Rais Mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania,Mh. Benjamin W. Mkapa akiwa katika mahojiano na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa,Bi Flora Nducha katika ofisi za Umoja wa Mataifa,jijini New York, Marekani.
Picha na Mtandao wa Vijana

Wasudan Kusini wapatao milioni 4 kuanzia Jumapili iliyopita Januari 9 wanapiga kura kuamua hatma yao, je Sudan Kusini ijitenge na Kaskazini na kuwa taiofa huru ala la.

Uamuzi wa kufanyika kura hiyo umo kwenye makubaliano ya amani ya 2005 yajulikanayo kama CPA. Kwa mujibu wa jopo la Umoja wa Mataifa la kuangalia kura hiyo hadi sasa mambo yamekwenda salama salimin, bila purukushani yoyote kubwa ya kutia dosari. Upigaji kura unakamilika Jumamosi hii Januari 15 na kitakachosubiriwa ni kutangazwa kwa matokeo.

Kama Wasudan kusini wataamua kujitenga basi wataandika historia ya kuwa taifa la 54 barani Afrika. Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa Flora Nducha amezungumza na mwenyekiti wa jopo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kuangalia kura hiyo Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa akiwa mjini Khartoum kuhusu mchakato mzima wa kura hiyo.

Kwa mahojiano kamilia basi bofya
http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili
au
http://www.facebook.com/UNRadioKis
au
http://twitter.com/redioyaum
au moja kwa moja kwenye mahojiano yenyewe
http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili/detail/120145.html

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...