


Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Poleni jamaa wote kwa maafa yaliyowakuta.M/mungu awape nafuu ya haraka kila la heri tupo wote pamoja.
ReplyDeleteSasa hapa sijui nani wa kulaumiwa kwani tukio kama hili limetokea miaka miwili iliyopita na bado tunashindwa kujifunza kutokana na makosa yaliyopita.Mwaka huu tunatimiza miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika tunashindwa hata kuwa na kikosi cha uokoji tunapopata maafa kama haya watu wa mekuwa wabinafsi kupita kiasi hamjali wala kuangalia thamani ya maisha ya binadamu wenzenu,kumbukeni mungu yupo na wote njia yetu ni moja.
ReplyDeletePoleni sana jamani.Kaka Michuzi na team yako asanteni sana kwa kutufikishia habari hii.Inasikitisha sana kuona katika karne hii jambo kama hili linatokea, inakuwaje jamani mpaka mabomu yanalipuka na kudhuru watu?
ReplyDeleteSerikali itueleze kwa kina kwa nini mabomu yanalipuka???????? na hii mara ya pili wananchi wanapata maafa alafu mahali pakukaa hawana wananyanyasika hawapewi hata hela ya kujenga nyumba zao ambazo zimebomoka,ichunguzwe kwanini yalipuke kuna kitu hapo kabisaaaaaaa tutaendelea kuwa masikini tuu kwa wengine kujinufaisha
ReplyDeleteJeshi na serikali lazima watupe maelezo kulikoni maana haya mabomu yamekuwa too much sasa.
ReplyDeletekutenda kosa sio kosa kurudia kosa ni kosa kubwa sana
ReplyDeleteKufanya kosa ni kurudia kosa. Serikali yetu na Jeshi ni nini kinaendelea? hali hii inaumiza sana maana tunapoteza ndugu zetu wengi na wengi kukosa makazi kabisa. Maisha haya mpaka lini jamani. Poleni sana wahanga. Tuko pamoja.
ReplyDeleteKwa kweli hii sasa imekua tatizo, Lazima serikali itoe tamko sababu ya hii milipuko. Mbona inatokea Dar es Salaam tu???? Huko mikoani hakuna maghala ya silaha??? Au silaha zinauzwa kisha kuchoma kupoteza ushahidi kwa ma'auditor??? inashangaza sana serikali isiyomakini kama hii...!!!
ReplyDeleteI am definitely Speechless.
ReplyDeleteTunaitaji vyombo vya habari vitukomboe, ili kujua kama bwawa lina ruba lazima utibue maji
ReplyDeletekambi za jeshi, na sehem za kuhifadhia silaha zilitakiwa ziwe nje ya mji ( uraian) amabpo mbali na nyumba za raia, tukio bhilo lilishatokea karibuni na wtu wazima na watoto waliathirika na kupoteza maisha, pale ndio ilikuwa pa kujifunza na hatua zingechukuliwa, kwasababu kama sasa hivi limetokezea tena na aliathirika ni raia, kama kambi zingekuwa nje ya uraiani haya angeepukika. lakni viongozi hawakuliona hilo, wanaona kama wangehamishia hizo kambi itawacost, laki saa hivi mtanzania ndie anaelipa hizo costza maisha yake. kufanya kosa ni kosa na kurudia kosa ni uzoefu wa makosa. maisha ya naraha jaman na kila mtu napenda roho yake, hakuna mtu amabe anataka kufa kwa excident za ajabu ajabbu na kwa vitu vinavyoweza kuepukia
ReplyDeleteMimi MOHAMED wa MUCE IRINGA: - Makambi ya jeshi yahamishwe mbali na makazi ya watu.Au wahamie Dodoma,haipendezi kuona Watanzania wakifanywa kuwa misitu ya kujaribia ubora au ubovu wa silaha.Najua si muda muafaka kuanza kulaumiana lakini kutokana na mabomu ya Mbagala tulijifunza nini? Na serikali ilituahidi nini? Mwaka huu wasiunde tume badalake wachukue hatua madhubuti dhidi ya matatizo kama haya.POLENI SANA WATANZANIA WENZANGU kwa wakati mgumu mlionao kwa sasa Mungu atawarehemu.
ReplyDeleteWaziri wa ulinzi Mwinyi na viongozi wa jeshi wajiudhuru hawawezi kazi. Watu wamekuwa kama wakimbizi ndani ya nchi yao?
ReplyDeletePoleni sana mliopatwa na maafa hayo. Serikali iwajibike kwa hili siasa pembeni
Ni vema na haki hili suala la mabomu kuweza kufanyiwa uchunguzi wa kina ili kupata ufafanuzi yakini. Nadhani jambo usiololielewa ni kama usiku wa giza. Binafsi sielewi ni nini hasa sababu ya milipuko hiyo na kama yaweza zuilika au la... sioni kama ni wakati wa kulaumiana lakini kutokana na ukubwa wa madhara yake inapotokea kwa niaba ya wananchi naomba serikali na vyombo vyote husika wafanye uchunguzi na kutoa ufafanuzi kwa wananchi. Ni muhimu sana wananchi ambao ndio waathirika wakubwa kulielewa hili jambo..Vinginevyo wananchi wanapokosa imani na serikali yao ni hatari kwa taifa zima. Mwisho nawapa pole wananchi wote walioathirika na shida hii last time mbagala na sasa gongo la mboto. Kikubwa tumtumaini Mungu lakini zaidi tushirikiane katika uwajibikaji wa kuzuia maafa kama haya.Shukrani.
ReplyDeleteMwananchi mzalendo,
Agnes
POLENI SANA WALIOPATWA NA HAYA MAAFA. Ila serikali yetu na wahusika wake katika kila nyanja huwa hawako makini au serious kwa kila jambo. Nina uhakika bongo watu wanaishi kwa kudra za mwenyezi Mungu na si vinginevyo. SERIKALI INABIDI IWAJIBIKE HASA KATIKA HILI.
ReplyDeleteMy Dear minister of defense i think its wise to resign now. Sympathise with the loss of lives. Accountability though not common in Tanzania, but this sounds too much.
ReplyDeletePlease do something to show the public that you care for them.
yani wanajeshi wa tanzania ni wazembe kwanini hawachukuwi uangalifu maana ni mara ya pili yani kila siku nasoma blong hii lakini wala sicomment lakini leo nimepatwa na hasira lohhh mnatuvunja nguvu kurudi nyumbani poleni waliopatwa na maafa halafu sidhani hata kama serekali itajali kulipa fidia
ReplyDeleteNI VEMA RAIS AU PM WAKATOA TAMKO KWA WALALA HOI WENZANGU! IWEJE KILA SIKU MALOFA NDO WANAKUMBWA NA MABALAA?? MBONA HAYATOKEI SEE VIEW AU MASAKI??
ReplyDeletePoleni wahanga wote.
ReplyDeleteTukumbuke kuwa haya ni mabomu ya ki-China - tena pengine ya miaka kama ishirini na mitano iliyopita!!!!!!!
Hakika serikali isipowajibika kupitia wizara husika, sidhani kama watanzania tutawaelewa. Hivi kweli pasipo aibu mnatuambia ni ajali tu, kwa hiyo ni kama vile bomba la maji kupasuka walio karibu hulowa na maji! Tuna tofauti gani na nchi zilizopo katika vita kwa sasa? kero zimezidi kupita kiasi, umeme shida, maji ni kitendawili na sasa mfululizo wa maafa ya mabomu, tuwaeleweje serikali iliyopo madarakani? Wahenga walisema ukila na kipofu usimshike mkono, sasa wamnyang'anya
ReplyDeletetonge mkononi?!!............madhara yake yaja hima.
Kwa kweli inasikitisha sana
ReplyDeleteHii ni maafa ya kitaifa. Je, serikali itatoa tamko rasmi kuhusu tukio?
ReplyDeleteNa ni kweli makambi ya jeshi yanatakiwa kuwa mbali na wananchi kuepeusha maafa ya kama hayo.
Mungu alaze roho za waliopoteza maisha yao mahala pema mbinguni. AMEN.
we are very sory for the ones who are directly or inderectly affected by the tragedy..!! i think ministirial responsibility must take place now.. we expected that, after the mbagala bombing, then army would have taken steps forward to ensure they counter check the rest of the camps counetry wise.. but the recent bombing is evident that they didnt do so..!! we expect the resignation of the minister responsible..!!!
ReplyDeletepoleni sana watanzania wenzangu..!!
MIMI MAFIKIRI KWA HILI SERIKARI HAINA CHA KUTUAMBIA INATAKIWA KUOMBA RADHI KWA WANANCHI NA KUWALIPA FIDIA ZA UKWELI SIYO MTU ANAKUFA AU ANAVUNJIKA MGUU ANALIPWA SHILINGI LAKI MBILI .INGEKUWA WALE WA MBAGALA WAMELIPWA IPASAVYO NADHANI SERIKALI ISINGEFANYA UZEMBE. HUU NI UZEMBE TU WALA SI KITU KINGINE NA WASISEME AJALI WASEME SERIKALI NI WAZEMBE NA WAWAOMBE WANANCHI MSAMAHA.
ReplyDeleteNILIDHANI SERIKALI IMEJIFUNZA YALE YALIYOTOKEA MBAGALA.SERIKALI NI WAZURI KATIKA KUJITETEA LAKINI MUNGU ATAWASIMAMIA HAO WALIOPATA MATATIZO.
NI VIZURI KUEPUSHA AJALI NA SIYO KUSUBILI YATOKEE NA WATU WAANZE KUUNGUA NA JUA NNA KUTOKWA NA JASHO KUFUATILIA VIJIHELA.
Like father, like Son. Dr Mwinyi tafadhali chukua hatua kama mzee mwinyi alizochukua alipokuwa waziri wa Mambo ya ndani.
ReplyDeleteinasikitisha sana,yaliyotokea mbagala haikua fundisho,na pia hata yaliyotokea mbagala ilikua ni uzembe,sasa kwa haya gongolamboto sijui hata tuseme nini,maana ni zaidi ya uzembe, kutojali maisha ya watu, kupuuzia kila kitu,ubinafsi, kutokuwajibika, kutokuipenda nchi na pia kutojali wananchi.maafa ni makubwa sana ingawa si rahisi kusema ukweli.wakipoteza maisha watu 200 tunaambiwa 2o.uongo kila sehemu,kweli Tanzania imeoza!tukizamia ughaibuni tunaomba msitulaumu,mambo kama haya yanachangi sana.
ReplyDeletemariam USA
Mwanzo kambi za jeshi zilikuwa mbali na uraiani. Lakini kila idadi ya watu mijini ikiongezeka, wananchi wanajenga karibu na kambi. Cha msingi ni kuwa jeshi la Tanzania halina tabia ya kuangalia usalama wa silaha kila kipindi fulani. Wakati umefika kufuata viwango vya kimataifa katika kila sekta nchini.
ReplyDeleteWANAJESHI WAMEKOSA UZALENDO JUU YA NCHI YAO NA WATANZANIA WENZAO.
ReplyDeleteHIVI HII IMEKUSUDIWA AU NI BAHATI MBAYA? NI MARA YA PILI SASA WANANCHI WASIO NA HATIA WANAPOTEZA MAISHA. SERIKALI ITUJALI JAMANIIII!!!! TUTAISHI KWA WASIWASI KAMA TUPO DAFU MPAKA LINI?