEWE. Sisi wafuasi wa CHADEMA, Kamwe hatutachoka kudai haki zetu hata ikigharimu damu yetu kumwagika kwa manufaa ya vizazi vyetu na Taifa kwa ujumla.
    Mungu ibariki CHADEMA, Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  12. Hivi mpo serious kabisa unaposema tatizo ni CHADEMA? Yaani wawe na madiwani 16 dhidi ya 14 wa CCM na bado CCM iwe na mayor wa jiji? Kweli kama una akili timamu unaona ni haki? Makalla ni mhazini wa CCM na wao wanayo access ya pesa zote za HAZINA kwanini asiweke maji jimboni kwake? CHADEMA hawana iyo luxuary na namna pekee ya wao kudhibiti mapato ni kwa kupata mameya ili wadhibiti pesa za budget za majiji na halmashauri walipo na wewe unasema vurugu? Mwenye vurugu ni nani alieuwa watu kumi au anaeandamana kupata haki? Said Mwema alitoa kibali cha mkutano wa CHADEMA lakini alikataa maandamano hivi kuna uwezekano wa watu kwenda mkutanoni mmoja mmoja? Kama unaishi Dar na kama ni mpenzi wa mpira ningewauliza kama mmewahi kwenda kwenye mechi ya Yanga na simba. Hivi umewahi kuiona mlundikano wa watu tokea Temeke na pengineko hadi barabara kufungwa? Hayo tuyaite maandamano? Mimi sio CHADEMa na wala siamini siasa maana wanasiasa wote waongo ila katika hili CCM wanadamu za waliokufa. JK asubiri ICC tui atake asitake.

    ReplyDelete
  13. Wewe unayejiita mdau wa marekani hula lolote. kwanza hukai bongo ndio maana huna uchungu na wananchi wenzako. Wenzako huku tumepandishiwa bei ya umeme lakini hatuna umeme. Deni la Dowans linalipwa kupitia kipato kodogo cha mtanzania masikini anayeishi chini ya dola moja kwa siku. Huo si unyanyasaji? wakati hao viongozi wakubwa wanakula na kusaza, kuna masikini ambao hawajui chai ni nini wala ubwabwa ni nini. Fikiria joto la Dar lilivyo kwa kipindi hiki halafu hakuna umeme. Bei ya bidhaa kibao imepanda kiasi kwamba mtanzania wa kipato cha chini hawezi kumudu.
    Halafu watu wakitaka kuonyesha hisia zao wanapigwa virungu na kuwekwa jela. Hao wananchi wa Arusha wamechoshwa na ufisadi unaofanywa na CCM hasa mkoani hapo. Hwbu fikiria mji wa kitalii kama ule lakini miundombinu ni mibovu utafikiri jangwa. Mji ni mchafu mpaka hao watalii wenyewe wanashangaa kwamba fedha zao wanazotoa kwa utalii kila wanapotembelea hawaoni zinafanya nini coz mji uko vilevile miaka nenda rudi.
    Halafu ujue kwamba kilichowafanya CHADEMA kuandamana ni kupinga uchaguzi wa meya wa jiji hilo. CCM wamepanga siku ya uchaguzi wa meya bila kuwashirikisha Chadema, wakamchagua meya ambaye wamemuandaa wao, tena si mkazi wa arusha. Wamepeleka malalamiko yao kunako husika lakini hakuta hatua yeyote iliyochukuliwa. Unafikiri wao wangefanyaje? CCM wanafanya mambo kama watakavyo wao. Acha ujinga wa kutetea jambo usilolijua. wewe unakaa huko marekani, yawezekana hujui arusha ikoje wala mchakato mzima wa siasa ukoje. Hii nchi imeoza kwa ufisadi. tena inanuka kuliko hata panya aliyeoza. Ni bora tungeendelea kutawaliwa na mkoloni kuliko hali ilivyo sasa.
    Michu usiibanie comment yangu japo ni ndefu.
    TML

    ReplyDelete
  14. NILIKUA NATAKA NITOE MAONI LAKINI NIMESHANGAZWA NA MABISHANO YA WADAU WA MAREKANI NIMEPENDA SANA MAONI YA MDAU WA KWANZA WA MAREKANI KUTOKANA NA MAONI NA MAWAZO YAKE. NA UYU WAPILI AMBAYE ANAJIFANYA YE KWELI YUKO MAREKANI HANA POINT NDIO MAANA ANATULETEA MBWEMBWE WEWE KAMA KWELI UKO MAREKANI TULITEGEMEA UWE NA EXPOSURE, NA UONGE FACTS NDIO MAANA MWENZIO KAKUJIBU KWA FACTS UKASHINDWA KUMJIBU UKAISHIA MBWEMBWE ZAKUA MAREKANI MBONA KUNA WADAU KUTOKA NCHI MBALIMBALI APO JUU AU KWAKUA KAANDIKA YUKO MAREKANI? WATANZANIA TUPENDANE KOKOTE TULIPO, MDAU MBEZI TANZANIA

    ReplyDelete
  15. Acha ujinga we mdau wa marekani watu wanataka haki naona haukuwa makini na hutuba za waheshimiwa, kwanini CCM ilivyokosa ubunge imekua kama wana hasira na hili jimbo kila watachokifanya CHADEMA wanona hakina maana???

    Unavyodai kubadilisha kwa katiba mpiya Muheshimiwa rais aligoma baada yasiku kadhaa ndio akasema anaandaa tume ya kuchakatua sio mtu mzuri kabisa huyu raisi wetu.
    Mbona kwenye umeme alisema watanzania tukubaliane na matukeo kwanini lakatiba hakusema hivyooooooooooo We mdau wa marekani acha hizooooooooooooooo. agalia na sikiliza vizuri lengo la CCM sio zuri kila kitu wao walikua wanataka Ubunge wao,udiwani wao, mkuu wa mkoa wao ili waichakachue vizuri ARUSHA. Mr. Lema , Ndesamburo,Slaha, mboye kaeni macho na hili jimbo mpigeni tafu lema wanamuonea kila atakchokifanya kwao ni kibaya mbona wenyewe wamekula nchi wamenyamaza kimya.

    ReplyDelete
  16. maisha mazuri yanakuja kwa njia ya watu fulani kujitoa kafala,leo hii upo marekani unakaa vizuri kwa amani kumbuka kuna marekani walijitoa kafala kwa amani na maisha mazuria hayo,Au wewe unapendezwa na lugha ya CCM ina wenyewe?na wenywe ndito akina Richmond?wakati mshahara wa Mtz kima cha chini akizidi ata 1moja unaleteawa bila ya umeme 60,000/=,ndiyo maisha?wacha CHADEMA waikomboe Tanzania kutoka kwa watu wachache na kuwa ya watanzania wote.na tunaamini hivyo...Mdau kutoka Mwanza Tz.

    ReplyDelete
  17. WE MDAU WA KWANZA NA UMAREKANI WAKO KAMA UMEPELEKWA HUKO KWA NGUVU YA CHAMA KAA KIMYA UNATUBOA, KWANZA HII COMMENT NILIKUWA NANGOJA UMEME URUDI NIWASHE PC WEWE HATA KERO HIZI HUZIJUI KAA KIMYA NA AKINA 50 CENT WENU

    ReplyDelete
  18. Maandamano ni haki ya kikatiba, kama watu hawafanyi fujo pilisi wanachotakiwa kufanya ni kuwalinda tu! haya mambo ya polisi kuwapiga waandamanaji wasiofanya fujo yamezidi sasa hapa Tanzania.. nadhani hii ni serikali ya baadhi ya watu na baadhi ya vyama na si ya watanzania wote! Polisi wetu hawana kazi nyingine zaidi ya kupiga watu jamani?

    ReplyDelete
  19. watu kumi wamepoteza maisha, ndio mapinduzi yenyewe hayo, hawa ndio seth benjamin wetu walalahoi, kumbuka azimio la nyerere lilianzia A town sasa ni mapambazuko azimio la wenye inchi linaanza rasmi, jamani tuamke kabla sisiemu hawajatuletea rage kuwa rais!!!! msomali wa dom

    ReplyDelete
  20. Mdau Wa MAREKANI,Pole sana nakuomba ufikirie na umuombe Mungu akujalie hekima kabla ya kuandika lolote katika blog hii. Personally infact sio CHADEMA wala CCM.

    Lkn kitendo kilicho fanywa na JESHI LA POLISI ni cha KIZABINA ZABINA kwa CCM. Jeshi la Polisi liko kulinda RAIA na MALI ZAO leo hii limegeuka shabiki wa SIASA. Hii yote ni kwa sababu ya utawala mbovu.

    Mdau wa Marekani, nadhani uko marekani na unaona marekani inavyofanya,nadhani umefika uingireza ukaona wanavofanya. Inapofika maslahi ya Taifa vyama vyao wanaweka pembeni ili wajenge nchi yao. Lkn kwa mtazamo wa Tanzania hawako tayari ndo maana unaona wizi wa kula,kutumia nguvu matokeo yake hakuna AMANI tena.

    Kama tunakubali kuwa Chama chochote cha kisiasa kinaweza kuingia madarakani basi haya yote hatutayaona.
    Hivyo basi nakuomba mdau wa MAREKANI ufikirie na MUNGU akujalie hekima.

    Wako,
    Dr Nshomile mpaka for VI but not College,Kashozi.

    ReplyDelete
  21. CCM cahama cha ufisaji but theres is a peace there. no chadema

    ReplyDelete
  22. Mdau wa marekani na mimi nipo na wewe naponda sana hizo pumba zako ulizoongea humu ndani ya blog ya jamii yaani ungeweka mawasiliano yako humu watu wangekutafuta wakakufanya kitu mbaya live bila kuogopa,kwa kufupi wewe huwezi kuwa shabiki wa Chadema hata kidogo na wala hujua chochote kuhusu chadema kaa kimya funga domo lako endelea kubeba mabox.

    We bwege kweli unajifanya umewachagua chadema umewachagua ukiwa unabeba box hizo...pxck*....suala la kuandamana na tunalijua sisi waandamanaji na tutaendelea kuandamana mpaka tufe wote ndio maandamano yataisha hivi wewe unajua watanzania maskini tunatakiwa kulipa tshs bilioni 184 kwenye kampuni ya kikundi fulani watu ndani ya CCM, na tumekwisha anza kulipa kama ujui fala wewe, umeme sasa hivi bongo wametupandia bei kwa 50% bila kujua ndio tunalipa hilo pesa. Watanzania wenye uchungu kama mimi tutaandamana tu.. hao polisi wapumbavu wanapiga watu walioandamana wakidai haki wanasahau wanaishi kwenye nyumba zilizojengwa kwa mabati na mshahara wao ni tsh 140,000 kwa mwezi chini ya hiyo serikali ya CCM we unaonekana hujui chochote ungejua kinachoendelea bongo usinge comment upuuzi wako huo.

    Kwa rasilimali tulizokuwa nazo bongo tunaweza kuishi kama maisha mazuri kupita ulaya lakini watu wachache ndani ya CCM ndio wanaishi maisha bora hawajui nini maana ya umasikini. na wewe ni mmoja wao

    ReplyDelete
  23. Jamani Jamani!!!!! wenzetu mnapotaka kwenda huko siko kabisa. Acha nitoe ushauri wa bure kwa viongozi wa Chadema, Jamani kama uchaguzi umeisha sasa kilichobaki ni kutekeleza Ahadi mlizotoa kwa wananchi sio kufanya fujo mfano MH.Mbowe,MH.Ndesamburo nyie wote mnaongoza majimbo kunaadi mmetoa kwa wananchi wenu huo ndio ulikuwa wakati mzuri wa kutatua matatizo ya wananchi wenu sasa hili la Katiba mnaenda nalo kidogokidogo hata kiongozi wa nchi kabuli katiba iangaliwe tena sasa fujo za nini? jipangeni 2015 sio mbali fanyeni mambo kwenye majimbo mlioshinda 2015 uraisi mtapata,majimbo yataongezeka tu huo ni ushauri wa bure.Mtafanya fujo mtapigwa watu wenu watapoteza maisha bure.

    ReplyDelete
  24. Mtoto akililia wembe mpe achezee ukimkata atajua mwenyewe haya ndio yaliowakuta chadema.

    ReplyDelete
  25. MH.Lucy Owenya, hongera mama naona unawakilisha wanabeiging wenzako kwenye kudai haki hongera mama naona upo fiti kinoma kila la heri mama kwenye kudai haki,Lakini angalia jamaa hawajua wewe mwanabeging au wewe chadema wao wanatwanga kotekote kazi kwako.

    ReplyDelete
  26. Tatizo kubwa Tanzania ni uelewa. Chama cha siasa sio sheria. Kuna Korti ndio zinazotoa haki ya kufanya jambo. Kama umeambiwa usiandamane basi kupinga kitendo hich nenda mahakamani. Kwa mfano UK wanafunzi wameruhusiwa kuandamana kwa amani, na walipoanza fujo na kuvunja majengo vyombo vya dola viliingilia kati na kurusha rungu. Kuna wanafunzi wako hospitali sasa, wengine wanatafutwa kwa makosa mbali mbali waliyoyafanya wakati wa maandamano. Chadema lengo lao hasa ni kuleta fujo mpaka waingizwe kwenye serikali.

    ReplyDelete
  27. kwa kweli watanzani waliowengi tuna upungufu wa akili tukianza na viongozi wetu,kama wana CHADEMA waliomba kuandamana kwanini jeshila polisi liingilie kati na kuwapiga watu?????? jeshi la polisi jamani kuweni na ustaarabu kwani mabomu ya machozi yaliyo rushwa jana ni kodi ya mtanzania mlala hoi ilitumika kuyanunua haijalishi ni wa ccm au chadema chamuhimu kufanya polisi wetu tumieni hizi zana pale panapokua na ulazima wa kuzitumia.

    ReplyDelete
  28. CHADEMA mlipe pesa za wazungu bila ya maandamano mmekosa Serikali basi..sasa ndio tunaona maana ya kuvaa sare za kombati na sera zenu za uhasama... asiye kubali kushindwa si mshindani... mlipe mliwaahidi wazungu mtawapa nuklia wapiiiiii...hahahaha mtajijuu mtajibeba..... leteni maaendeleo sio magawanyiko MwanaCCM kindakindaki

    ReplyDelete
  29. Chadema oyeee,watawapiga,watawau lakini fikra zenu zitabaki hai na zitaleta mabadiriko makubwa mbeleni.Hayo si mageni kwa serikari ya kiafrika.mungu ibariki tanzania na tusaidie kuleta mabadiriko yatakayo waondowa MAFISADI madarakani.

    ReplyDelete
  30. Nataka kujua hiyo ''intelijensia'' iliyomwambia Mwema kuwa maandamano yataleta vurugu, ilishindwa vp kumwambia kuyazuia hayo maandamano kungesababisha vurugu zaidi ? Where is ur intelligency on that Mr. Mwema ?

    Wenye mamlaka ktk hii nchi kwanini mnayapa majibu mepesi mambo magumu yanayowatatiza Wananchi walio wengi wa nchi hii ? Ondoeni siasa, sometimes u have to act proffessionally.

    Naamini Mr. Mwema angetumia proffessional yake vizuri na udhoefu wake wa muda mrefu mpaka kupewa dhamana ya kuongoza jeshi hili lenye dhamana kubwa ya kutunza usalama wa raia angeweza kuwashauri hao wanasiasa "intelijensia" waliomwamuru azuie maandamano kuwa kuzuia maandamano kungesababisha maafa makubwa kuliko kuyaruhusu yafanyike kwa amani. Mara ngapi maandamano yanafanyika kwa amani bila kuleta hizo intelijensia zao ? Kwa uhakika jeshi la polisi na wizara husika ya kutunza usalama wa rais wanatakiwa kuwajibika kwa hizo damu zilizomwagika huku wakijifanya wanatumia intelijensia.

    ReplyDelete
  31. Hakuna mtu anayeishi Marekani akawa anashabikia uonevu na udikteta. Labda hao waliokuja kutokea UK.

    Sisi tulioko huku USA sote tunapenda Liberty.
    Asiyependa Liberty ni mtu asiyetumia Brains kuendesha maisha yake na badala yake anategemea Coercion (mabavu). Marekani huwezi kupiga mwanamke virungu kama wanavyofanya hao polisi. Hata Muuaji chizi huko Florida aliruhusu kina mama na watoto watoke nje kabla ya kuanza kurusha risasi.

    ReplyDelete
  32. Samahani waheshimiwa, mjadala si kuzozana au kutukanana, bali kuelimishana. Ingawa mimi na suport CCM lakini naona wanachofanyiwa Chadema si haki.Wananchi wana haki ya kuandamana wakati wowote wanaposijisikia hawajatendewa haki. Awe mtu mmoja au kikundi ni haki yao. Wenzetu waliondelea kama Wamerekani wanaita(Freedom of speech, expression and asseamble)uhuru ya kuongea, kujieleza vile vile mkutano. Na hiyo imo kwenye katiba yao.Hamna cha kibali, wala nini, ila viongozi wa maandamano wanatoa taarifa kwa vyombo vya umma kwa sababu zifuatazo. 1.msaada iliwajipange na usumbufu wowote, 2.viongozi wanataka kuvutia watu kwenye maandamno yao,3.vyombo vya habari na watu wajue shida yao.
    Polisi wa kuwapiga wanachadema si cha haki ni unyama wa kikatili. Toka lini kiongozi (mmbunge)wa serikali na chama akawekwa jela kwa kutokubaliana kisiasa?Polisi hawatakiwi kumpiga mtu yoyote na kama wanafanya fujo basi wangewakamata na kuwaweka jela, mpaka kesi yao itakaposikilizwa. Ingawa mie muoga wa siasa na matusi yanayotembea kwenye blogs.imebidi nijitose tu kwa kitendo cha polisi kumpiga mke wa Dr. Slaa (hisani ya Darhotwire picha)kinakwendana kinyume na haki za binadamu. Toka lini polisi wanapiga mwanamke?Tena hadharani? Tuna mambo mengi ya kujadili Tanzania, lakini mwisho tu naona niwakumbushe viongozi ya kwamba ukimwaga damu tu, na wewe iko siku yatakukuta.Mifano, viongozi wa Kenya, Taylor wa Liberia, Governor wa zamani wa state ya Illinois-Ryan na hapa hapa bongo, Ditopile.Na siku hizi ulimwengu ni mdogo, utakimbilia wapi kama Waingereza na Wamerikani wamekugeukia kwa vile sio kiongozi tena? Asante

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...